Kutana na Sophia Makoyo

2016-01-21 21.16.32Kwajina naitwa Sophia Daudi Makoyo, naishi Shirati wilaya ya Rorya.  Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM). Nasomea shahada ya kwanza ya sheria  (barchelor of laws). Sababu iliyonisukuma mpaka nikaamu kusomea sheria ni swala zima la haki za wanawake na watoto! Nataka kutetea haki za wanawake pamoja na watoto generally nataka kutetea human rights. Natamania sana siku moja nijiunge na Tanzania Women Lawyers Association (TAWLA) iliniweze kutimiza ndoto zangu. 2016-01-21 21.15.21
 Kuhusu maisha ya chuo; maisha ya chuo yana changamoto especially kwa watoto wa kike hasa pale wanapokosa mkopo wanajikuta wanajihusisha na matendo maovu kama uhuni uliyopitiliza ili waweze kumudu gharama za maisha. Nimtihani mkubwa sana!
Unaelewaje dhana nzima ya mafanikio / success?………Kimtazamo wangu mimi kuhusu mtu kuwa successful; ni hali ya kuwa na mafanikio hasa pale unapofikia malengo yako. Kwamfano mimi naweza sema nipo successfully kwa kiasi fulani kwasababu half of the dreams na goals nilizo kuwa ni me set-up nimefikia. Nili dream kufika form six, kufika chuo kikuuu na kusomea law na nimefanikiwa though sijamaliza B.A yangu but I am almost done! FB_IMG_1453432262183
Katika maisha yangu naumizwa na vitu vingi lakini maisha ya kuwa yatima yanaumiza sana sana hasa pale unapohitaji support ya mzazi wako na unakosa. Unakuwa unajihisi mpweke sana wakati wote, namiss sana mapenzi ya mama yangu, ushauri, na  hasa kudeka deka. Japo nashukuru Mungu sijapata kuona watu waki ni treat vibaya kwasababu ya uyatima wangu. Namimi sijatumia uyatima wangu kama njia yakutenda maovu, au kukwepa adhabu yoyote ile. Siku zote natumia status ya uyatima wangu kwenye maswala ya shule tuu, hasa pale ninapoomba mikopo kutoka bodi ya elimu ya mikopo ya juu HELSB. 
FB_IMG_1453432212379
Unafikiria uyatima inaweza kuwa kikwazo cha mtu kutimiza ndoto zake?………….Mimi naamini kuwa yatima hakutanizuiya kufikia ndoto zangu kwani nakuwa inspired sana na ndugu zangu waliofanikiwa through hard work bila misaada ya wazazi. Japo lazima nikubali changamoto ni nyingi sana, kuu zaidi ni ukosefu wa pesa. Kitu kikubwa kinachonipa furaha moyoni ni kuona kuwa kuna watu nyuma yangu wana nisapoti na wako very proud of me hasa baba yangu Daudi Makoyo kwasababu wanafurahishwa na jitihada zangu. They are very happy to have me. Marehemu mama yangu alinifunza kuwa mtiifu, mvumilivu, mnyenyekevu, na kujifunza kusema neno Samahani / Nisamehe pale ninapokosea. Hivyo naamini hayo mafunzo yake ndiyo yamenifikisha hapa nilipo na naamini yatanifikisha mbali zaidi katika maisha yangu. 
Mwisho, katika maswala ya uhusiano japo siku hizi watu wengi wanaangalia “majina ya familia” lakini sidhani kama kuwa yatima itakuwa kikwazo cha mtu kumpata ukupendaye kwa dhati kwani mtu kuwa yatima si kwakupenda kwake bali ni mipango ya Mungu. Labda cha muhimu niwasihi wasibweteke. Wajitume wajifunze kujitegemea sio kuwa tegemezi kwa wanaume manake success does not come in a silver plate you have to go and get it! FB_IMG_1453432192175

8 thoughts on “Kutana na Sophia Makoyo”

  1. Hongera kwa kujitambua ndg yangu maisha Ni kujituma na kua makini hakuna Kinachoshindikana hapa duniani ukiwa na dhamira ya kweli cha muhimu mtangulize mungu. Kukosa mzazi moja Ni changamoto za maisha kwani mungu ndie anaepanga maisha yetu .wengine tuna historia ndefu Sana iliojaa changamoto nyingi ikiwepo kuwapoteza both parents sikukata tamaa Bali nilisema Mimi Nimebaki na majukumu mengi na makubwa Sana hivo mpaka Leo maisha yanaendelea .sophy maisha ndo kwanza unataka kuyaanza be strong enough my dia otherwise karibu buturi but naishi musoma na kwa Leo nipo safarini from Dar nitapita Ddma mchana mungu akubariki Sana katika your dreams Amin

  2. mungu akubariki. .japo mdogo wangu swaumu kashtuka kwa maamuzi yako kutoka bio had sheria. lakin huenda ni mjumbe wa mungu kaza kwenye msaada tutakusaidia. dogo huwa napenda watu wenye muono kama wako sababu ujitazam wewe unatazama wajane na watoto wadhurumiwa bila kujari hali zao kiuchum. hupo tayari hata kufa ili mradi haki itendeke poa. ntakuja dom na lovely sis swaum kukupa mkono au kukusaport mara ntakaporud tz. usiku mwema.

  3. Sawa umesikika mpendwa asante don’t stop to do that but mmh also me niyatima nimesoma kwa tabu cjabahatika kufikia malengo lkn now nipo nje ya Africa kitu ambacho namshukuru sana Mungu kufeli darasani sio kufeli maisha nimekupenda bureeee Mungu elibariki girl.

Leave a Reply