Kuna msemo unaosema”ukitaka kuwa Tajiri fanya vile vitu Matajiri wanafanya Eg, tembelea sehemu wanazotembelea, Vaa wanavyo Vaa na kula/kunywa wanakokunywa ” Inawezekana ukafanya hivyo ukaweza kupata connection ukawa Tajiri But myself I would suggest Otherwise……….Ukitaka kufanikiwa /kuwa Tajiri jiulize Waliofanikiwa na kutajirika WALIFANYA NINI HUKO NYUMA, hadi wakachomoka na leo tunawaona wana Pesa,wanaenda popote watakapo, wanavaa chochote wapendacho,wanajenga mansions/castles ,wanasomesha watoto Shule za ‘bei ghali’ or Abroad na kuwa na Power/Heshima ktk jamii ? Uki-copy wanachofanya sasa hivi myfriend utafilisika ?, wakienda kunywa Level 8,Cape Town fish market, karambezi, double tree, High spirit nk na wewe utaweza? au utaomba kwenda Toilet Bill ikija mezani? Wakienda shopping USA,UK,Dubai or SA Utaweza au utasumbua watu uletewe zawadi? Wakivaa Rolex utanunua fake au?
Hii ni hata makampuni,kuzikopi kampuni kubwa zenye uzalishaji mkubwa na kutengeneza pesa nyingi ktk uendeshaji wa kampuni yako yenye 2/3yrs ni risk! Wao wako computerised kila mahali na wana uwezo wa kuwa na sophisticated office systems &softwares! Kampuni ndogo huwezi anza leo na hapo hapo hapo ukaajiri na kuweka departments wakati Huna kipato cha kuwalipa staffs ,kulipa Utilities bills leave alone kulipa kodi ya pango .
So Kama ni kampuni inaanza jiulize KAMPUNI KUBWA ILIYOFANIKIWA LEO NA UNGETAMANI UFIKE HAPO JE UKO NYUMA WALIFANYA NINI KUWEZA KUVUKA VIKWAZO NA KUFIKIA WALIPO Then jipange kuyafanyia kazi kwa vitendo yale utakayojifunza.
Na hata vyeo makazini ni hivyo hivyo jiulize your CEO Alifanyaje kufika alipofika then angalia ni nini ufanye kwa mwaka huu 2016 kusogea hatua 1,2,3,4 …kufikia nafasi hiyo ya juu.
Wish you all the best!
God Bless you ?
Till then,
Haika Lawere
Mbezi Garden Hotel.