Our humble beggings!

2016-03-27 13.16.40Sikutegemea kuweka hapa hii picha siku ya leo. Lakini nimeona moyo wangu umenisukuma kuweka basi ngoja nifanye kile kitu roho napenda! Hii picha tulipigia tukiwa kijijini Utegi, Rorya, Mara mwaka 1987. Tulienda kusherekea siku kuu ya Christmas. Katika hii picha kuna watu wawili ambao hawapo nasi tena.

(1) aliyevaa sandals nyeupe. Yeye alikuwa mama yangu mkubwa mke wa marehemu baba yangu mkubwa mzee alijulikana kama Mama January

(2) Shangazi yangu kipenzi cha roho yangu. Theresia Obuoro Igogo. Ambaye amekaa karibu na mimi. Alikuwa msichana mmoja tu kwenye tumbo la bibi yangu mzaa baba. Yeye ndo mwanangu amepewa jina lake (Theresia a.k.a Teddy) in honoring of her. Ipo siku nitamuongelea kwa kirefu zaidi kwani yeye ndio chanzo cha mibaraka yote ambayo watu wanaiyona katika familia yetu!!

Wengine ni:- mama yangu mzazi? 

2016-04-10 12.13.10

dada yangu ambaye ninamfuata ? 2016-04-10 12.16.06mdogo wangu anaye nifuata kwa mara ya pili 2016-04-10 12.11.32 na mimi mwenyewe ? ??? what a massive #ThrowBackSunday..! 2016-04-10 09.41.02Hilo “banda” la udongo kwa upande wa kushoto lilikuwa ndiyo jiko la marehemu bibi yetu nyakati hizo (baadaye alijengewa lingine). Na kwa upande wa kulia ilikuwa ni sehemu wanalala mbuzi.

Everyone starts from somewhere! Hakuna kitu kinacho onekana hapa duniani ambacho hakina mwanzo wake au chanzo chake! #TheRoots Na huwa nikikumbuka tulipo toka then unakuta mtu anataka kuingilia mambo ya familia usizozijua chanzo chake!! I swear, naweza toa mtu ng’eo ya macho! Kama wewe hukuwepo nasi nyakati hizi then keep your nose where it belongs!!

Nilimtumia mdogo wangu na baba yangu hii picha. Wakashangaa sana. Mdogo wangu alikuwa hajawahi kuona hii picha vile vile maisha yao walivyo kuwa ni tofauti na sisi tulivyo kuwa wadogo. Hivyo hana kumbukumbu ya maisha haya ya hali ya chini. Hapo kwenye picha alikuwa na miaka mitatu  (3yrs). Basi hivi ndivyo alivyo sema ? 2016-04-10 09.46.05

 Na baba yangu yeye nilimtumia muda kidogo na hivi ndivyo alivyo sema ?  (Samahani kwa some typos) Screenshot_2016-04-10-13-10-38-1Anyway! That’s our humble beggings. I’m glad nime share nanyi kidogo ?

Leave a Reply