All posts by Alpha Igogo

Happy Mother’s Day to all mothers around the world!

Mdogo wangu Magreth, mimi mwenyewe, na mama, March 2017, Segerea, Tz….nyumbani kwa mdogo wangu mzee William Igogo

Nawatakieni kheri ya siku ya wakina mama wa mama wote katika dunia hii! Mungu awabariki sana na azidi kutupa khekima ya kuwalea watoto wetu katika njia mpasayo! Wale ambao wanategemea kuwa mama, basi Mungu akawatangulie mjifungue salama. Nao wanao tamani kuitwa mama basi Mungu akawajaze mibaraka hiyo kulingana na mapenzi yake!………..Tunapokuwa tukifurahia Siku hii kuu duniani tusisahau kuwaombea wamama wote ambao watoto wao wamelala usingizi wa mauti! Mungu awaponye na awape sababu ya kuwapa nguvu ya kuendelea na maisha. Na wale wamama ambao watoto zao ni wagonjwa Mungu awaponye upesi. Nawale  ambao kwanamna moja ama nyingine watoto wao wapo kwenye matatizo yoyote yale basi Mungu akafungue njia, awapiganie na shetani asipate nafasi kamwe!

Mimi mwenyewe na mama yangu, December 2016, Dar, Tz…..makazi yetu ya zamani

Nawasii wamama wenzangu tuwalee watoto katika upendo wa dhati na hofu ya Mungu! Watoto ambao hawajalele katika upendo wanakuwa tatizo kubwa si tu kwenye familia zao bali hata kwa jamii husika. Kumfundisha  mtoto kuwa strong katika maisha haimaanishi kuwa unfundishe mtoto wako roho mbaya, ukatili, kuwa bully, muongo, mnafiki, mchonganishi n.k! Hapana! Kama ni mtoto wakike mleee kama ndio the next queen! Nakama ni mtoto wa kiume mfunze kuwa a gentleman! There are too many evil men in this world let us save the world by raising our children in a Godly loving manner! ……..Happy Mother’s Day to all mothers! ❤❤

Mother and daughter moment

What a beautiful picture of Hoyce Temu and her beautiful lovely daughter Rubby! Priceless! Happy Mother’s to Hoyce Temu

Mother and daughter moment

Nimependa sana hii picha ya Nambua Cassandra na mama yake mzazi mama Mlaki. Hii ilikuwa wiki iliyopita kwenye babyshower ya Nambua. Mmh! So touchy, lovely, and priceless moment. Happy Mother’s Day to both of them!

Happy Mother’s Day!

Samahani wapendwa as much as I wish ningewekeza post picha za watu mbalimbali na mama zao, lakini inakuwa ngumu kwani nina commitments zingine! Naomba nichague chache ambazo zitawakilisha wa mama zetu wote. ……Hivyo nawatakieni kheri ya siku ya wakina mama wa mama wote bila kusahau mama Kimati na Mama Double G (George na Georgina) wenye picha hii! ??

“A man with dreams needs a woman with vision” Meck Mbwana

 “A man with dreams needs a woman with vision”  Wow! Need I say more?!! What a powerful simple sentence! Hakuna kitu kizuri kama mwanaume anaye thamini mchango na umuhimu wa mwanamke katika maisha yake. Kama kweli huyo mwanamke amemsaidia maana kuna wanawake wengi ni majanga tu ?? Well, can we talk?! I always keep it real ??

Womanhood!

“It ain’t about me, it’s about God, my family and ?…….#CircleTooSmall”~~~~~ Zari the bosslady

Don’t miss! Its free!

Haya kwa sichana wote ambao wapo chuoni na unaojiona kuwa umebarikiwa kuwa na mawazo chanya ya jinsi ya kusaidia wasichana wengine ila haujajua ni jinsi gani uweze kuweka haya mawazo yako katika vitendo basi event si ya kukosa. Haina kiingilio ni bure kabisa tarehe 16 May, 2017 hapo COSTECH Kijitonyama kuanzia saa kumi jioni mpaka kumi na mbili.

 

My weight loss journey…..!

Kama nilivyo waambia wiki iliyopita kuwa nitakuwa napima uzito wangu naku-share nanyi kila week. Basi leo nimepima na matokea ni kwamba bado sijaanza kupungua uzito. Labda kuanzia next week ndio nitaanza kuona matokeo. Bado nipo na weight ya LB225 ambazo ni karibia na Kg 92 hivi! Well the journey continues this is going to be my life style now. Guys, huwezi amini najisikia mwepesi, nguvu nyingi mno na very focus. Plus najisikia raha sana kwenda gym kila siku na mwanangu such a bonding moment as mwanangu kazi yake ipo very demanding hivyo muda huu wa gym ndio tuna spend sana pamoja. Sasa hivi katika list ya nyimbo zangu za mazoezi nimemuongeza #Darassa  Pale mwanzon pale kabla mazoezi hayajakolea namsikiliza yeye then zoezi likikolea na baki na Harmonize #IYOLA……..ok tukutane tena wiki ijayo. LOVE and PEACE!

Kusoma post ya nyuma bonyeza ?  MyWeightLossJourney

 

 

 

Cheka urefushe maisha!!

This is so true! Kuna maisha zaidi ya kuolewa enjoy life ladies! Kama wewe ni mama furahia uzazi wako fanya kumbukumbu nzuri na wanao hata siku ukiondoka hapa duniani wawe na kitu cha kuelezea jamii. Kama huna mtoto basi fuga hata mbwa / paka uwalee. Au tafuta kitu ambacho kina leta furaha na amani moyoni mwako ukifanye kwa nguvu zote. Tusiwe kama wakati wa Noah ambapo watu walikuwa busy na kula, kulewa, kuolewa na kuoa hata pale walipokuwa wakihubiriwa injili ya wakovu hawakusikia kabisa! Btw, hata Boaz alimkuta Ruth akiwa busy shambani akampenda na kumfanya malkia wake wa nguvu ??  Get a life!

“Eliminate the clutter from your life ladies…!”

Haya ujumbe kwa single ladies ambao wanatamani kuwa na “King” katika hemaya zao ?? Mnaambiwa hivi msipende kuongozana sana na wanaume au kuwa kwenye makundi ya wanaume pale mnapokuwa mnakwenda outing kwani wakaka ambao hawajaowa watashindwa kuelewa kama upo mwenyewe /single au umeshachukuliwa! Hata kama ni kaka zako usiwe unatokanao mara kwa mara as wanaume watakuogopa ? (nimekoleza tu). …………Mpendwa usijizibie bahati yako kwa kuongozana na marafiki wakiume kila wakati 😉 😉 

“Treat all women with respect and you will live a happy and peaceful life” Meck Mbwana

Nimependa sana huu ujumbe ulioandikwa na Meck Mbwana founder and owner of PUKU portable power bank. Ni ujumbe mzuri sana kwa generation ya sasa ambapo wanaume wengi bado wanashindwa kujua kiini cha furaha katika jamii na familia zetu inategemea kwa asilimia zote jinsi mwanamke anavyo jisikia. Happy mama happy home, happy community! Linda na heshimu mwanamke kwani wote mmekuja hapa duniani kwa kupitia viungo vya mwili wa mwanamke!! 

Dr. Ntuyabaliwe Foundation yakabidhi Library!

Naamini wengi mtakuwa mmesikia kuhusu hii giving back to community foundation ambayo inakwenda kwa jina la “Dr Ntuyabaliwe”. Kama hujawahi kusikia habari hiyo basi huu ni mfuko ulio anzishwa na Jacqueline Mengi kumuhenzi baba yake mzazi ambaye alikuwa medical Dr I believe alikuwa Gynecologist  (please kama nimekosea unaruhusiwa kunisahihisha) lakini naamini alikuwa Gynecologist. Anyway, Jacqueline amekuwa anasaidia mambo mbali mbali kwenye jamii kwa kutumia mfuko huu.  Amekuwa akitoa vifaa vya hospitali (incubator)  vya kutunzia watoto ambao wanazaliwa premature / njiti, madawati ya shule na vifaa mbalimbali vinavyotumika mashuleni. Wiki iliyopita alikabidhi Maktaba / Library kwa shule ya awali ya Makumbusho iliyopo jijini Dar es salaam. Na hii ilikuwa mara ya pili kwa Jacqueline kujenga library kwa shule kwa kutumia mfuko huu wenye jina la baba yake. Kama picha inavyo jieleza hapo ilikuwa wanakabidhi library ya kwanza. Hongera sanaaaaaa Jacqueline, such an inspirational. Kama unafatilia hii blog basi utakumbuka huko nyuma niliwahi kusema kuwa sasahivi Jacqueline yupo kwenye “public eyes”  hivyo jamii itapata nafasi ya kumjua Jacqueline ni nani haswa ( her character) and I have to  admit the more I look at her the more I love her! Just lovely and beautiful. Haya na Molocaho hiyo inakwenda Dubai kwa maonyesho. Mungu akisema Yes hakuna wa kukuzuia! You go girl! Hongera Sanaaaaaa ??

Dondoo za kuuweka mwili wako fit

Haya sasa nitakuwa nawaletea dondoo za kujiweka sawa kimwili kutoka kwa watu tofauti tofauti ambao nitaaona kuwa wanastahili 😉 ……….. Haya leo nawaletea huyu dada, kwakweli simfahamu but I normally check her Instagram kwani huwa ananifurahisha jinsi anavyo jiweka Ain’t she cute! Yani mie nataka nipungue but sitaki hatasikumoja kuwa kama “mode” yani mwili fulani kama wa huyu dada na sio chini ya hapo. Halafu simnajua Muhaya anapenda nyama ya mifupa au mifupa ya nyama ?????? inshort kila mtu ni mzuri kwa style yake but wembamba siyo wa kila mtu kama ulivyo unene. Kuna watu wanajikondesha wanapungua hata ukimuaangalia mvuto hakuna kabisa! Na kuna wanene ambao wanapendeza sana na unene wao jinsi walivyo. Just figure out who you are ndio utaweza kujua unataka unene au wembamba. But in all usiwe OVERWEIGHT or UNDERWEIGHT!

Je unamuhitaji huyo mtu maishani mwako? Je upo tayari kumvumilia tabia yake?

Swali la msingi hapo ni Je unamuhitaji mtu huyo maishani mwako? Je upo teyari kumvumilia tabia yake?!!….. Well, Maya Angelous said it very well “When people show you who they are believe them”!! This quote has been my guardian angel in picking and choosing who to be my friend and around me! Yes! Agree hakuna mtu aliye kamilika hapa duniani but there’s a distinctive line between mistake and evil!! Mtu yoyote anaweza fanya mistake lakini kuna mtu anafanya kitu au akanasema mpaka mtu unajiuliza hivi huyu ni binadamu wa kawaida? Kuna watu wana roho za kishetani kaa nao mbali na wala wasikudanganye na makeup wanazo paka, nguo wanazo vaa, elimu zao, wala uzuri wa sura zao! When someone does AN EVIL ACT to you that person is nothing but A DEVIL stay farrrrrr from him / her!

“You can never be faster than destiny.”

You can never be faster than destiny:Until its GOD’S time, it can never be your turn. When GOD is ready, everything and everybody will be forced to be ready. They will have no option than to work in your favor. Your helpers will have no rest until they locate you. Protocols will be broken for you to be promoted, elevated and celebrated. You will be unstoppable. (Collected)
#Akininspirational

“Nilianza kuuza hereni, bangili, na mikufu” Amyna Sanga

Kama wewe ni mwanafunzi au unatamani kuanza shule na kuna kitu kinakukwamisha basi embu soma kisa cha huyu dada hapa ?labda kitakupa moyo uwe na nguvu ya kusonga mbele……  

“Together we will get through this, God bless you we love you “~~~~ Idris Sultan

Wapendwa, huu msiba umeumiza watu wengi sana! Binafsi nikiona hii picha ya hawa watoto nashikwa na butwaa, huzuni inanijaa! Kuna post ya kuchekesha nilitaka kuweka kile kitendo cha kufungua blog na picha ya kwanza nakutana nayo ndiyo hiyo ya watoto hao washule yani nikajikuta nakuwa mdogo kama sisiminzi!! Nikaona ngoja niipotezee kwa leo. Seriously, the nation is still grieving, I don’t know how people will transit from this tragedy to their normal lives?!! O’Lord of mercy see Tanzanians through this!!…………  Basi nikaingia Instagram ndo nakutana na huu ujumbe wa Idris Sultan kwa Watanzania wote. Very touching, embu usome na wewe…..! 

Lucky Vicent Primary School: R.I.P innocent souls one day we shall meet again!

Imenichukua muda kupost hili tukio la kuhuzunisha na kusikitisha sana kwasababu this is not kind of posts ningependa kuzipost humu! Kifo cha mtu yoyote is horrifying let alone vifo vya watoto zaidi ya 30?!!  Its just too much pain for me!! ………As a mother, I am speechless over the death of these beautiful innocent souls! Like why? And how?!! As Mtanzania I am angry! very disappointed! And confused!! Like until When??!! Hizi ajali za Tanzania when will they end them?? Until when people???!! As I said before at this very moment am speechless can’t put it into right words right now!! Maybe some day I will but for now the only thing I can say; Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe milele zote! Mungu wa rehema awape faraja na amani wazazi,  wafiwa wote na Watanzania kwa ujumla! Poleni sana! May their souls R.I.P

The couple we like!

Mwajuma na la-azizi wake wakifanya yao! Wamependeza sana!??

“God did not create us to be the same our”

“God did not create us to be the same our story our category will never be the same there will always be that someone who is more richer more popular more beautiful or more successful … Run your own race at your own pace we all might be travelling same direction but our purpose and destinations would never be the same …….Never ever make a mistake of comparing yourself with one another in life those who evaluate their success based on others people achievements may never see any reason to be happy and grateful ever in life..your present situation is someone else heart desire…..Always remember delay is never denial If God answers your prayers His increasing your faith if your prayers are delayed He’s increasing your patience and if you’re not answered there something better for you and if He keeps you alive He has a better plan for you
#SpokenWithaReason
#positivity” ~~~~~Akinspirational, Akin Al-Ameen