@Regranned from @zamaradimketema - Ninapoongelea kufanya VITU VIDOGO katika hali ya UKUBWA maana yangu huwa ni hii. @porridge_point ameniinspire hata mimi, kwanza ni degree holder, na wasomi wengi huwa tunaona mawazo yao hata ya kibiashara huwa ni makubwamakubwa tu, ila huyu baada ya kukosa kazi ameamua kuuza UJI, biashara inayoonekana sio ya hadhi yake labda kutokana na elimu yake, ila hakuangalia hilo sababu aliifikiria kwa ukubwa, huenda sio ishu kuuza uji, ila jinsi anavyouza ndio kulikonivutia, kuna wauza uji wengi mitaani kwenye machupa, lakini yeye ameona AONGEZE THAMANI, ameamua kwenda extra mile na kuwa mbunifu kwa kuwa na hizo take away cups zinazofanya yeyote ajisikie hata fahari kubeba, na hata sehemu yake ya biashara ameifanya tofauti na jinsi wauza uji wengine wanavyojiachiaga. Sidhani kama nikikupa Laki itakusaidia zaidi ya hiki, nimeona nikupe muda wangu ili kuelezea Dunia nini unachokifanya,na zaidi kuweka contact zako hapa huenda ikafungua njia zaidi kwako, nimeona anasambaza hata kwenye mikutano ya kiofisi mbali na watu kumfata, kwa watakaopenda kuwasiliana nae namba zake ni 0654 197952, swipe kuona picha zaidi ama mfollow ili kuangalia anachokifanya. Hongera sana na MUNGU abariki juhudi zako mama - #regrann
All posts by Alpha Igogo
Mwanamuziki wa Kihaya mwenye asili ya “Donald Trump”!
Katika pita pita yangu huko Instagram nikakutana na huyu mwanamuziki wa Kihaya mwenye asili ya "Donald Trump'' ?? hapana chezea Wahaya siyo watu wa spoti spoti ati ?? wenyewe mambo yao ni ya kimataifa tu kama ilivyokuwa magonjwa yao hayana tiba ndani ya Tanzania dawa zao lazima ziagizwe nje ya nchi ????? wanajua kuringa hawa watu ?? Mzuri eeh! Anaitwa Abela, Instagram page yake ni "Abelamusic" embu follow her ukamsikie mwenyewe. Mie nimempenda sana, yani pamoja na kwamba ana ishi Marekani lakini anakwenda mpaka kwao Bukoba (naona baba yake ndio Muhaya) kusalimia ndugu zake, ana andika Kihaya bila shaka atakuwa anakiongea, huwezi amini anakula mpaka wale "funza wa Kagera" a.k.a "Senene" she is no Diva at all! Very down to earth just by looking at her pictures you can tell all!! Natamani nimjue zaidi! Pia na mama yake mzazi natamani nimjue ili aniambie ilikuwaje akamlea hivi maana wamama wengine mmh! I'm just saying, no judging ??? maybe I'm judging ?? ..........Abela if you happen to read here please get in touch with me ??
Kama hujawahi kwenda mtoni kuteka maji huwezi jua thamani ya tone la maji!
Watanzania wengi siku hizi wamekuwa na tabia ya kutaka kulazimisha kila mtu mwenye uwezo au mfanyabiashara mkubwa awe "mwanasiasa" au "mwana harakati wa siasa" kitu ambacho siyo sahii hata kidogo! Siyo kila raia wa Tanzania anatakiwa kujihusisha na siasa! Hapana! Kuwa kwenye siasa au ku support chama fulani hayo ni maamuzi binafsi, na biashara ni mtu binafsi! Mmiliki wa biashara ana hiyari ya kujihusisha moja kwa moja na siasa au akakataa, na lazima kila mtu haeshimu maamuzi yake! Unapoanzisha biashara unless ni biashara ya "siasa" then utalega kupata wanasiasa otherwise unafungua biashara kwaajili ya kuhudumia watu wote bila kujali itikadi zao! Kama hujawahi kwenda mtoni kuteka maji huwezi jua thamani ya tone la maji! Nasema hivi kwasababu watu wengi ambao mnalaumu baadhi ya wafanyabiashara ukiwachunguza utagundua kuwa hawajahi kujaribu kutengeneza kitu chochote au kuangaika from the scratch mpaka kitu kikatembea na watu wakaona ndio maana hamuwezi jua thamani ya kupoteza kitu chako ulicho kiangaikia wewe mwenyewe toka chini! Hamuwezi jua mtu alijinyima kiasi gani ili apate kitu chake mwenyewe! Hamjui mtu huyo alifunga na kuomba Dua kwa muda gani ili Mungu ambariki na biashara yake! Hamjui ni mara ngapi amelia akiona ndoto yake haifanikiwi! Halafu leo hii akubali tu kirahisi rahisi kuharibu mali zake kwasababu ya siasa?! Kuna njia nyingi za kushiriki kuleta amani na maendeleo katika nchi yako bila kujiingiza kwenye siasa! Siyo kila mtu anajali nani yupo madarakani, wengine wanachotaka ni amani kwani wanajua gharama ya kukosa amani! Msilazimishe kila mtu awe mwanasiasa au mshiriki wa chama fulani kwani kila mtu ana uhuru wa kufanya maamuzi yake na jinsi ya kuendesha maisha yake! Sasa leo mkilazimisha kila mtu awe mwanasiasa then what next? Mtakuja kulazimisha kila mtu awe Muislamu au Mkristo? Nahata katika ukristo bado kuna madhehebu, sasa itakuwaje? Mtakuja kulazimisha wakristo wote wasali Roman? Unafikiri mimi ambaye ni Msabato nitakubali?! Wakati najua thamani na raha ya kuwa Msabato!! ........ Embu acheni ujuaji usiyo na kichwa wala miguu! Mpaka siku ile utajifunza jinsi ya kubeba maji yako mwenyewe kutoka mtoni hauto kaa ujua gharama ya kumwagika kwa tone la maji!
My son enjoying his New Year breakfast!
Yaas! That is my son! Enjoying his New Year breakfast in Nairobi. At age 2 1/2 he got all his table manners in place ?? way to go son! Wasichana itabidi wajipange sana tu! Kama hawakufunzwa ustarabu na mama zao wakwende huko hatuwataki sisi ?? We are raising a gentleman right here I hope someone is raising a Queen for him ?? maana Mimi mama mkwe nitamkagua kabla hajaingia ndani ya nyumba ya mwanangu ??? chezea mama mkwe wa dotcom! Kama tunataka tuondoe unyanjasaji na ukiritimba kwa wanawake inabidi wakina mama muwe teyari kulea vijana wenu katika maadili, na mambo yanayofaa! Na mambo hayo huanzia katika umri huu! Usisubiri akifika sijui miaka 6 that is way too late! Pia watoto wakike muwafunze tabia njema, kujithamini, good touch and bad touch mara tu wanapojua kuongea na kutembea! Usingoje mtoto sijui aote maziwa ndio unaanza "kubwabwaja"!! Kama tunataka ukombozi wa mtoto wa kike na mabadiliko ya tabia za wanaume wa Kiafrika basi wakina mama lazima mkubali kubadilisha tabia ya malezi yale ya kizamani kuwa mtoto wa kiume ni "King" na mtoto wa kike ni "servant"!! Kuwa mtoto wakiume haitaji kupewa malezi yenye maadili ya jinsi ya kuwa kaka, baba, mume, na raia mwema isipokuwa toto wa kike tu! Yeye ndiyo anatakiwe afunzwe kuwa dada mwema, mama mzuri, mke bora, na raia mwema, swali linakuja awe mwema kwa nani?!! Mwaume mbakaji? Au mwanaume katili? Au a cold-hearted killer? Au mwanaume mnyanyasaji asiye hata na chembe chembe ya hofu ya Mungu?!! Mothers I'm raising my gentleman because I don't want him to be part of that ugly statistic!!What about you!! .........Happy New Year everybody!
Nawatakieni kheri katika kufunga mwaka na neema za mwaka mpya!
Wapendwa wasomaji wangu, ndugu jamaa, na marafiki, katika haya masaa machache yaliyobakia kumaliza mwaka huu wa 2017 napenda kuwatakia kheri katika kufunga mwaka na pia nawaombea neema na baraka zote za mwaka mpya ziwashukie na kukaa nanyi siku zote! Blog hii nili register rasmi tarehe 15th Dec, 2015 hivyo mpaka sasa ninakuwa nimetimiza miaka miwili na wiki kama mbili hivi! Mwaka wa kwanza nilifanya vizuri sana tena sana! I was very proud of myself! Mwaka wa pili niliyumba kidogo kwasababu "vidudu mtu" wale mafundi wa majungu na fitina wakaingilia kati! Hivyo kimaendeleo ya blog sikufanya vizuri japo wasomaji wangu wameongezeka kwa zaidi ya 300%++ ukilinganisha na mwaka wa kwanza Wanasemaga 'adui' ukimjua hakusumbui kichwa! Basi nami nashukuru kwa nafasi waliyonipa kwani nimewajua! Hawaniumizi kichwa, kwanza hata nguvu ya kusimama mbele yangu hawana! Wanajua sentence yangu moja inawatosha kuwapa "heart attack" ?? hawana uwezo wa kuniangusha mimi wamebakia kupiga majungu behind my back, and definitely that is where they belong "behind my back" I hope I "smell" good enough to make them stay there forever ?? Siwapi nafasi tena! Yani huwezi amini wengine mpaka nacheka nao lakini akili kwa kichwa ati!! 2018 narudi kwenye mstari! Nawahaidi mambo mazuri kama yale ya mwaka wa kwanza! Tutajifunza na kucheka sana! Life is too short embu tujifurahie siye!.....Malengo yangu ni kwamba kila miaka 5 na make major move, lakini kama nitaweza kufanya hizo major move kabla ya miaka 5 nitashukuru sana! Just pray for me as I pray for you na sote tubarikiwe! Ukiona mapungufu yangu chukulia kama "fursa" kwako, kwani hata mimi niliona mapungufu ya wengine nikaona ni "fursa" yangu! Hivyo siku zote jifunze kutokana na makosa ya wengine siyo lazima yakukute wewe! Safari yangu ya kupunguza uzito! ?? Japo siwataharifu kila wiki kama nilivyo haidi lakini bado iko pale pale. Na ninepungua, sema lile tumbo la chini ndio bado?? Niliacha kuwapa progress kila wiki kwani ilikuwa inanikatisha tamaa kuona wiki nzima napungua 1Lb?? nikaona bora nifanye mazoezi na diet kimya kimya ikifika mwezi wa 5 mwakani nawapa report iliyo kamilika! Nimepungua toka size 16 na 18 mpaka 12 na kuna nguo moja ndio 14, nafikiri inategemea na deaigner na material iliyotumika! Namshukuru Mungu kwa mambo mengi sana, na moja ya jambo ambalo ameweza kunibariki nalo mwaka huu ni kuonana na ndugu zangu. Miezi minne ya mwanzo mwaka huu nilikuwa Tanzania, nashukuru nimeweza kuonana na ndugu zangu wote! Mara nyingi nikiwa likizo kutoka na sababu za shule baadhi yao walikuwa nje ya Tanzania hivyo tulikuwa hatuwezi kukutana pamoja kwani ratiba zilikuwa tofauti sana. Mimi huwa siendi nyumbani mara kwa mara unless kuna kitu cha lazima ndio maana huwa nikienda nakaa miezi 3+! Mara nyingi kila baada ya miaka 2 ndio nakwenda. Kama kuna kitu nilifurahiya nilipo kuwa nyumbani ni kuwepo wakati wa birthday ya baba yangu! Miaka yote huwa na miss hii siku! Lakini safari hii Mungu alinibariki nilikuwa nyumbani na mimi ndio nilikuwa "master mind" behind hiyo surprise ?? Mimi hapa ndo huyo nimeshika camera ?? Kama kuna kitu namshukuru Mungu siku zote na nitamshukuru mpaka nakwenda kaburini ni zawadi ya hichi ? kiumbe! Sijui na wala sitaki kujua maisha yangu yangekuaje bila mwanangu! Mungu zidi kunilindia na kumbariki mtoto wangu! Jamani, nisiwachoshe na maneno mengi ?? Namshukuru Mungu kwa yote! Nawatakieni kheri ya kufunga mwaka na baraka na neema zote za mwaka mpya ziwashukie na kukaa nanyi! Happy New Year everybody! Love you all!
Family moment: Lyimo’s, Rweikiza’s, and Adhero’s
Familia tatu kwa pamoja wakifurahia siku kuu! Aliye kati kati ndio kiungo kikuu cha hizi familia tatu! Huyo ni shemeji mkubwa kutoka familia ya Lyimo. Na kulia ni Dennis Rweikiza ambaye amemuoa dada wa Jackson Lyimo. Mnakumbuka niliwapaga story yangu na Dennis Rweikiza? Soma ?? (MrAndMrsRweikiza). Na upande wa kushoto ni John Adhero ambaye pia amemuoa mdogo wake Jackson Lyimo. Na hao ni watoto wao! Hata kama utakuwa na marafiki milioni moja lakini familia bado ni muhimu zaidi ya vyote! Everyone needs a family! Marafiki wanakuja na kuondoka lakini family will always be there! Udugu haufutiki hata kwa bleach isipokuwa KIFO! Blood is thicker than water! Hata kama mtakuwa na mahusiano mabaya but that "bloodely thing" will always find a way kuwaweka pamoja! Marafiki ambao watakuwepo na wewe siku zote, wakati wa raha na shida, wakati unapitia misuko suko ya maisha na kila mtu anakuona haufai mbele ya macho yao, wakati wengine wanakukimbia lakini hao wachache au mmoja atakaa na kusimama na wewe mpaka mwisho basi naomba ujue huyo SI RAFIKI BALI NI NDUGU YAKO! Tofauti ya rafiki mwema na ndugu ni kwamba ndugu anaweza asiwe nawe wakati wote lakini ndio hivyo huwezi kumkana!! Ile damu iliyowaunganisha ndio itasimama siku zote! Lakini rafiki mwema lazima aonyeshe kuwa yeye ni rafiki mwema ili muwe na kitu kilicho waunganisha!! Ndugu yako anaweza asiwe rafiki yako lakini bado atabaki kuwa ndugu yako! Ili udugu ukolee na upendeze zaidi lazima kuwe na urafiki kama mnavyoona hizi familia tatu! Wameweza kuacha kazi zao na kukaa pamoja wakati huu wa siku kuu! Kama wangekuwa hawana urafiki hata kama ni ndugu usingeona haya yakitokea! Upendo hupo ndani yao, na Mungu ni pendo! Familia zilizo jaliwa kumjua na kumwamini Mungu utaziona tu! Kwenye Mungu kuna upendo, kwenye Mungu siku zote ni furaha na amani tele hata sura zao zitaonyesha zinakuwa na mvuto wa "Kimungu Mungu" tu ??......Pichani ni Jackson Lyimo na wadogo zake. Anita Lyimo Rweikiza upande wa kulia na Linda Lyimo Adhero upande kushoto What a family reunion!! Mtu kati hapo ndio wifi mkubwa mke wa Jackson Lyimo pamoja na wadogo zake Lyimo! ....wazurije sasa ???? .....Jamani nawatakieni kheri na baraka zote za kufunga mwaka 2017 ziambatane nanyi pia mwaka 2018! Mzidi kubarikiwa zaidi ya hapo na upendo wenu udumu siku zote!
My 2017 Hottest and Best Couple wakiwa na mziwanda wao!
Simnawakumbuka eeh! Hii ndio ilikuwa my 2017 Hottest And Best Couple Of The Year! Mr and Mrs Joseph Musira kutoka Kamunyonge, Musoma, Mara!…. kama ulipitwa soma ?? (2017HottestAndBestCouple) Hapo kwenye picha wapo na mziwanda wao baada ya kutoka kwenye ibada ya kufunga na kufungua mwaka! Nawatakia mwaka mpya mwema, upendo na neema za Mungu zikaambatane nao katika mwaka mpya! Nawapenda sana. Kama wewe ni mgeni wa hii blog hii blog basi naomba ujue kuwa kila mwaka siku ya Valentine huwa nachagua wapendanao wawili kuwa the best couple of the year. Hivyo ukitaka kujua nani atashika taji mwakani wewe endelea kutembelea hii blog bila kuchoka nani 2018 itapendeza zaidi ?? Mtu na daddy ake, deka mdogo wangu ??
RC Paul Makonda: haikuwa rahisi kama siyo Mungu kuwatumia wateule wake sijuwi leo nigekuwa wapi
@Regranned from @paulmakonda - Mwaka 2017 ni mwaka watofauti sana kwangu. Leo tunapojiandaa kupokea Mwaka 2018. Ni vyema nikayatazama maisha yangu ndani ya mwaka 2017 hakika huu ulikuwa mwaka wa aina yake. Ni mwaka ulionipa marafiki wa kweli, lakini kubwa kuliko ni Upendo na Maombi niliyoyapata kutoka Kwa Kipenzi changu Maria. Nikuambie kitu ndg msomaji...... haikuwa rahisi kama siyo Mungu kuwatumia wateule wake sijuwi leo nigekuwa wapi. Nimepewa kila jina baya, kila jambo baya nimefanya mimi ,matusi yote yalikuwa yangu na hata watu kutamani nisiwepo duniani. Lakini kwako Mpenzi ilikuwa tofauti, ulinitia moyo Kwa sauti ya upole,uliniombea na kunifuta machozi bila kuchoka. Tena Kwa kusema Nanukuu, Paul Mungu hajawahi kukuacha hata kama Dunia yote inakuona haufai nataka nikuambie Mungu amekupaka mafuta Kwa kazi hii simama na usonge mbele. Mwisho wa kunukuu”.Ndg zangu na wananchi wenzangu ni vyema mkajua kila mtu anayo hadithi ya kumweleza mwenzake ila kwangu inahitaji kitabu kuyaeleza mapito na njia nyembamba niliyoipita mwaka 2017. Itoshe kusema Mungu wa haki iko siku atasimama na kutoa hukumu ya kweli Kwa watu wote. Kwani yeye anatujua kila Mtu na matendo yetu tena kwake hakuna Siri ya maisha yetu.Nakupenda sana Maria wangu na ninathamini sana Mchango wako ktk utumishi wangu hapa Duniani. Uzidi kuwa Imara simba wangu ili niyafanye yote mema ambayo Mungu amepanga Kwa watu wake. Asante sana Mungu Kwa kunivusha mwaka 2017.
Mc.Pilipili: HUU NI UKICHAA WA MAPENZI
Regranned from @mcpilipili - HUU NI UKICHAA WA MAPENZI. ?Kushika mimba ukadhani ni mtego ili uolewe. ? Kutafuta mkamilifu wakati tabia zako tunakuvumilia tu. ? Kutafuta msichana mrembo wakati huna pesa. ? Kutafuta mke mwema kanisani wakati we unaenda kanisani wakati wa maombi ya Christmas tu. ? Kusema wanawake wote sawa. ? Kuendelea kuchagua wanaume wakati unajua waoaji siku hizi wachache. ? Kuishi na mpenzi wako kabla ya ndoa, unamfulia, unampikia na unampa penzi wakati unajua hujulikani kwao, ukiachwa unatafuta ushauri mitandaoni. ?Kusema umeokoka lakini unazini na mchumba kama kawaida kwa kisingizio kwamba soon mtakuwa mke na mume! ?Kuogopa kuongozana na msichana au mvulana eti mtaingia majaribuni, unajua kutamani tu ni uzinzi? ? Kufikiri kwamba utampata mtu mwenye sifa mia nane unazozitaka labda umuumbe mwenyewe! ?Kujifanya unapendwa wakati moyoni unajua wazi mtu kakuchoka, na amekwambia kabisa anatafuta mtu mwingine! ? Kumhonga mwanaume ili akuoe! ? Kudhani kwamba kutoolewa ni laana, hii ni bangi mbaya! ? Kumtongoza mchumba au mke wa rafiki yako! ? Kuoa wakati huna kazi /chanzo cha kipato! ? Kufikiri eti wanaume wa kiafrika wanaweza kufanya mambo ya kwenye tamthiliya za kifilipino. ? Kumsomesha mtu ili uje umuoe! ? Kumng'ang'ania mtu asiyekupenda, utazimia ukialikwa harusini! ?Kuwaeleza mashosti zako 'utam' anaokupa mtu wako! ? Kumwambia bebi wako anunue gari wakati amepanga chumba kimoja……..
Me, myself, and I #TBS
JNM: I’d like to share with you some of the things I’m including in my TAKE TO 01/01/2018 LIST
@Regranned from @j_n_mengi – As we are about to say bye to 2017 and welcome 2018 I’d like to share with you some of the things I’m including in my TAKE TO 01/01/2018 LIST:
1. Positivity and faith-I can’t even start to tell you how many things I manifested through my faith this year.
2. Honesty-though can seem difficult it’s the most liberating gift to self and others
3. Patience-a make or break in life but also the wisdom to know when to stop
4. Friendship-honest friends to laugh and cry with,by your side for no reason 5.Quality time spent with family-because you must always have a warm home to go to
6. Dreams-because dreams are what reality is made of and one must always have something to look forward to.
7. Doing what makes me happy-because I deserve it just like everyone else.
8. Facing my fears-because through this I get to discover my new strengths
9. Time out-because time alone allows me to connect to my inner self
10. Take it easy-what seems to be such a big deal today might not be that way tomorrow so it’s important not to take everything too seriously. Pls share with me yours too..
“Hatuna formula sometimes hata hatuelewi what we are doing…ila tunachojua tunapendana”
My 2017 best joke: If your man is acting single, act like a widow
??? I’m still laughing over this joke! Definitely one of the best!……. Soma post ya nyuma hapa ?? “IfYourMan“
My bestie and I #FBF
My bestie and I somewhere in Masaki, Dar es salaam earlier this year!……..Sidhani kama nilishawahi kuwaeleza kuwa huyu rafiki yangu kipenzi ni shemeji yake na Freeman Mbowe kabisaaaa! Napia ni daughter inlaw wa Dr. Reginald Mengi ?? anyway that is not the point nawala havihusiani na urafiki wetu! Sisi tulisoma wote college pale CBE, Dar napia tulikuwa room mates! Namtakia kheri ya kufunga mwaka 2017 na baraka zote za kuanza mwaka 2018! Love her dearly! #FBF #2017
My 2017 best family moment: The LB family
Huko nyuma nilishawahi kusema kuwa hii picha imekosha moyo wangu, soma ?? (HiziPichaZimenikosha) na mpaka sasa bado zinanikosha. One of the best family moment of the year kwa hii blog! Ukweli hata kama familia mnapendana kiasi gani lakini kama hamshirikiani katika maswala ya kujiinua kiuchumi, maendeleo, na kiroho basi upendo wenu ni BATILI! Yani ni upendo wa "kichina" kwakweli! Hii family ni mfano mzuri sana katika kitu kinaitwa family unite and family love! Sijasema ni PERFECT! Nope! Hakuna hapa duniani familia ambayo imekamilika! Kila familia ina matatizo yake, lakini kama kuna upendo wa kweli basi kila kitu kitaonekana sahii! Basi, kwa maana hiyo familia ya mwanamitindo wa kimataifa Linda Bezuidenhout nasema imeshinda nafasi hii is 2017 best family moment! Hapa ilikuwa ni ufunguzi wa duka la nguo za LB! Yani kama vile mbavyo mnaonaga LV, Zara, Nine West n.k wana maduka yao maalum basi ndivyo ilivyo kwa brand ya nguo za LB!
RC Paul Makonda ndani ya jiji la Suquian, China!
@Regranned from @paulmakonda – Nikiwa na Meya wa jiji la Suquian Bw. Wang Tianqi,jiji la jimbo la Jiangsu. Hili ni jiji jipya kati ya miji mingi iliyopo nchini China(limeanzishwa mwaka 1996). Jiji hili lina ukubwa wa km za mraba 8555 km na Wananchi milioni 4.7. Nikiwa jijini Suquian nimepata bahati ya kutembelea maeneo ya kiuchumi mbalimbali likiwemo eneo la *Suquian National Economic and Technological Development Area* (eneo la viwanda) lenye viwanda vya kati na juu kama viwanda vya chakula, mbao,mvinyo (Yanghe Breweries Industry),viwanda vya nguo n.k. Uchumi huo wa viwanda umesaidia Pato la mwananchi kufikia hadi Yuen 40930 kwa mwaka, sawa na $ 6292 ambayo ni sawa na tshs 14,124,910 2018niMwakaWauwekEzAjI
My 2017 best baby of the year: Mtoto wa Hamisa Mobetto
Huyu mtoto alisimamisha dunia ati!! Nani atasahau jinsi mamilioni ya watu around the globe walikaa chini kusikiliza interview ya Diamond na Clouds fm ili kutaka kujua mimba ilitungwa lini na kama kweli Diamond ndio baba halisi na halali wa Prince Dylan ??? Yap! Kuna baba wengine ni baba "halisi" lakini siyo "halali"!! Hiyo will be another topic next year ?? Kwakweli mimi siyo shabiki wa Hamisa, sipendi wanawake with such character! You can judge me but that is my opinion na hii ni blog yangu ?? Hata hivyo kwenye ukweli lazima tuseme kuwa mtoto wa Hamisa Mobetto kaweka history ndani na nje ya Tanzania! Na kwamaana hiyo alphaigogo.com inamtunuku kuwa the best baby of the year 2017! Kusoma post zilizopita bonyeza ?? HongeraDiamond ZariGiveUpTheFight
My 2017 best love drama: Ndoa ya Zamaradi Mketema
Kama kuna drama ya mapenzi ambayo ilishangaza wengi na watu wengi wakaguswa nayo ni break-up ya Zamaradi Mketema ma Ruge Mutahaba!! Siyo kitu rahisi kuachana na such a powerful figure like Ruge Mutahaba. Lakini jinsi Zamaradi alivyo ikabili (handled) swala zima its just amazing! She handled it like a real woman ambayo imemfanya siyo tu kupata heshima zaidi ndani ya Tanzania bali amekuwa mwanamke shujaa na mfano wa kuigwa kwa wasichana wote! Mwanamke kama Zamaradi anaweza akasimama kishujaa kabisa mbele ya watoto wakike na kuwafundiaha kuhusu maadili, jinsi ya kukataa na kuachana na unyanyasaji wa aina yoyote ile, kukataa mwanaume kukudhalilisha na watoto wakike wakatii kwani yeye mwenyewe ameonyesha mfano hai! Big up to Zamaradi! You have earned more respect from me, hivyo napenda kusema kuwa hii imekuwa my 2017 best love drama!
Kusoma post zilizopita bonyeza ??
My 2017 best song: Zezeta
Najua kuna nyimbo nyingi sana ambazo ni nzuri zilizo imbwa na wanamuziki mbali mbali lakini #Zezeta bado umekamata macho na masikio yangu! Huu wimbo gives me life kwakweli! Maneno yake yamepangiliwa vizuri, yanaeleweka, ujumbe unaleta maana, sauti na mdundo ni babkubwa! Video ndio usiseme!! Ipo kwenye ubora wakimataifa. Very clear, haina giza giza wala chenga, wachezaji wamevaa vizuri, na rangi za nguo zao ni rangi zilizo tulia hazichoshi macho! Hivyo natangaza rasmi kuwa huu ndio my 2017 best song ??
Mlee mtoto katika njia impasayo!
Kwanza naomba mniwie radhi wapendwa wangu ambao ni Waislam. Mimi ni Mkristo hiyo mambo mengi nikiongea nita refer to the Holy Bible kwani hicho ndicho kitabu nakijua na pia sipo hapa kwaajili ya dini hivyo sitokaa ni compare Quran na Bible! Sasa Biblia katika kitabu kile cha Mithali 22:6 inasema mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee! Hizi picha za birthday ya Nillan ambazo zinaonyesha wako mezani wakila chakula na kunywa zimenifanya nikumbuke hilo fungu la Mithali 22:6! Hivi wazazi wangapi mnawalea watoto wenu kwa kuwafundisha kuwa chakula ni kitu cha kuheshimiwa hivyo ukila lazima uwe na nidhamu?! Kuwa hupaswi kutembea huku unakula kama mkimbizi au mtu aliye vitani!! Unamfunza mtoto kuwa ni lazima ukae chini / mezani wakati wa kula napia ni marufuku kuongea nachakula mdomoni!! Kama wewe ni mzazi unaye ishi katika mazingira mazuri na ungependa mtoto wako aende mbali zaidi ya hapo ulipo wewe, je umemwandaa mtoto wako kukabiliana na mazingira hayo?! Kwamfano, ungependa mtoto wako awe na uwezo wa kwenda naye kwenye 5* hotel nakula chakula mbele za watu nilazima umfunze mwanao kukaa mezani wakati wakula na atulie mpaka atakapo maliza chakula. Nilazima umfunze mtoto kutumia visu, uma, na kijiko tena umfunze mara kwa mara ili azoee kuvitumia kama Zari alivyofanya kwa watoto wake. Hao watoto kukaa mezani kwa utulivu hivyo nakula kwa ustarabu si kitu ambacho wamefanya mara moja, hapana! Hao watakuwa wamefunzwa na wamezoea! Ni malezi mazuri sana haswa kwa karne hii ya 21 ambapo dunia imekuwa kama kijiji huwezi jua ni wapi na nani mwanao atakutana naye hivyo lazima kujua jinsi ya kumudu mazingira! Nilipokua nyumbani Tanzania mwanzoni mwa mwaka huu, watoto wake mdogo wangu walikuja kunitembelea. Sasa wakati wakula mie nikamwambia dada wa kazi kuwa haina haja ya kuweka chakula mezani aweke mkeka tukae chini tule! Tuliokulia kwenye mikeka utatujua tu ??? mwe! Kwani hao watoto waliweza kula?! Mara namuona yule mdogo anaangaika kuvuta kiti karibu na mkeka na mkubwa wa kike kalalia tumbo huku akijaribu kula ?? Nikawa nashanga, ndio mama yao akasema unajua wanangu hawajui kula huku wakiwa wamekaa kwenye mkeka!! Akasema "Wakenya hao wanajua kula ni mezani tu" ?? mbona yalinishuka ikabidi tuhamishie chakula mezani, basi wakawa na amani wakala kwa furaha! Mdogo wangu alipoona hizi picha za Tiffah akanitumia na kusema kama mtoto wake angepiga picha hiyo ambayo ameshikilia glass ya juice baada ya picha za birthday ya Nillan kutoka basi baadhi ya watu angefikiri kuwa ameiga kumbe hivyo ndivyo alivyo walea watoto wake!...... Wazazi embu achaneni na kuwapa watoto glass za plastic kwanza zinaleta Cancer ?? honestly, bora umpe mtoto kikombe cha bati kuliko plastic! Nunua zile glass ngumu mfundishe mtoto kushika na kutumia bila kuvunja ili siku ukiwanae 5* hotel upati shida kwani kazoea! #Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee!! ""* Picha zote za Tiffah nimezitoa kwa Instagram page ya princess_Tiffah***