Huu ni msemo wa wahenga ambao uhalisia wake unaonekana mara chache porini lakini hutokea sana kwa maisha ya binadamu. Naamini kuna watu walisha wahi kumwinda mjusi kipindi walipokuwa watoto na katika kumwinda mjusi gafla walipo toa jiwe wakakutana na nyoka, inapofika hapo lazima hali ya hatari itatokea.
Naiona nchi yangu kwa mbali inakaribisha hali ya hatari. Mkuu wa kaya alianza kuongoza nchi yake kwa misingi ya sheria huku akijitambulisha kuwa yeyeni mkali kwa maneno na matendo yake. Baada ya kuwa mkali sana watoto wakaanza kulalamika huku wakionesha kuto ridhika na maamuzi ya baba. Watoto wakaanza kumwinda baba kwa vifungu vya sheria huku wakimtangaza baba kuwa ni dikteta. Na kwa jinsi baba alivyo na msimamo, hakuwahi kurekebisha makosa yake hasa yale yaliyovunja sheria na hata kuonesha upendeleo wa wazi wazi huku akiwagawa watoto wake kwa kauli na matendo.
Kwa sasa hali imekuwa mbaya maana watoto wameanza kumkana baba yao kwa kutumia mama yao Katiba. Wana mshawishi mama yao (Katiba) awaoneshe baba mwingine kwa kutamka kuwa huyu sio baba mzazi na wamtafute baba mwingine.
Kwa hatua ya mawindo yalipo fikia, nawaona watoto wanahisi wanaye mwinda ana fanana na Mjusi hivyo wanaongeza jitiada za makusudi wakiamini nguvu za mjisi zipo mkiani na wala sio nguvu za kuogopesha kiasi cha kutaka kumtoa kwenye pango lake.
Lakini nahofia sana hasira za baba, baba akikasirika na kuamua kutumia nguvu zake basi anaweza akawalazimisha watoto kuendelea kuitwa baba kwa kumtishia mama na hata kuwa adhibu vikali watoto wanao kwenda naye kinyume, na akiona bado anapingwa basi anaweza kumbadili mama mwingine na kufunga ndoa ya kudumu. Kwa hatua hii, baba hatakuwa tena mjusi bali atakuwa ni nyoka.
Kwa sasa watoto wajiandae kukutana na nyoka katika mawindo yao, wasidhani wataendelea kukutana na mjusi walie mzoea kumwinda. Wajiandae na plan B,C na hata C ya kukutana na Nyoka.
By the way baba amesha geuza kichwa bado mkia wa nyoka tu aanze mashambulizi kwa watoto wanao winda.
If I apply for a job that requires a qualification A and I get offered the job on the basis of my qualification A, then if my employer finds out that, I didn’t possess that qualification, he/she will have the “legal basis” to terminate my employment on that fact……….But if I apply for a job that does not specify that it requires any qualification, but I falsely put down that I possess qualification A, my employer WOULD NOT HAVE any legal basis to terminate my employment on that fact. It is because, his decision to employ me was not influenced by the fact that I have or have not had that particular qualification.
For that reason, why do people ask for the resignation of Paul Makonda from the RC position? Did Magufuri’s decision to appoint him as the RC base on the qualification he claimed to have?!!! Do you need to even have a standard 7 qualification to be appointed as an RC??!! Leave the guy alone………….!!!
Peter Sarungi (The next time) Injili ya yesu ilipata kumnukuu Nabii Issa (Yesu Kristu) alipokuwa njiani kusulubiwa baada ya kukutana na wamama wakimlilia kwa uchungu, sehemu ya nukuu inasema ” ikiwa wanafanya haya kwa mti mbichi, je itakuwaje kwa mti mkavu????
Kwa kawaida mti mbichi una sifa za kuvumilia shida, ni mgumu kuvunjika lakini vilevile ni mti unao onesha uhai, wenye kuwa na afya ya kustawi na ni mti unao weza kuzaa matunda tofauti na sifa za mti mkavu ambao kwa ujumla unatambulika kama mti ulio kufa.
Namfananisha Mh. Nape Nnauye na mti mbichi ndani ya CCM. Kila mtu anajua mti huu mbichi ulivyo kuwa na uhai, wenye afya na aliyeweza kuitetea chama hadi kupata matunda ya kushika hatamu. Nape amesema alilala porini siku 28 kwaajili ya kuhakikisha chama inapata ushindi, amekipigania chama hadi kufikia kutoa utu wake kwa kukubali lawa, dhiaka na chuki kutokana vita ya kutetea chama kipindi kigumu cha uchaguzi 2015. Inawezekana ile kauli ya Bao la Mkono aliyosema Nape ndio aliyokuwa akitumikia porini kwa siku 28.
Lakini leo, Mti huu hauna tena dhamani mbele ya bashite, mti unatendewa yale wanao tendewa wapinzani wa leo.
Ikiwa haya yametendwa kwa mti mbichi kama Nape, Je ni nani aliye salama hasa kutoka mti mkavu kama mimi?????
Pole Nape, najua sasa zile akili za kushikiwa na chama utakuwa ume waachia wengine ambao bado wana imani ya kuchukua nafasi yako.
By the way wewe unaye jiita mwana CCM na mkereketwa wa zidumu fikra za mwenyekiti, anza kujiandaa kisaikolojia ili usije pata strock kwa maamuzi kama haya. Chama kwa sasa kina mwenyewe….
Baba naomba nianze kwa salamu; shikamoo baba!…….Baba naomba nikwambie dhumuni la barua hii si kukuomba hela za matumizi kwani hilo si tatizo langu kwa sasa! Pesa zipo tena wewe wenyewe ndio umeziweka hivyo nipo vizuri baba!
Baba ninachotaka kukwambia leo hii nakuomba utege masikio yako kwa makini sana baba yangu kwani mwanao nimejawa na hofu nyini sana! Wewe ni baba yangu ninaye kupenda sana na siku zote nilitembea bara-barani na kulala usingizi mnono sana nikijua tupo katika mikono salama! Lakini, sasa hivi uwoga umenishika sana, siyo tu kwa watu ambao siwajui bali hata kwa hawa wakuu wa mikoa yetu ulio wachagua. Na mbaya zaidi imani yangu juu yako imeshuka kwa kiasi kikubwa sana kitu ambacho si kizuri kabisa kwani wewe ni baba yangu!
Baba, naomba unisaidie kuelewa, kwani unampango wa kung’ang’ania madarakani? Au unataka nchi yetu iwe kama Rwanda ile ya mauwaji? Au kama Uganda ya Mseven? Au unatamani Tanzania iwe kama Congo ya Kabila, na Burundi ya Nkurunzinza?! Au iwe nchi ya ukabila kama ile nchi ya Jomo Kenyatta?!! Mimi sijui baba lakini natamani kujua, tafadhali nijuze ili nijuwe kama nianze kuomba ukimbizi nchi za jirani?! Nakama ni hivyo je, zitakua ni nchi zipi katika bara hili la Africa?!!
Baba, niwapi mimi binti yako nikimbilie maana dalili zinaonyesha kama hali itaendelea kuwa hivi na wewe ukaendelea kubariki kwa mikono yako miwili basi mimi mwanao sina budi kuanza kukimbia kuomba hifadhi nchi za jirani hata ng’ambo ya Magharibi kama itaibidi! Japo natafakari sana je nitakimbia mwenyewe au nimchukuwe na mama? Vipi kuhusu bibi na babu? Bila kumsahau mjukuu wako kipenzi! ooh! vipi na yule dada yako wa pekee aliye olewa kijiji cha Koromije mkoani Mwanza? tena yeye ni mlemavu wa miguu! Na binamu yako Zainabu ambaye ni mlemavu wa ngozi huwa awezi tembea juani! Hawa wote nawapenda sana na itakuwa ngumu sana kwangu mimi kuishi mbali nao, nifanyeje baba? Hivi mida ipi itakuwa mizuri kwetu sisi kuanza mwendo; mchana au usiku? Baba, nguvu zinaniishia! Baba kwani niwapi tulikosea? Mbona mambo yanakuwa tofauti na ahadi zako? Mimi niliwashawishi ndugu zetu wote, majirani, marafiki, na Watanzania wote kwa ujumla kuwa wakupigie kura ya “ndio” kwani nina imani nawe, na kwa uchapa kazi wako ulionyesha kuwa wewe unafaa sana! Nao kwa furaha na nderemo wakakupitisha kwa kishindo kuwa Rais wa nchi yao. Nami mwanao nikatembea kifua mbele tena kwa mikogo na madaha mengi sana kuwa sasa Tanzania mpya inakuja! Tanzania ya amani tele, iliyo jaa demokrasia nyingi na uhuru wa kujieleza bila vitisho! Tanzania ya viwanda na miundo mbinu ya kisasa!
Baba, sasa mbona mambo yanakwenda sivyo?! Uliahidi kuleta uongozi bora ulio tukuka, uongozi wa haki na wakufuata sheria. Uliahidi kutulinda sisi wanawake na watoto, ukatuhakikishia kuidumisha amani ndani ya nchi yetu tuipendayo sana! Imekuaje sasa? mbona wavunja sheria ndio unawatukuza na kuwatunuku shahada za uongozi bora?! Baba ni wapi tumekukwaza? Mbona viongozi wanao tishia usalama wa maisha yetu kwa kuvamia sehemu zetu za kazi kwa mitutu ya bunduki ndio unao wapenda sana? Usalama wetu upo wapi? Mbona ndugu zangu hata hawaruhusiwi kuongea kwa uhuru bila kutolewa silaha za moto?!
Baba, nampenda sana kaka yangu ambaye ulimchagua kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. Nimchapa kazi sana hilo halina upinzani lakini baba yeye si mkamilifu, ana mapungufu yake kama mwanadamu yoyote yule; hivyo kubali kuwa sanyingine naye hukosea. Basi anastahili kuadhibiwa kama unavyo tuadhibu sisi wanao wengine kwa makosa tunayo yafanya au pale tunapo kukwaza!
Baba, sababu ya mimi na Watanzania wengine kuomba umuadhibu huyu kaka yetu, si mbaya hata kidogo! Hatuna nia ya kumkomoa au kumuumiza bali nikutaka kuweka mfano mzuri kwa wadogo zetu ambao wanakutizama iliwajifunze kitu fulani kuhusu utawala bora wa sheria na haki. Maamuzi yako yatatuaminisha kuwa unamaanisha kile usemacho. Kufanya hivyo kutaondoa hofu tulionayo Watanzania. Au unaogoapa hutopata mchapa kazi kama yeye? mbona kule kanda ya ziwa wapo wachapakazi wengi sana, tena watiifu, na waaminifu, hawana uonevu wala kiburi?!
Baba, naomba nimalizie kwa kusema samahani sana kama tumekukosea. Lakini ukumbuke tu kuwa wewe ni baba wa wengi na si wa mtu mmoja tu, hivyo tunaomba utupende, na utulinde wote bila ubaguzi wa aina yoyote! Usitugawe baba sisi sote ni wana wako. Sisi ni ndugu moja japo wengine ni wembamba na wengine wanene. Japo wengine wafupi na wengine warefu, wengine weusi wa rangi ya ngozi na wengi ni maji ya kunde; sisi ni ndugu moja. Usitubague wala kututenga!
Nimesikitishwa sana na taarifa kutoka ikulu, ingawa niliona ishara hiyo kutokana na mwenendo uliopo. Pamoja na hayo Nampongeza sana Mh. Nape Nnauye kwa karata ya ushindi aliyo cheza jana kwa maamuzi ya kutetea ukweli. Kwa karati hii, watanzania wamefuta Hasira, dhiaka na chuki walizokuwa nazo toka kipindi ulipo kuwa Msemaji wa propaganda za chama. Leo Umekuwa shujaa wa uhuru wa habari na naamini hivi vyombo vya habari vitakutunuku kwa maneno na matendo kwa kutetea ukweli. Nakutakia safari njema ya siasa, ukiweza basi anzisheni chama chenu wanasiasa wote mnao tengwa na chama kwa kuwa tofauti na mkuu maana sioni chama mbadala kitakocho wapa uhuru wa kufanya siasa zenu.
TLS ; CHADEMA’s legal department or another opposition party?!!! There are legal boundaries within which these institutions can carry out their daily duties……using TLS as a mouthpiece to pursue some political agenda is a no-no-no-no!!!
How did I missed it!! But you know I love you JoJo! Wishing you countless blessings from Sir God, the one created the earth and heavens! Happy belated Jokate!
Mmeona shemeji yangu Ruge jinsi alivyo ongea kisomi?! ‘Kijana’ kaongea kwa ma-confidence kama Rais bwana (in Haya’s accent)! Yani huyu Muhaya ni kichwa usipime! Na sasa nimeamua kum- upgrade siyo Loser tena ni Hero wa Watanzania. Na kwakuwa ni mambo ya kupokezana kijiti basi kijiti chake kipo pending kwasasa mpaka report ile ya tume ya Nape Mnauye itakapo kamilika halafu tutamkabidhi mtu fulani 🙁 …… Huko nyuma nilisemaga hivi TheTwoBiggestLosers 🙂 🙂 kwakweli nimecheka sana! What was I thinking?! Kha! Ogopa mwanamke akiwa amekasirika 🙂 🙂
Halafu mimi sipendi tabia ya watu wanao bugudhi Wahaya!! Mnajua mie nina ubiya wa kudumu na Wahaya 🙂 🙂 leave my Hayas’ alone peeople!! …… Haya Ruge nitafute uchukue hela yako ya lunch umefanya kazi nzito sana 😉 😉
Ingawa ni vigumu kupata tamaduni za kuwajibika kwa viongozi wengi wa Afrika lakini bado kuna kila ulazima wa kuwakumbusha viongozi wetu na hata kuwafunza vijana ambao ni kizazi kinachochukua dhamana kutoka kwa wazee wetu juu ya umuhimu na faida za kuwajibika mwenyewe bila kushurutishwa.
Watanzania tunafunzwa na viongozi wetu kuwa na tabia za ajabu sana unapopata madaraka, tabia kama za ubabe, majivuno, dharau, ung’ang’anizi, ufisadi, uzembe na zingine nyingi ambazo tumekuwa tukizishuhudia kutoka kwa viongozi wetu. Tamko alilotoa Waziri wa Sheria la kupiga STOP ufungaji wa ndoa bila cheti cha kuzaliwa kuanzia mwezi wa tano na baada ya muda mfupi Mkuu wa kaya akatoa katazo la utekelezaji wa agilo la waziri wake.
Kwa tafakuri ndogo, inaonesha kwamba agizo hilo la waziri halikupata utafiti wa kutosha na pia halukupita kwenye vyombo vya ushauri kama Baraza la mawaziri. Pia inaonekana agizo hilo limemkera sana Mkuu wa kaya kiasi kwamba akalitolea tamko yeye mwenyewe bila kutumia wasaidizi wake kama vile waziri aliye husika kutoa agizo hilo.
Kwa maamuzi aliyoyafanya Mkuu wa nchi kwa Waziri husika lina fundisho kubwa sana na angalizo kwa waziri husika. Ningekuwa mimi ni waziri husika ninge jiwajibisha kwa kushindwa kufikia viwango vya mkuu wangu wa kazi, maana inawezekana akanitumbua ama akanisahau kwenye marekebisho ya baraza la mawaziri.
Nafikiri ni muda mzuri kwa Waziri Mwakiyembe kuji pumzisha ikiwa ni hatua ya kujiwajibisha ili aendelee kubaki na heshima yake iliyo tukuka kwa nchi. Kuna faida kubwa ya kujiwajibisha mwenyewe kuliko kusubiri kuwajibishwa tena kwa aibu, nasema hayo kwa sababu na mimi mpaka leo naendelea kunufaika na hii tabia ya kujiwajibisha ambayo nimewahi kuifanya sehemu mbalimbali za uongozi wangu.
By the way kuna kazi sana kutoa tonge kutoka kwenye midomo ya waafrika, wapo tayari kunyang’anywa kwa nguvu kuliko kulitema wenyewe hata kama tonge ni chungu.
Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Hon. Shy-Rose Bhanji ametoa salamu zake za kuguswa na kifo cha aliyekuwa mtumishi wa umma wa muda mrefu Sir George Kahama kwa kusema haya “Sir George Kahama ni moja ya Tunu za Taifa kwa mchango wake ktk Serikali za Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi na Mkapa…Asante kwa utumishi wako uliotukuka wa kulitumikia Taifa la Tanzania. Mungu akulaze pema Baba Pole nyingi kwa Familia yote Mungu awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu #SirGeorgeKahama #RIP” ……. Muheshimiwa Shy-Rose aliyasema hayo mapema leo kupitia kurasa zake za jamii (Facebook, Instagram). Nami naomba kuungana naye kwa niaba ya familia ya mzee O.O Igogo kuwatakia pole wana familia yote, ndugu, marafiki, na jamaa. Poleni sana kwa msiba huu Mungu aendelee kuwa nanyi wakati wote……….Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote!
Siasa safi zinahitaji kuwa na demokrasia ndani yake, kuwe na uhuru wa kutoa mawazo mbadala, kuwe na desturi ya kuvumiliana hasa pale mnapopingana mawazo na kuwe na tabia ya kutafuta na kusema ukweli hata kama ukweli huo utakuwa mchungu.
Mtindo wa vijana wengi wa sasa ni wa ajabu sana katika siasa. Mtindo ulio gubikwa na tabia za uongo, unafiki, fitina, wasaliti, ndumilakuwili, kujipendekeza, kutafuta sifa, kukurupuka, ushabiki, na unazi usiokuwa na tija kwa taifa. Tabia kama hizi zina fifisha ubunifu, uzalendo, umakini, ujasiri na umahiri kwa vijana katika uongozi na uwajibikaji. Tumejenga jamii ya vijana walio gawanyika kihisia, itikadi, maneno na kwa matendo yao, waoga wa kutetea ukweli, wepesi wa kushindwa na uovu, walio tayari kusema vya kukaririshwa. Ndio maana kuna vijana walio tayari kukosoa jambo lolote kutoka upande wa pili hata kama ni jambo jema kwa taifa na wapo tayari kusifia jambo lolote la upande wao hata kama ni sumu kwa Taifa. Wameamua kuwa baridi ama moto.
Mimi nimekataa kuwa sehemu yao, kuwa mtumwa wa fikra zao, kutumika katika malengo yao. Nimeamua kuwa mfuasi wa ukweli na kwa fikra huru. Nahitaji Ukweli ili uniweke Huru, ukweli utakao tibu Taifa ili vizazi vijavyo vipate kufaidika na ukweli huu.
Unga kuchagua ukweli ili tujenge Taifa lenye kuheshimu ukweli.
Peter Sarungi (The next Speaker)Ipo siku masikio yata ona badala ya kusikia na macho yatasikia badala ya kuona. Wakati ambapo utatamani ujifiche chini ya milima lakini haitawezekana, wakati ambao wanawake wengi wataomba kuitwa kwa jina la mwanaume mmoja huku wakijilisha na kujivisha wenyewe.
Kwa sasa namfananisha Tundu Lisu na mwanasiasa mkongwe wa vikwazo kutoka kwa jirani zetu Uganda Mh. Kiiza Besigye. Kwa hivi vikwazo vya kuwekwa korokoroni na kupewa kesi nyingi za uchochezi kwa Mh. Tundu Lissu huku akiendelea kuwa jarisi na mwenye kutetea ukweli na hata kutenda na kuheshimu sheria. Sasa ninaona umuhimi wa Tundu Lisu kuwa Raisi wa TLS maana kwa sasa tunahitaji viongozi wanao hoji mifumo kandamizi bila uoga ili kulinda maslahi ya Taifa na watu wake. Kwa courage aliyonayo Mh. Tundu Lissu katika siasa za kweli, naamini hichi ni kipindi cha watu kama akina Lissu kunyanyuka na kuungwa mkono kwa makusudi.
Ningekuwa ni mwanasheria, ningemchagua Lissu kuwa Raisi wa TLS. By the way hiyo TLS na majukumu yake nimeifahamu kipindi hiki kupitia Lissu na inawezekana sio mimi tu, tupo wengi.
Tabia ya wana siasa kabla ya kuwa watawala ni kama tabia za wachumba ambao bado hawajafunga ndoa. Tabia yao kuu ni kuhaidiana mazuri, kusifiana, kuelekezana kwa lugha ya kuvutia, kutiana moyo, kuoneshaana upendo wa agape lakini pia kuna tabia moja mbaya ya walioyo nayo ya kuficha udhaifu wao na mabaya yao.
Kila inapoitwa leo, napata fursa ya kujua tabia za mkuu wa nchi kupitia kauli zake na matendo yake. Niliwahi kukiri hapo mwanzo kwa kusema kuwa Mkuu wa kaya anasimamia vizuri kauli na matendo yake wakati wa kampeni nikidhani ataendelea kutawala kupitia kauli zake za kusisitiza umoja wa nchi. Nahisi ni mihemuko ya muda iliyo niathiri.
Pamoja na changamoto hizo bado maisha na siasa zitaendelea na ni lazima tuendelee kuwaoma wabunge hasa wa CCM ambao ni 75% kusimamia kwa kuikosoa, kuisema na hata kuipongeza serikali wanapo kuwa bungeni maana hiyo ndiyo kazi tuliyo watuma. Pamoja na mtikisiko huu ulio wapata wabunge kutoka kwa Mkuu wa kaya kama ilivyo ripotiwa na gazeti la mwananchi bado mtaendelea kuwa wabunge mlio pewa dhamana na wananchi ya kuwa wakilisha bungeni katika kuisimamia serikali.
Tusijenge Taifa la chuki na uadui unao tokana na siasa, tuki ruhusu hilo basi hatutokuwa salama maana ukweli ni kwamba chuki na uadui havina mipaka, nikikuchukia kwenye siasa usidhani nitakupenda uraiani. Hiyo ni mbegu mbaya itakayo tafuna jamii yetu.
Tujitahidi kujenga jamii ya kuvumiliana, kushauriana, inayo heshimu fikra tofauti na inayoweza kuwa karibu hata kama watakubali kutokukubaliana.
Ukichagua upendo kuendesha maisha yako utaishi kwa furaha na amani sana kwani utaonyesha upendo,utazungumza maneno yenye upendo,na utachagua upendo katika kila jambo,hata pale penye mchanganyiko wa chuki na upendo utachagua kuona upendo na kupuuza mengineyo.Siku zote wenye mioyo na fikra za upendo hubarikiwa zaidi na hiyo ndio siri ya maisha.
Nimepata taarifa juu ya kuzaliwa CCM mpya iliyo badilika katika muundo wa chama na uendeshaji lakini ikiendelea kubaki na itikadi yake ya zamani. CCM Mpya iliyosemwa na mwenyekiti wake kwamba itakuwa chama kwa wanachama yaani chama kitakacho milikiwa na wanachama wenyewe tofauti na mwanzo. Inasemekana kabla ya upya huu, chama kilikuwa kina endeshwa na wanachama wenye nguvu za fedha, vyeo na hata umaarufu. Sasa kwa upya huu, chama kitaendeshwa hata na mlalahoi bila kujali umaarufu wake, cheo chake ama fedha zake… (SAFIII SANAAA..)
LAKINI..????? Tafakuri yangu ni jinsi gani chama hiki kitaendeshwa na kumilikiwa na wanachama kama inavyoitwa CCM Mpya… ………Ikiwa kiwango cha uwakilishi wa wanachama hawa kwa idadi katika vikao muhimu na vinavyo toa maamuzi muhimu ya chama umepunguzwa kwa zaidi ya nusu??? Yaani kutoka mia tatu na kitu hadi mia moja na kitu..!!!Ikiwa idadi ya vikao vilivyokuwa viki tathmini utendaji wa chama na serikali vimepunguzwa???Chama chenye wanachama na wapenzi wapatao milion 8, kutoka mikoa 35, ikiwa na jumuiya mbalimbali karibia tano na matawi lukuki, chama kinacho ongoza nchi kuongozwa na wajumbe 165 badala ya 385 alafu tuna sema CCM mpya ya kumilikiwa na wanachama??
Hili panga ni kali na sijui kama hawa vijana wenzangu Benard R. Shigela ?na Yesaya Shamsele ?walio anza vizuri kujifunza siasa na uongozi kama watapata nafasi na fursa ya kuwepo kwenye vikao vya CCM mpyaJJk alidokeza sababu ya mabadiliko haya kuwa ni UKATA…. Tunasoma Namba.. Hii sababu ya kuifanya CCM kumilikiwa na wanachama bado kwangu haija ingia akilini labda wadau watufafanulie..