My family on their way to Utegi kwenye mazishi ya ndugu yetu Kenneth! Hapa walikuwa Singida jioni ya leo, umeona kitu cha “Utegi Mgahawa”? Kijiji chetu ni maharufu ati ?? ……. anyway, nawatakieni safari njema ndugu zangu, mfike salama na pia mrudi salama. Mazishi mema!
All posts by Alpha Igogo
Wema Sepetu: Peace of mind is everything for me
“Siwezi Kuendelea kuishi kwenye Nyumba inayo nikosesha amani… Peace of mind is everything for me… Natangaza Rasmi kuondoka Chadema na Kurudi Nyumbani…. #ThereIsNoPlaceLikeHome… Feels good to be Back…
“Wow! Kwaniaba ya mdogo wangu kipenzi Magreth Otieno Olung’a Igogo ambaye ni mmoja wa mashabiki wakubwa wa Wema Sepetu na pia ni mwanachama muaminifu wa CCM naomba nichukue fursa hii kumkaribisha our Tanzania Sweetheart #nyumbani! CCM oyeeeeeee! Kidumu chama ???? O’Lord of Mercy!!…….Honestly, nampongeza sana Wema kwa maamuzi haya. Huwezi kuwa na amani kwenye chama ambacho Mwenyekiti wake amekutaka kimapenzi! Ndio maana hata amabavyo hujaenda kumuona uncle wako Mhe. Tundu Lissu mie sijashangaa kwani nilijua ni ngumu sana kwako kuonana na Freeman Mbowe uso kwa uso! Nafikiri it’s high time kwa wanawake kushika uongozi kwani hawa wanaume wanatuchanganyia habari tuu! Hongera sana Wema ??? BTW, hivi mnajua jinsi gani mdogo wangu alikuwa anachukia niki mpost Zari humu zaidi ya Wema? Hahahaha! Haya Sasa nitakuwa na balance lol!
Dr. Shika kutambulishwa usikuwa wa 900 itapendeza!
Mara paa! Dr. Shika kwa celebrity! Jamani, it’s never too late to be you and achieve your dreams! Huwezi jua ni lini na kwa njia gani Mungu atakufungulia mlango wa kufikia malengo yako! Wewe fanya kazi zako kwa uwaminifu na kwa bidii mengine Mungu atakutimizia. Pia safari moja huwanzisha nyingine. Unaona hapa Dr. Shika alikwenda kwenye mnada wa kununua nyumba of his own dream japo mfukoni alikuwa “kachacha” lakini alithubutu. Mwenda bure si mkaa bure! Watanzania wangapi walikuwa wanamjua Dr. Shika lakini leo hii ndio the talk of the country! Katika umri huu kwa mazingira ya Africa haswa Tanzania sidhani kama hata yeye aliwahi kuwaza kua sentence yake moja tu “900 itapendeza” itaweza badilisha maisha yake na kumuweka kuwa wa level nyingine kabisa! Leo hii ana mkurugenzi na kualikwa sehemu mbali mbali kuelezea maisha yake. Nani alijua kuwa maisha ya mtu kama Dr. Shika yanaweza yakawa kivutio na yahamasa kwa Watanzani?! Somo hapa nikuwa wavumilivu katika safari za kufikia ndoto zetu kwani Mungu ndiye mpangaji na mtoaji wa vyote! Acha tamaa ya kutaka vitu kwa haraka! #900Itapendeza
Repost: women over 40!
Nimeipata hii article kwenye Facebook nikaona siyo mbaya ku share nanyi hapa. Mtaniwia radhi kwa wale msioelewa lugha hii ……..Picha zangu hazihusiani na hii story lakini mwakani itakuwa 41 so get your life ?? #TBT “Ladies and gentleman, this is a must read!!! THIS HAS BEEN WRITTEN BY A MAN……….This is for all you girls 40 years and over….. and for those who are turning 40, and for those who are scared of moving into their 40’s…AND for guys who are scared of girls over 40!!!!…. This was written by Andy Rooney from CBS 60 Minutes.
Andy Rooney says: As I grow in age, I value women who are over 40 most of all. Here are just a few reasons why: A woman over 40 will never wake you in the middle of the night to ask, “What are you thinking?” She doesn’t care what you think. If a woman over 40 doesn’t want to watch the game, she doesn’t sit around whining about it. She does something she wants to do. And, it’s usually something more interesting.
A woman over 40 knows herself well enough to be assured in who she is, what she is, what she wants and from whom. Few women past the age of 40 don’t give a damn about what you might think about her or what she’s doing. Women over 40 are dignified. They seldom have a screaming match with you at the opera or in the middle of an expensive restaurant. Of course, if you deserve it, they won’t hesitate to shoot you, if they think they can get away with it. Older women are generous with praise, often undeserved. They know what it’s like to be unappreciated.
A woman over 40 has the self-assurance to introduce you to her women friends. A younger woman with a man will often ignore even her best friend because she doesn’t trust the guy with other women. Women over 40 couldn’t care less if you’re attracted to her friends because she knows her friends won’t betray her.
Women get psychic as they age. You never have to confess your sins to a woman over 40. They Always Know. A woman over 40 looks good wearing bright red lipstick. This is not true of younger women. Once you get past a wrinkle or two, a woman over 40 is far sexier than her younger counterpart. Older women are forthright and honest. They’ll tell you right off if you are a Jerk if you are acting like one! You don’t ever have to wonder where you stand with her.
Yes, we praise women over 40 for a multitude of reasons. Unfortunately, it’s not reciprocal. For every stunning, smart, well-coiffed hot woman of 40+, there is a bald, paunchy relic in yellow pants making a fool of himself with some 22-year-old waitress. Ladies, I apologize. For all those men who say, “Why buy the cow when you can get the milk for free”. Here’s an update for you. Nowadays 80% of women are against marriage, why? Because women realize it’s not worth buying an entire Pig, just to get a little sausage!
Embu tucheke kidogo! Eti wewe waonaje kwa hili?
Juzi kati niliweka tangazo la msiba wa ndugu yangu kwa hii blog , nikaambatanisha na picha ambazo tulipiga akiwa hai ambapo ilikuwa mara ya mwisho kuonana naye Tazama hapa ?? (Tanzia). Sasa kuna mtu ameweka comment akishangazwa na picha niliyotumia kwani tulikuwa tuna tabasamu. Anasema tunatangazaje kifo kwa furaha hivyo? Soma ?? Nimecheka kwani kwangu imekuwa kichekesho,nikahisi huyu dada lazima atakuwa Muhaya maana Wahaya akili zao wanazijua wenyewe, na hilo pozi wala uulizi katoka mkoa gani ?? …… Hivi kuna kanuni ya picha ipi itumike kutangaza msiba? Ukishaweka picha ya marehemu akiwa mwenyewe zile zingine sizinakua ni kumbukumbu mlizopiga!! Jamani, mimi ni Msabato na Mjaluo vile vile hivyo kuna vitu vingine haswa kwenye swala la misiba mtanisamehe. Kwani kuomboleza kupo tu lakini huwezi kuomboleza kama mpagani! Halafu, tujenge tamaduni za kuonyesha upendo wa dhati kwa wale ambao wanagusa maisha yetu wakati bado wako hai! Mambo ya kumlilia mtu na maneno mazuri akisha kufa ni upuuzi mtupu! Yani mimi kama umeshindwa kunipenda nikiwa hai, hata salamu hutujuliani gafla nikisha kufa eti wewe ndo unakuja na makelele yako kunililia?! No! Sitaki! Kaa kwako nitashukuru zaidi, kuliko kuja kunililia kinafiki! Kwanza kuliliwa na wanafiki inaweza ikawa kikwazo cha kuingia Mbinguni ?? just saying! Sipendi wanafiki haswa nikisha kufa nawaomba msije! Nionyeshe unanipenda na kunijali nikiwa hai! Nami nitafanya vivyo hivyo!
THC Thanksgiving Gala 2017
Ok wasomaji wangu, sijapata muda wa kukusanya vitu vizuri kuwaletea msome au mtazame. Lakini siyo mbaya kuwaletea matukio yaliojiri kwenye community hii ya Watanzania wa Houston ambapo naishi…..Sorry sikuwepo kwenye hii but always there’s next time. Haya osheni macho na picha nzuri, hii ndio kamati iliyofanya mambo hayo. Hongereni sana mmefanya kazi nzuri na watu wamependeza sana. Kuona picha na maelezo zaidi bonyeza ??
Matukio katika picha: THC Thanksgiving Junior Gala 2017
I love this! Aliye anzisha hii event got brain and big heart! Safi sana. ……..Wapendwa, hii ni Thanksgiving event kwa ajili ya watoto ambayo iliandaliwa na jumuiya ya Watanzania waishio Houston, Texas. Kwa maelezo na picha zaidi bonyeza ?? ThanksgivingJuniorGala2017
Huyu best yangu mama yake na shoga yangu Abiah , yeye anaitwa Vivian. Kapendezaje sasa simple, beautiful, and classy! Just love her look! Next yr nitaku-join sijui nitakuwa na tumbo ama mtoto ?? whatever the Case will be I will be there, tuombeane uzima!
Tanzia: R.I.P Kenneth Alexander Igogo
Kwa masikitiko makubwa sana kwaniaba ya familia ya marehemu mzee Alexander Olung’a Igogo, familia ya mzee Otieno Olung’a Igogo, na familia yote ya babu mzee William Olung’a Igogo wa Utegi, Rorya, Mara. Naomba kutangaza kifo cha kaka yangu Kenneth Alexander Igogo a.k.a Ukombozi kilichotokea leo majira ya mchana saa za Africa Mashariki katika hospitali ya Bugando, Mwanza. Mipango ya mazishi inafanywa na ndugu wa marehemu. Mikusanyiko yote itafanyika nyumbani kwa baba mkubwa wa marehemu mzee Charles Olung’a Igogo pale Oyster Bay, Dar es salaam, Tanzania. Kwafaida ya wasomaji wangu, marehemu ni kaka (tumezaliwa mwaka mmoja kasoro miezi) yangu mtoto wa marehemu baba yangu mkubwa. Baba yake ni tumbo moja na baba yangu ndio wanafuatana kuzaliwa. Marehemu ameacha watoto wawili, mama mzazi, dada wanne, na kaka watatu, pamoja na nieces, nephews, na mjukuu mmoja. Hii picha tulipiga mwanzoni mwa mwaka huu (February, 2017) tulipokwenda kusalimia ndugu zetu kijijini kwetu Utegi ambapo marehemu alikuwa akiishi na familia yake. Yeye ndio mwenye Tshirt yenye mistari ya kijani kifuani pembeni yangu. Mwenye nguo nyekundu ni mama mzazi wa marehemu. Hao wengine ni wadogo zangu Magreth na Guka. …..Kifo hichi ni chakusikitisha sana kwa jinsi kilivyotokea!! Sina lakusema zaidi ya Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe milele zote, Amen!
Shout-out to my cousin Sophia Makoyo! New lawyer in town!
When I say beauty and brain, trust me I know it, seen it cause it runs in our family bloodstream ?? wenye wivu pandeni juu mkazibe ??……Hey lemme shout-out to my sweet, charming, smart cousin Sophia Makoyo for attaining her bachelor in law from University of Dodoma a.k.a UDOM! Hongera sana binamu yangu najua huu ni mwanzo tu, mazuri mengi yanakuja! Have faith and keep it up! Sky is just another platform! Hongera sana ???❤
#FBF #2010BongoStarSearch
Since its Friday, let us flash-back some memories ? Hapa ilikuwa Bongo Star Search ya 2010 behind the scene. Huyo binti ni mwanangu akiwa na Diamond Plutnumz, TMK-Wanaume, na Marlow. Yuko wapi Marlow siku hizi?! Anyway natumaini baadhi ya hizi picha zitakupa faraja na natumaini wewe uliyekata tamaa.! Muwe na weekend njema. Mbarikiwe wote
Malia Obama ndani ya “hot topics”!
Ule usemi uliotumika sana na wahenga wetu kuwa “mtoto umleavyo ndivyo ukuavyo” unaweza usilete maana sana katika kulewa watoto wa karne hii ya 21! Hivi karibuni kama wiki na siku kadhaa zilizopita binti wa Mstahafu Rais Baraka Obama, ajulikanae kama Malia Obama alikutwa akibusiana na mwanaume ambaye aliaminika kuwa ni boyfriend wake katika viwanja vya chuo kikuu cha Harvard university na pia alionekana akivuta sigara. Tazama kwenye hii video kuanzia dakika ya 22.50 kama inavyoelezewa na gwiji wa “hot topics” Wendy Williams ?
https://youtu.be/-BwVCA4b8gw
Sipati picha Michelle Obama alikasirikaje, unaweza zimia bila “kizimio” ?? Halafu sasa kutokana na sheria za huku Malia Obama anatambulika kama mtu mzima ambaye anaweza fanya maamuzi yake binafsi na wazazi wanatakiwa kuyaheshimu! Najua hata Africa ukishafika 18+ unatambulika wewe ni mtu mzima kwenye karatasi za serikali lakini kiuhalisia wazazi wetu wengi bado wanakuwa na mamlaka juu yetu na kutufanyia maamuzi mengi juu yetu. Ni mfumo wa tamaduni zetu ambao unafanya watu wengi kutokuwa na mawazo huru na kufanya maamuzi ambayo yanampendeza yeye na kwafaida yake kwanza. Funguo za furaha zetu zipo mikononi mwa watu kama wazazi, marafiki, na jamii na ndio maana wengi ni wanafiki na waongo kupita kiasi! Lakini vile vile lazima tukubaliane kuwa kila familia lazima iwe na identity yake! Kila mtu anazaliwa tofauti lakini kama familia lazima muwe na kitu kimoja ambacho watu watajua na kuwatambua nacho. Hivyo sishangai kwanini Michelle na Baraka wamekasirishwa na kitendo hicho. ……..Mungu atusaidie sisi ambao tunataka kuzaa na wale ambao wanalea katika karne hii ya 21 kwani changamoto ni nyingi mno!
Jokate Mwegelo: Magufuli na kisa cha Mussa na Wana wa Israeli
Magufuli na kisa cha Mussa na Wana wa Israeli
Musa alipitia vitu vingi ikiwemo kejeli, kujaribiwa na hatimae kufanikiwa kuwavusha Wana wa Israeli kuelekea nchi ya ahadi. Lakini kuna wakati wafuasi wake hao walipojaribiwa kidogo tu wakaanza kunung’unika na kumkebehi Musa kwamba ni kheri maisha waliyokuwa wanaishi Misri kwa Farao.
Rais John Pombe Magufuli ameianza safari yake nyingine baada ya Novemba 5 mwaka huu kufikisha miaka miwili madarakani. Napenda kuifananisha safari yake hiyo iliyosheheni mageuzi makubwa sawa na ile ya Wana wa Israeli walipokombolewa na Nabii Musa kutoka kwenye mikono ya utumwa chini ya Farao wa Misri. Uwajibikaji, Uzalendo, Utendaji
Kumekuwa na tatizo tatizo la watumishi wa Serikali kutokuheshimu misingi ya kazi zao katika utumishi wao wa umma, nidhamu ya kazi ilikuwa haipo. Ilifikia wakati watu walitunga safari za nje ilimradi tu wapate posho za kujiendeleza wao na familia zao.
Uzalendo wa nchi ukageuka kuwa uzalendo unaokimu mtu na familia yake na watu wake wa karibu. Fedha nyingi zikawa zinapotea angani na hata matunda ya safari tulikuwa hatuyaoni. Bado barabara na miundimbinu muhimu ilikuwa kasi yake ya kuimarishwa haikuwa nzuri sana.
Utendaji na ubunifu ulikuwa wa chini kwani hakukuwa na kitu kipya katika utendaji wa kazi kwa wengi zaidi ya kujitajirisha kupitia kodi za wananchi bila sababu zozote zile za msingi. Manung’uniko yalikuwa mengi juu ya rasilimali za taifa. Kulikuwa na makundi mengi yakizungumza kwa lawama namna rasilimali zilikuwa zinatumika vibaya. Makundi haya yakihusisha Wanasiasa, Wasomi na hata baadhi ya Wananchi wenye kufuatilia maslahi na rasilimali za taifa. Nchi yetu pendwa ya Tanzania ‘kuibiwa’ umekuwa ni mjadala wa muda mrefu bila utatuzi au hatua yoyote kuchukulliwa.
Kuna wakati, nikiamini kwa nia njema na uchungu wa nchi yao na si siasa, baadhi ya wanasiasa walipaza sauti kusema kuwa ni aibu kubwa kwa nchi yetu kushindwa hata kumiliki ndege yetu. Walihoji: “Tutatangazaje utalii bila ya kuwa na ndege yetu?” Kwa ufupi kila kitu kilikuwa kikionekana kwenda sivyo. Na hapa sijagusia issue ya “mafisadi”
Kuingia kwa Magufuli madarakani miaka miwili iliyopita, ukiyatazama maisha yake, utakubaliana nami kuwa huyu ni kiongozi anayeishi na kujituma kwa ajili ya maslahi ya wananchi. Hii inanikumbusha nilipokuwa masomoni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam miaka kadhaa ya nyuma, niliwahi kumuona Rais wetu ambaye kipindi kile alikuwa ni Waziri akila sehemu mmoja wanafunzi katika kijiwe maarufu cha misosi kiitwacho “Harvard”.
Pale chakula ni cha bei ya chini kabisa, mlo kamili mzuri ulikuwa hauzidi elfu 1000. Ilikuwa ni sehemu ya sisi wanafunzi wa kawaida kula kwa sababu ya bajeti zetu ndogo. Kumuona yeye kama waziri pale kulipelekea mimi kuanza kuelewa Dkt. Magufuli ni mtu wa aina gani. Ni wazi kwamba ni mtu wa watu, hana makuu, hajikwezi na anapenda “ku-budget.” Mageuzi na Mabadiliko
Sishangai miaka miwili tu ya uongozi wake akiwa ameacha tayari alama na mageuzi makubwa ya kukumbukwa. Kwa kifupi tu ametenda yafuatayo ya kukumbukwa:
· Kuwezesha elimu bure kuanzia shule ya Msingi hadi Sekondari;
· Kufufua shirika la ndege la ATCL kwa nunua ndege mpya sita;
· Kuongeza mapato ya ndani toka trilioni 9.9 kwa mwaka hadi trilioni 14 kwa mwaka;
· Kurejesha nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma;
· Ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania
· Kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma;
· Kutimiza ahadi ya Serikali kuhamia Dodoma;
· Kukamilisha miradi mikubwa wa umeme wa Kinyerezi I-extension na Kinyerezi II;
· Kuanza ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge;
· Uzalendo kusimamia raasilimali za taifa yakiwemo madini;
· Kuanza ujenzi wa barabara za juu Tazara, Ubungo na daraja la wapiti kwa miguu Furahisha;
· Ujenzi wa madaraja ya kisasa mfano la daraja la Kilombero;
· Kusimamia uhakika wa madawati maabara na maktaba katika shule zote nchini;
· Ujenzi wa maduka ya kisasa ya dawa za ndani ya kila hospitali ya Serikali;
· Kupambana vikali dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya nchini;
· Kutoa bima za afya za matibabu ya bure kwa wazee
· Kuhakikisha wanafunzi wanaostahili kupata mikopo ya elimu ya juu wanapatiwa
· Kuhakikisha Tanzania inakuwa na viwanda vya kutosha nchini
· Kufuta kodi na urasimu kwenye kilimo na uwekezaji nchini
· Kuhakikisha serikali inasimamia uuzwaji wa mazao ya wakulima masokoni na kupata faida. Mfano wakulima walikuwa wakiuza korosho zao kwa tsh 800 kwa kilo mpaka tsh 4000 kwak kilo.
Nimesukumwa kuzungumzia na kuorodhesha mafanikio haya kwa ufupi ili tujue shabaha ya rais wetu. Rais wetu anataka kurudhisha heshima. Heshima hailetwi kwa blah blah, heshima huletwa kwa vitendo na kufanya vitu kwa njia ya kuwa “disruptive”-kutokufanya vitu kikawaida au kwa mazoea. Msimamo mkali wa Rais
Rais Magufuli anataka kuona watu wakijituma na kuleta matokeo chanya. Hata ukiangalia safu zake za uongozi ni viongozi walioshiba kwenye nafasi zao. Na wanaonekana hawafai wanaondolewa. Ila bado kuna makundi ya watu kwenye jamii wanaona anachofanya ni kazi bure na kufikia hatua ya kuaminisha umma kuwa Serikali hii ya Awamu ya Tano imefanya hali imekuwa ngumu na eti haina malengo na kuwa imepoteza dira.
Hakuna ukombozi uliofanyika bila kutoa jasho, kutokwa damu na kutumia mbinu za kujifunga mikanda. Mheshimiwa Rais anafanya hilo, ni lazima kujitoa mhanga kwa kipindi hiki kwa ajili ya mafanikio ya muda mrefu. Nilifikiria viongozi wetu hasa wa upinzani wangefurahia mabadiliko haya kwa maana ndio kitu hasa walichokuwa wakikitamani na wakishiriki kikamilifu katika kutoa mawazo yenye kujenga ila hali imekuwa ni tofauti.
Hapa ndio maana nimekikumba kisa cha safari ya Mussa-maana nalifananisha hili na kadhia ya wale Wana wa Israeli kufikia hatua mpaka kumkufuru Mwenyezi Mungu na wakaona kuwa ni kheri wangebaki kule Misri. Kama kumbukumbu ya kuku, nao walisahau walipotoka. Ushauri
Natambua ni vigumu kumuaminisha kila mtu ukweli kama tayari anaamini uongo, kama ilivyo vigumu kumuaminisha uongo yule ambaye anaamini ukweli. Ila kama vijana na taifa lililo la vijana, imefika wakati wa kila mmoja kusimamia kila anachokiamini, LAKINI asiamini kile alichoaminishwa. Vijana tuache siasa za kupikwa na kuungaunga, tusimame katika ukweli na mambo yale ambayo yana maslahi kwa taifa letu na si maslahi binafsi. Tujiulize: Inakuwa vipi, wanasiasa na wanaharakati wale wale ambao walikuwa wanapigania vitu flani vifanyiwe kazi, sasa vinafanyiwa ndiyo wa kwanza kununa na kufanya ‘confusion’ mbele ya Jamii?
Ndani ya chama cha Mapinduzi tunaamini Umoja ni Ushindi. Huu ni wakati wa kuungana na Mheshimiwa Rais katika ukombozi wa Watanzania, lazima tuelewe shabaha ya Rais wetu kuwa ana nia njema na maendeleo ya nchi yetu.
Hii safari sio rahisi, hakuna aliyemkamilifu ila wote tunaitumainia Tanzania yenye neema. Vijana tuache kupokea mapokeo ya wanasiasa wasio na nia njema na nchi yetu, tufanye kazi kwa kushirikiana katika kuiletea nchi hii neema. Hapa Kazi Tu! Jokate Mwegelo,
Kaimu Katibu Idara Ya Uhamasishaji,
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) makao makuu.
**Chanzo cha habari hii ? JamiiForum**
Waziri Kairuki afanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini leo hii!
Waziri wa Madini Mhe Angellah Kairuki siku ya leo masaa ya Africa Mashariki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini. …..kwa picha na maelezo zaidi bonyeza ?? IssaMichuziblog
Happy Thanksgiving America!……. I’m thankful for you all, my good loyal readers. Mbarikiwe sana!
David Kafulila avua magwanda ya Chadema!
Lelya Bezuidenhout: baba yangu ni Magambo Makongoro Nyerere
Haya msikilize kwa makini muimbaji chipukizi anayekwenda kwa jina la Princess Lelya! Ni interview nzuri mtoto kaongea kwa confidence nzuri sana. Nakutakia mafanikio mema Lelya Bezuidenhout ?
Robert Mugabe ameng’oka!
https://youtu.be/7IlkoCl4nQQ
Ni nderemo zimerindima ndani ya nchi ya Zimbabwe!! Ameng’oka!! Robert Mugabe is no longer in power!…….Mimi siyo mwanasiasa hivyo sijui kama hii italeta amani na maendeleo zaidi au La! Lakini naweza sema ni mmoja ya watu ambao nilikuwa sipendezwi na kuwa na Rais mmoja kwa miaka yote hiyo! Kunatofauti kubwa sana kati ya chama kimoja kuwa madaraka na Rais mmoja kuwa madarakani!! Hivyo kwahili naungana na Wazimbabwe wote kusherekea ushindi huu!…..Mungu ibariki Africa!
Sir. O.O Igogo: Uwaminifu na huruma ni nguzo kuu ya maisha, zingatia.
Leo nimepewa somo na Sir O.O Igogo kuwa uwaminifu na huruma ni nguzo kuu ya maisha, hivyo nizingatie! Aliyasema hayo baada ya kunitumia picha ya aliyekuwa mke wa mmoja wa fundi wetu marehemu Tyson.
Mke wa Tyson alitokwa na machozi baada ya kukabidhiwa fedha ambazo ziligundulika kuwa zilikuwa hazijamaliziwa kulipwa katika kazi ya ujenzi wa ukuta wa nyumbani kwetu ambayo marehemu mumewe aliifanya mwaka 2014. Jamani msiwe wadhurumaji kwani hauto kaa ubarikiwe kamwe! Wengi wanashindwa kuelewa kwanini mafanikio yao huwa yanakuwa ya muda mfupi wakati wengine maisha yanawanyookea mika nenda miaka rudi! Acha dhuruma Mungu hapendi!! Machozi ya watu yanalaana sana! Btw, wangapi huwa mnaweka rekodi ya kila risiti na gharama za ujenzi wa nyumba zenu? Hii huwa naona sana kwetu kila jengo huwa nakitabu chake kila kitu kinarekodiwa na risiti zote zinatunzwa. Ujenzi ukikamilika basi kitabu kinakaguliwa na kufungwa na kuwekwa kwenye kumbu kumbu za kudumu. Sasa kama kuna mtu hakulipwa pesa zake kama marehemu Tyson au kuna kitu kilisahaulika kufatiliwaa basi kitafanyiwa kazi wakati huo. ………Anyway, poleni sana wafiwa. R.I.P Tyson!
Mwanasheria Alberto Msando arejea CCM kwa unyenyekevu!
Yule Mwanasheria wa kujitegemea, msomi wa kuaminiwa na mataifa yote, Alberto Msando arejea CCM kwa unyenyekevu mkuu! Akiri kuwa alipotea njia, alikuwa kipofu na sasa anaona kwani hataki kuongozwa na chama ambacho kina Mwenyekiti mmoja kwa zaidi ya miaka 10! Kwani huo pia ni udikteta ?? ……Alberto anakuwa mwanasheria wa pili (Lau Masha alirudi wiki iliyopita) ambao walikuwa upinzani na sasa wameamua kurudi kundini! ……As I always say, ” I’m not a politician” hence, my comment is respectfully reserved! Just wishing him the best of all!
Mama na wanawe! …..The Mashimi!
Mama na wanawe, the Mashimis’ katika ubora wao. Honestly nilikuwa napenda sana kupost family moments kama hizi because I strongly believe in family institution. Lakini wapika majungu na kamati ya ufitina wakaanza kupika majungu nakuwajaza watu hofu kiasi kwamba watu wakawa hawataki kuweka picha zao kwa hii blog. Hivyo siku hizi naweka only picha za watu ambao najua hawatakuja kusema “toa picha zangu kwenye blog yako”! Unless wewe mwenyewe uniruhusu, sito weka picha za watu humu. Ni za familia yangu na watu ambao najua they won’t bring drama to me!! Sitaki drama mimi I am too old for that crap!…….Anyway, nimependa hii picha, ni the Mashimis’ from Atlanta, Georgia. Wamependeza sana na ninawapenda ?❤