All posts by Alpha Igogo

Happy birthday Dr. Judith Odunga

Happy birthday aunty Dr. Judith Odunga! Nakutakia maisha marefu yalio jaa kheri, neema nyingi, na afya njema! Mungu azidi kukuangazia nuru katika mapito yako yote! Happy birthday shosti wangu, Love you!

Manhood!

The Hayaz! Mashemeji zangu hawa, wanaume wenye vichwa vilivyo tulia wakiongea hata ardhi inatetemeka ?? Hawa watakuwa walinyweshwa Uji wa Kijaluo walipokuwa wadogo, hawakupewa wale funza  (senene) maana akili zao ni Copy& Paste from Luo Land ?? #MuhambaNgomaNgoziHuvutiaKwake

Fahari ya kila mzazi!

These kids!!! Wazurijeee! Nimewapenda bure! Kheri tumbo lililo wazaa, kheri maziwa walio nyonya, Mungu abariki uzao wenu! Watoto ni fahari ya kila mzazi! Mungu awalinde hawa watoto na mashetani ya hii dunia.

Jojo! Katika ubora wake!

Need I say more! My girl Jojo looking A-maz-ing as always! Unajua siku zote hakikisha you look intelligent than “sexy” utaheshimika sana! Looking sexy is okay but its just not right!   My Jojo looks beautiful, elegant, and intelligent ? it!

“jukumu kubwa la nchi za Afrika ni kuhakikisha zinaweka mazingira wezeshi ya kuwaendeleza wanawake katika nyanja zote.”~~~~Mh. Samia Suluhu

Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema jukumu kubwa la nchi za Afrika ni kuhakikisha zinaweka mazingira wezeshi ya kuwaendeleza wanawake katika nyanja zote.  Samia ameyasema hayo leo kwenye Uzinduzi wa Jukwaa la Kuwawezesha na Kuwaendeleza Wanawake Afrika lililoandaliwa na Asasi ya Graca Machel na kufanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam. Makamu wa Rais alisema pamoja na kuwepo kwa jitihada mbalimbali za kuwaendeleza wanawake bado mazingira hayampi nafasi mwanamke haswa yule anayeishi kijijini. Aidha, aliainisha baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na sheria na sera zilizopo ambazo bado zinawanyima wanawake fursa ya kumiliki ardhi pamoja na haki ya kurithi hata kama haki hizo zipo kisheria. “Hii inatokana na utekelezaji mbaya wa sheria, unaosababishwa na uwepo wa mianya ya ubaguzi kwenye kwenye sheria hizo jambo ambalo linakinzana na mfumo rasmi wa kisheria zilizowekwa,” alisema Makamu wa Rais. Aidha alisema “Inasikitisha kuona kuwa ni zaidi ya miaka 20 baada ya Ulingo wa Beijing; kukamilika kwa utekelezaji wa Malengo ya Milenia; pamoja na kuanza kwa utekelezaji wa Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu ambapo kuna lengo la pekee linalosimamia masuala ya usawa na kuwawezesha wanawake na watoto wa kike, bado kuna baadhi wanawake miongoni mwetu ambao wapo kwenye lindi la umasikini, wanafanya kazi kwenye mazingira magumu; kupata kipato tofauti na wanaume kwa kazi sawa; kutokuwa na sauti ya kufanya maamuzi kwenye maisha yao wala maamuzi ya kisiasa; kutokuwa na fursa ya kumiliki na haki ya kurithi ardhi, kukosa huduma za mikopo, afya na elimu; Ingawa wamezingirwa na fursa tofauti na mazingira wezeshi bado wanawake wengi wa Afrika hawachukuliwi kuwa sawa na wenzao wa kiume mbele ya sheria. Alimalizia kwa kusema kuwa muda umefika sasa kwa wanawake kuwa mfano, Kuungana na kuinuana ilikuweza kumkomboa mwanamke wa Kiafrika na kuhakikisha hamna anayebaki nyuma kwenye fursa za maendeleo. . . ( Picha na Ofisi ya #MakamuWaRais )

***Copy & Paste from CloudsTV  Instagram  page***

Womanhood!

Hatuna budi kuwashukuru, kuwatambua na kuwaenzi dada, mama na bibi zetu waliotutengenezea njia kwa mengi tunayofurahia kama wanawake leo hii. Na hasa kujitambua na kutambua uwezo tulio nao. Asante mama Gertrude Mongella! #WAAFORUM2017 ~~~~ Faraja Nyalandu

wakati wao wakiendelea kutoa fact kuna wengine wanapiga hatua za vitendo ~~~~~ Zamaradi Mketema

Wabishi waliishi miaka mingi sana, chunguza hata katika wengi waliofanikiwa sio wenye elimu iliyopitiliza ama waliotoka kwenye familia zenye uwezo PEKEE hapana, ila ni wale waliokomaa na NDOTO ZAO haijalishi background zao ni zipi, leo hii wasomi wangapi wameachwa mbali na watu kutoka streets tu, wakati wao wakiendelea kutoa fact kuna wengine wanapiga hatua za vitendo kupigana na haya maisha na WANAFIKA, lengo ni kukupa moyo wewe uliekata tamaa ya maisha eti kwakuwa hukupata nafasi ya kusoma kutokana na uwezo, ama umetokea mtaani tu kwenye familia ya kawaida/maskini, huna connection nakadhalika, usiitumie hiyo kama excuse, nataka nikwambie INAWEZEKANA hebu taja baadhi ya waliofanikiwa KIUKWELI kutoka MITAANI hata kama hawajulikani ili kuwapa NGUVU wale waliokata tamaa na kuhisi Dunia ni ya watu fulani tu.

 

Job opportunity @ Amorette: Sales Excutive

 If you know how to talk to people, not afraid of strangers, then this exciting opportunity is all yours at the cost of your education level and work experience ? Yes! You must have a college degree education minimum a bachelor in Marketing / Interior design! …….please check the Ad below ? better hurry up because application  deadline is August 25th, 2017 

Peace! Peace! Peace! Is all that we need in Africa!

Whatever the outcome might be the most important thing is PEACE! We need to keep peace in Kenya, East Africa, and Africa in general! .........Goodluck on counting down the votes my neighbors and inlaws! #AmaniKwanza

Baba kasema yamekwisha sasa tujenge taifa!

Baba kafanya maamuzi yake! Rais Dr. Magufuli siku ya jana masaa ya Africa Mashariki kama wengi mlivyo sikia ameingilia kati na kumaliza mgogoro uliokuwepo kati ya marafiki wawili kaka yangu Paul Makonda na shemeji yangu Ruge ? mtaalamu wa kujikomba nimeanza ?? Well, kama hujui basi ndo hivyo Rais Dr. Magufuli ni my Guardian father, Paul Makonda kaka yangu, Ruge shemeji yangu, na Rais Donald Trump ni mjomba wangu, Ivanka Trump ni cousin-sister wangu, na Jared Kushner ni shemeji yangu ??? "Bongo mmeshaharibu na kwa Bush msiguse"  ? I'm feeling Juma Nature right now #Utajiju........  Anyway back kwa story yetu. Sasa naona Rais kaamua kutumia nafasi yake kama baba kumaliza hili zogo. Inaweza isieleweke kwa walio wengi kwanini amemaliza hili zogo kirahisi hivi kutokana na hali halisi ya tukio zima! Naomba watu mkumbuke kuwa hakukuwa na kesi yoyote mahakamani kuhusiana na zogo hili! Hakuna hata mtu mmoja kati ya wakurugenzi wa Clouds, wala wafanyakazi wao aliyefika Police na kufungua malalamiko/ mashtaka rasmi! Hivyo serikali inahaki ya kujiosha kuwa hawana taharifa. Pia shemeji yangu Ruge na kaka yangu Makonda ni mrafiki wa muda mrefu sana, hivyo kwa Makonda zile office za Clouds zilikuwa kama nyumbani! Ni rahisi kusema huu ugomvi Mh. Rais kauchukuli  more of morals than ethical and legal  issue na ndio maana kaumaliza the way he did! 
Lakini kumbuka kuwa hata Ruge huko nyuma kwenye ile "tell it all" interview yake na Clouds 360 alisema kuwa yeye hataki ugomvi na Paul Makonda, yakuwa amemsamehe! Sasa tatizo ni pale kaka yangu Paul Makonda alipo drag huu ugomvi na kumtolea kashfa shemeji yangu Ruge!........Ngoja nikwambie ni rahisi sana kwa mwanaume kumsamehe mwanamke anapo mvunjia heshima kuliko mwanaume mwenzie! Yani ugomvi huu unaweza ukaisha machoni pa watu lakini joto lake litabakia likiunguza chini ya carpet kwa muda mrefu sanaaaaa! Huu ugomvi kiuhalisia bado haujaisha!............ 

https://youtu.be/brO8UeHYW9s
Mimi bado nabakia na msimamo wangu kuwa simuungi kaka yangu RC. Makonda mkono kwa aliyo yatenda. Ningefurahia zaidi kuona anaomba msamaha kwa Ruge publicly hii siyo tu kwa ajili ya Ruge bali kwa manufaaa ya amani na maendeleo ya Taifa letu! Just humble yourself my brother utaheshimika zaidi! Lakini naomba ieleweke yakwamba; sina chuki yoyote ile juu ya RC Makonda wala familia yake!........

Plus, tujifunze kuweka mipaka ya urafiki wetu! Nakumbuka kuna siku baba yetu (Sir O.O Igogo) alikuwa anatuelezea kitu akasema, hivi mmeshawahi kuniona mimi nikiwaleta wafanyabiashara wenzangu kuzungumzia hapa nyumbani? Akafafanua kuwa, mambo yangu ya kazi na biashara zangu yote yanaishia pale mlangoni mwa ofisi za Utegi Tech. Hapa nyumbani kwangu ni mahala pa familia yangu na siyo ofisi!.......Mazoea yakizidi bila kujua kwanini mmezoeana yanaleta shida! Tuweke mipaka ya urafiki wetu kulingana na mahali husika. Marafiki wa kanisani basi wabaki kuwa marafiki wa kanisani na hivyo hivyo kwa wengine............ Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania.

New Song: Umoja ni nguvu by Leyla Bezuidenhout

 Princess Lelya katuletea wimbo wa kutuunganisha Watanzania wote. Msikilize  ☝ akijielezea katika radio 106 huko Atlanta, Georgia. Wimbo mzuri sana unakwenda kwa jina la “Umoja Ni Nguvu”!……… Nimeupenda sana kwani ameona mbali na kutokukubali kuingiza vyama vya siasa katika wimbo huu kwani isingekuwa na mvuto na nguvu ya wimbo ingepotea! …….Watu wa diaspora ni vizuri kuachana na mambo ya siasa ya “uchama”! Maendeleo hayana chama, kabila, wala dini! Hivyo nivizuri watu wakaungana kwa “U-Tanzania” wetu na kupigania haki na maendeleo ya Watanzania na sio chama fulani! ………Anyway, binafsi nimeupenda, chukua muda wako kuusikiliza na tafakari! …….. Hongera sana Lelya, well done!

Life has more to offer than just slaying ~~~~~ Akothee Akothee

Mwanamuziki toka Kenya Akothee Akothee, anasema hivi mjengee msingi mzuri wa maisha mtoto / watoto wako ili wawe na manufaa baadaye katika maisha yao! Maisha yanatoa maana nyingi zaidi ya kujipondoa tu! Mfundishe mwanao kupika, kufanya usafi, kuheshimu watu, jinsi ya kutumia na kutafuta pesa n.k Kuna wazazi wengine wamegeuza watoto kama toys! Yani ni kujiremba na fashion za nguo bila kujua watoto wanatakiwa kupewa muongozo wa maisha na maadili ya kuishi hapa duniani na kubwa zaidi kumjua, kumuheshimu, na kumtunikia Mwenyezi Mungu! ......... embu msome Build a foundation for your girlchild , so they become usefull in the near future , life has more to offer than just slaying , a woman has to know how to cook, we're learning how to cook ugali & chapati today , @ruebaby @ #teambigfive @fancy_makadia @veshashaillan we set 

Kama ulipitwa: Mali’s 50th birthday bash!

Wapendwa kama ulipitwa na hii event basi ngoja leo ni TBS right! Angalia hii video ime summarize the whole birthday bash kwa muda mfupi lakini inapendeza sana. ❤ It!

Btw, narudia kumpongeza sana Linda Bezuidenhout  (LB) kwa kufungua duka la kisasa kabisa kwenye mazingira mazuri ya kuvutia ndani ya Phipps Plaza hapo Georgia! Hongera sanaaaaaa ??

Mama Igogo katika ubora wake!

Mama Igogo akifanya yake katika ubora wake, na Tshirt yake ya “I ❤ Halotel”!  This lady can’t sit down ?? Yani ukimuona mama yangu amekaa chini yani kule ku-relax nyumbani absolutely doing nothing but enjoying yourself; basi jua ni mgonjwa siku hiyo ? Kupika aliacha long time ago, rarely utamkuta akipika ila mambo yake ni kama haya analima bustani zake za mboga, viazi vitamu, mahindi, n.k….. Kama hayupo kwenye bustani ya vyakula basi kwenye banda lake wa kuku wa kienyeji, ni shidaaaa! Btw, hapo ni nje tu ya nyumba yake hivyo haitaji dereva kumpeleka shamba ?? Mama yangu was raised with two great human being I have never met before! Babu yangu na bibi yangu mzaa mama walikuwa watu wakarimu mno! Wenye upendo wa hali ya juu, waungwa sana, na wanyenyekevu kupita kipimo! Hivyo simshangai sana mama yangu kuwa hivi alivyo! Namuombea maisha marefu yenye afya njema sana na amani tele ndani ya moyo wake! Huyu ni my niece Sarah! Ni mtoto wa dada yangu Grace-AnyangoNyoyoo, lakini analelewa na bibi yake (my parents). Naona yupo likizo sasa anadeka na kwa bibi na babu ? Missing you mwanangu mie, love you always! Janeth, katoka kwake Mbezi kuja kuchuma mboga kwa mama,  kaiba na ujuzi akaenda kulima kwake ?……… siye wengine kulima hatukusaidii lakini kwenye kuvuna tutavuna na kuvifaidi wote ?? …….. I ❤ my family!

Mother and son moment!

Wamependeza eeh! Glory na handsome boy wake! Nimependa sana nywele za Glory, zimempendeza mno! Nywele fupi zinawatu wake lazima kichwa kiwe kina "pembe" zilizo lingana  lasivyo utachekesha wafiwa ? .......Safi sana .....I ❤ it
Today's Quote : "Men are what their mothers made them."~~~~~~ Ralph Waldo Emerson
Eti jinsi mama umleavyo mtoto wako wa kiume ndivyo atakavyo kuwa atakapo kuwa baba / mume /mtu mzima! .......Kwa mfano, kama hauto mfundisha thamani ya mwanamke na jinsi ya kuwaheshimu wanawake basi hawezi elewa na akiwa mume / baba hatojua jinsi ya kuishi kwa kumuheshimu mumewe au watoto wake wakike kwani haukumfunza hivyo! Bible inasema mlee mtoto katika njia mpasayo naye hataiacha hata akiwa mzee! Anaweza akajikwaa na kutoka nje ya mafunzo au malezi uliompa lakini hato potea milele kwani lazima nafsi yake itamsuta kuwa haya niyatendayo siyo malezi niliyopewa na mama yangu. Hivyo atarudi katika njia sahii!...............Mbarikiwe sana wamama wote wenye mapenzi mema kwa watoto wenu.

My favorite people in one picture!

My new found mama. She’s such a poser???, so ICONIC. Africa’s Princess @yvonne_chakachaka ?#howmanytimesdoyougettopowderalegend #imeeeeean #rightbeforeshehitsthestage ☺️

Wow! There are some of my very few favorite people, all in one picture!!! I’m smiling like #Zezeta………. Yani utafikiri mie ndio Jojo katika picha, Jojo please kiss her some more just for me ?? ……. Powerful women in Africa right there representing two different generations! Look at that natural beauty #BlackDon’tCrack   ???❤❤

Ndugu wanapokutana…….!

Pale ndugu wanapokutana ni furaha kwa kwenda mbele! ........mama akipata kumbukumbu ya picha na binti yake kwa furaha ya kuonana tena baada ya miezi kadhaa kupitia! Magreth akimpokea dada yake Elline kwa furaha sana!..........  kwafaida ya wasomaji wangu, Elline ni dada yetu mkubwa, mimi ndio namfuata. Yeye alikuwa anaishi Geita lakini mwezi uliopita wamehamishiwa kikazi Makao Makuu (Dodoma). Hivyo sasa ni wakazi wa Dodoma! ........Tunamshukuru Mungu kwa yote! 

Kila mtu ni muhimu!~~~~~ Zamaradi Mketeme

Kuna watu hujishusha thamani wanapoangalia wengine wanaoonekana wamewazidi nafasi bila kujua wao huenda ni MUHIMU kuliko hata wanaowaangalia sababu ndio wanaowasababishia UKAMILIFU, 

Natamani ujue kitu kimoja hapo ulipo iwe wewe ni Mpishi, housegirl, shamba boy, messenger ama mwajiriwa tu wa ofisi fulani, thamini na RINGIA unachokifanya na usiruhusu mtu akudharau, hiko unachokifanya Boss wako hata awe na mamilioni bado hawezi kufanya na hiyo ni NGUVU. Ukichukua muda kuchunguza utagundua hakuna alie muhimu zaidi ya mwingine na KILA MTU NI MUHIMU, vipi leo mahousegirl wakigoma wote hata thamani ya hela yako utaiona!? 

Wamama wangapi nyumba zitawashinda, Jiulize Unaweza kufanya wanachokifanya wao fully!? Maana unaitwa Boss sababu kuna watu WALIOKUBALI kukutumikia, Ama hata Kama una ofisi wafanyakazi wakaondoka wote unaweza kufanya kwa ufanisi hiko wanachokifanya wao!?? Kitendo chochote cha kuweza kufanya asichoweza mwingine ni UPEKEE, na upekee ni NGUVU haijalishi unachokifanya ni kitu gani, hivyo usijidharau wala kuona kuna wanaostahili na wasiostahili.. hata kama we ni mpika maandazi mazuri mtaani RINGA, usijidharau halafu ukamuheshimu mama anaepaki gari kila siku kununua maandazi yako kwa kuhisi yeye ndio bora hapana, yeye hawezi kupika kama wewe ndiomana anapaki kwako, na huo uliopewa ni upekee mkubwa ambao wewe ndio wa kuamua uutumie vipi ili uwe na faida sababu hakuna mwingine anaepika kama wewe, 

MUNGU AMEKUPA NGUVU YAKO KUBWA kwa kukutunukia uwezo wa tofauti, hakuna alie BORA zaidi ya mwengine ila tuna MAJAALIWA TOFAUTI, asiekuwa na hiki unakuta ana kingine and viceversa, hivyo heshimu ulichonacho na UJITHAMINI, na zaidi tafuta njia ya kukifanya kwa UKUBWA hata kama ni kitu kidogo kiasi gani maana ndicho ulichopewa na MUNGU!! penye upekee wako ndipo UTAJIRI ULIPO. Haina maana kwakuwa UNATUMWA ukahisi wewe sio muhimu ama anaekutuma ndio mtu hapana, haijalishi unachokifanya ni nini since unaemfanyia hawezi kukifanya mwenyewe basi jua wewe ni wa muhimu pia.

Happy birthday Lawyer!

Kheri ya siku ya kuzaliwa Mwanasheria wa kimataifa! Baraka, ulinzi, na amani ya Bwana Yesu vikaandamane nawe katika mwaka huu na siku zote, milele Amina! We love you!

Matatizo yanaweza kuisha na kuwa furaha ~~~ Jackline Mengi

Kwanini usononeke na kukata tamaa kwasababu ya matatizo uliyonayo leo wakati unafahamu kuwa maisha yanaweza kubadilika, matatizo yanaweza kuisha na kuwa na furaha inawezekana? Unaamini haya kwasababu tumeshaona mifano mingi ya waliopitia kwenye shida na taabu nyingi lakini ikafika wakati wakawa na furaha na ndoto zao zikatimia. Hata kwako wewe inawezekana. Mkumbushe unaempenda na unaedhani anahitaji kusikia maneno haya leo.