Jumapili ya tarehe 06/18/2023, mida ya 12:30 asubuhi (masaa ya AfricaMashariki). Mchungaji Aketch wa kanisa la Menonite lililopo Dar es salaam, Tanzania, jimbo la Segerea; alifanya ubatizo wa kuzaliwa upya kwa njia ya maji mengi kwenye bwawa la Golden Tulip hotel, Oysterbay. Miongoni mwa waumini wapya hao katika Bwana, alikuwemo Mzee Otieno Olung’a Igogo ambaye ni baba yangu mzazi.
Juu ni Mzee O.O Igogo akibatwizwa kwa maji mengi. Hongera sana kwake, Mwenyezi Mungu azidi tembea naye kwenye safari hii ya kiroho.
Mchungaji Aketch pamoja na mama Mchungaji (mwenye nguo nyekundu) wakiwa na mtoto aliyezaliwa upya siku ya leo mzee O.O Igogo na mama Igogo.
Baadhi ya wanafamilia ya mzee O.O Igogo kutoka Segerea siku ya jana jioni waliungana na wanafamilia ya mzee O.O Igogo ya Kibada, wakapata chakula cha jioni pamoja, wakapumzika, na leo asubuhi waliamka mapema sana kwaajili ya kumsindikiza baba /Babu yao kipenzi kwenye safari yake mpya ya kiroho ambapo atabatizwa kwa maji mengi. …. Sifa na utukufu vyote twamrudishia yeye aliye umba Mbingu na nchi. Amen.
Andrews university ndio chuo kilichonipa nafasi mimi ya kuja Marekani. Ngoja niwape story fupi ya safari yangu ya kuingia hapa.
Siku zote nilikuwa natamani kusoma /kuishi nje ya Tanzania. Na mara nyingi nilikuwa napenda Australia, UK, na Marekani. Ilikuwa rahisi kujenga hisia zangu na maeneo hayo kwani mara nyingi nilivahatika kupata vijuzuu vinavyoonesha shule mbalimbali za nchi hizo. Basi, nikiwa katika muhula wa mwisho wa kumaliza chuo pale C.B.E siku moja nikiwa kanisani Temeke SDA, katika matangazo nikasikia wakitangaza kuwa chuo cha Andrew wanapokea wanafunzi kwa muhula wa Fall (Fall semester), na wakasema kuna vijuzuu kama kuna mtu angependa kwenda akachukue ili ujuwe jinsi ya kujiunga. Mara baada tu ya ibada, nikaenda kuchukua kijizuu. Baada ya siku kadhaa nikaenda kwenye intranet Cafe fulani ilikuwa karibu na chuo cha C.B.E. Ndio kwa mara yakwanza nafungua email akaunti yangu 🙈 Nikajaza fomu siku hiyo. Baada ya muda wa miezi kadhaa nilitumiwa barua kwa njia ya posta kuwa wamenikubali kuingia chuoni hapo kwaajili ya degree ya kwanza. Wakati huo nilikuwa nimesha hitimu C.B.E sasa natafuta chuo cha kwenda.
Nakumbuka mmoja wa wadogo zangu (cousin sister) aitwaye Detta alikuwa akipenda kunitania kuwa “aah wewe ni wa hapa hapa tu” namwambia mie nakwenda zangu Marekani subiri utaona. Hapo sijajua kama nitachaguliwa au la! Ila yeye alikuwa anasema hivyo kwasababu dada yangu mkubwa alisoma China, kaka yangu alikuwa UK, na mdogo wangu yeye alikuwa anasoma South Africa. Hivyo akawa anasema mie nitabaki Bongo.
Ghafla, siku moja naletewa barua nikiwa job (niliajiriwa na Utegi Technical Enterprises Ltd baada ya kumaliza chuo), kuangalia ilipotoka nakuta ni Andrews University. Nikaifungua haraka sana! Nikakuta ni barua ya kukubaliwa kujiunga na chuo ila sasa muda ulikuwa umebaki wiki 2 tu shule ianze 🙆🏽♀️🙆🏽♀️ Nikachanganyikiwa maana hizo hela zinazo hitajika na muda uliobaki, dah! Yule mzee kutoka kanda maalum nitamuingiaje?! 🤣 Mtu wakwanza kumwambia alikuwa ni mama. Yeye akanipa moyo akasema hongera sana, mwambie baba haraka sana. Sasa kesho yake hasubui tumesha maliza kunywa chai tunataka kwenda kazini, mama akalipua bomu kimtindo. 🙆🏽♀️
Akasema “Umesha mwambia baba?”, nikajifanya kutoa macho 😅 baba akauliza nini unataka kusema? Akasema (Akaniita kwa jina langu la kilugha) kaa chini “let’s talk ni nini”. Ikabidi nimwambie. Akasema sasa kwanini naogopa kusema jambo zuri kama hilo. Nikamwambie mzee nikienda siku yakwanza tu inatakiwa malipo ya awali ya nusu semester (muhula) au ada nzima. Kanijibu sasa tatizo ni nini? Kwani wewe ndio unatoa hizo pesa? Basi mzee wa watu siku hiyo akasimamisha shughuli zake zote, kuhakikisha napata documents zote zinazohitajika na kuzituma kwa njia ya fax na DHL. Chuo nao walikuwa shapu walipoamka tu wakatuma email kua sawa wanasubiria documents za DHL halafu watatuma I-20 (form maalum yakuombea viza ya shule). Mzee aliwaambia kutoka na muda watume kwa DHL halafu atawalipa hiyo pesa. Basi baada ya wiki 1-20 imefika. Nikaweka appointment ya kuomba viza. Tukaenda kwenye Viza, kumbuka nina siku tu zakuripoti shule, hivyo ticket ya ndege ilibidi nikate kabla hata ya kupata viza. Kwenye viza si kidogo watuzingue! 🤣🤣
Basi, tumefika kwenye viza wala sikuhojiwa maswali mengi, wakasema kila kitu kipo vizuri lakini cheti changu cha form 4 ni “Fake”! 🙆🏽♀️🙆🏽♀️ Wakadai tumepiga simu wizara ya elimu wamesema hizo namba sio zake. 🥺🥺 Wakasema kama mnaweza kwenda wizarani mkahakiki nendeni kisha mrudi hapa. Wakatupa reference namba, na jina la mtu walie ongea naye hapo wizarani. Basi, tukatoka mbio kwenda wizarani, tunafika getini tukasema jina la mtu tunayekwenda kumuona, wakampigia simu huyo mtu kumwambia kua kuna wageni hapa wanahitaji kukuona. Yule mtu akaomba aongee na baba, akasema samahani rudini ubalozini wanawasubiria kule tumesha tatua tatizo. Alikosea kusoma namba. 🤣🤣🤣 Baba akasema lakini nilimuuliza unahuwakika kuwa cheti cha binti yangu ni feki na akanijibu kuwa “100% sure”. Mzee hasira zikamshika lakini sasa atafanyaje inabidi turudi tena ubalozini. Sasa wakati baba anamaliza kuongea na yule.mtu wa wizarani, secretary wake akapiga simu muda huo huo akasema “baba mnatafutwa na ubalozi wa Marekani wamesema mwende sasa hivi”, baba akamwambia ndio tunaelekea huko, lakini hawa watu leo ndio watanijua mimi ni nani! 🤣🤣🤣 Usichezee mzee wa kutoka kanda maalum.
Basi tukafika ubalozini, tukapokelewa vizuri, yule mdada akaomba msamaha kwa usumbufu, akachukua passport yangu akasema kesho asubuhi uje uchukue na nakutakia masomo mema. Mzee Igogo sasa akaanza, “young lady I need an official oppology letter” 🤣🤣 Eti huwezi kunifedhehesha mbele za watu halafu unaomba msamaha kiholela holela namna hiyo. 🙈🙈 Yani mie I was like just give my passport am ready to board. Nyie muendelee na drama yenu kimpango wenu. 🤣🤣 Nilipata passport asubuhi, usiku nikaondoka zangu siku hiyo hiyo.
Ilikuwa mara yangu yakwanza kutoka nje ya East Africa. Niliondoka na ndege ya British Airways, business class 😍😍 mzee Igogo sijui alifikiri nikipanda economy nitachelewa 🙈 Mwe! Nilifurahi sana. Tukafika UK, tukapelekwa hotelini kwa ajili ya kupumzika mpaka asubuhi kuanza safari ya kuelekea Chicago O’Hare International Airport. Baada ya kufika Chicago shulenilinielekeza kuchukua basi lakuelea Indiana. Waliniambia nishuke kituo cha mwisho ambapo ni Indiana Airport na hapo nitakuta gari la chuo cha Andrews likinisubiria. Nilifata maelekezo nikafika shule salama kabisa.
Nilifikia kwenye dormitories za chuo. Jamani acha tu! Unaingia kwenye dormitory ya chuo kama hotel vile. 😍 Nilikuwa na roommate mzungu kutoka Canada, alikuwa anaitwa Melissa Gonzalez. Vyumba ni self contained, mna bathroom na shower yenu kwa chumba, for a minute nikakumbuka mabafu ya C.B.E mabafu 3 watu zaidi ya 20 ni mwendo wa kusubiriana wengine wanaamua kuoga< kwenye kolido🤣🤣 Kwakweli,.Andrews ni shule nzuri sana sema gharama zake sasa! 🙆🏽♀️🙆🏽♀️Pasua kichwa.
Siku ya tarehe 02, 04, 2023 ilikuwa ni siku ya kumbukizi ya mfanano wa siku ya kuzaliwa mwanangu Mercy.
Birthday girl akiingia kwenye mgahawa
Kama video inavyo onyesha hapo juu 👆🏿 Alianza kusherekea siku moja kabla ya siku yake maaalum kuwasaili, ambayo siku hiyo ilikuwa ni Jumosi ya tarehe 04/01/2023. Sambamba na marafiki zake walikuwa pamoja chakula cha usiku katika mgahawa ujulikanao kama Tourão Brazilian Churrasqueria uliopo downtown Houston, Texas. 😍😍
Mtu na mama yake
Basi siku yenyewe ilipofika tulikuwa na muda mzuri pamoja asubuhi na jioni tukaenda tena kufanya kile twapendelea kufanya zaidi 😍😍 Kwakweli sina kingine mwaka huu zaidi ya kusema Asante Mungu wangu. Sifa na utukufu zote ni zako wewe Baba muumba wa Mningu na nchi na vyote vilivyoko. 🙏🏿🙏🏿
“HAKIKA mimi👆 Unipendaye, LEO tumshukuru Mola wetu Muumba na mpaji wa UHAI, kwa kuniwezesha kuhitimu elimu maisha ya MIONGO 7🙏🏿🙏🏿Nikiwa na Afya ya mwili na akili njema siku zote. Furaha niliyo nayo moyoni ni Upendo na Heshima unayonipa kama👉🏿Baba&Babu&Best wako #001 NAKUSHUKURU SANA, SANA👏🏿” ***Sir O.O Igogo***
Naam, hapo juu hiyo ilikuwa ndio salamu yake mzee O.O Igogo siku ya leo ambapo Mwenyezi Mungu amemjalia kutimiza umri wa miaka 70. Kusema ukweli siku zote nilikuwa nikasikia ndugu na marafiki wakisema kuwa baba/mama/bibi yangu ametimiza miaka 70 au 75 basi nafurahia sana. Chaajabu hata siku moja sikuwahi kuwazia wazazi wangu kufika umri huu. 😅😅 Sio kwamba sikujua kuwa wataufikia, hapana! Nivile tu sikuwahi kuwatengenezea picha ya kufikirika wakiwa katika umri huu. Sounds weird eh! 🙈 Twamshukuru Mungu kwa kutupa afya njema ambayo imetuwezesha kushuhudia siku hii ya leo.
Mimi mwenyewe na birthday boy
Nami nilimuandikia ujumbe wakumtakia kheri kwa siku hii muhimu. …”Happy70th birthday to the most influential man in my life! I’m blessed to call you dad. You deserve all that’s beautiful and precious in life. I wish you nothing but absolute happiness, love, peace, and good health on this superb milestone. Happy birthday Jategi, love you much. Otieno Igogo”⁷
Kwakweli tunashukuru sana Mungu kwa kutupa mbaraka huu wa pekee. Tunamtakia maisha marefu yaliyojaa furaha, amani, upendo, na afya njema.
Baba, Blessing, na mama
Recap: Mzee 0.O Igogo 70th birthday 👆🏿 …… Thank you so much, Robin Thomas Edson, @pixelspro_films, for capturing all these beautiful and precious moments on our dad’s 70th year of life journey on this planet. Ubarikiwe sana.
Masaa kadhaa kabla ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake niliamua kuangalia na ku-share tena baadhi ya video za Mzee O.O Igogo zilizo nivutia na kunikosha moyo 😍😍 na 👆🏿 👇🏿 ni sehemu ya hizo baadhi zilizo zipenda zaidi. Haya enjoy them 😜😜
Muwe na weekend njema sana, sikuu njema ya kufunga mwaka 2022, na kheri na baraka ya kufungua mwaka 2023. Mbarikiwe sana. ❤️ Have a very wonderful weekend, great end of year 2022 celebration, and a peaceful beginning of 2023. Blessings to you all. ❤️
Baraka za kufunga mwaka 2022 ziambatane nanyi katika kufungua mwaka 2023 na zikae nanyi siku zote. ❤️
Maisha yamejaa changamoto ambazo hazikwepeki, na mbaya zaidi zinakuja bila taharifa. Mwezi wa kumi.mwaka huu dada yangu mkubwa (pichani juu) alipatwa na ajali ya kuungua moto.
Akiwa hospitalini
Nisingependa kuelezea undani wa ajali hii kwani huo ni ushuhuda wake yeye, mimi namshukuru Mungu kwa miujiza ya uponyaji wa haraka ambao kwa imani yetu haba hatukuweza kuona ukija. Hali ilikuwa mbaya sana sema ni vile tu siwezi kuweka picha zake humu kwani kama nilivyosema ni ushuda wake yeye. Alilazwa hospitali ya Tabora (Tabora ndipo makazi yao yalipo kwa sasa) kwa muda kisha akahamishiwa Muhimbili ambapo alilazwa takribani zaidi ya mwezi mmoja.
Baada ya kutoka hospitali wanandugu walikusanyika nyumbani kwao huko Yombo Vituka kwaajili ya kumshukuru Mungu kwa maajabu ya uponyaji wake aliyompatia dada yetu.
Mungu ni mwema sana na siku zote anajibu maombi yetu zaidi ya imani yetu. Tutalisifu na kulitukuza jina lake milele na milele.
ikafika muda wa kusema ‘kwaheri’ neno ambalo si rafiki kwa vinywa vya watu wengi kwasababu ya uhalisia wa neno hilo! Basi hii ndio ilikuwa siku yangu ya mwisho Tanzania kwa mwaka 2022. Pichani kutoka kushoto ni mdogo wangu Janeth (mzaliwa wa nne), mimi mwenyewe mtu kati hapo (mzaliwa wa tatu), Magreth Nyasungu (mzaliwa wa tano), na Guka (mzaliwa wa sita).
baba na mama Alpha 😍Mama Bear and her cubs 😍
Our prayers warrior, the glue that keeps our family together, our iron lady , our super woman, the centerpiece of our blessings, mama Igogo we love you, Mama. May our Almighty God continue to keep you well.
DubaiTanzanite Business lounge-JKN International Airport
Namshukuru Mungu kwa yote naomba azidi kutupa afya njema na ulinzi wa kutosha ili tuonane tena na tena sio kwa ajili yetu bali kwa ajili ya utukufu wa jina lake. 🙏🏿❤️🙏🏿
Namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kuonana na marafiki zangu wanguvu! Ulikuwa ni wakati wanfuraha sana nilipo onana na kaka yangu Jerry Minja. Kwakweli Mungu yu mwema sana. Huyu kaka yangu ni tuliishi naye huko Kalamazoo, Michigan kabla ya yeye kuamua kurudi Tanzania na kuanzisha familia huko.
Pia nilifurahi sana kuonana na rafiki dada yangu Dr Flora Myamba. Huyu bidada naweza andika kitabu kizimaaaa kwaajili yake 😅😅 she’s my ride or die friend l! Yani hata kumuita rafiki naona kama nakosea jamani acha tu nimuite ninavyo jisikia, dada yangu! Wenye wivu wakanywe sumu wafe 😅😅😅 Huyu bidada na familia yake na ndugu zake wote ni binadamu na nusu!! Yani roho zao ni mfano wa Malaika!! Nafikiri ndio urafiki wetu umeweza kudumu kwa kiwango kilekile cha “grade A” muda huu wote kwasababu tabia na roho zetu zinafafana kwa kiwango kikubwa sema mie SINA uvumilivu wa watu wasiojitambua / wanafiki kama alionao Dr. Flora. 😅😅😅 Yani mie nikakujua wewe ni “wakichina” nakupa mkno wakwaheri haraka sanaaaaaaa. 😅😅😅 Sijui ku-vibe na fake people. Hiyo imenishinda kabisa mpaka leo hii. 🙆🏽♀️🙆🏽♀️🙈 Hapo tulikuwa nje ya ofisi yake.
Tukiwa ofisini kwa Dr. Flora Tukiwa site
Baada ya kutoka ofisini kwake akanipeleka site kuona mjengo wao watakao hamia hivi karibuni. Jamani, furaha niliyokuwanayo utasema mjengo wangu mimi!! 😍😍 this mansion is 🔥🔥🔥 Can’t wait kuanza kufanya party zetu like the way we used to do it in Michigan yoo! 😍😍💃💃
Ma’am! My friend got money, yo! Msimchukulie poa kabisa, ni level nyingine hii wengi wenu bado sanaaaaaaa kufika level yake! 😅😅 Happy and proud of her💃💃💃
Siku ambayo nilikwenda limsalimia kaka yangu Jerry huyu mpwa wangu hakuwepo. Alitamani kumuona aunt Alpha naye aunt Alpha hakusita kufunga safari kwenda kumuona. Ndio mtoto wa kwanza na wapekee (kwasasa 😜) wa Mr and Mrs Jerry Minja.
Muheshimiwa ndio alikuwa nami siku hiyo, hivyo Kristos alionana na aunt Alpha na aunt Magreth. Mungu ni mwema sana.
Hapa ilikuwa siku nyingine mimi na Dr. Flora tulikwenda kula mishikaki ya Samaki pale Container, Mikocheni. 😍😍 love you Dr.
Namshukuru Mungu kwa kutupa nafasi ya kutembelea familia ya mdogo wangu Janeth/ familia ya Nyagilo. Mimi nilikuwa sijawahi kufika kwenye huu mji wao mpya kwani walipo maliza ujenzi na kuhamia nilikuwa sipo. Wanaishi Mbweni walihamia huko takriban miaka 2 iliyopita.
Safari yetu ilianzia nyumbani Kibada ambapo nilipata ukodaki moment na mtoto wa kaka yangu aitwae Mary, huyu ni mjukuu namba 3. Na kulia kwangu ni kijana wa dada yangu mkubwa anitwa Daniel, yeye ni mjukuu namba 2 na pia ndio mjukuu mkubwa wa kiume.
Mercy
Bidada hapo juu ndio mjukuu namba moja, na wazazi wangu hupendelea kumtambulisha hivyo kwa watu “mjukuu namba moja” 😍😍 Eeh! Niliwapiga chenga wakubwa zangu nikaleta mjukuu wa kwanza! 😅😅
Hapo juu naye ni mpwa wangu, mtoto wa pili kuzaliwa kati ya watatu. Anaitwa Evin Otieno Nyagilo, bali mie napenda kumuita “my International nephew” 😍😍
Alipewa jina la kati la baba yetu. Pia mtoto wa dada yangu Daniel naye alipewa jina la kati la baba yetu-Otieno. Mbaaraka mkubwa sana. Mary yeye alipewa hilo jina kwasababu alizaliwa siku ya Christmas 25th, December huko U.K. She’s a Christmas baby. 😍😍 Huwa napenda kumuita Kitukuu cha Queen Elizabeth, Muingereza mwenye ngozi ya Chocolate. 😜😍😍
Kwakweli, tulipokelewa vizuri sanaaaaaaa! Tulikula, tukanywa, na kusaza! Tukacheza na kufanya utalii wa mji wa Mbweni. Jamani huko watu wamejengaje sasa?! Yani ni kibabe sana.
Sisters
Hapo ni wadada wa tumbo moja, Wakwanza kwa madada ndio mama Daniel, halafu mimi-mama Mercy, halafu Janeth -mama Evin. Yani Magreth a.k.a Mrs Jacob Massawe ndio alikosekana hapo. Alikwenda Moshi kwenye harusi ya shemeji yake.
Pia Blessing pichani juu naye hakuwepo, yeye ndio mtoto wa mwisho kwa baba. Anafanya tunakuwa na idadi ya watoto 5 wakike. Mungu wetu ni mwema sana twamshukuru kwa yote.
Twamshukuru Mungu kwa pumzi ya uhai anayotupatia kila siku ambayo ilituwezesha kuona na kusherekea siku ya kumbukizi ya kuzaliwa wapendwa wetu. Kulikuwa na birthday tatu mwezi wa Nane. Yakwanza ni ya mdogo wangu Janeth kama video inavyo onyesha hapo juu 👆🏿,
Tulikutana Johari Rotana hotel tukala, tukanywa, na kufurahi pamoja sisi kama madada na wifi yetu mke wa kaka yetu. Yani hapo katika madada aliyekosekana ni Blessing peke yake. 😍😍
Ikafuatiwa na ya mume wake Janeth, shemeji Tobby mtu kati hapo juu!
kisha ya mama yetu mkuwa Mama Sarungi. Tulifurahi sana.
Siku zote tukipata nafasi ya kuwa pamoja huwa namshukuru Mungu sana, na huwa naakikisha nampa mwanangu 100% ya my attention! 😍😍 She’s everything to me! Kutokana na ratiba yake ya shule pamoja na kazi muda mwingi huwa tunapishana. Hivyo nyakati kama hizi ni muhimu sana kwetu sote. Si kwa uwezo wetu bali ni kwa neema yake Mungu Mwenyezi. 🙏🏿❤️🙏🏿
Haya nawatakieni weekend njema na Sabato njema sana kwa waaminio.
July 31st, 2022 siku kadhaa baada ya mimi kufika nyumbani wanafamilia walikusanyika kwaajili ya kusalimiana na kufurahia pamoja kama familia. Zifuatazo ni baadhi ya picha na video ya siku hiyo.
Baba na wanawe
Yani hapo juu ni picha hadimu sanaaaaaaa! Kitendo cha kaka yetu mkubwa kuwepo kwenye picha ni kitendo kinachotekea kwa NADRA mno. Hapendi kupiga picha kabisa yani hata hapo tulimlazimisha kweli akaona aibu akakubali 😅😅
Mzee 0.O Igogo na kaya zake 😍Mabinti wa marehemu mzee Cornel Awiti
Pichani juu ni mama yangu mzazi na wadogo zake wa tumbo moja. Warembo wa marehemu mzee Cornel Awiti na marehemu Valeria Awiti, hapo wamekosekana mabinti watatu tu nao ni; Felista Awiti (Mrs Joseph Musira) huyu ndio wakwanza kuzaliwa. Wapili kuzaliwa ni Mwalimu Anna Awiti (Mrs. John Obure), na Yacinta Awiti (Mrs Amos Onditi) huyu kuzaliwa ni wapili kutoka mwisho kati ya watoto 18. Mtoto wa mwisho kuzaliwa ni huyo mwenye gauni lenye maua meusi na meupe hapo juu anitwa Julia Awiti (Mrs Airo).
Wakwe nao hawakubaki nyuma 😍😍 Mmoja hakuwepo ila aliwakilishwa vyema na mkewe (dada mkubwa) mwenye gauni la blue.
Jamani rahaaa! Mwenzenu naringaje sasa kadogo kangu kanakuwa kadada. The two digits era began just like that ma’am! 😍😍
Mwenye birthday yake katika pozi na tabasamu kama lote kufurahia miaka 10 ya uhai wenye afya na baraka tele. Sifa na utukufu twamrudishia Mungu Mwenyezi. 🙏🏿❤️🙏🏿
I’m lost of words! She’s a beautiful young lady. Mungu azidi kutembea nawe mdogo wangu ukawe kiumbe kizuri umpendeze Mungu kisha mwanadamu.
Akiwa kwenye matembezi huko Turkey wakati wa summer mwaka huu. Sasa hiyo kijana inafanana na ragi ya chama pendwa ya dad yako 😅😅
Awwih! Once again, happy 10th birthday Blessing. Love you mingi.
Kamanilivyosema kwenye posti yangu iliyopita somahapa yakwamba mwaka 2022 ulikuwa na baraka zake nyingi sana. Basi katika kuhesabu mibaraka yangu naweza sema huu nao ni moja ya mbaraka mkuu. Ni jambo ambalo lilinifurahisha zaidi 😍😍 Ni surprise niliyo wafanyia wazazi wangu.
Tarehe 25 mwenzi wa Saba, mwaka huu wa 2022 (07/25th/2022) ilikuwa siku ya furaha sana baada ya mipango yangu ya kuwafanyia wazazi wangu haswa mama yangu safari ya kuwasalimia bila ya kuwapa taharifa kama ilivyokua huko nyuma. Nimpango ambao nilipanga na mdogo wangu aitwaye Magreth Otieno Igogo a.k.a Mrs Jacob Massawe kuwa tutamfanyia mama surprise wakati wa siku yake ya kuzaliwa ambayo ni tarehe 27th July. Bahati mbaya ratiba yangu ilibidi nifike siku mbili kabla ya birthday yake. Mimi nilichukua likizo na kuandaa safari bila kumwambia mtu yoyote nyumbani isipokuwa mdogo wangu, mume wake na mwanangu tu. Sikutaka mama ajue kabisa hivyo kuzuia wanafamilia wengine kujua hata marafiki ilikuwa muhimu sana. Nashukuru Mungu kila kitu kilikwenda vizuri kama tulivyopanga tuliomba kibali cha Mungu kwa kumkabidhi mipango yetu naye akaibariki ikatimia. 😍🙏🏿😍Safari yangu ilianzia Houston, Texas.
Nakumbuka siku nakwenda airport tulimpigia mama simu, akiwa nyumbani na baba na shangazi yetu fulani wakipiga story zao, nikaanza kumuuliza anampango gani na birthday yake?! Akawa anasema nahamu namtoko fulani amazing 😅😅 lakini ameshapanga kwenda Fun city na watoto wake wa shule (school trip). Nikamwambia kwautani nikikutumia Dola Mia ($100) uongezee kwenye hiyo trip itatosha? akasema itatosha sana. Nikamwambia basi nitakutumia tarehe 25, ambayo ndio tarehe nilikuwa najua naingia nyumbani. 😅😅😅 Basi nikamalizia kwa kumwambia wakifunga shule apange trip yeye na wadogo zake na dada zake waende kutembea Zanzibar au mbuga za wanyama, wafanye bageti halafu anijulishe. Akashukuru kweli kweli bila kujua mimi hapo naingia uwanja wa ndege teyari kwa kum-surprise! 😍😍
Sasa, ilikuhakikisha chumba changu kipo katika hali nzuri mdogo wangu alimdanganya mama kuwa ana wifi yake anakuja toka Japan na ana mtoto mdogo hivyo anaomba aandae chumba cha dada Alpha (eeh usishangae sana, nina chumba changu kwa mama yangu 😍😍) ili afikie humo kwa siku kadhaa kabla ya kwenda Moshi. 😅😅 mdogo wangu wanaishi nyuma tu na kwa mama. Basi mama naye bila shaka wala kinyongo akamkubalia pasi kujua mwenye chumba yupo njiani. 😅😅Nilipofika airport nilipokelewa na mdogo wangu pamoja na mume wake. Tukiwa njiani mdogo wangu akampigia mama simu akamdanganya kuwa amekutana na rafiki yake walikuwa wote huko kijijini Kowak (kijiji alipozaliwa mama yetu), na anasema hawezi kwenda kwake mpaka afike kumsalimia. Mama akanza kuuliza ninani? mdogo wangu alikataa kata kata kusema akamwambia ni surprise akifika hapo itabidi asikilize sauti yake ili amtambue ni nani! Mama alimbembeleza sana amwambie ni nani huyo lakini mdogo wangu alishikilia msimamo kuwa utamuona wakifika. Mama kidogo akawa kama amechukia kwani alikua anasema unakuja na mgeni mimi hata kupika sijapika hata juice ndo kwanza wanatengeneza sio vizuri na hapendi kabisa. 😅😅 mdogo wangu hakubadilisha msimamo wake mpaka tukafika nyumbani, na mengine yote yamebaki kuwa historia kama hiyo video ya tukio hilo inavyo onyesha. 😅😅
Hii ni mara ya pili sasa nafanikiwa kuwa-surprise wazazi wangu. Tarehe 07 mwezi wa tatu, mwaka 2017 kwa kushirikiana na wadogo zangu pamoja na baadhi wafanyakazi wa Utegi Technical Enterprises Ltd (kampuni anapofanyia kazi baba yetu) tulifanikiwa kum-surprise baba yetu ofisini kwake, ilikuwa siku ya birthday yake. 😍😍 Tuliwahi sana ofisini kabla yake kitu ambacho hajazoea kwani siku zote yeye ndio anakuaga wakwanza kufika. Tukaingia ofisini tukazima taa sehemu ya mapokezi ili akiwa kwa nje ajue hakuna mtu. halafu tukamwambia mlizi arudishie tu mlango asifunge na funguo, na geti arudishie bila kuweka kufuli ili akifika tu ashtuke na akasirike (just to annoy him) kuwa waliacha mlango na geti wazi jana jioni. Sasa alipofika mlangoni anakuta ipo wazi akasema ooh! Tumesha ibiwa hapa, hasira zikamshika kuwa geti halikufungwa jana jioni. Halafu mdogo wetu aitwaye Guka ndio tulimuacha nje awe ana mmonita (monitoring him) kwa kutupa taharifa kwa simu kuwa ameshafika kwa parking lot. 😅😅 Na Guka alikuwa anawasiliana na dereva kusema wapo wapi. 😅😅 Tazama video hapo chini 👇🏿😅😅
Basi, alipopita tu mapokezi kuingia eneo la secretary wote tukasema “surprise” kwa nguvu na furaha huku mmoja wetu alikuwa kwenye switch ya kwashia taa, tukaanza kuimba “happy birthday to you” 😅😅😍 alishangaaje, hasira zote zikaisha hapo hapo. 😅😅😅😅 Hakuamini kuwa watu waliweza kuwahi kazini mapema hivyo ilitu wam-surprise! Alishukuru sana na furaha nyingi mno.
unaweza itazama video yote ya surprise kwa kupitia YouTube yangu hapo chini 👇🏿
Baba na mwana 😍
Kwakweli ni furaha kufanya jambo ambalo linamfanya mtu mwingine kuwa na furaha na kujisikia vizuri kwa kujiona mwenye thamani, lakini nifuraha zaidi kufanya jambo linalowafurahisha wazazi wako. Nafurahia na najisikia vizuri pale ninapoweza kuwafanya wazazi wangu wafurahi zaidi. Ni mbaraka wa pekee. 😍😍 Counting my blessings ma’am! 😅😍
Chumba cha dada Alpha
Na story zitaendelea maana mama Igogo alikuwa haamini alichokiona. 😍😍
Surprise ya mwisho iliharibika 😅😅 tulitaka dada yetu naye am-surprise mama lakini dakika za mwisho akaamua kumwambia kua anakuja halafu hata hakutuambia kuwa kamwambia mama hivyo ikawa surprise kwetu. 😅😅🙈🙈 kwakweli hii ni the best moment for 2022.
Cecy-mama mzazi
Miaka takriban 3 iliyopita dada yangu naye alim-surprise mama big time. Alikuwa mjamzito na wakati uchungu umeanza akampigia mama kumsalimia basi wakaagana vizuri. Ndani ya masaa 2 mume wake anampigia mama simu kuwa mama Dani amejifungua mtoto wa kike na wameamua kumrithisha jina la mama. Mama akawa hataki kuamini anasema mbona mama Dani nimeongea naye muda sio mrefu? 🤣🤣🤣 akaambiwa pale anakupigia alikuwa ameshikwa na uchungu na tulikua njia kwenda hospitali. 😅😅 Na mtoto mwenyewe ndo huyo hapo 👆🏿 juu. 🤩🤩
Two digits counting has officially begun! Happy 10th birthday twin babysister! Wishing you a marvelous year and many more to come. Happy birthday mdogo wa mimi. 😘❤️
sisterhood!.😍😍
Mimi mwenyewe na pacha wangu nyumbani Kibada. 😍😍
Pachaa kama pacha! Kwaraha zetu ndani ya Serena hotel, Dar es salaam.
Mwaka 2021 niliufunga vyema na kuufungua 2022 vizuri sana. Namshukuru Mungu kwani umekua mwaka mwema sana wenye mibaraka mingi. Changamoto katika maisha hazikosekani kwani hatuwezi kujua tu imara kiasi gani kama hatutapitishwa katika changamoto hizo.
Daughter
Wanasema dhahabu au madini yoyote ya thamani hayapatikani juu ya barabara wala kando kando ya maji! Nilazima yachimbwe chini ya ardhi na yapitishwe kwenye moto mkali ndipo yawe haya madini tunayofurahia kuyaona. Hivyo, sikuzote tukipata changamoto tusikimbilie kusema “kwanini mimi?” Bali tumwambie Mungu najua hili ni darasa unanipitisha japo somo bado sijalielewa, naomba unipe HEKIMA ya kuweza kulielewa somo hili ili nifuzu mafunzo yangu vyema. Najua maumivu ninayopitia nikwaajili ya utukufu wako na mimi ndiye uliyenichagua kuwa kielelezo cha utukufu wako.
Basi kwa kusema hayo, naomba niweke kumbukunbu ya matukio yaliyozunguka maisha yangu mwaka huu wa 2022. Tukumbushane kushukuru katika kila jambo. Sikuzote tuhesabu mibaraka yetu kwani ni mingi mno sema tunafunikwa na upofu kwa kuangalia maisha ya watu wengine na kudhani kuwa wamebarikiwa kutuzidi. Hapana! Mungu anatubari sote kwa jinsi impendavyo yeye kwa wakati wake.
Hizi ni baadhi ya picha tulipiga mwanzoni mwa Dec 2021 tulikuwa maeneo ya tunako ishi karibu na NASA Space Center, Houston, Texas
Baadhi ya picha tulizopiga kwenye Christmas party 20021 iliyofanyika Hilton hotel, Houston, Texas.
2021 THC Thanksgiving GalaApril 2nd 2022
Mwenyezi Mungu alitubariki tukafurahia kuona mwanangu ameongeza mwaka mwingine. Ilikuwa siku ya Jumosi tarehe mbili mwezi wa Nne! Na zifuatazo ni baadhi ya picha ya siku hiyo.
Hello wapendwa wasomaji wangu, poleni kwa kutokua nanyi toka mwaka 2022 uanze. Nitarejea muda si mrefu, kuna plugins ambazo zinatakiwa ziwe updated lakini kila nikijaribu zinaleta shida kwa blog. Hivyo WordPress na Godady wanashughulikia. Yani hata hapa nafanya majaribio.
Asanteni sana kwa uvumilivu,mbarikiwe sana.
“Ilianza kwa ajali ya kugongwa na pikipiki, ukavunjika mfupa wa nyonga, hospitalini ulikimbizwa kupata huduma, ukiwa umenyamaza kimya bila kujitambua, siku tatu baadaye uliizinduka na kuwatambua wanao, hata kwenye simu ukaongea na Otieno, kuimarika kwako iliwaruhusu madaktari kukusudia ufanyiwe upasuaji, wa kuunganisha palipovunjika, ukiwa na uhai wako wakakuchoma nusu kaputi, nayo ikazua balaa la kupoteza fahamu hadi jioni hii umetutoka Mama yetu ANNA NYOLWENGO, dada yako Rhoda alitangulia, ukabakia nasi ukooni, leo umetutoweka kwa utashi wa Mola TUNASHUKURU ????????” …… Sir O.O Igogo
Marehemu ni mdogo wake na bibi yangu mzaa baba! Pia mimi nilipewa jina la mama yao mzazi yani bibi yake baba mzaa mama! Jina langu hilo ni ARUA japo baba yangu huwa analiandika ARWA! ?? Marehemu bibi yangu mzaa baba wao asiliyao ni Kenya, ambapo ndipo na mdogo wake alipokuwa akiishi mpaka maiti ilipo mfika.
Hii wheelchair alinunuliwa wiki iliyopita wakiwa na tegemeo kuwa angetoka hospital salama baada ya kufanyiwa upasuaji. Wao walipanga kama wanadamu lakini mapenzi ya Mungu yametimuzwa! …… Poleni wanandugu na ukoo wote wa Nyolwengo. May our beloved grandmother Anna Rest In Eternal Peace! ????
“And said, “Naked came I out of my mother’s womb, and naked shall I return thither. The Lord gave, and the Lord hath taken away; blessed be the name of the Lord.” ………. Job 1:21
Mama Igogo akitazama kwa furaha picha iliyochorwa kwa taswira yake.
Wanao onekana kwenye video hapo juu ni baadhi ya wafanyakazi wa Temeke SDA Nursery and Primary School walifika nyumbani kwa mama Igogo mchana wa jana tarehe 09/27/2021, masaa ya Africa Mashariki, kwaajili ya kutoa shukrani zao za dhati kwa mchango wake wa hali na mali ambao aliutoa toka kuwaza yakwamba kanisa la Temeke SDA linahitaji kuwa na shule, kuisimamia kuanzishwa kwakwe toka elimu ya awali ya chekechea (Nursery school) mpaka kufikia kuwa na darasa la kwanza mpaka la saba.
Kuhakikisha kuna kuwa na boarding (hostel) kwa wanafunzi wanao kaa mbali haswa wanafunzi wa jinsia ya kike! Mama Igogo alikuwa full time Mkurugenzi mkuu (Director) ambaye hakuwai kulipwa mshahara hata mara moja kwa miaka 7! Alifanya kazi ya kujitolea kwa asilimia 100%! Na baada ya miaka 7 aliomba “kung’atuka” na kuwaachia vijana waikimbize. Yeye alibakia kuwa mshauri kwenye bodi ya shule. Mungu ni mwema shule ilisimama na inaendelea vizuri! Mwanangu ni mmoja wa wanafunzi wa mwanzo kabisa wa shule hii! Alianzia Nursery hadi darasa la sita. Mungu azidi wabariki wote walimu, wanafunzi, pamoja na watu wote wanaojitoa kwaajili ya huduma hii muhimu sana kwa jamii. ????
Kwenye video ya pili ni Mama Igogo akitoa shukrani zake za dhati baada ya kupokea shukrani na zawadi ya picha kutoka kwa wafanyakazi wa Temeke SDA Nursery and Primary School.
Na hapa, mama Igogo akitoa ufafanuzi wa zawadi ya picha iliyochorwa kutoka kwenye moja ya picha zake ambazo alipiga akiwa kwenye Makao Makuu ya Wasabato ulimwenguni yaliopo Silver Springs, Maryland/ Washington DC eneo la kumbukumbu za Ellen G. White (mmoja wa waasisi wa dhehebu la Wasabato). Mama yangu hajatembea dunia nzima, Mungu ni mwema amembariki kutembelea nchi kadhaa hapa dunia na ameona mengi; lakini safari ya kutembelea kijiji cha history ya Wasabato huko Battle Creek, Michigan na safari ya kutembelea Makao makuu ya Wasabato ulimwenguni kwakweli ni moja ya safari ambazo zimemgusa sana moyo wake na siku zote huwa anaziongelea kwa hisia sana! Namshukuru Mungu kuwa amenichagua mimi binti yake kuwa kiungo kikuu cha mbaraka huo. Si kwamba asingeweza kufika Marekani hapana! Naamini Mungu kama alimpangia kufika angefika tu bila ya mimi kuwepo kama hizo nchi zingine alizo tembelea bila mimi kuwepo! Lakini kufika sehemu kama hizo kwa urahisi na kwa furaha kupitia mwanae naamini nikitu kinampa faraja kubwa sana moyoni! ?? No mama ain’t done yet! Mungu atupe uhai utakula more good time very soon! ?????
Mzee O.O Igogo, Magreth Otieno Igogo, na mama Igogo
Hapa juu ni moja ya picha waliyopiga wakati walikuwa wamekwenda kutembelea kijiji cha historia ya Wasabato huko Battle Creek, Michigan mwaka 2014 mwezi wa 11. Picha A siku hii zipo nyingi lakini zipo kwenye Flashdisk, sijapata muda wa kuziangalia.
Siku ya leo tarehe 08/16/2021 majira ya mchana masaa ya Africa Mashariki, mwanangu katimiza moja ya shahuku yake kubwa au nawezasema moja ya ndoto yake!
Amekutana na mmoja wa madaktari walio nihudumia na kuhakikisha anaingia katika dunia hii akiwa salama! ?? Marehemu Dr Amood alikuwa ndio my primary Dr lakini alinikabidhi kwa Dr. Kapesa na Dr Kaisi kama mbadala wake pindi yeye anapokuwa na majukumu mengine. Siku ya kujifungua Dr Kaisi ndio aliyekuwepo zamu, Dr Amood aliitwa na alipofika Mercy alikuwa teyari kazaliwa! ??
Mungu azidi wabariki wote Dr Kapesa na Dr Kaisi! Bahatimbaya Dr Kaisi alipatwa na stroke (kiharusi) hivyo kwasasa amepumzika kufanya kazi za utabibu aliyosomea.
BTW, nilikuwa natibiwa Tanzania Maternity Service ambapo madaktari hawa wote walikuwa business partners!