Regrann from @j_n_mengi – @molocaho_by_amorette is giving you a ONE DAY ONLY Easter sale 20% off on everything bought on the 31st March. – #regrann
All posts by Alpha Igogo
Zamaradi Mketema: Mtazamo wangu- Part 1
Regrann from @zamaradimketema - PART 1 Wanawake kulegalega kwenye majukumu yao kunachangiwa sana na wanaume kuacha na kusahau WAJIBU wao ndani ya nyumba, lazima tuwe wakweli hivi vitu vinaenda pamoja Kumekuwa na malalamiko mengi juu ya wanawake sikuhizi kuwa si watu wa kujali nyumba zao kama ilivyokuwa awali, na mzigo mkubwa wa lawama unatupiwa wanawake bila kuangalia kulia na kushoto kwenye MIANYA ya VYANZO vya namna hii Katika majumba mengi sikuhizi ni ngumu kutofautisha nguvu ya mwanamke na mwanaume katika kile kinachowekwa mezani (kipato), zamani ilikuwa Baba ndio anaengaliwa kwa macho yote lakini sikuhizi wamama wamekuwa na mchango mkubwa sana kwenye familia nyingi, kitu ambacho ni kizuri na wote tunakubali, TUNACHOSAHAU kila Zuri linakuja na athari zake, tusifurahie tu mazuri halafu tukataka kufumbia macho NGUVU ZINAZOTUMIKA na JASHO LINALOTOKA katika kuleta mazuri hayo. Hata vitabu vya MUNGU naamini vya pande zote vilizungumza juu ya MWANAMKE KUZAA KWA UCHUNGU na MWANAUME ATATAFUTA KWA JASHO. Lakini leo hii vitu ni tofauti, mwanamke haangaliwi kama mwanamke tena, na ndiomana hata waoaji wengi wa sikuhizi (sio wote) wanataka mwanamke atakaekuwa angalau na mchango kwenye familia, matokeo yake mwanamke anabeba misalaba yote na zaidi, atazaa kwa uchungu, atalea kwa mapenzi, na sio watoto tu hadi Baba, ataangalia na kulinda nyumba, na majukumu yote ya mwanamke yanayoonekana ni ya kwake, na pamoja na hayo yote BADO ATATAFUTA KWA JASHO, ambalo si jukumu lake, na kwa jinsi wanawake wa sikuhizi wanavyoweza kuchakarika hakuna ajabu ya kuona anachokileta nyumbani yeye ni kikubwa kuliko cha baba, kweli bila hata kufikiri mara mbili unaendelea kulaumu nwanamke wa namna hii kuwa labda hakai chini kumfulia mumewe n.k, hebu jiulize kuna MAJUKUMU MANGAPI yasiyo ya kwake anayojikuta ameyabeba!! Na huenda yalistahili kufanywa na mwanaume, Kazi yake sio kutafuta kwa jasho lakini anatafuta, na huenda bila yeye kuhangaika watoto hawatasoma inavyostahili, mbali na hiyo bado atahangaika kuhakikisha kila kitu kiko sawa nyumbani hata anapokuwa mbali, hali ya kuwa Baba ni Baba tu na jukumu lake moja tena mara nyingine HALIFANYI INAVYOTAKIWA, maana wanaume wengine utakuta aki
Wema Sepetu: Kama najiona meza ya mbele kabisa
Regrann from @wemasepetu - Kama najiona Meza ya mbele kabisa... sio kwa nilivyo wamiss jamani... A show not to miss... . Miaka 14 hatujazisikia sauti pendwa ,Mziki mzuri, na burudani ya Baba na mwana Sasa kwa kulitambua Hilo Roof top entertainment na King solomoni wanakuletea *The Vikings*.. huku *mzee nguza* pale *Papi kocha* na ndugu zao *Barnaba*, *bushoke* wakiwa na *the Mafik Band* woooote hao katika stage Moja.. Usiku wa Tar 10/03/2018, *King solomon Namanga*. VVIP table ni milion moja, VIP 50,000 na VIM ni 20,000tu. Book mapema meza kupitia 0684083083 na 0677900731 Burudani Kali wa watu wakali Tanzania. Njoo burudike na *Baba akiwa na mwana*✨@papiikocha2 - #regrann
Mrs Nyagilo: Happy 11th Wedding Anniversary to me and the husband of my youth
Happy 11th Wedding Anniversary to me n the husband of my youth, my business partner, my best friend, father of my kids, chaupole wangu hanaga neno mwenyewe...If I could choose again, I'd still choose u. Missing u and I can't wait to come back home. To my In laws, please bring some more cows to my parents??. Love u all
Happy 11th Wedding Anniversary!
Happy 11th Wedding Anniversary to Mr and Mrs Nyagilo. Miaka 11 ya ndoa hatujasikia kesi wala kushuhudia majibizano kati yenu, lakini wengine hata ndoa bado kesi zimezagaa kila kona ??? Kweli watoto wa mwenye 'haki' ni baraka kwa wengine!..... Happy Anniversary my babysister what a lovely day to celebrate it with me ??❤
Watoto wa mwenye haki! Zaburi 37:25-26
Zaburi 37: 25-26 :-
“25 Nilikuwa kijana na sasa ni mzee;
kamwe sijaona mwadilifu ameachwa na Mungu,
au watoto wake wakiombaomba chakula.
26 Daima huwapa wengine kwa furaha na kukopesha,
na watoto wake ni baraka.”
❤
❤
❤
Psalms 37: 25 -26 :-
“25 I have been young, and now am old,
yet I have not seen the righteous forsaken
or his children begging for bread.
26 He is ever lending generously,
and his children become a blessing.”
Once you stop hating, you’ll start loving. Once you stop loving, you’ll start hating. Make love your choice!
Regrann from @cheyennebbostock – Yes, we descend from Africa, yes our ancestors were brought here against their free will, yes they were raped, tortured and killed, yes they were sold into slavery, yes they were not paid for their labor, yes we are still affected mentally, emotionally, and financially as a result of their wrong doings, yes racism still exists, BUT… what was done to our ancestors is nothing in comparison to what was done to Jesus and he forgave them, and he died for us. Are you willing to forgive and love again? Not just black people, but ALL people. Even your enemies.
Once you stop hating, you’ll start loving. Once you stop loving, you’ll start hating. Make love your choice! We all have sins we wish could be forgiven and forgotten. Extend the same grace you would want others to extend to you. Everyday should be Love Day! Everyday is Black History and ALL History! Make love your choice! Not hate. ?? – #regrann
Rabierth Samrabs: Watanzania tuipende nchi yetu. Siasa si vita
Ukomavu wa Kisiasa Si Kuleta Maandamano na machafuko ya Kisiasa Katika Nchi. Nchi iliyokomaa Kisiasa huzingatia Amani na Usalama wa Raia wake. Watanzania Tuipende Nchi yetu. Siasa si vita. Siasa ni ukombozi wa Kifikra Kwa Lengo la Maendeleo ya Taifa.
Jokate Mwegelo: USIKATE TAMAA, BADO LIPO TUMAINI
Kabla hujakata tamaa hebu jiulize ni watu wangapi wanaokutegemea? Ni wangapi walioko nyuma yako ambao wanatiwa moyo na mafanikio yako? Ni wangapi ambao wanaku-support? Ndio ujue kuwa kukata kwako tamaa kutaumiza wengi. Hata kama unahisi kuchoka hebu jitie moyo kwaajili ya hawa. Kumbuka maadamu unapumua bado unaweza kufanikiwa. USIKATE TAMAA, BADO LIPO TUMAINI. (Luka 18:1) #KIDOTI cc @pastor_nick_shaboka ❤
The Taste of Tanzania by Miriam Kinunda
Miriam Kinunda ni author of the Taste Of Tanzania. Kitabu cha mapishi kinachoelezea kwa mahiri jinsi ya kupika mapishi ya Kitanzania na East Africa. Kitabu kinapatika Amazon. Kuona kipaji chake cha mapishi nenda kwa YouTube channel yake, na Instagram page yake; vyote vinapatikana kwa kuandika jina lake Miriam Kinunda.
Zamaradi Mketema: Ni Makosa yetu wanawake
Regrann from @zamaradimketema -Kwenye comments nimegundua wanawake wanalalamika na mzigo wanaoubeba wao kwenye majukumu ya familia, ila MAKOSA mara nyingi yanaanzia kwetu, wanawake wengi WANAWALEMAZA sana wanaume wao wenyewe kwa kuhisi wanawasaidia, kwa bahati mbaya hii haina faida kubwa mbele ila hasara.
Tukirudi kwenye nature mwanamke ameumbwa kutunzwa hata vitabu vyote vya Dini vinasema hivyo, na ndiomana ikiwa tofauti madhara tunayaona, mwache mwanaume awe mwanaume hata kama umemzidi kipato, nature ya mwanaume ni KUTOA na kujihisi ANAMILIKI na ndio uanaume wake unapokuja, anapokutunza anafeel uanaume wake, hata uwezo wa kunguruma anaupata ndani, mpe hiyo nafasi usimnyime, hata kama wewe una mia yeye ana kumi hakikisha katika kumi yake lazima utaratibu wake wa kulisha nyumba ubaki palepale kwa kidogo chake hikohiko, we utatumia tu akili jinsi ya KUMSAIDIA ila usimlemaze akaona wewe ndio kilakitu na kumpa nafasi ya kutulia, hakikisha kila anapotoka anaacha kinachostahili hata kama ni mia tano, mfanye awe mume, maana athari za wewe kuibeba familia mara nyingine zinaenda pabaya zaidi hadi kuharibu mahusiano.
Na ndiomana kuna fikra isiyo rasmi kuwa wanaume wengi wanaoishi na wanawake wenye uwezo zaidi yao hutafuta nyumba ndogo pembeni za hali ya chini na kuzihudumia kwa hikohiko kidogo, lengo ni kutaka kuutoa uanaume wake, anataka mamlaka yake yaonekane, anataka akiongea asikilizwe, mpe nafasi hata kama una uwezo, hiyo ndiomaana ya kuwa KICHWA mfanye awe kichwa kwa vitendo, hata kwa umasikini wake onesha unamtegemea yeye na umtie moyo afanye kadiri ya uwezo wake, sio ndio unazo basi yeye anakuwa kama mtoto mdogo sasa ndani unamuacha moja kwa moja hapana, au unajifanya huhitaji kitu kwake unakosea. Ukitaka kujua hii ni nature hata kwa upande wa wanawake ndiomana hakuna feeling nzuri kama kupewa/kutunzwa na mwanaume wako hata kama una kilakitu, sababu nature iko hivyo!! Ndiomana si ajabu kukuta mwanamke tajiri lakini akamtamania mwenzie wa hali ya chini kwa kununuliwa mkufu tu, pamoja na kupata kilakitu kwa jasho lake bado kuna kitu kinamiss, kuona mtu anasimama kwake kama MLINZI na mtunzaji wa maisha yake, MUNGU ndio kaumba hivyo!! Ila siku hizi eti wanaume ndio wanalindwa. Ni Kosa!! Regrann from Zamaradi Mketema
Usitumie simu ikiwa kwenye umeme, ni hatari!….. Don’t use cellphone while charging, it is dangerous!
Binti ameungua uso baada ya simu ya mkononi kulipuka usoni mwake! Binti huyu ambaye anasadikika kuwa ni mdogo wake Mansour Yussof Himid na Shadya Karume alikuwa akitumia simu wakati ikiwa kwenye charger nahapo ndipo ilipo mlipukia na kuunguza uso wake vibaya sana kama inavyo onekana kwenye video! Jamani tahadharini kutumia simu ikiwa iko kwenye charge please! Na watoto pia musiwaruhusu kutumia simu mda mrefu zina athari mbaya please!
You may heard the warning before you thought was just a rumor and cared less! Or nobody warned you before and now it’s time to take it seriously! Using cellphone while charging it is DANGEROUS!! It may explode right on your face. See the video attached how that beautiful girl’s face is damaged from using her phone while was charging! Don’t do it!!
Rais Magufuli: Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria
Jokate Mwegelo: Hukustahili kufa kwa namna ulivyouawa
Regrann from @jokatemwegelo - Such a beautiful innocent young woman. ??❤ Aquilina Akwilini Baftaha, umefariki ukiwa kijana mdogo sana, kwa wakati ambao ndiyo haswa unatakiwa katika Jamii. Kifo chako kimetushtua na kimetugusa. Inawezekana tumeguswa kwa sababu mbali mbali na tofauti, ila tu uhakika ni kuwa imetuuma. Wengi tulikuwa hatukufahamu, lakini leo hii unawakilisha kundi kubwa la vijana wadogo kama wewe walio chuoni, na katika mioyo yetu tunajua inavyouma kumpoteza mtu wa hivyo. Haswa kwa namna ambayo umepoteza maisha kama mshumaa uliozimwa ghafla. Hukustahili kufa kwa namna ulivyouawa. Mwenyezi Mungu awape nguvu, imani na amani ndugu na jamaa wako wa karibu na kila aliyeguswa kwa kifo hiki cha kusikitisha. R.I.P Aqualina ❤ - #regrann
Aquilina, pumzika kwa amani ya Bwana Mungu!
Nashindwa niandikaje kwa jinsi nilivyo umizwa na kifo cha huyu binti! This is too painful, inhumanity, and wrong in all levels!! Siwezi kunyamaza kwani mimi ni Mtanzania! Siwezi kunyamaza kwani mimi ni mama! Siwezi kunyamaza kwani mimi ni mwanamke!! Nimekataa kunyamaza kwa hili!!! Baba yangu Dr John Pombe Magufuli nakuomba ukemee huu unyama hadharani!!! This has everything to do with humanity and leadership. As a leader of our country you should condemn these kind of acts!! As a father of many, this beautiful, precious soul could have been one of yours!! You need to take action ASAP!! This should have never happened, it's scary that it is a fact its happening in Tanzania right in front our very own eyes!! That is not the Tanzania we want!! Mambo kama haya siyo ya kuyanyamazia hata kidogo!! .... Rest in eternal peace Aquilina, justice we surely be done!!
Maria Makonda: Kamwe sitakuacha wala kuinamisha sura yangu na moyo kusononeka juu yako
@Regranned from @nikypal8585 - Asante Mungu kwa wema wako na fadhili zako juu ya maisha yangu mimi na Mume wangu kipenzi nipendezwae nae kila siku. Nakushukuru Mungu kwa ajili ya zawadi ya mume wangu huyu kwani amekuwa rafiki na mlezi kwangu hata kama kunachangamoto nyingi ktk maisha kamwe sitakuacha wala kuinamisha sura yangu na moyo kusononeka juu yako. Wewe ni furaha yangu kila siku? ninakuombea sana kila gumu na baya lipite mbali kwani hata Mungu aliye mbinguni anajua mlinzi wako na mke wako wa pekee yuko kazini kumwita juu ya maisha yako. Wewe ni zawadi na moyo wangu hauna kipingamizi. Heri ya kuzaliwa roho yangu ,mume wangu mwenyewe nakupenda sana???❤❤????❤❤❤? - #regrann. Happy birthday brother Paul Makonda! Ubarikiwe sanaaaa! Much ❤
Zari Hassan: I have decided to end my relationship with Diamond, as my RESPECT, INTEGRITY, DIGNITY & WELL BEING cannot be compromised
@Regranned from @zarithebosslady - Understand that this is very difficult for me to do. There have been multiple rumors some with evidence floating around in ALL SORTS of media in regards to Diamond’s constant cheating and sadly I have decided to end my relationship with Diamond, as my RESPECT, INTEGRITY, DIGNITY & WELL BEING cannot be compromised. We are separating as partners but not as parents. This doesn’t reduce me as a self-made individual, and as a caring mother, and the boss lady you have all come to know. I will continue to build as a mogul, I will inspire the world of women to become boss ladies too. I will teach my four sons to always respect women, and teach my daughter what self-respect means. Unlike many, I’ve been in the entertainment industry for 12 years, and through all my challenges I came out a victor because I am a winner, and so are all of you Zari supporters. HAPPY VALENTINE'S - #regrann
2018 Hottest And Best Couple Of The Year
Tulikutana na mke wangu Sayuni kwenye harusi ya mdogo wangu Linda iliyofanyika Dar miaka saba iliyopita. Sayuni alikuwa mmoja wa wasimamizi kwenye harusi ya Linda na walisoma darasa moja Chuo Kikuu cha Mlimani Dar. Tuliendelea kuwasiliana niliporudi Columbus na mwaka uliofuata alihamia Columbus..Tulikuwa katika urafiki kwa muda wa karibu miaka miwili na uhusiano wetu ulizidi kuimarika na kufikia makubaliano ya kuoana. Tulipendana na kukubaliana kufunga ndoa Septemba 2012 hapa Columbus. Ni mambo mengi yalinivutia kwake na kunifanya nizidi kumpenda na hasa busara zake na ushirikiano wake katika mambo mbalimbali ya maisha. Baada ya kukubaliana kuoana, tulianza maandalizi ya harusi. Tulipata ushirikiano mkubwa wa marafiki na ndugu mbalimbali hapa Columbus na nje ya Columbus. Tulifanya vikao vya maandalizi na tunamshukuru Mungu tulipata ushirikiano mkubwa na mzuri kutoka kwa kamati ya maandalizi. Kama nilivyosema hapo juu, busara za Sayuni na ushirikiano zilizidi kunivutia. Kila nilipokuwa napata changamoto za kazini au za kimaisha na kumshirikisha alikuwa akinishauri vizuri na kufikia hatua ya kuaminiana zaidi. Na mpaka sasa ni mshauri wangu mkubwa na ninathamini hekima na busara zake. Vilevile Sayuni ni mtu asiye kata tamaa katika kutimiza malengo aliyoyapanga au malengo tuliyokubaliana kuyatimiza. Nimezaliwa na kukulia katika familia ya kikristo. Moja ya imani niliyokuwa nayo ni kumcha na kumwamini Mungu. Ninaamini kwamba ndoa ni baraka na pia agizo la Mungu hasa inapofika muda wa kuanzisha familia. Katika sala zangu ilikuwa ni pamoja na kumwomba Mungu anifunulie na kunionyesha mke mwenye busara, hekima, mcha Mungu na tutakayeelewana. Hivyo kabla hatujaoana na Sayuni, niliona hizi sifa nilizokuwa nikiziweka kwenye sala zangu. Katika ndoa, sio wakati wote ni wa raha. Kuna wakati ambao tunatofautiana katika maamuzi. Kutofautiana ni jambo la kawaida. Kwa mtazamo wangu, kutofautiana katika maamuzi/mitazamo ndio kunakamilisha mapungufu ya kila mmoja wetu. Hivyo, ni vema kila mmoja akaheshimu tofauti za mwenzake hata kama hakubaliani nazo. Hii inachangia kuendelea kujenga uhusiano imara na kila mmoja kuwa wazi kwa mwenzake badala ya kuogopana. Communication is the key thing to us. Pia learning to compromise/meet each other half way inatusaidia kuimarisha umoja wetu.
Mimi ni kaka mkubwa katika familia yetu, ninapenda kuona wadogo zangu hasa wa kike waliopo kwenye ndoa wana amani na furaha na ndoa zao. Ushauri wangu kwa vijana wanaotaka kuoa, ndoa ni baraka. Kila ndoa ina changamoto zake. Kabla ya kufikia hatua ya ndoa, omba Mungu akuongoze katika kumpata mke mtakayeelewana na kupendana. Wapendwa wasomaji wangu, niliwaahidi kuwa sita waangusha! Hii ndio 2018 Hottest And Best Couple Of The Year. Nakumbuka katika busara za marehemu Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere siku moja alikua akitoa busara juu ya kuchagua viongozi wa Taifa la Tanzania alisihi Watanzania kuwa mchague kiongozi ambaye hata wakimtizama machoni utajua huyu anasema kweli tunaimani naye! Basi hivyo ndivyo nami nilivyo itizama hii couple haswa nimemtizama kwa kina sana kaka yangu Jackson Lyimo nikaona moyo wangu unaimani naye, na hata macho yake yananipa imani kuwa siyo tu kaka bora bali pia ni mume mwema! Heshima yake kwa wanawake ni kubwa sana, matendo yake yanajidhihirisha hilo! Hivyo pasipo shaka naomba nitamke rasmi kuwa hii couple ndio chaguo langu kwa mwaka huu. Nawaombea ndoa njema sana, iliyojaa baraka nyingi mno na amani tele. Wabarikiwe wao na uzao wa tumbo lao pamoja na wageni wote waingiao ndani ya malango yao!. Congratulations to Mr and Mrs Lyimo and happy Valentine's Day. I love you guys so much ??
Happy Valentine’s Day to you!
Happy Anniversary Mr and Mrs Nyongo
" O God, we thank you that you have given us another year of life together. We thank you for the love which grows more precious and for the bonds which grow more close each day. We thank you for the happiness we have known together; for the sorrows we have faced together; for all the experiences of sunshine and of shadow through which we have come, up to today. Talitha Koum ♡ Happy Anniversary to US #Mr&MrsNyongo# AKA #Son&DaughterofMajorOne#Happy Anniversary, Aidan Nyongo ! I love you deeply! Dear God, I pray that you would continually bless our marriage! That You would be the center that holds us together. That you would clothe us with You, so that we may continually love & respect one another! Thank-you for bringing us together, & for these precious years we have had the privilege of spending together!To my Valentine on our anniversary! "♡♡♡♡ Mrs Nyongo Happy Anniversary Mr and Mrs Nyongo! Mungu azidi wabariki sana, ndoa yenu idumu milele katika Bwana! Ukabarikiwe uzao wenu wote hata kizazi cha tatu na cha nne na wote waingiao ndani ya malango yenu! Happy Valentine's day to you! happy anniversary to you! I love you guys ?