2016 ULIKUWA NI MWAKA MGUMU SANA ULIOKUWA NA MABADILIKO YA GHAFLA YA JPM by Peter Sarungi

Ni desturi yangu kutathmini mwaka unapofikia mwisho. Nianze kwa kuimba wimbo wangu kwa Tanzania.

“Tanzania eeee, Nakupenda sana x2”

“Hata kama nikilala porini lakini ni ndani ya Tanzania bado nitajivunia”

“Najua wengi wanakutamani ingawa uchaguzi wako bado upo mashakani”

“Nakuaga mwaka kwa maumivu ingawa ni maumivu ya mpito”

“Naamini sasa ni muda wa kula matunda ndani ya mwaka unao anza”

Kwa kifupi mwaka 2016 ulikuwa ni mwaka mchungu na mgumu kwa watanzania masikini na wanyonge wasio jua leo yao itakwishaje na kesho itaanzaje baada ya kuletewa utaratibu wa kufanya kazi kabla ya kula ingawa kazi zenyewe hazipatikani na zingine zinezuiwa kupisha uchunguzi wa HEWA.

Ni mwaka uliokuwa mgumu kwa watumishi wa umma baada ya kulazimishwa mabadiliko makubwa ya utumishi wa serikali na hasa baada ya kuziba mianya mikubwa ya ubadhilifu wa pesa za umma pamoja na kuziba hadi vitundu vidogo vya posho kwaajili ua motisha ya watumishi.

Ni mwaka mgumu kwa wana siasa feki walio ingia kwenye siasa kwa maslahi ya kutajirika. kuna wabunge na madiwani walio tumia nguvu nyingi kupata uongozi, kwa sasa wanajuta ni kwanini walichagua siasa na wengine wana lia hadharani bila kuficha. Lakini pia ni Mwaka mgumu sana kwa wapenda mabadiliko, wana harakati na wapenda demokrasia baada ya kusitishwa kwa shuguli zao za siasa za majukwaa na harakati zingine kama maandamano.

Ni mwaka mgumu sana kwa uchumi wa taifa na wananchi hasa baada ya kutanda kwa UKATA wa hali ya juu sana. imefika mahala ambapo heshima ya ndoa imerejea, heshima ya mshahara imerejea, heshima ya mlo imerejea na hata heshima ya kazi imerejea. Ukuaji wa Uchumi wa nchi kwa mwaka huu nimeufananisha kuwa na kasi  kama ya konokono dhidi ya farasi. Naamini imekuwa hivyo kwa sababu JPM ametumia mwaka huu kuweka misingi sawa, tuangalie mwaka 2017

Umekuwa ni mwaka wa Matamko mbalimbali machungu kwa wanchi katika sekta mbalimbali. Tumepata matamko mengi ya wakuu wa mikoa mbalimbali hasa Dar, matamko ya wakuu katika Mfumo wa Elimu, Afya, Ardhi, Kodi, Usafirishaji, kilimo, Ufugaji, bomoa bomoa, Madini, Umeme na maeneo mengine yaliyo acha alama ya maumivu kwa wananchi.

Tumeshuhudia hadithi za mfalme Juha na simuzili za kusadikika kutoka kwa Polepole, Ben sa8, Yericko nyerere, Faru John, Magoiga, Menuka, Malisa na wengine wengi waliokuwa mstari wa mbele kutupigia hadithi nzuri kwa kila upande kwa mwaka mzima.

Ulikuwa ni mwaka mchungu sana kwa watumishi wa umma zaidi ya 300 walio tumbuliwa mwaka huu kutokana sababu mbalimbali kupitia kauli mbiu ya KUTUMBUA inayoongozwa na mkuu wa kaya akisaidiwa na wasaidizi wake kila idara.

Ulikuwa ni mwaka mchungu sana kwa wafanya biashara za utalii, mahoteli, mabasi, nguo, bar, ujenzi, usafirishaji wa mizigo, wamachinga, madalali, vyuo na mashule, biashara za mitaji na biashara za Bank. Maana tumeshuhudia taatifa za kufilisika kwa baadhi ya biashara hizo kwa sababu ya mdororo wa uchumi. Tusife moyo, mwaka ulikuwa ni wa mapito.  

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

#MyTake

Mwaka umekwisha na changamoto zake, ikiwa mwaka unao anza utakuwa na changamoto hizi basi tujue ni sisi wenyewe tutakuwa tumezitengeneza. Huu ulikuwa ni mwaka wa majaribio ya mabadiliko makubwa, naamini tutajipanga sasa kukubali na kukabiliana na magumu yanayotokana na Mabadiliko haya kutoka kwa Mkuu wa Kaya…….Mwaka 2017 ukiwa mchungu tena kwako basi jua ni kati ya wewe au serikali kuna mmoja atakuwa ni mzembe wa mabadiliko.

Leave a Reply