Rais wa jumuiya ya Watanzania waishio katika jimbo la Houston, Texas Hon. Lambert Tibaigana akielezea kwa kina baadhi ya maazimio ambayo yalijadiliwa na kupitishwa na wana jumuiya hiyo na pia akigusia mambo machache ya msingi ambayo katiba ya jumuiya hiyo imezingatia.
Kama wewe ni Mtanzania unayeishi katika mji wa Houston na vitongoji vyake basi tunakuomba ujiunge na wanajumuiya wengine katika kuiendeleza jumuiya yetu. Tafadhali jiunge na jumuiya yetu, saidia viongozi wetu kwa kumtaharifu kila Mtanzania unaye mjua kuwa anaombwa ajiunge na jumuiya hii kwani inafaida sana kwa vizazi vyetu vilivyopo sasa na vijavyo! Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki THC.
Binti ameungua uso baada ya simu ya mkononi kulipuka usoni mwake! Binti huyu ambaye anasadikika kuwa ni mdogo wake Mansour Yussof Himid na Shadya Karume alikuwa akitumia simu wakati ikiwa kwenye charger nahapo ndipo ilipo mlipukia na kuunguza uso wake vibaya sana kama inavyo onekana kwenye video! Jamani tahadharini kutumia simu ikiwa iko kwenye charge please! Na watoto pia musiwaruhusu kutumia simu mda mrefu zina athari mbaya please!
You may heard the warning before you thought was just a rumor and cared less! Or nobody warned you before and now it’s time to take it seriously! Using cellphone while charging it is DANGEROUS!! It may explode right on your face. See the video attached how that beautiful girl’s face is damaged from using her phone while was charging! Don’t do it!!
Hii issue ya Joyce inasikitisha sana japo siyo jambo lakunishangaza kusikia unyanyasaji kama huo!..... Ma'am, nashindwa hata niandikaje kwani swala la domestic abuse kwa wanawake na watoto ni swala ambalo liko very near and dear to my heart but at the same time very sensitive to me! Niswala ambalo sipendi kuliongelea sana kwani bado linanikumbisha machungu mengi sana haswa kuhusiana na my dearest aunt ambaye ametangulia mbele ya haki!! Bado sijioni kama nina nguvu ya kuliongelea mbele za watu! Siku mwanaume akanyanyua mkono wake kunipiga aisee nitahakikisha hadi mama yake mzazi anapata "ngeo" ya kudumu!! Wala simpigi mimi namkodishia wahuni tu!! Stupid kabisa!! Hii karne ya 21 nani bado anapiga mwanamke?!! Tena hadharani kwenye gari?!! Halafu eti wapuuzi wanasema umekosea kusema hadharani, gosh! Anipige mimi aone mpaka CNN watamjua!.... Siku zote ukiona mwanamke amefikia hatua ya kuongea mambo yake ya ndani hadharani basi jua yamemfika!! Hana pakukimbilia asipo yasema ataishia kujiua!! Siyo kwamba hampendi mumewe hapana anampenda enough kutaka msaada wa nje waweze kumsaidia. You do what is best for you Joyce as long will save your life!! Wewe unafikiri kwanini mimi pia niliamua kuanzisha hii blog yangu?!! Niliona uonevu ninaofanyiwa nawapika majungu na kwakuwa Wabongo wengi ni wepesi wa kuamini uongo kuliko ukweli hivyo nikasema I need my own platform ambayo nitakuwa huru kueleze mambo yangu na kuweka ukweli hadharani ili kila mtu ajue! Niliona jinsi marafiki na ndugu walivyotumiwa kuwa maadui wangu number moja nikasema I am taking it to the public ili waone! Nakama mjuavyo njia ya muongo ni fupi, sasa hivi wenyewe wamefyata mkia! ......Hivyo Joyce usione haya wewe sema tu wenye akili zetu tulinakuelewa sana! Hapo utakuta umeangaika kwa ndugu na hakuna msaada wowote zaidi ya vikao visivyo na mbele wala nyuma! Halafu siku hizi unakuta kila kitu wanaingiza siasa hata maswala ya familia yani kweli siku za mwisho Biblia inasema shetani ataharibu familia na ndoa, na ndio haya tunashuhudia!! Kwanza huyo mumeo nikiongozi sasa kiongozi gani ambaye familia yake tu yawatu ambao naamini hawazidi 10 imemshinda kuongoza mpaka anampiga mkewe sasa ataongozaje jamii yenye maelfu ya watu?!!
Hii issue yako umenikumbusha kifo cha mtoto wa kaka yangu alikuwa anaitwa Joyce Kibindi. Mtoto wa watu aliangaika na mumewe eti ngoja yeye awe mjasiliamali uku amsapoti mumewe kwenda chuo kwani aliamini mumewe akimaliza degree vizuri basi atapata kazi nzuri na hali ya maisha yao itakuwa nzuri kidogo!! Ma'am, how wrong was she!!
Mume kamaliza chuo kapata kazi yenye mshahara nzuri kwani alikumbuka fadhila za mkewe!! Pombe na wanawake ndio walikuwa "mashosti" zake! Mke na watoto hana habari nao kabisa! Mtoto kaangaika kulalamika na kuitisha vikao kwa ndugu, wapi!! Wakina mama nao wimbo ni ule ule vumilia tu yanapita!! Mtoto wa watu alivumilia uvumilivu ukamshinda hakawa haoni pakukimbilia tena ISIPOKUWA KABURI!! At age of 28 with so much to live for Joyce committed suicide!!
Kifo cha Joyce kinaniuma sana mpaka wa leo hii, yani hata hapa naandika machozi yananitoka kwani nakumbuka jinsi alivyokuwa mzuri, smart, charming, very kind lakini maisha yake yalifupishwa because of the failed society!! Yes, hii jamii inayolea wanaume kuwa "cold hearted killers" kwa kuweka mazingira ya malezi ya kunyanyasa watoto wakike ndio inayoleta matatizo haya yote!! Nawakina mama ambao wanashindwa kusimama kidete na binti zao kwa kukemea hizi tabia hadharani ndio wanao ongeza matatizo haya! Embu fikira kama mume wa Joyce angekuwa muungwana angesema kuwa mkewe ndio asome kwanza si Joyce leo angekuwa bado yupo hai na familia ikawa salama! Yani kuna baadhi ya wanaume wa Tanzania wana roho za paka!! Niwakatili sijaona mfano hata hawa walioko huku nje ya nchi wana roho zakishetani!!
Halafu watajifanya kusingizia "siasa"!! Wengine wanataka uongozi wa communities ili tu kuficha maovu yao!! Kwakweli hii inafanya unaogopa hata kumsapoti mtu kwani hizi betrays ni nyingi mno!! ........Sasa baadhi ya wanawake wanaojifanya wasomi ndio wapumbavu hakuna mfano!! Sitaki hata kuwasikia!! Anyway, pole sana Joyce, nakama unajisikia kusema wewe sema tuu usije kufa bure kwa kujifanya shujaa ushwara!! Wewe kuongea haya yote yanakufanya uwe shujaa kwa wanawake wengi tu including me!! Hata Mungu anasema jisaidie kabla sijakusaidia!!
@Regranned from @joycekiriasuperwoman - Changamoto kubwa 2018 #Kipigo
Sikutegemea kama ipo siku kwa mkono wako ungeunyanya KUNIPIGA @kilewo2020mwanga ???? * Ukasahau kabisa! Ukasahau yooooote.. nimeharibu career yangu kupigania ndoto yako kwa kugawa watu wangu kwenye biashara zangu, nimepoteza ndugu jamaa na marafiki, umeniachia nimebeba mzigo wa familia kwa muda wote... Malipo yako ni KUNIPIGA/ KUNIDHALILISHA/ KUNITOA MACHOZI???
Umenipiga kwa sababu Mimi Ni MNYONGE siyo! SINA NGUVU, kwa sababu ni MWANAMKE Sina nguvu za kupigana na MWANAUME ... Umeniumiza mwili wangu unauma kila mahali umefiria damu na kichwa ukanigongesha kwenye gari, ili iweje? Nia yako ilikuwa ninini? kuniua??? Mungu amenipigania.
Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua...?????? Kama NI Mimi niliandamana na watoto, nikakufanyia kampeni na deni kubwa nikaingia mpaka nikafungiwa Kipindi hewami, ninakutunza wewe na Watoto wako kwa miaka yote, MUNGU YUPO.... LEO UMENIPIGA @kilewo2020mwanga ??? Sawa watakusifia hao wanaokusifu ujinga, wanaokuambiaga Mimi sikuheshimu, badala wakwambie ufanye kazi utunze familia, Leo watakuona wewe ni MWANAUME kwa KUNIPIGA... - #regrann
@Regranned from @mutwiba – Wakati Rais akifanya maamuzi ya kuwaachia familia ya Nguza Viking, anafungua mjadala mpya na muhimu wa kisheria na haki Tanzania
Binafsi ningependa kujua ni kipi ambacho Mahakama ZOTE zilijithibitisha “beyond shadow of a doubt” kwamba familia hii ilitenda makosa yaliyosababisha kuhukumiwa kifungo na kunyimwa dhamana na hata msamaha walioomba, na umekuwaje sasa imejulikana kwamba hayakutendeka?Swali la ziada (ambalo siamini kama kuna atakayeuliza waziwazi ??♂) ni kwamba……
Baada ya Rais kujithibitisha kwamba hali haikuwa imetendeka, ni nini kinafuata kwa waliohusika ama mfumo mzima kuhakikisha kwamba hawatokei kina Babu Seya wengine? – #regrann
Watanzania wengi wamefurahishwa na huu msamaha! Sasa imenibidi niwaze je, hukumu yao ilikuwa ya uonevu hivyo wanastahi msamaha huo? au nikosa lingine linafanywa kwa pressure ya jamii nakwa mara nyingine siasa inachembe chembe zake humo?! Mimi binasfi, kulingana na kesi hii ilivyokuwa na maswala yote ya ushaihidi nimeshindwa kujua ni wapi nisimamie!
Maswala ya kulawiti na ubakaji ni maswala nyeti sana, ambapo jamii inatakiwa kuwa makini sana lasivyo watu wazima na watoto wengi wataendelea kufanyiwa huu unyanyasaji bila kupata msaada wowote ule kutoka kwa jamii pamoja na kwenye vyombo vya haki! Stigmazation kwenye maswala haya bado nikubwa sana kwenye jamii yetu; hivyo watu hawapo huru kutoka hadharani na kuripoti mambo kama haya, familia nyingi bado wanaficha mambo kama haya yakitokea kwenye familia zao! Jamii tuwe waangalifu sana kwa hili. Lakini wakati huo huo tusije hukumu watu kwa kuwapa adhabu nzito wakati hawakutenda kosa lolote! Kumbua kesi ya marehemu Michael Jackson wa hapa Marekani! Saa nyingine chuki binfsi huwa zinafanya watu wanasingizia wengine mambo kama haya ili kuwafedhehesha na kuataka kupata pesa!
Vile vile mtu akiwa amekutwa na hatia ya makosa kama hayo ni vizuri jamii na serikali ikawa na utaratibu wa kuwaangalia hawa watu na nyenendo zao zote kwa kipindi fulani. Wasiruhusiwe kukaa na watoto sehemu yoyote ile bila uangalizi wa watu wengine! Nawala wasiruhusiwe kuwa sehemu ambayo kuna watoto kama kwenye shule, sehemu za michezo n.k! Once a convicted rapist always will be! Maybe they were able to get away with it this time, lakini kama kweli hiyo ni tabia yao basi amini watafanya tena! Jamii kuweni macho! Parents beware!…….. Otherwise, hongereni kwa kupata msamaha wa Rais! Mungu ibariki ?? ?
Sasasahivi in our Society tunatengeneza Vijana wengi Lesbians na Mashoga na hakuna anayejaribu hata kuliongelea kwa mapana au chanzo cha hili tatizo ni tatizo kwa sababu we are creating a Society of confused Youths ambao ndio Taifa la kesho! Nilichojifunza Bongo ni hakuna anayetaka kukubali kuwa tunalo tatizo na hakuna anayetaka kuongelea solutions so we are creating a TIME BOMB. Siku moja litakuja kulipuka vijana wetu kuanza kudai ndoa za Jinsia Moja tutaanza kutafutana kurundikana Rumande na Jela kumbe tuna wakati wa kutosha kulirekebisha hili tatizo now!……… As a Society tunatokea kwenye Mila na Desturi ambazo sasa hivi zinapitia a big test of kama ni kweli zilikuwa strong enough from the West Culture ambayo imekuja na sera za Wawekezaji na hasa the Television Culture ambayo Baba wa Taifa aliikataa sana. Sometimes ninajiuliza sana je kwanini Mwalimu alikuwa muoga sana na the Western Culture? Je alikuwa na wasi wasi na how fragile our Culture is?! Maana ukienda Zanzibar hata wao wana Television pia lakini Mila na Desturi kwao hazijaharibiwa na Western Culture kama sisi huku Bara it is a FACT! ndio maana hapa mjini mitaa yetu imejaa watoto wasiokuwa na wazazi as opposed na Visiwani, wenzetu hawana hilo tatizo ……….Tanzania tumefanikiwa sana ku maintain Swahili as our Language na ni by the Fact that tulishituka mapema na kuunda Baraza la Kiswahili now nashangaa kwanini hatukuunda mapema chombo cha kusimamia Maadili na Utamaduni wetu au huenda tunavyo lakini they are toothless!………Vijana wetu wa sasa hawawezi kubeba na kuyakubali Maumivu ya Maisha ambalo ni tatizo namba moja la The West. So kule kuna Chama cha wamiliki wa Bunduki kinaitwa NRA ambacho agenda yake ni kubwa sana Dunia nzima kwa kushirkiana na NGO za Mashoga na Lesbians kule Holywood kama ulikuwa hujui wao ndio wamiliki wakubwa wa the Culture of Television ambayo unamuachia mtoto wako mdogo huku Bongo kuangalia siku nzima ………. Usichokijua kipindi cha TV cha Dakika 15 to 30 kinalazimishwa kutoa maswali na majibu ya maisha kwa matatizo ya vijana ndipo hao NRA huingiza agenda ya kutumia Bastola au kubadili jinsia kama the Kardeshians! TUKATAE HUO UTAMADUNI! – le Mutuz –
Jamani najua nipo break lakini hili tangazo pamoja na hukumu ya Lulu imenibidi leo ni blog ?? wapenda “ubuyu” utatujua tu ?? ……Jamani kesho msikose kusiliza asubuhi na mapema saa za Afrika Mashariki baba Shubi atanguruma Live bila chenga kwenye Clouds 360! Mie nitamsikiliza jioni ya huku Texas, Marekani hivyo kama kuna cha kusema nitasema siku ya JumaTano! …….#Usikose
Wiki kama mbili zilizopita muingizaji wa kimataifa Lupita Nyong’o alikuwa ni mmoja wa wanawake waliojitokeza hadharani nakusema kuwa naye ni mmoja wa wanawake waliotaka kufanyiwa unyama na Weinstein Harvey! Wapendwa mambo haya yanatendeka sana hata kwenye jumuiya zetu siyo tu kwa celebrities peke yao! 
Kama wewe ni mtoto wa kike au wakiume ambaye umepitia hili tatizo la mtu kukuomba mapenzi ndio akusaidie au kwasababu amekusaidia naomba ujue kuwa hauko peke yako nawala usiiogope kusema hadharani. Ni muda sasa wakuwaumbua watu wote wenye hizi tabia. Hakuna mtu anatakiwa kufanyiwa unyama wa namna hii kwasababu yoyote ile!
Kuna wengine ni marafiki umemuamini rafiki yako kama hapo Lupita alivyofanya kumuamini rafiki halafu anakubadilikia!! Ni muda sasa wakuwasema hadharani!! Wasichana wengi wanateseka na hawa watu kwasababu wengi wa hawa watu ni wanaume ambao wamejijengea uwezo mkubwa wa kuaminiwa kwenye jamii kama huyo Weinstein Harvey! lakini hii ni karne ya 21 huna sababu yakuogopa tena kwani watu wengi kwenye jamii wamechoka na watu wenye hii tabia. Kama Joe Biden alivyo ongea hapa kwa hasira…..msikilize
Halafu hakuna kitu kinaniuma kama kuona wanawake ambao kwakujua kabisa wanaamua kutumika kuwakandamiza victims!! Hivi kama angekua ni mtoto wake au mdogo wake ungefanya au kusema hayo anayo yasema! Any kind of abuse hurts, itakuwa sexual abuse!?! So sad!
Wenye ujasiri wa kuongea hadharani ndio utapigwa vita kwa nguvu zote na kuzushiwa kila aina ya uwongo kama akina Alpha hapa! Lakini mimi siku hizi nimekubali kuchukiwa lakini nitasimama kwenye ukweli!! As a victim of abuse I can’t afford to see any woman going through the pain and suffering I went through!! #Silent is Complicity!!
“We are blessed to set up the first locally owned Call Centre in Tanzania. Utel Global Co. Ltd to be launched on 01st Nov, 2017 Is your business at stake because of insufficient customer support? We can bridge the gap between you and your customers with our 24×7 call center phone answering services. Start experiencing increased sales and better conversion rates along with the satisfied customers. Please Find us at PPF Tower 3rd Floor.”~~~~Utel Global team Mrs Janeth Igogo-Nyagilo Utel Global representative
Nimesha sema mara nyingi na siku zote nitasema kuwa mimi si mwanasiasa nawala sitegemei kuingia kwenye siasa, na wala hata siku moja sitamtetea mwanasiasa yoyote yule! Mambo ya siasa nawaachia mwanasiasa wenyewe wateteane! Lakini naomba ieleweke kuna mambo ambayo yataniwia vigumu kunyamaza kama hill la kwenye video! Nahapa nitaongea kama Mtanzania, na kama mama! ……….Kwakweli hili swala limenihuzunisha sana! Hii hali siyo yakukubalika haswa katika karne hii ya 21! Nikiwa kama Mtanzania niliyezaliwa katika mazingira duni na wengi wa ndugu zangu bado wanaishi kwenye mazingira duni hivyo, hawa watoto licha ya kwamba ni Watanzania yawezekana pia wakawa ni watoto wa ndugu zangu!! Hivyo siwezi kunyamaza kwa hili! Lazima jambo kama hill linalo hatarisha maisha ya watoto zetu likemewe na lipigwe marufuku mara moja!! Ni juzi tu tumepoteza watoto 32 wa LuckyVincent sec school (somahapa) halafu bado tu mambo kama haya ambayo yanahatarisha uhai wa watoto wetu hayajakemewa na kuweka sheria kali!?! Ni lini tutajifunza kuzuia majanga na siyo kutibu!! Watoto wanatakiwa kwenda shule kusoma siyo kutafuta na kubeba maji visimani!! Huu ni unyanyasaji wa watoto na kuwakatisha tamaa ya kusoma!! My brother Paul Makonda nimesikia hii ni Kinyerezi ambapo ipo ndani ya Mkoa wako, tafadhali naomba ufatilie hili swala!
A must watch to all African men!! Hii video niliiona almost two months ago, but nikawa nasubiria a “proper” day kuiweka. Sasa kwakuwa bado tupo kwenye furaha ya maadhimisho ya mtoto wa kike duniani basi nimeona ni vyema kuiweka! Kwakweli huu ni ukweli kabisa! Watoto wa Africa haswa wakike wamewekwa kwenye “pressure” of how to become a good citizens, great mothers, wives, sisters, and aunties bila kujua kuwa it always takes two to tangle!! Unakuta mtoto wa kike very well organized mentally, spiritually, physically, na hata financially lakini anaangukia kwenye mikono ya mwanume asiye jielewa kabisa!! Mnyanyasaji na mambo mengi ambayo yanafanya maisha yao kutokuwa na furaha! A totally unprepared man for familyhood!! Na ukijaribu kuuliza hawa wadada utasikia ma’am! “All men are the same”!! Hivyo hakuwa na chaguo zaidi ya ku settle down for less!! ………Wazazi, waleeni vijana wenu ukijua kuwa kesho atakuwa mume wa mtu, mmoja ya wana jumuiya hivyo lazima awe teyari kuwa good citizen! Kuwa na hela doesn’t make someone a good citizen or good husband tabia yake na malezi ndio vitaeleza huyo kijana wako ni mtu wa namna gani! Nimeona vijana wenye pesa na ni wanyanyasaji wa wanawake mpaka inaogopesha! Wengine ni rapists and molesters! Tuwalee watoto katika njia ipasayo ili wasiwe mzigo kwa wengine na taifa analo ishi ni jukumu lako wewe kama mzazi!
“Kinachoendelea muda huu hapa Tarime, kongamano linalohusisha Wazee wa Mila, watoto wa kike, na wadau wa Maendeleo – Siku ya mtoto wa kike 2017 ni ??… Unapitwaje jamani.. kauli mbiu ni “Tokomeza Mimba za Utotoni kufikia uchumi wa viwanda.. Wewe unawalinda vipi watoto ???? Ni jukumu letu sote ?” Joyce Kiria
“Please help me vote for my mama, the most outstanding woman in media, period!! Click link to vote http://www.intombie.com/vote.html“~~~~~ Jokate Mwegelo
Nawauliza walimwengu wa Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla, yuko wapi Jokate wangu???? Mimi sitaki matani ya hivyo!!! Siku zaidi ya kumi hajaonekana yuko wapi?? Na nini mbaya imemkuta?!! Kamanda Sirro, please check on my baby sister please!! Kaka yangu Paul Makonda nakuomba unitafutie Jojo wangu, tafadhali hii siyo powa kabisa!! Jojo, I miss you beautiful where are you my babysister? Please, I want to see your beautiful face and cute smile please!! I hope you’re well wherever you’re! Let me know baby girl! Love you ??
Haya leo nawaletea designer mpya anakwenda kwa jina la Bonuzi! Nimeangalia kazi zake nimeridhika nazo. Ndio maana namleta kwenu. Tafadhali m-follow kwa Instagram yake na uweze kujionea mwenyewe! Safi sana!
Haya sale ya nguvu kwa wale wanaopenda vitu vizuri vya kupendezasha nyumba na vyumba vya kulala! Nikutoka kwa Molocaho furniture by Amorette! Sale inaanza kesho asubuhi September Mosi (Sept.1st) masaa ya Africa Mashariki na kumalizika September 8th. Wahi kesho ujipatie furniture zenye ubora wa kimataifa kwa bei karibu na bure! Halafu siunajua asilimia fulani ya mauzo inakwenda kwenye ule mfuko wa kusaidia jamii wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation! Basi nenda kaunge mkono tusaidie jamii yetu!
Tunaendelea kutoa elimu mpya kwa jamii inayo zunguka watu wenye ulemavu ili kuondokana na fikra potofu.
Alhamisi 24/8/2017 Asubuhi ya saa mbili tutakuwa mubashara Azam Two tukijadili mada isemayo;
“Je nini kifanyike ili kuendeleza ustawi wa jamii ya watu wenye ulemavu nchini??”
Karibu tujadili na kujifunza wote. Kama una maoni, maswali na hata ushauri kuhusiana na mada hii una ruhusiwa kushiriki katika ukurasa wangu wa fb na tutazisoma hewani mubashara.
Karibu #ADDfriends tujenge ustawi mzuri kwa jamii ya walemavu.
Zari, this is all for you. I want you to take a moment and watch these clips or you can watch the whole episode on YouTube and see if you can relate yourself to Evelyn Lozada or learn something worthy to apply in your life! I see the “bling bling ” is off again! Not sure for how long will it be this time!!
Nilipoanza na 10 days wallahy sikujua kama zitaenda fast kiasi hichi… Zimebaki 3 days yaani in other words tuna masaa 72 tu yamebaki… Wow…!!! Wow…!!! Wow…!!! Najua kuna walio mbali na wanajiuliza watapataje pataje kuona hii Kazi ya mikono yangu… Jibu kamili ni WemaApp tu… Will make sure unafanikiwa kujionea kazi hii kiganjani mwako… Ama nene… Lakini Pia, pale Mlimani City Tunaenda kwa Slogan moja tu ambayo ni, “Are you invited..???” Kama hutopata chance siku hio basi kutakuwa na After party …. Details zote ntawaletea Baadae…. ??? #RoadToHeavensentPremiere