All posts by Alpha Igogo

cheka urefushe maisha!

🙂 🙂 🙂 hilo nalo neno lol!………Wapendwa naomba mnivumilie kidogo I’m dealing with some family issues right now, hivyo nitakua nachungulia humu mara moja moja! Samahani sana na asanteni!

Happy birthday Foster Mbuna-Mkapa!

Another year, another chapter. God you have been so Good to me and you have been with me stage by stage. So many challenges that have made me stronger, disappointments that have taught me to work harder and not to depend on people 100%, I helped a few people going through complex issues which means some people think am wise and feel that they can get words of Wisdom from me. All these and many more my Precious God you have given me freely and I thank you for that. Apart from good, health, wealth, parents, husband, sons, friends and family you have given me inner peace, joy and happiness. Lord I give you all the Glory and Honour for taking me thus far. 

So, as am celebrating the gift of life and a second chance to re edit my story, I pray that you give me more Love for others, humility, joy, inner peace, patience, a heart that forgives and forget the worst, wisdom and a heart that hungers and thirst for you only. Seeking you and dwelling in your presence everyday.  As am celebrating my birthday today am celebrating me. The baby/ daughter of Joe and Evalyne Mbuna, a wife, a mother, a God mother, sister to so many, a friend to many, an aunt, a cousin a sister in law and so many things that I am to different people. 

I celebrate the Girl that I was,  The Lady that  I am Now and The Classic Lady That Am Yet to Be! Thank you to all of you who have been part of my growth and progress and Thank you for your wonderful wishes. Be blessed and Highly Favoured!Happy birthday beautiful and sweet soul, woman of God, wonderful wife, amazing mother, precious daughter, and great friend! Wishing you more joy, more inner piece, good health, and more amazing life and good friendship!…..Happy birthday Foster! Ubarikiwe sana!

Ubaguzi wa watu wenye ulemavu nani alaumiwe na nini kifanyike?!

Hongera sana shule direct kwa jitihada zenu za kuokoa maisha ya watoto katika nyanja ya elimu!……Binafsi najiuliza hivi nani wakulaumiwa na nini kifanyike juu ya watu wenye ulemavu?! Mimi nasema ni ubaguzi wa wazi wazi kwa watu hawa na jamii imelifumbia macho! …….Miaka ya nyuma tulisema kuwa watu hawana uwelewa na leo hii je tunasemaje?! Shule moja ya secondary ya viziwi tena ni private?! Majengo mengi yanajengwa bila kujali kuwa tunao walemavu katika jamii yetu!! Majengo na maeneo mengi hakuna parking za magari specific kwa walemavu! Makanisa mengi sana hayana wakalimani wa viziwi! n.k………Huu ubaguzi ni mpaka lini? Nani wakulaumiwa? Na nini kifanyike? ……..Tafakari na chukua hatua!

Mother and daughter moment!

Mimi hapa na mommy angu ? hapa ni siku ya Juma Mosi iliyopita tukiwa nyumbani Keko Juu teyari kwa mtoko wa harusi ya mtoto wa jirani yetu and a good friend to mama…….Jamani sasa hivi tunaishi mbali hivyo tukitaka kwenda kwenye sherehe za maeneo ya Tabata, Mbezi n.k inatubidi tulale kwenye mji wetu wa zamani (Keko Juu) kwani wakati wakurudi kuna kuwa mbali na kabla ya kufika home kuna pori fulani hivi huwa hatupendi kupita usiku sana….Sasa hivi nafikiri itabidi kuangalia sana sherehe za kwenda kwani usalama wetu ni muhimu sana japo so far hatujawahi sikia kitu chochote kile ambacho ni cha kutishia amani au usalama wa eneo hilo!

Cheka urefushe maisha!

Womanhood!

Malezi ya watoto na changamoto zake!

Pole sana mpendwa, tunamuombea uponyaji wa haraka! …….tukio hili limenikumbusha jinsi my cousin brother alivyo “piga pasi” tumbo lake!  kaka yangu alikuwa na tabia ya kunyoosha sehemu za shati lake ambazo zimejikunja huku akiwa teyari amevaa!! Kumbe mtoto anamuangalia na siku moja akachukua pasi iliyokuwa yamoto Akanyoosha tumbo lake! It was an awful experience! He was  2.5 yrs old by then sasa hivi anakwenda miaka 30 na sidhani kama anakumbuka hilo tukio!…….Anyway, malezi ya watoto yana changamoto nyingi sana. Wewe mzazi unaweza kuwa makini lakini watu unao ishi nao wakawa ni majanga! Nikuomba Mungu tu kama una amini kuwa Mungu yupo!…..Juzi nilisimuliwa kisa cha mtoto wa cousi-sister wangu ambaye house girl alimfungia ndani ya nyumba akiwa amelala halafu yeye akaenda shule kumfata mtoto mkubwa, with a assumption kuwa “atawahi kurudi”! Too bad alipofika shule, siku hiyo walikuwa wamekwenda picnic picnic wakawa wamechelewa kurudi ikabidi dada wa kazi amsubiri! Mtoto aliye achwa nyumbani he is barely 3 yrs old!! Aliamka usingizini haoni mtu ndani ya nyumba! Mtoto kalia mpaka kachoka ma njaa juu! Mama mtu anarudi nyumbani anakutana na hayo majanga! Yani ni alimfukuza house girl siku hiyo hiyo!…..Sasa can you imagine kama moto ungewaka ndani ya nyumba na mtoto kachwa mwenyewe? Au mtoto angechezea jiko la gas ambalo wanalo hapo ndani! Hivi ingekuwaje?! . ……Malezi ya watoto yanahitaji maombi ya ziada kwani bila Mungu hatuwezi!

Vita ya drugs inatakiwa kuanza na sisi wenyewe majumbani mwetu- Lemutuz

Cheka uongeze maisha!

Katika kuitafuta furaha usimuumize mtu mwingine ili wewe uwe na furaha- Dina Marios

Katika kuitafuta furaha usimuumize mtu mwingine ili wewe uwe na furaha.Kila lililopangwa kuja kwako litakuja tu kama Mungu amelipanga kuja.  Huwa nayatazama maua yakiwa bustanini.Ni maua ya aina tofauti lakini hupokezana kuchanua.Hili litakaa miezi hata tisa bila kuchanua lakini siku likichanua linapendeza kweli kweli,lingine huwa limechanua mara zote,lingine huitaji jua kali ili lichanue na kupendeza.Ndivyo hata sisi tulivyo hatufanani na kila mmoja ana wakati wake wa kuchanua…wakati wake wa kufanikiwa.Sidhani kama yale maua huwa yanaoneana wivu mbona yule kachanua mimi sijachanua?Usiitazame furaha ya mwenzako ukateseka nayo,mafanikio yake ukateseka nayo na wewe ukaitaka pengine na yeye ni kama lile ua linalokaa miezi tisa ndio lichanue.Itazame safari yako na wewe wakati wako ukifika utachanua Utang’ara.

Katika  kuitafuta furaha na mafanikio njiani usimkanyage mtu,usimuumize mtu.Unaweza kufanikiwa leo lakini sio milele.Kufumba na kufumbua mambo yanaweza kubadilika.Unaweza kuwa kwenye nguvu na control leo lakini huwezi kuushinda muda…muda hubadilika….Good morning!

Womanhood!

MATOKEO YA KELELE ZA #BringBackBenAlive NI YAPI NA YAMEISHIA WAPI?- Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Watu wa Makabila yanayo patikana mkoa wa Mara (Kwetu Pazuri) wana desturi ya kuwa jasiri, wakweli na wenye uwezo wa kusimamia jambo analo liamini. Lakini huku jijini Dar tulipokuja kutafuta maisha, mambo yake yanaendeshwa kwa usanii, unafiki, uoga, dilli, uongo na kutafuta kicky pasipo sababu ya msingi.

Uozo huu umeingia hadi kwenye siasa kiasi kwamba huwezi kutofautisha siasa za chama tawala na zile za Upinzani yaani wote wamekuwa wafuasi wa mambo hayo ya jijini.

Wahusika Tuelezeni, kwanini mpo kimya kwa swala mlilo lianzisha? na mtuambie matokeo chanya ya #Bring_Back_Ben_Alive ?

Msianzishe kampeni katika mitandao halafu mkaziacha katikati bila kujua hatima yake, What if Ben amedhurika? Kelele zenu na ukimya wa Ghafla utakuwa umemsaidia nini Ben? Tafakari, Chukua hatua… 

SIASA NA DEMOKRASIA YA KENYA….. TUNAJIFUNZA NINI KATIKA MIFUMO YAO??-Peter Sarungi

 

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Taarifa zinaonesha kuwa kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Jamhuri ya watu wa Kenya ndio nchi ambayo ina mifumo inayo tekeleza Siasa huru na Demokrasia ya kiwango kizuri ukilinganishs na nchi zingine katika ukanda huo. Pamoja na kuwepo kwa Siasa za Ukanda na Makabila kwa muda mrefu lakini bado siasa zao zimekuwa ni za mfano kupita zetu za Tanzania.

Je, tunajifunza nini? kuna lipi unalo lijua kuhusu mfumo wao ambacho kwetu hakipo? Je, wananchi wao na wana siasa wao wana tabia gani ambazo ni tofauti na kwetu Tanzania? Saidia kujadili ili tupate Ufahamu.

Ladies! Pursuing man is nowhere in the Bible!

KILA MTU ABEBE MZIGO WAKE….. LASIVYO, MWAFA! -Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Naunga mkono kauli ya Mkuu wa Kaya kwa watani (Wajukuu) wangu wa mkoa wa kagera lakini naunga mkono kwa utani maana tulilia pamoja wakati wa msiba sasa ni lazima niwatanie kidogo kipindi hiki cha matanga.

Naamini hata Mkuu wa Kaya alikuwa anawatania ili kuwarudisha katika hali ya Kazi Tu ingawa bado sijafahamu kama Mkuu wa Kaya ni mtani wenu kikabila au kisiasa, naendelea kufanya utafiti kwa kina.

Huu ndio utani wa kisiasa, wanasiasa wana tabia ya kubadilika badilika kama walivyo wananchi wenyewe (No guarantee at all)Ni Utani tu kwa Wajukuu zangu, dont take seriousl

SABABU ZA UGIZA WA AFRIKA- Peter Sarungi

Ptr 1. DINI/IMANI YA WAAFRIKA NI IPI..?

Sababu ya kujiuliza maswali hayo ya juu ni kutokana na udhaifu, udumazi na ufinyu wa fikra zetu sisi watu weusi katika kuendeleza jamii zetu na bara letu. Kuna msemo inasema kuwa “Ukubwa wa matatizo ndio kipimo cha akili” na katika kutafakari kwangu nikakutana na falsafa ya mwimbaji hodari wa Tanzania Marehemu Remy Ongala (R.I.P) Alipoimba kilio cha samaki (Live perfomance). Wimbo wake umeniachia maswali mengi ya kutafuta majibu na kumepanua uwezo wa kufikiri zaidi tena tofauti ili tu nipate majibu.

Swali la kwanza: ni ipi Imani/ Dini ya watu weusi? Kabla ya kupata jibu hilo ni lazima tujue kuwa Imani ni hali ya kuwa na uhakika na vitu/ jambo lisilokuwa bayana yaani kuwa na uhakika na jambo usilolijua uwepo wake. Imani huponya, uhadhibu, huelekeza na hutatua matatizo katika jamii. Jamii ni lazima iwe na imani katika kujibu swali kuu la maisha baada ya kifo au kujibu matatizo yaliyoshindwa kuelezeka ama kutibika. Hivyo jamii nyingi zinataka kufanana katika imani ndani ya bara moja, mfano wazungu wanaamini katika kristo, wachina wana imani yao, wahindi wana imani yao, waarabu wana imani yao, wajamaica wana imani yao, wakorea wana imani yao na hata warusi wana imani yao. Na hizo ni imani zao ambazo hawaku iga kutoka katika jamii zingine bali zilibuniwa na wazee wa kale wa mwanzoni ili kujenga fikra za jamii zao kstika imani waliyoona inawafaa.

Je waafrika tulikuwa na imani ipi? maana imani ya ukristo na uislamu ni imani zilizoletwa kipindi cha ukoloni, ni imani tulizolazimishwa kupokea chini ya ukatili na utumwa wa kikoloni. kila mtu anajua athari za ukoloni, ukoloni ulisababisha tukawa wanyonge katika dunia, tukawa watumwa na wajenzi wa uchumi za wengine katika duni, tukalaani na kuacha mila&desturi na tamaduni zetu, tukapoteza imani zetu, tukadharau sayansi na teknologia zetu, tuacha mafundisho yetu, tukatupa fikra zetu na kununua elimu ya wakoloni, tukaacha majina yetu na kukumbatia majine ya wenzetu na tukaacha mitindo ya maisha yetu tukaegemea mitindi ya wakoloni. Ukoloni ulipoteza dira ya waafrika, ukapandikiza mbegu ya imani ngeni, mbegu ya elimu yao, mbegu ya kuiga kila kitu chao na kukiona ni kizuri, Mbegu ya kujidharau, kujinyenyekeza, kujipendekeza na kujishusha, Mbegu ya kushindwa kufikiri tofauti na mkoloni yaani waafrika tuna amini mkoloni ndio kila kitu hata maandiko ya imani zao zinatuaminisha kuwa wao ni wateule na lugha zao ndizo teule.

Waafrika tuliweza kumfukuza mkoloni na kupata uhuru kutokana na wazee wetu walio pambana kwa njia zote hadi za imani zetu kipindi hicho mfano vita ya majimaji. Pamoja na kumwondoa mkoloni lakini mkoloni aliweza kuacha mbegu zake za Imani, mafundisho na elimu katika lugha yao. Hizi mbegu ndizo ambazo zinasumbua sana kwa mtu mweusi kuwa huru katika kufikiri. Fikra zetu zimewekewa ukomo wa kufikiri katika kutatua matatizo ya jamii zetu. 

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

#MyTake

Waafrika hatupendani kwa sababu ya mbegu ya mkoloni, IQ za kufikiri ni ndogo kwa sababu ya mbegu ya mkoloni, tumekuwa wanafiki na waongo kwa wana nchi kwa sababu ya mbegu ya mkoloni, tumekuwa wabinafsi na wasaliti katika siasa zetu kwa sababu ya mbegu ya mkoloni, tumekosa dira na hata malengo thabiti ya miaka 30 ijayo kwa sababu ya mbegu ya mkoloni.

Tafakari na uchukue hatua

Ruth did not pursue Boaz. Nor did God tell Ruth to pursue him!

TANZANIA INAHITAJI MIFUMO IMARA KULIKO VIONGOZI IMARA- Peter Sarungi

Bara la Africa ni moja kati bara lililo wahi kutawaliwa na viongozi washupavu, majasiri na imara kwa muda mrefu bila mafanikio. Historia imeshuhudia viongozi jasiri na imara kama Mandela, Kwame Nkuruma, Gadafi, Idd Amini, Nyerere, Samwel Doo, Samora, Patrick Lumumba, Mugabe, Kawawa Simba wa vita, Mobutu Seseko, Savimbi, Karume, Kabila sr, Kenyatta sr, Obotte, Kagame, Satta na wengine wengi ambao walitikisa Afrika wakati wa utawala wao na wengine wapo mpaka sasa. Historia inaonesha kuwa watawala hawa walikuwa Imara ingawa wengine walitawala kwa mabavu, vita, mauaji ya alaiki na wengi walitawala nje ya mfumo wa demokrasia kupitia chama kimoja. Pamoja na uimara na ujasiri wa hawa viongozi bado Afrika imeendelea kulia na kuteseka na umasikini, maradhi na ujinga kwa viongozi na wananchi wao, Bado Afrika imeendelea kumwaga damu yao wenyewe kwa wenyewe, Bado Afrika imeendelea kuwa dhaifu kutokana na utengano dhidi ya mataifa ya magharibi na Asia, Bado Afrika imeendelea kuwa tegemezi katika afya, elimu, teknolojia, biashara, uchumi, utawala na mengi ambayo yanatoka nje ya afrika.

Tanzania tumebahatika kupata kiongozi imara, shupavu, jasiri na mwenye msimamo. Kiongozi anayeweza kufanya maamuzi na akasimamia maamuzi yake bila kutetereka hata kama yatakuwa na makosa, kiongozi anayethubutu kupita viongozi watatu waliopita. Huyu ni Dr John Pombe Magufuli (Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), Mimi binafsi namkubali sana Mhe. JPM ingawa ana baadhi ya mapungufu kama binadamu lakini bado ameonesha kuwa yeye ni imara. JPM kwa sasa amekuwa ni gumzo kwa bara letu la Afrika na dunia kwa ujumla. Nimepata kuona taarifa nyingi sana kutoka nchi zingine Afrika na Duniani kuhusu uimara wa JPM na hata mwaka uliopita JPM amekuwa ni Raisi wa Afrika aliyejadiliwa na kupata umaarufu mkubwa kuliko maraisi wengine. Hii ni tunu na sifa nzuri kwa utawala wake.

Pamoja Uimara wa JPM, Bado Tanzania tumendelea kulia kilio cha uchumi duni, afya mbovu, elimu duni, demokrasia na udikteta, uhuru wa kujieleza, upatikanaji wa haki mahakamani, utawala bora, utumiaji wa nguvu na vitisho, wajibu wa bunge na wabunge, uelewa wa haki na wajibu wa raia, uchaguzi huru na wa haki, uzalendo na utaifa. Haya ni mambo yanayo endelea kurudisha nyuma maendelea ya taifa letu kwa kasi kubwa sana.

Hii ina sababishwa na Mifumo mibovu, kandamizi na yenye mianya ya kutenda maovu. Mifumo inatoa nguvu nyingi kwa kiongozi mmoja bila kuwa na njia za kudhibiti akikosea, mifumo inayo elekeza kiongozi kuwa juu ya sheria kwa kauli na matendo, mifumo inayo weza kuyumbishwa mda wowote bila kujali athari, mifumo inayo unganisha chama na serikali kuwa kitu kimoja, Mifumo tegemezi katika taasisi za nchi.

Hii mifumo mibovu ndio chanzo cha wana nchi kuendelea kulia vilia vilivyo zoeleka. Kwa aina ya mifumo hii, hata aje malaika kutoka mbinguni kuja kutawala bila kubadili ni sawa na kutwanga maji ndani ya kinu. Tunaweza kuwa viongozi imara kam JPM hata 50 lakini kwa mifumo yetu bado tutaendelea kuumia kila siku.

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

#MyTake

Bora kuwa na Mifumo imara itakayo weza kulinda maslahi ya nchi na wananchi wake hata kama kiongozi wa mfumo atakuwa legelege, bado mfumo utamnyoosha na kumlinda kuliko kuwa na kiongozi imara ndani ya mifumo dhaifu, maana siku kiongozi imara akibadilika basi nchi itarudi nyuma tena.

Mhe. JPM ni kiongozi Imara lakini mifumo ya serikali na taasisi zake bado zinaonesha udhaifu mkubwa na ndio maana utumbuaji ni mkubwa mno, Yaani kila kiongozi anayeguswa katika taasisi ni kama ameoza kwa rushwa, uzembe, uvivu na mengine mengi.

Tunahitaji mifumo imara kama ya jirani zetu Kenya na Zambia wanaoweza kusimamia matakwa ya wana nchi kisheria bila kutetereka.

Couple we like!

Couple yangu. Best and Hottest couple ya  2016 ; sijutii kuichagua kwani sikufanya makosa! Wanastahili!

The Makondas’! Beautiful couple with amazing souls!

Da Tuma na barafu ya moyo wake! Wamependeza! 

BADILIKA, THIS IS 2017–Daniel Sarungi

 

  • Kipenga kimeshapulizwa wenye mbio zao wameshatoka, wewe bado uko kitandani unaandika happy new year kwenye mitandao ya kijamii
  • Kipenga kimeshapulizwa wewe maliza bajet yote leo kwenye starehe alafu uanze kulalamika eti Mwezi wa kwanza Mgumu utadhani umeubonyeza
  • Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaenda na kasi ya Magufuli, wewe bado unapiga vibomu alafu unalalamika uchumi mbovu
  • Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaenda porini kutafuta pesa na kuja kuzitumia mjini wanaenzi ule msemo wa Mali utaipata shambani /porini wewe unatafuta pesa kati kati ya mji, my friend utapata nauli tu
  • Kipenga kimeshapulizwa wanasiasa wenzako wanaleta matokeo chanya kwenye jamii, wewe umekwama na siasa zako za Maigizo, utaisoma namba vizuri
  • Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatengeneza ajira na kulipa mishahara, wewe umeajiriwa mwaka wa 10 unasubiri bonus, increment na kubagain ongezeko la mshahara alafu bado unataka kuwa celebrity, my friend labda celebrity wa mikopo
  • Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatafuta matatizo ili yawe fursa kwao, wewe ukiona changamoto unakimbia na kuilalamikia serikali, utasubiri sana
  • Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatafuta kazi kwa kufanya kazi za kujitolea kujenga nchi, wewe unasubiri interview, hiyo experience utaipata ndotoni
  • Kipenga kimeshapulizwa wakati wenzako wanahojiwa na forbes magazine wamewezaje kuleta impact Africa nzima, we unakazana kujisifu unafollowers wengi instagram alafu Huna hata mmoja ambae ni rafiki wa kusaidiana.
  • Kipenga kimeshapulizwa wakati wenzako wakipost kwenye mitandao yao ya kijamii wanalipwa, wewe kazi yako ni kuretweet/kurepost na kulike siku nzima bila kupata faida yoyote
  • Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaoipenda nchi yao wanachangia matembezi ya tembo na faru yatakayofanyika Morogoro kwa kununua tshirt, wewe bado unazungusha bia na nyama choma alafu unalalamika watalii wamepungua, unataka waje wakuangalie wewe?

BADILIKA This is 2017 my friend. Sarungi 2017