Napenda kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa mdogo wangu Charles Manongi. Mungu azidi kukubariki, uwe na afya njema, maisha marefu yenye amani na furaha nyingi. Charles yeye ni mdogo wake na kaka yangu kipenzi Noah Manongi. Ni mtoto wa mwisho kwa familia ya mzee Manongi……….Happy birthday Charles, be blessed!
All posts by Alpha Igogo
Pumzika kwa amani Mh. Celina Kombani!
Kwa makasikitiko makubwa sana, naomba nitowe salama za pole kwa familia ya marehemu Waziri Celina Kombani na Watanzania wote walioguswa na msiba huu. Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa rehema apate kuwatia nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Kwa walio wengi ulijulikana kama mwanasiasa wa chama cha Mapinduzi, na mfanyakazi wa Umma lakini kwa familia ya Otieno Igogo wewe ulikuwa sehemu ya familia. Japo mimi binasfi (Alpha) sikuwahi kujaliwa kukuona uso kwa uso lakini upendo wako na ukarimu wako kwa familia yetu ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kujihisi kuwa tulishawahi kuonana. You were our Shero! Daima utadumu ndani ya myoyo yetu.
Utakumbukwa sana na rafiki yako kipenzi ambaye alifanya familia nzima ikujuwe (Mr. O.O Igogo) na kwaniaba yake na familia yake yote kwa pamoja tunasema mpaka siku ile ya hasubuhi ya fahari itakapo fika; pumzika kwa amani mama yetu. Poleni wanafamilia wote.
“Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.” 2 Timothy 4: 7-8
Birthday wishes
Kheri ya siku ya kuzaliwa rafiki yangu Prisca. Mwenyezi Mungu azidi kukubariki, akupe afya njema, maisha mazuri na bora. Hapa Prisca alikuwa ametoka Geita anapo ishi kuja kunisalimia mimi rafiki yake. Prisca tulisoma wote Kowak Girls Secondary school. Urafiki wetu ulianzia shule na mpaka leo hii umedumu. Asante sana Prisca. Hapa ni Halima, Prisca na mimi, unaweza ku-imagine story za mashosti ambao hawajaonana kwa muda mrefu wote ni waanzilishi / wanafunzi wa kwanza kabisa wa Kowak Girls Secondary school………Happy birthday Prisca, ubarikiwe sana.
Hot shot of the day
Wow! Nimependaje hizi picha za dada yetu kipenzi ShyRose Bhanji akiogelea huko visiwa vya Zanzibar! Nivizuri kupumzisha akili na mwili baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu. Hii nikukusaidia kuwa na afya njema na kuishi maisha marefu. Jamani mie naona hata aibu kusema kuwa SIJUI KUOGELEA ??? nimeshaimba kujifunza siku na miaka inakatika tuu ??? lakini bado nina nia hivyo najua ipo siku nitaingia darasani ??? Miguu ya wanawake wa “kanda ya ziwa” utaijua tuu mizurijee?! ???
Mother and sons moment
Nimependa sana hii picha ya jeshi la mutu 3 na mama yao halafu kwa nyuma pale chief commander (baba yao) anawarekodi. Hapa walikuwa kanisani wakiimba kama ilivyo kawaida yao. Wenzetu wanasema game kuwa familia inayo Sali na kuomba pamoja siku zote hushikamana. Mbarikiwe sana mama na baba watatu pamoja na watoto wenu wote.
#FBF
Mother and daughter moment
Mama na binti yake, wamependeza sana. Malaika ni mrembo sana sana. Safi sana! Ukitaka kuona picha zingine “amazing” tembelea www.maisafari.com au bonyeza hapa, utafurahia sana.
Manhood
Hot shot of the day
Mrembo na mama aliyeumbwa akaumbika Mrs Lyimo. Kapendeza sana! Kitu kutoka Kanda ya Ziwa maeneo ya Musoma line hiyo ?Mwanamke mguu ati haswa siye wa kanda ya ziwa yani woman’s leg is part- compulsory of your beauty…………..watu wa kanda ya ziwa wanaangalia miguu ya mwanamke sanaaaaaa! Wanaamini wanawake wenye miguu membamba (wanaita mironjo) wengi ni chakaramu (yani wanaongea kupitia kiasi) na huwa wana roho fulani hivi ‘not amazing’ ??? Sina huwakika kama imethibitishwa na wanasayansi ila najua wanasayansi wamethibisha kuwa wanawake wenye hips kubwa wengi huwa wana akili sana.
Kutoka Facebook
Happy 8th birthday Malaika
Happy 8th belated birthday to gorgeous Malaika Kakoschke. May Almighty God continue to protect you, bless you with happy-healthy life and makes all your dreams true. Malaika’ birthday was yesterday Sunday September 20th. She enjoyed her day, surrounded by family and wrapped with their love. Malaika and her handsome brother Iman. Wazurije sasa ?? God bless them………….Happy birthday beautiful!
Tafadhali kwa picha nzuri zaidi za maisha yao tembelea maisafari.com au bonyeza hapa
Manhood
How do you party?!
How do you party?! Nimeamua kuanzisha hichi kipengele cha “how do you party?!” Nitakuwa naweka picha za matukio tofauti ya watu wanavyo kula raha ? na leo naanza na wana San Francisco. Hapa walikuwa kwenye Concert. Regina, gal! You are too cute! God bless you Ukishikwa Sharti ushikamane ati! Wenye bahati zao ☺ I am not jealous just being honest ?
Mr and Mrs Lyimo
Hot shot of the day
Dada yetu kipenzi chetu ShyRose Bhanji akiwa na mama yake (aunt / mlezi) nyumbani kwao Mwitongo, Musoma vijijini. Safi sana, nani kama mama. Tafadhali hapa alienda msalimia mama. Hizo uniform za chama alizovaa ni mapenzi yake kwa chama chake na ukizingatia sasa hivi ni wakati wa campaign. Ubarikiwe sana dada yetu.
Kutoka Facebook
Tuwapende na kuwaheshimu walimu wetu
Kila mtu hapa dunia amejifunza kitu fulani kwa maana ya kuwa hakuna aliyezaliwa akijua kituchochote bali ni kwakujifunza. Mfumo ya kujifunza ipo ya aina mbili formal (mfumo rasmi) na informal (mfumo usio rasmi). Haijalishi ni mfumo gani umetumia kujifunza kwani yote lengo lake ni kutoa elimu. Na wale watu wanao tumika kutoa elimu wanaitwa walimu kwasababu wanakuelimisha. Continue reading Tuwapende na kuwaheshimu walimu wetu
Happy 12th Wedding Anniversary to Mr and Mrs Nyagaswa!
Napenda kuwapongeza Mr and Mrs Nyagaswa kwa kutimiza miaka 12 katika ndoa yao. Mungu awalinde, awabariki sana, mapenzi yao yazidi kusonga mbele na wadumu pamoja mpaka kifo kitakapo watatenganisha. Hapa ilikuwa siku ile kuu, siku ya ndoa yao miaka 12 iliyopita. “Thank you Lord for our 12 wedding anniversary. ” Hayo ndiyo maneno machache sana lakini ni mazito kutoka kwa mke mwema Dr. Elizabeth Daniel Oming’o. Kwani ni Mungu tuu bila Mungu hak uh na kitu!!………..Happy 12th wedding anniversary my darling cousin. Mbarikiwe sana.
Happy 51st Wedding Anniversary to Mr and Mrs Musira
Napenda kuwatakia mama yangu mkubwa pamoja na baba yangu kheri na furaha ya miaka 51 ya ndoa yao. Mungu azidi kuwalinda, kuwabariki sana, upendo, furaha na amani vizidi kutawala maisha yenu na nyumba yenu. Mmekuwa mfano nzuri si kwetu sisi watoto wenu hata kwa watu wengine. Mbarikiwe sana. Kwa faida ya wengi; mama Musira au Mrs Musira ni dada yake mkubwa na mama yangu mzazi. Yeye ndiyo mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya mama yangu. Pia alikuwa mlezi wa mama yangu wakati anasoma secondary huko nyumbani kwa watani zangu Rugambwa Secondary. Vile vile walikuwa ni walezi wangu mimi wakati nasoma Kowak Girls Secondary school. Mzee Musira ndiyo alikuwa akija kwa mikutano ya wazazi pale wazazi wangu walipo shindwa fika, kwani ilikuwa ni rahisi kwa mzee Musira kufika si tuu kutokana na ukaribu wa wanapoishi bali pia alikuwa Mkurugenzi wa Elimu wa diocese ya Musoma (kwa kanisa la Catholic) hivyo kila mkutano lazima anakuwepo. Asante sana baba na mama. Hapa ni mwaka jana waliokuwa wanasherekea Jubilee ya ndoa yao. Atukuzwe Baba Mungu aishie mahali pa juu Mbinguni. Hapa ni mimi na wadogo zangu Janeth na Magreth pamoja na mama mkubwa. Tulienda wasalimia huko Kamnyonge, Musoma mwaka 2013.
Kwenye picha hizi ☝ ni mimi na wadogo zangu pamoja na baadhi ya watoto wa mama mkubwa Neema (mwenye top nyeupe na nyeusi) pamoja na Yacinta (mwenye pink na black)…………Happy 51st Wedding Anniversary wazazi wetu. Tunawapenda sana.
Je, unaishi mikononi mwa Farao?!
Kuna wakati unakuwa inlove lakini actuallywewe ni kama Mtumwa aliyeko Misri kwenye himaya ya Farao! Umekazana kulia na kumfurahisha mpenzi wako ambaye hana tofauti na Farao. Lina roho ngumu, hajali hisia zako, anaku-treat wewe kama object halafu wewe unavumilia na kupoteza muda wako wakati hata ndoa hujafunga naye! Wakati huku nje kuna akina Musa kibao wanajaribu kukutoa utumwani Misri ili uingie Kaanani, nchi ya ahadi, nchi yenye maziwa na asali, nchi iliyojaa upendo na furaha. Lakini wewe cha ajabu, unasema “you are in love?” na Farao?? Yani hupo teyari kufunga maktaba na shetani? Mateso yote anayokupa na kukutumikisha lakini you still think ipo siku life itabadilika na Farao atakuwa mwema! Farao hawezi kuwa mwema kamwe, hata siku Misri ibadilike haiwezi kuwa na Maziwa na Asali!!
Wake up, go after your destiny, toka Misri nenda Kaanani uishi kwa raha. Mapenzi yana raha sana ukiwa Kaanani, huyo Farao unaloling’ang’ania wala halikupendi na halina future na wewe. Poleni wale mnaodate na Farao, fungueni macho, Musa anawasubiri!!