NAAMKA HIVI –Ukiniuliza tatizo KUU sio serikali kuingilia biashara bali ni biashara kuingilia serikali na siasa kwa ujumla kwa takribani miaka 20 sasa.
Hapa tulipofika ni zao la siasa kutumikia wafanyabiashara wachache wenye nia ya kulinda maslai binafsi hata kwa kuigarimu serikali na taifa letu.
Hatuwezi rekebisha hii hali bila kupitia mkondo huo huo uliotufikisha hapa. Naamini hapa ndio tutaona tofauti ya siasa za kusaka dola na utawala baada ya kuikamata dola.
Tukisha chagua viongozi tunategemea waunde serikali na kutawala/kudhibiti nchi sio kupiga siasa tu siku ziende tu bila suluhisho.
Tukubaliane ‘kibongo bongo’ hakuna anaeTAKA mabadiliko ya kweli pamoja na kuyaHITAJI. Kwa wengi ‘mabadiliko’ ni kauli mbiu tu. Ukiwa kiongozi Tz lazima uwe mnafiki aka roho mbaya au kauzu aka roho ngumu.
Siasa mwisho chalinze, HAPA KAZI TU! ?