All posts by Alpha Igogo

Pope Francisco: FAMILY, PLACE OF FORGIVENESS

"FAMILY, PLACE OF FORGIVENESS: 

There is no perfect family. We do not have perfect parents, we are not perfect, we do not marry a perfect person or have perfect children. 
We have complaints from each other. We disappoint each other. So there is no healthy marriage or healthy family without the exercise of forgiveness. 
Forgiveness is vital to our emotional health and spiritual survival. Without forgiveness the family becomes an arena of conflict and a stronghold of hurt.
Without forgiveness, the family becomes ill. Forgiveness is the a sepsis of the soul, the cleansing of the mind and the liberation of the heart.  Whoever does not forgive does not have peace in the soul nor communion with God. Hurt is poison that intoxicates and kills. Keeping heartache in the heart is a self-destructive gesture. It's autophagy. 
Those who do not forgive are physically, emotionally and spiritually ill.

That is why the family must be a place of life, not of death; 
Territory of cure and not of illness; 
Stage of forgiveness and not guilt. 
Forgiveness brings joy where sorrow has produced sadness; 
Healing, where sorrow has caused disease."

            ** by  Pope Francisco **

Family ni msingi wa kila kitu ufanyacho!

 
           Kuna wakati familia huwa inaamua kukutana kwasababu tu wamejisikia kukutana. Saa nyingine mnajikuta wote mmetembelea eneo moja kwa wakati mmoja bila kujua hivyo mnakuwa mmekutana bila kukusudia. Mida mwingine familia inakuwa imekutana kwasababu kuna sababu maalumu ambayo inawalazimu wote kuwepo. Basi ndivyo ilivyokuwa hapa kwa familia ya mama na baba yangu. Walikutana kwa sababu maalum japo kwa leo sitaweza sema ni sababu gani iliyowakutanisha, hivyo wewe endelea kufurahia picha na pia endelea kutembelea blog hii kwani siku si nyingi nitakwambia ni kwanini family hii ya Mzee O.O Igogo iliamua kukutanisha ndugu zao siku ya jana Sunday July 8th, 2018.  Najua nawe utafurahia nami siku hiyo! 

Familia ni kitu ambacho kinathamani kuliko dhahabu na lulu. Ukiona mtu hajali familia yake au anapenda marafiki zaidi ya familia basi jua kunatatizo kubwa kwa akili yake!! Maamuzi ambayo tunafanya kila siku kwenye maisha yetu yanategemea sana tena sana nanfamilia tulizo kulia. Siku zote tupende na kujali familia zetu kwani ni hekalu dogo la Mungu.Hawa ni wadogo zangu wote. Msiwaone hapa wamekuwa wakubwa nimewaogesha na wengine nimewabadilisha nepi ? walikuwa wanaitwa "Bomoa group" yani ukipika "mahanjumati" lazima upike vya nyongeza maana hawafanyagi utani kwenye maakuli ?
 Hawa ni mashosti wa miaka mingi sana wamekuwa kama madada wa tumbo moja.



Mungu ibariki hii familia na familia zote duniani katika jina la Yesu ??

Kesha la asubuhi: Karama ya uponyaji

                  *Kesha la asubuhi*

                         *Juma Tatu* 

                           *9/7/2018*

                  *Karama ya Uponyaji* ?Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa. Yakobo 5:14, 15./em>

?Uwezo wa Kristo wa kukomesha maradhi umedhihirishwa katika siku zilizopita kwa namna ya ajabu. Kabla ya wakati ambapo tulibarikiwa kwa taasisi ambamo ndani yake wagonjwa wanaweza kupata msaada kutoka katika maradhi, kwa matibabu ya uangalifu na maombi ya dhati ya imani kwa Mungu, tulishughulika kwa mafanikio na wagonjwa ambao walionekana kutokuwa na matumaini ya kupona. Leo Bwana anawaalika wanaoteseka kuwa na imani kwake. Hitaji la mwanadamu ni fursa kwa Mungu.

?Akatoka huko, akafika mpaka nchi ya kwao; wanafunzi wake wakamfuata. Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake. Wala hakuweza kufanya mwujiza wo wote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya. Akastaajabu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazunguka-zunguka katika vile vijiji, akifundisha.” (Marko 6:1-6).

?Pamoja na matibabu yetu yote yanayotolewa kwa mgonjwa, maombi sahili ya dhati yanapaswa kutolewa kwa ajili ya baraka ya uponyaji. Tunapaswa kumwelekeza mgonjwa kwa Mwokozi mwenye huruma, na uwezo wake wa kusamehe na kuponya. Kupitia katika majaliwa yake ya neema wanaweza kurejeshwa. Waelekeze wanaoumia kwa Mtetezi wao aliye katika nyua za mbinguni. Waambie kwamba Kristo ataponya wagonjwa, iwapo watatubu na kuacha kuzihalifu sheria za Mungu. Yupo Mwokozi ambaye atajidhihirisha mwenyewe katika vituo vyetu vya tiba ili kuwaokoa wale ambao watajisalimisha kwake. Wale wanye maumivu wanaweza kuungana nanyi katika maombi, huku wakikiri dhambi zao, na kupokea msamaha.-Manuscript Releases, vol. 8, uk. 267, 268.

Mr and Mrs Abayo wedding

Harusi ilifungwa siku ya Jumapili July 1st, 2018 katika kanisa la Houston International S.D.A…. bibi harusi alisindikizwa  na kukabidhiwa kwa Bwana harusi na kaka yake (mdogo wake) aitwaye Robert.  Mchungaji aliye fungisha ndoa alikuwa mtumishi wa Mungu Pastor Caleb Migombo kutoka North Carolina.  Maharusi wakitoka kanisani baada ya kuunganishwa kuwa mwili mmoja. Tunawaombea kheri katika safari yao hii.

MUngu awatangulie katika yote, hongereni sana ??

Bibi harusi mtarajiwa na wageni wake!

Mrembo wetu mgeni wetu wa heshima akiwa na muheshimiwa mpambe wake! Wamependezaje sasa, simple hakuna madoido mengi ?? embracing their natural beauty ?❤

 Mimi mwenyewe simmeniona aaa! Ningekosaje ukodak moment na bibi harusi, kuna mibaraka kupiga picha na bibi harusi ati ?? Msije mkaanza kuwaganda maharusi kupiga picha lol! 

    Hii sherehe ilikuwa ya kipekee sana, simnaona watu wamefunga Khanga na wengine wamebeba, basi kila mtu alipewa zawadi ya khanga na mwiko wa kupikia  all the way from Bongoland ? wewe ulishawahi kwenda kwenye sherehe halafu ukapewa zawadi za huwakika kama hizi? Rachel siyo mtu wa spoti spoti ati ???
 
          

Mtarajiwa wetu katika pozi!

 Jumapili ndio siku yake kuu, hivyo naomba nitumie siku hizi mbili kwa ajili yake ?? Huyu ni dada yangu bwana na furaha sana kwa ajili yake. Yani nyie siku nikifunga harusi yani ni miezi mitatu picha zangu tuu ?? mtakomaje sasa ??
 Akikata keki iliyotenezwa kiumaridadi kabisa
Tulimpa zawadi chache lakini zauwakika! Ni zawadi ambazo atakuwa anatumia mara nyingi, ubora na viwango vilizingatiwa sana, siyo mambo ya buy one get one free hapana ? chezea sisi ?

Mwenyezi Mungu amuweke salama Jumapili tushuhudie akiapa kiapo kitakatifu mbele zake Mungu nasi wengine tukiwa mashahidi wa hapa duniani! ??

Wema Sepetu: Alafu sasa bado kuna wabishi watabisha

Regrann from @wemasepetu – Ninapokuita Mtetezi wa wanyonge Ninakuaga na Uhakika wa asilimia zoooooote… Alafu sasa bado kuna wabishi watabisha… Jamani eeh nasema hivi, “Kuna kufanya na Kuna kuthubutu…” Nini huwa kinaanza kati ya hayo mawili…??? Tunaanzaga kwa Kuthubutu alafu ndo tunafanya…… Kaka angu hapo juu, (sina haja ya kumtambulisha) alipothubutu kuliingilia swala zima la janga la kuuziwa makazi na malazi ya watu mbali mbali tena na mahakama wengi wenu mlimbeza na kurusha maneno ya kila aina… Oooh anakurupuka, oooh hana mamlaka, oooh HATOWEZA… Oooh Tutaona… Nadhani leo hii mmeinamisha vichwa chini kwa aibu… Na mimi nasema Aluta Continua… The Saga Continues.  Mwenyewe anasemaga kitu kimoja… Ametumwa kutetea wanyonge… Sio Mungu yeye wala Malaika kusema kwamba atafanya kila kitu Perfectly… Ila kwenye ukweli pasemwe ukweli… We are Blessed to have you as Our RC… Iko siku wataelewa tu… Na watakuwa wameshaelewa sema si unajua UBISHI ndo jadi yetu… Sana sana sisi Wana Mkoa wako… Umesaidia wengi sana na unazidi kuendelea kufanya hivyo kila iitwayo leo… Mungu anazidi kukupigania Mtumishi wake… Akupe Uhai mrefu… Uzidi kuona Juhudi na Uthubutu wako ukizaa matunda.Wana Dar tunakupenda sana… Mungu Ibariki Tanzania..

Mungu Ibariki Africa..

Mungu Mbariki RC Wangu..

Mungu Mbariki Rais Wangu…

Viva RC Viva…

@paulmakonda @paulmakonda @paulmakonda @paulmakonda

#IkikuchomaImeruhusiwa…??? – #regrann

Matukio katika picha: Rachel’s bridal shower

 Zifuatazo ni picha za sherehe ndogo ambayo bibi harusi mtarajiwa Rachel alifanyia na marafiki zake wa karibu pamoja na baadhi ya ndugu zake kama siju yao ya kufurahi pamoja kabla hajala kiapo kitakatifu ambacho siyo tu kitabadilisha cheong chake to Miss to Mrs bali hata majukumu yake pia yatabadilika. Lakini yote ni kwa utukufu wa Bwana. Shere hii ilifanyika nyumbani kwa rafiki yake Rachel aitwaye Mary (kulia), huko Manvel, Texas. Rachel na Mary wamekuwa marafiki kwa zaidi ya miaka 20, tangu wakiwa Secondary Jangwani, wakanda wote college, wakaishi wote Wichita, Kansas,  na mpaka leo hii wako hapa wote katika state ya Texas.  Hivyo kutokana na urafiki wao huo ambao umedumu zaidi ya miaka 20, nanupendo wao ukiwa imara kabisa bibi harusi ameona ni vyema akawa ndio msimamizi wake mkuu katika harusi yake (Maid of honor)  Picha ni nzuri na nyingi sana, hivyo nawaleta bila kuwa kwenye mpangilio maalumu. Bado             

https://youtu.be/O5-LlA9BnUA

Hapo ? Rachel akitambulisha wageni na wenyeji wake. Bibi harusi aliona anajukumu la kutoa utamvulisho kwani watu wote waliofika hapo wamegusa maisha yake kwa njia moja ama nyingine.

mmmh! Mahanjumati! Wadada walipika  (nimesema walipika eeh ??) vikapikika haswa watu tukala mpaka vikasaza! Hii ni sehemu ya kwanza picha zipo nyingi nitawaletea zingine baadaye ??

Reginald Mengi: I can, I must, I will

Regrann from @lemutuz_superbrand - Dk @regmengi akupa maisha yake katika kitabu

UNAWEZA kuwa na maswali mengi kuhusu Mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Dk. Reginald Mengi,alivyoweza kufikia nafasi aliyonayo kwa sasa akimiliki makampuni kadhaa na mengine kuwa na hisa hapa nchini na ughaibuni.

Majibu ya maswali hayo na maelezo mengine yatapatikana katika kitabu chake cha kumbukumbu kuelekea utajiri ambacho kitazinduliwa Juni 30 mwaka huu.

Kitabu hicho chenye taarifa muhimu kwanza za kumfahamu Mengi ni nani kisha safari yake ndefu kufikia ustawi alionao leo akiwa na makampuni yaliyotawanyika nchini na katika nchi za majirani na mataifa tajiri duniani lakini kubwa linakupa kanuni za kufikia na kumpita pale alipofikia yeye. Usikose kitabu hiki “I Can, I Will, I Must…The Spirit of Success” (Naweza, Nitaweza, Nitafanya na Moyo wa Mafanikio)

Dk Reginald Mengi Juni 30 anazindua kitabu chenye kujaa maarifa na taarifa. Kitabu hiki kimepongezwa na wanazuoni wastaafu wa Chuo Kikuu Cha Harvard, Profess Daniel Isenberg na Profesa Sujata Bhatia kutokana na kuelezea kwa ufasaha na kiufundi mifumo ya kiuchumi na kisiasa nchini kwa miongo minne iliyopita ilivyoweza kuathiri jitihada za ujasiriamali nchini Tanzania na kuelezea nini kinahitajika katika kutafuta mafanikio.

Unaweza pia kupata updates zaidi kuelekea uzinduzi wa kitabu chake kupitia akaunti yake ya twitter @regmengi
8 days to I CAN,I MUST,I WILL book launch #iCaniMustiWill #RegMengi ‭ - #regrann

Kamwe usibishane na pepo!

Wapendwa wasomaji wangu, za siku mbili tatu ? Haya leo ngoja niongee kidogo kuhusu pepo au mapepo. Unajua humu kwenye mitandao au hata kwenye maisha yetu tumezungukwa na mapepo wachafu. Hao au hili pepo anaweza akawa ndugu, rafiki, mfanyakazi wako, au mtu baki kabisa ambaye hana undugu wala ujamaa na wewe. 

Utakuta hili pepo kazi yake ni kuchukizwa na wengine wakiwa na furaha. Yani akiona watu wengine wana amani hata kama ni masikini kuliko yeye basi yeye roho yake inatahabika sana! Kinachofuata nikutafuta kila njia ya kufanya ile amani au furaha uliyonayo itoweke! Kama ni familia inafuraha basi atatafuta kila njia ya kuondoa furaha kwenye hiyo familia. Atagombanisha watu hata kwa kutumia watu wengine ili yeye asijulikane! Hapendi kuona watu wanaishi kwa amani na furaha kugombanisha watu ndio furaha yake yeye!

Sasa hata humu kwenye mitandao yapo haya mapepo! Kwa sisi Wakristo, Bible inatuambia "utawajua kwa matendo yao"! Yani ukiona mtu kutwa yeye nikugombanisha watu kwenye hii mitandao, kutwa kutukana watu kwakutumia sababu yoyote ile, amekalia kuvuruga familia za watu kwasababu wanafuraha? Yani muongo na umbea ndio maisha yake; mpendwa, basi jua huyo ni PEPO! Kamwe! Nasema tena Kamwe! usijibishane na Pepo! Pepo unalikemea kwa Jina la Yesu! Ukijibishana na pepo atakuambukiza mapepo yake! Hivyo njia nzuri ya kulishinda pepo ni kulikemea likafie mbali huko, hakuna jina ambalo pepo linaogopa kama jina la Mungu. Wewe kemea usimpe nafasi ya kukusogelea!

Huwa napendaga sana huu wimbo wa Rose Muhando "Nipishe nipite" haswa kwenye chorus. Huu wimbo unamkemea pepo au kwa jina lingine shetani. Huu ni mfano mzuri kabisa, kuwa pepo unalipa 'amri' nasio kuongea nalo! 

"Wewe ulimwasi Mungu, nipishe nipite 

Uliwadanganya Adamu na Eva, songea nipite 

Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako 

 wewe shetani mlaaniwa, mwenyeji wa kuzimu 

Sasa nipishe nipite "Wapendwa tukemee mapepo yanayotuzunguka na kutufata fata kwa nguvu usicheke wala kulemba lemba maneno kwa pepo! Mpe amri, mwambie wewe  ulimwasi Mungu songea nipite, wewe shetani mlaaniwa mwenyeji wa kuzimu nasema sasa sogea nipite katika jina la Yesu! 

*** Kama humjui huyo kwenye picha ni mdogo wangu kipenzi Jokate Mwegelo. Missing you, love you dearly****

https://youtu.be/92aWCMy0c2k

Happy Father’s Day King Kiba!

Wow! Wamenoga eeh! Happy Father’s Day the real King,  Mfalme Ali Kiba! Mungu akujalie busara na hekima nyingi ya jinsi ya kuwa baba bora na mwema. Akutunzie wanao, wakuwe kwa kimo na hekima. Ubarikiwe sana. Watoto wako wazurije sasa! ? ? Happy Father’s Day King!

Monalisa kaua, kamaliza kabisa!

  Regrann from @monalisatz  -  Happy fathers day kwa mibaba yote iliyotelekeza wanawake wajawazito,wakatelekeza na watoto wao au kuwakana kabisa watoto wao kwa sababu wanazozijua wao,siku ya Leo iwakumbushe kwamba wao ni viumbe wajinga kuliko yeyote yule kwenye dunia hii Hata yule Nguruwe aliyetabiri Nigeria kufika nusu fainali za World Cup ana akili kuliko wao.Siku ya Leo kila watakachokula wakaharishe mfyuuu.Watakachoongea wawe wanakohoa kohoa tu ovyo wajinga kabisa nyie...hamuoni haya siku ya Leo wababa wenzenu wako so proud na watoto wao,nyie mmetumbua mimacho tu na wengine MNA vitambi kama wajawazito. Haya Happy father's day kwenu wehu nyie  - #regrann

Faraja Nyalandu: Nikifeli au nikiharibu shuleni hakuongea na mimi kwa ukali, aliongea na mimi kwa uchungu

Regrann from @farajanyalandu  -  Baba yangu alikuwa ni rafiki yangu. Mimi ni wale wanaoitwa daddy's girl. Ukilelewa huku una dhana ya kupenda na kupendwa inakujengea imani na ujasiri kwasababu unakua ukijua unastahili kutoa na kupokea. Una thamani. Unastahili. Nikifeli au nikiharibu shuleni hakuongea na mimi kwa ukali, aliongea na mimi kwa uchungu. Ilikuwa ni balance nzuri kwasababu nikikosea mama yangu aliongea kwa ukali. Kuna siku nilimpa report ya shule, baada ya kuizingatia kwa muda akisikitika, akaniambia anaomba report yangu. Kimoyo moyo nikasema uzee unamjia vibaya, ananiombaje report yangu wakati kaishika mkononi. Akaniambia anajua uwezo nilionao na ile report mbaya haiwezi kuwa yangu. Ni ule uchungu ulioniuma na kunifanya nisitake kumuumiza tena baba yangu. Hakuwahi kunichapa. Lakini nimekula sana vibao na mwiko wa kupikia kwa mama. Hofu pia ilinirudisha kwenye mstari. Nilitambua nikipewa haki inakuja na wajibu ninaotarajiwa kutimiza. Alinijengea nafasi ya kumwambia kila kitu, kizuri na kibaya. Na yeye aliniambia vingi, alivyokosea na alivyopatia, alivyoona vikipatiwa na kukosewa. Aliniambia yeye si mkamilifu na wala mimi si mkamilifu lakini natosha. Katika vyote alivyonipa, namshukuru kwa kuniwezesha kujiamini, kujitambua na kutaka kuwa bora. Hivi vitu haviuzwi dukani. Sina hakika kuna shule itavifundisha ipasavyo. Pengine hizi #weekendwisdom ni matokeo ya uhusiano wetu. Mwambie binti yako anatosha, jenga msingi imara asitokee mtu mwingine kumuaminisha vinginevyo. 

Happy Father's Day Fathers!  - #regrann

Happy Father’s Day to this great father and grandfather to our children!

   Hatuna la kusema zaidi ya Asante kwako na asante kwa Mungu Baba aliyekuchagua wewe kuwa baba yetu na babu wa watoto zetu! Unaweza usionekana kama baba bora mbele ya macho ya watu wengine, hiyo ni sawa tu kwani hata aliyekuumba anajua hakuna aliyekamilika lakini siku zote fahamu ukamili kwetu sisi watoto zako na wajukuu zako! God created you perfect for us! Thus why you are our father not theirs!  For that we are greatly appreciate and love you..... Happy Father's Day my baba! ❤ 

Happy Father’s Day baba Cookie!

Regrann from @auntyezekiel  -  Kabla ya kufanya Maamuzi ya kuwa na Mtoto niliwaza sana Mwanaume wa kuzaa nae Mana nilikuwa na hofu na kuogopa hasa ukiona Mababa au malalamiko ya wamama wakilalamika  wanayofanyiwa na wababa sikuogopa kukosa matumizi Hapana sikuogopa kukosa kusomeshewa mtoto hapa mana yote hayo niliamini naweza kupambana na nikayamudu....Nilichoogopa kupata baba asiyejua Umuhimu au majukumu yake kwa mtoto huyo na hata akakosa Upendo na Muda na Mtoto tutakayekuwa nae .... Hakuna kitu Nafurahi kama kuona Mwanangu akipata Upendo kutoka sehemu anayopenda Nashukuru Mungu alinipa Ww kama Baba wa Mtoto wang Mana umekuwa na Mapenzi ndani ya Familia hii na Mtoto wako zaidi ya yale niliyoyawaza jua hiyo ni bahati tuu hiyo ndio Maana ya Baba bora na Sio bora Baba Siwezi kumaliza bwana .....HAPPY FATHER'S DAY BABA COOKIE WW NI BABA BORA .....@moseiyobo  - #regrann

Happy Father’s Day the Bosslady and all single Mothers out there!

Regrann from @zarithebosslady – Happy father’s day to me, the late Don and all the women playing both roles. We are the real MVPs….. gone but you still here for us in all possible ways. We miss you! – #regrann

 May I extend my sincere wishes to all single mothers around the world, Happy Father’s Day to you single mothers!  Have been there, done it! #SingleMom So I truly understand what Zari is saying.  Some people love to be called “Father” but have no clue what it takes to raise a child! One needs to nurture that child to grow spiritually, emotionally, physically, and financially! 100% provider, 100% supporter, 100% gurdian, 100% protector of  your children if you want to be called Father!! When you plant a seed somewhere you need to take care of  it to grow, you need to nurture it! Sio unapandikiza mbegu halafu unakuja kuitizama baada ya miezi mitano, kwani nani ni “shamba boy” wako umemuacha akutunzie???!  These are human being need their father to father them!! Children are not toys don’t use them for show-off !! Happy Father’s Day to all single mothers and all single Fathers in this world! You rock!

Happy Father’s Day to you great father out there!

Happy Father's Day to all great fathers out there who've been taking their responsibilities with a sense of pride and warm smile! God bless you abundantly! For those who are longing to be called "papa" just keep on praying your time is so never,  our God is faithful, full of mercy and grace, He always answer  prayers beyond our imaginations!Nawatakieni furaha na baraka ya siku ya wakina baba duniani kote kwa wababa wote wanaotimiza majukumu yao kwa furaha na ufahari mkubwa bila "kushurutishwa" na RC Paul Makonda! Kwa wale ambao wanatamani kuitwa baba lakini bado  hamu hiyo Mungu ajakutolea basi wewe endelea kuomba bila kukata tamaa zamu yako inakuja kwani Mungu wetu ni muaminifu, mwenye wingi wa rehema na neema hujibu maombi azidi ya tuombavyo!

Happy Father’s Day to you all ❤

Wanaopenda kushangaa ndio wajanja!

Baadhi ya watu haswa sisi Watanzania huwa tunatabia yakutokupenda kuwa wadadisi wa jambo au mambo matokeo yake our ignorance is very High! 
Yani tupo radhi tuamini katika uongo au majungu / umbea kuliko kuchukua muda wako na kukisoma / chunguza kitu wewe mwenyewe ili uwe na huwakika wa kile unachokiongea. Utakuta mtu anahadithia kitu wewe utaamini ni kweli ameiona mwenyewe kwa macho yake au amesikia yeye mwenyewe kwa masikio yake kumbe naye kasimuliwa na rafiki yake ambaye nae huyo rafiki kasimuliwa na mtu mwingine ?‍♂️?‍♂️
Hiii no karai ya Chicago
Hii tabia kutopenda kuchukua muda wetu na kujifunza jambo fulani au kufatilia habari fulani bila ya wewe kuweka uongo wowote ndio imefanya Watanzania wengi wanapenda majungu sana, wanaamini ili uweze fanikiwa basi lazima umuharibie mwingine haswa kama yupo kwenye biashara au jambo ambalo na wewe unafanya! Inasikitisha sana kwani kwa hii tabia maendeleo ya taifa letu yatahitaji dictator!!  Juzi niliamua kwenda kuangalia hili 'karai' kubwa ambalo limeletwa hapa Houston, Texas kwenye chuo cha sanaa. Hili karai limetengenezwa Ulaya likaletwa hapa. Ni urembo wa aina unao vutia sana.  Katika mji wa Chicago nao wanao 'karai' kama hili limetengenezwa na mtu mmoja. Ila la Chikago limeinamishwa (kama inavyo onekana kwenye picha ya pili kutoka juu) hivyo watu wanaweza ingia katikati ya hili 'karai' nakupiga picha nzuri sana kama anavyoonekana mwanangu hapo pichani ☝ na pia tizama picha ya mama yangu na mdogo wangu hapo chini ?
Hizo picha zilipigwa miaka 6 iliyopita kwenye hilo karai la Chicago. Kwa maoni yangu binafsi mimi napenda ya Chicago zaidi kwani imewekwa vizuri kwa watu kupiga picha na kitendo cha kulazwa chini imefanya hiyo sehemu iliyoingia ndani kuwa sehemu ya kivutionzaidi cha kupigia picha. Halafu maua na urembo ulioko pembezoni unahakisiwa na hiyo karai ambayo pia nikivutio.
Nilichotaka kuwaambia Watanzania wenzangu ni kuwa usiogope kushangaa! Hakuna njia nzuri ya kujifunza kitu kama kushangaa. Tena ukimpata mtu anayekupa maelezo basi wewe zidisha kushangaa ili akupe maelezo zaidi. Wanaopenda kushangaa ndio wajanja!

Kesha la asubuhi: Hata watoto wanaweza kushuhudia imani yao

                  *KESHA LA ASUBUHI*

                           JUMATANO

                           13/06/2018

          _HATA WATOTO WANAWEZA

            KUSHUHUDIA *IMANI* YAO._? *“Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Walikasirika, wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa?” (Mathayo 21:15, 16).*

✍?Bendera ya neno la kweli inaweza kuinuliwa na wanaume na wanawake wanyenyekevu; na vijana, na hata watoto, wanaweza kuwa baraka kwa wengine, kwa kudhihirisha kile ambacho kweli hiyo imewafanyia.

✍? Mungu atawatumia mawakala dhaifu zaidi ikiwa wamejisalimisha kikamilifu Kwake. Anaweza kutenda kazi kupitia wao ili kuzifikia roho ambazo mchungaji asingeweza kuzifikia. Kuna njia kuu na vichochoro vinavyopaswa kuchunguzwa. Mkiwa na Biblia yenu mkononi mwenu, moyo wenu ukichangamka na kung’aa kwa upendo wa Mungu, mnaweza kuondoka kwenda kuwaambia wengine uzoefu wenu;

✍? mnaweza kuwajulisha kweli ambayo imeugusa moyo wenu, mkiomba kwa imani kwamba afanye jitihada zenu ziwe na mafanikio katika wokovu wao. Wasilisha nuru, nanyi mtapata nuru zaidi ili kuwasilisha. Kwa namna hiyo mnaweza kuwa watendakazi pamoja na Mungu.

✍?Mungu anatamani kwamba watoto Wake watumie juhudi zao zote, kwamba katika kutenda kazi ili kuwabariki wengine, waweze kuimarika katika nguvu ya Yesu. Mnaweza msiwe na elimu; mnaweza msifikiriwe kuwa na uwezo wa kumfanyia Mungu kazi kubwa; lakini yapo mambo mnayoweza kufanya. Mnaweza kuifanya nuru yenu iwaangazie wengine.

??‍♂```Kila mmoja anaweza kupata ufahamu wa neno la kweli, na kuwa na mvuto mwema. Hivyo nendeni mkafanye kazi, ndugu na dada zangu. Jipatieni uzoefu kwa kufanya kazi kwa ajili ya wengine. 

??‍♂Mnaweza kufanya makosa; lakini hili haliwezi kuzidi kile ambacho wale wenye maarifa zaidi, na wale walioko katika nyadhaifa za mamlaka, wamefanya tena na tena. Hamtapata mafanikio wakati wote; lakini hamwezi kamwe kujua matokeo ya juhudi duni, isiyotafuta manufaa binafsi ili kuwasaidia wale waliomo gizani. 

??‍♂Kupitia utendaji wa Roho Mtakatifu, mnaweza kuongoa roho kutoka gizani kuja kwenye kweli, na kwa kufanya hivyo roho zenu wenyewe zitajawa upendo wa Mungu.```

*MUNGU AWE NANYI MNAPOTAFAKARI*

Happy birthday Mrs Mapigano Peter

"Women are many, but wifely women are not only few, but they are very rare. Actually, true wives are gotten from God, im not hesitant to declare you are wife from God. Your blessings are innumerous to me since we got wedded. I cant mention all, among them being the peace i enjoy being with you, the beautiful kids you gave me, the great care you manifested to both live and stay with my great mummy something that few women could do.I pray that God gives us a gift to inherit the kingdom of heaven together with our beautiful kids. That when God comes the 2nd time, we together meet the Lord in the granduer of heaven and in surpassed glory of our Lord Jesus Christ. HAPPY BIRTHDAY MY DEAR GREAT WIFE! Amen. Salome Achayo" ~~~ from caring husband Mapigano Peter

Happy birthday Mrs Mapigano, Mungu wa rehema akuzidishie baraka zake katika kila utendalo na utamanialo. Uzidi kuwa baraka sio tu kwa mumeo na familia yenu bali kwa kila mtu aingiaye ndani ya malango yako na popote pale upitapo. Happy birthday Salome!.... Napenda sana nikiona kama zangu wakimimina hisia zao kwa wake zao kwa upendo na furaha kama hivi mbele ya jamii. Inaonyesha mwanaume anaye jitambua, kujiamini, kujali, na kumpenda mkeo bila kuogopa. Nashindwaga kuelewa wale waliokula viapo vya ndoa mbele ya kadamnasi lakini hutakaa umsikie hata siku moja akimsifu au kumshukuru mkewe mbele za watu! ?? Mwanaume wa kweli lazima amsifu na kumshukuru mkewe in public and in private! Lasivyo kunashetani ananyemelea ndoa yenu ?