Wapendwa wangu Sina cha Kuwalipa Zaidi ya kusema ASANTENI sana kwa 4M followers.
Ninyi Ni Ma Ndugu kwangu, Mmekua Nami Bega Kwa Bega Kwenye Shida na Raha. Sasa Mnichiangieni $1 kila mtu tujenge clinic ya wanawake sehemu yoyote dar, Najua tukiipata Baba Magufuli atatupa kiwanja....?? #JustSaying
PENDA SANA NYINYI.❤
THANK YOU SO MUCH FOR 4M.
LOVE YOU ALL? - #regrann
Yes! That's my lady! Let support our Bosslady, the real Major General! Mimi naanza kwa dola kumi ($10 ), haya baba yangu Dr John Pombe Magufuli tunaomba kiwanja hicho tena kiwe kule maeneo ya Kigamboni, au Kibada, au Mbagala ?? somewhere in Temeke District au Kigamboni please. Zari fungua hizo account watu waanze kumimina hizo pesa please! This is great! And we will call it Zarina Hassan Women Clinic ???? Jamani ni dola moja tu ($1) kwa kila mtu hatushindwi! Ila unaruhusiwa kuchangia zaidi ya hapo! Okowa maisha ya mwanamke uokoe jamii!! Mungu atubariki wote ?
Mimi naheshimu sana kitu cha mtu yoyote yule! Yani mtu akiniazima kitu au kunipa kitu huwa nakitunza zaidi ya chakwangu! Naonaga mpaka mtu kutoa kitu chake kakupa au kukuazima inamaana sio tu amekuheshimu bali anakuamini! Trust is essential to me! Nina picha nilipewa na wanafunzi wenzangu Kowak Girls secondary school hizo picha mpaka leo ninazo hapa Marekani, sidhani hata kama wao wanakumbuka! Hivyo ndivyo nilivyo mimi! Na huwa nachukizwa sana nikiona mtu haeshimu kitu cha mtu mwingine kwani inaonyesha wewe unaweza kuwa na vielement vya tabia za kichawi chawi ???
Sasa jana jioni nilikuwa natafuta kitu kwenye closet (ambapo kuna washer and dryer sio kwenye nguo) nikakutana na hii GPS! Yes that how GPS monitors used to be ?? Wahenga mtatujua tu! ? ?Hii GPS niliazima kutoka kwa my good friend aitwae Sammy mwaka 2009. Alikuwa akihiitaji nampelekea nami ikitokea nahitaji naifata au ananiletea. Mwishowe ikaishia kwangu. Kusahau na mambo kuwa mengi sikufanikiwa kumrudishia.
Lakini kwakuwa nilijua niliazima sikupewa moja kwa moja miaka yote nimejisikia kuwa na wajibu wa kuitunza mpaka hapo nitakapo mpa tena. Believe me, nilipokuwa nahama Michigan to Texas, niliipaki vizuri nikaja nayo ?? nimeihifadhi vizuri sana mpaka stand yake ipo ? nafikiri it’s about time kumrudishia mwenye GPS yake akitaka kuitupa aitupe mwenyewe! Sindioo au niendelee kumtunzia kama yeye alivyokua akinitunzia vya kwangu ???? #HeshimuVyawatuZaidiYaChako
Regrann from @zarithebosslady - World's greatest ignorance 'ASSUME' ASS/U/ME assuming makes you and me an ass. ..... let's stop ASSUMING things!!!!! With assuming comes, judging, untruthful accusation and all sorts of things. If you have a functional brain, read through the lines! #Unapologetic - #regrann
Lazima uwe na IQ ya A+ kuelewa huu ujumbe lasivyo utabidi uhisi hisi vitu usivyo vijua undani wake. Kuhisi ni chanzo cha dhambi nyingi! Ndio maana wanasema kuwa HISIA sio kitu cha kuchezea! Mtu anaweza akahisi kuwa wewe ni muhuni na akaweka akilini kabisa kuwa fulani muhuni. Hiyo inamaana wamesha kuhukumu kuwa wewe ni muhuni pasipo na uwakika wa akihisicho!! Mbaya zaidi nipale atakapo anza kuhisisha wengine kuwa wewe ni muhuni #majungu na wao kuamini hisia za uongo! Matokeo yake unajikuta mnahukumu na hata kusababisha kifo cha mtu kwa Kuhisi!! Mungu atusaidie hasa sisi Watanzania tuachane na dhambi ya kuhisi hisi mambo kwani hii dhambi inaitafuna taifa!!
#World's greatest ignorance 'ASSUME'
KESHA LA ASUBUHI
ALHAMISI- JUNE 07, 2018
WATENDAKAZI PAMOJA NA MUNGU“Maana sisi tu wafanyakazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.” (1 Wakorintho 3:9).
▶Lazima Roho Mtakatifu awe wakala hai wa kusadikisha juu ya dhambi. Wakala huyu wa kiungu humwasilishia mzungumzaji manufaa ya kafara iliyotolewa msalabani; na kadiri neno hili la kweli linapofikishwa kwa roho zilizopo, Kristo hujitwalia, na hutenda kazi ili kubadilisha tabia yao. Yuko tayari kusaidia udhaifu wetu, kutufundisha, kutuongoza, na kutuhamasisha kwa mawazo yenye asili ya mbinguni.
▶Ni kidogo jinsi gani wawezavyo kufanya wanadamu katika kazi ya kuokoa roho, na hata hivyo ni kubwa kiasi gani wanaweza kufanya kupitia Kristo, endapo wakijazwa Roho Wake! Mwalimu mwanadamu hawezi kusoma mioyo ya wasikilizaji wake; lakini Yesu hukirimu neema ambayo kila roho huhitaji. Yeye hufahamu vipaji vya mwanadamu, udhaifu na uimara wake.
▶Bwana anatenda kazi ndani ya moyo wa mwanadamu; na mchungaji anaweza kuwa harufu ya mauti iletayo mauti kwa roho zinazoyasikiliza maneno yake, akiwageuzia mbali na Kristo; au, kama amejiweka wakfu, mcha-Mungu, asiyejitumainia nafsi, bali humwangalia Yesu, anaweza kuwa harufu ya uzima iletayo uzima kwa roho ambazo tayari ziko chini ya nguvu ya usadikisho wa Roho Mtakatifu, na ambao katika mioyo yao Bwana anaandaa njia kwa ajili ya ujumbe ambao amempatia wakala wa kibinadamu. Kwa namna hiyo moyo wa asiyeamini huguswa, naye huitikia na kuupokea ujumbe wa neno la kweli.
▶“Sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu.” Miguso ya usadikisho iliyopandikizwa moyoni, na kuelimishwa kwa ufahamu kupitia upokeaji wa Neno, hutenda kazi katika upatanifu kamili. Kweli iliyoletwa akilini ina uwezo wa kuamsha nguvu za roho zilizokufa. Roho wa Mungu atendaye kazi moyoni hushirikiana na utendaji wa Mungu kupitia mawakala Wake wa kibinadamu.
▶Tena na tena nimeoneshwa kwamba watu wa Mungu katika siku hizi za mwisho wasingeweza kuwa salama kwa kuwatumainia wanadamu, na kuufanya mwili kuwa tegemeo lao. Shoka imara la neno la kweli limewachimbua kutoka ulimwenguni wakiwa kama mawe yakwaruzayo yanayopaswa kuchongwa na kunyooshwa na kulainishwa kwa ajili ya jengo la mbunguni. Wanapaswa kuchongwa na manabii kwa makaripio, maonyo, nasaha, na ushauri, ili waumbwe wafanane na Kielelezo cha kiungu; hii ndiyo kazi maalumu ya Mfariji—kubadilisha moyo na tabia, ili wanadamu waifuate njia ya Bwana.
Regrann from @lemutuz_superbrand - LIVE STRAIGHT TALK: FACTS The Art of Love and Hate takwimu zinaonyesha kati ya Mwaka 2016 na leo 2018 Jumla ya Wananchi 341 wameuliwa na Wapenzi wao kati yao ni Wanawake ndio waliouliwa zaidi yaani Wanawake 247 na waliobaki ni Wanaume waliouliwa ni 94 wote wamekufa kwenye mapenzi na hasa ndoa inasikitisha sana ...kinachosikitisha sana ni the fact that Jamii imenyamaza kimya Wabunge wetu hawana hata habari na Wanasiasa wetu ndio wamekuwa mabubu kabisa sababu? ni Maadili yetu zaidii ya kuficha mapungufu ya Ndoa kwa Mwanaume kulalamika kwa jamii kuwa hamuelewi mke wake ni Aibu sana na Mwanamke kulalamika kwa jamii kuwa hamuelewi mumewe pia ni Aibu ya kuahindwa kuficha mambo ya ndani ya ndoa na matokeo yake ndio haya Taifa limepoteza Nguvu kazi ya Wananchi 341 ...nani anatakiwa kuhusika na afanye nini? ndipo tunapokwama na ninarudia tena na tena kwamba huu ni wakati muafaka Serikali ikaanza kulitupia macho hili tatizo ambalo chanzo chake ni Mapenzi na hata kwenye kuua huwa wanajiamini kwamba wanafanya kitu sawa kwa niaba ya mapenzi yao kwa wanaowaua ...tunatakiwa kuimarisha our Social Welfare Services ziwe na Professionals wanaoweza kusuluhisha matatizo ya Ndoa mara wanapoarifiwa tu na hata wapewe nguvu za kisheria za kuwaweka Rumande Wanaume na Wanawake waanaonekana kuwa chanzo cha matatizo ya kufikia kupigana katika ndoa au mapenzi ....ninasema hivi hatuwezi kuwa na Viwanda imara kama hatuna Wananchi Imara na sisi wananchi its about time sasa tukaanza kuamka usingizini hakuna mapenzi ya kupigana pigana mpenzi yoyote yule anayekupiga kuna siku ATAKUUWA TU sio mtu wa kumchezea I mean mpenzi anayepiga ni hatari sana ni most of the times ni kwa sababu amekulia kwenye ndoa ya Mama yake kupigwa na Baba yake au Baba yake kupigwa na Mama yake guys usicheze na mpenzi wa aina hiyo cause atakuuwa ....ndio maana USA watu wa namna hii wakifungwa jela huwa hawachiwi maana hakuna Therapy wala Rehab inayoweza kuwasaidia isipokuwa kuishi jela tu ...kwa mnaopigwa na Wapenzi wenu please take action now kama hawezi kuacha muwache cause ataishia kukuuwa! - @lemutuz_superbrand - #regrann
KESHA LA ASUBUHI
JUMATANO
06 June 2018
_*KUSHIRIKIANA NA
NGUVU YA MUNGU.*_? *“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” (Matendo 1:8).*
✍?Mungu amekusudia kutoacha chochote kisifanyike ili kumrejesha mwanadamu kutoka kwenye taabu za adui. Baada ya kupaa kwa Kristo, Roho Mtakatifu alikabidhiwa kwa mwanadamu ili awasaidie wote ambao wangependa kushirikiana Naye katika kuiumba upya na kuijenga upya tabia yake. Sehemu ya Roho Mtakatifu katika kazi hii imefasiliwa na Mwokozi wetu. Anasema, “Atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu” (Yohana 16:8). Roho Mtakatifu ni msadikishaji, na pia ni mtakasaji.
✍?Kwa vile hakuna anayeweza kutubu dhambi zake hadi pale anapokuwa amesadikishwa, ulazima wa kuungana na Roho katika kazi yetu ili kuwafikia walioanguka ni dhahiri. Vipaji vyetu vyote vya kibinadamu vitatumiwa bure isipokuwa kama tumeungana na mawakala wa mbinguni.
✍? Ni kupitia ukosefu wa maarifa ya kweli zihuishazo, na nguvu potofu ya uovu, ndiyo maana watu wamedhoofika kiasi hicho, wamezama katika vina vya1
auharibifu wa dhambi. Malaika na wanadamu hawana budi kutenda kazi kwa upatanifu ili kuifundisha kweli ya Mungu kwa wale wasioijua, ili wawekwe huru dhidi ya vifungo vya dhambi. Ni kweli pekee ndiyo iwawekayo wanadamu huru. Uhuru huu upatikanao kupitia maarifa ya neno la kweli, unapaswa kutangazwa kwa kila kiumbe.
??♂```Yesu Kristo, Mungu Mwenyewe, na malaika wa mbinguni wanavutiwa na kazi hii kuu na takatifu. Mwanadamu amepewa heshima iliyotukuka ya kudhihirisha tabia ya kiungu kwa kujihusisha pasipo ubinafsi katika jitihada za kumwokoa mdhambi kutoka kwenye shimo la uharibifu ambamo ametumbukia.
??♂ Kila mtu atakayejisalimisha ili aelimishwe na Roho Mtakatifu atatumiwa kwa ajili ya ufanikishaji wa kusudi hili lililoasisiwa na mbingu. Kristo ndiye kiongozi wa kanisa Lake, na itamtukuza zaidi pale ambapo kila kipengele cha kanisa hilo kitajihusisha katika kazi ya wokovu wa roho. Lakini watendakazi wa kibinadamu wanahitaji kuacha nafasi zaidi kwa ajili ya Roho Mtakatifu kufanya kazi, ili watumishi wafungamanishwe pamoja; na kusonga mbele katika nguvu ya kundi moja la askari. Hebu wote wakumbuke kwamba sisi tu “tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na wanadamu.” (1 Wakorintho 4:9).```
*MUNGU AWE NANYI MNAPOJIKABIDHI KWAKE*
Okay! I believe we all had a chance to listen to Diamonds ft Ravvyn new song #Iyena kwangu mimi naona wimbo upo kawaida japo video ni nzuri na nafikiri uwepo wa Zari mule umeongezea mvuto kwa kiasi kikubwa! Kama hujaona tazama ?
Lakini sijali sana kuhu wimbo, ujumbe wangu ni kwa Zari kwani nineona mashabiki "maandazi" wanavyo ongea eti "warudiane" na Diamond ?? I am like for real!! Who in a right mind will dare to say that?! Seriously people? let us be real here for a second!! Hivi ni huyu huyu Diamond aliye m-cheat Zari na kuzaa nje baadaye akaomba msamaha Zari akamsamehe kwa moyo mkunjuvu na akasema "I made peace with his mistakes"!! Baada ya hapo nini kilitokea?!! Sindio akarudi kutoka South nakupokelewa na Wema Sepetu ukumbini na familia yake yote ikiwepo na Wema?! Na hapo ni baada ya mama Diamond kukaa South Africa kwa Zari zaidi ya mwezi pamoja na mumewe halafu kafika Bongo ndio huyo yupo busy na Wema? (With all due respect to Wema, mimi sinaga mambo ya timu bali nataka nifikishe ujumbe wangu vizuri ndio maana namtaja) Na bado picha na video akiwa na wanawake wengine zilirushwa kwenye mitandao na kila mtu anaona! Nyie watu acheni mzaha!!
To you Zari, I'm not sure if you consider yourself "a celebrity" or a business lady who happened to be a "celebrity"! Celebrity is a culture, if you want to live a celebrities culture then forget about your integrity, take Diamond back and prepare to lose respect from many people! What I am trying to say here you're way better off without Diamond! You stand as a very strong and powerful woman right now than those days you used to zoom around with Diamond everywhere like a homeless lady!!
You have added your value by showing people who you real are, how strong you can be, please don't trap kwa mama Diamond childish games! Adults, young girls and boys are looking up to you so do your children please don't let them down eti kisa nyimbo! Think about your daughter, you are laying a foundation of how boys and men should treat her be wise like snake! Build good foundation that every man will think twice before holding your daughter's hand! Teach young boys that women are not tools but rather are fellow human beings treat them with respect and dignity, not using them as "money making" machines!! Please, find a healthy co-parenting way with Diamond and his family but don't take them back as family. That family is perfect but not for you, is perfect for those other women (if you know what I mean)! Achana nayo kabisa they don't deserve you even for a second. You were raised by a strong woman, whom she raised all those strong children alone why letting her down!! Usiseme eti watoto hata yatima pia ni watoto lakini wanakua!! That family isn't a healthy family to raise children with labda uwe unavuta bangi! Money is good but Not all money is great!! Choose your paycheck wisely!
After all, you look more matured, focused, and well kept right now than ulipokuwa na Diamond. He stressed you out, took the strength out of you, misused your love, you didn't have peace at all. Try to look at your old pictures you will agree with me!! They degraded you to accommodate and keep up with their uncivilized characters!! Trying to make money by destroying every woman that Diamond is involving with, I hope you are awake enough to smell the nasty coffee!!
Plus this babydaddy of yours care less about your life, he doesn't care if he would leave your children motherless perhaps even no parents at all that why he can't use any kind of protection-HIV is real woman! And what about Hippies, and Hepatitis C for God's sake!! Look how he was fooling around with those ladies, let them recorded him with no fear or shame then shared them in social media?!! Guess what, that is the PROOF THAT HE DOESN'T LOVE YOU!! He is just using you! Selfish to the core!! If someone loves you will care about you, will always think about you before taking any action!! No one is perfect but some people are evil!! This is nothing but pure evil!!
You can do business with him but make sure every thing is clearly written and well documented. Make sure he is not a beneficiary of any of your money even if you happen to die today! Let ALL your children be the first beneficiaries, and your sisters legal guardian. You're better than this Zari don't let this family destroy the woman you are!! ..... In the end, it's your life we are just cheerleaders!!
KESHA LA ASUBUHI
Juma Pili 3/6/2018
**CHUMVI YA DUNIA**“Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu” Mathayo 5:13
Mungu atatenda kazi pamoja na kanisa, lakini si bila ushirikiano wao. Hebu kila mmoja wenu aliyeonja Neno zuri la Mungu “nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni” (Mathayo 5:16). Yesu anasema, “Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.” Chumvi inayookoa, yaani mvuto wa Mkristo, ni upendo wa Yesu moyoni, ni haki ya Kristo inayotawala rohoni. Ikiwa yule anayedai kuwa mtu wa dini atatunza ufanisi wa imani yake unaookoa, imempasa kuiweka haki ya Kristo mbele yake daima, na kuwa na utukufu wa Bwana kama thawabu. Ndipo uweza wa Kristo utakapofunuliwa katika maisha na tabia.
Oh, tutakapofika kwenye malango ya dhahabu, na kuingia katika mji wa Mungu, je, kuna yeyote atakayeingia pale ambaye atajutia kwamba aliyatoa maisha yake kikamilifu kwa Kristo? Hebu sasa tumpende kwa upendo ulio kamili, na kushirikiana na viumbe wa mbinguni, ili tupate kuwa watendakazi pamoja na Mungu, na kwa kufanywa washirika wa tabia ya Uungu, tuweze kumdhihirisha Kristo kwa wengine. oh, laiti tungepokea ubatizo wa Roho Mtakatifu! Laiti miale miangavu ya Jua la Haki ingeangaza katika vyumba vya mioyo yetu na akili zetu, ili kwamba kila sanamu iondolewe na kufukuzwa kutoka katika hekalu la moyo! Laiti ndimi zetu zingefunguliwa ili kuzungumzia wema wake, na kueleza juu ya uweza wake!
Kama ukiitikia kuvutwa na Kristo, 6hutashindwa kuwa na mvuto kwa mtu fulani kupitia uzuri na uweza wa neema ya Kristo. Hebu tumwangalie na kubadilishwa katika mfano wake Yeye ambaye ndani yake unakaa utimilifu wote wa Mungu kwa jinsi ya mwili, na kutambua kuwa tumekubalika katika huyo Mpendwa, “mmetimilika katika Yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka” (Wakolosai 2:10). – Bible Echo, Feb. 15, 1892.
Regrann from @open_kitchen2014 - Mwanamke anayejiamini she looks so sexy and classy mwanamke anayetambua thamani yake always anajiheshimu na anasimamia kile anachokiamini na hata mume wake atamuheshimu daima milele kwasababu anajua umuhimu wake na mchango wake katika familia ? ? Lakini pia heshima hiyo na kujiamini huko hakuji kwa urahisi kwasababu ni kitu ambacho anajengewa toka akiwa mdogo na wazazi (Mwenyezi Mungu awarehemu wazazi wangu ) lakini namshukuru sana mama yangu kwa kunilea na kunifundisha what it means kuwa mwanamke na sio mwanamke tu bali mwanamke anayejiamini
Kila siku alikuwa anatufundisha ukijua kufanya kazi na kusimamia familia basi ujue kamwe hakuna atakaye kuangusha kirahisi utaheshimika kuanzia na wadogo zako mpaka watu wazima kila utakapo ingia mahali kila mtu atatambua uwepo wako na atakupa heshima yako iwe ni nyumbani kwako ,kazini kwako,au popote pale ?
? Malezi na misingi mizuri ya maisha ndio zawadi bora kabisa ambayo mama anaweza kumpa mtoto
Ukimpenda sana mtoto wako lakini ukashindwa kumlea katika misingi mizuri na kumwongoza aweze kujua nini maana ya kujiheshimu ,kukuheshimu ,na kuheshimika ni sawa na kupaka chokaa kwenye nyumba ya nyasi TAFAKARI ?
MWANAMKE USIPOJITAMBUA NA KUJIELEWA UKAJIAMINI UKAWA NA MSIMAMO BASI UJUE UTATUMIKA KILA SIKU NA KILA MTU KAMA KOPO LA CHOO CHA KULIPIA ??????? - #regrann
KESHA LA ASUBUHI
JUMAMOSI 02/05/2018
*NURU YA ULIMWENGU*
? _“Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima” Mathayo 5:14_
✍?Uaminifu wetu kwa kanuni za Ukristo unatuita kwa huduma ya utendaji kwa ajili ya Mungu. Wale ambao hawatumii talanta zao katika kazi na kusudi la Mungu hawatakuwa na sehemu pamoja na Kristo katika utukufu wake. Nuru haina budi kuangaza kutoka katika kila roho iliyopokea neema ya Mungu. Roho nyingi zimo gizani, lakini wengi wanajisikia pumziko, raha na utulivu katika hali hiyo!
✍?Maelfu wanafurahia nuru kubwa na fursa za thamani, lakini hawafanyi cho chote kwa mvuto wao au fedha yao, ili kuwaangazia wengine nuru. Hawachukui hata jukumu la kutunza roho zao wenyewe katika upendo wa Mungu, ili kwamba wasiwe mzigo kwa kanisa.
✍?Watu wa jinsi hiyo watakuwa ni mzigo na kizuizi mbinguni. Kwa ajili ya Kristo, kwa ajili ya ile kweli, na kwa ajili yao wenyewe, wanapaswa kuamka na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya umilele. Makao ya mbinguni yanaandaliwa kwa ajili ya wale ambao watakubaliana na masharti yaliyowekwa wazi katika Neno la Mungu.
✍?Kwa niaba ya roho zile ambazo Kristo alizifia, wale ambao wamo katika giza la makosa, wafuasi wote waaminifu wa Kristo wameamriwa kuwa nuru kwa ulimwengu. Mungu amefanya sehemu yake katika kazi hii kuu, na anangojea ushiriki wa wafuasi wake.
✍? Mpango wa wokovu umekamilika kabisa. Damu ya Yesu Kristo imetolewa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, Neno la Mungu linazungumza na binadamu katika mashauri, makaripio, maonyo, ahadi, na kutia moyo, na ufanisi wa Roho Mtakatifu unatolewa ili kumsaidia katika juhudi zake zote. Lakini pamoja na nuru yote hiyo ulimwengu bado unaangamia gizani, ukiwa umezama katika makosa na dhambi.
??♂```Ni nani watakaokuwa watendakazi pamoja na Mungu, ili kuleta hizi roho katika kweli? Ni nani atakayewapelekea habari njema za wokovu? Watu ambao Mungu amewabariki kwa nuru na kweli wanapaswa kuwa wajumbe wa rehema.Utajiri wao unapaswa kutiririka kupitia katika mfereji wa kimbingu.
??♂Juhudi zao za dhati hazina budi kuonekana. Imewapasa kuwa watendakazi pamoja na Mungu, wenye kujikana nafsi, wenye kujitolea, sawa na Yesu, ambaye kwa ajili yetu alikuwa maskini, ili kwamba kupitia umaskini wake, sisi tupate kuwa matajiri. – Review and Herald, Machi 1, 1887.```
*MUNGU AKUBARIKI MUWE NA SIKU NJEMA*
Hata Kama Mambo Yanakwenda Vibaya, Fanya Hivi
Ni rahisi sana kuwa na hasira, kukatishwa tamaa na hata msongo wa mawazo. Hiki ni kiu ambacho kila mtu anaweza akawa nacho kwenye maisha yake.
Nikiwa na maana kila mtu akikasirishwa, anaweza akakasirika sana au mtu akikatishwa tamaa anaweza akakata tamaa pia sana.
Lakini yote hiyo haiwezi kusaidia kitu. Busara na ukomavu wako wa kimaisha unakuja pale hasa unapokwenda kinyume na mambo hayo.
Ni kweli unaweza ukawa umekasirishwa na ukatamani upige mtu sana, sasa je, kwani ni lazima ifike mahali ukakakasirika kwa kiasi hicho?
Ni kweli unaweza ukawa umekatishwa tamaa, lakini kwa wewe haina haja kuendelea kufanya mambo ambayo yanakukatisha tamaa zaidi.
Unachotakiwa kufanya au kujifunza ni kuweza kugeuza mambo ya hovyo na yakawa bora zaidi hata kama imetokea hali ya kukasirishwa au kukatishwa tamaa.
Kufanya hali mbaya ambayo tayari naweza kusema umeshapewa na ikawa ni nzuri, huo ni ukomavu wa hali ya juu utakaokufanya uishi vizuri sana duniani.
Mtu amekuuzi sana na wewe huhitaji kuendelea kufoka au kuumia zaidi. Unatakiwa kutuliza akili yako na kufanya mambo ili yawe mazuri.
Kufanya mambo yawe mazuri hasa pale yanapokuwa yameharibika ni kitu ambacho unatakiwa ujifunze nacho sana karibu kila siku.
Kila siku na kila wakati endelea kuweka juhudi za kuwa mtu chanya, mpaka maisha yako yalete utofauti mkubwa na kwa wengine.
Ni watu wachache sana ambao wako tayari kubadilisha hali mbaya ya msongo wa mawazo walionayo, kukatishwa tamaa na kukasirishwa kuwa nzuri.
Wengi wakikasirishwa na wengine hukasirika na kukasirisha zaidi. Hivyo, unatakiwa usiwe miongoni mwao. Unatakiwa uwe mtu wa kubadilisha hali.
Kufanya hali yoyote iwe bora ni zoezi ambalo unaweza ukalifanya karibu kila siku kwenye maisha yako pale ambapo unakuwa unaona mambo hayajakwenda sawa.
Unatakiwa uelewe hili, pale mambo yako yanapokwenda hovyo, fanya mambo hayo yawe bora. Jitahidi kubadili hali hiyo kwa busara na ikawa bora.
**By Mapigano**
Hayo ? ni maneno yake kaka yangu RC Paul Makonda! Wow! Hongereni wote maharusi watarajiwa lakini zaidi hongera sana Lulu! Jamani! Jamani! Binadamu watakesha wakitaka kukuangusha lakini Mungu atakapoamua kukuinua hakuna anayeweza simama mbele yako! Jinsi watu alivyokuwa wakikucheka kuwa unamkosi leo hii the same people wapo busy kukupongeza! Dah! Watanzania Mungu atusaidie. Hivi kama haya si mapenzi ya kweli mtasema ni kitu gani?!! Hizi ndizo katika tabu na raha ambazo Biblia inazungumzia. Siyo kupigana mangumi na kuchinjana mapanga!! Wanaume kama Majizzo ni wanaume wachache sanaaa haswa kwa watu wa Africa!! Ubarikiwe sana Majizzo kwa kuonyesha mfano bora haswa kwa vijana wa leo. Hongera Lulu enjoy every single moment ya maandalizi yako mpaka harusi. Make sure you got your dreamed wedding wala usiogope. Huu ndio wakati wako wa kuinuliwa juu simama kishujaa tena kwa madaha. Mungu awamiminie neema zake! ?
**Mimi na dedicate wimbo huu wa Hezekiah Walker " God favored me" kwako Lulu** ?
Regrann from @lemutuz_superbrand - LIVE STRAIGHT TALK: The Art Of Self -confidence I mean huwa ninashindwa kuamini ninampigia simu Mbebezz anapokea Mwanaume na kujifanya kujitunisha please stop that guys unakuwa mjinga na utaishia kujiua cause Mwanaume unatafuta nini kwenye simu ya Mbebezz wala sio mke wako na hata kama angekuwa Mwanaume huingii kwenye simu ya Mbebezz cause utayakuta unayoyatafuta yaani Ugonjwa wa moyo ..kila binadam anahitaji nafasi au space to be themeselves sometimes na hakuna binadam anayeweza kumchunga mwingjne na mpaka kufanikiwa HAYUPO nina maana Mwanaume huwezi kumchunga Mbebezz ukafanikiwa utakwama tu kila binadam anahitaji uhuru wa kufanya mambo yake bila kuchungwa na kwenye mapenzi tunatakiwa kuongozwa na TRUST!
Now what is TRUST kwenye mapenzi wewe hakikisha you dont Cheat ukiweza hilo ujue na Mbebezz wako hata ku cheat ila kama wewe Mamen una Cheat ujue 100% Mbebezz wako naye ata Cheat tu yaani wewe ule wabebezz wa wenzako ila wako asiliwe wewe nani hapa.Duniani na nani kakudanganya kuwa inawezekana? ...guys kuna Sheria ya maisha sijaitunga mimi kua ukiona una cheat mke wako hakukamati ujue na yeye ana Cheat cause giza ni kwa giza na mwanga ni kwa mwanga babe yaani haiwezekani wewe U cheat mke wako asi cheat no way UNAJIDANGANYA TU hahahaha ...halafu guys acha utoto mpenzi wako akiamua kuku cheat haina maana hakupendi ila ni mapungufu tu ya kibinadam wote huwa tunapitiwa na jifunze kuwa kama mimi Sheria yangu ya maisha ni mpaka NIMKUTE MBEBEZZ WANGU RED HANDED ANA CHEAT ndio nitaamini ila siwezi kusikiliza maneno ya watu au majungu majungu au kwa vile nimeona sms ni Ujuha wa hali ya juu sana kukosa Kujiamini ...sawa mapenzi mapenzi lakini jifunze kwamba unampenda binadam mpungufu kwama wewe ulivyo so mpe nafasi usimbane mpaka anakosa pumzi U know ...kumpenda mpenzi wako sio kumfuatilia kwenye simu hapana mpe mapenzi ya kweli ataona huzuni na aibu kukuibia na ukiona mbebezz anaruka ruka ujue kuna kitu anakosa kwako muulize kwa upole atakuambia tu kuliko kujifanya mbabe na unajua kuchunga cause huwezi ...guys Mwanamke ni kama kisima cha maji huwezi kujua kuna mtu kachota ndoo moja mpaka umuone kama hukumuona hutajua so relax and chill like me! - @lemutuz_superbrand - #regrann
*Kesha la Asubuhi*
*Alhamisi*
*Tarehe 31/5/2018*
*Roho Hatimaye
Aondolewa*??Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Ufunuo 22:11.
??Wakati ujumbe wa malaika wa tatu utakapofungwa, rehema haitaendelea kusihi tena kwa ajili ya wakazi wa dunia wenye hatia. Watu wa Mungu wametimiza kazi yao. Wamepokea “mvua ya masika,” “kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana” (Matendo ya Mitume 3:19), na wako tayari kwa ajili ya saa ya majaribio iliyoko mbele yao. Malaika wanaharakisha kwenda mbele na kurudi nyuma kule mbinguni. Malaika mmoja anarudi kutoka duniani na kutangaza kuwa kazi imekwisha; jaribio la mwisho limeletwa juu ya dunia, na wote waliojithibitisha wenyewe kuwa ni waaminifu kwa sheria za Mungu wamepokea “muhuri ya Mungu aliye hai” (Ufunuo 7:2).
??Kisha Yesu anaacha kazi yake ya upatanisho katika patakatifu pa mbinguni. Anainua mikono na kwa sauti kuu anasema, “Imekwisha,” na jeshi lote la malaika wanaweka chini taji zao anapotoa tangazo makini: “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu: na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu: na mwenye haki na azidi kufanya haki: na mtakatifu na azidi kutakaswa.” (Ufunuo 22:11). Kila kesi imeamuliwa kwa ajili ya uzima au mauti. Kristo amefanya upatanisho kwa ajili ya watu wake na kufutilia mbali dhambi zao. Idadi ya watu wake imekamilishwa; “ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote” (Danieli 7:27), inakaribia kupewa kwa warithi wa wokovu, na Yesu atawale kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.
??Anapotoka katika patakatifu, giza linawafunika wakazi wa dunia. Katika wakati ule wa kuogofya watakatifu inabidi waishi mbele za Mungu aliye mtakatifu bila kuwa na Mwombezi. Kizuizi ambacho kimekuwapo juu ya waovu kinaondolewa, na Shetani anakuwa na mamlaka kamili juu ya wale ambao hatimaye hawakutubu. Uvumilivu wa Mungu umefika mwisho. Dunia imekataa rehema yake, imedharau upendo wake, na kuikanyaga chini ya miguu yao sheria yake. Waovu wamevuka mpaka wao wa rehema; Roho wa Mungu, akiwa ameendelea kupingwa, hatimaye sasa anaondolewa. - The Great Controversy, uk. 613, 614.
Regrann from @zarithebosslady - WCW inspirational moment: I always knew I wanted the good life, like I wont even lie about it but then again dont we all? Well, at 30 I was already employing 258 employees and that alone on its own made me grow up mentally. The responsibility that comes with managing companies in a foreign country where you are always targeted as a foreigner least i forget the tight competition especially if your on top of your game wasnt easy...... so whatever you do, do it with passion. Fall down 99 times, get up the 100th. One day, and I say it again one day, the universe will respond. #Persistence #Consistence (See my life at 30, huge office with a personal boardroom?) me and Don started out in 2 offices, one PA, had just abit of ideas, got experts on board which we couldn't afford but they saw potential in us, did our logos which will forever remain a trademark and here is our recognized brand in the whole of SA www.brooklyncitycollege.co.za - #regrann Awiih! That's my gal! My true inspiration. The real BossLady. Hakuiba kwa mume wa mtu akuuuu mtoto wa watu! Katafuta masiki mwenzake wakaanza kusaga visigido!! #I'mTheFoundationNotTheRoof ......I want good life too and hope to catch up with your achievement though I am in my 40s! Don't look down on me only God sits that high ? ??..... You go Zari! Keep winning! Keep shinning!
*KESHA LA ASUBUHI*
JUMATANO MEI 30, 2018
*Muda U Karibu wa Kuondoka kwa Roho*Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure. Ufunuo 22:17.
? Kipindi cha rehema hakitaendelea kwa muda mrefu zaidi. Sasa Mungu anaondoa mkono wake unaozuia kutoka katika dunia. Kwa muda mrefu amekuwa akizungumza na wanaume na wanawake kupitia katika uwakala wa Roho Mtakatifu wake; lakini hawajasikia wito huu. Sasa anazungumza na watu wake, na kwa ulimwengu, kwa hukumu zake. Muda wa hukumu hizi ni muda wa rehema kwa wale ambao bado hawajapata fursa ya kujifunza ukweli ni nini. Kwa upole Bwana atawatazama. Moyo wake wa rehema unaguswa; mkono wake bado umenyoshwa ili kuokoa. Watu wengi watapokelewa katika zizi lenye usalama ambao katika siku hizi za mwisho watausikia ukweli kwa mara ya kwanza.
? Bwana anawaita wale wanaomwamini kuwa watendakazi pamoja na yeye. Wakati maisha yangalipo, hawapaswi kujisikia kuwa kazi yao imekwisha. Je tutaruhusu ishara za mwisho wa wakati kutimizwa pasipo kuwaambia watu kuhusu kile kinachoujia ulimwengu? Je tutawaruhusu waende chini gizani bila kuwa tumewasisitizia hitaji la matayarisho ya kukutana na Bwana wao? Isipokuwa sisi wenyewe tumetenda wajibu wetu kwa wale wanaotuzunguka, siku ya Mungu itakuja juu yetu kama mwivi. Machafuko yameujaza ulimwengu, na hofu kuu iko karibu kuja juu ya wanadamu. Mwisho uko karibu sana. Sisi tunaoufahamu ukweli tunapaswa kuwa tunajitayarisha kwa ajili ya kile ambacho kiko karibu sana kuujia ulimwengu kama mshangao wa ajabu mno.
? Kama kanisa ni lazima tuweke tayari njia kwa ajili ya Bwana, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Injili inapaswa kutangazwa katika usafi wake. Kijito cha maji ya uzima kinapaswa kuongeza kina na kupanuka katika mwendo wake. Katika viwanja vya karibu na vya mbali, watu wataitwa kuacha plau-majembe ya kukokotwa na wanyama, na kutoka katika kazi za kawaida za biashara, na wataelimishwa pamoja na watu wale wenye uzoefu. Kadiri wanavyojifunza kufanya kazi kwa ufanisi, watatangaza ukweli kwa nguvu. Kupitia katika utendaji wa ajabu kabisa wa majaliwa ya Mungu, milima ya magumu itaondolewa.
? Ujumbe wenye maana sana kwa wakazi walioko juu ya dunia utasikika na kueleweka. Watu watafahamu ukweli ni nini. Mbele, na mbele zaidi, kazi itaendelea, hadi dunia yote itakapokuwa imeonywa. Na ndipo mwisho utakapokuja. -Review and Herald, Nov. 22, 1906.
*MUNGU AKUBARIKI*
Wapendwa wasomaji wangu haswa wanawake wenzangu, naomba msinishangae kwanini sijazungumzia vifo vya kinyama vya wanawake wawili vilivyotokea wiki iliyopita. Kwanza nawapa pole wafiwa wote na familia zao, Mungu awape faraja katika mapito haya.
Pili, mimi maswala haya ya domestic abuse haswa kwa wanawake nilishawahi waeleze huko nyuma kuwa ni mambo ambayo sina nguvu sana ya kuyaelezea kwani vinakuwa vinanikumbusha maumivu makali sana ambayo sitaki kuyafikiria wala kuyazungumzia kwa sasa. Siku nikijiona nina nguvu ya kuongelea basi nitawaelezea. Ila kwa sasa acha watu kama akina Joyce Kiria wayaongelee. Ndio maana hata yule dada aliyeuliwa na mumewe kule London sikusema kitu siyo kwamba sijali ila ninakuwa na maumivu yaliyo changanyika na hasira hivyo naona ni bora kunyamaza kuliko kuongea nikiwa na hasira.
Tatu, wanawake wenzangu, hawa wanaouliwa haikutokea tu pasipo kuonyesha dadalili za ukatili ambazo zitaashiria kifo! Haya mambo yanaanza kidogo kidogo na kadri unavyojaribu kuvumilia ukatili huo unao uona ni mdogo ndio unavyomjengea mazingira mazuri ya kukumaliza kabisa! Kataa ukatili wa aina yoyote ile, Hawaanzi kwa kupiga huwa wanaanza kwa kukutenganisha na ndugu na marafiki zako wa karibu ili usiwe na msaada wowote. Ukisha ona mumeo au mpenzi wako anaonyesha dalili za kutaka utengane na ndugu zako au wazazi wako basi anza kulala macho wazi!! Halafu utakuta yeye ndio anataka wewe uonekane mbaya yupo busy kuongelea udhaifu wako kwa watu bila kusema makosa yake ogopa sana! Kwanza mwanaume anayekupenda hata mgombane vipi hawezi zungumzia matatizo yenu kwa watu, mtagombana wenyewe na kuyamaliza wenyewe!!
Ogopa sana mwanaume asiyejali hisia zako! Emotional abuse ni dalili kubwa ya pili katika maswala ya unyanyasaji. Akisha kutenga na ndugu zako basi lazima kinacho fuata ni ukatili wa kihisia na baada ya hapo atakupiga kama hata kuuwa basi atakuachia kilema cha maisha!
Jamani hii ni karne 21 nani bado anataka kuishi maisha ya zama za giza? Eti mwanaume anakupiga mpaka mimba inatoka halafu bado unamwita mume wangu? Au mtu eti mwanaume anakwambia utoe mimba kwasababu hataki watoto wa kike nawe unakubali??? halafu unjiita msomi?! ??
Jamani, Joyce Kiria anongea kwa sauti mwenye masikio na asikie asiyetaka shauri yake. Dalili huwa zinaanza mapema uwamuzi ni wako kuzikemea au kuzilea mpaka utolewe roho. Nachoomba tu tuwafundishe watoto zetu wa kike kwamba ukatili HAPANA! Napia watoto wetu wa kiume wafundishwe kupenda na kuheshimu wanawake kwani hata mama zao ni wanawake vile vile!
*KESHA LA ASUBUHI*
Jumanne Mei 29, 2018
*Bidii Katika Kutoa Onyo la
Mwisho*_Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Ufunuo 18:1_
? Siku hadi siku hupita na kuwa milele, ikituleta karibu zaidi na kufungwa kwa mlango wa rehema. Sasa inatubidi kuomba kwa jinsi ambavyo kamwe hatujawahi kuomba kwa ajili ya Roho Mtakatifu kuwekwa kwa wingi zaidi juu yetu, na lazima tutafute uwezo wake unaotakasa upate kuja juu ya watendakazi, ili watu ambao wanawafanyia kazi wapate kufahamu kuwa wamekuwa pamoja na Yesu na kujifunza kutoka kwake. Tunahitaji uwezo wa kuona kwa macho ya kiroho sasa kuliko wakati wo wote uliopita, ili tupate kuona mbali, na kwamba tupate kutambua mitego na njama za adui, na kama walinzi waaminifu kutangaza hatari. Tunahitaji nguvu za kiroho ili tupate kupokea kadiri ambavyo akili ya mwanadamu inaweza kupokea, mada kuu za Ukristo, na jinsi ambavyo kanuni zake ni za kudumu.
? Watu wa Mungu wanaponyenyekesha roho mbele zake, kama mtu mmoja mmoja akitafuta Roho Mtakatifu wake kwa moyo wote, itasikika kutoka katika vinywa vya wanadamu ushuhuda kama ule unaowasilishwa katika Maandiko: “Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake” (Ufunuo 18:1). Kutakuwapo na nyuso zinazong’aa kwa upendo wa Mungu, zikisema, “damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.” (1 Yohana 1:7). Wale walioko chini ya uwezo wa Roho Mtakatifu wa Mungu hawatakuwa washupavu wa dini, bali watulivu, imara, huru kutokana na ubadhirifu. Lakini hebu wale wote ambao wameipata nuru ya ukweli ikiwaka wazi na dhahiri katika njia zao, wawe waangalifu katika jinsi wanavyotamka amani na usalama. Mwe waangalifu ni mvuto gani mnaoweka wakati huu.
? Yesu anatamani sana kuweka majaliwa ya mbinguni kwa kipimo kikubwa juu ya watu wake. Maombi yanapanda kwenda kwa Mungu kwa ajili ya utimilizwaji wa ahadi hii; na hakuna ombi hata moja lililotolewa kwa imani linapotea. Kristo alipaa juu, aliteka mateka, akawapa wanadamu vipawa. Wakati, baada ya kupaa kwa Kristo, Roho alipokuja chini kama ilivyoahidiwa, kama upepo wenye nguvu unaokimbia haraka, akijaza sehemu yote ambapo wanafunzi walikusanyika, matokeo yake yalikuwa nini?
Maelfu waliongolewa katika siku moja. Tumefundisha, tumetegemea kuwa malaika atashuka kutoka mbinguni, kwamba dunia itaangazwa kwa utukufu wake, pale tutakapoona uvunaji wa roho sawa na ule ulioshuhudiwa katika siku ya Pentekoste. - Home Missionary, Nov. 1, 1893.
*TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI*
#WAISLAMU_NA_WAKRISTO SOTE TU TAIFA MOJA IMARASiku tukianza kukumbatia tofauti zetu za kidini (ukristo na uislamu) ni sawa na kujichimbia kaburi la pamoja (mass grave) mchana kweupeeee kabisa.
Ukumbukwe tu ya kuwa si kitendo cha wakristo kuwatenga waislamu ndicho kitaweza kutuhakikishia maboresho katika mfumo wetu wa elimu ambao watoto wa dini hii kuu mbili wanapaswa kunufaika nao kama vijana tegemeo wa taifa la kesho, na wala si kwa;
kitendo cha waislamu kuwatenga wakristo ndicho kitahakikisha utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa maji vijijini ambapo takribani 90% ya watanzania waumini wa dini hizi kuu mbili wanapatikana.
Ili nchi hii isonge mbele, ni lazima tuhubiri umoja, na isiishie tu katika mahubiri, hapana, bali juhudi na mikakati ya makusudi kabisa lazima iwepo na itekelezwe ili kuhakikisha Tanzania inakuwa moja kwa leo na inaendelea kuwa moja na imara zaidi hata vizazi vijavyo.
Regrann from @zarithebosslady - Pale unaposkia pesa za urithi... apo vipi. Success isnt sexually transmitted my dear. Endeleeni kudanga thinking some rich guy will knock you off your feet and success will happen over night. Even if he did you will be like part of the furniture he has a right to take out old ones and bring in new ones, as for me its not easy to get rid of me. IAM THE FOUNDATION not the roof...haha. Anyway we are commemorating Ivans one year since his passing and i thought I'd motivate someone out there with these old images.
Dont downlook broke guys, God is for all, tables turn! Poor thing worked day and night to get me this car at 22 because he saw the woman in me. And yes, it didnt work out no matter how much i tried, Started from the bottom, right! Rest his soul in peace! - #regrann Ni maneno mazito sana kaandika Zari katika kukumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo cha Ivan Ssemwanga ambaye alikuwa mume wake na walijaliwa kupata watoto watatu. Ujumbe huu mzuri sana kwa wale wanaofikiria na kutwa kumsakama Zari kuwa anafuataga pesa kwa wanaume aliokua nao. Haya ushahidi huo mmeuona sasa muache kumsakama mtoto wa watu na mumpe heshima yake anayostahili!! Jibu safi sana kawapa "I am the FOUNDATION not the Roof"?? Ten ? across the board!! Ngoja leo niseme; katika wanawake wote ninaowapenda kwenye Social media kwakweli I have to sincerely admit Zari is number one!! Nikiangalia alipotoka na mambo aliyopitia, na jinsi anavyo yakabili kwakweli she is MORE than 'Woman and half'!! Hivi utawezaje kuvunja Msingi!! Kama ni nyumba inamaana lazima greda lipite nyumba yote idondoke ndio ufutilie mbali Msingi! Only fools do that!!!
Kama mnakumbuka huko nyuma niliwahi kuandika kuwa kuna wanawake wengine huwezi kupata "mbadala wake" you can not replace her no matter what (soma ? In loving memory of Ivan Ssemwanga: "I think I was prepared for death") na Zari ni one of those very few women! Yani kama vile Oprah, hakutakaa kutokee Oprah mwingine duniani! Wengine watajaribu kuwa kama yeye lakini they will never be her! Sio kwasababu ni wazuri wasura na maumbile, hapana! Is the Brain, the courage, behind that beauty is a whole game changer ma'am!! Unfortunately I have to say this, with all due respect to Ivan Ssemwanga, but he was part of Zari's journey and not the destiny!! The best of Zari is yet to come!! So do Diamond, yale yalikuwa ni mapito tuu lakini safari ya Zari inaendele na ni nzuri zaidi kuliko alivyokuwa na Diamond!! Just keep watching her. Yani naamini hata Diamond huko aliko anajuta sana kimoyo moyo kwani anajua kuwa hata hafanyeje haitokaa apate mwanamke kama Zari. Atapata hao wauza sura wakupenda drama na ujinga wa social media but not another Zari! He was just soooooo lucky to have Zari on his hands! Na bahati haiji mara mbili! Kwanza Zari sasa hivi ndio mambo ??? Keep on shining Zari! ? ❤ #IamTheFoundationNotTheRoof