All posts by Alpha Igogo

Mother and daughter moment!

Wema atinga Chadema bega kwa bega na mama yake! Limekuwa si jambo la kushangaza sana kuona mama Sepetu akiwa mguu kwa mguu katika maswala yanayo muhusu binti yake Wema Sepetu, japo kwa safari hii imekuwa tofauti kidogo na matukio mengine anayo yafanya!…….Wema amemwaga manyanga ya CCM na kubeba manyanga ya Chadema juu tena kwa madaha na mbwembwe nyingi huku mama yake mzazi akiziunga mkono na kuzibariki mbwembwe hizo!…….  Je, nguvu ya mrembo huyo yatosha kumng’oa Magufuli  / CCM madarakani?!! Mimi sijui kwani Siasa isn’t my cup of StrawberryMango smoothie! Bali naweza sema tuombeane uzima ili tushuhudie mambo 2020!……wishing her the best in her handover!

A woman will give you all the physical attention you want if ……!

Women to women event, dare not to miss it!

2020 ni Pagumu!- Peter Sarungi

                    2020 NI PAGUMU!

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

 Ikatokea Mungu akakubariki kufika 2020 ukiwa hai na mwenye afya nzuri basi utakumbana na changamoto ya joto kali la siasa ambalo halijawahi kutokea nchini. Kwa Lowasa Edward, 2020 ni mwaka wake wa mwisho kujaribu kufikia ndoto zake za kutawala nchi, ni kama ana bunduki iliyobaki na risasi moja ndani ya mapambano, hivyo ni lazima apambane kwa akili sana tena kimya kimya ili kutafuta target sahihi ya kufyatua risasi yake kwa adui. Ndio maana kwa sasa Lowassa anajipanga kimya kimya akiamini matokeo yake ni 2020.Kwa JPM, 2020 ni mwaka wake wa kuimarisha utawala wake na hasa kupata matokeo yatakayo leta taswira ya kupwaya kwa upinzani nchini. Hivyo kwa sasa anajipanga kwa matendo na kwa mifumo ndani ya chama na nje. Kutokana na nguvu alizopewa Raisi kupitia katiba ya nchi, ni kazi nyepesi sana kutengeneza mfumo utakao kusapoti mbele ya safari hivyo tutegemee mifumo hiyo kukamilika 2019.  

Kwa wananchi, 2020 ni mwaka wa majaribu sana kwao. Mpaka sasa bado wananchi wengi hawajui mwisho wa utawala huu ukoje, hawajui kama kutakuwa na mazuri ama mabaya ndani ya miaka hii mitatu iliyobaki (2017, 2018 na 2019) ikitokea uchumi wa mwananchi ukakua hadi kufika kipindi cha JK basi JPM atakuwa amepiga risasi ya ushindi kwa wananchi maana mpaka sasa amefaulu sehemu kubwa hasa ya ufisadi na nidhamu lakini amefeli kwenye UKATA wa wananchi, kuna malaika wameanza kuishi kama mashetani. 

Kuna Hash tag mbili zinazovuma mitandaoni

1# Nitamchagua tena 2020

2# Usirudie kosa 2020

 

Tafakari…. Chukua Hatua.

Womanhood!

Kama unazifahamu tuambie!-Jackline Mengi

“Women are everywhere but Queens are scarce”!

Thank you from Mr and Mrs A. Banduka 

We would like to thank you for all the love and support you have given us over the course of our lives and for being in the midst of this exciting and memorable adventure. We appreciate each of you and recognize your participation. We’re honored that you came to celebrate and witnessed our love and vows to each other. To each and everyone of you, you mean so much to us and we’re beyond thankful to have you in our lives. Finally, to all of those who have given us their time and helping hands with planning this wedding, WE THANK YOU. From the bottom of our hearts we could not have done this without you.

“hardcore truth”!

Hardcore Truth!  Huwezi kuoa au kutembea na warembo wote, wanawake wazuri siku zote wataendelea kuwepo, kila siku utakutana nao wapya. jifunze kuwa na adabu (self discpline) pamoja na kujidhibiti (self control).

Chagua mmoja tu, mjenge awe wako, mfanye awe malikia wako! hii itakupunguzia gharama, itakutunzia muda wako, drama pamoja na magonjwa.

Vile vile hakuna medali, tuzo au nishani ya juu ya ushindi wa kuwa na wanawake wengi, bali ni kuzifungia baraka ambazo Mungu anataka kukupa na kujipeleka mwenyewe kaburini mapema. Jiongeze brother!

Busara yangu; A realman sees no other females becoz he only has eyes for his girl! Mwl Tweve Hezron.

Nitarejea…….!

Hello wapendwa wasomaji wangu, natumaini wote hamjambo. Mie mzima wa afya hofu na mashaka ni nyie mlio mbali na upeo wa macho yangu 🙂 🙂 🙂 ……..wapendwa nime wamiss sana ila naomba mnivumilie tu simnajua nipo Bongoland na mambo ni mengi lakini soon tutarudi katika hali yetu ya kawaida na kwa nguvu mpya!…..Hata hivyo nawashukuru sana Halotel kwa  internet  ya uhakika! Nawasii wote tumieni mtandao wa Halotel kwa mawasiliano yenye viwango vya kimataifa!……..Nitarejea….!

The most attractive quality any man could have is integrity!

Jojo and the Carters’!

Awwwih! Umesoma hiyo caption?! Isn’t that something! Nilisema last year around October or November kuwa Jokate is our “Princes Diana” she is going to be big kuliko unavyo fikiria and conquer the unconquerable! Keep on shining Jojo vijana wa Tanzania na Africa wanakutegemea sana. Show them the way!  We love you!Wow! Mungu ajalie kheri tu kwani tunawakaribisha kwa mikono miwili!

2017-Hottest And Best Couple Of The Year!

Mr and Mrs Joseph Musira ndio Hottest And Best Couple of the Year!……Sababu haswa ya kuichagua hii couple kwanza nimeamua kwa mwaka huu ni enzi wazee wetu. Pili miaka 53 ya ndoa si kitu kidogo lazima kiheshimiwe! Napia ni kwasababu wanastahili!!……Basi ifuatayo ni historia yao fupi ambayo nitaieleza kwa kutumia picha zao za sherehe ya miaka 50 ya ndoa yao (Golden Jubilee of their wedding) ambayo ilifanyika huko Musoma, Mara miaka 3 iliyopita! Sherehe hiyo ilianzia kanisani ambapo walibariki ndoa yao na kuvaa pete ya nadhiri ya miaka hamsini!…….Haya furahia picha and Happy Valentine’s Day to you all! Maombi na kiapo yakiendelea ……….. Mr Joseph Musira na Felister Awiti wao ni wazaliwa wa mkoa wa Mara. Walikutana kwa katika kijiji kimoja kijulikanacho kama Kowak katika wilaya ya Rorya mkoani Mara. Felister yeye ni mzaliwa wa kijiji hicho cha Kowak akiwa ni mtoto wa kwanza wa mzee Cornel Awiti. Wakivishana pete baada ya ndoa kubarikiwa!…….Mzee Joseph Musira yeye ni Mwalimu kwa taaluma; hivyo wakati alipokutana na Felister alikuwa ni Mwalimu wa Kowak Middle School ambayo ipo chini ya missionary ya Wakatoliki. Kwasasa shule hiyo imebadilishwa na kuwa secondary ya wasichana ijulikanao kama Kowak Girls Secondary School ambayo mimi nilikuwa ni miongoni mwa wanafunzi walio fungua shule hiyo kwa mara ya kwanza. Mdogo wangu anaye nifuata kuzaliwa naye alisoma hapo! Picha ya pamoja na viongozi wa Diocese ya Musoma ambapo mzee Musira amekuwa mtumishi wao mpaka leo hii! Alianza kwa kufundisha kama Mwalimu, baadaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa shule zote za mkoa wa Mara ambazo zinamilikiwa na kanisa Katoliki mkoani humo! Ali stahafu akiwa katika cheo hicho zaidi ya miaka 5 iliyopita, lakini kwa uwadilifu wake na maadili mema kazini walimuomba kuongoza charity organization ambayo ipo chini la kanisa hilo hapo Mwembeni street, Musoma. 

Cheti kiki kabidhiwa toka Vatican kwa Papa!….. Furaha iliyoje! Wakielekea ukumbini kwenye sherehe!…..Kama nilivyo waeleza hapo mwanzo kuwa Mzee Musira alikutana na bibi Felister katika kijiji cha Kowak akiwa Mwalimu. Basi naye bibi Felister alikuwa ni Registered Nurse katika hospitali ya Kowak Mission ambayo nayo ipo chini ya missionary ya Wakatoliki. Ambapo pia baba yake mzazi bibi Felister alikuwa akifanya kazi kama Clinical officer katika hospitali hiyo…….Miaka miwili baada ya wapenzi hawa kukutana waliamua kufunga ndoa, kula kiapo kitakatifu mbele za Mungu na uso wa dunia! Hapo ilikuwa tarehe 12 / September / 1964! Kama mnavyo jua kuwa maswala ya kuoa katika familia za Kiafrika si kitu cha mchezo kama wenzetu wa dunia ya Magharibi ambapo wapenzi wanaweza kuwataharifu wazazi wao kupitia Facebook, text msg, Tweeter, na Instagram kuwa wao wamepanga kuoana siku fulani na wazazi wakafurahia kabisa kwa furaha kuu! Hapana, ndoa ni agano takatifu lazima liheshiwe sana kwa kufata taratibu maalum za kimila na kidini! Basi ndivyo hivyo kama wafanyavyo wengine naye alifanya! Mzee Musira alifata mila za Waluo ili kuweza kumchumbia na kumuoa bibi Felister! Yeye aliambiwa atoe mahali ya ng’ombe 12 na pia amjengee mama nkwe nyumba ya mabati ya vyumba vitatu na sebule! Awwwh! Huu ukoo wa Awiti siyo watu wa sport sport ati 🙂 🙂 🙂  Si mnajua kuwa bibi Felister alikuwa msomi (Registered Nurse) wa nguvu 🙂 🙂 hivyo baba mtu hakutaka mchezo na binti yake! …….Ukisikia “mapenzi mubashara” basi haya ndo yenyewe kwani mzee Musira alitekeleza hayo masharti yote bila pingamizi! Hiyo nyumba ndio mama mkwe wake aliishi mpaka mauti ilipo mkuta mwaka 2014! Tutakiane mkono wa amani mpenzi wangu, tumetoka mbali sana. Asante sana kwa “mapenzi mubashara”…..,hayo yalikuwa maneno matamu kabisa kutoka kwa mzee Musira kwenda kwa la azizi wake bibi Felister ???   Champaign zikifunguliwa na watu wenye nyuso za furaha kabisa! Aliye vaa vazi la kitenge ni mdogo wake bibi Felister aitwaye Anna Cornel au Mrs Obure. Yeye ndiye anaye mfuatia Felister, ni Mwalimu mstahafu hapo Musoma. Baada ya kufunga ndoa bibi Felister ilibidi ahame kwenye nyumba aliyopewa kuishi kama nurse mkuu hapo mission na pia alibadili jina lake la mwisho kutoka Awiti kwenda Musira. Hapo ndipo walifanya maamuzi ya kuhamia Musoma, na miezi michache baadaye mzee Musira alipelekwa Germany kuongezea utaalamu zaidi katika fani yake! …….Waliishi Musoma kwa miaka kadhaa na baadaye mwaka wa 1970 waliamishiwa Moshi ambapo waliishi kwa zaidi ya miaka 10 kabla ya kurudishwa tena Musoma……. Mr na Mrs Musira wao wamebarikiwa kupata watoto 6. Watatu wa kiume (Musira, Gerald, na Peter) na watatu wakike (Eddina, Yasinter, na Neema). Eddina a.k.a Eddi yeye ndio mtoto wa kwanza na Neema ndio wa mwisho! Kwa bahati mbaya kijana wao aitwaye Peter yeye alisha lala usingizi wa mauti; hivyo hayupo nao tena! May his soul continue to rest in peace!Mungu pia amewajalia kupata wajukuu wanne! Wakiume watatu na wa kike mmoja!  Wakinyweshana kinywaji maalum cha siku hiyo Mahaba mahabani! Kama walivyo shikamana siku ya kwanza pale Kowak basi ndivyo watakavyo shikana mikono yao mpaka mauti itakapo watenganisha! Waki kata keki kwa upendo na furaha Nilishe nikulishe ndio ishara ya upendo Mungu ni pendo. Penye Mungu kuna upendo mwingi na furaha isiyo elezeka! Hapa siongelei tu ndoa za “maigizo”, zile ndoa za ku-show off picha kwenye mitandao ya kijamii wakati ndani ya nyumba zenu wengine hawahemi! hapana! Naongelea real marriage, real commitment, honoring your vowels!!………. Miaka 53 ya ndoa hakuna michepuko wala mtoto wa “bandia”! Jamani, inawezekana!! These are real people in our communities; nina huwakika wapo wengine wengi tu!………Ee Mwenyezi Mungu endelea kumimina baraka zako kwenye hii ndoa na familia yao, Amen!

Couples we like!

Mother and daughter moment

Katika wazazi ambao nawahurumia pia na mu-admire sana ni mama yake Wema Sepetu! Ni mmoja wa wazazi ambao wanapitia changamoto nyingi sana katika maisha ya kila siku kutokana na maisha ambayo binti yake ameamua kuishi; hivyo kahilo namuhurumia sana! Lakini kama nilivyowai kusema huko nyuma (somahapa) kuwa ni mama ambaye ananifurahisha sana na jinsi anavyo simama bega kwa bega na binti yake, katika mabaya na mazuri! Kwa wazazi wa Kiafrika ni ngumu sana! Wachache mno wanaweza fanya afanyavyo mama Sepetu! Na kwasababu hiyo anakua mfano mzuri sana wa kuigwa! Mtoto wako ni mzigo wako mpaka kifo. Huwezi mkana au mkataa mtoto wako eti kwasababu tu haendani na maisha utakayo! Big up mama Wema!

 

ASANTE JPM KUBARIKI VITA HII (Sehemu ya II)- Peter Sarungi

 

Na Peter Sarungi (Next Speaker)“Vita ya dawa za kulevya haina umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu anahusika mkamateni” Raisi Dkt. Magufuli…….Katika vita hii, nilikuwa nasubiri kauli ya mkuu wa kaya ya kutoa support ya ulinzi, usalama na hata kubariki vita hivi alivyo vianzisha Mh. Makonda (RC. Dar)  Kauli alizozitoa Mkuu wa kaya wakati wa kumwapisha Mkuu wa Majeshi Tanzania yana ashiria ushiriki wa moja kwa moja wa mkuu wa kaya. Majibu ya JPM kwa kauli ya Mh. Nape ni firimbi kwa viongozi wengine wanao leta sababu nyingi za kunyamazisha vita hii wakati vijana wana angamia. 

“Kauli ya Raisi ni agizo linalo hutaji utekelezaji bila kusita” Peter Sarungi @2017

Mother and son moment

Penny na kijana wake wakifurahia weekend. Wamependeza sana! Mwaju na first born wake. Wamependeza sana! The smile tells it all!

Je, upo tayari?! Couple yangu ya pili -2016

Are you ready!!! Hii ndio ilikuwa couple yangu ya pili kuichagua. Mpaka sasa sijajutia kuichagua. Yani couple zote bado zipo kwenye mahaba mazito sana!! Nawaombea Mungu ndoa zao zidumu milele na awatangulie katika kila jambo! Kama ulipitwa soma HottestAndBestCouple-2016 …….. Je, upo tayari kwa 2017?!! Stay tuned!

Pastor Caleb Migombo: If we looked only at the headlines every day……!

If we looked only at the headlines every day, we would have good reason to be pessimistic about the future. But don’t forget two important truths.

First, the future is in God’s hands, and nothing takes Him by surprise. He is sovereign over the history of the world as well as our own personal histories, and behind the scenes He is at work to accomplish His purposes.

Second, never forget that even when the future is unclear, God is with those of us who are trusting Christ as our Savior and Lord, and He helps us. No matter what the future holds for you-no matter what today holds for you-you do not face it alone if you know Christ.

The Lord reigns forever.

Psalm 146:10  Kama tungeliangalia tu vichwa vya habari za kila siku, tungekuwa na kila sababu ya kukata tamaa juu ya siku zijazo mbele yetu. Lakini imetupasa kutosahau ukweli huu.

Kwanza, siku zijazo mbele yetu ziko mikononiu mwa Mungu, hakuna kinachomshangaza au kumshitukiza Mungu. Yeye ni Mtawala juu ya tawala zote za dunia, juu ya matukio yote ya historia ya ulimwengu, na hata matukio na historia ya maisha yetu binafsi. Nyuma ya pazia ya matukio yote haya, Yeye yuko kazini usiku na mchana  kutimiza makusudi yake.

Pili, Kamwe usisahau kwamba hata pale ambapo siku zijazo hazielewekieleweki zitakuwaje (unapoona giza), Mungu yupo pamoja nasi na wote wanaomtumainia Bwana katika maisha yao. Yuko tayari kutusaidia siku zote. Bila kujali lipi litatokea kwako katika siku za usoni- bila kujali leo itakuwaje kwako- kumbuka kuwa hutayakabili maisha na siku zake pekee yako, kama unamjua, na umempa Kristo moyo wako. 

Bwana anamiliki Milele…Kizazi hata kizazi. Haleluya

Zabri 146:10

je, upo tayari?! Couple yangu ya kwanza -2015

Nilipo anza ku-blog ilikuwa ni mwezi wa Pili mwaka 2015. Na hii ndio ilikuwa couple yangu ya kwanza kabisa kuichagua kama Hottest and Best Couple of the yr kwa mwaka huo! Nikitu niliamua kufanya kila tarehe 14/2 ya mwaka (siku ya Valentine day) nitatangaza couple moja iliyonivutia ambayo pia naona kuwa ni mfano mzuri wa kuigwa katika jamii! Kama ulipitwa na tangazo hilo tazama hapa ? HottestAndBestCouple-2015

Je, upo tayari kwa mwaka huu?? Stay tuned!!