Category Archives: Appreciation

AMETIMIZA MOJA YA NDOTO ZAKE!

Mercy akiwa na Dr Kapesa

Siku ya leo tarehe 08/16/2021 majira ya mchana masaa ya Africa Mashariki, mwanangu katimiza moja ya shahuku yake kubwa au nawezasema moja ya ndoto yake!

Amekutana na mmoja wa madaktari walio nihudumia na kuhakikisha anaingia katika dunia hii akiwa salama! ?? Marehemu Dr Amood alikuwa ndio my primary Dr lakini alinikabidhi kwa Dr. Kapesa na Dr Kaisi kama mbadala wake pindi yeye anapokuwa na majukumu mengine. Siku ya kujifungua Dr Kaisi ndio aliyekuwepo zamu, Dr Amood aliitwa na alipofika Mercy alikuwa teyari kazaliwa! ??

Mungu azidi wabariki wote Dr Kapesa na Dr Kaisi! Bahatimbaya Dr Kaisi alipatwa na stroke (kiharusi) hivyo kwasasa amepumzika kufanya kazi za utabibu aliyosomea.

BTW, nilikuwa natibiwa Tanzania Maternity Service ambapo madaktari hawa wote walikuwa business partners!

Nawatakieni kheri ya kufunga mwaka 2018 na baraka za kufungua mwaka 2019!

Katika mwaka 2018 kuna mambo mengi sana yametokea, mengine yalikuwa mazuri sana, mengine ya kuhuzunisha na mengine japo yalikuwa ni changamoto za kutesa moyo na hisia lakini yamezidi kutuimarisha sisi kama familia. Shetani alitujaribu sana lakini ametukuta tupo ngangari imani yetu kwa Muumba wetu haitetereki. Kwajinsi tulivyo pitishwa kwenye hayo majaribu ambayo makali yake yalikuwa kama makaa ya moto nabado tukaishika imani yetu!? Basi nina kila sababu ya kusema kuwa kamwe imani yetu haitokaa kutetereka kwani tumeuona mkono wa Mungu hatuto uwacha milele! 

Kama nilivyo amua kuishi maisha yangu kwamba siku zote nita ipa nguvu mambo ambayo yananipa furaha na sio huzuni. Basi kwa mwaka huu wa 2018 vitu vingi sana vimenipa hufura lakini hivi ni vilinipa furaha zaidi. Kutembelewa na mama yangu mzazi, wadogo zangu, na mama yangu mdogo hapa kwetu Houston, Texas ni mbaraka wa peke sana. Nina kila sababu ya kusema Asante kweli wewe ni Mungu! Nitalisifu jina lako milele!
Jambo lingine ambalo limenifurahisha sana mwaka huu ni ujauzito wa my best friend, a sister near and deer to my heart. Mungu amembariki mtoto wa kike na amemuita jina Mercy sawa na jina la mwanangu mimi. Kwakweli namshukuru Mungu sana kwa huu mbaraka. Tunaomba amlinde na amkuze mwanentu. Atupe hekima na busara za kuweza kulea vyema watoto wetu ??

The three pillars to the well being of Mr. Otieno Igogo

The three pillars to the well being of Mr. Otieno Igogo and all of you who are direct and indirect benefitting from the sources of Mzee Igogo Otieno. 1. Min Gwethrhoda (mama Gwethrhoda / Blessing) 2. Min Vetto 3. Nyategi (Nyategi means a girl / lady born from Utegi village) /Mrs Mabada . I salute them all.
Hao wamama watatu ni Mashujaa wa karne, wanaishi maisha ya kimbingu kwa kusema ukweli siku zote za maisha yao, wanaheshimu na kuitukuza Sabato ya Bwana kila wiki na miaka yote, wachapakazi wasio mfano maofisini na nyumbani, wanapenda kusaidia watu wote kiushauri na mali, pasipo mipaka wala tabaka, Naye Mwenyezi Mungu kawapa kipawa cha hekima, busara na Upendo wa pekee kwa Mzee mwasisi wa familia yao. Nawaheshimu na kuwathamini kupindukia. Asemavyo Mzee OOI.

Mama Keagan: Asante Mungu

Regrann from @nikypal8585  - Asante Mungu wewe ndio uliyenipa huyu mtoto  keagan P .Makonda ? wewe ndio mtendaji na msemaji wa mwisho.Umefanya kwa wakati ulio ona ni sahihi ???? umenipa mtoto wangu Keagan  najua ulikuwa na sababu kwanini haikutokea wakati nilipotaka mimi. Mimi ni ushuhuda kamili katika maisha ya kila mwanamke au msichana aliyekata tamaa. Usiogope  kaa kimya jipe moyo tamka hili neno moyoni mwako MIMI NI USHUHUDA  ULIOKAMILI SITA TETEREKA KAMWE MUNGU NITENDEE  JAMBO LANGU KWA WAKATI  ULIOSAHIHI NA ULIO UPANGA  WEWE  AMEN???????  -  
Asante Mungu kwa ajili ya mume wangu Paul (Baba keagan)hakika wewe ni jeshi lisilo tetereka kwani imani yako imepimwa kwa njia tofauti ila ulisimama imara??kwa machozi ya kishujaa,ulinitia moyo  sana ukuchoka kusema mke wangu wakati  wa Bwana huwa ni sahihi pangusa machozi mshukuru Mungu kwani  alikuwa amekuandalia faraja ya kudumu.Hakika nimemwona Mungu kila wakati nilipo pata jaribu nilijifunza kukaa kimya na kujipa moyo wa ushujaa na kusema hakuna mwanadamu anayeweza kukamilisha hii furaha ya mimi kuitwa mama na kupakata mtoto aliyetoka kwenye tumbo langu.Nasema tena  na tena upendo wa Mungu kwangu hauna kipimo kwani kanipa kicheko na rafiki wa kudumu .Nawapenda wanangu #PK nitawaleanakuwaombea daima ❤️❤️❤️❤️❤️❤️ASANTE MUNGU????  - #regrann

Yes! You go Zari, we’re very proud of you!

Regrann from @zarithebosslady –

Wapendwa wangu Sina cha Kuwalipa Zaidi ya kusema ASANTENI sana kwa 4M followers.
Ninyi Ni Ma Ndugu kwangu, Mmekua Nami Bega Kwa Bega Kwenye Shida na Raha. Sasa Mnichiangieni $1 kila mtu tujenge clinic ya wanawake sehemu yoyote dar, Najua tukiipata Baba Magufuli atatupa kiwanja....?? #JustSaying
PENDA SANA NYINYI.❤
THANK YOU SO MUCH FOR 4M. 
LOVE YOU ALL? - #regrann

Yes! That's my lady! Let support our Bosslady, the real Major General! Mimi naanza kwa dola kumi ($10 ), haya baba yangu Dr John Pombe Magufuli tunaomba kiwanja hicho tena kiwe kule maeneo ya Kigamboni, au Kibada, au Mbagala ?? somewhere in Temeke District au Kigamboni please. Zari fungua hizo account watu waanze kumimina hizo pesa please! This is great! And we will call it Zarina Hassan Women Clinic ???? Jamani ni dola moja tu ($1) kwa kila mtu hatushindwi! Ila unaruhusiwa kuchangia zaidi ya hapo! Okowa maisha ya mwanamke uokoe jamii!! Mungu atubariki wote ?

Hoyce Temu: shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ?? Mh. John Magufuli na mkewe Mama Janet

@Regranned from @hoycetemu  -  Done! Mungu ni Mkubwa na kwa Mara nyingine miminatanzania inatoa shukrani za Pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ?? Mh. John Magufuli na mkewe Mama Janet kwa kuchangia milioni 15 ambapo Sasa zikichanganywa na milioni 15 zilizopatikana kutoka kwa watanzania kupitia miminatanzania tutakuwa tumefikia kiwango na hata kuvuka. @wastara84 mdogo wangu, kila la kheri na muamini Allah na usikate tamaa. Hivyo basi mahesabu ni kama Ifuatavyo: Mh. Rais-15m, Miminatanzania 15m, Msamaria mwema aliyeweka kwenye account ya Hospitali India 7m, familia ya Wastara 5m JUMLA ni 42m zaidi ya lengo la milioni 37! Kila la kheri Wastara! Asante Tanzania! ????#tumeweza #jamii

Zamaradi Mketema: Namshukuru kwa yote yaliowahi kutokea kwenye maisha yangu….!

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote waliotenga muda wao kwa mapenzi kabisa kunitakia heri katika siku yangu ya kuzaliwa, kwa kila alieniwish hata kama sijaona nataka utambue NATHAMINI SANA SANA SANA, MUNGU awabariki kwa upendo wenu kwangu na asanteni sana kwa Dua njema Birthday ya mwaka huu kwangu ni kubwa mno na yenye Baraka nyingi, nitakuwa kiumbe wa ajabu kama SITAMSHUKURU SANA MUNGU kwa mengi aliyoyatenda kwenye maisha yangu, hii sio akili yangu, wala sina maarifa ya kuzidi wengine ila huyu ni WEWE MUNGU WANGU. Namshukuru kwa KUNISHIKA MKONO, namshukuru kwa KUNIONGOZA, namshukuru kwa KUNISIMAMIA, namshukuru kwa KUNILINDA NA KUNIPIGANIA, na namshukuru kwa yote yaliowahi kutokea kwenye maisha yangu haijalishi kwa wengine yalikuwa na sura gani lakini naamini mengi ni ngazi ya kunifikisha nilipo. Naendelea kujikabidhi na kukabidhi kila kilicho changu mikononi mwake na kumuomba aendelee kunilinda na kunilindia maana mimi kama binaadamu sina ninachokiweza. Bila kusahau wazazi wangu waliotangulia mbele za haki, Zamaradi wa leo ni taswira yenu, asanteni kwa malezi yenu na asanteni kwa kila MLICHOKIPANDA kwangu, Nawaombea kwa MUNGU aendelee kuwapumzisha kwa amani na awape makazi yaliyo mema INSHA’ALLAH Na kwa kila mwenye mapenzi mema, ndugu, jamaa na marafiki wote mfahamu NAWAPENDA NA ASANTENI SANA SANA.

Dr. Ntuyabaliwe Foundation doing community work in my district!!

” Today I visited a Primary School in Temeke district representing @drntuyabaliwe_foundation to discuss about setting up a school library for them.I was very excited to hear that “Reading(Maktaba)” has been introduced as part of the curriculum this year so our library donations will really help kids to have the right environment for that subject.This school started before I was born and they’ve never had a school library. ” ~~~JNM

I’m happy to see the representative of Dr. Ntuyabaliwe Foundation Jacqueline Mengi a.k.a  Mama wawili doing community work in my district- Temeke! Yes, was born and raised in that district for that thank you Dr. Ntuyabaliwe Foundation for thinking of us. ?

Thank you Jacqueline, Mrs billionaire ??❤

Bodi ya TANLAP yamuaga Dr Judith Odunga!

Bodi ya chama cha msaada wa kisheria- TANLAP (Tanzania Network Of Legal Aide Providers) siku ya leo masaa ya Afrika Mashariki walikutana na kufanya sherehe fupi ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wao Dr. Judith Odunga na kumkaribisha Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Dr. Helen Bisimba. Sherehe hiyo ilifanyika katika hotel ya Millennium Seashells, Dar es salaam, Tanzania........Hongera sana my aunt and shosti wangu Dr Judith Odunga. Tunakutakia retirement njema. Natunaimani kuwa Dr. Helen Basimba atafanya kazi nzuri kwa manufaa ya taifa letu nasio maslahi benafsi!

Dr. Judith Odunga (In white & black outfit) and Dr. Helen Bisimba in aqua blue outfit

The outgoing TANLAP Board Chairperson Dr. Judith Odunga (sitting second left) with the new chairperson Dr. Helen Bisimba (first left) and Christina Kamili (ED) plus other Board Members and TANLAP staff at a farewell party held at the Millennium Seashells Hotel, DSM.  

Huyu ndie Mwalimu wangu aliyenifundisha kuandika!

Leo naomba niwaonyeshe mama yangu kipenzi na Mwalimu wangu aliyenifundisha kuumba herufi, kutofautisha herufi  kubwa na ndogo na wapi pakuzitumia. Kisha akanifundisha jinsi ya kuandika neno moja moja, na jinsi ya kuandika maneno zaidi ya moja ili kuitwa sentence. 

Hili somo lilikuwa linaitwa "Mwandiko" nilikuwa darasa la kwanza pale Mgulani Chini Primary school! Yeye anaitwa Mwalimu Massam, lakini kwa heshima zaidi tulikuwa tunamuita Mwalimu-mama Massam! Kwani kwanza alitupenda wanafunzi kama wanae, alitufundisha kwa upendo na unyeyekevu mwingi sanaaaaaa! Such a humble Mwalimu. Pia alikuwa jirani yetu hivyo kumuita mama ilikuwa si jambo la kushangaza!

Mwalimu-mama Massam

Namshukuru sana kwa msingi wa elimu aliyo tupatia.......Pendo na wadogo zako najua mtasoma huu ujumbe tafadhali naomba mumfikishie ujumbe huu mama yangu. Mungu azidi mbariki sana. Nikija lazima nimtafute. 
#NeverForgetYourRoots 
#MyHumbleBeginnings

 

In loving memory of late aunt-inlaw Janet Anyango Owino!

Yeasterday (East Africa time) the bury and final wedding ceremony of our aunt-inlaw Janet took place in Kagan, Kenya! All of her children from U.S.A, Philippines, and other places were able to attend including all immediate family members and close friends! The village has been shocked and mourning her death as she was mother of many, raising orphans and children of family members for more than 25 years! Her good deeds, kind heart, and pure love was one of its own kind and no one can fill in her space anytime soon!

My International brother-in-law, sister inlaw (daughter to the late) , and Janeth Igogo (daughter inlaw)

 She was the one who raised my 'International brother-in-law' and his siblings (five kids) from the tender age after the death of their mother whom was an elder sister to aunt Janet!......... As she has been laid down in her temporary home; now it's time to celebrate the life well lived with full love and kindness! The Lord gives, and the Lord takes way. Blessed His Holy name! R.I.P aunt inlaw! .....Enjoy the pictures.....

My babysister!….Poleni sana ndugu zangu

My people!

     My International in laws' and my babysister ???❤      

The Nyagilos’ ?❤❤

Readprevious post ?? 
AuntInlawJanet

“MTOTO ANAFUNDISHWA NYUMBANI.”~~~~~`Zamaradi Mketema

TV host Zamaradi Mketema

Kwangu mtoto kufanya hivi sio fahari ni Aibu, Hawa ndio aina ya watoto anakuwa anawaza kitu kimoja tu kichwani mwake, Kumridhisha mwanaume, juhudi zake atazielekeza kwenye kutafuta style mpya, bila kusahau vitu mbalimbali vya kupagawisha wanaume. Na wengi wa aina hii bahati mbaya waliowazunguka wanaendelea kuwatengenezea mazingira ya namna hii, wanakuwa wakiamini MAISHA NI MWANAUME TU, na ili uishi nae nguvu yako uilekeze kwenye KITANDA TU. Asilimia kubwa ya maongezi yao yamejaa hayo akiamini ndio UBORA, wanasahaulishwa kabisa kuwa kuna zaidi ya hayo kwenye maisha, wanabaki na mawazo mgando na kubaki kwenye dunia yao ya peke yao, ndio wale utasikia wanamtukana mwanamke mwenzao eti HUJAFUNDWA WEWE!!

Hapondiohuwainachekeshasababukwabahatimbayaufundajimwingiunaangaliasehemumoja tu and am sorry to say wengi WALIOUABUDU wanakuwa na mawazomgando mno yanayopeleke akuachwa na Dunia nyingine. Wadogozangu kitanda ni muhimu lakini haijawahi kuwasehemu KUU pekee ya UKAMILIFU wa mwanamke ama kumshika mwanaume, na kwa ulimwengu wa sasa kama unachojua ni kitanda tu.kunaathari nyingi utakazo kumbananazo hata katika hiyo ndoa unayoiabudu, na hakuna faida yoyote utakayo ipata, maishani zaidi ya kitanda. Mapenzi ni zaidi ya style mpya! Wamama tunaokuja tujitahidi kutotengeneza kizazi cha aina hii, tunaumiza watoto wetu, wanaishia kuwa malosers, washamba, akili ndogo, na hakuna cha maana kwenye maisha yao. Ninachoamini mtoto hafundwi siku moja, wiki moja, wala mwezi mmoja. Mtoto anaanza kufundwa tangu anazaliwa na katika ukuaji wake, MTOTO ANAFUNDISHWA NYUMBANI, Na ndio mafunzo mazuri au mabaya yanapotokea kulingana na imani unayomlisha, mazingira unayomkuza nayo na hata picha unayoionesha.

Hajawahi tabia mbaya alioishi nayo mtoto ndani ya miaka 13 au 14 ikabadilika ndani ya wiki moja za kumuweka ndani, hakuna!! Atawasikiliza tu lakini kama ana asili ya uchoyo ataendelea kuwa mchoyo, kama ana kaumalaya katakua, n.k Tuangalie RIGHT TIME ya kuwafunza hata hayo tulioamua kuwafunza kama ndio kudumisha mila na tamaduni, hakuna ubaya wa kumfunda mtu anaeingia kwenye ndoa lakini hakuna utamu wowote wa kumfunda mtoto wa miaka 12, 13, 14 au 15 ambae hana pa kuyapeleka hayo mafunzo, na hata hao wanaoingia kwenye ndoa kuna haja ya kuwapa LIFE SKILLS na sio kuwashibisha kimoja tu kisichokuwa na faida ya moja kwa moja katika ndoa yake!! Maisha yana changamoto nyingi sana, tusiwatengenezee utumwa wa akili na kuwafunga humo, kwanza angalia hata watoto ama wasichana wengi waliokulia kwenye imani ya kufundwa na kufundana katika hali ya kuabudu walivyo ama wanavyoishi kwenye jamii zao ama ndoa, kama hajaachika basi ana ndoa ya pili au ya tatu, wengi WANASHINDWA KULINDA NDOA ZAO na mpaka sasa nimefeli kujua kwanini!!

Walichokishiba wao ni kimoja tu. Hakuna bingwa wa malezi lakini mengine tunayatengeneza wenyewe, maana hapo utakuta mama yuko pembeni anashangilia na kupiga makofi huku akiona fahari mwanae anavyoyakata, jamani hata ukate mauno mpaka juu ya dari kama kuna vitu huna na hujielewi na kujitambua HAUTATHAMINIKA hata siku moja kwenye ndoa yako, na hao unaowaita wasiofundwa wataishia kukupiga bao tu kwenye maisha. TUAMKE.

Nilipenda hii…..!

Unajua zawadi sio lazima iwe material things au kitu cha bei kubwa eti ndio iwe na thamani! Kitu chochote kinachoweza mfanya mtu ajione kuwa unamthamini na kujali uwepo wake basi kinafaa kuwa zawadi! Basi hii ndio ilikuwa Mother’s Day gift / msg ya mdogo wangu Magreth kwa mama! Was just a simple msg ambayo inaleta kumbukumbu nzuri ya mambo yaliotekea katika hisia tofauti na ya furaha zaidi! Yote haya aliosema ni kweli kabisa!

Mimi (kushoto), Mama, na Magreth. …..Kalamazoo, Michigan 2012

Katika picha hii ni mama na mdogo wangu Magreth walipokuja U.S.A pamoja na baba mzazi mwaka 2012! Ni moja ya tukio la furaha sana kwangu, kwani kutembelewa na wazazi wangu pamoja na mdogo wangu kwa wakati mmoja was something very special, was really big deal to me! ………..Haya Father’s Day inakuja June 17 tafakari nini cha kumwambia au kumfanyia mzee wako!

Jumbo Camera House ni duka bora kwa mahitaji yako ya Camera za aina zote!

Jumbo Camera House ni moja ya sehemu ambayo nilikwenda nikiwa Tanzania nikapata customer service nzuri sanaaaaaa! Camera yangu ilikuwa inanisumbua kwenye setting na battery  ilikuwa inaisha kwa muda mfupi hivyo nilihitaji wataalamu kuniangalizia tatizo ni nini na pia wanifanyie setting. Kwakweli hawa watu walitufanyia mapokezi mazuri sana japo Camera hatukununua kwako (ilikuwa ni zawadi) hawakutuonyesha “nyodo” za aina yoyote ile! Walikuwa very professional, friendly and welcoming! Tulihudumiwa vizuri sana and Yes! I bought something kuwaunga mkono as all the services walitufanyia ya kuangalia tatizo kwenye battery na ku-program my camera  walisema hatuhitaji kulipa was just free!…….Jamani msifikirie hawa hawatu walikuwa wanatujua hapa!! Hawanijui, na hata mimi na mdogo wangu tulikuwa hatuwajui tulienda kwao as to see kama wataweza kutusaidia, hivyo naamini kama walituhudumia sisi kwa furaha na upendo namna hile basi inanifanya niamini kuwa hivyo ndivyo walivyo kwa wateja wao wote!Hapo ? ni address yao na njia zao za mawasiliano kama utahitaji kupata huduma zao!

“Nimekuweza, Umeniweza, Tumewezana”- Zamaradi Mketema

Zamaradi, I salute you mke mwenzangu! Umenena mama kama mwanamke anaye jitambua na kujithamini! Hands-off ? Angalau sasa nina uhakika kuwa shemeji yangu ana kwakwe sio #Yakhaya ??………. Mungu akujaliye yale yote mema ambayo roho yako inatamani! Lovely!

HATA KWETU TUNAO MALKIA WA NGUVU.  HONGERA SANA MADAM SOPHEY MBEYELA. -Peter Sarungi

 

 Nikiwa kama mwanaharakati wa kutetea haki na kukuza utu wa watu wenye ulemavu, jukumu langu kubwa ni kukusogeza karibu na jamii hii ili sote tujue mazingira ya watu wenye ulemavu kwa kukuonesha changamoto na mafanikio yetu katika kuchangia maendeleo ya jamii. Tunaamini ushirikiano wako kwetu utaongezwa ikiwa utajua mazingira yetu.

Leo natumia jumapili hii kupongeza mafanikio aliyoyapata dada yangu Sophey Mbeyela baada ya kutwaa Tunzo ya Malkia wa Nguvu kwa mwaka 2017 kutoka Clouds Media kupitia kampeni yao ya kuwatafuta Malkia wa Nguvu kila mwaka. Anapenda aitwe Madam Sophey, ni moja kati ya akina dada shupavu, asiye kata tamaa na mwenye kufuata ndoto yake kutoka katika kundi la watu wenye ulemavu. Kazi yake kubwa ni mwalimu lakini pia ni mwamasijashi (Motivator) mzuri sana anaye warudisha vijana walio kata tamaa katika msitari, pia amekuwa akiamini katika kutoa na hivyo ameendelea kutoa misaada mbalimbali kwa jamii yenye mahitaji maalum kama vile watoto na watu wenye ulemavu hasa wanafunzi. Record yake ni nzuri sana kwa jamii yetu ya walemavu na amekuwa akichukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha jamii inapata ustawi.

Nichukue fursa hii kumpongeza sana kwa mafanikio anayo endelea kuyapata na nimtie moyo kwa kusema HAKIKA  HIYO NDIO DUNIA YAKE ALIYOPEWA NA MUNGU, ASITAFUTE DUNIA NYINGINE..

Tafadhali kama unapendezwa na mafanikio haya kutoka katika jamii ya watu weye ulemavu basi andika chochote cha kumpa nguvu Madam azidi kutoa mchango kwa jamii.

HAPPY WOMEN’S DAY 2017- Peter Sarungi

Peter Sarungi (The next Speaker)

 Nitumie siku hii ya leo kuwatakia heri wanawake wote duniani kwa mchango wao mkubwa na wa kutukuka katika kuendeleza dunia. 

Kipekee nimshukuru Mama yangu kipenzi Bi. Martina Sarungi kwa kuendelea kuwa mama bora kwa watoto wake. Nimtakie maisha marefu na yenye furaha na afya tele ili hata wajukuu na vitukuu waje wafaidike kwa busara na maombi yake.

Pia nimpongeze Mama fidel kwa kuchagua kuwa mama mwema na mwenye malezi yenye maadili, nampongeza kwa kuitwa mama na akumbuke kwamba mafunzo yake kwa mtoto wakati wa malezi ndio nguzo kwa mtoto ukubwani. Sipati picha maisha yangekuwaje bila wanawake, fikiria na wewe alafu naamini utajifunza umuhimu wa wanawake duniani.

Leo natoa dedication ya wimbo wa “power of the women” kwa wanawake wote wanao itwa Grace au Neema maana majina hayo yamebeba historia kubwa sana kwangu. Awe ni bibi, mama, dada, mke, mchepuko ama binti yote hayo ni majini lakini yanasimama kwa wanawake. Nawapenda sana na Mungu azidi kuwapa nguvu katika kutimiza majukumu yenu.

Happy women’s Day to all women!

Happy Women’s Day to all women around the world! Let us fight for Women’s rights because women’s rights are human rights we all deserve it and we need it!

MALENGO YA JUKWAA LA WALEMAVU TANZANIA. -na Peter Sarungi

 Nitumie fursa hii kutoa tafsiri ya katiba juu ya Malengo yake kwa kufuata Ibara ya II.C. Malengo hayo yatajumuisha yafuatayo.

  1.  Jukwaa litasimama kama sauti ya kuwakilisha maoni na mapendekezo ya watu wenye ulemavu.
  2. Kusimamia maoni na mapendekezo yanafanyiwa kazi katika vyombo vya serikali, mashirika, almashauri na taasidi mbalimbali wakati wa kuunda sera na sheria katika jamii.
  3. Kuratibu vikao, mikutano na makongamano ya kueneza na kukuza uelewa wa watu wenye ulemavu juu ya sera, taratibu na sheria katika kupata fursa mbalimbali za nchi.
  4.  Kujenga mahusiano na muingiliano mzuri kati ya jamii ya watu wenye ulemavu wenyewe na jamii zingine tukilenga ushirikishwaji katika kutumia fursa mbalimbali.
  5. Kufanya tafiti mbalimbali za maswala ya watu wenye ulemavu kwa kutumia chombo kitakachoundwa ili kutambua changamoto na mafanikio ya utekelezaji wa sheria na sera mbalimbali zinazohusu watu wenye ulemavu.
  6. Kutoa taarifa mbalimbali zenye lengo la kubainisha fursa za kijamii, siasa na uchumi zilizopo kitaifa na kimataifa ili kuhamasisha ushiriki wa watu wenye ulemavu.
  7. Kuratibu uanzishwaji wa vikundi mbalimali vyenye malengo ya kuungana ili kupata fursa za uchumi na jamii ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa majukwaa madogo ya ukanda, mikoa,miji na vijiji katika kueneza sauti ya watu wenye ulemavu.
  8. Kushawishi, kutetea na kukuza haki na wajibu wa watu wenye ulemavu kupitia usimamizi wa sera na sheria No.9 ya watu wenye ulemavu.

Hayo ndio malengo hasa ya kuanzisha Jukwaa hili. Nitaanza kuchambua umuhimu wa kila lengo ili kujua uhitaji wa lengo hilo katika jamii ya watu wenye ulemavu.  

Tafadhali share, like, tag na comment kushiriki katika malengo haya ili jamii na wadau woye wapate taarifa.

Asanteni sana.

JUKWAA LA WATU WENYE ULEMAVU TANZANIA-na Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (The next Speaker)

 Nitumie fursa hii kutoa shukurani kwa wote walio jitolea na hata kufuatilia kwa karibu juu ya uundwaji wa Jukwaa la Watu wenye Ulemavu Tanzania. Mpaka sasa tumekamilisha 95% ya taratibu za kusajili Taasisi hii muhimu kwa walemavu. Jamii ya watu wenye ulemavu imeendelea kutengwa katika mipango mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa sababu ya kukaa kimya bila kusema juu ya changamoto zetu, uwezo wetu, vikwazo tunavyokumbana navyo na hata mafanikio yetu. Ni muda sasa umefika wa kusema kwa nia ya kutetea na kushawishi maswala ya watu wenye ulemavu Tanzania ili na sisi Tanzania tufanane na wenzetu wa Afrika Mashariki walio amua kutekeleza kwa maneno na vitendo mkataba wa UN unao husu jamii ya walemavu na ni mkataba ambao Mh. Mkapa aliridhia na kusaini kisha Mh. Kikwete kuruhusu utungwaji wa sera na sheria no.9 ya watu wenye ulemavu na sasa kilichobaki ni kupiga kelele juu ya utekelezaji wake.

Ni jukumu letu sote kupiga kelele tena bila utengano na kwa sauti moja hata kama wewe sio mtu mwenye ulemavu lakini ukiguswa na hili basi ni sahihi kusema kwa nguvu hadi jamii, serikali na wadau wengine wapate kusikia ujumbe huu. Kuna msemo unasema hivi…

“Mtoto anayelia na kupiga kelele sana ndiye anaye pewa nyonyo na mama yake, ukinyamaza maana yake umeshiba”

Sidhani kama sisi watu wenye ulemavu tumeshiba katika nchi yetu, la hasha ila tuna ugulia kimya huku tukifa na tai shigoni. Ukimya wetu ndio unao tufunga, unao turudisha nyuma, unao tififisha ndoto zetu, unao tukosesha thamani na ndio sababu ya kutengwa na fursa.

Tanzania amka useme jambo kwa jamii hii ili na wewe ushiriki katika kutetea na kushawishi maswala ya watu wenye ulemavu Tanzania.