All posts by Alpha Igogo

Don’t miss, the Mother and Child Gala April 22, 2017!

o.k.

Malkia wa nguvu 2017: Hongera sana Mwanaidi Mayowela, pongezi kwa Clouds TV!

Nilikuwa sijapata muda wa kuwapongeza washindi na waandaaji wa sherehe za “Malkia wa nguvu” hivyo naomba nichukue muda huu kuwapongeza!…………Kwakweli kama kuna kitu ambacho kimenivutia sana na kunigusa kwenye TV za Bongoland; basi ni hii sherehe ya Malkia wa nguvu. Sababu kuu yakunivutia nikuona kuwa waandaaji walichukua muda wao kufanya kazi ya kujua nani anastahili kupewa tuzo hiyo ambapo imekuwa tofauti sana na events /awards nyingi sana za “Wabongo” wengi kwani mara nyingi ni zakujuana juana. Yani authentication ya awards inakuwa haipo kabisa!!

https://youtu.be/LVNGUI6vtAQ

Hongera sanaaaaaa Clouds TV mmenifanya niangalie hii event mara zote mlikuwa mkiirusha hewani! Natumaini na wengine wataiga mfano wenu. Pia hongera sana dada Mwanaidi Mayowela kwa kulitwaa taji kwani unastahili kwakweli! Ubarikiwe sanaaaaaa wewe na familia yako! Nawashindi wengine wote pia nanyi nawapongeza sana. Mungu azidi wabariki.

Malkia wa nguvu; Mchapa Kazi, Mbunifu,  Jasiri!

UN Youth Envoy

“Its time for young women to showcase by example our ability to lead and potential to deliver for all youth &that we’re not too young to lead From Tanzania I and my sister @victoria.mwanziva have declared interest to run for #UNYouthEnvoy post. Please support us. If you are a youth-led or youth organisation, you can nominate us through link in our Bio. Our win Is your win”~~~Rebecca Gyumi Wishing you all the best, najua lazima mmoja wenu atatutoa kimaso maso!

In loving memory of Ontlametse Phalatse

Ontlametse ni mtoto alikuwa ana ni-inspire sana! Nilikuwa namfatilia sana kwa Instagram, nilivutiwa sana na inspirational speech zake na jinsi wazazi wake walivyo mlea na kumjengea confidence kubwa sana ya kujikubali jinsi alivyo, kujiamini kuwa anaweza na anastahili kuishi kama wengine, na kujipenda! Nimeguswa sana na kifo chake, may her soul rest in peace! ……Ee Mungu naomba uniongezee ujasiri niweze ku-overcome all my fear and conquer them with greatness just like Ontlametse, Amen! 

Cheka urefushe maisha

Cheka urefushe maisha!

“Only a black person would go to a butchery and buy bones and only to complain that ‘these bones got no meat’.

My brother you said you want bones,stop being emotional,you need deliverance and 365 bottles of anointing oil.” -Tusiime

“Tusimame pamoja kama Watanzania kupambana na uovu kwenye jamii” -ShyRose Bhanji

CHADEMA HAINA HATI MILIKI YA KUWA UPINZANI PEKEE NCHINI. -Peter Sarungi

 Nilipokuwa natafakari maamuzi ya kwenda kugombea Spika wa bunge niligundua kuwa kama wewe ni mchezaji mzuri wa mpira wa miguu na unajiamini basi si lazima usajiliwe na timu kubwa kama Simba, Yanga ana Azam ili ucheze ligi kuu, kumbe unaweza kucheza ligi kuu hata kupitia Mbao Fc, Ndanda Fc, majimaji au hata Costal Union. Kinachotakiwa ni siku timu yako ikikutana na Simba ama Yanga hakikisha unafunga walau goli moja tu hata kama wao wataifunga timu yako kwa magoli 10. Hilo goli lako wataondoka nalo likiwa na jina lako. Hii ni bora zaidi kuliko kusajiliwa Simba ama Yanga halafu ukakaa benchi kwa sababu wachezaji ni wengi. Nchi yetu ni nchi ya demokrasia na nchi yenye kufunya siasa ya vyama vingi. Kuwepo kwa wingi wa vyama vya siasa ni moja ya tendo la demokrasia tunayo ikubali kila siku. Tanzania kuna vyama vya siasa zaidi ya 25 vyenye usajili wa kudumu vinavyo ruhusiwa kushiriki katika siasa zote za nchi. Ni kwa bahati mbaya Chama tawala hakijawahi kupoteza kushika dola huku vyama vya upinzani viki badilika badilika katika kuwa na wafuasi na nguvu za kisiasa hadi kupewa kijiti cha kuitwa chama kikuu cha upinzani. TLP, NCCR Mageuzi na CUF zimewahi kuwa na nguvu katika chaguzi zilizopita na kuwa chama kikuu cha upinzani wakati huo vyama kama Chadema Tanzania vilikuwa vipo chini sana na vilikuwa havijulikani kwa Watanzania walio wengi. 

Leo Bunge la Tanzania lina vyama 5 vyenye uwakilishi Bungeni huku CHADEMA kupitia muunganiko wa UKAWA wakiwa ni chama kikuu cha upinzani. Ukawa inabebwa na wabunge kutoka CUF, CDM na NCCR huku ACT ikiwa iko peke yake lakini katima kapu la upinzani ikiwa na haki zote kikatiba na hata kwa sheria za uchaguzi na za bunge.

Kumetokea taharuki kidogo juu ya nafasi za wabunge wa Afrika Mashariki hasa kwa upande wa vyama vya upinzani. Mnyukano ulikuwa ni kati ya UKAWA na ACT wazalendo juu ya nafasi 3 za upinzani. Mnyukano huo umeendelea hadi yalipo patikana maamuzi kutoka kwa Speaker juu ya mgawanyo.

Kilicho nisikitisha katika mnyukano huo wa hoja ni baadhi ya makada wa CDM kwa makusudi ama kwa kutojua kuhamisha mjadala wa kibunge na kuuweka kwa wananchi huku wakitoa lawama, matusi, kejeli na hata dharau kwa hoja iliyo tolewa na ACT kupitia mwakilishi wake Mh. Zitto Zuber Kabwe iliyotaka ACT wapate nafasi ya kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. 

ZZK ametukanwa sana na baadhi ya makada wa mtandaoni wa CDM huku wakiamini wao ndio wapinzani pekee walio teuliwa na Mungu kuja kuwasemea watanzania. Mimi niwakumbushe tu makada wa CDM kwamba hata wao walikuwa kama mchicha kipindi CUF wakiwa Upinzani imara, Pia wakumbuke hata wao hawana HATI MILIKI ya kuwa UPINZANI pekee nchini. Wasikasirike, kubeza na kupinga wanapoona mbegu zingine za upinzani zinapo chepua kwa kasi, ipo siku mtahitaji ushirika wao ili kufikia malengo yenu.

By the way, inasemekana hata mgogoro wa CUF unawafurahisha sana CDM kuliko CCM, Maana wapo tayari na wamefungua milango kwaajili ya kuwasajili akina Seifu, Mtatiro na wengine pindi chama hicho kikifutwa kama alivyo sema Lissu kwenye mahojiano ya Azam… Daah kufa kufaana.

Msijisahau mkalewa kwa sifa na ubinafsi, ni kweli umoja ni nguvu lakini ni umoja wenye maslahi sawiha ulio Imara na wenye Nguvu.

Wasalam.

SIMBA ANAPO LAZIMISHWA KULA MIWA. -Peter Sarungi

Utani wa jadi huwa una raha na karaha zake. Ushindi wa timu yangu Yanga jana haukunishawishi kuandika chochoye juu yao maana naijua timu yangu hasa katika dakika za lala salama kama hizi. Lakini kufungwa kwa watani zangu Simba kumenishawishi kuandika post hii japo kuwasabahi kwa ushindani wao. Moja ya uchawi katika soka ni historia. Hata makampuni ya bahati nasibu (kubeti) huwa wanatumia historia katika kuweka rate, mara nyingi wanaweka rate ndogo kwa timu iliyopata ushindi kwa wingi huku wakiweka rate kubwa kwa timu iliyopata kushindwa mara nyingi pale timu hizo zinapo kutana. Lakini pia wanaangalia historia ya michezo hiyi ugenini na nyumbani.

Historia inaonesha timu ya simba imekuwa ikipata taabu sana wanapo kutana na Kagera Fc hasa wanapo safiri hadi bukoba. Simba imekuwa ikipata matokeo ya ovyo sana kama ya leo ya kufungwa bila huruma. Hawa wakulima wa miwa wamekuwa wakiwalisha Simba miwa bila kupenda huku mabingwa watetezi tukianza kuwasha taa za hatari kwa watani zetu juu ya Ubingwa wa mwaka huu 2017. 

Peter Sarungi (The next time)

Matokeo ya watani zangu yawe dedication kwa marafiki zangu wa zaidi ya miaka 20 iliyopita ambao ni watani zangu akiwemo Godlove Mpandiko, Nelly Peter Namasambillo na Swaleh Madjapa.

Lakini pia matokeo haya yakwende kwa ndugu zangu wa damu waliokuwa kwenye kikao wakiongozwa na mwenyekiti Mzee Busara, Sabasaba Sarungi, Daniel Sarungi, Nyakwar Omwami Bonnie Sarungi, Mourice Leonard Sarungi, Hamisi Sarungi na wengine wanao shabikia Simba.

Niwakumbushe kuwa kilele kinamilikiwa na Yanga. Asanteni sana.

Matukio katika picha!

Hizi picha naweka tu ili ufurahishe macho kwani najua saa zingine unahitaji break ya kusoma articles  😉 😉 …….. Ni picha zilipigwa kwenye mji wa Beijing, China, kwenye picha nipamoja na Sir O.O. Igogo na binti yake Advocate Janeth Igogo (Mrs Nyagilo), na Mwanasheria Tarimo. Hii ni moja ya board meetings ambazo wanazifanya kila mwaka na wamekuwa wakikutana hivyo kwa muda wa miaka 10 sasa. Na mara nyingi huwa wana alternate kati ya Tanzania na China. Mwaka jana ilifanyika Tanzania soma ? HolleyPharm …… Haya enjoy the pictures 

SIASA ZENYE MLENGO WA UCHUMI. -Peter Sarungi

SIASA ZENYE MLENGO WA UCHUMI.

Peter Sarungi (The next time)

Kuna Siasa za kuegemea uchumi (Political Economy), Siasa za kisayansi (Political Science) na Siasa za Kisanii (Political Art).

Hizi aina zote zina faida na hasara zake na kila moja ina nafasi yake katika kustawisha jamii.

Nimegundua kuwa serikali ya JPM inafanya siasa zenye kuegemea uchumi. Nasema hayo kutokana na budget ya sasa inayoonesha vipaumbele vya utawala huu ni vile vinavyo chochea uchumi ikiwa ni sector ya usafirishaji na miundo mbinu. Tunaona budget ikitupilia mbali miradi mipya ya afya, elimu, michezo, kilimo, viwanda, maji, umeme, utalii, uvuvi, ajira na kukuza sector binafsi. Budget imeweka mkazo kwenye Ujenzi, Ujenzi,Ujenzi pamoja na ununuzi wa ndege.

Kwa budget hii, fedha nyingi bado zitakwenda kwa wageni ambao watahusika na ukandarasi wa ujenzi wa Reli inayokusudiwa, ujenzi wa fly overs zinazokusudiwa na kampuni ya kutengeneza ndege. Kwa maana hiyo bado pesa haitakuwepo kwenye mzunguko wa ndani wa fedha, matokeo yake ni UKATA, UKATA. 

Aina hii ya siasa ina faida ya kukuza uchumi wa nchi na serikali yake baada ya mda wa miaka 3 na kuendelea. Serikali inakuwa na uchumi mzuri kuliko sector binafsi, Serikali inakuwa imejiingiza katika kushikilia vyanzo vya kuendesha uchumi. Ubaya wa aina hii ya siasa ni wananchi kudhoofika kiuchumi kiasi kwamba wanakuwa tegemezi kwa kila kitu kwa serikali yao. Tatizo lingine ni kwa serikali kuwa na tabia ya  kujiondoa katika kusimamia na kuendeleza miradi yenye kutoa huduma za jamii kwa wananchi wake, hili ni Tatizo kubwa sana mbeleni.

Hongera sana Dr. Mwele Malecela! -Alpha Igogo

Kulia nataka na kucheka nashindwa kwani it’s a “Bittersweet moment” kwa Watanzania wazalendo! Kuondolewa kwako kulituumiza sana kwani wengi tunajua dhamani yako na umuhimu wako kwa taifa la Tanzania! Soma hapa ? Dr.Mwele Lakini kama wasemavyo Mungu si Athumani, na kamwe Mungu hamtupi mja wake; basi hatuna budi kusema hongera sana Dr. Mwele kwa kazi yako mpya kwenye shirika la afya duniani -WHO (Africa)! 

Mungu akuongoze na akubariki katika kila jambo jema ulitendalo. I’m very happy for you! Just go and shine-out as you always do! Congratulations! 

PIGO KWA JAMII YA WALEMAVU! R.I.P Mh. Dr Macha

Jamii ya watu wenye ulemavu imesikitika sana kupokea taarifa za msiba wa mama yetu na mtetezi wetu aliyekuwa anatuwakilisha bungeni kama mbunge viti maalum wanawake kwa upande wa walemavu Mh. Dr. Elly Macha kupitia Chadema Tanzania. Dr. Macha amefariki dunia akiwa nchini Uingereza kwenye Matibabu.

Binafsi mara ya mwisho kuonana na huyu mtetezi ni mwaka 2015 nilipokuwa naomba fursa ya kuwa spika, maneno yake yalinipa nguvu na sababu za kuendelea kutetea jamii ya walemavu katika nchi na hata kimataifa. Aliamini mabadiliko ya kuikomboa jamii ya walemavu yatapatikana kupitia walemavu wenyewe na ikiwa watashiriki katika vyombo vya maamuzi kama bunge, mahakama na hata ndani ya serikali. Bado naamini katika maneno yake na yataendelea kuishi na ipo siku yatatimizwa na walemavu wenyewe. 

Peter Sarungi (The next time)

Natoa pole kwa familia yake,jamii ya watu wenye ulemavu, ndugu, jamaa, marafiki, viongozi na wapenzi wote wa CHADEMA kwa kumpoteza mama yetu tuliye mpenda lakini Mungu amempenda zaidi yetu. Tuwe wavumilivu na wenye matumaini katika kipindi hiki kigumu huku tukiamini ipo siku tuta onana naye.

Amen  Nami naomba nitoe salamu zangu za pole nyingi sana kwa wana familia, ndugu, jamaa, marafiki, pamoja na jukwaa zima la walemavu Tanzania na duniani kote! Taifa limepoteza msomi mmoja ambaye pengo lake halito zibika!

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe!……. R.I.P Mh. Dr. Macha

HATA KWETU TUNAO MALKIA WA NGUVU.  HONGERA SANA MADAM SOPHEY MBEYELA. -Peter Sarungi

 

 Nikiwa kama mwanaharakati wa kutetea haki na kukuza utu wa watu wenye ulemavu, jukumu langu kubwa ni kukusogeza karibu na jamii hii ili sote tujue mazingira ya watu wenye ulemavu kwa kukuonesha changamoto na mafanikio yetu katika kuchangia maendeleo ya jamii. Tunaamini ushirikiano wako kwetu utaongezwa ikiwa utajua mazingira yetu.

Leo natumia jumapili hii kupongeza mafanikio aliyoyapata dada yangu Sophey Mbeyela baada ya kutwaa Tunzo ya Malkia wa Nguvu kwa mwaka 2017 kutoka Clouds Media kupitia kampeni yao ya kuwatafuta Malkia wa Nguvu kila mwaka. Anapenda aitwe Madam Sophey, ni moja kati ya akina dada shupavu, asiye kata tamaa na mwenye kufuata ndoto yake kutoka katika kundi la watu wenye ulemavu. Kazi yake kubwa ni mwalimu lakini pia ni mwamasijashi (Motivator) mzuri sana anaye warudisha vijana walio kata tamaa katika msitari, pia amekuwa akiamini katika kutoa na hivyo ameendelea kutoa misaada mbalimbali kwa jamii yenye mahitaji maalum kama vile watoto na watu wenye ulemavu hasa wanafunzi. Record yake ni nzuri sana kwa jamii yetu ya walemavu na amekuwa akichukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha jamii inapata ustawi.

Nichukue fursa hii kumpongeza sana kwa mafanikio anayo endelea kuyapata na nimtie moyo kwa kusema HAKIKA  HIYO NDIO DUNIA YAKE ALIYOPEWA NA MUNGU, ASITAFUTE DUNIA NYINGINE..

Tafadhali kama unapendezwa na mafanikio haya kutoka katika jamii ya watu weye ulemavu basi andika chochote cha kumpa nguvu Madam azidi kutoa mchango kwa jamii.

Happy birthday my darling daughter

Wishing you a very happiest day on this special day! My wishes to you are the same as always and my love has never changed! Surely, never will it change! …….Happy birthday my Queen, my joy, my life!

Walk for autism!

Kesho ni siku ya Autism duniani. Ni siku ua kuelimisha jamii zinazo tuzunguka juu ya ugonjwa huu, na changamoto ambazo wazazi pamoja na watoto wanazipata!……..Mwaka jana nilitoa ahadi ya kushiriki matembezi haya (Autism ) lakini kwa bahati mbaya kutoka na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wangu sitaweza. Mungu wangu anajua kuwa ninajali na ninaomba afungue njia kwa madaktari waweze kujua chanzo cha ugonjwa huu na tiba yake! ………..Tafadhali, kama unaguswa basi shiriki matembezi haya kesho nawe utabarikiwa sana!

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU-2 -Peter Sarungi

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU 2

Peter Sarungi (The next time)

Sehemu ya II – Ijue Sector ya Madini Tz

Sector ya madili ilianza kutambulika rasmi wakati wa utawala wa awamu ya tatu chini ya Raisi mstaafu Mh. Ben Mkapa kupitia sera ya uwekezaji. Mh. Mkapa aliamini maendeleo ya nchi yatasaidiwa ikiwa tuta ruhusu uwekezaji mbalimbali ikiwemo sector ya madili. Aliamini nchi itafaidika kwa kupata teknolojia mpya, mitaji mikubwa, elimu mpya katika sector hiyo pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi na mapato ya serikali. Wawekezaji wakubwa walianza kujitokeza mwaka 2001 Geita na Kahama. Madini yanayopatikana nchi ni mengi kwa aina tofauti kama vile dhahabu, almasi, ruby, Tanzanite, Copper, Silver na mengine mengi ingawa zaidi ya 80% ya machimbo nchini yanajihusisha na uchimbaji wa madini ya Dhahabu. 

UZALISHAJI WA DHAHABU

Mpaka sasa tuna machimbo makubwa ya dhahabu yapatayo sita ambayo ni Bulyanhulu(BGM), Geita(GGM), Buzwagi(BZGM), Biharamulo, North Mara na New Luika. Kwa mwaka migodi hii huzalisha 1.37Million troy ounce ambayo ni zaidi ya kilogram 50,600 ya dhahabu safi kwa mwaka huku GGM ikiongoza kwa uzalishaji wa 38.6% na ya mwisho ikizalisha 1.5%. Kwa viwango hivi, Dhahabu inachangia zaidi ya 90% ya uzalishaji wa madini yote inchini kwa mwaka.

               NJIA ZA UZALISHAJI

Uzalishaji wa dhahabu upo wa aina mbili maarufu ingawa kuna nyingine ya tatu, aina hizi zinatokana na utofauti wa miamba ambayo dhahabu hupatikana. Kuna miamba ambayo ina oxide na zingine zina sulphide.

Dhahabu inayopatikana katika Miamba yenye oxide ina zalishwa kupitia njia za gravity na Cabon process (cabon in loucher CIL na cabon in pulmp CIP). Njia hizi ni common na zipo nyingi katika migodi yetu hadi kwa wachimbaji wa kati. Migodi yenye miamba ya oxide inayotumia njia hii ni nne kati ya zile sita yaani GGM, North Mara, Biharamulo na New Luika. Hivyo uzalishaji katika migodi hii hufanyika na kumalizika ndani ya nchi. Migodi hii haisafirishi mchanga kwenda nje.

Dhahabu inayopatikana katika miamba yenye sulphide ina zalishwa kupitia njia ya gravity, caborn process na kuhitimishwa na smelter. Njia za gravity na Carbon process huzaliza 40% pekee huku smelter ikizalisha 60% ya dhahabu. Dhahabu inayopatikana katika miamba yenye sulphide ina ugumu wa kunyonywa kupitia njia zilizopo nchini kutokana na dhahabu hiyo kuungana na madini mengine ya copper na silver, hivyo ili kuitoa dhahabu hiyo ni lazima uwe na tanuru kubwa (smelter) lenye uwezo wa kuyetenganisha madini hayo kutokana na utofauti wa melting point za madini hayo. Hivyo ni lazima mchanga unaozalishwa baada ya mchujo kwa njia za kwanza usafirishwe kwenda nje kwaajili ya kuzalisha 60% iliyobaki. Migodi yenye miamba yenye sulphide inayotumia njia hizi zipo 2 kati ya sita nazo ni BGM na BZGM. Migodi hii ndioyo husafirisha mchanga kwenda china na japan ?? kwaajili ya uchenjuaji.

Mpaka hapo kama kuna swali unaweza kuuliza kabla sijakwenda mbele zaidi. Uliza ndani ya maelezo hayo, usitoke nje maana bado kuna makala nyingi zinakuja

Asanteni.

“A vindictive askofu……….askofu Gwijima……” Chege Kilahala

Continue reading “A vindictive askofu……….askofu Gwijima……” Chege Kilahala

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU -Peter Sarungi

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU

Peter Sarungi (The next time)

Sehemu ya I – Utangulizi

Mkuu wa Kaya ali ahidi kusimamia sector ya madini kwa umakini ili sector hiyo iweze kuleta tija na faida kwa Taifa. Hivyo serikali ya Mkuu wa kaya imezuia usafirijashi wa mchanga wa dhahabu kwa makampuni ya uchimbaji yaliyopo nchini kwa muda usio julikana.

Lengo la zuio hilo lililotokana na kauli za mkuu wa kaya ni kuhakikisha serikali ina ondoa mianya ya kuibiwa madini hayo ambayo yana chujwa nje ya nchi huku sisi tukipewa mrejesho ambao kwa hisia za mkuu wa kaya anao mrejesho bado una ukakasi. Lakini pia mkuu wa kaya alitamani kabla ya kuwa Mkuu na anaendelea kutamani kujengwa kwa hilo Tanuru kubwa la kuchuja dhahabu, shaba na copper hapa Tanzania ili kufikia ndoto za kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Pamoja na dhamira njema ya mkuu wa kaya, ni vizuri na sisi watanzania tukajua kinachoendelea katika sector hii ili tupate kujua faida na hasara za zuio hili ikiwa ni pamoja na changamoto za kufikia shauku la mkuu wa kaya la kuwa na Tanuru hilo lijulikanalo kama Copper Concetrate Smelter  Hivyo nita toa makala ya kueleza hali halisi za sector hii ikiwa ni sehemu ya kwanza na makala nyingine ya kueleza faida, hasara na changamoto ya kufikia ndoto ya mkuu wa kaya ya kuwa na Tanuru la kuchuja madini hayo Tanzania.

Nitatumia vikao mbalimbali nilivyoweza kuudhuria vya wataalum wa madini, ripoti mbalimbali kutoka TMAA na machapisho mbalimbali ya kimataifa kama vyanzo vya habari katika kusapoti andiko langu.

Asanteni

“Republicans and their “pipe dream” of appealing and replacing Obamacare.” – Chege Kilahala

Republicans and their “pipe dream” of appealing and replacing Obamacare…….

If you can’t marshal enough votes in a house (the congress) where you have a comfortable majority. Then your chance of passing it the senate where you have a very thin majority is non-existent…..

Now, we can toast and celebrate that, Obamacare is the law of the land….and it will carry on being so…….I look forward to seeing a universal healthcare system in the USA; one day soon. Just like whats found in Canada and Scandinavian countries….