Are you an absentee parent?

2015-04-22 21.13.43Je wewe ni yule mtu anaitwa mzazi kwasababu ulizaa tu lakini hutekelezi majukumu yako kama mzazi?! Unapenda kuitwa mama / baba lakini hujui wala hutaki kutimiza majukumu ya hizo title? basi huyo mtoto ☝ anaongea na wewe kwakuwa mtoto wako analia hapo nyumbani na haumsikilizi!

Wazazi wengi (bila kujali kizazi kipi) nafikiri wanaona watoto kama ‘midoli’ fulani hivi au property!  Wako busy na marafiki na mambo mengine yasiyo na maana bila kufikiria je mtoto wangu anapata upendo wa dhati kutoka kwangu? Je, mtoto wangu anajua nampenda unconditionally na siku zote yeye kwanza wengine baadaye? Je una weka muda maalum kwa ajili ya wanao / mwanao?

Watoto si ‘midoli’ bali ni viumbe vyenye  uhai na utashi ambao wanatakiwa kufunzwa maadili, kupewa elimu bora ya duniani na ya kiroho. Chakushangaza wazazi wengi wa kizazi hichi wana concentrate na vitu kama mavazi na nywele  na kuacha mambo ya msingi ambayo yataisaidia mtoto kukuwa kiakili na kiroho. Napia itamfanya awe raia mwema katika jamii inayo mzunguka na hata popote pale atakapo ishi hapa duniani. Sijasema mtoto avalishwe maronya ronya, hapana! Lakini pia jali mambo mengine ya msingi.bonnie-religious-fathers-dayMsiache wafanyakazi wa ndani ndio wakawalelea watoto kwani wanaweza wafundisha mambo ambayo yataharibu future ya mtoto / watoto wako na hakuna wakulaumiwa bali wewe mwemyewe mzazi! Kumbuka watoto hujifunza kwa kuangalia wazazi wao wanafanya nini na siyo wanasema nini! Kama wewe mzazi unawaambia wanao wasiibe wakati wewe mwenyewe ni mwizi wa mali za umma basi kumbuka watoto wako nao watakuwa hivyo hivyo! Ukipanda mahindi utavuna mahindi! Hata kama utamwagilia maji usiku na mchana usitegemee kuvuna mahindi wakati ulipanda michongoma!

Wazazi wengi siku hizi wameamua  co-parent na technology! #SMH yani watoto ulelewa na mitandao! Wapo ndani ya nyumba kama “misekule”! Wanaonekana kwenye bills  na vyeti vya watoto zao lakini si kwenye maisha ya watoto! Instead of taking their children to school they rather send them to school! Umeshawahi ona wale wazazi ambao wanalipa ada ya shule lakini hajui mwanae anafundishwa nini?  Wazazi ambao wako busy ku entertain marafiki na ndugu baki lakini hawezi ku entertain au ku socialize na watoto wao! Inasikitisha sana kwani hao hao wanakuwa wakwanza ku criticise watoto pale wanapo kwenda kinyume na matakwa yao!

Hizi tabia ni za kuridhi! Kama umekuwa makini kuangalia kwa kina hawa wazazi ambao ni absentee parent wa kizazi  cha sasa nafikiri utakubaliana na mimi kuwa hicho ndicho walicho jifunza toka kwa wazazi wao. Kwahiyo wao kwakusudia au bila kukusudia wanarudia makosa yale yale ambao wazazi wao wamefanya. It needs an outsider  to  give them a wake up call! Mabadiliko yana anza na wewe, usikubali kuwa sehemu ya hii laana! Fanya mabadiliko sasa!

Leave a Reply