“When we go a wrong path in life, God grieves over our foolishness, because He knows we are only hurting ourselves. He also knows that this is our natural tendency, because we
-like sheep-easily wonder and stray from the only Shepherd who can guide us and keep us safe.
What decision are you facing today? Don’t rely only on your own wisdom, or even on the wisdom of others. Instead, seek God’s will, and ask Him to guide you and show you His will.
Remember: His way is always best-always. We all, like sheep, have gone astray,
each of us has turned to his own way [Isaiah 53:6]” Yani Mungu huyu!! Nilikuwa Facebook kabla sijafunga nakutana na ☝ hilo hubiri toka kwa Pastor Caleb Migombo, nikajikuta ghafla nimekuwa mpole. Unajua maybe because I love Zari so I put my emotions to her situation nakusahau kuwa kuna Mungu! Eeh, Mungu nisamehe! And let me withdraw my words about the Zari situation: Zari whatever God tells you to do, you follow Him! Mlilie Mungu akupe hekima ya uwamuzi wa kufanya not us human being for we all are sinners in God’s eyes! …….As I said whatever decision you make I will respect you. But seek God’s wisdom only!! Be blessed
Zari my dear, I can only image what you’re going through right now as I’ve never been in your shoes and I will never wish to wear them even for a minute!! But the only thing I know for sure is that, this family including Diamond doesn’t deserve you!! Zari just give up the fight and concentrate on the wellbeing of your children!! ………Sikiliza Zari this picture na nyingine nyingi ambazo familia ya Diamond wamepiga na Hamisa speaks volumes!! Hamisa is not a sidechick or just a babymama Hamisa ni mke mwenzio my darling!! Huo ndio ukweli!! Sasa uwamuzi ni wako kuwa kukubali ukweli kuwa mpo wawili au achana na Diamond uendelee na maisha yako but you can not fight Hamisa!! Mtoto kapewa jina la baba yake Nasib na wazazi wote wapo Tanzania? Zari you can’t fight this!! Yani hata hizo picha watakazopiga wakati wa parenting time hata kama Hamisa hato kuwepo lazima zitakukera!!
Mimi ningekuwa wewe ningetafuta njia ya co-parenting na Diamond kama ulivyofanya na marehemu Ivan Ssemwanga!! Ningetoka kabisa kwenye social media for now na kuishi a very low key profile life. Yani concentrate na mambo yako na watoto zako basi! Achana na marafiki just your family members only!! Once ukiona uko powa then come back kwenye social media life again! For now ungeacha kwanza ………..Hachana na hii family as I said before they don’t deserve you!! Fikiria jinsi Diamond alivyokuwa anachekwa kuwa “HAZAI” magazeti yote yakamwandika jinsi his girlfriends wanasema hazai!! At your age you took the fall, with all the risks na kumzalia sio mtoto bali watoto and look how they repay you!! Achilia mbali jinsi ulivyo muonyesha njia ya kuweza kufanikiwa kimaisha hayo yote hawakujali ndio kwanza anamleta mwanamke kwenye kitanda anacho lala na wewe?!! This makes me sick whenever I think about it!!……..Unajua kuzaa na mwanamke mwingine unaweza piga moyo konde ukasamehe, lakini the fact kuwa this happened in your bedroom in the same bed you sleep with him!! That’s something else woman!! Mtu akudharau lakini si kwa kiwango hichi jamani!! Hamisa yupo comfortable in your bedroom utafikiri pale ni chumbani kwake??!! O’Lord of mercy!! Then mama mtu yupo sawa kabisa na mambo haya yote tena yanatendeka mbele yake!! Nimemshusha heshima huyu mama!! Something is wrong somewhere!! The whole management knew about it and no one said anything to you? Isn’t this how Michael Jackson died? People are selfish!! …………But in the end this is your life, you decide what’s best for you. I will surely respect your decision!! Just remember you once said you left Ivan Ssemwanga because you didn’t want your boys to think was OK to mistreat woman!! Think deep you got your daughter now, think deep!!……Pole sana!!
Kwanza nianze kwa kusema hongera sana Diamond na Hamisa Mabetto kwa kujaliwa mtoto wa kiume. Kwakweli Mungu kawajalia mtoto mzuri mno and he got ‘blue’ eyes?! Wow! Hongereni sana……… Diamond umefanya uwamuzi bora wa kumkubali mwanao mtoto hakustahili drama hizi zote ili wewe ukubali hadharani. But nothing worth of respect like a personal who accept and take accountability of his mistake! Own your mistake no matter how bad they are!! And for that, I salute you!! Mungu awatunzie mwanenu I can see another super star in the making!! Congratulations to both of you!
Over the weekend I visited a young girl from Singida who I had sent to India for treatment during my days as a politician. She wasn’t feeling well, so I made it a point to be there for her during her doctors visit in Dar Es Salaam. #CharityBeginsAtHome ????
I’m super happy my beautiful, smart, elegant, kind, loving, and “environmental friendly” babysister is back just like the way I wished!! ?? Yes! Such an environmental friendly lady; wanawake wengine ni hatari kwa mazingira yetu tunayo ishi!! Maongezi yao yamejaa chuki na uchochezi tuuu! Kazi yao is to pollute hali ya hewa ili kila mtu awe miserable kama wao! Wanawake kama Jojo ni wanawake adimu sana siku hizi! Woman with class!…….so happy! Welcome back baby girl you look AMAZING! Gorgeous is understatement kwakweli……….. We love you Jojo!?? ??
“Half time is not full time and HIS calendar for your life is not man’s calendar. BE ENCOURAGED! DON’T GIVE UP. With God all things are still possible!” Everyday is a fresh start with potentials. .. keep the faith…. keep on believing in God. God is the referee of all referees until He says it is over. Have a blessed week ahead….”~~~~~ Zari the BossLady
Nawauliza walimwengu wa Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla, yuko wapi Jokate wangu???? Mimi sitaki matani ya hivyo!!! Siku zaidi ya kumi hajaonekana yuko wapi?? Na nini mbaya imemkuta?!! Kamanda Sirro, please check on my baby sister please!! Kaka yangu Paul Makonda nakuomba unitafutie Jojo wangu, tafadhali hii siyo powa kabisa!! Jojo, I miss you beautiful where are you my babysister? Please, I want to see your beautiful face and cute smile please!! I hope you’re well wherever you’re! Let me know baby girl! Love you ??
“Watu wanafanyaga mambo magumu halafu wanategemea matokeo yawe rahisi INASHANGAZA SANA!!” ~~~~ Zamaradi Mketema
Dah! Ujumbe mzito huu! Bado natafakari! Lakini ni kweli kabisa kwani huwezi tengeneza uji wa vitumbua ukitegemea kupata maandazi!! Huu ujumbe umenichoma ?? moyo in a positive way!!
LIVE STRAIGHT TALK:- The Art of growing up process historia inatakiwa kuwa @diamondplatnumz ndiye Mtanzania wa kwanza kuandika mafanikio makubwa ya music kuliko Wanamuziki wote wa Taifa hili walio hai na wasiokuwa hilo by FACTS halina ubishi ...leo ninaomba kuwakumbusha WaTanzania wenzangu kwamba kuna wakati tunakosea sana tunapomuhukumu huyu kijana mdogo kwa mapungufu yake huwa tunasahau kuwa ni Kijana mdogo sana mwenye umri wa the 20s so Scientifically au Theologically ni HAKI YAKE YA KIMSINGI kufanya makosa mengi kwa sababu umri wake unamruhusu ...tunamharakisha sana kuwa mtumzima wakati he is not yaani kama Wanawake wengi wanavyowalalamikia Waume zao kuwa hayupo hivi au hayupo vile ukweli ni kwamba he is not what you want now muache au baki naye ila nyamaza ...I mean hebu wale wote mnaomlaumu sana huyu Kijana mdogo sit down and look back ulipokuwa kwenye umri alioano wa the 20s akili zako zilikuwa zinafananaje? makosa mangapi uliyafanya? inaitwa process na ndio makosa makubwa Baba yake Michael Jackson aliyafanya kwa mtoto wake kwa kujali sana kipaji cha mtoto wake bila kujali ubinadam wake akaishia kumnyima nafasi ya kuwa mtoto mpaka kijana matokeo Michael alipokuwa mtu akawa hajielewi kama ni mtoto mdogo au mtumzima now na sisi kama Jamii tunataka kurudia makosa yale yale ya kumnyima Diamond process ya ku Grow up tunataka awe mtumzima ghafla kusudi afanane na muziki wake au our imaginations it is wrong TUNAKOSEA SANA ...sometimes ninashangazwa sana na hata yule Mpenzi wake anapomfanyia mambo ya kumrushia maneno ya shombo kwenye Social Media on a serious note huwa kwa sisi wenye AKILI KUBWAZZ anajichoresha cause alitegemea nini kumpenda Kijana mdogo in his 20s? ....I mean guys everybody back off tumpe nafasi kijana mdogo aishi maisha yake akosee awe sawa ni process ya kukua ambayo wote tumeipitia ..I mean unakuta yule Kibibi kule USA mtumzima Mama wa Watoto 3 Baba mbali mbali kimeachwa na Mume Jobless, Homeless hana hata Taifa maana hawezi kurudi tena Tanzania hata akiwa amekufa na yeye unamkuta anashambulia mapungufu ya Diamond kama vile na yeye ni kijana mdogo badala ya KUJITAFAKARI ATAZIKIWA WAPI NA NANI! ...guys tumuache Diamond awe Diamond! - le Mutuz
Ok LeMutuz, uliyoyasema yote ni ya ukweli kabisa nakubaliana na wewe lakini kumbuka Diamond himself decided to wear "big boy's shoes" thus must accept all the responsibilities that comes with it!! Ingekuwa ni mtoto wa kike anafanya hayo afanyayo Diamond naamini hata wewe ungekuwa mmoja wa watu wanaomponda! Tuache double-standard! Kama ameamua kuwa na watoto then he needs to act like someone's parent not a teenager anymore!! Plus ashukuru kuna watu wanajali hata kuamua kumwambia ukweli ili asiangamie kabisa japo wengine ni wivu na roho mbaya ndio zinawasumbua!................When comes to his relationship with Zari; you're absolutely right! Zari should have known the consequences of being in a relationship with a post-teenager boy!! Kwenye hii situation, she's the one who's grown thus she needs to make some grownup decision to either let Diamond go or pull-up her "big girl panties" and suck it sincerely!! It seems to me Zari wants husband around but Diamond is not ready to seattle down, he wants to "play house"! It's sad but is the truth!
Napenda kuchukua nafasi hii kwa kumpa pongezi na hongera nyingi sana Bertha kwa kutolewa mahali, kuvikwa pete ya uchumba, na kufanyiwa send-off party ya nguvu sana. Mungu awalinde awaweke salama mpaka siku ya harusi yenu. Mkawe na ndoa yenye furaha, amani, na upendo mwingi, Mungu atawale maisha yenu, awe ndio kimbilio lenu, na ngao yenu wakati wote. Hongera sana. Wapendwa Bertha ni ndugu yake na Foster Mbuna-Mkapa. Hivyo hizi picha zote kwa hisani ya Foster. ?? Foster katika ubora wake! I love everything on her! Beautiful ladies! Na hizo shape, mashallah ?
Elimu juu ya maisha sio lazima ujifunze kutoka kwako au kwa wazazi wako. Muda mwingine unaweza jifunza kitu kikubwa ambacho kitabadilisha mwenendo wako au mtazamo wako wa maisha, jinsi unavyo tafakari mambo, na jinsi unavyo fanya maamuzi toka kwa marafiki au a total stranger!. Sasa Steve Harvey alijifunza kuwa njia pekee ya wajukuu na vitukuu wake kumkumbuka na kujua jina lake ni kuishi maisha yake lakini kwa wakati huo huo lazima awe na “legacy” yake ambayo hata akifa wajukuu na vitukuu wake watamjua jina lake! Na somo hili alijifunza toka kwa bibi wa rafiki yake wakati akimpa wosia kabla hajafariki.
Kuwa na mipango endelevu ni swala hata Biblia (kwa Wakristo) inatuambia ni vizuri kuwa na mipango endelevu, kuzaliana na pia kujiendeleza kiuchumi. Hii kwa Africa ilikuwa ni kuwa na watoto “wakiume” wengi kwasababu watabeba jina la baba forever, waliamini mtoto wakike akisha olewa sio wako tena na anatakiwa kuchukua jina la mumewe!! Mwe, mie shangazi zangu walisema ni mwiko kuchukua jina la mumeo kwani sio baba yako ?? shangazi zangu hakuna aliyebadilisha jina, hata dada zangu / wadogo zangu walio olewa sijaona aliyebadilisha jina. Siku hizi ni wachache sana wanafanya hivyo kutokana na carrier kuanza kubadilisha ni process ndefu sana. Hivyo wanaishia ku hyphenated. Haya nawe jifunze hilo, kama unataka wajukuu na vitukuu wako wakukumbuke anza kuwa na mipango endelevu sio kula bata tu! Kwa mfano, hawa wajukuu wa baba yangu unafikiri watamsahau babu yao? Hata kidogo! kwasababu amewapa kumbukumbu ya kudumu. Sio lazima uache mali hata mafunzo fulani ya hekima kwa wanao ambayo yataishi ndani yao milele nao wata waeleza watoto zao kuwa walifundishwa na baba / mama yake…….. Ishi maisha yako lakini uwe na mipango endelevu ili wajukuu na vitukuu vyako wakumbuke jina lako.
Ain’t they beautiful! Rafiki yangu kipenzi na college mate wangu Dinnah (kulia) akiwa na rafiki yake waliosoma wote secondary, anaitwa Erica. ……..hapo wapo South Africa enjoying some quality time together. Dinnah ni owner wa Masaki Computer and Printing hivyo nawaomba follow hiyo account ya Masaki kwenye Instagram na pia kwa wale mliko Tanzania tafadhali muungeni mkono rafiki yangu ??
Haya msikilize mzee wetu Dr. Lennard Tenende akielezea historia ya maisha yake. Naona ni mzee mwenye uzoefu mzuri sana katika mambo mbali mbali ya taaluma na kijamii. Msikilize mwenyewe.
Kumbe mzee Tenende ndio muanzilishi wa DICOTA?! Mmh! Mimi sio mpenzi wa DICOTA, maybe I need more education about DICOTA lakini niliwahi kumuuliza "Dr Ndaga" alipokuwa President wa DICOTA akasema "ni chama cha Educated Elite" ambao wanafanya mambo "makubwa makubwa" sio kuandaa BBQ na baby-shower parties!! Sasa mimi I don't consider myself "educate" or "elite" hivyo siwezi kujihusisha na DICOTA. Plus inawezekana DICOTA ina nia na malengo mazuri lakini naamini kuna watu fulani wameingia kwenye uongozi wa DICOTA ambao hawana nia nzuri na wataivuruga sana hiyo DICOTA! Kama mnaweza kuwatoa muwatoe. Lakini hayo ni maoni yangu tu, you can ignore me as I'm not a part of "Educated Elite" ??? So funny!.......?? Btw, wale walio wasema Bungeni ni wanachama wa Chadema sio mimi naomba ieleweke hivyo.
"Ni kati ya achievement ni kubwa kuliko hayo ma-PhD unayo yasema"! Hayo ni maneno yake mzee Dr Lennard Tenende kuhusu mkewe. Wow! What a humble man! Yani mwingine angekazana kusifia hayo ma-PhD yake wee mpaka mngekoma, Wahaya mpo? ?? Dr. Mwakasisi umemsikia mwenzako ?? ............. Halafu nyie wadada wa 21st century mnaona wazee wetu walikuwa hawaangalii kama umepaka poda, wewe kwenye mchaka mchaka akaona mdada mrembo wa kuoa! Sasa nyie poda mnapaka na editing juu halafu ndoa baada ya miezi 6 imekwisha ?? Stop being so fake, let the man fall in love with your heart and character not your makeup and lipstick ??............... Nimeona. Mzee Tenende amekuwa emotional kidogo kuhusu kuwa na watoto wengi, amesema kitu ambacho Vivica Fox alisema kwa Oprah (SomaHapa) kuwa anajutia kutokuwa na watoto, kama angelijua angezaa hata watano! It really got me thinking ??....... nice interview!
"Karibu uraiani Sanjay ?? (Ni hali tu wote tutayapitia nitaingia mimi nitoke Sunil Sheti) #SioHabari"??? Nacheka siyo kwamba mazuri but the "humor" is so for really! ?? Yani huyu Idriss is a true Comedian, mtu ambaye anaweza geuza kitu cha huzuni kuwa chakawaida mpaka kuchekesha, then in the end unabaki unajiuza kwa kina about life! Like kumbe Manji asingekuwa na pesa ndefu ni mkaka/baba wa kawaida sana, then unajipa moyo kumbe hata mimi si mbaya "pesa ndio kidogo na matumizi ni mengi" in Akothee Akothee's voice ?? huyo ni comedian mzuri sana!
Japo kwa kuchelewa siku moja , naomba niwatakie kheri na furaha ya kutimiza miaka 53 ya ndoa kwa baba na mama yangu mkubwa- Mr and Mrs Joseph Musira. Anniversary yao ilikuwa jana tarehe 09/12. Hawa ndio walikuwa my 2017-Hottest And Best Couple Of The Year! (SomaHapa) Naomba Mungu awazidishie baraka zake na awaweke salama mpaka tutakapo onana! Happy Anniversary wazazi wangu.
"When you meet person with means, a person that is well-off you think is successful that you always wanted to be; don't go there asking for money" Hayo ni maneno yake Comedian na TV host Steve Harvey kwenye Oprah Master Class. Master Class ni show ambayo watu wengi waliofanikiwa katika nyanja mbali mbali za maisha wanaelezea mafanikio yao kwa undani zaidi toka walivyokuwa wadogo mpaka walipo fikia. Changamoto zipi walipata, vipi waliweza kuvumilia, kumudu hizo changamoto, na hata kufanikiwa.Unapopata nafasi ya kukutana na mtu au watu ambao unawaangalia kama "role mode / icon" katika maisha yako usiwaombe pesa waombe wakuelimishe nini walifanya kufikia hapo walipo. Watu wengi wapo wepesi wa kuomba pesa kwa mtu aliyejaliwa kuwa nazo kwa ajili ya kujikimu na hiyo shida aliyonayo. Nautakuta muda mwingi shida hiyo haiishi ni kaituliza tu kwa muda. Hii yote nikwasababu wengi tunapungukiwa hekima ya kujua kuwa ni kheri mtu akupe elimu ya maisha ya nini alikifanya mpaka kufika hapo ili uone kama na wewe unaweza tumia njia hiyo kufikia malengo yako au kujikwamua kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Au utakuta wengine tumepingukiwa hekima ya kuona mafanikio ya watu ni maovu mbele zetu nakuanza kutafuta njia ya kumuangusha bila kujua kuwa anguko lake ni maafa kwako pia. .......Hivyo tuwe waelevu kama nyoka na wenye hekima kama Solomon ili tuweze kujifunza kutoka kwa wengine haswa ambao tunaona wana tija katika maisha yetu.
Pale watu wanapokukatisha tamaa wewe piga moyo konde usiwasikilize. Kwanza mimi kwa experience yangu binasfi watu wengi wenyekukatisha watu tamaa ni watu ambao hawajiamini na pia hawapendi kuonekana kuwa wao wameshindwa katika kufikia kile wakitakacho hivyo hamna la zaidi zaidi ya kupiga makelele ili uwe muoga. Wakati ukweli wanatamani wangekuwa na ujasiri kama wako. Utaona wanakuja na maneno mengi ya kejeli ikishindikana wataingilia personal attack "hajaolewa", "mnene", "hana nywele" , "mbeba mabox" yani ukishaona mtu anaenda kwa personal attacks jua maumivu yamemuhelemea ?? Nasiku hizi social media, basi watatafuta kila event au tukio lenye viongozi waende kupiga picha ili warushe kwa Facebook / Instagram basi tu ufikirie kuwa there really happy and making it, wakati rohoni wanatamani wawe na kipaji au nafasi kama yako. ?? Wanasaikolojia wanasema mara nyingi watu wanao ongelea wengine vibaya muda wote huwa kuna mambo ambayo hayopo sawa kwa upande wao sasa kwasababu hawataki watu wajue hiyo wanageuza attention kwa wengine! Na huo ndio ukweli! Usikate! Nawala usiache mashauzi yao yasio na kichwa wala nguu yakuumize au yakutoe kwenye malengo yako.
Mimi nilivyoanza hii blog yangu nimetungiwa uzushi wa kila namna; ooh huyo muhuni anatafuta mwanaume, huyo FBI, huyo kada wa CCM (utafikiri walishaniona na kadi ya CCM au nimevaa gwanda la CCM ??), mara anatafuta umaaharufu, mara mkabila, mdini, yani maneno mengi mno wengine wakadiri hata kwenda kwetu kuchunguza maisha ya kwetu nakuja kuongea kwenye magroup yao. Mara kazi yake kudhalilisha watu. Eti huyo anagombania mali za wazazi wake ?? Wengine wakazunguka kuwaambia watu wasiweke picha zao kwa hii blog. Yani hayo yote walifikiri nitaacha kublog!! Lakini nipo hapa and I'm here to stay! Mimi najua ninachofanya na ninako kwenda hivyo sijali. Waliokua wanasema mimi kazi yangu ni ku copy and paste ndio hao hao wanakosa raha kwani wanatamani niwaweke humu kwa blog yangu nami hata habari nao sina ?? Ni maumuvi makali sana wanapata. Wewe songa tu, wakikwambia huwezi wambie wewe ni nani hata useme hivyo! Kitu kingine usiamini kila rafiki. Yani ukiona mtu ambaye ni rafiki yako anachukia maendeleo au mafanikio ya mwingine achana na huyo rafiki mara moja. Kwani inamaana wewe ni rafiki yake Kwasababu haujamzidi kimaendeleo lakini siku ukitaka kunyanyuka atakuwa wakwanza kukuangamiza! Niamini nimeyaona!
Siku zote kuna mtu mmoja ambaye atakuelewa na ambaye atakuwa yupo teyari kukusaidia kufikia malengo yako. Mungu huwa hamtupi mja wake! Kama nipesa basi huyo mtu anaweza kusaidia, kama ni mawazo yanini ufanye ili ufanikiwe basi huyo mtu atakuwa yupo tayari kutoa ushauri. It means that person believes in you and truly cares about you! When it looks like nobody cares trust me someone is out there who really cares about you! Muda ukifika Mungu atamleta kwako. Usikate tamaa!
Our family wish you a very blessed Sunday! Word to consider!
Never receive counsel from unproductive people. Never discuss your problems with someone incapable of contributing to the solution. Because those who never succeed themselves are always first to tell you how! Not everyone has a right to speak into your life!
We love you all our good friends?
Wapendwa kama mjuavyo mimi ni TV addict but stupidity never entertained me!! Yani huwa na penda show zenye kunielimisha kimwili na kiroho, pia za kunifurahisha lakini siyo show zenye mambo ambayo hayana mana. Sasa mwezi uliopita kwenye OWN channel Oprah akatangaza hii show mpya inaitwa “BlackLoveDoc” ambapo wapenzi/ wanandoa wenye asili ya watu weusi (blacks couple) wanaelezea their love story, parenthood, na challenge walizopitia na how they overcome them. Inahusisha celebrities na watu wakawaida. Yani I literally said to myself, huyu Oprah is reading my mind or what? Kwasababu hiyo ndio nilianzia hapa kwa blog yangu na kila mwaka on Valentine’s day huwa nataja couple of the year!………. Anyway, show ni nzuri sanaaaa! Nimeipenda mno,
Wenye mapenzi ya kweli utawaona tu toka mwanzo, wewe saa kumi asubuhi mtu anapiga simu Kwasababu kasikia kuna Earthquake? Ndugu zangu mliopigwa na Hurricane Harvey mlipokea hata text za pole ?? wahenga walisema kuwa uyaone ??
Show inapatikana kwa YouTube unaweza angalia katika muda wako.
Mama wawili nimependa sana picha yako na caption yake. But forgive my ignorance; unajua in my mind I never pictured you driving alone! Yani nilikuwa na picha ya wewe kuwa na driver 24/7 ?? kabisa in a counter kwamba you are "Mrs billionaire" why not while you can afford it! Kweli wewe sio mwanamke wa spoti spoti! I give 10 ? across the board!
"Mwana apollo wa kwanza mwanamke kuanza kuzama chini kuchimba tanzanite migodini Mererani! Anaitwa Pili Hussein lakini alibatizwa jina la Mjomba Hussein. Alilazimika awe kama mwanaume kuweza kujichanganya na wanaume aweze kuchimba madini. Wanawake walikuwa hawaruhusiwi kuzama chini migodini...HER HUSTLE IS TOO REAL!! Ukisikia vyuma vimekaza, hii ndio #vyumavimekaza #kilakitubalaa #inspired #watumpakawanazamachini #sisihukujuutunafanyanini? #badounasubirifursa #mjombahussein" ~~~~~Faraja Nyalandu
***Please note hiyo picha ya Faraja na Pili Hussein ni post ya mwaka jana nimerudia tu!***