All posts by Alpha Igogo

Hongera Dr. Tulia Ackson (Naibu Spika)

PIX2-1Hongera sana Dr. Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge 11 la serikali ya 5 ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwakweli binafsi nilitamani sana wewe ndiwe uwe Spika wa Bunge hili, lakini naona uzowefu umewekwa mbele bila kujali uwadilifu! Serikali ya Tanzania inakataza watu wasijichukulie sheria mkononi lakini serikali hiyo hiyo kupitia watu hao hao wanatunga sheria tunaona wanamtunuku mtu aliyekosa maadili ya uwongozi kuwa Spika wa Bunge! Kiongozi ambaye anajichukulia sheria mkononi?! Sijui wanafundisha nini taifa hili! SMH!

Anyway, it is what it is life goes on! Hongera sana na kila la kheri katika utumishi wako wa umma!

Kutoka Facebook

FB_IMG_1447958577684Nimependa sana hizi picha za da Eddah Gachuma toka DMV! Hapa alikuwa amekwenda kumuangalia mwanae akicheza mpira. Kijana wake anavaa  number 88 ndo maana unaona naye kavaa hiyo number! FB_IMG_1447958571009As I said to you da Eddah usinisahau kwenye ule mgao wa paycheck ?? mbarikiwe sana wapendwa, Mungu amlinde, na amuongoze afike mbali zaidi ya hapo. Amen! 

Nawe pia unalalaga na make-up usoni?

Screenshot_2015-11-17-14-33-13-1Madam Rita juzi kati aliweka hii picha na kuweka maneno haya “good night”! Licha ya kupenda picha na mazingira ya kitanda chake lakini nikajikuta najiuliza hili swali, “inamaana madam Rita analala akiwa amepaka make-up usoni, au ni mapozi ya picha tuu?”

Hii ilinikumbusha mmoja ya wadada ambao nilisoma nao secondary. Yeye alituambia kuwa hawezi lala bila kupaka wanja na kuakikisha anaonekana mrembo kwani anaogopa kama ikatokea amelala usingizi wa mauti basi alale akiwa amependeza! ?? je nawewe ni mmoja ya watu wanao lala na poda usoni? Basi ngoja nikujuze, wataalamu wanasema upakaji wa poda wakati wa kulala si mzuri kwani unafanya ngozi yako izeeke haraka. Pia kupaka poda kila wakati napo si nzuri kwa ngozi yako. Ndo maana unaona hawa ma-celebrity wengi wanaishia kufanya ‘medical skin enhancement’ kwani ngozi zao zinajikunja na kuzeeka haraka kuliko umri wao.

Jalibu kupaka make-up pale inapobidi siyo kila wakati. Jiamini na ujikubali jinsi ulivyo that’s the best make-up any woman can wear. Nothing like self confidence! Mbarikiwe!

Hongera Mh. Kassim Majaliwa Kassim (PM)

IMG-20151119-WA0000Hongera sana Mh. Kassim Majaliwa Kassim kwa kuteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya tano. Japo wengi hatujawahi hata kukusaidia lakini ushuhuda wa watu walio wengi haswa wabunge wenzako inaonyesha wewe ni chaguo sahihi kwa inchi yetu haswa kwa wakati huu! Nakutakia kila la kheri katika uwongozi wako.

Nampongeza sana Rais Dr. Magufuli uteuzi huu kwani ameweza kuonyesha kuwa yeye analeta CCM ile ya baba wa taifa!  CCM ambayo hakuwa na makini wala viongozi ambao wanadhani wana Hati miliki ya inchi! Naona yale majina ya wanasiasa ambao walifanya cheo / madaraka ni mali ya familia au ukoo sasa yataanza kupoteza. Hongera sana Rais kwa ushujaa wako wa kuvunja nguvu zao pamoja na makundi ambayo yanaigawa Tanzania!

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Africa na watu wake.

#TBT

FB_IMG_1447950191658-1Me, Myself, and I……….Fall 2010 on my way home after spending a day in Michigan Adventure with my daughter and her friends ……….mwanamke khanga haswa ukiwa na kiuno cha kufungia ???

Hot shot of the day

FB_IMG_1447787668544-1Rosemary Jairo kutoka Bongoland! Wow! Kapendezajeee?! Gorgeous! Love it!

Peter Sarungi atoa shukrani zake za dhati!

HITIMISHO LA HATUA ZA KUELEKEA KUWA SPIKA WA BUNGE: KURA HAZIKUTOSHA. FB_IMG_1447783174533Ndugu jamaa marafiki na wadau wangu wote na popote walipo, nitoe shukrani zangu za dhati kwa sappoti yenu toka nilivyoanza hatua ya kwenda kuwa spika wa bunge. Ki ukweli nimefarijika sana na mapenzi yenu makubwa kwangu na kunichangia kwa hali na mali pamoja na ushauri mliokuwa mkinipa na kunifariji. Nilikwenda kushindana lakini pia nilikwenda kuzindua hatua zangu nyingi za mbele katika siasa. Nashukuru malengo yangu yamefanikiwa kwa 90% na huu ni ushindi kwangu kwa kuweza kufanikisha sauti yangu ya siasa kusikika kwa nchi nzima na kwa watawala wa nchi kwa mara ya kwanza. Niwashukuru sana Chama changu cha AFP kwa kunipa fursa pasipokujali hali yangu ya ulemavu, niwatie moyo kwamba mmefanya maamuzi sahihi kwa jamii ya walemavu na Mungu awabariki sana. Pia nimshukuru mama yangu mzazi kwa kunilea katika ujasiri huu mkubwa ulioweza kunifikisha hapa. Nichukue fursa hii kusema kwamba; nimeanzisha rasmi safari yangu ya kisiasa Tanzania. Hivyo mtarajie mengi ya kujenga jamii ya watanzania kutoka kwangu. Nawashukuru sana na Mungu awabariki zaidi ya jana. Amen… Share, Like, Comment na Tag kusambaza ujumbe huu ili kuwatia moyo watu wa makundi maalum wanaotamani kusikilizwa sauti yao. FB_IMG_1447783206038

Kutoka Faceebook

Screenshot_2015-11-12-12-59-29-1-1Leo nimependa hizi picha kutoka kwa mdogo wangu. Nimependa mpangilio wa rangi, na jinsi nguo zilivyo mkaa. Kapendeza sana ? Screenshot_2015-11-13-15-33-44-1-1such a beatful and lovely smile! Love it ?

Mother and daughter moment

FB_IMG_1447787537691-1Mama na binti yake wamependeza sana! Bernadeta na mwanae anaitwa Brighet mmh! Not sure kama nimepatia spelling but nafikiri nipo sahihi ? mbarikiwe wapendwa!

Charlie Sheen HIV+ confession!

sheenLeo asubuhi muigizaji wa muda mrefu Charlie Sheen ametangazia dunia kuwa yeye ni muathirika wa HIV kwa muda wa miaka minne sasa. Alisema hayo wakati wa mahojiano maalum kati yake na Matt Lauer wa Today’s show katika channel ya NBC.

Wapendwa wasomaji, mkiona mtu ana fanya mambo ambayo ni tofauti kabisa na mlivyo mzowea; embu jaribu kumchunguza kwa karibu au tafuta nia ya kuwa naye karibu ili ujuwe nini haswa kinacho msibu. Watu wengi hufanya vitu ambavyo vitawatowa katika uwalisia watatizo walilonalo haswa likiwa nikitu ambacho hawana uwezo wa kuki control. Utakuta mtu anaingia kwenye ulevi ulio pindukia, au uwongo usio na mbele wa nyuma, au anakuwa mtu wa starehe 24/7 na kupoteza focus ya maisha, au anaingia kwenye madawa ya kulevya, au ghafla anaingia kwenye ulokole usio elezeka (haijalishi wa thehebu gani), au anakua muislamu yule wa siasa kali (udini ulio pitiliza), au anafanya mambo ya ajabu ajabu yasio eleweka wala elezeka, au anajenga chuki na mtu pasipo sababu yoyote hata kama huyo mtu anamaisha duni kuliko yeye, au anakonda kupita kiasi kwa madai ya “diet”, au anakuwa na uncontrollable waight gain, na mambo mengine kama hayo. Tusiwe wepesi wa kucheka na kuhukumu watu bila kujua ukweli wa jambo. Wengi huwa wana go through stuff and they don’t what to share with people for the fair of being judged or because they have trust issues!

Kwanini nimesema hayo? Kwa miaka kadhaa sasa dunia immeshudia jinsi Charlie Sheen alivyo ingia kwenye ulevi usio elezeka, drug use, na tabia nyingine nyingi zisizo elezeka. Watu waka m-judge na kusema maneno yote mabovu juu yake bila kujua ukweli kuwa anamatatizo ambayo yame  mu-affect psychologically (ni baada ya kujua ana HIV+)! Basi wapendwa muwe na roho ya kiubinadamu japo najua ‘vidudu watu’ pua wapo humu duniani, lakini inawezekani tukawa wakarimu kwa wengine!

Manhood! “Smart Luo Man”!

FB_IMG_1447692190148-1Hahahahah! Nimependa hayo maneno ya kwenye Tshirt “Smart Luo Man”! Huyu kama humfahamu ni mdogo yake na mimi. Yani huyu ndo alikuwa kitenda mimba kwenye familia yetu. Mara Blessing huyo akaja ?? sasa Blessing ndio mdogo wetu wa mwisho, I guess ?? FB_IMG_1447692237389-1Yeye ni Dr.  wa mifugo na hapo I guess alikuwa kazini maana naona kama mabanda ya mifugo kwa nyuma.

Hot shot of the day

FB_IMG_1447690203344Gorgeous pic of former Miss Tanzania-UK! Very hot indeed!

Mother and son moment

FB_IMG_1447599544425-1Mama akifurahiya kijana wake kurudi nyumbani baada ya kumaliza elimu ya Secondary  (Form 4).  Hongera sana mama kwa kulea, na pongezi nyingi kwa kijana kwa kukazania elimu. Mbarikiwe wote!

Kutoka Facebook

FB_IMG_1447689474051-1-1Ninependa sana hii picha ya my beautiful mtani. Kapendeza sana ??

Weka ubinadamu mbele ewe Mtanzania!

Kwa masikitiko makubwa naomba niseme yangu ya moyoni. Kwakweli inasikitisha sana kuona baadhi ya watu situu wamekosa kustaharabika bali pia wamepungukiwa na ubinadamu kiasi cha kuhuzunisha sana. Hivi jamani kwanini hatuwezi kuheshimu watu haswa katika maswala ya “privacy”? Kwanini tunawavunjia watu heshima hata pale ambapo hawawezi kujitetea au kuzungumza nasi kueleza hisia zao? Imekuwa nitabia ya Watanzania kuweka picha za watu ambao wamefikwa na mauti kwenye mitandao bila kujali ni jinsi gani familia zao, ndugu, na marafiki watajisikiaje watakapo ziona hizo picha.

Matukio kama haya tumeyaona mengi lakini leo naomba niongelee hili la Mtanzania mwenzetu marehemu Alphonce Mawazo. Ambaye alikuwa mwanachama wa Chadema huko Geita kama sijakosea. Watu wameweka picha zake ambazo zinaonyesha jjnsi alivyo uliwa bila hata kuficha sehemu ya sura yake? Huko wapi ubinadamu wetu enyi taifa la Nyerere!! Ni technology ni ndiyo imetufanya tukose ubinadamu kiasi hichi?! Hivi mnajua kuwa hao marehemu wana ndugu zao? Wana watoto na wake /waume zao ambao wasingependa kuona ndugu zao wana dhalilishwa kiasi hichi?! 2015-11-15 09.18.18Mfano mmoja wapo ni jinsi Joyce Kiria alivyo weka picha za marehemu kwenye IG  bila hata huruma wala woga wowote hajaficha wala kuomba radhi watu kwa kuweka hizo picha. Nasio posti moja, hapana! Katika posti zote mbili zenye picha tofauti wala hajali kuwa kitendo hicho si kizuri kabisa! (Picha hizo za juu ni mimi ndio nimefunika sura ya marehemu Alphonce Mawazo, lakini Joyce Kiria kaweka kama zilivyo pigwa huko eneo la tukio). 

Saa nyingine unakuta mtu kaweka picha ya mtu ambaye yupo kwenye geneza bila hata kuficha sura ya marehemu!! Au mtu mgonjwa hospitali bila kupata idhini yake! Kwamfano, juzi tumeona tukio la Rais kutembelea hospital ya Muhimbili. Ndio ni jambo jema, lakini nani aliwapa vibaya vya kuknyesha sura za wagonjwa kwenye media? Kwanini hawakufunika sura zao? Je mnajua mnakiuka haki za msingi za wagonjwa? Mnafikiri familia zao zilijisiaje kuona ndugu zao walio taabani sura zao zikisambazwa kwenye mitandao na Tv? Je unafikiri yule mgonjwa pale siku akiona zile video atajisikiaje? Au kwasababu uwezo wao wa kifedha ni mdogo ndio maana hakuna anayejitambua na kujali haki zao? Wengine ndiyo utakuta wanatumia picha za marehemu kutasaka umaharufu na “kiki” za social media!! Jamani!! SMHH!!

Watanzania wenzangu embu weka ubinadamu mbele kabla ya yote. Mambo kama haya ndio maana wenzetu huwa wanatoka kadri za watu wanaopaswa kuhudhuria ibada za maisha ya ndugu zao au hata kusema nani anaweza kutembelea hospitali pale anapokuwa anaumwa. Hizi tabia za kishetani na zakinyama inabidi tuziache wapendwa!Badilika! FB_IMG_1447608434427

Pumzika kwa amani ndugu Alphonce Mawazo. Ulichofanyiwa ni unyama wa hali ya juu. Walaaniwe wote walio shiriki katika kifo chako. Natumaini sheria utafuata na hatua kali zitachukuliwa! R.I.P!

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Africa na watu wake.

Juma’a Kareem!

FB_IMG_1447015482950-1Nawatakieni Ijumaa njema kwani wote. Wale wanaokwenda swala ya Ijumaa basi muwe na swala njema mtukumbuke na sisi katika dua zenu. Wale wanao jiandaa na Sabato nawatakieni maandalizi mema na muwe na Sabato njema. Walipo makazi, shuleni, n.k muwe na siku njema. Wagonjwa na wenye shida mbali mbali Mwenyezi Mungu awaponye na kuwajalia kulingana na mapenzi yake. Muwe na weekend njema wapendwa. ?

#FBF

FB_IMG_1447342148487-1#FBF Me, Myself, and I back in 1992…………..cheka uwongeze siku za kuishi ?? nafikiri tabia ya kuweka family pictures ukutani nime irithi toka kwetu. I still do that and I love it ?? mwanangu sasa hapendii! chaajabu anapenda kuweka chumani kwake lakini siyo living room  ??

Hot shot of the day

FB_IMG_1447083305149-1Mwajuma looking HOTT! Kapendeza sanaaaaaa. Be blessed

Kutoka Facebook

image-4-1Nimezipenda hizi picha za mdogo wangu anaitwa Magreth. Hapa ni nyumbani kwa mdogo wangu mwingine tunamwita Mzee William.  Naona dada alikuwa ameenda kusalimia mdogo wake.  image-3Nimependa mazingira pamoja na mwenye picha ?

Blessing anawatakieni wiki njema!

2015-11-09 09.42.59Blessing anasema weekend yake ilikuwa kama hivi, looking cute and fabulous ? Hapa ilikuwa siku ya Sabato teyari kwenda church. Anasema amewaombea  wote ?? 2015-11-09 09.42.21haya yalikuwa mapozi ya picha akiwa home kabla ya kwenda church ?? kapendeza sana mdogo wangu na mie! 2015-11-09 09.39.20 Sasa leo anasema muwe na week njema yenye baraka 2015-11-09 09.41.26hapana chezea mdogo wangu, si kwamapozi haya ati! 2015-11-09 09.44.06Si kwa tabasamu hili jamani lol! 2015-11-09 09.44.47Umeona alivyo fanya mdomo hahaha! Yani hapo amesema mfanye kazi kwa bidii. Mkae kwenye office zenu sio mabara barani halafu akamalizia na ‘mmmmh!’ (In Wendy’s voice) ???