All posts by Alpha Igogo

Kesha la asubuhi: UTAKATIFU

*Kesha la Asubuhi*

*J, tano Tarehe 28/3/2018*

*UTAKATIFU*

?? *Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao. Waebrania* *12:14*

??Tangu milele, Mungu alichagua watu wawe watakatifu. “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu” (1 Wathesalonike 4:3). Mwangwi wa sauti yake unatujia, daima ukisema, “Utakatifu zaidi, Utakatifu zaidi.” Na jibu letu daima yafaa liwe, “Ndiyo Bwana, watakatifu.”

??Hakuna mtu anayepokea utakatifu kama haki ya kuzaliwa, au kama zawadi kutoka mwanadamu mwingine yeyote. Utakatifu ni zawadi ya Mungu kupitia kwa Kristo. Wale wanaompokea Mwokozi wanakuwa wana wa Mungu. Hawa ndio watoto wake wa kiroho, waliozaliwa upya, waliofanywa upya katika haki na utakatifu wa kweli. Nia zao zimebadilishwa. Wanaona mambo halisi ya milele kwa maono yaliyo wazi zaidi. Hawa wamefanywa kuwa sehemu ya familia ya Mungu nao wanapatanishwa na sura yake, wanabadilishwa na Roho wake kutoka utukufu hadi utukufu. Kutoka katika kufurahia hali ya kupenda nafsi katika viwango vya juu sana, wanafikia hatua ya kufurahia upendo wa juu kwa Mungu na kwa Kristo. “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo” (Warumi 5:1). Kuhesabiwa haki kunamaanisha msamaha. Kunamaanisha kwamba moyo, ukiwa umesafishwa na kuondolewa matendo yaletayo mauti, umeandaliwa kupokea baraka ya utakaso. Mungu ametuambia kile ambacho ni lazima tufanye ili tupokee baraka hii. “Utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu” (Wafilipi 2:12-15).

??Upendo wa Mungu, ukihifadhiwa moyoni na kudhihirishwa katika maneno na matendo, utafanya sehemu kubwa ya kujenga na kuadilisha wanadamu kuliko jambo lingine lolote lile. Katika maisha ya Kristo, upendo huu uliweza kuonekana kikamilifu na bila upungufu. Msalabani pa Kristo, Mwokozi alifanya upatanisho kwa ajili ya jamii ya watu iliyokuwa imeanguka dhambini. Utakatifu ni tunda la kafara hii. Ni kwa sababu alikufa kwa ajili yetu ndiyo maana tunaahidiwa karama hii kuu. Hivyo ni shauku ya Kristo kutupatia karama hii. Ni shauku yake kwamba tuweze kuwa washirika wa tabia yake. Ni shauku yake kuokoa wale ambao kutokana na dhambi wamejitenga na Mungu. Yeye anawaita wachague huduma yake, wajitoe wenyewe kikamilifu kuwa chini ya utawala wake, wajifunze kutoka kwake namna ya kufanya mapenzi ya Mungu. – Signs of the Times, Des. 17, 1902.
*MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI NENO LAKE*

Faraja Nyalandu: Huu ni uhitaji ambao kila binadamu ana

Regrann from @farajanyalandu  -  Oprah Winfrey amefanya interview na marais, waimbaji, wanamichezo na mashujaa wa matukio mbalimbali. Kila mmoja akiwa ni mtu aliyefanikiwa katika eneo fulani. Hawa ni watu walioenda mbele zaidi na kujitofautisha na wengi. Lakini wote wakimaliza mahojiano, camera zikizimwa, huwa wana swali moja kwa Oprah. How did I do? Sina tafsiri ya moja kwa moja lakini ni swali ambalo wanataka kujua iwapo walipatia au walikosea. Sana sana wakitamani kusikia walifanya vizuri na interview yao ilikuwa bora. Huu ni uhitaji ambao kila binadamu anao. Si udhaifu kwasababu ni katika harakati za kujitambua. Ni vile tunataka kufanya vizuri na tungependa kupewa feedback na wakati mwingine kupewa moyo kuwa tunaenda sawa. Ni muhimu kuwa na neno la upendo kwa wengine. Tusione watu wanatembea ni wazima kumbe ndani wana vidonda. Pengine wewe ndio utakuwa wa kwanza na pengine utamuwahi kabla hajakata tamaa na kudhani hana thamani. Tutibiane vidonda. Tuthaminishane. Tukubaliane tofauti zetu. Tukosoane kwa upendo. Sisi ni watoto wa Mungu na Mungu ni pendo. Let's validate each other! #WeekendWisdom ?  - #regrann

Kesha la asubuhi: Ujasiri

```KESHA LA ASUBUHI```

*JUMATATU MACHI 26, 2018*

*Ujasiri*
_Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Waebrania 10:35._

? Yohana anasema, “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba” (1 Yohana 5:14, 15). Hebu tudumishe zaidi wazo hili kwa watu, ili mawazo yao yapate kupanuliwa, imani yao iongezeke.

? Hebu watiwe moyo kuomba kwa upana zaidi na kutegemea bila mashaka utajiri wa neema yake; kwani kupitia kwa Yesu tunaweza kuja kwenye chumba cha kuzungumza naye Aliye Juu. Kupitia kwa stahili zake tunayo fursa ya kumfikia Baba kupitia kwa Roho huyu mmoja.

? Laiti tungekuwa na uzoefu mkubwa zaidi katika maombi! Tunaweza kumjia Mungu kwa ujasiri, tukijua maana ya kuwepo kwa Roho Mtakatifu na nguvu yake. Tunaweza kuungama dhambi zetu na pale pale, huku tukiomba, tujue kwamba Yeye anasamehe makosa yetu, kwani ameahidi kusamehe. Ni lazima tuiweke imani katika matendo na kudhihirisha uaminifu wa kweli na unyenyekevu.

? Kamwe hatuwezi kufanya hivi bila neema ya Roho Mtakatifu. Ni lazima tulale chini miguuni pa Yesu na tusiendekeze ubinafsi, tusioneshe namna yoyote ya kuiinua nafsi, lakini tumtafute Bwana kwa namna iliyo sahili, tukimwomba Roho wake Mtakatifu kama mtoto mdogo aombavyo mkate kutoka kwa wazazi wake. Ni lazima tufanye sehemu yetu, tumchukue Kristo kama Mwokozi wetu binafsi, nasi, huku tukisimama chini ya msalaba wa Kalvari, “Tutazame na tuishi.”

? Mungu anajitengea watoto wake kwa ajili yake mwenyewe. Nao wanapounganika Naye, wanakuwa na nguvu pamoja na Mungu na kushinda. Kwa uwezo wetu hatuwezi kufanya lolote; bali kupitia kwa neema ya Roho wake Mtakatifu, tunapewa uzima na nuru, nayo nafsi hujazwa na shauku ya dhati na hamu ya Mungu, na ya utakatifu. Hapo ndipo Kristo anapotuongoza kwenye kiti cha enzi cha neema na kutuvisha kwa haki yake; kwani Bwana Mungu wa mbinguni anatupenda.

? Kuwa na wakaidi na wenye mashaka kwa makusudi ndiko kunakoweza kutufanya kuwa na mashaka kwamba moyo wake huwa unatuelekea sisi. Wakati Yesu, Mpatanishi wetu, anapotuombea mbinguni, Roho Mtakatifu huwa anafanya kazi ndani yetu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. Mbingu zote huwa zinapendezwa na wokovu wa roho moja. Sasa, tunayo sababu gani ya kuwa na mashaka kwamba Bwana anatusaidia na atatusaidia? –Signs of the Times, Okt. 3, 1892.

```MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI UJUMBE WA LEO```

Hapa kazi tu!

Roving camera of mzee  Igogo caught these two young street boys at work, carrying a wooden box to their homestead along Indhra Gandhi street, in Dar es salaam, Tanzania. When asked why, the elder one responded that ” HAPA KAZI TU”! ………..  Wishing you all a very productive and fruitful week. #HapaKaziTu

Open_Kitchen2014: lazima ifike mahali tuelewe kuwa fadhila za watoto wetu ni baraka hatutakiwi kuwafanya watoto wetu ndio mtaji wetu

Regrann from @open_kitchen2014 - Wanawake , wasichana , wamama tunanapigana usiku na mchana , tunavumilia mengi na mengi ni siri yetu kwasababu tunataka the best kwa ajili ya watoto wetu nguvu zetu jasho letu , vyote ni kwa ajili ya watoto wetu .
Ila wamama......lazima ifike mahali tuelewe kuwa fadhila za watoto wetu ni baraka hatutakiwi kuwafanya watoto wetu ndio mtaji wetu au watoto wetu ndio mahali tulipofanya uwekezaji basi kila kitu mimi mama yako nililala nje kwasababu yako , mimi mama yako nilipigwa nikavumilia kwasababu yako , mimi mama yako niliuza mali nikusomeshe , mimi mama yako sijui nilibeba mimba nikateseka kushinda wa mama wote duniani kwa sababu yako ?????(kicheko sunna) ..kila mama na story yake ilimradi ajenge sympathy kwa mtoto wake .

.la hasha mtoto lazima umpe freedom yake wewe kama mama yes umeteseka , yes umepitia wakati mgumu ,yes umepambana usiku kucha but hiyo ndio nature ya mama ndio maana mama siku zote amebarikiwa sana so leo tusiwatese watoto wetu na kuwanyima uhuru wao furaha yao just because wewe mama unataka mtoto wako awe a certain way asome kile ambacho kilikuwa dream yako inafika mahali mpaka mama unataka mtoto wako kuoa au kuolewa na yule wewe unayemwona ndio perfect kwako mwenzangu wamama siku hizi tumegeuka kuwa manabiii pia ???? .

Tumebarikiwa kuwa wamama watoto wetu tunatakiwa kuwasomesha , na kuwaongoza katika misingi bora but watoto wetu sio vitega uchumi , watoto wetu lazima wawe na maamuzi yao hata kama ni maamuzi yasiyokufurahisha kama mzazi all we need to do ni kuwa guide na kuwaelekeza kuwa the choice has consequences hizi so yeye ataamua which way to go but not to condem or command them to do wewe mama unavyotaka au unavyotarajia 
Tunawapoteza watoto wetu simply because tunawanyima UHURU WAO MOTHERS WE MUST LEARN TO LET GO AND STOP IMPOSING SO MUCH FEAR AND SADNESS INTO OUR CHILDREN 
BECAUSE THIS AFFECTS THEM SO MUCH WANAJIONA KAMA WANADENI KUBWA SANA TOWARDS MAKING US HAPPY WHICH IS NOT RIGHT . .AS MOTHER'S WE ARE BLESSED LET'S CARRY OUR BLESSINGS IN A POSITIVE WAY .
. .. - #regrann

Kesha la asubuhi: Utii

*KESHA LA ASUBUHI*

```JUMAPILI MACHI 25, 2018```

*UTII*
_Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote. 1 Petro 1:14, 15._

? Mungu anahitaji nini? Ukamilifu, ukamilifu usio na upungufu wowote. Lakini ikiwa tunataka kuwa wakamilifu, ni lazima tusiweke imani yetu katika nafsi. Kila siku ni lazima tujue na kuelewa kwamba haifai kuitumainia nafsi. Tunahitajika kushikilia ahadi za Mungu kwa imani thabiti. Tunahitajika kuomba kupewa Roho Mtakatifu huku tukitambua kikamilifu hali yetu ya kutojiweza. Kisha, Roho Mtakatifu akitenda kazi hatutaipa nafsi utukufu.

? Kwa uzuri, Roho Mtakatifu atauchukua moyo katika hifadhi yake, huku akiuletea mionzi angavu ya Jua la haki. Tutatunzwa na nguvu ya Mungu kwa njia ya imani.
Tukiwa chini ya utawala wa Roho wa Mungu kila siku, tutakuwa watu wenye kuzishika amri. Tunaweza kuionesha dunia kwamba utii wa amri za Mungu unakuja na thawabu yake, hata katika maisha haya na katika maisha yajayo baraka za milele.

? Bila kujali kukiri kwetu imani, Bwana ambaye anapima matendo yetu, anaona jinsi tulivyopungua katika kumwakilisha Kristo. Ametangaza kwamba hali ya namna hiyo ya mambo haiwezi kumtukuza.Kuamua kukabidhi nafsi kwa Mungu kuna maana kubwa. Inamaanisha kwamba inatupasa tuishi na kutembea kwa imani, siyo kwa kuitumainia au kuitukuza nafsi, bali kumtazama Yesu kama Wakili wetu, kama mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu.

? Roho Mtakatifu atafanya kazi yake kwenye moyo uliotubu, lakini kamwe hatafanya kazi kwenye moyo unaoweka umuhimu katika nafsi, unaojitafutia haki yake. Katika hekima yake mwenyewe, mtu wa namna hiyo hujaribu kujirekebisha mwenyewe. Huwa anakuwa akiingilia kati ya nafsi na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu atafanya kazi kama nafsi haitaingilia kati.

? Tunaegemea wapi? Msaada wetu uko wapi? Neno la Mungu linatuambia: “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” (Yohana 14:26). Roho Mtakatifu yuko tayari kushirikiana na wale wote watakaompokea na kufundishwa naYeye. Wale wote wanaoishikilia ile kweli na kutakaswa kupitia katika ile kweli huwa wanakuwa wameunganishwa vizuri na Kristo kiasi kwamba wanaweza kumwakilisha Yeye katika maneno na matendo. – Manuscript Releases, kit. 12, uk. 52, 53.

*MUNGU AKUBARIKI MWANA WA MFALME*

Mo Dewji: safari ya mtu mwingine HAIWEZI KUKUZUIA WEWE kufanikiwa kwenye safari yako

Regrann from @moodewji  -  Kila wakati kumbuka kuwa, safari ya mtu mwingine HAIWEZI KUKUZUIA WEWE kufanikiwa kwenye safari yako. Usipoteze muda kwenye mawazo yasiyo kuwa na umuhimu. — Mo // Always remember that, someone else's journey WILL NOT STOP YOU from succeeding in yours. Don't waste time on unnecessary thoughts. — Mo  - #regrann

Jacqueline Mengi: I believe him because in his lifetime he’s done so many businesses and succeeded in each one

Regrann from @j_n_mengi -  I’m blessed to have the best business teacher in the world, my hubby ❤! He is the reason why I’m an entrepreneur today, he inspires me and he has taught me everything I know about business. He says to me ,because you already know how to do business you’ll be able to do any kind of business and succeed at it. I believe him because in his lifetime he’s done so many businesses and succeeded in each one. The knowledge I’ve gained from him is my treasure and I look forward to passing it on to our children, I’ve already started anyway ? Me and my kids talk business during our meals almost everyday!Im truly grateful. - #regrann

Kesha la asubuhi: Umaridadi wa nje

*KESHA LA ASUBUHI*

“`JUMAMOSI MACHI 24, 2018“`

*Umaridadi wa Nje*Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani. Mithali 31:21, 22._

✍? Elimisha, elimisha, elimisha. Wazazi wanaopokea ile kweli yapasa wapatanishe mazoea na desturi zao na maelekezo ambayo Mungu ameyatoa. Ni shauku ya Mungu kwamba wote wakumbuke kwamba utumishi wa Mungu ni msafi na mtakatifu na kwamba wale wanaopokea ile kweli ni lazima wasafishwe katika mielekeo, tabia, mioyo, mazungumzo, katika mavazi, na nyumbani, ili malaika wa Mungu ambao hawawaoni, wapate kuja na kuhudumia wale watakaokuwa warithi wa wokovu.

✍? Wale wote wanaojiunga na kanisa sharti wadhihirishe badiliko la tabia inayoonesha kicho chao kwa mambo matakatifu. Sharti maisha yao yote yajengwe kulingana na uzuri wa Kristo Yesu. Wale wanaojiunga na kanisa yapasa wawe wanyenyekevu kiasi cha kutosha kupokea maelekezo katika maeneo ambayo hawajawa makini kwayo na ambayo wanaweza na ni lazima wabadilike katika hayo.

✍? Ni lazima waoneshe mvuto wa Kikristo. Wale wasiofanya mabadiliko katika maneno au mwenendo, katika namna yao ya kuvaa au katika nyumba zao, huwa wanaishi kwa ajili yao wenyewe na sio kwa ajili ya Kristo. Hawajaumbwa upya katika Kristo Yesu, hata kufikia usafi wa moyo na mazingira ya nje. Wakristo watatambuliwa kutokana na tunda wanalolionesha katika kazi ya matengenezo. Kila Mkristo wa kweli ataonesha kile ambacho ukweli wa injili umekifanya kwake. Yeye ambaye amefanywa kuwa mwana wa Mungu ni lazima awe na mazoea ya kutenda kwa unadhifu na usafi.

✍? Kila tendo, hata liwe dogo kiasi gani, lina mvuto wake. Bwana anatamani kumfanya kila mtu kuwa wakala ambaye kupitia kwake Kristo anaweza kudhihirisha Roho wake Mtakatifu. Kwa namna yoyote haipasi Wakristo wawe wazembe au wasiojali suala la mwonekano wao wa nje. Inapasa wawe maridadi, japo bila mapambo. Inapasa wawe wasafi ndani na nje. – Testimonies to Southern Africa, uk. 87.

*MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI SOMO LA LEO*

Je, unaye rafiki mwema na mwaminifu?!

Unaye rafiki mwema ambaye ni mwaminifu kwako wakati wote? Can we find a friend so faithful Who will all our sorrows share?! Rafiki wa kweli ni hazina kwako, lakini rafiki wa kweli ambaye ni mwema na mwaminifu huyo siyo rafiki bali ni ndugu! ...... Mzee Igogo akiwa Gongolamboto, Ukonga akiwa amekwenda kutembelea familia ya rafiki yake Daudi. Wachunguze marafiki zako kwa makini, na ujiridhishe kuwa ni marafiki wema na waaminifu.

 

Kesha la asubuhi: Heri wenye moyo safi; maana hao watamwona Mungu

*KESHA LA ASUBUHI*

ijumaa. *23/03/2018*

*Usafi*

?

*Heri wenye moyo safi; maana hao watamwona Mungu. Mathayo 5:8.* ??. Mtu akiwa ameondolewa ubinafsi kabisa, wakati kila mungu wa uongo anapoondolewa kutoka moyoni, ombwe hujazwa kwa mtiririko wa Roho wa Kristo. Mtu wa namna hiyo huwa anayo imani itendayo kazi kwa upendo na kusafisha moyo kutokana na kila uchafu wa kimaadili na kiroho. Roho Mtakatifu, Mfariji, anaweza kufanya kazi moyoni, akiweka mvuto na kuongoza, kiasi cha mtu huyo kufurahia mambo ya kiroho. Mtu huyo anakuwa “aifuataye Roho” (Warumi 8:5), naye huyafikiri mambo ya Roho. Huyu anakuwa haweki tumaini katika nafsi; Kristo ndiye yote katika yote. Bila kukoma, ukweli unakuwa ukifunguliwa na Roho Mtakatifu; naye hupokea kwa upole neno linalopandikizwa na kumpa Bwana utukufu wote, akisema, “Mungu ametufunulia sisi kwa Roho” (1 Wakorintho 2:10). “Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu” (aya 12).

??. Roho anayefunua pia hutenda kazi ndani yake katika kutoa matunda ya haki. Kristo anakuwa ndani yake, “chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele” (Yohana 4:14). Yeye ni tawi la Mzabibu wa Kweli nalo huzaa vishada vilivyosheheni vya matunda kwa utukufu wa Mungu. Matunda yanayozaliwa yana tabia gani? “Tunda la Roho ni upendo.” Zingatia maneno haya – upendo, siyo chuki; ni furaha, siyo hali ya kutoridhika na kuomboleza; amani, siyo harara, fadhaa, majaribu yaliyotengenezwa. Ni “uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria” (Wagalatia 5:22, 23).

?? Wale wenye Roho huyu watakuwa watendakazi wenye bidii pamoja na Mungu; wajumbe wa mbinguni watashirikiana nao na wanakwenda wakiwa na uzito wa Roho mwenye ujumbe wa kweli ambao wanaubeba. Hawa wanakuwa tamasha kwa ulimwengu, kwa malaika na kwa watu. Hawa wanakuwa wameadilishwa, wametakaswa, kupitia kwa utakaso wa Roho na imani ya ile kweli. Hawa hawajaleta kwenye hazina ya nafsi; kuni, majani, visiki, bali dhahabu, fedha na mawe ya thamani. Hawa hunena maneno yenye uzito wa maana na kutoka kwenye hazina za moyo huleta mambo safi na matakatifu kulingana na mfano wa Kristo. – Home Missionary, Nov. 1, 1893.

*tafakari... Njema*"""
.
.

Zamaradi Mketema: Katika kipindi cha Dawa usikimbie Dozi, na wala usilaumu mtu kwa ugonjwa wako

Regrann from @zamaradimketema - Kabla ya kupona kila mtu lazima apate Dawa yake, nyingine huwa chungu, nyingine tamu lakini ndio DAWA. Kwa bahati malengo ya dawa si mabaya ila kukusimamisha tena, kukufanya uogope ugonjwa ulioumwa ili uepuke vyanzo vyake, kutahadharisha na wengine waepuke sababu unajua uchungu wa matibabu yake, kwenye maisha DAWA tunazipata kupitia MATOKEO ya matendo yetu, yale tuliyoyatengeneza ndio yanatupa majibu yake, kwenye dawa hapa unaweza kudhalilika, kuumia, kutaka hata kujiua, kushuka thamani na vingi vingine, kutegemea ukubwa wa ugonjwa wako na ndio Dozi itakavyoenda, lakini uzuri ukishatambua unachoumwa na kukubaliana na hali bila kusahau kufata masharti ya ugonjwa unavyotaka unapona tu na mwisho wa siku maisha yanarudi kuwa mapya. Katika kipindi cha Dawa usikimbie Dozi, na wala usilaumu mtu kwa ugonjwa wako, pambana nao mpaka usimame upya, kiufupi usiyakwepe masharti maana kipindi cha Dawa ndio kipindi cha kujifunza, jua tu SIO PEKE YAKO mwenye ugonjwa huo, kuna wengi walioamua kuugua kwa siri ama kuficha matokeo yake tumewazika, kataa kuondoka na gonjwa lolote, ujinga ni wakati wa kwenda hivyo kikubwa jifunze athari zinazoweza kusababishwa na matendo yako, na kupona kwake ni kutotafuta yeyote wa kumuangushia mzigo wa lawama ila kuangalia mianya uliyoitoa iliyosababisha ugonjwa kuingia, kisha chaguo ni lako kuidhibiti ama kuachia nafasi ya ugonjwa kukushambulia kwa mara nyingine. - #regrann

Kesha la asubuhi: UKARIMU

*KESHA LA ASUBUHI*

_JUMATANO MACHI 21, 2018_


*Ukarimu*
```Maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. 2 Wakorintho 8:2.```


? Ni pale tu makusudi ya Mkristo yanapotambulika kikamilifu na dhamiri inapoamshwa kwa ajili ya wajibu, ambapo nuru ya Mungu huweka mguso kwenye moyo na tabia, huo ubinafsi unashindwa na nia ya Kristo inadhihirishwa. Roho Mtakatifu, akifanya kazi mioyoni mwa watu na tabia zao, ataondolea mbali mielekeo yote ya tamaa, mielekeo ya kufanya mambo kwa udanganyifu.

? Mjumbe wa Bwana anapokuwa akiuleta ujumbe kanisani, Mungu ananena kwa watu, akiamsha dhamiri zao zione kwamba hawajaleta zaka kwa uaminifu kwa Bwana, na kwamba pale ambapo haikuonekana kuwa muda unaofaa kutoa, wameshindwa kumletea sadaka yao. Wametumia pesa iliyo mali ya Bwana kwa ajili yao wenyewe, katika kujenga majumba, katika kununua farasi, vyombo vya usafiri, au ardhi. Huwa wanafanya hili wakitumaini kupata mapato makubwa na kila mwaka udhuru wao ni huo huo. “Je, mwanadamu atamwibia Mungu?” (Malaki 3:8). Kwa kweli, amekuwa akilifanya hili mara nyingi, kwa sababu hajawa mtu wa kiroho, kuweza kuona mambo ya kiroho.

? Kwa wapenda dunia, wabinafsi, Bwana amekuwa akitenda nyakati fulani, kwa namna iliyo wazi kabisa. Akili zao ziliangazwa kwa Roho Mtakatifu, mioyo yao ikahisi mguso wake unaolainisha na kunyenyekeza. Kutokana na utambuzi wa wingi wa rehema na neema ya Mungu, walijisikia kuwa ni wajibu wao kuhimiza mpango wake, kuujenga ufalme wake. Walikumbuka sharti, “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi” (Mathayo 6:19, 20).

? Walijisikia kuwa na shauku ya kuwa na sehemu kwenye ufalme wa Mungu, nao wakaahidi kutoa pesa zao kwa ajili ya baadhi ya shughuli mbalimbali katika kazi ya Mungu. Ahadi hiyo haikutolewa kwa mwanadamu, bali kwa Mungu mbele za malaika zake, ambao walikuwa wakipita mioyoni mwa hawa watu wabinafsi, wapendao pesa. – Review and Herald, Mei 23, 1893.

*MUNGU AKUBARIKI MWANA WA MFALME*

Happy birthday Tanzanian Princess and African pride!

Regrann from @jokatemwegelo – March Baby ??. March Queen ????‍???‍?. Soon to be somebody’s Wife ??and Mummy??. God is Great and Faithful. Grown but forever a baby girl ??. Ni kwa neema tu na rehema. Thank you loves for dragging me out to take these @divaglam_beauty @petefarasi9 @jacquescollection Nawapenda ❤ ~ otherwise I couldn’t be bothered ? #Kidoti #Kidoti2018 – #regrann

Happy birthday to our one and only one Jokate Mwegelo, Tanzanian Princess and African Pride! Wishing you abundantly blessings, endless happy momoments, and forever love! ……. Awwih! Am happy to hear the good news please usininyime mualiko hata kama sina hela nitakopa kwa baba yangu Dr Magufuli ili tu nije  kwa send off na harusi yako ??? (I am very serious though). Nakutakia kheri milele zote. Love you sanaaa ?❤

 

Happy birthday Hoyce Temu!

Leo wamezaliwa wanawake wa nguvu,  wanawake washoka,  malkia wa nguvu, fahari ya Tanzania. Siku ya kama ya leo katika nyakati na majira tofauti walizaliwa vipenzi vyetu Jokate na Hoyce. Kama wote mumjuavyo Hoyce siyo tu ni mwanamke wa Kitanzania bali ni moja ya hazina ambayo Tanzania inajivunia kuwa nayo! Hivyo tunamshukuru Mungu kwa kutuletea hichi kiumbe katika ardhi ya Tanzania. Tunaomba aendelee kututunzia na kumiminia neema zake. Happy birthday the Queen of Tanzania. Enjoy your day ?❤

Jokate Mwegelo: Namshukuru Mungu kwaajili ya wazazi wangu kwa kunilea katika maadili mema na hasa kunielekeza kwa Mungu na kunisisitizia elimu

Regrann from @jokatemwegelo - Miaka kadhaa iliyopita tarehe kama ya leo, taarifa zilienea Mama Kidoti amejifungua salama mtoto wa kike. Nilizaliwa kama watoto wengine wa kitanzania, wapo waliofurahia ujio wangu, na naamini wapo waliotamani ningekuwa mtoto wa kiume ?. Lakini Mwenyezi Mungu kwa hekima zake alinileta mwanamke. Hakuna aliyejua nimebeba nini ndani yangu kwa kuniangalia kwa macho, wala hakuna aliyejua nitakuja kuwa nani. Hayo yote Mungu aliyaficha katika hekima yake. Namshukuru Mungu kwaajili ya wazazi wangu kwa kunilea katika maadili mema na hasa kunielekeza kwa Mungu na kunisisitizia elimu, pia kuamini ndoto zangu, hata leo nimefika hapa nilipofika. Nawashukuru wote walioniamini na kuni-support hata wakati ambao mwenyewe sikujiamini katika ndoto kubwa nilizokuwa nazo. Naishukuru team yangu ya KIDOTI, partners wangu, na watanzania wote kwa ujumla kwa kuendelea kusimama na mimi kila hatua. Nakiri kwamba peke yangu nisingeweza kufanya chochote.
.
.
Ninayo furaha kubwa kuongeza mwaka katika maisha yangu hapa duniani, ni fursa ya kipekee kuwa hai. Wengi walikuwa na ndoto kubwa huenda kuliko zangu lakini hawapo nasi. Uhai ni zawadi na kwa hilo namshukuru Mungu. Maadam Mungu ameniacha hai ni ishara kuwa ana mipango mikubwa na maisha yangu ili niliishi kusudi lake na kutimiza kile aliniumba kufanya Tanzania na ulimwenguni kwa ujumla.

NI KWA NEEMA NINAISHI. HAPPY BIRTHDAY TO ME.
#KIDOTI #BIRTHDAYGIRL #KIDOTI2018 ?❤?? cc @rapture1913 @mkolikoli @cmagavilla ? - #regrann

Jokate Mwegelo: You embrace new age and say your age proudly

Regrann from @jokatemwegelo – Guess who else is a March Baby ???!?  The OG African Princess. The Iconic and my mama dearest @yvonne_chakachaka ….. Thank you for being amazing in every way possible. Drawing from your speech during women’s month at the University of Joburg last year, you said; here paraphrasing – celebrating life and being a year older isn’t something you shy away from. You embrace new age and say your age proudly because after many years of working extensively with children through Unicef and seeing babies die before the age of 5 and how nations strategize to eradicate such, you realize how life is just too precious and becoming older becomes more meaningful ☺. I pray this new age comes with more happiness and blessings. Nakupenda sana mama ❤❤❤ #Kidoti – #regrann  

Happy belated birthday to our African Princess! Wishing you many more happy years!

 

Kesha la asubuhi: Upendano wa ndugu

*KESHA LA ASUBUHI*

```JUMANNE MACHI 20, 2018```

  *Upendano wa Ndugu*


Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu. Warumi 12:10. ✍? Roho Mtakatifu anapoingia kwenye mawazo ya mtu, malalamiko na mashtaka madogo madogo baina ya mtu na watu wenzake yatatupiliwa mbali. Mionzi angavu ya Jua la Haki itang’aa kwenye vyumba vya moyo na akili. Katika ibada yetu kwa Mungu hakutakuwa na kutofautisha kati ya matajiri na maskini, weupe na weusi. Ubaguzi wote utayeyuka. Tunapomkaribia Mungu, itakuwa kama undugu mmoja. Sisi sote ni wasafiri na wageni, tunaoelekea kwenye nchi iliyo bora, ile ya mbinguni. Pale, kiburi chote, mashtaka yote, hali yote ya kujidanganya, vitakuwa vimekoma milele. Kila namna ya kificho kitaondolewa nasi “tutamwona kama alivyo” (1 Yohana 3:2). Pale nyimbo zetu zitachukua mada yenye kutia moyo nazo sifa na shukrani zitapanda kwake Mungu. – Review and Herald, Okt. 24, 1899.


✍? Bwana Yesu alikuja katika dunia yetu ili aokoe wanaume na wanawake wa mataifa yote… Yesu alikuja kueneza nuru kwa ulimwengu wote. Mwanzoni mwa huduma yake aliitamka nia yake: “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” (Luka 4:18, 19)…

✍? Jicho la Bwana li juu ya viumbe wake wote; anawapenda wote naye haweki tofauti kati ya weupe na weusi, isipokuwa kwamba Yeye huwa ana huruma maalumu kwa ajili ya wale walioitwa kuchukua mizigo mizito zaidi kuliko wengine. Wale wampendao Mungu na kumwamini Kristo kama Mkombozi wao, huku wakilazimika kukabiliana na majaribu na matatizo yanayokuwa njiani mwao, bado yawapasa wakubaliane na maisha kama yalivyo kwa moyo uliochangamka, wakikumbuka kwamba Mungu mbinguni anaona mambo haya, na kwa yale ambayo dunia inapuuzia kuwapa, Yeye atawalipa kwa fadhila zilizo bora zaidi. – Selected Messages, kit. 2, uk. 487, 488.

*UBARIKIWE MWANA WA MFALME*

Kesha la hasubuhi: Umoja

KESHA LA ASUBUHI

JUMAPILI- MARCH 18, 2018

UMOJA

“Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.” Yohana 17:20, 21.

▶Upatanifu na umoja unapokuwepo kati ya watu wenye tabia mbalimbali ni ushuhuda wenye nguvu zaidi uwezao kuonesha kwamba Mungu alimtuma Mwana Wake duniani kuokoa wenye dhambi. Ni fursa ya pekee ambayo tumepewa kudhihirisha hili. Lakini, ili tulifanye hili, ni lazima sisi wenyewe tujiweke chini ya agizo la Kristo. Ni lazima tabia zetu zitengenezwe kuwa katika upatanifu na tabia yake, nia zetu ni lazima zisalimishwe kwa nia Yake. Hapo tutatenda kazi pamoja bila hata wazo la kugombana.

▶Kudumu katika tofauti ndogo ndogo kutatufikisha katika kutenda yale yatakayoharibu ushirika wa Kikristo. Tusimruhusu adui apate nafasi dhidi yetu kwa namna hiyo. Hebu na tudumu kumkaribia Mungu na kukaribiana sisi kwa sisi. Ndipo tutakapokuwa kama miti ya haki, iliyopandwa na Bwana na kumwagiliwa na mto wa uzima. Nasi tutaweza kuzaa ajabu! Je, Kristo hakusema; “Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana” (Yohana 15:8)?

▶Moyo wa Mwokozi umeelekezwa kwa utimilifu wa kusudi la Mungu unaofanywa na wafuasi wake katika urefu wake na upana wake wote. Inawapasa wawe wamoja na Mungu, japo wawe wameenea duniani kote. Lakini Mungu hawezi kuwafanya kuwa wamoja katika Kristo wasipokuwa tayari kuchukua njia yake badala ya njia yao.

▶Sala ya Kristo itakapokuwa imeaminiwa kikamilifu, maelekezo yake yatakapokuwa yameingizwa katika maisha ya kila siku ya watu wa Mungu, umoja katika matendo utaonekana katika jamii zetu. Mtu atashikamanishwa na mwingine kwa kamba za dhahabu za upendo wa Kristo. Roho wa Mungu pekee ndiye awezaye kuleta umoja huu. Yeye aliyejitakasa mwenyewe, anaweza kutakasa wanafunzi wake. Wakiwa wameunganishwa naye, wataunganishwa kila mmoja na mwingine katika imani iliyo takatifu sana. Tunapopambana kwa ajili ya umoja huu kama ilivyo shauku ya Mungu kwamba tuutafute, utatujia. – Testimonies, kit cha 8, uk. 242,243.

If someone shows you that he can live without you, show him that you were born without him

Regrann from @zarithebosslady "if someone shows you that he / she can live without you, show him that you were born without him/ her ???- Mama 5 ?.... Stay humble but keep an inner beast that doesn't back down.? - #regrann

 Siku zote kuwa mtu wa kujinyenyekeza lakini usikubali kuwa mtumwa katika jambo lolote lile! Usikubali kumfanya binadamu mwenzio kuwa "Mungu mdogo" Yani bila yeye maisha yako hayaendi wakati ulizaliwa kutoka kwenye viungo cha mama yako ukiwa mwenyewe kwa uwezo wa Mungu aliye juu! Hata kama unampenda mtu kiasi gani epuka kumwambia  kuwa I can't live without you! Huo ni uwongo uliuopitiliza kwani watu wanafiwa na watoto zao na bado wanaishi baada ya mazishi! Sasa huyo mwanaume au mwanamke ambaye mmekutana  ukiwa unajua mema na mabaya ana nini haswa cha kukufanya ushindwe kuishi bila yaye?! Pia kumfanya mtu kuwa nimuhimu sana kiasi cha kugharimu maisha yako inamaana umemuweka huyo mtu katika nafasi ya Mungu! Na hiyo ni dhambi! I love yoy but I love you enough to let you go! Usikubali kuwa mtumwa kwa mtu asiye kujali au kudhamini utu wako. "if someone shows you that he / she can live without you, show him that you were born without him /her"! Kama wakionyesha kuwa uwepo wako au kutokuwepo kwako hakuadhiri kitu chochote katika maisha yao basi nawe huna budi kuwakumbusha kuwa ulizaliwa bila wao kuwepo!