Tulikutana na mke wangu Sayuni kwenye harusi ya mdogo wangu Linda iliyofanyika Dar miaka saba iliyopita. Sayuni alikuwa mmoja wa wasimamizi kwenye harusi ya Linda na walisoma darasa moja Chuo Kikuu cha Mlimani Dar. Tuliendelea kuwasiliana niliporudi Columbus na mwaka uliofuata alihamia Columbus..Tulikuwa katika urafiki kwa muda wa karibu miaka miwili na uhusiano wetu ulizidi kuimarika na kufikia makubaliano ya kuoana. Tulipendana na kukubaliana kufunga ndoa Septemba 2012 hapa Columbus. Ni mambo mengi yalinivutia kwake na kunifanya nizidi kumpenda na hasa busara zake na ushirikiano wake katika mambo mbalimbali ya maisha. Baada ya kukubaliana kuoana, tulianza maandalizi ya harusi. Tulipata ushirikiano mkubwa wa marafiki na ndugu mbalimbali hapa Columbus na nje ya Columbus. Tulifanya vikao vya maandalizi na tunamshukuru Mungu tulipata ushirikiano mkubwa na mzuri kutoka kwa kamati ya maandalizi. Kama nilivyosema hapo juu, busara za Sayuni na ushirikiano zilizidi kunivutia. Kila nilipokuwa napata changamoto za kazini au za kimaisha na kumshirikisha alikuwa akinishauri vizuri na kufikia hatua ya kuaminiana zaidi. Na mpaka sasa ni mshauri wangu mkubwa na ninathamini hekima na busara zake. Vilevile Sayuni ni mtu asiye kata tamaa katika kutimiza malengo aliyoyapanga au malengo tuliyokubaliana kuyatimiza.
Nimezaliwa na kukulia katika familia ya kikristo. Moja ya imani niliyokuwa nayo ni kumcha na kumwamini Mungu. Ninaamini kwamba ndoa ni baraka na pia agizo la Mungu hasa inapofika muda wa kuanzisha familia. Katika sala zangu ilikuwa ni pamoja na kumwomba Mungu anifunulie na kunionyesha mke mwenye busara, hekima, mcha Mungu na tutakayeelewana. Hivyo kabla hatujaoana na Sayuni, niliona hizi sifa nilizokuwa nikiziweka kwenye sala zangu. Katika ndoa, sio wakati wote ni wa raha. Kuna wakati ambao tunatofautiana katika maamuzi. Kutofautiana ni jambo la kawaida. Kwa mtazamo wangu, kutofautiana katika maamuzi/mitazamo ndio kunakamilisha mapungufu ya kila mmoja wetu. Hivyo, ni vema kila mmoja akaheshimu tofauti za mwenzake hata kama hakubaliani nazo. Hii inachangia kuendelea kujenga uhusiano imara na kila mmoja kuwa wazi kwa mwenzake badala ya kuogopana. Communication is the key thing to us. Pia learning to compromise/meet each other half way inatusaidia kuimarisha umoja wetu.
Mimi ni kaka mkubwa katika familia yetu, ninapenda kuona wadogo zangu hasa wa kike waliopo kwenye ndoa wana amani na furaha na ndoa zao. Ushauri wangu kwa vijana wanaotaka kuoa, ndoa ni baraka. Kila ndoa ina changamoto zake. Kabla ya kufikia hatua ya ndoa, omba Mungu akuongoze katika kumpata mke mtakayeelewana na kupendana.
Wapendwa wasomaji wangu, niliwaahidi kuwa sita waangusha! Hii ndio 2018 Hottest And Best Couple Of The Year. Nakumbuka katika busara za marehemu Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere siku moja alikua akitoa busara juu ya kuchagua viongozi wa Taifa la Tanzania alisihi Watanzania kuwa mchague kiongozi ambaye hata wakimtizama machoni utajua huyu anasema kweli tunaimani naye! Basi hivyo ndivyo nami nilivyo itizama hii couple haswa nimemtizama kwa kina sana kaka yangu Jackson Lyimo nikaona moyo wangu unaimani naye, na hata macho yake yananipa imani kuwa siyo tu kaka bora bali pia ni mume mwema! Heshima yake kwa wanawake ni kubwa sana, matendo yake yanajidhihirisha hilo! Hivyo pasipo shaka naomba nitamke rasmi kuwa hii couple ndio chaguo langu kwa mwaka huu.
Nawaombea ndoa njema sana, iliyojaa baraka nyingi mno na amani tele. Wabarikiwe wao na uzao wa tumbo lao pamoja na wageni wote waingiao ndani ya malango yao!. Congratulations to Mr and Mrs Lyimo and happy Valentine's Day. I love you guys so much ??