All posts by Alpha Igogo

“Usikubali kutawaliwa akili na binadamu mwingine kwa sababu yoyote ile”- Hoyce Temu

screenshot_2016-10-26-01-57-58-1 screenshot_2016-10-26-01-57-37-1

Picha iliyo nivutia zaidi

screenshot_2016-10-25-23-40-53-1Very true!…….I’m very happy for you Mwaju. Mbarikiwe sana

A measure of a man!

fb_img_1477457094286fb_img_1472436063790Tabia ya mtu utaijua vizuri pale anapo kuwa hana kitu na pale anapokuwa ana pesa! Je binadamu wote kwake ni sawa? Au? ……..Jamani ipo siku nitawasimulia story yangu na experience yangu ya Watanzania hapa Marekani na pia na ndugu ambao hawaoni thamani ya undugu wako kwao mpaka pale wanapoona kuna kitu “kinang’aa” kwako!…….Ee Mungu endelea kumbariki huyu baba!

“Mwili mzuri bila akili ni sawa na gari zuri bila mafuta” – Lemutuz

screenshot_2016-10-25-22-21-00-1

Would you attend your ex’s parents funeral?

screenshot_2016-10-25-22-44-53-1???? Jamani huko Instagram ni kuna vihoja kha! Nimekutana na haya maswali kutoka kwa huyu kaka ambaye ni Muandishi wa vitabu kuhusu maswala ya Relationship. Maswali haya ukiyasoma kwa juu juu bila kutafakari utaishia kucheka tu! Lakini ni maswali ya msingi sana!………. Mie nasema inategemea katika maswali yote mawili! Ninaposema inategemea ni kutokana na sababu kuu mbili:- (1) kama kuna watoto wapo involve na hao watoto ni under age! Nakumbuka nilimpelekaga mwanangu kwenye msiba wa babu yake mzaa baba na shangazi yake kwasababu alikuwa bado yupo under 18 pia babu yake alikuwa ana nipenda sana so do the shangazi….. (2) mahusiano tuliyokuwa nayo huko nyuma yatachangia sana mimi kwenda. Sasa hapo kama hatuna watoto alafu tulizinguana basi nitasema ACHA WAFU WAZIKANE ??  Don’t get mad at me! Someone is “EX” for a reason ??…………. What about you? ……. Soma maoni ya wengine! screenshot_2016-10-25-22-45-20-1screenshot_2016-10-25-22-44-44-1

Please Vote for Dr. Magufuli

screenshot_2016-10-25-22-22-12-1

Haya twende sasa tuka VOTE! Mimi nimesha vote kama inavyo onekana hapo chini ? Na mpaka sasa Dr. John Pombe Magufuli anaongoza kwa 81% ……….haya basi tufanye kazi ya kupiga kura tulete ushindi nyumbani ?img_20161025_231937

Wewe ni mwanaume / mume / baba wa aina gani?

fb_img_1475669607547fb_img_1475895366588Kama wewe ni baba au unategemea kuwa baba basi haya ni maneno ya kutafakari sana. Je mambo unayo yafanya kwa mwanamke uliye naye akitendewa binti yako utajisikiaje?! Kama haufurahii basi huna budi kubadilika! Na hii si tu kwa wale wenye watoto wa kike, hata kama una watoto wa kiume jiulize! Je, ungependa wafate nyayo zako au! Je, unawafundisha na kuwaandaa kuwa wanaume na baba wa aina gani! Badilika sasa!

“TIT FOR TAT” YA LEMA YAWEZA SAIDIA UPINZANI KUWA IMARA? – Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

Andiko langu lililopita nilijaribu kuwatahadharisha Upinzani juu ya kupooza kwao katika siasa za sasa. Niliwakumbusha na kuwa sihii wabadili mbinu na mikakati yao juu ya kuendesha siasa zao na hata kuleta maendeleo kwa wananchi walio wachagua.

Leo nimeona video inayomuonesha G.Lema (MB) mbunge wa Arusha akitoa msimamo juu ya kadhia aliyoipata kutoka kwa Mkuu wake wa mkoa RC M.Gambo akisema:

“kuanzia leo ikitokea kiongozi wa upinzani amedhalilishwa na ikiwa protocal na itifaki za serikali haikufuatwa kwao hata ikiwa ni mbele ya Raisi basi watafanya TIT FOR TAT hapo hapo.”

Kwa maana yangu binafsi nilivyo ielewa kauli hii ni kwamba Mbunge wa Arusha anakuja na mkakati mpya wa kujibu mapigo ya papo kwa papo hata kama itakuwa ni mbele ya Raisi as long itifaki na protocal za serikali hazikufuatwa kwa viongozi wa upinzani kama alikuwa anastahili.

Hasara za mkakati huu..
1. Ikiwa itafanyika hivi mbele ya wageni kama ilivyofanyika Arusha basi huu utakuwa ni Uhuni wa kulaani.
2. Mkakati huu bado hauoneshi nidhamu ya viongozi wetu na inaweza kuwachukiza wananchi ambao ni wastaarabu.
3. Yaweza kusababisha serikali kukwepa kushirikisha viongozi wa upinzani katika hafla mbalimbali kwa hofu ya kutokea vurugu na aibu kwa jamii.

Faida za Mkakati huu.
1. Ikiwa itafanywa kwa ustadi mkubwa na matokeo yakawa ni makubwa kwa jamii basi yaweza kuwa ni moja ya mkakati mzuri wa kuondoa kadhia hii ya kutengwa na kubezwa kwa upinzani. Maana serikali zetu mara nyingi hutatua tatizo baada ya kuona matokeo ya tatizo.
2. Ikiwa itafanywa vizuri basi yaweza kuwa ni “KIK” ya kisiasa na inaweza kuteka vyombo vingi vya habari. ukweli ni kwamba chakula cha mwanasiasa yoyote ni kutoka kwa habari zake nzuri na za harakati kuonesha ana tetea wananchi wake kama serikali ya sasa inavyofanya.

#Mytake.
Ni vizuri kubadilika kila mara ili adui yako asikufahamu vizuri lakini tumia mbinu zenye matokeo makubwa kwa wakati mmoja ili kulinda nyakati zingine. Mbinu hii ni ndogo sana ukilinganisha na tatizo la demokrasia na siasa zilizopo sasa, kuna haja ya kuja na mbinu nyingi zaidi mipya itakayo shitua ulevi wa madaraka mnao ulalamikia. Endeleeni kufikirisha vichwa vyenu maana kuchagua kuwa Mpinzani katika nchi yetu sio raha hata kidogo, Ni Mzigo mkubwa wenye kuhitaji mapambano ya ziada ili kufikia malengo.

asanteni.

Mother and daughter moment

screenshot_2016-10-25-12-13-57-1 fb_img_1472436063790Isn’t that lovely! Too cute to say the least!!…… Sina mpango wala nia ya kuzaa tena mtoto mwingine. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa mtoto wangu mmoja aliyenipa bila kuangaika kama wanawake wengine wanavyo angaika! Nampenda sana mtoto wangu, and always I feel proud to say “she is my only biological child / daughter”!! She’s just PERFECT the way she is (only child)! Nasikiaga na kusoma wanawake wengine wanasema kuwa “he completed me” wakimaanisha WAUME zao. But ma’am! To me is definitely different MY DAUGHTER COMPLETED ME!………Lakini pamoja na kuwa sina mpango wa kuzaa tena haimaanishi siwezi furahiya wanawake wenzangu ambao wapo kwenye ‘parenthood’! Mie sinaga hizo! Furaha ya mtu mwingine naona sawa na furaha yangu! Hivyo sipatagi shida kumsifia mtu au kufurahiya kizuri cha mtu mwingine hata kama anijui!…………. Anyway, napenda sana huu muamko ambao watu wamekuwa nao siku hizi wa kuvaa SARE na watoto zao! Inapendeza sana. screenshot_2016-10-25-12-14-33-1Niliona hiyo picha ya juu kwa Wema Sepetu nika Click link ya Aunt Ezekiel nakukutana na picha zaidi……,…Wamependeza sana. Mungu awabariki siku zote!

Don’t fight the process!

screenshot_2016-10-25-12-06-55-1fb_img_1475439167019Let them fall! Let them go away! Let God control and lead the process and He will let you enjoy your journey and destiny!

Kauli / Maneno yana ishi -Peter Sarungi

Hii ni kauli na maneno ya Mh. JPM alipokuwa anajinadi na kuomba kura kwa wananchi wa Tanzania. fb_img_1477415913995“Nasema kweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu, kwenye serikali yangu hamna mwanafunzi atakaye kosa mkopo eti ashindwe kuendelea na elimu ya chuo kikuu” inaendelea…….. “Hii nchi ni Tajiri kweli kweli, kwenye serikali yangu nita hakikisha kila mwanafunzi ananufaika na mkopo. Haiwezekani nchi kama Tanzania wanafunzi waanze kuandamana kisa mkopo, huyo waziri niliye mteua ajiandae kuondoka”

Naomba kauli na maneno haya yaendane na matendo ya sasa kwa wanafunzi wa vyuo. Lakini kwa utaratibu mpya sasa wa Mikopo kwa wanafunzi, naona kuna walakini katika kutimiza Ahadi ya JPM.

Najaribu kutafakari, tusaidiane kutafakari kwa pamoja kabla ya maafa.

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

asanteni sana.

Kiss cam catches Baraka and Michelle Obama

fb_img_1477318530875

https://m.youtube.com/watch?v=CeDZ4gte3AM

?????????

Never heard! Paul Makonda, you are a man and a half!!!…… Happy 5th Wedding Anniversary Mr and Mrs Makonda

screenshot_2016-10-24-16-19-10-1screenshot_2016-10-24-16-17-34-1screenshot_2016-10-24-16-18-16-1screenshot_2016-10-24-16-18-48-1screenshot_2016-10-24-16-18-37-1fb_img_1472436063790Wow! What a great way to honor your wife!!! I have to admit sijawahi ona mwanaume wa Kitanzania kijana kama Paul Makonda aki shame and curse the devil out of his marriage by empowering and boosting his wife confidence out in the open like this!! SIJAWAHI ONA!! TRULY YOU ARE A MAN AND HALF!!  You spoke from the heart even the devil heard you! You poured your heart like a grown up man, a man with tremendous respect to women and fear of God! BRAVO!!………. Umeonyesha mfano mzuri sana kwa vijana wa leo! Ubarikiwe siku zote. Happy 5th Wedding Anniversary to Paul and Maria Makonda. Mungu awe nanyi milele zote ??

Picha nilizopenda siku ya leo

fb_img_1477240353145-1 Monica muke ya Masanja Mkandamizaji! Kapendeza sana na kipara chake……natural beauty on point??fb_img_1477254539531-1 East West home is best! Mh. ShyRose Bhanji akichuma maembe huko Butiama alipokwenda kwenye sherehe za Nyerere Dayfb_img_1477254324665Huyu dada nimesahau jina lake la kwanza ila nakumbuka last name ni Mwaipaja! Nimeona picha yake huko Facebook nikapenda jinsi alivyo simple na kapendeza pia her skin texture is just amazing!fb_img_1477240421717Teddy Sakaya muke ya Engineer Evans Mashimi pendeza sana in a casual look!Naona mazoezi yanalipa sasa, hongera sana

Keeping Up with Blessing!

img-20161019-wa0006fb_img_1475868161992

Throw that 50/50 stuff out of the window…!!

fb_img_1476361366009fb_img_1477318530875

“UPINZANI TANZANIA UMEPOOZA, BADILISHENI MBINU ZA MAPAMBANO. MSIPO BADILIKA MTAZAA UASI WA NCHI.”-Peter Sarungi

fb_img_1477317177774Nchi yoyote inayofuata utawala na siasa za kidemokrasia ni lazima kuwe na upinzani imara kwa manufaa ya utawala bora kwa nchi. Tanzania ni moja ya nchi yenye siasa za kidemokrasia kupitia vyama vingi. Moja ya Upinzani Imara kuwahi kutokea Tanzania ni pale vyama vinne vya siasa vilivyoamua kujiunga pamoja na kuunda muungano uitwao UKAWA. Ni Ukweli kuwa nguvu kubwa ya UKAWA inatokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na hii imetokana na mbinu nyingi za siasa zilizotumiwa na CHADEMA kwa kipindi cha miaka 10 ya utawala wa Mh. J. Kikwete ambayo iliweza kuimarisha Upinzani nchini. Tulishuhudia mbinu mbalimbali zilizo teka fikra za watanzania pamoja na vyombo vya habari Mfano Operation Sangara iliyofanyika kanda ya ziwa iliyovuna wafuasi kwa wingi kama Sangara anavyovuliwa baharini, Kulikuwepo na vuguvugu la kutaka mabadiliko M4C iliyorindima kwa wananchi kupitia makundi mbalimbali ya vijana, wanavyuo, wafanyakazi, wanawake na kada mabalimbali na matokeo yake tulishuhudia migomo na maandamano ya kudai haki na kutaka kusikilizwa kutoka kwa makundi hayo kama vile migomo ya waalimu nchi nzima, migomo ya wanavyuo, migomo ya wananchi kama kule Mtwara na migomo ya wafanyakazi nchi nzima. Tulishuhudia Sera na kelele za kupambana na Rushwa ziliyoibua madudu mengi yaliyokuwa yakifanywa na watawala pamoja na watumishi wa Umma kama vile Scandal za Richmond, EPA, Meremeta, Tegeta Escrow, IPL, Kagoda na nyingi zilizo ibuliwa na kuiacha Serikali na Chama tawala ikiwa uchi kisiasa na hapo ndipo neno FISADI na Ufisadi lilipopata umaarufu. pamoja na hayo Upinzania uliweza kubadili fikra ya wananchi juu ya rasilimali zao, kufuatilia mapato na matumizi ya Serikali pamoja na kujua Haki za binadamu na haki za kikatiba kama vile Uhuru wa kujieleza, kutoa maoni yako na kusikilizwa. Kwa jitihada hizi za Upinzani Imara tuliweza kuona Serikali ikitoa maelezo ya kujitetea, ikichukua hatua mbalimbali ikiwa ni njia ya kurespond malalamiko ya wananchi. Yote haya yalifanyika kwa sababu ya Upinzani Imara.

Leo tupo katika utawala wa tano, utawala unaojinasibu kwa maneno ya HAPA KAZI TU, Utawala uliojiapiza kutetea wanachi wanyonge walio wengi na walio teseka kwa mda mrefu, Utawala uliojiapiza kupambana na Mafisadi, Utawala uliojiapiza kurudisha nidhamu ya watumishi wa umma juu ya rasilimali za nchi, Utawala usio hitaji siasa wakati wa kazi, Utawala usio taka kugaramia garama za demokrasia kama kuonesha Bunge Live, Utawala unaochukua maamuzi kwa maslahi ya nchi, Utawala uliojiapiza kupita katika njia za ahadi za Raisi na kuzitimiza kama vile kufufua shirika la ndege ATC, Utawala usio hitaji kupelekeshwa wala kujaribiwa, Utawala ulio amua kwenda kinyume na utawala uliopita wa JK yaani utawala ulio amua kufanya mengi yaliyo lalamikiwa na wapinzani wa JK na kutofanya yale mema yaliyofurahiwa na wapinzani wa JK kama vile kulinda na kuheshimu demokrasia.

Kwa zama hizi za JPM, Upinzani unaonekana kupooza sana nchini. Kupooza kwa Upinzani kunatokana na matokeo hasi ya mikakati yao ya kisiasa wanayofanya dhidi ya mikakati ya kisiasa inayofanywa na serikali ya JPM kwa wapinzani. Mikakati inayofanywa na serikali ya JPM ni ya makusudi na yenye ufundi wa hali ya juu na yenye kufuata udhaifu wa sheria zetu zinazotungwa bungeni. JPM amesoma tabia na desturi za wapinzani, amesoma njia zao na mbinu zao, amesoma uwezo wa watu muhimu katika upinzani (key people) na mwisho akasoma udhaifu uliopo katika kila idara ya uendeshaji wa Upinzani. Matokeo yake ni JPM kuja na mbinu tofauti na zile zilizo zoeleka na Upinzani kipindi cha JK, ndio maana ameweza kudhibiti vyanzo vyote vya kuimarisha Upinzani kama vile Bunge, Siasa za majukwaa, Maandamano, Migomo, vyanzo vya mapato, demokrasia katika chaguzi za sasa na mengine mengi yanayoweza kififisha demokrasia na vyama vya Upinzani.

Kwa Bahati mbaya sana, Upinzani bado haujashitukia mchezo unavyochezwa, bado wana mikakati, njia, tabia, desturi na mbinu zilezile na key people walewale waliodumu kwa miaka 10 ya JK. Bado wapinzani hawajabadilika kwa fikra na mienendo, Mfano: Bado wanaamini katika maandamano na migomo, Bado wanaamini katika matamko yasiyo fanyiwa kazi na bado wanaamini katika kususia vikao hata vile muhimu kisa tu wanatendewa ndivyo sivyo. Kwa muundo huu wa Upinzani usiobadilika na kwa mikakati hii JPM kuna uwezekano Upinzani ukafifia na kudorora ifikapo 2020, kuna haja ya Upinzani kubadilika tena haraka ili kutopoteza imani waliyoijenga kwa muda mrefu kwa wananchi.

Kuna hasara kubwa kama upinzani hautabadilika kutoka sasa. Tabia ya kususa vikao mbalimbali halali vya kuwasemea wananchi walio wachagua hauna tija kwa sasa maana una nyima haki ya wananchi kuwakilishwa na mwisho wa siku yanapatikana maamuzi yasiyojali wananchi walio wengi,
mfano: upinzani ulisusia Bunge la katiba na matokeo yake ikapatikana katiba yenye maslahi ya chama kimoja, Wamesusia Bunge la bajeti na matokeo yake ikapatikana bajeti iliyokuwa na mapungufu mengi ya sera za uchumi, wamesusia uchaguzi wa meya wa kinondoni na matokeo yake amepatikana meya kwa kura 18 za ccm. Hii tabia inakera sana na inawagarimu wananchi walio wapigia kura katika mazingira magumu na wengine walipata ulemavu wa kudumu katika kutimiza na kulinda haki zao. Kwanini msipambane kwa njia zote katika kupata haki zenu? kwanini mkimbilie kususa na kutoka nje? kwa nini mnafanya siasa ya maneno badala ya kufanya siasa ya matendo?
Mmeitisha maandamano ya nchi nzima, mmekuja na UKUTA na mwisho mka airisha kwa sababu ya uimara wa JPM.

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

#Mytake
Upinzani ukiendelea kufanya siasa za maneno na kuacha matendo nyuma, Upinzani ukiendelea kung’ang’ania mbinu na mikakati ya kipindi cha JK bila kubadilika, watajikuta wanapandikiza mbegu za chuki, hasira, vurugu na uhasama dhidi ya Serikali na itafika kipindi watazaa WAASI wa nchi watao sababisha Machafuko ya nchi. Upinzani hauna chaguo mbadala zaidi ya kubadili mbinu na miakakati ya siasa zao maana ni kweli bado tunahitaji uimara wa upinzani nchini katika kuleta mabadiliko na maendeleo ya wananchi. Siasa zina Ishi na zitaendelwa kuwepo hata aje malaika kutoka mbinguni kuja kutawala bado siasa itazaa wapinzani kwa hoja na kwa kupingana katika fikra na ndio maana hata katika utawala wa mbinguni bado siasa ilijitokeza na malaika mkuu akahasi na akawa mpinzani mkuu wa Mungu. pamoja na hayo bado Mungu alimpa Shetani Uhuru wa kufanya siasa ili apate wafuasi ingawa Mungu alikuwa na sababu na uwezo wote wa kuangamiza upinzani wa Shetani kwa watu wake.

asanteni.

Job interview part 4: by Hoyce Temu

screenshot_2016-10-22-19-29-59-1screenshot_2016-10-22-19-29-27-1

Cheka urefushe maisha!

fb_img_1477254759825-1fb_img_1472436063790Je umebahatika kuona Ushuhuda wa Masanja katika harakati za kujikwamua na kujiendeleza kiuchumi? Kama bado basi pitia page yake ya Facebook tafuta hubiri lake liendalo kwa jina la “Komaa mpaka kieleweke”! Naamini kama wewe bado upo katika harakati za kufanikisha ndoto zako basi itakusaidia sana !

“I never cared that I was different” – Jackline Mengi!

screenshot_2016-10-22-23-44-26-1screenshot_2016-10-22-23-44-31-1