ARUSHA ACHENI SIASA NA UTAWALA WA KIHUNI~~~Peter Sarungi

Nimeshawahi kuandika kuwa kuna tofauti katika kushabikia club za mpira na vyama vya siasa. Siasa inagusa maisha ya kila siku ya mwanadamu, ukiingiza ushabiki usio kuwa na tija kama wa club za mpira katika siasa ni wazi utakuwa una cheza na maisha ya watu na inawezekana uka angamiza ndoto za wananchi. Kilichotokea katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha afya ya mama na mtoto jijini Arusha ni dhairi kuwa bado tuna safari ndefu sana ya kutoa elimu ya kujitambua sio kwa wananchi pekee bali hadi kwa viongozi tunao wachagua na wale wanao teuliwa na mamlaka za juu. Haya matukio ndio yanayo akisi ukweli wa kauli ya Donald Trump aliposema “Afrika bado inahitaji kutawaliwa kwa mda mrefu zaidi” akimaanisha bado viongozi wetu tunao wachagua ili kutuongoza na kututawala hawajitambui, hawana weledi na utashi mzuri wa siasa na utawala, wana ubinafsi na sifa zilizopitiliza, hawajui kutofautisha siasa na harakati, wengi wana akili na tabia za kitoto katika kufanya maamuzi, wengi wana angukia kwenye utafiti wa Twaweza hasa kundi la Vichaa, wengi wana ongoza na kutawala kwa kutumia propaganda chafu kwa maslai yao na ya vyama vyao. Ukweli ni kwamba tunao pata Hasara ni sisi wananchi tunao kaa pembeni kusubiria utashi wa wana siasa kama hawa. fb_img_1476910893576Huu ni UHUNI wa kulaani bila kupepesa macho, haiwezekani tukakubali kupata aibu tena aibu inayotokana na Ufinyu wa Busara kutoka kwa viongozi wetu tunao waamini watuongoze, Uhuni unaoletwa kwa maslahi binafsi ya watu wawili, Uhuni unaoletwa na Akili ndogo ambazo hazipaswi kupewa dhamana, Uhuni wa kutengeneza kwa makusudi kabisa wa kutaka sifa bila kujali athari za akina mama na watoto, Uhuni wa mwisho kabisa kuvumilika.

Mrisho Gambo (RC) na Godbles Lema (MP) hamtutendei haki hata kidogo na kamwe siwezi kusapoti UHUNI huu, yaani jambo dogo linawafanya mnakosa busara mbele ya wageni tena wafadhili walio kubali kuweka mabilioni ya pesa kwaajili ya kutatua matatizo ya wananchi wenu, sasa umuhimu wa nyinyi kuwa viongozi wakati hamtaki maendeleo ni upi? Mnataka sifa kwa kutumia Propaganda ili iweje? Hopeless kabisa na vizuri mkajichunguza akili zenu kupitia Twaweza.

Matokeo ya Tukio hili……..

1. Tukio linaonesha kutokuwepo kwa uhusiano kati ya Mbunge na Mkuu wa Mkoa, hii inamaanisha maendeleo ya jiji la Arusha yapo njia panda.

2. Mbunge hana busara za uongozi hasa baada ya kuhamaki kwa jazba mbele ya wageni.

3. Mbunge hana nidhamu kwa mkuu wa mkoa na hajali itifaki /protocal na hivyo kuzidisha mgororo kati yao.

4. RC hana busara za utawala hasa baasa ya kudharau na kubeza jitiada za Mbunge katika project husika.

5. RC yupo kwa malengo tofauti na mendeleo ya wananchi anao waongoza na anatumia uongozi wake kufanikisha hayo malengo yake.

6. Wafadhili watamini maneno ya Trump na watakuwa wamefadhaishwa sana na kitendo hicho.

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

#Mytake.
1. Ni kweli tunahitaji viongozi wabunifu, wachapakazi na wanao tafuta maendeleo kama G.Lema lakini ni kweli pia kwamba hatuhitaji viongozi wasio na nidhamu na wasioweza kulinda maendeleo waliyo yatafuta kama G.Lema. Acha jazba za kihuni katika ku handle issues za maendeleo. Mchezo huu hautaki Hasira kaka..

2. Mrisho Gambo, usitafute sifa zinazo kuzidi uwezo. Kasi ya JPM ni ya kupongeza yetote yule anaye leta maendeleo katika nchi anayo iongoza. Usiwe kikwazo katika hili na wala usitake sifa ya kuwa RC anaye ponda kila kitu cha upinzani, hao wapinzani nao wamepewa dhamana ya kuongoza Arusha tena na wanachi. Usipo badilika basi unafaa kutumbuliwa na JPM.

Asanteni sana

BAADHI YA MAONI: screenshot_2016-10-19-16-00-35-1 screenshot_2016-10-19-16-00-42-1

 

Leave a Reply