Awii! Sister sister! Mabinti wa mzee Mwita Gachuma all the way from Alcott, Maryland. Warembo toka Ukuryani hao ? wamependeza sanaaaaaa. Mbarikiwe sana wapendwa.
All posts by Alpha Igogo
Family time-the Mashimis
Wapendwa wasomaji wangu, naomba mnisamehe leo nilikuwa nimebanwa hivyo sikuweza weka picha za family asubuhi kama ilivyo kawaida yetu. Si unajua kila JumaPili tunafurahia familia. Basi pichani ni familia ya Evans Mashimis toka ATL! Wamependeza sana. Sijui kama nilishawahi kutowa utambulisho humu ndani. Mke wa Evans a.k.a Teddy Sakaya ni shangazi yake mwanangu Mercy. Yeye ni last born kwa familia ya baba yake. Pia ni my childhood friend. Tumekulia mtaa mmoja. Mbarikiwe sana wapendwa.
Happy 18th birthday Nathad Mwambeli!
Happy 18th birthday Nathad! May you be happy, healthy, and many more joyful years. The goodness of being an adult is that you have the responsibility to spread your love to many others! May you touch someone’s life in doing so. Happy 18th birthday Nathad. We all love you!
Linda Bezuidenhout machoni pangu mimi!
Wapendwa wasomaji wangu. Niliahidi wiki hii nitamzungumzia mwanamitindo wetu maarufu anayetamba katika anga za kimataifa Ms Linda Bezuidenhout. Napia nini msimamo wangu juu ya kile kinacho onekana kama maugomvi katika social media! Naomba kwanza muelewa kuwa mambo ya campaign yameisha, sasa tunarudi katika maisha yetu yakawaida. Wakati wa campaign mimi na Linda tulikuwa tumesimama pande mbili tofauti. Linda yeye ni mwanachama mwaminifu wa Chadema a.k.a UKAWA hivyo alikuwa anam-support Mr. Edward Lowassa kama mgombea urais kwa upande huo. Mimi nilikuwa na msupport Dr. John Pombe Magufuli kama mgombea urais. Lakini pamoja na kutofautiana kwetu hatujuwahi kutupiana maneno ya kashfa wala matusi. Wote tulipigia “debe” wagombea wetu huku tukiendelea kuheshimiana! Hivyo sina sababu yoyote ya mimi kutokuendelea kumpa support Linda kwa kazi zake anazo zifanya kwani nikitu ambacho nilikuwa nafanya siku zote! Kunawatu walishawahi kutoa comment ya kuniuliza mbona kwenye interview zangu nilizofanya na Linda sijagusia ‘maugomvi’ ya Linda kwenye social media? Sikuwahi kujibu chochote lakini leo naomba nijibu kwa mara ya kwanza na ya mwisho!Siwezi kukataa kuwa hayo maugomvi hayapo kwani mie unafiki siuwezi! Ndio, maugomvi yapo lakini “mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!” Kama nilivyo sema hapo mwanzo kuwa haya maugomvi yapo kwenye social media. Nakama tukiwa wakweli na waungwana basi tutakubali kuwa hata huko kwenye social media hayakufati kwenye profile / account yako! Ni vitu ambavyo lazima uvitafute wewe mwenye! Kwamfano mimi mwanzoni nilikuwa sijawahi yaona mpaka juzi juzi tuu nilipofungua IG account na kuamua kuyatafuta kwani niliona watu wakimtaja jina lake mahala fulani. Lakini kiukweli kama nisingeangaika kuyatafuta huko inamaana nisingeyaona! Hivyo mimi siwezi kujiingiza kwenye mambo au maugomvi nisiyo yajua mwanzo wake wala mwisho wake! Nimejaribu kutafakari sana na kujiweka katika nafasi ya Linda nikajiuliza je ningekuwa mimi ningefanyaje?! Jibu langu ni SIJUI! Kwani kila mtu ana react tofauti na kila mtu anakiwango chake cha uvumilivu! Hivyo who am I to judge anybody! Na haswa ukizingatia kuwa sijui nini kiini cha maugomvi yao! Pia ukizingatia kuwa hivi ni vitu ambavyo mtu mwenye uwamue kuvitafuta ndipo utakutana navyo lakini ukiamua kutokufuata hizo account / profile ukweli hutokaa ujuwe kuwa kuna ugomvi wowote! Labda niseme watu wa kulaumiwa ni nyie mnaofuata hayo maugomvi huko na kwakutumia account zenu zenye majina fake mnatukana na kuchochea maugomvi ambayo ukiulizwa unajua chanzo chake au yanakuhusu vipi hutokaa uwe na jibu!! Nyinyi wenye account fake ndio wa kulaumiwa na kulaaniwa vikali sana. Naomba Mungu awalipe kulingana na mnavyo stahili!! Labda niwaelezee kidogo jinsi Linda alivyo macho pangu mimi Alpha Igogo! Linda ni mtu mmoja muungwana sana, mkarimu, ana roho nzuri mno, mcheshi na mwenye upendo mwingi sana! Narudia kusema “mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!” basi niacheni nimpe Linda haki yake kwani anastahili! Jamani jinsi mnavyo muona Linda alivyo mzuri wa sura na maumbile basi ndivyo alivyo na roho yake! ni watu wachache sanaaaaaa tena sanaaaaaa ambao wamebarikiwa kupata vyote kama Linda, yani uzuri wa sura na roho! Linda mnayemuona pamoja na familia yake walinikaribisha kwao na kuniudumia kana kwamba mimi ni mtoto wa mfalme fulani! Mimi na hii familia tulikuwa hatujuani wala hatujawahi kuongea hata siku moja. Walipewa utambulisho wangu na kaka yangu Dj Luke wa Vijimambo blog lakini walivyo nipokea na kunihudumia utafikiri mtu ambaye wamenijua miaka nenda rudi. Tena hapa Marekani ambapo watu wengi hawapendi kukaribisha watu kwenye nyumba zao?! Lakini Linda na familia yake ikanikaribisha kwa moyo mkunjufu na kunifanya nijione kama sehemu ya familia yao! Halafu eti mimi leo watu mnataka nigeuze shingo yangu nakuitenga hii familia kisa na mkasa eti maugomvi ya kwenye social media ambayo siyajui mwanzo wala mwisho wake!! Tena maugomvi yenyewe mpaka uyatafute huko?! Jamani, si hata Mungu ataniadhibu! Hivi mnajua ni jinsi gani inavyo uma unapo mkaribisha mtu kwako kwa moyo mweupe kabisa, mtu ambaye ulikuwa hata humjui, ukaacha kazi zako, ukachukua muda wako kumpikia, na kumu-entertain, na pia kuwapeleka kwenye hotel nzuri ya gharama kula nao dinner halafu kesho yake unamuona ameungana na watu ambao umetofautiana nao kisa kakasirishwa na reaction yako?! Unajua huo ni unyama na moja ya ukatili wa hali ya juu?! Au kwasababu watu wengi si wakarimu ndio maana mnadiriki kuniuliza mimi nasimama wapi katika hili?! Don’t get me wrong, sishabikii hata siku moja maugomvi yanayo endelea kwenye social media za wabongo! Nalaani vikali mno! Lakini hivyo haviwezi kuniondolea utu wangu wakuthamini uungwana na ukarimu walionao hii familia! Nitakuwa mtu mbaya sana kama nitanyanyua mdomo wangu na kusema vibaya hii familia au kuungana na watu walio gombana nao kwasababu ya ushabiki tuu! Mimi sio NYUMBU! NAKATAA SITOFANYA HIVYO HATA MARA MOJA! Hivyo naamini mtaniacha mimi kama Alpha Igogo nisimame kama Alpha Igogo. Niendelee kuwa huru kuisupport na kupenda hii familia bila kipingamizi chochote! Naomba msiniuhusishe na kitu au ugomvi wowote hule ambao haunihusu! Sishabikii ugomvi wowote lakini napenda kusimamia ukweli. Na ukweli ni kwamba Linda wala familia yake hawajawai kunikosea wala kunivunjia heshima, hivyo sitaki kuchuma dhambi na kujipa laana kwa vitu visivyo nihusu! Linda dada yangu, Mungu amekupa mume anaye kupenda kwa moyo wote. Naomba umuonee huruma huyu baba. Najua uliumia sana, lakini imetosha sasa, mpe mmeo heshima anayo stahili! Naomba dada yangu uachane na hayo maugomvi. Umepewa karama ya upendo ambayo wengi hawana lakini umefanya watu wameshindwa kuona karama yako ya ukarimu na upendo kwasababu ya haya maugomvi. Nyinyi nyote mnaogombana ni watu wazima wenye familia zenu hivyo siwezi sema mengi kwani nyinyi wenyewe ndio mnamaamuzi ya mwisho ya nini kifanyike! Mimi nasema kama Alpha lakini muamuzi ni Linda mwenyewe na maamuzi yako nitayaheshimu sikuzote! Nafikiri ni wakati muafaka sasa wakuona si tuu Wamerekani wakivaa nguo zako bali watu walio au wanao heshimika katika taifa letu la Tanzania kama mama Janeth Magufuli au kwakuwa wewe ni shabiki wa Chadema basi watu kama mama Regina Lowassa waanze kuvaa nguo zako kwani unastahili na unamapenzi sana na Tanzania. Lakini ninahuwakika kama utaendekeza haya maugomvi itakuwa ni ngumu sana kwao kukupa support yao. Kumbuka si kila mtu amepata nafasi ya kukujua kama mimi Alpha Igogo nilivyo kujua! Na si wote utakaowapa au uliowapa nafasi ya kukujua wanauwezo wa kusimamia ukweli! Watu walio wengi wanajali “reputation” zao katika macho ya watu, bila kujua character zao ndizo zitakazo simama siku ya siku! Hivyo ni nadra sana kukuta watu wakasimama na wewe kwani wanahofia kuharibu reputation zao. Natuamaini nimejieleza vya kutosha, wenye kunielewa watakuwa wamenielewa. Naambao hawatanielewa basi naomba tukubaliane kuto kukubaliana. Kila mmoja abaki na msimamo wake, muhimu tuheshimiane. Linda na familia yako, naomba nirudie kusema asante sana kwa ukarimu wenu Mungu azidi kuwalinda na kuwapa maisha marefu yenye amani, furaha, upendo, na afya njema. Asante.
Hot shot of the day
Hongera kwa baba yangu!
Hakuna hatua ambayo unaweza kupiga halafu ukasema hiyo hatua ni ndogo hivyo haistahili kujipongeza au kupongezwa, kwani hakuna mtu alianza kusimama na kutembea bila kutambaa angalau kwa siku kadhaa! Japo najua baba yangu kuna mambo mengi na makubwa amefanya na amepongezwa sana si tu ndani ya Tanzania bali hata inchi za ugenini, lakini kama nilivyo wahi kusema huko nyuma moja ya nia kuu ya hii blog ni ku inspire watu kwa kutumia mifano halisi (real life experience / stories) ili iwasaidie kwa njia moja ama nyingine kutokukata tamaa na kuona kuwa hakuna lisilowezekana! Basi kwa maana hiyo naomba nitumie mwanya huu kumpongeza baba yangu. Hongera kwa kuteuliwa kwake kuwa Makamu Mwenyekiti wa World Green Design Organization upande wa Tanzania. Hii sasa ni kwa mara ya pili kwa nonprofit organizations kubwa duniani kumteuwa kuwakilisha Tanzania. Zaidi ya miaka 17 iliyopita chama cha walipa kodi duniani (World Tax Payers Association) kilimteuwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Tanzania ambapo mpaka leo hii bado ni mwanachama wao na ni mmoja wa Board of Directors wa chama hicho.
Hongera sana Sir. Otty, sky’s the limit!
#TBT# Tabu akapata “tabu”!
Wapendwa wasomaji, wiki iliyopita niliwaletea mahojiano maalum kutoka kwa dada Zawadi Kakoschke. Katika mahojiahano hayo moja ya maswali ambayo nili muuliza ni kama kuna huusiano kati ya majina ambayo wazazi wanawapa watoto wao na mafanikio au tabia ya watoto hao. Sehemu ya mahojiano hayo yalikuwa kama ifuatavyo:- Wewe binasfi unaamini majina ambayo wazazi wana wapa watoto wao yanachangia katika mafanikio yao kiuchumi, kielimu, na tabia zingine? Kwa mfano majina kama Amani anaweza akawa mtu wa kupenda amani siku zote, au majina kama Tabu, Sikujua yanaweza yaka changia mototo kuwa na matatizo katika maisha yake? Majina yanachangia sana katika maisha ya watoto wetu. Ndio maana mimi nilijitahidi sana kukaa na kufikiria majina ya kuwapa watoto wangu. Nimekua naamini hili kwa miaka mingi sana kuwa majina yana nguvu sana katika kujenga au kubomoa maisha ya muhusika. Huwa nashukuru sana kwa wazazi wangu kuamua kunipa jina la Zawadi nina imani kubwa hili jina limenisaidia kwa namna moja ua nyingine.
Kwakweli majibu ya dada Zawadi yalinikumbusha binamu yangu mmoja aitwaye Tabu Obago ☝ikabidi ni wasiliane naye na kumuomba nifanye mahojiano naye mafupi haswa kutaka kujua kama jina lake limekuwa nuru kwakwe au la! Na hivi ndivyo ilivyo……Tabu naomba utuelezee, je jina la Tabu libekuwa “tabu” kweli au nuru kwako, tupe historia yako kwanza? Mimi ni dada niliye zaliwa kutoka katika mkowa wa Mara, lakini kwa sasa makazi yangu yapo katika kitongoji cha Mbagala. Mimi ni mama wa watoto wawili Jack na Julieth. Mmh! Tabu, kama jina lenyewe linavyotamkwa au maana halisi ya ili jina hakika limeambatana na mimi katika maisha yangu yote. Nimekuwa na taabu nyingi sana kama mjomba Otieno Igogo alivyo kuwa akipenda kusema mara kwa mara “Tabu, unatabu kama jina lako.” Kuhusu kuzaliwa kwangu mimi ni mtoto wa pekee kwa mama yangu, marehemu Rosebela Olung’a Igogo. Kusema ukweli swala hili la kuwa mototo pekee kwa mama yangu huko nyuma lilikuwa linanisononesha hasa nilipowaona wenzangu na ndugu zao wa kuzaliwa tumbo moja. Lakini nilipopata watoto wangu nahisi wameziba hiyo hali ya upweke na sasa nina furaha na amani moyoni mwamgu. Japo katika maisha yangu nime ambatana na matukio ya kusitisha, lakini kwa kweli siwezi na wala sitamani kufuta kitu chochote kwenye historia yangu. Historia (past) ni historia iwe mbaya au nzuri ndo inaleta “leo” ya mtu. Labda niseme hivi, kwa upande wangu kitu ambacho najutia sana ambacho ningependa kufuta (edit) kwenye historia yangu ni maisha yangu ya shule. Kwani NAJUTA SANA TENA SANA nilivyochezea pesa za mama yangu shuleni na kupoteza muda. Leo hii jinsi ninavyo angaika kuwasomesha binti zangu ndo nahisi uchungu aliokuwa anaupata mama yangu. Tabu, Wewe si tuu yatima bali pia ni mjane; niwapi huwa unapata nguvu ya kuendelea na maisha bila kukata tama? Ni kweli mimi ni yatima na pia mjane tena mara mbili namaanisha kwa ndoa mbili!! Kinachonipa nguvu na msukumo wa kuendesha maisha yangu bila kukata tamaa ni wanangu Jack na Julieth. Natamani sana kurekebisha nilipo haribu japo ni ngumu mno. Lakini ugumu wa maisha na changamoto nilizopitia zimekuwa shule iliyonipa elimu kubwa sana. Nikitu gani unajivunia sana? Najivunia kusimama imara katika maisha na hasa kuamua kuishi katika Leo yangu na siyo kujutia ya nyuma. Naweza kusema mpaka hapa nimeweza kujiweka sawa kama siyo ku(edit) lifestyle yangu. Una ujumbe kwa watu wote watakao soma hii story yako? (1) Kwa watoto zangu hakuna jipya chini ya jua. Mkipelekwa shule someni sana. (2) Kwa wenzangu namaanisha wa umri wangu (42) msikate tamaa unaweza ukiamua iwe (3) Kwa yatima na wajane wenzangu naomba niwausie ujane siyo ulemavu wala huyatima siyo kufungwa tujifunze kusimama wenyewe na Mungu anakusaidia. Mwisho, haijalishi uko chini au una udhaifu gani muujiza pia hipo ila naamini mpaka uitafute siyo ikutafute.
Asante sana Tabu Obago. Nakutakia mafanikio mema na makubwa zaidi ya hayo.
Ref: Mahojiano haya yamefanywa na Alpha Igogo
Kutoka Facebook
Happy 15th wedding anniversary to my dearest brother!
Happy 15th wedding anniversary to my dear brother Vetto and my lovely sister in-law Anna. May the love of God be with you. His peace dwell in your house forever.
His power protects you and your whole family every single day. May happiness be your companion and your days together be good and long upon the earth and may Hebless the work of your hands. You have come a long way and I am sure mom and dad are very proud of you two! Happy 15th wedding anniversary! I love you deep!!
Happy 9th of Dec to you all!
Japo najua ni kesho lakini naomba nichukuwe nafasi hii kuwatakia kheri ya siku ya kuzaliwa Tanganyika! Muwe na siku nje, mkajitokeze kwa wingi na nguvu katika maeneo yenu husika mkalisafishe jiji / kijiji / katakana mnazo ishi. Kumbukeni kuliombea taifa letu, Rais, na viongozi wetu wote. Happy Independence Day to you all the sons and daughters of Nyerere! Mbarikiwe sana ?
Hot shot of the day
Motherhood!
Wow! Wamependezaje jamani? Dada yangu kipenzi Esther Kachare na wanawe. Wazurije sasa! Na furahia sana kuona watu ambao tunafahamiana toka utoto, tumependa na kuishi kama ndugu, na bado mpaka leo hii tunapendana na kuthaminiana bila kinyongo! Mwe, sijui niseme ??? familia ya mzee Kachare inamkono wa baraka katika maendeleo ya familia ya mzee Otty Igogo ?? undugu ni kufaana sio kufanana! Mbarikiwe sanaaaaaa ndugu zangu! ???
Joke of the day!
Usikate tamaa!
watu tunapitia maisha tofauti inategemea na chimbuko la kila mmoja wetu alipotokea yani background yako. Wapo watu ambao wamezaliwa na kukuta kila kitu kipo. Yani mazingira mazuri anayoishi na anauwezo wa kupata maitihitaji ya ziada. Kuna wanao zaliwa na kukutana maisha ya yakawaida, yani si mazuri sana na wala si mabaya. Wanauwezo wa kupata mahitaji muhimu lakini huwezo wa kupata vya ziada hawana. Na wapo wale ambao wamezaliwa katika dhiki na shida nyingi. Yani hata kupata mlolongo wa siku ni tabu. Hivyo wanajikuta wanatumia nguvu za ziada siyo tu kutimiza ndoto zao bali kujikwamua kutoka katika hali duni ya maisha na kupata maisha ya kawaida. Chamuhimu katika yeto ni kuto kukata tamaa. Mungu ndiye mtowaji wa yote naye amesema, ‘watu wangu hawatokuwa mkia’ hivyo ‘ukigangamara’ na kumuweka yeye mbele basi ipo siku utavuka vikwazo! Jana usiku niliweka hii picha kwenye Facebook yangu na kuuliza swali “je ulishawahi kuishi kwenye nyumba ya kupanga ndani ya bongoland? Experience yako ilikuwaje?” Basi baadhi ya watu watoa maoni yao kama ifiatavyo ?
Kwakweli mtu ukishapitia mambo fulani magumu au vikwazo ukavivuka salama mara nyingi huwa ukikaa chini na kutafakari unakuwa ni kichekesho au kitu cha kukufanya ucheke! Ninachoweza kusema ni kwamba; umasikini si kilema. Wenye lugha zao wanasema “it is just a condition” na kitu chochote ambayo ni conditional inamaana inaweza change anytime! Haidumu! Hivyo usikate tamamaa wala kusikiliza watu waliopungukiwa na hekima!
Kutoka Facebook
Leo kutoka Facebook nimependa sana hii picha ya classmate wangu henzi za Nurulyakini Secondary school. Yeye anaitwa Shahan Nyamasagara na huyo ndio “barafu” wa moyo wake ? pendeza sana met ake na mimi. Wewe nakuaminia kuwa wifi yangu yupo kwenye mikono salama kabisaaaa! ? Mungu azidi ilinda ndoa yenu, upendo, amani, furaha, vikadumu ndani yenu. Mbarikiwe sana wapendwa
Father and daughter moment
A word of wisdom!
Happy 3rd birthday my darling sister!
I can hardly believe it has been 3 years! It was Dec 7th, 2012 when such a beautiful, gorgeous, bright eyed baby girl said hello to us and the whole family welcomed her with joyfully and thankful heart! Just like your name, Blessing; you have been nothing but a truly great blessing to all of us and I couldn’t be luckier to call you my babysister! Happy 3rd birthday cutest, gorgeous. Sweetest, charming, smart, and darling babysister of mine! May Almighty God be with you in every step of the way and shower you with aboundantly blessings! Well, gotta tell you this; as your big-sister it is my every right to let you be babysister! it’s your every duty to do exactly what babysister normally do (driving your big-sister crazy ???)! And I will love you even more ???hahaha! When you are in America better act like Americans right?! ? Spending time with you is always a pleasure, summer 2014 was one of the best summer ever! can’t wait to see you in 2016!May your day be filled with joy, love, and happiness! Happy 3rd birthday my darling babysister. Live long to conquer the whole world! I ❤ You!
#TBS# Linda Bezuidenhout (LB)
Leo nimeamua ku Throwback video za interview ambazo nilifanya na mwanamitindo wa kimataifa Ms. Linda Bezuidenhout mnamo mwezi wa pili mwaka huu 2015!
https://youtu.be/7tmJgxbmB1A
Hapo juu ? nisehemu ya kwanza ya mahojiano. Na hapa chini ? nisehemu ya pili au ya mwisho ya mahojiano yetu. Haya yalikuwa ni mahojiano yangu ya kwanza kabisa kufanya huku nikirekodiwa. Nilipewa hii nafasi ghafla, yani nilijua nataka kufanya mahojiano na Linda lakini sikujua lini yatafanyika. Mara ilikuwa siku ya juma Tatu napigiwa simu na kaka yangu Dj Luke wa Vijimambo blog nakuambiwa kuwa Linda ametukaribisha kwake siku ya Juma Mosi na yupo teyari kufanya mahojiano nami! Nilisita, lakini kaka yangu akasema nitaweza nisiogope! Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa. Kama hujawahi yaona basi nakuomba uyatazame na niruhusa kutoa maoni yako!
https://youtu.be/rELfTBwva9g
Wiki hii inayo anza kesho, Mungu akijalia nitaelezea mambo fulani kuhusu Linda, na nini msimamo wangu mimi kama Alpha Igogo kuhusu mambo au maugomvi ambayo Linda anahusika nayo kwenye mitandao. Najua kuna baadhi yenu mnataka kujua mimi nasimama wapi kwani mlishawahi kuniuliza. Basi tuombeane uzima. Mbarikiwe wote!