All posts by Alpha Igogo

Zamaradi Mketema: Usiangalie mawe kama SILAHA ukayakimbia ila badala yake yafanye ZANA katika kusimamisha himaya yako. MAWE yanasaidia KUJENGA!!

Sisi Binaadamu wengi ni watu tunaohofia MAWE, tunaishi katika hali ya kutafuta njia za kila aina za kukwepa kabisa kurushiwa na kuziba mianya yote itayoweza kutoa chakusema kwa adui zako kitu kinachopelekea kujikuta unaishi hadi maisha FAKE kwa kuhofia tu binaadamu, bila kufahamu mara nyingine ni vizuri kuyaacha yaje ili kujua yanatokea upande gani, yana sababu gani, yatakusaidia vipi na yatabadilisha nini pia kwenye maisha yako. Kwa upande wangu NIMECHAGUA kuyaokota na kujengea NYUMBA yangu, kila jiwe litakalorushwa kwangu nahakikisha siachi lipotee, nitaliokota na kuliongezea tu kwenye ujenzi wa nyumba yangu, hata kama lengo la mawe ni kuniumiza, nitahakikisha yananisaidia pia. Mawe ni BARAKA, mawe ni ongezo, na ni mafundisho pia. Tunajifunza mengi kupitia mawe yanayorushwa kwetu, tunakua zaidi, tunaimarika na kujijenga, tunafahamu nguvu tulizonazo na zaidi tunajifunza hata KUJIHADHARI Kupitia unavyonifikiria na kuyawaza juu yangu unafanya nijue nini natakiwa kufanya, unanifundisha wapi sitakiwi kuwepo nakadhalika, kiufupi UNANIAMSHA, na hata ule udhaifu unaohisi unaniumiza nao usichofahamu unanifundisha jinsi ya kuishi nao na zaidi kuufanyia kazi na kuufuta kabisa kama upo. Unaposema na kunisimanga juu ya jambo ni kunizindua juu ya jambo hilohilo hivyo kama lengo ni kukomoa unajikuta unafeli maana athari njema ulizoziacha utakuja kugundua ni nyingi kuliko zile mbaya ulizodhamiria.

Angalia kila jambo katika hali chanya na utaona faida yake, Usiangalie mawe kama SILAHA ukayakimbia ila badala yake yafanye ZANA katika kusimamisha himaya yako. MAWE yanasaidia KUJENGA!!

Better late than never!……Hongera sana Diamond!

 Japo karibia wiki inafika tangu ushindi huu upatikane -AFRIMMA 2017 Best Male East Africa hakuna ubaya kwa mimi kutoa pongezi kwa kuchelewa kwani wenzetu wanasema “better late than never”!……..Hongera sana Diamond hakika umeitangaza?? Tanzania katika nafasi ya kipekee sana. Ubarikiwe zaidi ya hapa! We are all proud of you the former ” Tandale” boy!  #Viva Diamond #Viva Wasafi ??

Hili halikubaliki! Mh. Paul Makonda tafadhali fuatilia hili!

 Nimesha sema mara nyingi na siku zote nitasema kuwa mimi si mwanasiasa nawala sitegemei kuingia kwenye siasa, na wala hata siku moja sitamtetea mwanasiasa yoyote yule! Mambo ya siasa nawaachia mwanasiasa wenyewe wateteane! Lakini naomba ieleweke kuna mambo ambayo yataniwia vigumu kunyamaza kama hill la kwenye video! Nahapa nitaongea kama Mtanzania, na kama mama! ……….Kwakweli hili swala limenihuzunisha sana! Hii hali siyo yakukubalika haswa katika karne hii ya 21! Nikiwa kama Mtanzania niliyezaliwa katika mazingira duni na wengi wa ndugu zangu bado wanaishi kwenye mazingira duni  hivyo, hawa watoto licha ya kwamba ni Watanzania yawezekana pia wakawa ni watoto wa ndugu zangu!! Hivyo siwezi kunyamaza kwa hili! Lazima jambo kama hill linalo hatarisha maisha ya watoto zetu likemewe na lipigwe marufuku mara moja!! Ni juzi tu tumepoteza watoto 32 wa LuckyVincent sec school (somahapa) halafu bado tu mambo kama haya ambayo yanahatarisha uhai wa watoto wetu hayajakemewa na kuweka sheria kali!?! Ni lini tutajifunza kuzuia majanga na siyo kutibu!! Watoto wanatakiwa kwenda shule kusoma siyo kutafuta na kubeba maji visimani!! Huu ni unyanyasaji wa watoto na kuwakatisha tamaa ya kusoma!! My brother Paul Makonda nimesikia hii ni Kinyerezi ambapo ipo ndani ya Mkoa wako, tafadhali naomba ufatilie hili swala!

#Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Africa!

“KAMA HAJAKUOA BASI SI MUME WAKO SOMA KISA HIKI CHA HUYU DADA.”

KAMA HAJAKUOA BASI SI MUME WAKO SOMA KISA HIKI CHA HUYU DADA.

Kuna watu wengine ambao unakutana nao katika maisha halafu wanaishia kukupa hasira tu, unawaza hivi ni kwanini sikukutana nao miaka kadhaa kabla nakutana nao sasa, lakini yote ni mipango ya Mungu.

Miaka mitatu iliyopita nilikua katika kipindi cha kupigania ndoa, kipindi ambacho nililazimika kufanya vitu vingi vya ajabu ili tu mwanaume anikubali, nilikua nadhindani na wengi hivyo nikiamini kua mimi ndiyo napendwa zaidi nilijua nitaolewa mimi.

Lakini mpenzi wangu hakujali hilo, baada tu ya kunipata alinigeuza kama ka ATM kake, wote tulikua wafanyakazi wa serikali, alitaka kununua gari, hakua na pesa za kutosha na aliniomba nimkopeshe. Nikiwa najua kabisa hatanilipa nilitoa kiakiba changu cha miaka miwili ambacho nilipanga kufungulia biashara na kumpa. Hiyo ilikua ni baada ya kumbembeleza na kumshauri sana kuwa kwanini afanye vile, kwanini tusingejenga kwanza.

Jibu lake lilikua yeye ni mwanaume siwezi kumpangia. Aliniambia kama nataka kumpanda kichwani wakati bado hajanioa akinioa itakuwaje? Niliufyata mkia nikanyamaza nikampa zile pesa lakini hata gari yenyewe hakununua, aliishia kuhonga Malaya wake.

Nilijua kwani walinipigia simu kunitukana kua mimi natafuta na wao wanahongwa, niliumia sana lakini baada ya kumaliza zile pesa basi alikuja kuniomba msamaha. Alijutia sana na kama unavyojua mwalimu wetu kipofu aliniambia msamehe, hakuna mwanadamu aliyakamilika.

Lakini sasa nilimpa mashariti kua tunapaswa kuwekeza katika maisha yetu, aliniambia anatafuta pesa anunue kiwanja na anataka kunioa. Kama kawaida ukisikia ndoa unchanganyikiwa, ingawa kwetu walikua wanamfahamu lakini sa alijitambulisha rasmi.
Alinivalisha pete ya uchumba kuonyesha kua alikua siriasi na mimi. Maisha yaliendelea na baada ya kuvalishwa pete nilivyokua mpumbavu nikageuka kua mke tena, nikijua kuwa nikikaa naye ndiyo nitamdhibiti nilihama kwangu na kwenda kuishi kwake, ndiyo ni upumbavu kuwa mke kabla hujaolewa.

Kabla hata sijaolewa basi tulianza kuishi pamoja nikiamini pete ndiyo cheti cha ndoa. Nilihamishia vitu vyangu kwake na tukawa mwili mmoja, hapo ndipo nilianza kuona chungu ya pilipili. Sio kwamba tu alizidi kuninyanyasa lakini alinipiga pia.

Akichelewa kurudi nikiuliza napigwa ananiuliza mimi ni Malaya tu kaniweka ndani na si mke. Lakini sinishavalishwa pete nilivumilia kwa wimbo uleule wa ndoa ni uvumilivu sijui hata nilikua navumilia nini wakati ndoa yenyewe hata sikua nayo.

Alinunua kiwanja kitu ambacho nilikua namshauri kila siku na akataka tuanze ujenzi, hapo nilijua mwanaume kabadilika, kwakua kipato chetu cha kawaida si unajua mishahara yetu hii basi aliniambia nichukue mkopo ili tukichanganya na kipato chake kidogo basi tujenge.

Nikijua kuwa tutakuja kufunga ndoa karibuni nilichukua mkopo, ujenzi ukaanza na Mungu si Athumani alijalia pamoja na vidilidili vyake vya kazini basi tulifanikiwa kumalizia ujenzi. Katika kipindi chote hicho tunajenga aligeuka na kua malaika, akiwahi kurudi na kufanya kila kitu kama mume mwema.

Lakini baada ya kumaliza kujenga, nikitaka kuhamia hapo ndipo ilizuka kasheshe. Wanaume ni washenzi ndugu zangu na hapa ndiyo najuta kwanini Kaka iddi sikukuona mapema nikasoma makala zako. Unakumbuka makala moja ulisema kama mwanaume hajakuoa si mumeo chako ni chako na chake ni chake. Hilo ndiyo lilinitokea, nikijua najenga na mume wangu mtarajiwa kumbe nayeye alikua anajenga na mtu mwingine.

Yule mwanaume hakutumia hata senti tano katika lile jengo, alikua na mwanamke mwingine ambaye naye kama mimi alichukua mkopo tena wakwake wa benki kibiashara na kuwekeza kwenye ile nyumba. Lakini yule mchaga alinizidi kete, wakati mimi nasubiri kuambiwa tuhamie yeye alihamia kabisa.

Ndiyo kwa mbinde alianza kuishi pale kwenye ile nyumba, nilipotaka kwenda na mwanaume alikataa hakutaka twende, nilipokazania sana alinipiga na kunifukuza, ndiyo alinifukuza na kuniambia sina changu, nililazimika kuondoka na kwenda kuishi na rafiki yangu.
Wakati nikiwa huko nikagundua kua nina ujauzito wa wiki mbili, namuambia ananiambia hanijui. Yaani sijui nini kilitokea lakini nilisikia katangaza ndoa na yule mwanamke aliyekua akiishi naye, kabla hata sijastuka naambiwa wameoana ndoa ya kiserikali.

Ndiyo nikabakia na mimba yangu, yaani nilibaki nalia tu, nilitamani hata kujiua lakini maisha ilikua ni lazima yaendelee. Ilinibidi kuanza upya kwani mbali na ujauzito lakini mshahara mzima ulikua unaishia kulipa mkopo wa nyumba ambayo nilishanyang’anywa.

Mpaka leo hii nalipia mkopo na mpaka leo hii nawaona tu wakipita wapo na furaha na maisha yao. Yaani mimi nina mtoto wangu na wao yule mwanamke kumbe alishazaa naye mtoto mmoja mimi sijui na sasa ana mimba nyingine.

Natamani hata niende niichome moto ile nyumba kwani napata uchungu kila siku nikiangalia Salary Sleep yangu, kwa bahati mbaya wote tunaishi hapahapa Dar hivyo haiwezi pita wiki sijawaona. Nina hasira sio kwasababu nimedhulumiwa tu bali nina hasira na wewe Kaka Iddi kwanini sikukujua mapema nikasoma makala zako mapema. Nina uhakika asilimia mia nisingefanya upuuzi nilioufanya. Kama unakumbuka tulishaongea niliponunua kitabu chako.
Nimeandika hivi ili wanawake wenzangu ambao wanabembelezea ndoa nao waamke na wasiwe mabwege kama mimi. Natamani hata kila siku uirudie ile makala yako kuwa kama mwanaume hajakuoa basi mali zake hazikuhusu.

Kuna wengi tu humu mnajifanya mnapendwa lakini siku likiwatokea mnawalaumu wahusika kumbe makosa ni yenu. Nimejifunza maisha yanaendelea ila nashukuru Mungu nilikupata kwani nilishakata tamaa, ila kwa ushauri wako kaka nimeanza biashara na inaenda vizuri.
Nashukuru kwa kitabu chako pia kimeniamsha sasa najielewa. Sipo kwenye ndoa wala mahusiano kwa sasa ila najua kabisa kuhusu wanaume, nimejifunza mengi kupitia makala zako na zaidi katika kitabu chako, kaka umeniponya.  Sasa hivi nataka kulipa kisasi, sitaki kulipa kisasi cha kuchoma nyumba yao moto bali cha kujenga nyumba yangu na kufanikiwa zaidi. Nakumbuka siku ya mwisho tulipoongea uliniambia hakuna kisasi kizuri kama kua na furaha zaidi ya mtu aliyekuumiza kumuonyesha kuwa humhitaji yeye kufurahi Ahsante kaka Iddi.

 

#Nimekopi kutoka Facebook na kuleta hapa kwa blog. Sijui muhusika!

Imbumba Yamadoda: What I am doing for myself I am actually doing it for you! And what you are doing for yourself you also doing for me!

A must watch to all African men!! Hii video niliiona almost two months ago, but nikawa nasubiria a “proper” day kuiweka. Sasa kwakuwa bado tupo kwenye furaha ya maadhimisho ya mtoto wa kike duniani basi nimeona ni vyema kuiweka! Kwakweli huu ni ukweli kabisa! Watoto wa Africa haswa wakike wamewekwa kwenye “pressure” of how to become a good citizens, great mothers, wives, sisters, and aunties bila kujua kuwa it always takes two to tangle!! Unakuta mtoto wa kike very well organized mentally, spiritually,  physically, na hata financially lakini anaangukia kwenye mikono ya mwanume asiye jielewa kabisa!! Mnyanyasaji na mambo mengi ambayo yanafanya maisha yao kutokuwa na furaha! A totally unprepared man for familyhood!! Na ukijaribu kuuliza hawa wadada utasikia ma’am! “All men are the same”!! Hivyo hakuwa na chaguo zaidi ya ku settle down for less!! ………Wazazi, waleeni vijana wenu ukijua kuwa kesho atakuwa mume wa mtu, mmoja ya wana jumuiya hivyo lazima awe teyari kuwa good citizen! Kuwa na hela doesn’t make someone a good citizen or good husband tabia yake na malezi ndio vitaeleza huyo kijana wako ni mtu wa namna gani! Nimeona vijana wenye pesa na ni wanyanyasaji wa wanawake mpaka inaogopesha! Wengine ni rapists and molesters! Tuwalee watoto katika njia ipasayo ili wasiwe mzigo kwa wengine na taifa analo ishi ni jukumu lako wewe kama mzazi!

 

Siku ya mtoto wa kike duniani: “Thamani ya Binti Na Uongozi wa Maadili”

“Thamani ya Binti Na Uongozi wa Maadili”  “Mcis Kelvin kutoka skonga kushoto Katikati ni Dada Glory kutoka @mwanamke_na_uongozi Mwisho ni @temidayo_gm Photo credits. @timesfmtz”

Flaviana Matata: The truth is that we can only unleash the power of young girls through access to quality and safe education.

“Today is #InternationalDayOfTheGirl and the focus is on the power of adolescent girl. The truth is that we can only unleash the power of young girls through access to quality and safe education. I am here with one of our scholars Nyamizi who is in her last year of high school. Young girls like Nyamizi have the potential to be scientists, teachers, farmers, artists, mothers, but that is only possible if they are provided with a conducive environment to thrive. @flavianamatatafoundation strongly believes that an educated girl will be a better mother that will nurture and raise her children to be better citizens. Educating a girl is a smart investment because it’s an investment into the prosperity of communities and nations. #FlavianaMatata”

Ridhiwani Kikwete: #sikuyamtotowakike; Huyu ni Binti yangu. Furaha yangu Ukamilika ninapomuona amefurahi

“#sikuyamtotowakike Huyu ni Binti yangu. Furaha yangu Ukamilika ninapomuona amefurahi. Namuona Mama,Namuona Mlezi, Najiona Mimi , Ninaiona Tanzania. Nakupenda sana Mwanangu.”~~~~~~ Mbunge. Ridhiwani Kikwete

Siku ya mtoto wa kike duniani: Tokomeza mimba za utotoni kufikia uchumi wa viwanda

“Kinachoendelea muda huu hapa Tarime, kongamano linalohusisha Wazee wa Mila, watoto wa kike, na wadau wa Maendeleo – Siku ya mtoto wa kike 2017 ni ??… Unapitwaje jamani.. kauli mbiu ni “Tokomeza Mimba za Utotoni kufikia uchumi wa viwanda.. Wewe unawalinda vipi watoto ???? Ni jukumu letu sote ?” Joyce Kiria

Siku ya mtoto wa kike duniani: Jokate awa mgeni rasmi shule ya Turiani, Magomeni, Dar!

 

Jokate Mwegelo ndie aliye kuwa Mgeni Rasmi siku ya leo ambayo ni siku ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani yaliyofanyika katika shule ya sekondary ya Turiani Magomeni. Alipata nafasi ya kuongea na wanafunzi wa kidato cha kwanza na tatu yaliyo andaliwa na taasisi ya @mwanamke_na_uongozi Iliyokuwa na kauli mbiu Thamani Ya Binti Na Uongozi Wa Maadili! “Walikuja kunitembelea, nikawaalika chakula tukala wote then tukapozi kwa picha ?” J. Mwegelo

Mama na mwana: Hakika wema na fadhili zako zitanifuata siku zote za maisha yangu!

Ni kwa neema tu! Nasema ni kwa neema yake Mungu kwani akili yangu haikuwai kuwaza kuwa ipo siku kama hii! Hivyo namshukuru sana Mungu kwani ni hakika wema na fadhili zake zitanifuata siku zote za maisha yangu, nami nitadumu ndani yake! Nimeweza kuona ukuu wa Mungu kwa kufanikisha uumbaji wake! Amenibariki na rafiki wa kweli ambaye upendo wetu utadumu milele na milele!  ………Najua tunamipango mingi sana naomba Mungu azidi kutuwezesha katika kila jambo! Moja ya vitu ambavyo nasubiri kwa hamu sana ni passport ya mwanangu!! Yes! her American passport!! Ee Mwenyezi Mungu mimina baraka zako!! Yani can’t wait!! Maana tutatembe hii dunia mpaka ndege zinune  zigome kabisa kuruka ?? ……..Anyway, namshukuru Mungu kwa mbaraka  wa huyu mtoto! Naomba azidi kunilindia na kumuongoza katika kila jambo haswa kiroho, asikae mbali naye!

Hongera sana Waziri Angellah Jasmine Kairuki!

Naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri mpya wa Madini, Mh Angellah Jasmine Kairuki! .......Kama kumbukumbu zangu zipo sawa basi naamini wewe ndio Waziri wa KWANZA MWANAMKE aliyewahi kushika wizara hiyo nyeti! Naamini utendaji wako unatija kwa taifa letu la Tanzania ndio maana Rais Dr. John Pombe Magufuli pamoja na washauri wake wakaona ni vyema ukabidhiwe hiyo wizara. ........Nakutakia utendaji na uongozi mwema ukizidi kuweka maslahi ya taifa letu mbele. Hongera sanaaaaaa! #Mungu Ibariki Tanzania #Mungu Ibariki Africa

Edwin Kihore: KEEP YOUR CROWN

                KEEP YOUR CROWN
You are a person of great value! In fact, God has crowned you with his glory and honor.
REVELATION 3:11 “Tells us to hold fast to what we have and not let anyone take our crown. Our Crown represents our destiny, dream, goal, talents, authority in Christ and God’s blessings and favor in our life. Yet, many people have let other’s words or unfair situation knock off their crown. Jesus says JOHN 5:41 “Your approval or disapproval means nothing to me.” He was saying that it doesn’t matter what other people say, or think or do, He has give is approval and bless. Start build you confidence back. So, you can do everything through Christ.

Kheri ya siku ya kuzaliwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete!

Nakutakia kheri katika siku yako kuu! Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa rehema akuzidishie baraka zake, akazidi kukupa afya njema na amani nyingi moyoni! Asante sana kwa kuliongoza taifa letu la Tanzania kwa miaka 10. Ubarikiwe sana. Happy birthday baba Ridhiwani!  ?

Zamaradi Mketema: Namshukuru kwa yote yaliowahi kutokea kwenye maisha yangu….!

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote waliotenga muda wao kwa mapenzi kabisa kunitakia heri katika siku yangu ya kuzaliwa, kwa kila alieniwish hata kama sijaona nataka utambue NATHAMINI SANA SANA SANA, MUNGU awabariki kwa upendo wenu kwangu na asanteni sana kwa Dua njema Birthday ya mwaka huu kwangu ni kubwa mno na yenye Baraka nyingi, nitakuwa kiumbe wa ajabu kama SITAMSHUKURU SANA MUNGU kwa mengi aliyoyatenda kwenye maisha yangu, hii sio akili yangu, wala sina maarifa ya kuzidi wengine ila huyu ni WEWE MUNGU WANGU. Namshukuru kwa KUNISHIKA MKONO, namshukuru kwa KUNIONGOZA, namshukuru kwa KUNISIMAMIA, namshukuru kwa KUNILINDA NA KUNIPIGANIA, na namshukuru kwa yote yaliowahi kutokea kwenye maisha yangu haijalishi kwa wengine yalikuwa na sura gani lakini naamini mengi ni ngazi ya kunifikisha nilipo. Naendelea kujikabidhi na kukabidhi kila kilicho changu mikononi mwake na kumuomba aendelee kunilinda na kunilindia maana mimi kama binaadamu sina ninachokiweza. Bila kusahau wazazi wangu waliotangulia mbele za haki, Zamaradi wa leo ni taswira yenu, asanteni kwa malezi yenu na asanteni kwa kila MLICHOKIPANDA kwangu, Nawaombea kwa MUNGU aendelee kuwapumzisha kwa amani na awape makazi yaliyo mema INSHA’ALLAH Na kwa kila mwenye mapenzi mema, ndugu, jamaa na marafiki wote mfahamu NAWAPENDA NA ASANTENI SANA SANA.

Okay!! Major General, what is real going on?!

First of all, I love your conservative-modesty look! Umependeza sana but nywele not feeling it lol!……… Secondly, what is really going on Major General!?! So many rumors are going on, from “it might be over” to ” DNA has proven the baby boy is not his”!! As your fans we really deserve to know the truth, only from your mouth! And some of us don’t do “snapchat” thus better be an interview or. Live Instagram video ?? Please, we need to hear from you!

Jacqueline Mengi: Apendwae akajua haachi kujishauwa!

If the only prayer you said in your whole life was “thank you” that would suffice. Meister Eckhart

Nimekwenda kwenye Instagram page ya Jacqueline Mengi nikakuta ame post msemo huu “Apendwae akajua haachi kujishaua”!………… Kwakweli hata mimi nakubaliana na huo msemo! Raha sana kupendwa na mtu anayekupenda kwa right reasons and in a right way!! Kuna watu wanaweza kukupenda in a wrong way kama Bobby  Brown na Whitney Houston! Bobby Brown alikiri kuwa alimpenda Whitney Houston but he didn’t love her in a right way!! Sikiliza sehemu ya hiyo interview hapa ??

Hapo ni vile mtu anakupenda lakini anashindwa kukukataza au kukuzuia kwenda kwenye njia mbaya badala yake na yeye ana support njia zako mbovu in the name of “LOVE” halafau wote mnaangamia. Sasa kwa hawa aliye salimika ni Bobby peke yake Whitney na binti ya ke BobbiChristina wakafariki kwa drugs….. Mtu anyekupenda katika njia sahihi na kwa sababu zilizo sahii siku zote ata wish to see the best of you! Mtu huyo atapigana mchana na usiku kuwakikisha hauingii gizani na kupotea. ………Hivyo ukimpata mtu wa namna hiyo huna budi kushukuru Mungu na kama binadamu basi kujishaua lazima!…….. Wewe jishaue tu Mrs Billionaire, acha wenye wivu wajinyonge tu ??? kama hawana kamba tutawanunulia waseme tu ???

Siku ya walimu duniani: Leo ni siku ya walimu duniani. Je nimwalimu yupi unamkumbuka?!

Leo ilikuwa siku ya walimu duniani. Jokate akauliza je, ni Mwalimu yupi unamkumbuka?………….. Binafsi nawakumbuka walimu wangu wote kuanzia vidudu mpaka secondary lakini hawa walimu wangu wa vyuoni nawakumbu baadhi tu kwasababu ni wengi na wanakufundisha kwa semester! …….Kwa elimu yangu ya vidudu / cheke chea na grade one to two namkumbuka Mwalimu Jenifer ambaye alinifundisha vidudu pale Mgulani chini! Grade one and two namkumbuka sana Mama Mwalimu Massamu. Japo walimu wote ni muhimu sana katika kila level ya elimu lakini hawa walimu wangu wa elimu ya awali nawashukuru sana tena mno! Wanasema kuwa Mwalimu ni wito lakini kufundisha elimu ya awali ni zaidi ya wito! Mungu awabariki walimu wote duniani ambao wanafundisha kulingana na maadili ya uwalimu!

Jokate Mwegelo: You can check me out featured in this months @ Elle South Africa magazine. ?

You can check me out featured in this months @ellesouthafrica magazine. ?” ~~~~~ Jokate Mwegelo My Jojo looking ???……. I love them sneakers ??

LeMutuz: vijana wadogo sana wanaojaribu kutafuta muongozo wa maisha nyuma yenu kuna vijana ambao majumbani mwao na familia zao hakuna muongozo bora wa maisha ndio sababu wapo Instagram kujifunza

 LIVE STRAIGHT TALK:- The Art of peace hii picha ni kumbukumbu sana ya siku ya pili ya kuanza kwa mahusiano yao yaani @diamondplatnumz & @zarithebosslady na jana Instagram nzima tumeshuhudia mambo yasiyokuwa ya kiungwana baina yao...my appeal to both of them ni spare us your close friends and your fans cause wote kwa pamoja mna wafuasi Millioni 7 wengi ni vijana wadogo sana wanaojaribu kutafuta muongozo wa maisha nyuma yenu kuna vijana ambao majumbani mwao na familia zao hakuna muongozo bora wa maisha ndio sababu wapo Instagram kujifunza now kwa you guys Icons wa maisha ambayo Vijana wengi wangependa kuwa nayo mkianza kuwaonyesha kwamba mkifarakana cha msingi ni kwanza kuionyesha Dunia kwa kutumia kuunfollow each other huku kwenye KIOO yaani Instagram mtawavuruga sana vijana wadogo Instagram ...na the worst of all ni sisi marafiki wa karibu mtatupa wakati mgumu sana wa kuchagua sides baina yenu that is not fair to us your friends ...again ninawaomba sana mtumie busara na uungwana wote sio wageni wa Mapenzi na watuwazima kila mmoja anajua anachokifanya kupendana na kuachana ni mambo ya kawaida na infact hata kurudiana tena ni kawaida sana so please guys calm down and solve your ishus kwa manufaa ya wafuasi wenu Milioni 7 they deserve better than what you guys did yesterday ...please I am again appealing to both of you @zarithebosslady and @diamondplatnumz please spare us na msipokuwa makini mtawapa maadui wenu wakubwa mwanya wa kuingia hapa kati yenu na kuwavuruga zaidi ....kwenye mapenzi kufarakana ni kawaida na kuachana ni kawaida na kurudiana ni kawaida pia ila angalieni msije mbele ya safari mkaja kushindwa ku overcome the distarctions you are about to bring to yourself wazungu wanaita SELF DISTRACTIONS ....love U all guys but please tuoneeni huruma mashabiki na marafiki zenu tusifikie kuchagua sides baina yenu......MATATIZO KWENYE MAPENZI YANATATULIWA YAKISHINDIKANA MNAACHANA KWA AMANI!....... MUNGU AWATANGULIE WOTE! - le Mutuz