All posts by Alpha Igogo

TUSIBEZE VITA HII (Sehemu ya I)- Peter Sarungi

 Tusibeze uthubutu wa mtu tena kijana wa kawaida ambaye bado hajawa nguli katika siasa wala uongozi. Tumpe muda maana hiyo vita aliyoichagua ni vita ngumu inayo hatarisha maisha yake. Huyu ndiye kiongozi pekee wa kumuombea tofauti na wengine. Huyu yupo kwenye vita ambavyo kama wewe ungepewa fursa ya kuwa mkuu wa mkoa huu basi inawezekana ungeshindwa kudeal hata na dagaa kama Makonda alivyoanza. Tumpe moyo mkuu na kumwombea kwa Mungu apigane vita vizuri, naamini hata kama hatashindwa kufikia mafanikio tunayoyataka lakini atakuwa amefanya sehemu flani ya kutatua uovu huu ambapo mwingine atakaye jitokeza katika vita hiyo ataanza alipo ishia Makonda. Hatuwezi kunyamaza kimya kwa tatizo kubwa kama hili na asitokee hata mtu mmoja wa kusema hata kidogo alafu tukajiona tupo samala, Laa hasha kukaa kimya ni kuhalalisha uwepo wa tatizo. Vijana wengi wana angamia na kupoteza nguvu kazi na vipaji kwa sababu ya kukaa kimya na hata kubeza jitiada hizi ndogo zinazo chukuliwa na Makonda. Tuungane na Makonda kutenda na kufikiri tofauti kwa kuchukua hatua za kutenda badala ya malalamiko na matamko yasiyo isha wala kusaidia jamii. Tuweke siasa pembeni kwenye majanga makubwa kama haya ili kuunga kila hatua zitakazo chukuliwa na yeyote katikakupambana na Tatizo hili. 

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

Asanteni..

Sabato Njema wana wa Mungu.

If you sign up for a “sex only” relationship in the beginning…..! Don’t ask him to wait if you can’t!

Ujumbe huu unajieleza wazi kabisa! Kama wewe nia yako ni kuwa na mume basi usitafute boyfriend kwani nia ya malengo yako hayata timia! Kama nia yako ni kuwa na mtu wa ku share naye mapenzi maisha yako yote basi usikubali tittle ya “my lover au mwanamke wangu” kwani hivyo ndivyo utakavyo ishia! Respect is earned not given!…………. Na usimwambie mwanaume ngoja mpaka tufunge ndoa wakati wewe si bikira! 😉 😉 ……….. Happy early Valentine to you all!

WIZARA INA MIKAKATI GANI JUU YA WATU WENYE WALEMAVU TANZANIA?- Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

Watu wenye ulemavu ni moja ya jamii iliyo katika makundi nyonge (kwa sasa tumefika milioni 4 kwa idadi). Makundi mengine ni kama wazee, watoto na wanawake, makundi haya yanaitwa ni makundi nyonge kwa sababu yana mahitaji maalumu ya kibinadamu na hayawezi kumudu ushindani ulio sawa katika jamii hivyo ni lazima jamii pamoja na serikali iyatizame kwa jicho la tatu lenye utu, huruma na upendo ili nao wajione wapo katika nchi yao na waweze kuonesha uwezo wao ambao Mungu amewakirimu pasipo kujali mapungufu waliyo nayo. 

Peter Sarungi akiwa na dada zake; Alpha Igogo (kushoto) na Magreth Igogo (kulia) nyumbani kwa Peter huko Chanika.

Mimi ni Mlemavu lakini hata wewe ni Mlemavu mtarajiwa maana kama bado unaishi duniani basi jua Mungu bado anaendeleza uumbaji wake kwako. Hivyo linapotokea jambo linalohusu ulemavu basi jihisi na wewe ni mhusika kwa namna moja ama nyingine.

Katika uchaguzi uliopita 2015, nilitoa tamko kupitia jumuiya za watu wenye ulemavu Tanzania ambao ulilenga kueleza changamoto za walemavu pamoja na mapendekezo yake. Changamto kuu nilizoziainisha kwa msisitizo ni ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika vyombo vya maamuzi pamoja na muundo wa kusimamia maswala ya watu wenye ulemavu. Niliamini kuwa ili kutibu changamoto hizi za elimu, ajira, afya, uchumi, siasa na huduma zingine ni vizuri tukashirikishwa katika kupika chakula na kukiandaa mezani.

Nilifarijika sana baada ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza baraza la Mawaziri pamoja na muundo wa wizara zake, kwa kweli mhe. JPM alitutendea haki ambayo haikuwahi kutendwa na tawala tangu kupatikana kwa uhuru wa nchi. JPM alisikia kilio cha watu wenye ulemavu kwa kutenga wizara itakayo husika na maswala ya walemavu tena ikiwa chini ya ofisi ya waziri mkuu kama tulivyotoa kwenye tamko na pia akateua waziri mwenye asili ya ulemavu (dr. Abdallah posy) na makatibu wa wizara wawili wenye ulemavu akiwemo mwanasiasa Amon Mpanju ili kushiriki kupika chakula cha walemavu. Hakika baada ya uteuzi huu, jamii ya qatu wenye walemavu tulianza kuona nuru na kuona matumaini ya kula chakula tulichoshiriki kukipika na kukiandaa mezani. Nampongeza sana Raisi kwa moyo huu wa kujali makundi manyonge katika jamii(Mungu azidi kumpa afya tele na azidi kutetea wanyonge kama anavyofanya sasa)

TATIZO NI NINI?????

Kwa mtazamo wangu, bado naona hakuna mabadiliko chanya yanayoletwa na wizara hii hasa kutoka kwa waziri husika Mh.Posy. Bado mifumo ya unyonyaji imeendelea kuwepo kwenye vyama vya watu wenye ulemavu, bado uchumi umezidi kudorora kwa watu wenye ulemavu, bado Elimu imekua duni na garama kwa watu wenye ulemavu, Bado siasa haiwatambui watu wenye ulemavu kwa vitendo, Bado sheria No 10 ya watu wenye ulemavu imewekwa kando, Bado ajiri imekuwa ngumu na ya kubagua watu wenye ulemavu na bado huduma bora imekuwa ni kitendawili kwa watu wenye ulemavu.

Je ni nani wa kututetea? Ni nani wa kutusemea kama sio Mh. Posy na wenzake akina stella ikupa, Dr. Macha, Amina Mollel, Amon Mpanju na wengine walio katika kundi hili?. Ni nani wa kulaumiwa ikiwa JPM ametupa nafasi kupitia hawa wenzetu alafu wamekaa kimya? Ni nani wa kuonesha mfano na kuaminisha jamii juu ya uwezo wetu kama sio akina Posy, Mpanju, macha, stella na wenzake? Ni nani wa kupiga kelele juu ya mateso na manyanyaso wanayoyapata wafanyabiashara walemavu wa Tanzania kama sio akina Mh. Posy, Mpanju na wenzake waliopata fursa? Ni nani wa kutuunganisha watu wenye ulemavu na kupata fursa za uchumi na siasa kama sio hawa walio teuliwa na JPM? Mbona wamejisahau utafikiri hawajatoka katika kundi hili? Au wanadhani fursa waliyopata ni kwaajili yao peke yao? Au ndo kusema ni aibu na dhihaka kuwa mlemavu na kutetea jamiiyako? Mbona kasi ya JPM inawaacha mbali? Tatizo ni nini?

Tulikaa kimya na kuwapa ushirikiano ili kuona matunda ya kushirikishwa katika kupika chakula lakini inakaribia mwaka sasa hatuoni kama chakula mnachotupikia ni kizuri…

Tafakarini na chukueni Hatua…. 

Tafadhali, naomba ifahamike yakuwa hii article iliandikwa wiki mbili zilizopita wakati Dr. Posy akiwa bado ni Waziri. Lakini sasa nafasi yake ipo wazi!

Womanhood!

“Sometimes I really wonder!”- Sandra Mushi

Sometimes I really wonder! How we can just wake up and pull ‘sherias’ out of our hats. Sasa ati no spot lights, no fog lights and no tints …

How about you install street lights on ALL streets and actually have them ON and working; and how about having proper and working security measures including when I come report a theft, you actually attend to it and FOLLOW it up!  Instead of asking for ‘chai’ na ‘nauli’ kila kukichwa.

Those lights are our safety so I don’t have to worry about driving into a bridge on a dark night.  They are my safety so I can see clearly on a rainy day.  They are my safety so I can see that drunkard staggering from a far even before I get to that corner.

Those tints are our safety so I don’t have my windows broken as I am sitting in a meeting simply because the street boy saw my gym bag on the back seat.  They are my safety so when they want to follow me home they are not sure who is in the car.  They are my safety so that conniving motor cyclist does not see that its a lone woman driving.

Hembu do your due diligence basi and assure us of our safety before you mercilessly start imposing this ‘out of the hat’ sheria on us.

You do your part and we will humbly oblige and do ours.

Cheka urefushe maisha!

Jokate wetu! chaguo letu! Katika ubora wake!

Nani kaka Jojo?! Mwanamke wa shoka! Mrembo mwenye akili ya maendeleo na maadili!…… Keep on shinning mrembo wetu, wewe ndio chaguo letu hakuna mwingine!……. We love you Jojo!

“Hii ni sababu mojawapo kwa nini ni lazima kuachia ya nyuma yapite”- Pastor Caleb Migombo

Umeshagundua kuwa ukiendelea kumchukia mtu, chochote kile walichokutendea kitaendelea kukuumiza maisha yako yote? Hasira zetu na chuki huzidi kutonesha vidonda vya majeraha ya huko nyuma (zamani).

Hii ni sababu mojawapo kwa nini ni lazima kuachia ya nyuma yapite na – kwa msaada wa Mungu – kufungulia hasira na chuki vitoke kabisa katika  maishani mwetu, na badala yake turuhusu Upendo wa Mungu kukaa ndani yetu. Kama tusipofanya hivyo, mioyo yetu itatiwa sumu na kujaa chuki na uchungu maisha yetu yote yaliyosalia, badala ya kuakisi upendo na rehema za Kristo.  

Kumbuka Yesu anasema: “ Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowaudhii” Mt 5:44. 

Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya. Waef. 4:31

My people! #WhenItsFamily

Vote! Vote! Vote!……Piga kura tafadhali!!

TAIFA LA JANA, LEO NA KESHO…. na Peter Sarungi

Imeandikwa….

1. Baba bora ni yule anayelinda na kutetea familia yake, anaye tengeneza urithi mzuri kwa watoto, wajukuu hadi vitukuu na anaye hashimu familia yake.

2. Mke mwema ni yule anaye jenga familia yake bila kuharibu kwa mikono yake, anaye lea watoto katika maadili mema na anaye simama imara na mumewe katika hali ya hatari, dhiki, shida, raha, hofu, furaha, matatizo kama ya siasa, umasikini, chuki, wakati wa ujana na uzee, wakati wa afya na magonjwa.

3. Mtoto bora ni yule anaye heshimu wazazi wake na kujifunza maadili na maarifa kutoka kwa walio mtangulia. Ambaye anapenda kuwa kichwa na si mkia. 

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

#MyTake.

Vijana ambao wamefika umri wa kujenga familia wachukue hatua kufanya hivyo, wasisubiri harusi na madoido ya kifahari maana kuna maisha ya ndoa baada ya kupata sifa za harusi.

??Fidel Pilato alikuwa akiangalia post zangu  za nyuma huku akijaribu kuuliza maswali katika lugha nisiyo tambua.???…Hao ndio watu wazima wadogo, Taifa la kesho. NIWATAKIE MWANZO MZURI WA WIKI………MUNGU BARIKI KAZI YA MIKONO/AKILI ZENU.

Wametugusa sana; watakumbukwa daima!

Rais Obama anaweza asiwe the best President in American history. Lakini ni ukweli usio pingika kuwa they were the best 1st family ever!!……..Wamegusa miyoyo yetu, wamebadilisha mitizamo ya familia nyingi kwa kuonyesha jinsi gani family should look like! Mr and Mrs Obama wameonyesha mfano bora wa jinsi gani couple  should respect and support each other for the goodness of the family and your country! Wamekuwa mfano mwema wa wazazi jinsi ya kulea humble children pamoja na kuwa na access to everything they wanted! Wamegusa nafsi za watu wengi sana na kuacha their own legacy kwenye hii dunia! Tutawakumbuka siku zote, Mungu azidi wabariki!

Pastor Caleb Migombo: The Most important advice for life’s crossroads is this:

Pastor Caleb Migombo

The Most important advice for life’s crossroads is this:

” Seek God’s will.” He knows what’s best for you and me, and He doesn’t want us to wonder aimlessly through life.

Never forget: God made you, and He knows all about you-including the gifts and abilities He gave you. More that, He loves you and wants what is best for you. Maybe you’ve been living for yourself and for the moment rather for Him and for things eternal. But don’t stay on that path; you will only end up at a blank wall if you ignore God’s plan for your life. 

“I will instruct you and teach you in the way you should go; I will counsel you and watch over you” Psa 32:8

Foster Collection

Mwavionaje viwalo hivyo?!,Kwakweli vimekwenda shule sana! Mimi nimevipenda vyote japo naona hiyo ya yellow imevutia macho yangu zaidi!……Haya basi viangalie vizuri nawe uige kupendeza kama Foster. Halafu, siyo tu unashangaa picha hapana! Piga “chabo” kwenye mambo ya bustani ili ujifunze kitu, pia mambo ya upambaji na mpangilio wa nyumba. Pamoja na urembo wa mwili!…..soon nitawaambia ni wapi Foster huwa anakwenda kusafishwa na kufanyiwa massage ! Si unajua yale mambo ya SPA? Muhimu kwa mwili!

Rwanda has started legislative process to Make Swahili one of the official languages!

Hon. ShyRose Bhanji

Presenting the Motion to congratulate Rwanda for Starting a legislative process to make Kiswahili one of the official languages in Rwanda. This is highly commendable move and should be strongly supported by all stakeholders who have EAC integration at heart. #Kiswahili #OnePeopleOneDestiny …. #Nikiwasilisha Hoja bungeni ya kuipongeza Rwanda kwa Kuanza mchakato wa kutunga sheria ya kukifanya Kiswahili kuwa moja ya lugha rasmi nchini Rwanda. Hatua hii inahitaji kuungwa mkono na wadau wote ambao ni waumini wa mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. #UmojaWetuNiNguzoYetu

#EalaInKampala

Matukio katika picha: Jesse 11th birthday

Kheri ya siku ya kuzaliwa mwanetu Jesse! Mungu azidi kukulinda, akuongoze, na azidi kukubariku katika ukuaji wako! Ukawe mtoto mwema sana Wapendwa, naomba niseme kidogo kuhusu undugu wangu Jesse……..Bibi yake Jesse mzaa baba ni mtoto wa pili kuzaliwa kwa familia ya mama yangu (familia ya marehemu mzee Cornel Awiti); hivyo Jesse ni mpwa wangu! Siku ya tarehe January 16, 2017 Jesse alitimiza miaka kumi na moja tangu kuzaliwa kwake! Alisherekea na wazazi wake Dr. Joseph Obure, mama yake Venny Mwita, na mdogo wake Jason!  Jesse na wazazi wake wana ishi huko North Carolina, U.S.A Mama na birthday boy!  Lovely! Happy 11th birthday Jesse!

HUYU ANA MOYO MKUU…..by Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker)Kwa sasa ni nadra sana kupata binadamu walio umbwa na Moyo Mkuu, moyo unao weza kuhimili shida, kejeli, dharau, matusi ma vikwazo mbalimbali vyenye lengo la kulainisha Moyo. Mh. Lowasa Edward alikumbwa na kashfa akiwa CCM tena Waziri Mkuu, akasemwa na kutukanwa na viongozi, wanachama na wapenzi wa chama kikuu cha upinzani Chadema Tanzania, huku akiitwa Fisadi nchi nzima… Alikaa kimya bila kujibu.

Alipo hama CCM kwenda CDM, CCM walimuona kama msaliti ingawa kwa CDM alibadilika na kuwa Malaika. Bado aliendelea kutukanwa, kudharauliwa na hata kuombewa mabaya na viongozi, wanachama na wapenzi wa chama tawala kipindi cha uchaguzi 2015… Alikaa kimya bila kujibu.

Pamoja na yote hayo, bado ameendelea kuwa na Moyo Mkuu kwa nchi yake. Huyu namfananisha na Mh. Raila Odinga wa Kenya na Mh. Kiiza Besige wa Uganda kutokana vikwazo wanavyopitia. Mungu awatimizie haja ya mioyo yao.

Tujifunze kitu hapo, unajifunza nini?

Womanhood!

MH. LOWASSA ANAIJUA SIASA YA TANZANIA-Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a Next Speaker a.k.a Baba Pilato

Siasa za Tanzania bado hazieleweki kwa wananchi wengi na mimi nikiwemo. Wengine wanaiita siasa maji taka, siasa za kujipendekeza, siasa za mafigisu, siasa za mamluki na usaliti, siasa za propaganda, siasa za nguvu ya umma na nguvu ya dola, siasa za uongo, siasa za kidiplomasia, siasa za matukio, siasa za maigizo, siasa za maonyesho na mimi kwa sasa naziita siasa za Mwendo Kasi.Kwa Tanzania, ni Mh. Lowasa Edward pekee anaye jua siasa za nchi, anayeweza kubadili njano kuwa nyekundu, anayeweza kupanga na kupangua, anayeweza kubadilika kutokana na mazingira, anayeweza kumpenda adui yake hata kwa unafiki, anayeweza kubadili msimamo wa mpinzani wake, anayeweza kumbadili mpinzani kuwa mfuasi wake, anayeweza kupiga ngoma kisha serikali ikacheza, anayeweza kuwa na chama ndani ya chama, anayeweza kusababisha mafuriko ama hata kuyatengeneza, anayeweza kusababisha taharuki mtaani anapo onekana nahata kuwapa hofu watawala.

Kumekuwepo na kauli nyingi za kukubali ama kukataa uwepo wa njaa na uhaba wa chakula kwa muda wa zaidi ya wiki bila kuwepo kwa solution. Lakini Mh. Lowassa alipokuja na kauli ya kuwa na nia ya kutafuta chakula kwa ajili ya wahanga kwa madai kuwa Mkuu kakataa kutoa chakula kwa wahanga ikiwa ni sehemu ya kuleta suluisho la tatizo, jana serikali ikajibu mapigo kwa kusema ita sambaza chakula na ina hifadhi tosha ya chakula.

Viongozi kama akina Mh. Lowassa ni muhimu sana kwa jamii yetu hata kama wasipo weza kutawala nchi lakini uwepo wao na uwezo wao katika siasa za nchi intosha kufanya mabadiliko nje ya ya mfumo rasmi na kuleta matokeo chanya ya maendeleo..

Tutafakari kwa matendo bila hisia za vyama.

Tafadhali, embu m-follow Miss Universe wetu please!

Wapendwa wasomaji wangu, mmemuona mrembo wetu?! Miss Universe-Tz 2017!! Si mnamuona anavyo lipa? Je, ume m-follow?! Kwanini bado?! Basi mpendwa fanya hima m-follow leo kich weka comments nzuri za kumtia moyo japo “number don’t lie” she is doing great! Please let support our very own Jihan Dimack!………Soon nitakuja na maelezo ya jinsi ya kumpigia kura! Asanteni!