Wahenga walisema furaha ya dunia watoto! Na hakuna kitu kizuri kama kuwa mtoto maana huna bills zozote zile za kulipa, yani wewe kazi yako ni kula, kucheza, na kulala. Kazi ngumu ni kucheza kama unavyo waona watoto hawa walivyo busy na michezo na pozi katika picha. Mungu awalinde na azidi kuwabariki wa toto wote.
All posts by Alpha Igogo
Happy Wedding Anniversary
Happy 18th wedding anniversary to Mr. And Mrs. Ngeli
“18 years ago God gave me a best friend, a partner in crime, a person to love, care and pray for. I learned a lot from you darling and most of all you have encouraged me to be strong, confident, and successful woman I am today. And most of all you have made me a queen. I will do it all over again with you because I have enjoyed every minute of it. Thank you and Happy anniversary my husband” ……….those sweet, sincere, and touchy words are from the wife- Tumaini.
To read my interview with da Tumaini click Here
Birthday wishes
Kutoka Facebook
Birthday wishes
Mahojiano Maalum-Linda Bezuidenhout (LB)
http://youtu.be/7tmJgxbmB1A
News Alert!
KESHO JUMATATU MAHOJIANO YA HUYU NA YULE USIKOSE KUJUA USIRI WA MAISHA YA LINDA
NI MENGI AMEZUNGUMUZA AMBAYO MIMI NA WEWE HATUKUYAJUA
Kesho Jumatatu katika kipindi cha mahojiano cha Huyu na Yule usikose mahojiano na mwanamitindo mbunifu wa LB kutoka Atlanta, Georgia atakapoelezea historia yake yenye milima na mabonde historia ya maisha yake yenye huzuni na furaha wakati mwingine Linda akitokwa na machozi kwa kukumbuka maisha aliyopitia.
Je Mume wake Mali walijuana nae wapi? na mengine mengi kuhusu maisha yake ikiwemo kampuni yake ya LB na malengo yake ya kupeperusha bendera ya Tanzania anga za kimataifa. USIKOSE mahojiano yaliyofanywa na mwakilishi wa Vijimambo na kwanza production Michigan Alpha Igogo ambae alitaka kujua undani wa maisha ya mwanadada Linda
Alpha Igogo akifanya mahojiano na Linda jijini Atlanta
Maswali yalikua moto Linda akipumua na kumkumbatia Alpha Igogo baada ya mahojiano kufikia mwisho
visit my blog at http://lukemusicfactory.blogspot.com/
Family Time
Kutoka Facebook
“Nani kama mama! Mano Mamawa, Jaber NyarKowak, Nyar Awiti, Nyamin gi Leo Awiti, Iber ndi merwa”…….basi hayo ndo yalikuwa maneno yake Advocate Janeth Igogo kwenye hiyo picha ya mama yetu kipenzi.
Kama huifahamu hiyo lugha ni lugha ya Kiluo, kutoka mkowa wa Mara wilaya ya Rorya. Na tafsiri yake ni kama ifuatavyo :-
Nani kama mama! Huyo ni mama yetu, mrembo binti wa Kowak (Kowak ni kijijini alipo zaliwa mama yetu), binti wa Awiti, dada yake na Leo Awiti (Mzee Leo Awiti ndiyo kaka mkubwa katik familia ya mama yetu), wewe ni mrembo sana mama yetu! mmmmh! so touchy!
God keep blessing our mama and all good responsible mothers out there! We love you so much NyarAwiti!
Family Time
Nilishawahi kusema huko nyuma na sito choka kusema kwani naelewa na naheshimu umuhimu wa familia. Ukitaka kuiua society yoyote ile anza kwa kuvuja marriage and family institution basi mengine yote yatafata kirahisi kabisa.
Hivyo basi, hii blog itatumika sana kuhamasisha umuhimu wa familia. Kila jumapili Mungu akinijalia nitakuwa nawawekea picha za familia mbali mbali. Kama utapenda kushare picha zako au una ujumbe kuhusu familia ungependa kushare, tafadhali wasiliana nasi.
Hii ni familia ya “Mama na baba watatu” kama wanavyopenda kujiita. Wao wanaishi Ohio, Marekani. Naipenda sana hii familia, na pia inanifurahisha zaidi kwani nilishuudia kuundwa kwake (ndoa yao) miaka zaidi ya mitano iliyopita, wakati huo walikuwa Mr. and Mrs (-) watoto. Mungu azidi kuibariki familia hii, idumu katika Bwana siku zote. Amina!
Linda Bezuidenhount
April 14, 2015 Linda BezuidenhountApril was invited to attend the New York Festivals International Television & Film Gala. The event took place at the Westgate Las Vegas Resort and Casino, Las Vegas, Nevada. Here are some photos to share with you, as usual Linda is rocking hee own design from LB Apparel. Hongera Linda.
Mkumbuke Muumba wako
Ujumbe wa leo ni kwamba mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako ukiwa bado unanguvu na muda mwingi sana. Usisubiri mpaka majanga yakukute au use kwenye near death situation ndo uwanze kumtumikia Mungu. Ni jumbe kwetu wote, nashukuru dada yeti kipenzi Shy-Rose ameweza kutukumbusha kwa kutokujikweza mfanikio.
Mh. Shy-Rose aliudhuria ibada ya Ijumaa iliyopita alipokuwa mjini Mwanza kwa shughuli za kichama. Ubarikiwe sana dada yetu.
Kutoka Facebook
Watoto na vipaji
Kama mmoja ya wazazi walio zaliwa na kukulia katika mazingira ya kiafrica ambapo wengi wazazi wengi miaka ya nyumba hawakuwapa watoto wao uhuru wa kukuza vipaji vyao. Wazazi wengi walikuwa na mtazamo yao ya ni nini wanataka watoto wao wawe wanafanya wanapo kuwa wakubwa. Basi nami kwakweli nilijikuta nikiwa na mtazamo huo huo wakumnyima mwanangu uhuru wa kupata full “exposure” ya vitu vile alivyokuwa akionyesha kuvipenda au niseme kuwa talented navyo kwani nilikuwa teyari nina picha ya ni nini mwanangu anatakiwa kufanya au kuwa.
Mwanangu ni anapenda sana basketball, mwanzoni nilimuacha ashiri mchezo huo alipokuwa elementary school. Alicheza mpaka darasa la saba lakini baadaye nilimzuia. Sababu haswa nilitaka a-constraint kwenye masomo zaidi kuliko michezo. Kitu ambacho kwa upande mmoja au mwingine hakikuwa kizuri kwani nili mnyima haki yake ya kuendeleza kile kitu ambacho roho uake inapenda sana.
Najua kuna wazazi wengi ambao bado wana mtazamo kama wangu, basi ngoja nikushauri kama utapenda. Ukiona mtoto wako anapenda kitu fulani au anaonyesha uwezo wa kitu fulani basi usidharau au kukatisha tamaa unless iwe ni kitu ambacho si kizuri kama kudokoa n.k Usiweke nguvu myingi (pressure) kumuhiza akazanie no-no! Ila muonyeshe kuwa unam-support kile anacho kifanya. Nasema usitumie nguvu sana kwani kama ni kipaji chake basi utazidi kuiona, na kama ni kitu cha mpito tuu basi baada ya muda atapoteza interest ya hicho kitu.
Dunia ya leo ni vizuri mtoto akiwa malt-talented. Dunia ya sasa si kama ile ya wazazi wetu ambapo kama mtu ni Manager wa kapuni basi utakuta ana kuwa na ma secretary wawili, leo hii wanataka Manager ambaye ajua kutype na basic computer skills kwa kwasababu ya mambo ya confidentiality makampuni mengi wanapenda Managers wa type na kuhifadhi baru wenyewe ili kupunguza risk za kuvuja kwa siri za kampuni.
Ok. Nawatakieni malezi mema 🙂 🙂
Kutoka Facebook
Tatizo la technology
Jamani hakuna kitu kina nikera na ninaweza kusema sikipendi kabisa kama ninavyo ona watu wako busy wakati wa mambo ya muhimu kama hapo kwenye picha chini!!
Mwanzoni nilifikiri ni mwanangu tuu ndo anahii tabia mbovu laakini kumbe watu wengi tuu; inawezekana hili likawa “janga la dunia.” Kwani si watoo, si vijana, na wala si watu wazima yani wote wana hili tatizo. Najiuliza why? Ndo madhara ya technology au ni watu tuu kujiendekeza? Mie sielewi kwani hii tabia sina, labda kutoka na field niliosoma imenifanya kidogo niwe mwangalifu sana wa tabia kama hizi.
Utakuta mtu kaalikwa kwenye sherehe, lakini yupo busy na simu it’s just so rude! Wewe umealikwa kwenye sherehe ya mwenzio kwanini usiweke mawazo pale, onyesha heshima kwa wenye shughuli. Na kama unaona ina ku bore si uondoke kimya kimya?
Wengine bila aibu wala hofu ya Mungu utakuta kanisani (not sure about Msikitini) yupo busy na simu utafikiri ni standby surgeon!! Na wengine hata kwenye ibada za mazishi wao wapo busy, yani roho ngumu kama kazaliwa na Farao!!
Embu kama unaweza badilika basi jitahidi ubadilike. Mie hapa napiga kelele sikuhizi amepunguza kidogo ila sito nyamaza mpaka atakapo acha 😉 😉
Kutoka Facebook
Simplicity Is Always The Best
Shout out to my cute cousin-sister Lisa Makoyo. Kwa kweli si tu kapendeza bali uzuri wake wa asili na rangi yake ya chocolate inavutia sana.
Kuna baadhi ya wanawake ambao wanafikiria kupendeza ni lazima uvae nguo za expensive designers na upake poda, na marangi rangi mengi usoni, kumbe wala si kweli. Hivi hujawahi ona watu wanavaa vitu vya pesa nyingi nabado wanaonekana “kituko” bara barani? Yani utakuta mtu kapaka heavy makeup, aye shadow za rangi za kung’aa, bangili, hereni yani makoro koro kibao usoni. Basi hapo ndo mkute ana nguo yake ya sijui designer gani na lipstick juu, ukimwangalia utazani yule ndege mwenye mdomo mrefu aitwae Kasuku!!
Halafu pia kupendeza siyo lazima uvae nguo za bei ya ghali. Kinachotakiwa kikubwa ni usafi wa mwili na mavazi. Unaweza ukavaa nguo yako uliyo ishona kwa fundi “Chochote” na bado ukapendeza zaidi ya yule aliye vaa nguo ya bei “chafu.” Kupendeza ni muhimu sana kwa kila mwanamke lakini kujiweka mapambo mengi inaonyesha kuwa ni mwanamke mwenye low-selfesteem (hujiamini).
Jamani kwa kifupi, simplicity is always the best, and too much of anything is harmful!! Tuige mfano wa Lisa Makoyo.
BTW, Black Girls Rock 🙂 🙂
Cecilia Hairdressing Salon
Furaha ya Pasaka
Hivi ndivyo baadhi ya wasomaji wetu walivyo shereke siku kuu ya kufufuka kwa Bwana Yesu (Pasaka).
Mambo yalikuwa kama ifuatavyo pande za Atlanta, Georgia kwa designer maharufu Linda Bezuidenhout(owner of Lb apparel). Linda kama kawaida yake amevaa vazi la ubunifu wake yeye mwenyewe.
Na hivi ndivyo ilivyokuwa pande za Mbagala, Dar es salaam. “Undugu ndo hazina yetu” hayo maneno aliyo sema Felister Sarungi wakati akisherekea ufufuo wa Mfalme Yesu pamoja na shangazi yake Tabu Obago pamoja na Jack na Juliet (binti wa Tabu).