All posts by Alpha Igogo

Makamu wa Rais asherekea siku yake yakuzaliwa na watoto yatima!

Muheshiwa Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan siku ya Jana ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa. Katika kuadhimisha siku hiyo muhimuhi Makamu wa Rais alijumuika na watoto yatima wa kituo cha Mtakatifu Gaspar kilichopo mjini Dodoma na kula nao chakula cha jioni. 

Kwa kupita account yake ya Instagram Mh. Makamu wa Rais alisema  “Jioni ya leo nimejumuika na Baadhi ya Watoto Yatima wa kituo cha Mtakatifu Gaspar cha mjini Dodoma kwenye chakula cha jioni ikiwa sehemu ya kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa.”  Hayo ndio yalikuwa maneno yake ya shukran ya siku yake kuu. 

Nasi kwa Mara nyingine tuna mtakia kheri, baraka, na afya njema mama yetu. Mungu azidi kukuongoza na kukulinda ili uzidi kulitumikia taifa letu vyema!  Happy birthday mama! ??

Hoyce Temu: shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ?? Mh. John Magufuli na mkewe Mama Janet

@Regranned from @hoycetemu  -  Done! Mungu ni Mkubwa na kwa Mara nyingine miminatanzania inatoa shukrani za Pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ?? Mh. John Magufuli na mkewe Mama Janet kwa kuchangia milioni 15 ambapo Sasa zikichanganywa na milioni 15 zilizopatikana kutoka kwa watanzania kupitia miminatanzania tutakuwa tumefikia kiwango na hata kuvuka. @wastara84 mdogo wangu, kila la kheri na muamini Allah na usikate tamaa. Hivyo basi mahesabu ni kama Ifuatavyo: Mh. Rais-15m, Miminatanzania 15m, Msamaria mwema aliyeweka kwenye account ya Hospitali India 7m, familia ya Wastara 5m JUMLA ni 42m zaidi ya lengo la milioni 37! Kila la kheri Wastara! Asante Tanzania! ????#tumeweza #jamii

Mzaha, mzaha, hutumbua usaha!

Katika maisha kuna vitu vya kufanyia mzaha na vingine usijaribu hata siku moja! Kitu chochote kinacho husisha HISIA za mtu usifanyie mzaha hata siku moja! Kumbuka hisia za mtu ndizo zinazomfanya huyo mtu kuwa mtu, sasa kuzichezea hisia za mtu kwanza ni unyanyasaji wa hali ya juu, pili unaweza kuleta madhara makubwa sana kwa muhusika ambayo saa nyingine yanaweza sababisha kifo! Siku zote kumbuka  "mzaha, mzaha utumbua usaha"! Naomba niongee na watoto wa kike kwa hili, ogopa sana mwanaume anayekufanyia vituko halafu badala ya kukuomba msamaha anakimbilia kwa ndugu na marafiki zako kujisafisha kuwa alikuwa anatania tu au kukufanya wewe uonekani ni mtu ambaye ni tabu to get along with! Kama hujaoana na huyo mtu basi kaa naye mbali kabisa kwani huyo mtu ni MNYANYASAJI! Na anachokifanya hapo ni kuweka mazingira mazuri ya kukunyanyasa pindi atakapo kuoa na wewe usiwe na pakukimbilia kwani amesha "brainwashed" watu wako wakaribu kuwa wewe ni hard personal to get along with au wewe ni mtu unayechukulia kila kitu too seriously!! 

Mtu anayecheza na  hisia zako bila ya huruma huyo mtu ni wakuogopa kwani hisia za mtu siyo jambo la kuchezea! Halafu unapo taka kuliongelea wewe ndio mtu mbaya?! Kwa mfano, eti mtu anakudhalilisha kwa kupiga picha na mwanamke aliye zaa naye au mwanamke aliyekuwa akimdeti kabla yako nakuweka hizo picha kila kona za media halafu anasema "was just a joke"?! Tena anafanya hivyo zaidi ya mara moja? My friend, mkimbie huyo mwanaume kama unavyoweza kukimbia kifo! Unless unataka kuwa "celebrity" basi utakubaliana na unyanyasaji huo simnamuona Zari anavyo fanyiwa na Diamond?? Ndo Ucelebrity huo ??? No! Ain't Zari! I'm just a normal girl from KekoJuu who deserves love, respect, and happiness ??  Au kwa mfano, mlisikia ile mvua kubwa iliyonyesha hapo Dar es salaam  ambayo ikasababisha maafa makubwa sana na watu kupoteza maisha? Sasa wewe ndio mwanamke unaishi Dar es salaam, maeneo ya Jangwani, halafu mwanaume yupo Morogoro cha ajabu hata kukupigia simu kujua kama upo salama au umekufa hakuna! Tena unamuona yupo online akifanya yake? Then mtu huyu akisema anakupenda wewe  mtoto wa kike bado unamuamini?!! ??? Unless you want to marry your killer ndio utakubaliana na huo upuuzi kwani wanaume wa hivyo hakuheshimu wewe wala mahusiano yenu! Mwanaume wa hivyo hakujali wewe wala roho yako! Yani kifo chako hakimsumbui! 

Ukiyakubali mambo kama hayo kabla hujaolewa halafu ukaja olewa na huyo mtu basi tegemea hizo tabia ataendelea nazo mpaka ndani ya ndoa yenu na hautakuwa nalakusema! Atakapo sema mbona hayo nilikufanyia kabla ya ndoa na ukakubali kunioa utasema nini?! Au mfano mwingine, mwanaume anataka kukuoa wewe lakini mipango ya maisha yenu anaongea na watu wengine bila kukuhusisha?! ?? What does that tell you? You are just going to be a "trophy wife"!! definitely that is not a man to have family with!! Ipo siku atataka kukutoa roho yako halafu atasema alikua anataka kuona how will you react!! Emotional abuse siyo kitu cha kufanyia mzaha hata kidogo kwani mzaha, mzaha hutumbua usaha!

Pole sana Joyce Kiria!

Hii issue ya Joyce inasikitisha sana japo siyo jambo lakunishangaza kusikia unyanyasaji kama huo!..... Ma'am, nashindwa hata niandikaje kwani swala la domestic abuse kwa wanawake na watoto ni swala ambalo liko very near and dear to my heart but at the same time very sensitive to me! Niswala ambalo sipendi kuliongelea sana kwani bado linanikumbisha machungu mengi sana haswa kuhusiana na my dearest aunt ambaye ametangulia mbele ya haki!! Bado sijioni kama nina nguvu ya kuliongelea mbele za watu! Siku mwanaume akanyanyua mkono wake kunipiga aisee nitahakikisha hadi mama yake mzazi anapata "ngeo" ya kudumu!! Wala simpigi mimi namkodishia wahuni tu!! Stupid kabisa!! Hii karne ya 21 nani bado anapiga mwanamke?!! Tena hadharani kwenye gari?!! Halafu eti wapuuzi wanasema umekosea kusema hadharani, gosh! Anipige mimi aone mpaka CNN watamjua!.... Siku zote ukiona mwanamke amefikia hatua ya kuongea mambo yake ya ndani hadharani basi jua yamemfika!! Hana pakukimbilia asipo yasema ataishia kujiua!! Siyo kwamba hampendi mumewe hapana anampenda enough kutaka msaada wa nje waweze kumsaidia. You do what is best for you Joyce as long will save your life!! Wewe unafikiri kwanini mimi pia niliamua kuanzisha hii blog yangu?!! Niliona uonevu ninaofanyiwa nawapika majungu na kwakuwa Wabongo wengi ni wepesi wa kuamini uongo kuliko ukweli hivyo nikasema I need my own platform ambayo nitakuwa huru kueleze mambo yangu na kuweka ukweli hadharani ili kila mtu ajue! Niliona jinsi marafiki na ndugu walivyotumiwa kuwa maadui wangu number moja nikasema I am taking it to the public ili waone! Nakama mjuavyo njia ya muongo ni fupi, sasa hivi wenyewe wamefyata mkia! ......Hivyo Joyce usione haya wewe sema tu wenye akili zetu  tulinakuelewa sana! Hapo utakuta umeangaika kwa ndugu na hakuna msaada wowote zaidi ya vikao visivyo na mbele wala nyuma! Halafu siku hizi unakuta kila kitu wanaingiza siasa hata maswala ya familia yani kweli siku za mwisho Biblia  inasema shetani ataharibu familia na ndoa, na ndio haya tunashuhudia!! Kwanza huyo mumeo nikiongozi sasa kiongozi gani ambaye familia yake tu yawatu ambao naamini hawazidi 10 imemshinda kuongoza mpaka anampiga mkewe sasa ataongozaje jamii yenye maelfu ya watu?!! 

 Hii issue yako umenikumbusha kifo cha mtoto wa kaka yangu alikuwa anaitwa Joyce Kibindi. Mtoto wa watu aliangaika na mumewe eti ngoja yeye awe mjasiliamali uku amsapoti mumewe kwenda chuo kwani aliamini mumewe akimaliza degree vizuri basi atapata kazi nzuri na hali ya maisha yao itakuwa nzuri kidogo!! Ma'am, how wrong was she!! 

Mume kamaliza  chuo kapata kazi yenye mshahara nzuri kwani alikumbuka fadhila za mkewe!! Pombe na wanawake ndio walikuwa "mashosti" zake! Mke na watoto hana habari nao kabisa! Mtoto kaangaika kulalamika na kuitisha vikao kwa ndugu, wapi!! Wakina mama nao wimbo ni ule ule vumilia tu yanapita!! Mtoto wa watu alivumilia uvumilivu ukamshinda hakawa haoni pakukimbilia tena ISIPOKUWA KABURI!! At age of 28 with so much to live for Joyce committed suicide!! 

Kifo cha Joyce kinaniuma sana mpaka wa leo hii, yani hata hapa naandika machozi yananitoka kwani nakumbuka jinsi alivyokuwa mzuri, smart, charming, very kind lakini maisha yake yalifupishwa because of the failed society!! Yes, hii jamii inayolea wanaume kuwa "cold hearted killers" kwa kuweka mazingira ya malezi ya kunyanyasa watoto wakike ndio inayoleta matatizo haya yote!! Nawakina mama ambao wanashindwa kusimama kidete na binti zao kwa kukemea hizi tabia hadharani ndio wanao ongeza matatizo haya! Embu fikira kama mume wa Joyce angekuwa muungwana angesema kuwa mkewe ndio asome kwanza si Joyce leo angekuwa bado yupo hai na familia ikawa salama! Yani kuna baadhi ya wanaume wa Tanzania wana roho za paka!! Niwakatili sijaona mfano hata hawa walioko huku nje ya nchi wana roho zakishetani!! 

Halafu watajifanya kusingizia "siasa"!!  Wengine wanataka uongozi wa communities ili tu kuficha maovu yao!! Kwakweli hii inafanya unaogopa hata kumsapoti mtu kwani hizi betrays ni nyingi mno!! ........Sasa baadhi ya wanawake wanaojifanya wasomi ndio wapumbavu hakuna mfano!! Sitaki hata kuwasikia!! Anyway, pole sana Joyce, nakama unajisikia kusema wewe sema tuu usije kufa bure kwa kujifanya shujaa ushwara!! Wewe kuongea haya yote yanakufanya uwe shujaa kwa wanawake wengi tu including me!! Hata Mungu anasema jisaidie kabla sijakusaidia!!

Haya wale wapendanao siku yenu itakuwa hivi…!

@Regranned from @jidejaydee – Tickets Zinapatikana |
Samaki Samaki zote |
Shear Illusion ~Mlimani City|
Jackies Bar ~Masaki |
Serena Hotel |
#ValentinesDayNaLadyJayDee
#AllAboutLove
#AllBlackEverything
#JideLove2018

Hongera Mr and Mrs Uchebe

Vitu kama harusi au interview ukiona nimechelewa kuweka jua bado sijatizama nikitizama lazima niweke. Bora niwe wa mwisho kutoa pongezi au kusema lakini niseme kitu ambacho ni sahihi! Mimi siyo shabiki wa "breaking news" hivyo nablog kwa style yangu ambayo napenda nikiandika kitu naandika  from the heart na siyo ushabiki "maandazi"! Naamini ndio maana wasomaji wangu wako loyal sana kwani kunakuwa na emotional attachment.  ??? Imenibidi nicheke kwanza, mnamkumbuka Muhaya eeh? Naye amekuwa zilipendwa ?? Nani anataka kufa kwa stress maisha yenyewe mafupi haya ?? Sasa kuna siku aliniambia kuwa eti "wasomi" wengi hawana emotional attachment kwa watu au situation kwani hicho ndio kitu kikubwa wanafundishwa shuleni ???? halafu huyo huyo akimaliza kuongea na wewe anasema "I love you" ??? I wonder kumbe ndio maana maisha ya wasomi wengi wa Tanzania ni Fake kama degree zao eeh!! Ile degree ya Dr Mengi ndio yakweli  peke yake ?? ?? well,  mimi sijui kuishi a fake life sina sababu ya kunifanya niishi maisha ya uongo and I don't consider myself msomi so wakwende huko na degree zao ??........ Anyway back to Mr and Mrs Uchebe Hii harusi ya Shishi babe binti wa Donald Trump  niliona picha  nikampa hongera kwa Instagram account yake lakini nilijua lazima nikipata muda wa kuitazama nitatoa pongezi rasmi hapa kwa blog! Wenyewe  wanasemaga "better late than never"! ....... Hongera sana Mr and Mrs Uchebe, ndoa yenu idumu katika Bwana. Ukabarikiwe uzao wa tumbo lenu milele na milele!

Shilole ulipendeza sana mno! Ulikuwa kama katoto fulani hivi ambaye baba yake anapesa fulani za kumwagwa ?? tatizo sasa bibi harusi wewe ukawa unaongea utadhani MC ??  jamaniii! Najua unapenda kuongea lakini kha!  Mpaka unamwita mtu " Mbwa wewe" ? wewe kiboko ?? Halafu Mungu alivyokujalia sasa amekupa mume mpole utadhani siyo Muhaya ???  Yani huyu kaka ni muungwana sana, halafu siyo mtu wa social media muombe Mungu sana ili aendelee hivyo hivyo! Huyu Shilole atakufaa sana hakuna raha kama kuwa na mume mwenye kumjua na kumpenda Mungu na anajitahidi kukuweka wewe karibu na Mungu! Maisha bila Mungu ni ushetani mtupu asikwambie mtu! Mpende mumeo mwaya!

Nimempenda sana jinsi marafiki zako walivyokupa zawadi za kukujenga! Yale mambo ya kununuliwa dinner set na TV is sooo 70's!! Watu wanakuletea zawadi ya vyombo vya plastic?!  vyanini? kwanza vinaleta cancer ??? hizi ndio zawadi!

My JoJo!! Kanoga eeh!! CCM oyee indeed ??  Hongera sana kwa kumpa zawadi nzuri sana hakuna kama elimu haswa ya kujua jinsi ya kufanya kile kitu unacho kipenda! ........ Halafu nyie wasichana ambao mnajiita "celebrity" embu muige mfano wa kuongea kama Jokate hapo! Hakuna kitu kina boa nakuonyesha some sort of kutokuwa smart and insecure kama msichana asiyejua kuongea kwa mpangilio wa maneno ya kueleweka!!! Yani wale wasichana ambao wanaongea utadhani ndio wanaanza kuota meno!! Au utafikiri hajui kiswahili kabisa anaishia  na "aaa" nyingi zisizo na mpango!! It's just boaring kwakweli! ..........Mwisho huyo MC aliyevaa T-shirt like really!!! Huo ni utovu wa nidhamu kwakweli! Umeonyesha dharau sana kwa Mr and Mrs Uchebe!! Shame on you!! Kila vazi na mahali pake, huwezi hata siku moja ukavaaa T-shirt au ndala kwenye harusi ya mtu!! Labda kama wewe unaroho ya kichawi!! Halafu T-shirt yenyewe mbaya utafikiri umetoka mazoezini!! Kwa mara nyingine tena, hongera sana Mr and Mrs Uchebe, mbarikiwe sana.

Joyce Kiria: Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua

@Regranned from @joycekiriasuperwoman - Changamoto kubwa 2018 #Kipigo
Sikutegemea kama ipo siku kwa mkono wako ungeunyanya KUNIPIGA @kilewo2020mwanga ???? * Ukasahau kabisa! Ukasahau yooooote.. nimeharibu career yangu kupigania ndoto yako kwa kugawa watu wangu kwenye biashara zangu, nimepoteza ndugu jamaa na marafiki, umeniachia nimebeba mzigo wa familia kwa muda wote... Malipo yako ni KUNIPIGA/ KUNIDHALILISHA/ KUNITOA MACHOZI???
Umenipiga kwa sababu Mimi Ni MNYONGE siyo! SINA NGUVU, kwa sababu ni MWANAMKE Sina nguvu za kupigana na MWANAUME ... Umeniumiza mwili wangu unauma kila mahali umefiria damu na kichwa ukanigongesha kwenye gari, ili iweje? Nia yako ilikuwa ninini? kuniua??? Mungu amenipigania.

 Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua...?????? Kama NI Mimi niliandamana na watoto, nikakufanyia kampeni na deni kubwa nikaingia mpaka nikafungiwa Kipindi hewami, ninakutunza wewe na Watoto wako kwa miaka yote, MUNGU YUPO.... LEO UMENIPIGA @kilewo2020mwanga ??? Sawa watakusifia hao wanaokusifu ujinga, wanaokuambiaga Mimi sikuheshimu, badala wakwambie ufanye kazi utunze familia, Leo watakuona wewe ni MWANAUME kwa KUNIPIGA... - #regrann

Akin Al-Ameen: There is no such thing as fighting for love unless you’re both on the same page fighting for the same cause

Some people are naturally difficult, very hard to love. Never allow such people to take your happiness away. No matter how good your intentions are, never force kindness on people against their wish. Most people think loving them is a weakness. Always have a boundary. Sometimes accepting everything doesn’t mean you’re peaceful, it means you’re vulnerable and desperate for love. If you take everything, people will give you anything. Love is peace, and love is sweet but “IF LOVING SOMEONE IS GIVING YOU MORE SADNESS THAN JOY, LEAVE THEM ALONE AND LOVE THEM FROM FAR AWAY”. Never lose yourself while searching for the right person. The best you can do is to make yourself a right person. Try your best to save your relationship but if giving your best is not good enough, you’re probably giving it to the wrong person.

Mercy, Sammy, and Alpha

There is nothing bad in loving people from distance, that doesn’t mean you stop loving them, it simply mean you respect yourself and cherish your peace of mind. Always remember that everybody in life needs help. Sometimes staying out of some people’s life is the best way to help them. Love is not a favor, don’t beg for it. It’s not a war, don’t force it. You can never be in a relationship alone. There is no such thing as fighting for love unless you’re both on the same page fighting for the same cause. If your dream partner cannot see you in his/her own dreams means it’s time for you to wake up and stop dreaming alone. Never mistake a SITUATIONSHIP for RELATIONSHIP if you want peace of mind. Be honest with yourself. Never make a life changing decision based on your emotions alone.

Akin Al-Ameen®™2018

***My picture has nothing to do with the story***

Jokate Mwegelo: Muhimu kujipanga kutumia fursa hizi zinazotengenezwa na serikali zetu hizi

Jokate Mwegelo
Tarehe 14/01/2018. Rais Magufuli wa Tanzania alimkaribisha Rais @paulkagame wa Rwanda, Dar es Salaam- Tanzania katika ziara ya kikazi.  Katika ziara hii walirejea mazungumzo juu ya ujenzi wa reli kati ya Isaka na Kigali lakini pia reli hii itaenda mpaka Musongati- Burundi kupitia Keza. Reli iliyopo hivi sasa ni kati ya Isaka ambako kuna bandari kavu na Dar yenye urefu wa kilometa 970- reli ya kati. Na hii reli mpya kati ya Isaka na Kigali itakuwa ya urefu wa kilometa 494. Ujenzi huu utasaidia usafirishaji wa bidhaa na watu kwa urahisi na kupunguza gharama za usafirishaji lakini pia itasaidia kuboresha maendeleo ya kiuchumi. Nchi za Rwanda na Burundi na mpaka DRC ambazo ni “landlocked” watazidi kuona unafuu katika kutumia bandari yetu kutokana na usafiri kuwa wa kuaminika. Mradi huu unabeba pia dhima za EAC, CEPGL na COMESA zenye kuhamasisha “inter-state transportation structures”. Hizi ni hesabu nyepesi. Kwa miaka mingi maendeleo ya biashara ya bidhaa, huduma na usafirishaji wa mazao ya kilomo, madini mbalimbali n.k kati ya nchi za Afrika zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya gharama kubwa za uzalishaji ambapo pamoja na sababu nyingi zingine zimechangiwa sana na ukosefu wa usafirishaji wenye kueleweka. Ujenzi huu utasaidia kufungua maeneo haya na kugusa makundi mengi hasa vijana kiuchumi. Muhimu kujipanga kutumia fursa hizi zinazotengenezwa na serikali zetu hizi. Tufuate kule serikali inapowekeza na kuona jinsi gani tutaweza faidika. Pia tupende kujifunza juu ya mipango ya serikali na tuone tunanufaika vipi na tuhoji. Niwatakie siku njema. ❤️ 

Tegemeo Sambili: Ili tuendelee kwa haraka na watu wayaone maendeleo, nashauri tuongeze nguvu kwenye yafuatayo:-

Moja ya Makosa tunayoyafanya ni Kutaka Kuendelea kama Walivyoendelea Wajeruman, Wamarekan, China, France……. Kwa Upande wangu, Maendeleo yanaanza kwa Kula vizuri, Kulala vizuri, Kuvaa vizuri na kuwa na Afya njema. Ili tuendelee kwa Haraka na Watu Wayaone Maendeleo, nashauri tuongeze nguvu kwenye Yafuatayo:-

1. Kilimo Tulime sana kiasi cha kuwawezesha Watanzania kupata Chakula bora na cha kutosha. Nataman kuona Chakula kinakuwa kingi kiasi cha kilo 1 ya unga iwe Tsh 500, kilo 1 ya mchele iwe Tsh 1200, Karoti 1 iwe Tsh 50,pilipili hoho iwe Tsh 50, Nyanya fungu 1 liwe Tsh 200, Vitunguu Tsh 50, Nyama, Samaki….vipatikane kwa bei nafuu. Ikiwa Watu watapata Chakula bora, kwanza watakuwa na Afya , Miili yao itakuwa na uwezo wa Kujikinga na magonjwa na Wataweza kuishi miaka mingi. Life span ya Watanzania ni Fupi kwa sababu ya Chakula dhaifu…. JKT itumike kulima Chakula kwa ajili ya Watanzania.

2. Nyumba na Makazi bora Nataman kuona kila Kaya inaishi kwenye Nyumba ya kisasa.Lazima tuhakikishe watu wetu wanalala sehemu nzuri na salala.Katika kutekeleza hilo, serikali kwa kutumia Watalamu wa Majengo na Mipango miji, Wanaweza kuandaa Ramani za Nyumba za Mwongozo, zitakazoelekeza aina ya Nyumba ambazo watu Watatakiwa kujenga na Zigawiwe bure. Vifaa vya ujenzi Viondolewe Kodi na Serikali inaweza kushiriki katika kuvisafirisha hasa maeneo ya Vijijini ili Wakazi wa maeneo hayo Waweze kuvipata kwa gharama Nafuu. Serikali iwahamasishe watu Kujenga nyumba zao..

3. Mavazi Tuongeze nguvu katika kujenga Viwanda vya nguo. Watalamu wa Mavazi, wabuni nguo zinazowafaa Watanzania wa kike na kiume.Watu maarufu kama akina Kikwete watumike kuzitangaza ili kuwahamasisha Vijana kuvaa nguo hizo.Vijana wetu wanavaa uchi Kwa sababu wamehamasishwa kufanya hivyo na Hatuna Mavazi yetu mazuri

4. Huduma za Afya Tuwekeze nguvu kwanza katika kutokomeza vyanzo vya magonjwa…Pili tuhakikishe huduma bora za afya Zinazotibu Maradhi yanayowasumbua watu wetu haraka. Kuongezeka kwa Vituo vya tiba mbadala ni Ishara kwamba Hospital zetu zimeshindwa kutibu Maradhi yanayowasumbua watu wetu. Tukitaka kuendelea kama Wao, Hatutafika Leo wala kesho…… Tukiyafanya Mambo haya, Maendeleo yataonekana kwa kila MTU na kila Kaya ndani ya muda mfupi. Tunataka Kuona Tanzania inakuwa nchi ya kwanza Dunian kwa Watu wake Kula Vizuri…. Kulala vizuri , Kuvaa vizuri…..na kuwa na Afya njema… 

Dina Marios: Nilifanya kazi kama miezi minne bila kulipwa mshahara wala chochote.

Nakumbuka wakati naanza kazi 2005 nilifanya kazi kama miezi minne bila kulipwa mshahara wala chochote. Nilikuwa natembea umbali mrefu sana wakati mwingine sababu ya kukosa nauli ili kwenda kazini. Na hata nilipoanza kulipwa nakumbuka mshahara wangu ulikuwa 45,000 ulikuwa mdogo sana na hautoshi.Ila niliridhika kwa sababu nilikuwa najua ni mwanzo wa safari yangu na bado sina ujuzi kivile wala uwezo mkubwa.

Leo hii vijana wengi ninaokutana nao kutafuta ajira swala la kujitolea ni gumu kwao?kusubiri ni ngumu kwao kwanza wengi wavivu na bado wanataka kufanikiwa na kupata pesa.Mtu hafanyi kitu bila kuuliza nitapata nini???

Katika kutafuta kufanikiwa wakati mwingine fanya kazi hata za kujitolea usitangulize malipo.Hili litakupa nafasi ya kujijengea uwezo na kukupa wasifu utakaokusaidia kujipanga vizuri na pengine ukawa mwanga wa ajira ya malipo hapo baadae.

Mdogo wangu Mimi alonifatia alipomaliza chuo sehemu alikuwa anafanyia field waliona uwezo wake wakampa ajira lakini sababu alikuwa bado mdogo wakawa wanamlipa kidogo sana akawafanyia kazi miaka 4 bila mshahara kupanda. Kila siku ananiambia sister mshahara mdogo sana mie nataka kuacha kazi.

Nikamwambia usijihisi upo kazini fanya kazi kama vile upo chuoni chukua ujuzi na mafunzo. Fanya kazi kwa bidii am sure siku ukitoka hapo basi uwe umepata sehemu yenye kukulipa vyema na waseme wamepata jembe haswaaa. Mwaka mmoja baadae akapata kazi tena kwa kufuatwa sio yeye kuomba ambayo wanamlipa vizuri sanaaa na ameweza kutimiza malengo yake mengi sana.

Jiwekee malengo na mikakati hata malengo makubwa huanza kwa udogo. Sawa una elimu kijana na pengine ulihisi ukimaliza chuo tu utapata kazi ya ndoto yako na mshahara mnono. Ukija kwenye ukweli mambo wakati mwingine hayaendagi hivyo. 


Ukipata sehemu hata kama wanakwambia fanya bila malipo......fanya huo ndio mwanzo wako.Jijengee maarifa na uwezo.Jamani acheni uvivu.......acheni kutaka ghafla uwe una mihela unalipwa vizuri.Jitumeni mie nawaona wengi humu makazini wavivu. Na usigelezee mwingine alianzaje ukadhani mna safari moja hapa duniani.

Good Morning!

Edward Julius: BABA WA FAMILIA NI LAZIMA ADUMISHE UHUSIANO MWEMA NA JIRANI ZAKE

Edward Julius

BABA WA FAMILIA NI LAZIMA ADUMISHE UHUSIANO MWEMA NA JIRANI ZAKE:

Kiongozi makini ni yule ambaye anatambua ya kuwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi yake hayaji kwa nchi kujitenga na kujifanyia mambo yake peke yake, bali huletwa kwa juhudi za wananchi wake pamoja na kushirikiana vema na nchi majirani zake pamoja na jumuiya nzima ya kimataifa kwa mapana.  #VIVA_JPM

Happy birthday Foster Mbuna Mkapa!

" You (God) give beauty for ashes, comfort for pain and laughter for gladness in your name" (Isaiah 61) My heart is full of joy and gratitude as I look back at how far I have come. If it was not for you my heavenly father carrying and walking me through I don't know where I would be. I have seen myself growing physically, emotionally and spiritually. 

*I have faced pain so that I could comfort those in pain. 

*I have experienced loss so that I know the importance of having people around me.

* I have experienced reject to know the importance of not ignoring people or categorizing them because in your sight we are all equal. 

*I have experienced sickness to learn to appreciate good health.

* I have experienced happiness, satisfaction and peace to know that intangible things are what matter than materialistic things.

* I have encountered obstacles to learn that all blessings come from you and not to be judgmental because your timing is the best. I have learnt humility.

*I have encountered strangers who made my journey smooth to realise that the world is not cruel and strangers can turn to be your relatives/ friends if your don't confine yourself in your tiny world. Just do your part and the rest will fall into the right place.

* I have realized that change begins with me by letting go of all the negativity/grudges and the power of these 3 words; I am Sorry/ Please forgive me, Thank you and I Love you! 

Mama Foster na Foster
As I celebrate my birthday today, I am grateful to know that I am here alive today because that's exactly what and where you wanted me to be. I give you Glory and Honour because you knew me before I was formed, you know me from head to toe, you know my destination and you have great plans for me. As I live my life, may I walk and conduct myself according to your master plan. Help me to fulfil all my roles to the best of my abilities without complaining so that I can bring you back the Glory and Praise that you deserve. Grant me a compassionate, loving and a forgiving heart. Thank you for my parents, my husband, my sons, siblings, relatives and friends that make my life colourful, fun and meaningful. May I make their lives and worlds meaningful and wonderful as well. Amen. Happy birthday to me!
Ujumbe wako wa  shukrani kwa Mungu umetulia Sana!........Nami naomba nikutakie kheri na baraka zote za kuongeza mwaka mwingine katika maisha yako. Mungu azidi kukubariki wewe na uzao wa tumbo lako pamoja na watu wote waingiao ndani ya malango ya nyumba yako......Nimefurahi kumbe tulizaliwa hospitali moja ?? Ocean Road born babies we Rock!??..... Happy birthday beautiful ??

Mama Mbuna: Mungu wangu ninaye mtumikia akubariki milele yote

Wooh Mungu ni mwema mno. Ilikuwa siku kama ya leo (Alhamisi), tarehe kama ya leo (11/01/ mwaka uleeee, mnamo saa 09:30 mchana, mvua yenye utulivu ikiwa inanyesha, nikiwa pale Ocean Road Hospital, BWANA alinipatia mtoto mzuri wa kike tunayemuita Foster Mbuna Mkapa. Aliyefanya CV yangu ibadilike na kuanza kuitwa mama Foster tangu siku hiyo.  Nakutakia baraka zote za rohoni na za mwilini unapoisherehekea siku yako hii ya kuzaliwa. Kwa imani nakutamkia neno hili kwamba "hakuna silaha yoyote itakayo inuka juu yako ambayo itafanikiwa." Mungu wangu ninaye mtumikia akubariki milele yote. HAPPY BIRTHDAY TO YOU. MUMMY LOVES YOU!!!!!!

Embu tucheke kidogo

??? Inaelekea bangi ni “chakula” kinachopatikana kwa urahisi na bei nafuu sana Tanzania ????? Lemme just stay safely in America ??

Mh.Edward Lowassa: Amenifanyia siku yangu kuwa njema sana. He has made my day

Siasa ni sera na itikadi siyo chuki wala uwadui! Wenyewe wenye lugha zao wanasema 'Politics is just a game'!  Na hapo ndio mimi nasema tusilazimishane kuupenda au kucheza mchezo huu!! Acha wale wanaopenda siasa wahubiri siasa, wale wanaopenda mambo ya kumtukuza Mungu wahubiri injili ya Mungu, wambea na wadaku wote washinde Facebook na Instagram kufuatilia maisha ya watu!! Kila mtu afanye kile kitu roho napenda!! Kwani siyo wote tunaoweza cheza mchezo huu wa siasa, wengine hatujui ku-control hisia zetu kuweka siasa kwenye maswala ya msingi!! Nasisitiza mimi sio mwanasiasa! Tusipangiane maisha!!

https://youtu.be/ObH667FC0tc

"He has made my day" hayo ni baadhi ya maneno ya Mh. Edward Lowassa baada ya kuonana na Rais Dr. John Pombe Magufuli siku ya jana. Naona wanachama wengi wa  Chadema wana lalamika kuwa wamesalitiwa??! Nikabaki kujiuliza, wamesalitiwa?? ?? na nani tena?! Kama ni usaliti basi ulifanyika 2015 pale kiongozi wenu alipo mchukua mtu ambaye hakuwa mwanachama wenu na kumpa nafasi ya kugombea urais bila hata aibu!! Ule ndio ulikuwa usaliti!!  Eti kwanini Mh. Lowassa hakushirikisha viongozi wa chama kabla ya kwenda kumuona Rais?!! ?? What a madness!! Are these people really know what they are saying! Hivi ukiwa mwanachama wa Chadema maisha yako yote ni mali ya chama??!! ?? ....Anyway Mh. Mbowe kawaelimisheni vizuri sana katika hili.  Msikilize hapo ?? Mh. Lowassa ni raia wa Tanzania kama walivyo raia wengine, kuonana na Rais ni haki yake kimsingi!! Haitaji kibali cha mtu yoyote yule kuendesha maisha yake nje ya chama.

Kuna maisha nje ya siasa na hayo ni maisha yako wewe mwenyewe  hayamilikiwi na mtu yoyote! Una uhuru wa kujumuika, kufanya biashara, kula, kuoa, kusali na mtu mwingine yoyote yule ambaye siyo adui (mf. Mtu ambaye gaidi) wa inchi yako! Siyo ndugu zako wote ni wanasiasa au wafuasi wa chama chako sasa utavunja undugu kwasababu ya Siasa?!! Kuna watu naona wanaingiza siasa mpaka kwenye maswala ya ndoa? Jamani hivi hii ni Siasa au ushetani!! Ndoa ni agano takatifu, leo hii mnataka watu waliokula kiapo mbele za Mungu waachane kwasababu ya Siasa?!! Huyu shetani anaye waingia Watanzania niwakukemewa kwa nguvu zote!! Embu turudi nyuma kidogo, sinimekwambia kuwa wenyewe wanasemaga Siasa ni mchezo tu! Sasa hapo mastering wa hii game kwa upande wa Chadema ni Mh. Edward Lowassa na Mh. Freeman Mbowe! Kumbuka Mh. Lowassa alijiunga na Chadema kwa mkataba wa kupewa nafasi ya kugombea urais na hiyo ndio imekuwa nia na lengo lake mpaka wiki kama tatu zilizopita, msikilize ?? akiwa bado anaomba Mungu amsaidie kushinda Urais 2020

Umemsikia eeh! Wakati huo huo Mh. Mbowe ameshaona kuwa Mh. Lowassa is not a great candidate kwa 2020 hivyo target yake ni Mh. Tundu  Lissu.  Lakini kwakuwa bado anamuhitaji Mh. Lowassa kwaajili ya nguvu ya umma na kifedha inabidi aendelee kumlaghai akae ndani ya chama mpaka 2020 halafu wamfanyie ule mchezo aliomfanyia Dr. Slaa  ?? but Mh. Lowassa is too smart for that ndio maana anaanza kuwafanyia maigizo kwani ameshaona dalili za yeye kufanyiwa mchezo aliomfanyia Dr Slaa! ??? Hivi huwa wanasema eti "Karma is a........" and what goes around always huwa linarudi kinyume nyume eeh ?? I love it when politicians played themselves! Mh. Edward Lowassa amekwishaona hana tena maslahi yakudumu na Chadema sasa sibora arekebishe huku kwingine before it's too late! Nammemsikia akisema anaona miaka mingine 5-10 ya uongozi bora wa Dr Magufuli ??? should I say CCM oyee ee on behalf of CCM members or will I be morally wrong since I am a blogger I should stay neutral and keep my mouth shut ?? #IHatePolitics #HeHasMadeMyDay  Btw, swala la Mh. Lowassa kuwa ni mtu muungwana na mstarabu hata mimi niliwahi sema huko nyuma, soma ?? Mr&MrsMkapaGoldenAnniversary
NilisemagaHukoNyuma

2020, je! Oprah Winfrey atajitosa kugombea urais wa Marekani?!

Hatuba fupi aliyoitoa Oprah Winfrey wakati akipokea tuzo za Cecil B. de Mille Awards kwenye Golden Globes hapo juzi kati imefanya watu wengi wajiulize kama mwanadada huyo ambaye ni billionaire mwenye mvuto mkubwa wa kushawishi watu atakuja kugombea kiti cha urais ifikapo 2020! Oprah Winfrey aliongea kwa hisia kali kuelezea jinsi wanawake wanavyokuwa wakinyanyasika, kudhalilishwa katika nyanja zote za maisha, malalamiko yao yamekuwa yakipuuzwa siku zote nasasa wakati wa hawa wanaume wanyanyasaji  umefika mwisho, "their time is up" Oprah alisema kwa ushujaa huku watu wakimshangilia. Embu msikilize kwanza ?

https://youtu.be/fN5HV79_8B8

Kwakweli mimi nilikuaga siyo mapenzi au shabiki sana wa kuona Rais mwanamke, lakini jinsi nilivyokaa nikachukua muda wangu kuwatizama hawa wanasiasa wa kiume, honestly I now strongly supporting for a Female President! Their time is up for real! Labda tukiwa na viongozi wakuu wakike wengi kwenye dunia hii hali itabadilika kidogo, we may make this world a better place to live again! Hawa wanaume hakuna wanafanya zaidi ya ku-feed their stupid ego and using women as tools!!
Oprah Winfrey na mpenzi wake Stedman Graham
Kama Oprah aliweza kumfanikisha Rais Baraka Obama kuwa Rais wa kwanza mwenye ngozi nyeusi hapa Marekani, trust me with what is going on right now in America? Oprah Winfrey will definitely be the First Female President in America and she is BLACK!! .......Katika tuzo hiyo Oprah Winfrey ndio mwanamke wa kwanza muafrica aliyewahi pata tuzo hiyo. Sydney Portie're ndio alikuwa muafrica wa kwanza kupata, hivyo mpaka sasa ni hao wawili tu kwa upande wa watu weusi ambao wamefanikiwa kupata tuzo hiyo!

Je ulishawahi kufanya makosa kama yangu?

 Watu wengi wanatabia ya kupenda kuhisi vitu au kumuhisia mtu badala ya kumuuliza muhusika ili wajue ukweli! Hiyo caption kwenye picha ya Dina Marios imenifanya nikumbuke makosa yangu niliyowahi kufanya huko nyuma. Dina ameweka caption ?? isemayo "Msomali wa Kihaya"  kitu ambacho kimenishangaza kidogo kwani siku zote mimi nilihisi kuwa Dina ni Mchaga ?? Sijui kwanini lakini hivyo ndivyo nilivyo muhisi!   

@Regranned from @dinamarious – Msomali wa kihaya
#VipichaPicha
 Sasa haya mambo ya kuhisi vitu kwakweli siyo mazuri hata kidogo kama unayo hiyo tabia basi kuanzia leo anza kujifinza kuuliza kwa kila jambo ambalo hujui kwani itakusaidia sana! Mimi nilipokuwa secondary mmoja wa rafiki zangu alikuwa anaitwa Msolwa Mgawe, sasa huyu Msolwa kwa muda wote tupo shule sikuwahi kumsikia akimtaja baba yake katika maongezi yake. Utasikia kamtaja mama, kaka, na dada zake lakini si baba yake hivyo kwa akili yangu yakupenda kuhisi nikahisi kuwa huwenda baba yake alikwisha fariki hivyo hataki kumuongelea ?? ............ Sasa siku mmoja katika story sijui tulikuwa tunapanga kufanya nini ila akasema kuwa  yeye hatoweza kwani "mshua leo anarudi" akimaanisha baba yake anarudi! Nikashangaa, ikabidi nimwambie kuwa mimi nilihisi baba yake amefariki miaka mingi kwani sijawahi msikia akimuongelea baba yake! Yani group zima lilikufa kwa kicheko ??? Msolwa akasema Alpha sidhani kama una akili timamu ??? ..............Jamani kuuliza si ujinga bali ni kutaka kujua, na hata siku moja hakuna swali la kijinga isipokuwa wajinga ndio huwa hawaulizi maswali! Hacha kuhisi vitu au kumuhisia mtu kitu siku zote kama unaweza uliza but don't assume!! Kuhisi ni kubaya sana!

Msikilize Aunty Ezekiel akieleza historia yake na Moses

 Kama kuna wapendanao ambao nawapenda sana kwenye hii kitu inaitwa Bongo movie / Bongo flava basi ni hii couple! Mie sijawahi kaa kuangalia Bongo movie toka enzi ya Mambo Hayo (wahenga mtatujua tu ?) hata movies za marehemu Kanumba sijawahi kaa nikaangalia!Mimi siogopi kusema ukweli as truth will always set me free napia inanipunguzia marafiki wasio na tija ?? Mambo ya hawa wasanii wa siku hizi honestly yana nikera sana! Wengi tunawajua kwa scandle zao kuliko talent zao! Lakini kwakweli lazima nikubali kuwa Aunty na Moses wamenifanya nianze kuwachambua mmoja mmoja nakugundua kuwa kumbe kuna wengine wanajielewa na huwenda ipo siku moja nitakaa chini kuangalia Bongo movie tena! Natamani wasanii wakike wa aina zote wangekataa huu udhalilishaji wa wanawake unaotumiwa na promoters na media eti "kutafuta Kiki" kwa kuwekwa kwenye scandle zisizo na kichwa wala miguu ili kazi yako au kipaji chako kionekane! Huu ni udhalilishaji period!! Kama mtu ana talent tafuta njia sahihi ya watu kuona talent yake nasio kuwapa kashfa za kutembea na wanaume!! If someone got talent people will see it!! Chema chajiuza kibaya chajitembeza!!!

Anyway, back to Aunty Ezekiel na Moses wake, kumbe jina la Aunty ni jina lake halisi aliyopewa na baba yake! Mimi nilifikiria ni jina la kuigiza ? ......Halafu wewe Moses wewe huyo shetani aliyekuingia sijui alitokea wapi, sasa sisi tungemuona wapi Cookie?! ......... Please people interview ipo very raw  yani Aunty Ezekiel kafunguka haswa lakini usishangae sana kwani hayo ya kutoa mimba na kwenda kwa waganga ni mambo alifanya wakati huo yupo kwenye "giza nene" Ni mambo ya kale! Don't judge  if you know what I mean ???  Hey every Saint has a past, every sinner has a future, and who are you to judge anyone!

Babu Sea anakuja na nyimbo ya Kijaluo?!

Nimekutana na news za Babu Sea na wanawe wakitangaza kurudi kwenye uwanja wa muziki kwa nguvu zote! Sasa nikasikiliza hii video fupi ya mahojiano yao, katika hizo nyimbo mbili zilizopigwa chorus zake hiyo ya pili imeimbwa kwa Kijaluo! Au Wajaluo wenzangu mnasemaje? Nimesikia vibaya hayo maneno au ni Kijaluo chenyewe?!! Embu msilikize….

https://youtu.be/y1L_qid_t-Q

Kijaluo lugha hatari eeh! Inapendwa kila kona, haya mtuletee tuisikilize but honestly I don’t know how to sincerely feel about it! Anyway, who am I to judge!