*BAADA YA KUFA NINI
KINAENDELEA?*VIFUATAVYO NI VITU VINAVYOTOKEA. I. *UKIFA HAUWEZI KUFAHAMU NENO LOLOTE* ....MHUBIRI 9:5-6,10 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua. Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe II. *MWANADAMU ANAPOKUFA HANA TOFAUTI NA MNYAMA* ....MHUBIRI 3:19-20 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena, ZABURI 49:12 Lakini mwanadamu hadumu katika heshima, Bali amefanana na wanyama wapoteao III. *UKIFA HAUWEZI KUJUA WATOTO WAKO WANAENDELEAJE* ..... AYUBU 14:21 Wanawe hufikilia heshima, wala yeye hajui; Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao IV. *UKIFA HAUWEZI TENA KUMSIFU MUNGU BALI UKIWA HAI* ........ ZABURI 146:2,4 Nitamsifu Bwana muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai. Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea V. *WALIOKUFA WOTE BADO WAMELALA MAKABURINI WATAFUFULIWA YESU ANAPORUDI MARA YA PILI* ...... 1 WATHESALONIKE 4:13-18 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo. Isaya 26:19 Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa VI. *JE MUNGU ANAO UWEZO WA KUMRUDISHIA KILA KIUNGO AMBACHO MWANADAMU ANAKUWA NACHO WAKATI WA UHAI WAKE MF.NGOZI,NYAMA,,MIFUPA,,,!* ....... EZEKIELI 37:3-10 Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe. Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la Bwana. Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. asi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe. Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake; lakini haikuwamo pumzi ndani yake. Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi. Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno. VII. *HAIRUHUSIWI KUFANYA IBADA YA WAFU AU KUWAOMBEA ETI MUNGU AWABARIKI/AWASAMEHE* TORATI 18:9-11 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, WALA MTU AWAOMBAYE WAFU VIII. *JE NI KWELI WAFU WAKIFA BAADAYE HUWATOKEA NDUGU ZAO?* ...... 2 WAKORINTHO 11:13-15 Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao. JIBU NI HAPANA -Wafu wanaowatokea watu na kuongea nao tena wanafanana kabisa na ndugu zao waliokufa hizo huwa ni roho za mashetani zinazojigeuza katika maumbile mbalimbali ya marehemu ili kuwadanganya watu kuwa hawafi huo ni udanganyifu mkubwa wa shetani *TAHADHARI:* Wafu hawaendi mbinguni wanapokufa bali huzikwa kaburini, pia hawawezi kusamehewa kama walikufa bila kuungama dhambi zao.
Related