Happy birthday my brother Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato ! Nakuombea kheri na baraka nyingi sana katika maisha yako na familia yako. Mungu azidi kukuongoza uendelee kuwa baba, mme, na kaka mwema katika jamii inayo kuzunguka.. Zaidi ya hapo ukapate mtumikia yeye! …..Happy birthday kaka!
All posts by Alpha Igogo
Habari nyepesi nyepesi ni kuwa Ivanka Trump ndio ata play the FirstLady role!
Inasemekana ya kwamba Ivanka Trump ndio aka “act” as FirstLady kwenye uongozi wa baba yake. Nimeweka “….” kwasababu haiwezi ikafanywa official kwani kisheria hairuhusiwi lakini hiyo haimaanishi hawezi fanya hivyo. Yani anaweza akawa active kwenye maswala mengi kama mtoto wa Rais napia kwenda kumuwakilisha FirstLady kwenye mikutano yote. Lakini hato lipwa mshahara wala benefits zozote kama FirstLady………….
https://youtu.be/JnzUzf6kHr0
Ivanka alikuwa very active kwenye campaign management team ya baba yake na sasa ni Adviser kwenye transition team ya baba yake ambapo hata kaka zake nao wapo. Vile vile inasadikika kuwa Ivanka Trump takuwa the most powerful First-Daughter in USA history!…….
Wiki hii walikuwa wanatafuta nyumba ya kununua karibu na WhiteHouse hapo DC. Nahilo ndilo linawapa watu imani kuwa nikweli she’s going to “act” as FirstLady sababu kwani Trump wana hotel ya kifahari hapo karibu na WhiteHouse na ina suite (chumba) specific for Ivanka Trump hivyo kama ni kumsalimia baba walikuwa na sehemu ya kulala na hata wangeweza kukaa ndani ya WhiteHouse!….. Inasemekana watoto wakiume ndio watakuwa wakiendelea kuendesha business zao………Anyway, time will tell!
Kitu ambacho sikujua kuwa Ivanka Trump na mme wake ni Wasabato kama mimi ? ? Ivanka alibatizwa kwenye Usabato baada ya kukutana na mumewe. Wakati mumewe ni Msabato wakuzaliwa. ……..You go Ivanka one day I will meet you ?? simnajua baba yangu ni President Dr. Magufuli ??
This wedding!!!! Rayvanny is not a joke!
Shughuli ni watu haswa kama wanajua nini kimewaleta ?? Harusi au shughuli yoyote ile inapendeza sana kama watu wote wanafuraha na kuchangamka namna hii! Sio watu wanakwenda kwenye harusi au shughuli ya mwenzio halafu unaleta nyodo nyingiiii zisizo na mpango si ungekaa kwako oo!!……. Hongereni wenye shughuli mmependeza sana na mmejua kuipendezesha mno! The wedding imenifanya nikumbuke watani zangu ?? Na huyu Ravnnay anakuja juu eeh! Napenda sana ule wimbo wake wa #NatafutaKiki…..
Womanhood!
Please keep voting for our Queen! / Tafadhali endelea kumpigia kura Malkia wetu!
We need you all on board with us!
Asante Mr Kimaro kwa kuwa mmoja wa wanaume wanaopinga hadharani unyanyasaji dhidi ya wanawake! Tunahitaji watu wote wake kwa waume kupiga vita unyanyasaji wowote ule dhidi ya wanawake. Hata hivyo tunahitaji wanaume wengi zaidi kushiriki vita hivi kwani hiyo itatuonyesha kuwa kweli mpo teyari kubadilika na kutulinda! We need you all on board with us!
Hongera sana Rebeca Ngyumi! 2016 African Women Of The Year in Civil Society And Activism!
Hongera sana Rebeca kwa tuzo ulizopata! Wow! Wanawake Watanzania ndio watakao ubadilisha na kuondoa mfumo dume wa unyanyasji wanawake na watoto ndani ya Tanzania na Africa kwa ujumla! Umeonyesha ujasiri mkubwa sana, mfano mzuri mno kwetu sote! “Sina ambacho nitahathirika endapo serikali itasema hii sheria iendelee lakini nafikiri tunajukumu kama wana nchi kuhakikisha tunaweka mifumo mizuri ya sheria ambayo inalinda wana nchi wengine nasiyo tu sisi peke yetu”! Nimependa sana hayo maneno yako! Tatizo kubwa linalo sumbua Bara la Africa ni UBINAFSI! Tuondoe ubinafsi kuwa hilo halinihusu! Sikiliza nikwambie ee mwanamke mwenzangu; kama limemkuta mwanamke au msichana mwenzio basi hilo pia ni LAKO LINAKUHUSU SANA! Kwani laweza kutokea kwako wakati wowote ule au kwa vizazi vyako! Ngoja niseme ule msemo wa Mboni Masimba kuwa “Sauti ya mwanamke ni sauti ya jamii”!! Hivyo ondoa ubinafsi kwa faida ya taifa lako!Kitu ambacho nimeshindwa kuelewa ni kwanini serikali ilikata rufaa?!! Baba yangu Dr. Magufuli hawa waliokata rufaa nao ni #JIPU tu wanahitaji kutumbuliwa kwakweli!!……….. Unajua hizi bangi za ukubwani ni shida sana, mie hapa ninakaribia kugonga 40 na ndoa bado naigopa kama gereza la Keko halafu eti watu wanapinga maamuzi ya Mahakama?! Kha! Natamani niwajue hawa watu, walikuwa Wanaume au Wanawake? Na nini haswa ilikuwa nia yao!
Wanawake kwa pamoja tunaweza badilisha Africa lakini kumbuka kuwa siku zote mabadiliko huanza na wewe!!………Hongera sana Rebeca, well done! Very well deserved!!
R.I.P Leo Mapunda Mwakitalu
Naomba niungane na Watanzania wote waishio Marekani na nyumbani Tanzania katika kuomboleza kifo cha ndugu yetu Leo Mapunda Mwakitalu. Binafsi sikubahatika kumfahamu marehemu wala kumuona lakini pamoja na hayo naomba nitoe pole zangu za dhati kabisa kwa familia ya marehemu, ndugu wote, marafiki, jamaa, na Watanzania wote……….Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote. R.I.P Leo!
Hongera sana Lyne Charles
“Stop telling your big dreams to small-Minded people”-Steve Harvey
https://youtu.be/_5OqUnguixQ
Ushauri umetolewa na Steve Harvey kuwa acha ku-share ndoto zako na watu wenye UFINYU wa mawazo au kwa lugha ya kisasa wanasema watu wenye MAWAZO MGANDO!………. Wanaposema “small-minded” people haina maana kuwa ni watu wenye shida ya pesa au hawana elimu! Hapana! Small-minded people niwale watu ambao hawapendi kuona mwingine anafanikiwa! Niwale watu ambao wana roho za kwanini na yuko tayari kufanya lolote lile ili kumuangusha au kumuumiza mwingine kwasababu tu ya chuki binafsi juu ya maendeleo ya mwingine! Ni watu ambao wanapenda kutoa kasoro kwa mambo ya watu bila ku-offer any solution. Ni watu ambao wanaona mapungufu ya wengine lakini si ya kwao! Ni watu ambao hufurahia anguko la mwingine. Watu wenye elimu lakini hawajaelimika! Hawezi msaidia mtu bila kunyamaza lazima watu wote wajue kuwa alikusaidia………….Kuna watu ambao ni masikini wa pesa lakini tajiri wa roho! Watu kama hawa siku zote wanaamini katika ule msemo usemao WEMA HAUOZI! Kwani kwayeye kutenda wema kwako ndipo Mungu naye atambariki katika mambo yake. Kwahiyo unaweza ukawa hauna pesa lakini una akili na roho kubwa!…,,Stop Telling Your Big Dreams To Small-Minded People!
“Vijana wa sasa hampendani kabisa ni chuki na wivu tu ni hatari sana kwa maendeleo ya society yetu”-Lemutuz
#LeanInTogether: Together Women can
Cheka urefushe maisha!
“She is the Tanzanian Designer of the century-the ExtraOrdinaire Kiki Zimba”-Mwamvita Makamba
Jamani mie mgeni Bongoland sijui pakupata viwalo vizuri wala designer mwenye hadhi ya kimataifa. Sasa Mwamvita Makamba katuhakikishia kuwa hakuna designer kama Kiki Zimba ndiyo mambo yote! Tafadhali mpigie kura ya ndio katika kile kipengele cha The Best Designer of the Yr kwa brand yake ya Kiki Fashion ??
…….let them drown
La Princesa! Leyla Makongoro Bezuidenhout!
La Princesa! Damu ya kwetu hii! Mjukuu wa Chief Makongoro! Kweli kama umelizaliwa kwenye ukoo wa kifalme au ukoo wa ki-chief utaonekana tuu hata kama hukulelewa ndani ya himaya hicho! DNA Don’t Lie!…..Pendeza sana our Princess, that dress a is must have!!…… Girl, we need to make a trip to Butiama to see your grandmother Mama Maria Nyerere and other siblings, please! ??
Ukimwi upo lakini tiba yake hakuna!
Leo ni maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani! Jamani, tunakubali yakwamba UKIMWI ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine lakini tofauti yake ni kuwa UKIMWI HAUNA TIBA NA UNAWEZA KUUEPUKA! Kama unao basi wewe fata masharti ya kula vizuri na kuzuia kuambukiza wengine, kisha mwombe Mungu akupe hekima na amani kwa maisha yako kama wengine kwani wote hapa duniani tunaishi kwa “matumaini” hakuna ajuae atakufa lini, wote sisi ni marehemu watarajiwa!
#UkimwiUpoLakiniTibaYakeHakuna
#Unaepukika
Kama hauna mazuri ya kuangali kwenye maisha yako binafsi ni vigumu sana kuyaona mazuri kwenye maisha ya mwingine!-Lemutuz
You don’t belong at the wedding!
Binasfi nachukulia harusi ni swala personal sana, yani ndugu zako pekee na wale watu ambao kweli wamegusa maisha yako au wenye kukutakia mema siku zote ndio wanatakiwa kuja kwa harusi yako! Harusi ni kitu kina tokea mara moja katika maisha yako (if no divorce) hivyo lazima uifanye iwe na kumbukumbu za watu au marafiki ambao kweli wana umuhimu kwako……….Kama hujaalikwa kaa kwako utulie!Tafadhali hii picha haina huusiano wowote na story hii. She is my niece!