MUDA huongea sana..... muda huponya.. muda hutibu majeraha... Muda hutenganisha ukweli na Uongo.... Muda Hutoa majibu Muda hukomaza n.k Katika jambo lolote lile lipe muda Hata ukishika mimba si unaipa muda ili ikue na mtoto azaliwe? Hata ukipanda mbegu shambani si unazipa muda zichipue na baadae mazao yakue na kuja kuvunwa. Hakuna jambo linakwenda kwenda tu yoote yanakwenda na muda. Basi hata maswali ujiulizayo ambayo hujapata majibu,yape muda ipo siku utapata majibu. Kuna mambo huko nyuma nilikuwa sina ujuzi nayo....sina taarifa nayo lakini baada ya MUDA nikayajua na kujifunza. Hivi unajua uliwahi kuwa mtoto mchanga?unaelishwa na kunyonya?unavalishwa nepi ya vipande vya khanga lakini MUDA ulipita sasa upo hivyo ulivyo. Katika kila jambo lipe muda.....good morning
All posts by Alpha Igogo
Embu tucheke kidogo na Mc PiliPili
??? huyu Mc Pilipili analeta utani na vyuo vyetu eeh! Eti utapata wapo mchumba wakati unasoma VETA ?? So fuuny!
Je, umewahi sikia history ya madam Rita Paulsen!
Sasa katika kuchungulia kwangu huko Instagram ili nione nini cha kuwaleta hapa, sinikakutana na page ya Madam Rita Paulsen. Nikaamua kuipiga chabo kidogo ?? Mbali na picha zake nzuri nikaona videos clips mbalimbali, nyingine Charles Hillary akicheza. Basi nikaamua kuitazama kwakuwa ilikuwa fupi nikasema ngoja niende kwa YouTube nikaiangalie zaidi. Dah! Si ndio nakutana na hii interview yake alifanya na Mkasi. Hivi kwanza, Mkasi bado ipo au imekufa? Mimi sijui, hata ile Bongo Star Search sijui kama bado ipo. Au ni mimi ndio niko nyuma ya ratiba ?? btw, mimi ni TV addict! Yani kitu Radio hata sijawahi sikiliza unless nipo kwenye gari la mtu au nyumba ya mtu that I'm NOT free enough kusema zima ?? tofauti na mdogo wangu Magreth na dada yangu Elline hawa wawili na Radio huwatenganishi Anyway, back to our story.......Sasa katika kujieleza nikagundua kuwa kumbe naye kama mimi! Alizaa akiwa underage (only 14 yrs old). Dah! Amenigusa sanaaaaaa! Can you imagine having a baby at 14 yrs old?! Jamani, hivi vitu visikie tu kwa mwingine yasikukute! Kama mimi kuzaa at 18 yrs old, nilichekwa na kudhihakiwa hivi yeye aliyezaa at 14 ilikuwaje!! I feel like I wanna hear more about it! Embu msikilize mwenyewe ?
Sasa huyu Madam Rita, mbona sikusikia akipaza sauti yake kuhusu kauli ya kuzuia watoto waliopata mimba kwenda shule? Akaniacha mimi kidogo nimtoe "roho" mama yangu kipenzi mama Salma Kikwete ?? Madam Rita kama utasoma hapa please we need you to be the voice of the voiceless. Denzel Washington anasema, "don't just aspire to make a living, aspire to make a difference". Tafadhali amka madam. Nimependa your new talk show. So nice!
“kumbuka BOX ni rahisi kulipata popote, ila cha thamani ya kukaa ndani ya Box ndio kigumu,”~~~~ Zamaradi Mketema
Katika maisha ya kawaida zawadi huja zikiwa zimefungwa bila kujua kilichomo ndani, na kwakuwa ZIMEFUNGWA unaweza jikuta unalidharau Box la hovyohovyo ambalo huenda ndio lenye kitu cha thamani ndani, ama ukalipapatikia box kubwa lililofungwa vizuri ambalo ukija kulifungua unakutana na mauzauza. Na ndio hata BARAKA ZETU zinavyokuja pia, sio mara zote MUNGU huziweka wazi mwanzo, ila huzifunga kwasababu yake maalum, na mpaka unapokuja kutambua hiyo ni ZAWADI ambayo MUNGU amekutunukia kuna mengi yanaweza kuwa yamepita ambayo yanaweza kukujenga ama hata kukufunza kuithamini. Mara nyingi NJE kuna uongo mwingi, Kwenye kila jambo yatupasa tuangalie vitu kiundani zaidi na sio juujuu, iwe ni kazi, mapenzi, maisha ama chochote kile, Nje kunaweza kukawa kwa kupendeza lakini uhalisia usiwe kama panavyoonekana, kumbuka BOX ni rahisi kulipata popote, ila cha thamani ya kukaa ndani ya Box ndio kigumu, na mara nyingi nje panapendezeshwa na wengi kwa MAKUSUDI sababu ndio panapoonekana hivyo usiamini sana NJE NA PICHA YAKE, huwa zinatengenezwa kukuvutia, Hivyo kwenye kila jambo jifunze kuangalia kwa picha ya mbali, kutokudharau kitu na kuwa na subira, usije ukatupa zawadi ya thamani kwa kuhangaika na mabox ya nje yanayogeuka dissapointment baada ya kufunguliwa.
Womanhood!
Vazi la Michelle Obama laleta tafran’ kwa Facebook!
Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Marekani kabla ya Donald Trump, Malia Obama asubuhi ya leo alipost picha ya mama yake akiwa vacation kwenye visiwa fulani huku akiwa amevalia vazi la ufukweni. Mama Obama alionekana kama alikuwa anapanda kwenye boat ambapo upepo ulipuliza na kuacha sehemu kubwa ya mapaja yake wazi. Kuna watu ambao hawakupendezwa na hiyo picha kuonyeshwa kwenye public, kuna wengine hawakupendezwa kwa jinsi alivyo vaa mbele ya macho ya watu wengi wameona kama hastahili kuvaa hivyo kwani ni mtu ambaye anaheshimika sana na alikuwa First Lady wa Marekani. Mmmh! Embu wee tizama picha halafu useme jinsi uonavyo; mimi sijaona ubaya wa hiyo picha kwani vazi lilikuwa sahihi na alipokuwa. Nilisha sema huko nyuma (SomaHapa) picha kama hiyo kuwekwa kwa public ni maamuzi binafsi na ujasiri wake. …… Maoni ya watu yapo kwa lugha ya English kama uwelewi basi tafuta mtu akutafsirie!
“Lakini nilikuwa nahudhuria sana wakati wa makambi” ~~ Rais Dr. John Pombe Magufuli
Siku ya jana September 2, 2017 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli pamoja na mkewake mama Janeth Magufuli walishiriki ibada pamoja na waumini wengine wa kanisa la Wasabato Magomeni, Dar es salaam, Tanzani. Rais aliongea machache na kutoa mchango wake wa kumalizia ujenzi wa kanisa hilo kama hiyo ☝ video inavyo onyesha pia soma ? Binafsi kama mshiriki wa dhehebu hilo nimefurahi sana. Naomba Mungu siku nyingine akiingia katika kanisa lolote lile la Wasabato asije akaingia kushiriki ibada kama mgeni bali kama mshiriki wa dhehebu hilo. Lakini, mapenzi ya Bwana yatimizwe! Amen!
Je, Zari ataweza kubeba “bendera” za nchi mbili!?!
Katika Biblia kuna maneno yanasema ‘hakuna mtu awezae kutumikia mabwana wawili’! Yani kiufupi lazima mmoja utampendelea na mwingine utamuonea kwa mapenzi ya uwongo! Sasa, wote tumeshuhudia maisha ya Zari na Ivan mpaka kuachana kwao. Lakini pamoja na hayo Ivan bado hakuona mtu mwingine ambaye angefaa kulinda mali zake, watoto wake, na kuhakikisha kuwa his Legacy forever lives zaidi ya Zari. Na Zari mwenyewe kwa mdomo wake alitamka mbele ya kadamnasi siku ya mazishi ya Ivan Ssemwanga (SomaHapa) kua atavaa viatu vya Ivan Ssemwanga, kwani yupo tayari, anaona kama she was prepared enough for it!! Na kwamba she will do it for his boys, his family, friends, and his legacy! Swali ambalo ninajiuliza will Zari be able to be a “flag bearer” for the two men from different countries?! Can she honestly, sincerely, and lovingly serve the “two masters”! ……..Personally, I’m not sure but very curious to see how will this go down considering one of her “men” is still living and 100% involving in her life!………Will Zari disappoint many or will she continue to shine and come-out as a shero? Will this be Zari’s downfall as she may lose some sort of “respect” from Ugandans who are / were hardcore fans of the “Rich Gang” particularly The Don- Ivan Ssemwanga?! Will Watanzania accept Zari and give her 100% support to carry their flag as Diamond’s wife especially after his bizarre behaviors of abusing and disrespecting women!?! Remember “The B**** is dying for fame” and “the baby is not mine”! And finally, the boys are growing up, one day they will have bunch of questions to ask! How will her children feel? Will they feel a sense of betrayal from their own mother; the only living parent?! Can’t get any better than this!! I will surely keep up with the story. And You be the judge!
Zilipendwa by WCB!
Ok, let us talk! Zilipendwa ndio wimbo mpya wa Diamond ambao amewashirikisha wasanii wengine toka Wasafi. Tukubali ukweli kuwa wimbo ni mzuri sana. Na video yake nampa 100% kwani you can see talents and creativity kutoka mwanzo mpaka mwisho wa wimbo. Ni kitu unique! Lakini ukweli kabisa, watu tumechoshwa na tabia za Diamond!! Nafikiri huu ndio muda muafaka wa yeye kufanya mabadiliko lasivyo anguko kuu linakuja!! Watu wamechoshwa na tabia yake ya kudhalilisha watoto wakike! Matusi na skendo zisizo isha!! Diamond badilika kabla hujachelewa, ule mfagio uliotumika kumsafisha Eric Shingongo na magazeti yake ya udaku utatumika kukusafisha wewe hivi karibuni! Believe me if you want! Fanya mziki! Na nani anasingiziwa mtoto karne hii?! Hujui pakufanyia DNA test hapo Dar? Kha! Badilika! ........Otherwise hongera.
“Naamini bado nina nafasi kwenye moyo wako please usiniangushe”!
Umeshawi kumpenda mtu asiyekupenda? Well, naamini wengi tu imeshawatokea. Pengine utakuta kama ni mwanamke basi anakubali hata kuwekwa kimada miaka nenda rudi basi tu mlimradi naye aseme nipo kwenye “relationship” au “married” ?? hiyo yote nikupenda asiye kupenda. Nawengine ndio wanakuwa na ujasiri zaidi kama huyu mrembo Teddy! Jamani hii siyo hadithi ya kutunga, ni kitu cha kweli kabisa. Teddy Lacoste ni binti mzuri sana, na mchakarikaji. Kwakweli ametokea kumpenda kijana Tuma. Kwa bahati mbaya Tuma anampenda Teddy kama rafiki tu / kama dada. Lakini Teddy anaona kuwa yeye na Tuma ni “soul mate” match made from Heaven! Hivyo amekuwa akimbembeleza Tuma wawe pamoja naikiwezekana waoane wawe mke na mume wazae watoto! Ameshakuwa akimbembeleza Tuma kwa zaidi ya miaka 2 sasa kwa kutumia lugha zote za mapenzi, in private lakini ikashindikana. Sasa akaamua kuja public kwa social media. Yani ni anapost picha na status za kumuomba Tuma amkubali #Live lakini Tuma kagoma!! Tuma ni kama mdogo wangu, age mate na wadogo zangu, amekuwa nikimuona pale mtaani kwetu KJ. Hivyo amenizoea ananiita dada. Sasa, mwaka jana mie nikaona Relationship status ya Teddy kwa Facebook kuwa “engaged to Tuma” na picha ya pete. Halafu na Tuma aka “Like” hiyo status. Basi mie nisifurahi nikaja ipost humu (somahapa) si ndio Tuma anakuja niambia kuwa it’s not true haja mu-engaged ni vituko vya Teddy ?? mbona yalinishuka, nami nikagoma kuiondoa kwani yeye Tuma huwa ana “LIKE” hizo status za Teddy! Sasa jana nikamwambia Tuma kuwa leo nakuja kuanika hii story yao kwa blog ili watu wengine watoe ushauri wao. Kwani mie hiyo kesi ilinishinda pale Teddy alipoileta kwangu mwaka jana. Nilimwambia mapenzi ya kutongozewa au kulazimisha mtu hayanaga mema mengi! Nimeona wengi huwa hawana furaha ya kweli. Ni shida. Hivyo yeye mwenyewe ndo itabidi aendelee kum #Seduce Tuma mpaka aukubali wimbo ?? Though moyoni natamani kama wangekuwa pamoja. I love both of them ?? ……. Haya wewe una ushauri gani kwa Teddy na Tuma?
Seduce Me imeleta “kizaazaa” kwenye send-off!
Wimbo wa #SeduceMe umependwa na wengi katika kila kona ya hii dunia. Na sasa mabibi harusi watarajiwa wanautumia katika send-off party zao kama unavyomuona huyo bibi harusi mtarajiwa akiingia ukumbini kwa madaha mengi akionyesha furaha yake huku akim-seduce bwana harusi mtarajiwa kwa kucheza kwa hisia zote! Yani huyu dada kautendea haki huu wimbo, natamani ingekuwa ndio video yenyewe ya huu wimbo. Can you imagine watu wangapi wangevutiwa zaidi? Nakwambia si wazee wala si vijana wote wangekuwa hawachoshwi na huu wimbo. Natamani King Kiba angefanya "Redo" ya wimbo halafu huyu dada ndio awe anacheza hivi, so sexy and classy! She nailed it. Halafu alivyo vaa simple with natural look, just perfect!??........ Mnaona watu wenye ndoa zao halali wanavyoingia ukumbini kwa maringo yote? Sio kama wakina fulani umewekwa kimada unakwenda bandika status kwa Facebook "Married" ?? jamani wewe kama ni kimada kubali tu mbona sisi wengine tupo single na tunasema tu bila wasiwasi ??.......Sorry but no sorry kwani nimemtaja mtu jina?! ???.........Hongera sana bibi harusi. Video hii was fowarded to me sijui source yake.
Hongera Nancy Sumari na Jokate Mwegelo
God is able. God is able to dream bigger dreams for you, than you can ever dream for yourself. Mungu anaweza. Mungu ana uwezo wa kukunyanyua kwa namna haukuwahi kutarajia maishani mwako. #Amini #Trust #Believe #Thankful #Grateful #Blessed #HappyWednesday #HeIsAble #MIYA100Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu katika kila jambo, familia, marafiki na Watanzania wote kwa ujumla. Siku zote hakuna mafanikio yaliyokosa changamoto,na ili ufikie kilele cha mafanikio hunabudi kutumia jitihada, maarifa na nguvu zaidi. Na maombi ya nguvu juu bila kusahau heshima kwa wote wakubwa na wadogo. Napenda kuwashukuru wananchi wote kwa ujumla mnaonipa support na kunipa moyo juu ya niyafanyayo. Nikiwa kama mwanamke kijana nimejitahidi kuiinua #Kidoti katika daraja la juu zaidi, ni nyinyi mnaonipa motisha na chachu ya mafanikio yangu, kwa maombi yenu na sapoti yenu kwa hakika nitazidi kusonga mbele na kuwapa hamasa vijana wengi. Wanasema katika kila jambo mshukuru Mungu. Liwe dogo au kubwa, baya au zuri maana kila kitu kina mchango katika kutengeneza wewe unayesimama leo. Nashukuru Mungu juhudi zangu zinazidi kutambulika nje ya mipaka. Sio jambo jepesi kama mwanamke na kijana kusimama katika kile unachoamini na kujitengenezea njia mahali ambapo hiyo njia haikuwepo. Naomba niseme hii ni kwa ajili ya vijana wote wa Kitanzania wanaokatishwa tamaa katika kufuata kitu tofauti na matarajio ya wengi, katika kufuata ndoto zao. Utabezwa ila usikate tamaa, kaza moyo. Maisha ni safari hakuna kukata tamaa mpaka mwisho wa maisha yako duniani. Kuna siku nitazungumzia safari ya maisha yangu kuna vitu vingi sivisemi ila siku hiyo nitavisema ili tu wewe kama kijana na Mtanzania uweze kuhamasika na safari yako katika kile unachokifanya. #BeYou #BeKidotified #MISA100 ???
What’s your source of joy?
“What’s your source of joy? Mine is love. I’m happiest when I’m surrounded with love.”
Mimi binfsi furaha yangu inatokana na Love from my immediate family marafiki wa karibu. Yani upendo kutoka kwa mwanangu, wazazi, ndugu zangu haswa ndugu zangu wa karibu ni muhimu sana kwangu mimi na inanipa amani na furaha ya pekee. Pia marafiki zangu wakaribu wale wenye mapenzi mema. Huwa I care less hata kama nina rafiki mmoja lakini najua she / he has genuine love for me kwakweli huyo anatosha kunipa furaha. Sipendi watu wanaokupenda huku wakiwa na hiden agenda Or benefits!
Embu tucheke kidogo na Shilole!
Shilole anaomba Kevin Hart amsaidie kuelewa nini anakisema kwani yeye anajua “Yuston” alisha kufa sasa hizo ;ela za nini? Na anataja celebrities mbona na yeye ni celebrity toka East Africa ???, Shilole you killed it ? kidogo kidogo utaelewa tu mama! Lol!……….alichokisema Kevin Hart ni hiki ?
“I love & appreciate you all for your support. @therock @nickiminaj @chrisbrownofficial @troubleman31 “The Kardashian Family” @kandi @wendyshow @djkhaled @cp3 & Chain Smokers and everyone else that has donated. Let’s all keep Houston as well as the surrounding cities that are being affected in our prayers. ??????”
Tafadhali follow Bonuzi kwa Instagram!
Sale ya nguvu @Molocaho furniture by Amorette, kuanzia Sept. 1-8!
Haya sale ya nguvu kwa wale wanaopenda vitu vizuri vya kupendezasha nyumba na vyumba vya kulala! Nikutoka kwa Molocaho furniture by Amorette! Sale inaanza kesho asubuhi September Mosi (Sept.1st) masaa ya Africa Mashariki na kumalizika September 8th. Wahi kesho ujipatie furniture zenye ubora wa kimataifa kwa bei karibu na bure! Halafu siunajua asilimia fulani ya mauzo inakwenda kwenye ule mfuko wa kusaidia jamii wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation! Basi nenda kaunge mkono tusaidie jamii yetu!
Mother and daughter moment
?? ngoja nicheke kwanza, maana Akothee ananifurahisha sana! I think she is a sister I need ??? ……. Yani Akothee anajua how to do a “role” change! Akiwa kanisani siku ya Sabato utamjua ndo yeye anavaaga Vi-min na kukatika kwa stage ?? Yani hadi kilemba ile Luo style anafunga siku ya Sabato na sadaka anakusanya. Na akiwa anakula #bata ni anakula kweli kweli. Sasa kama hapa yupo na mama yake mzazi, muangalie alivyo tega masikio kwa usikivu utafikiri sio yeye. So funny! Wamependeza sana! …….Akothee I know you are my loyal reader, but I want you to be my sister please, I know my sisters love me but they don’t mind to share with you at all ?? We will drive this world crazy, I can tell ??……. Nice pic Akothee, say hello to mama!
The Untold: Siku 30 kwenye koma, jela miezi 27, na madawa ya kulevya!?!
Wahenga wanasema ukiona kwako kwaungua basi jua kwamwenzio kwa teketea! Yani kama wewe unafikiri unamatatizo au umepitia shida na vizingiti katika maisha basi kajaribu kummwambia jirani yako akusimulie yakwake! Utabaki mdomo wazi! …….Embu sikiliza history ya maisha ya Wasia Maya jinsi alivyokuja hapa Marekani, mambo yalimkuta na mitihani aliyopitia utachoka mwenyewe! Kuna wakati alikuwa kwenye koma kwa siku 30, kafungwa jela kwa miezi 27, na tamaa ya kufanikiwa kwa njia za mkato ambazo zilipelekea kutaka kuuza madawa ya kulevya!
Yani the devil! Wewe mwenzio katoka kutumikia miezi 27 jela bado tu unamuweka kwa wishawishi vya madawa ya kulevya?!! Lakini kama roho wa Mungu bado yupo ndani yako kwakweli hawezi kukuacha ukaangamia. Atakugusa kwa mguso wa pekee ambao utatosha kubadili njia zako!
“Sasa nina amani……… Nipo comfortable with my life”! Hongera sana kaka Wasia Maya, najua hii story yako itagusa vijana wengi na kuangalia maisha katika njia tofauti. Ubarikiwe sana.
ADD Friends Campaign – Epsd 019: Adhabu ya Vyoo vya jamii kwa Watu wenye Ulemavu.
ADD Friends Campaign - Epsd 019: Adhabu ya Vyoo vya jamii kwa Watu wenye Ulemavu. Na Peter Sarungi (The Next Speaker) Haja ndogo na kubwa ni moja ya matendo ya mwili ya lazima kwa viumbe vingi akiwemo binadamu. Umuhimu wake unatokana na kazi ya mfumo wa mkojo ambayo ni kutoa taka na sumu za mwili. Kwahivyo mwili huwa hauwezi kusubiri kwa mda mrefu badala yake kuna point inalazimika kutoa uchafu huo bila kujali uko katika mazingira gani. Jamii inayo tuzunguka imekuwa ikitupa adhabu sana katika kupata huduma hii maana vyoo wanavyo jenga ni kwaajili ya kukidhi mahitaji yao ambayo mara nyingi kwa ustaarabu mdogo walio nao wengi wanachafua na kuweka hali hatarishi kwa jamii ya watu wenye ulemavu. Lakini pia vyoo hivyo vinakosa mazingira rafiki ya miundo mbinu kwa mtumiaji mwenye ulemavu kama vile vipimo vya milango, uwepo wa ngazi, maegemeo ndani ya choo, aina ya kifaa cha choo pamoja na uwepo wa maji safi na salama. Jamii ya namna hii inayo tuzunguka haijali usalama wa afya na utu wa mtu mwenye ulemavu na hii ndio imekuwa ni changamoto kubwa kwa mtu mwenye ulemavu pale unapo amua kutoka katika mazingira uliyopo kwenda kwenye mazingira mageni wakati unapo toka ili kushiriki shughuli za uchumi, siasa na za kijamii. Hili ni tatizo kubwa sana kwa mtu mwenye ulemavu, ni lazima awe mchaguzi sana katika kutafuta nyumba ya kupanga, awe makini sana katika kutumia vyombo vyetu vya usafiri wa umma, awe makini katika kuchagua mahala pa kufanya starehe na kadhalika. #ADDfriends_Campaign tumeamua kubadili fikra hii ya mateso kwa mtu mwenye ulemavu. Ungana nasi kupaza sauti ili kujenga jamii ya walemavu iliyo salama. Itaendelea.....
Hongera sana King Alli Kiba!
Hongera sana Alli Kiba tha King! Naona umeleta tafaruku kwa Instagram ?? Nasikia kuwa “mama wa mashauzi yanataka pesa” kakukodishia watu wakafanya mambo ?? ………..Anyway in a serious talk; wimbo nimeupenda sana lakini video hujaitendea haki! Too dark na hakuna the “wow” factor kwenye video. Wimbo ule wa “Aje” video yake ni super sana ukilinganisha na huu!Nimefurahi unaposema kuwa huimbi kwa kushindana na mtu! Safi sana. Mimi siku zote naamini kama Mungu ameshasema hichi ni “Kiti” chako basi hata watu wafanyenye hakuna atakaye kalia hata kama itakuchukua miaka 100 kwako wewe kukikalia lakini No one will be you and take your spot! Hivyo mtu yoyote yule akitaka kushindana na wewe jua kuwa teyari upo juu yake na anaogopa ndio maana anataka akushushe katika level yake. Ukisha jua hilo wala huangaiki kushindana na mtu you just keep moving! Michelle Obama said it well “when they go Low you go High. When they go High you go Low”. Fanya yako, let others be the judge!…….. Hongera sana.