Category Archives: Awareness!

Walk for autism!

Kesho ni siku ya Autism duniani. Ni siku ua kuelimisha jamii zinazo tuzunguka juu ya ugonjwa huu, na changamoto ambazo wazazi pamoja na watoto wanazipata!……..Mwaka jana nilitoa ahadi ya kushiriki matembezi haya (Autism ) lakini kwa bahati mbaya kutoka na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wangu sitaweza. Mungu wangu anajua kuwa ninajali na ninaomba afungue njia kwa madaktari waweze kujua chanzo cha ugonjwa huu na tiba yake! ………..Tafadhali, kama unaguswa basi shiriki matembezi haya kesho nawe utabarikiwa sana!

Women to women is an event you don’t want to miss it out!

MALENGO YA JUKWAA LA WALEMAVU TANZANIA. -na Peter Sarungi

 Nitumie fursa hii kutoa tafsiri ya katiba juu ya Malengo yake kwa kufuata Ibara ya II.C. Malengo hayo yatajumuisha yafuatayo.

  1.  Jukwaa litasimama kama sauti ya kuwakilisha maoni na mapendekezo ya watu wenye ulemavu.
  2. Kusimamia maoni na mapendekezo yanafanyiwa kazi katika vyombo vya serikali, mashirika, almashauri na taasidi mbalimbali wakati wa kuunda sera na sheria katika jamii.
  3. Kuratibu vikao, mikutano na makongamano ya kueneza na kukuza uelewa wa watu wenye ulemavu juu ya sera, taratibu na sheria katika kupata fursa mbalimbali za nchi.
  4.  Kujenga mahusiano na muingiliano mzuri kati ya jamii ya watu wenye ulemavu wenyewe na jamii zingine tukilenga ushirikishwaji katika kutumia fursa mbalimbali.
  5. Kufanya tafiti mbalimbali za maswala ya watu wenye ulemavu kwa kutumia chombo kitakachoundwa ili kutambua changamoto na mafanikio ya utekelezaji wa sheria na sera mbalimbali zinazohusu watu wenye ulemavu.
  6. Kutoa taarifa mbalimbali zenye lengo la kubainisha fursa za kijamii, siasa na uchumi zilizopo kitaifa na kimataifa ili kuhamasisha ushiriki wa watu wenye ulemavu.
  7. Kuratibu uanzishwaji wa vikundi mbalimali vyenye malengo ya kuungana ili kupata fursa za uchumi na jamii ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa majukwaa madogo ya ukanda, mikoa,miji na vijiji katika kueneza sauti ya watu wenye ulemavu.
  8. Kushawishi, kutetea na kukuza haki na wajibu wa watu wenye ulemavu kupitia usimamizi wa sera na sheria No.9 ya watu wenye ulemavu.

Hayo ndio malengo hasa ya kuanzisha Jukwaa hili. Nitaanza kuchambua umuhimu wa kila lengo ili kujua uhitaji wa lengo hilo katika jamii ya watu wenye ulemavu.  

Tafadhali share, like, tag na comment kushiriki katika malengo haya ili jamii na wadau woye wapate taarifa.

Asanteni sana.

WIZARA INA MIKAKATI GANI JUU YA WATU WENYE WALEMAVU TANZANIA?- Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

Watu wenye ulemavu ni moja ya jamii iliyo katika makundi nyonge (kwa sasa tumefika milioni 4 kwa idadi). Makundi mengine ni kama wazee, watoto na wanawake, makundi haya yanaitwa ni makundi nyonge kwa sababu yana mahitaji maalumu ya kibinadamu na hayawezi kumudu ushindani ulio sawa katika jamii hivyo ni lazima jamii pamoja na serikali iyatizame kwa jicho la tatu lenye utu, huruma na upendo ili nao wajione wapo katika nchi yao na waweze kuonesha uwezo wao ambao Mungu amewakirimu pasipo kujali mapungufu waliyo nayo. 

Peter Sarungi akiwa na dada zake; Alpha Igogo (kushoto) na Magreth Igogo (kulia) nyumbani kwa Peter huko Chanika.

Mimi ni Mlemavu lakini hata wewe ni Mlemavu mtarajiwa maana kama bado unaishi duniani basi jua Mungu bado anaendeleza uumbaji wake kwako. Hivyo linapotokea jambo linalohusu ulemavu basi jihisi na wewe ni mhusika kwa namna moja ama nyingine.

Katika uchaguzi uliopita 2015, nilitoa tamko kupitia jumuiya za watu wenye ulemavu Tanzania ambao ulilenga kueleza changamoto za walemavu pamoja na mapendekezo yake. Changamto kuu nilizoziainisha kwa msisitizo ni ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika vyombo vya maamuzi pamoja na muundo wa kusimamia maswala ya watu wenye ulemavu. Niliamini kuwa ili kutibu changamoto hizi za elimu, ajira, afya, uchumi, siasa na huduma zingine ni vizuri tukashirikishwa katika kupika chakula na kukiandaa mezani.

Nilifarijika sana baada ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza baraza la Mawaziri pamoja na muundo wa wizara zake, kwa kweli mhe. JPM alitutendea haki ambayo haikuwahi kutendwa na tawala tangu kupatikana kwa uhuru wa nchi. JPM alisikia kilio cha watu wenye ulemavu kwa kutenga wizara itakayo husika na maswala ya walemavu tena ikiwa chini ya ofisi ya waziri mkuu kama tulivyotoa kwenye tamko na pia akateua waziri mwenye asili ya ulemavu (dr. Abdallah posy) na makatibu wa wizara wawili wenye ulemavu akiwemo mwanasiasa Amon Mpanju ili kushiriki kupika chakula cha walemavu. Hakika baada ya uteuzi huu, jamii ya qatu wenye walemavu tulianza kuona nuru na kuona matumaini ya kula chakula tulichoshiriki kukipika na kukiandaa mezani. Nampongeza sana Raisi kwa moyo huu wa kujali makundi manyonge katika jamii(Mungu azidi kumpa afya tele na azidi kutetea wanyonge kama anavyofanya sasa)

TATIZO NI NINI?????

Kwa mtazamo wangu, bado naona hakuna mabadiliko chanya yanayoletwa na wizara hii hasa kutoka kwa waziri husika Mh.Posy. Bado mifumo ya unyonyaji imeendelea kuwepo kwenye vyama vya watu wenye ulemavu, bado uchumi umezidi kudorora kwa watu wenye ulemavu, bado Elimu imekua duni na garama kwa watu wenye ulemavu, Bado siasa haiwatambui watu wenye ulemavu kwa vitendo, Bado sheria No 10 ya watu wenye ulemavu imewekwa kando, Bado ajiri imekuwa ngumu na ya kubagua watu wenye ulemavu na bado huduma bora imekuwa ni kitendawili kwa watu wenye ulemavu.

Je ni nani wa kututetea? Ni nani wa kutusemea kama sio Mh. Posy na wenzake akina stella ikupa, Dr. Macha, Amina Mollel, Amon Mpanju na wengine walio katika kundi hili?. Ni nani wa kulaumiwa ikiwa JPM ametupa nafasi kupitia hawa wenzetu alafu wamekaa kimya? Ni nani wa kuonesha mfano na kuaminisha jamii juu ya uwezo wetu kama sio akina Posy, Mpanju, macha, stella na wenzake? Ni nani wa kupiga kelele juu ya mateso na manyanyaso wanayoyapata wafanyabiashara walemavu wa Tanzania kama sio akina Mh. Posy, Mpanju na wenzake waliopata fursa? Ni nani wa kutuunganisha watu wenye ulemavu na kupata fursa za uchumi na siasa kama sio hawa walio teuliwa na JPM? Mbona wamejisahau utafikiri hawajatoka katika kundi hili? Au wanadhani fursa waliyopata ni kwaajili yao peke yao? Au ndo kusema ni aibu na dhihaka kuwa mlemavu na kutetea jamiiyako? Mbona kasi ya JPM inawaacha mbali? Tatizo ni nini?

Tulikaa kimya na kuwapa ushirikiano ili kuona matunda ya kushirikishwa katika kupika chakula lakini inakaribia mwaka sasa hatuoni kama chakula mnachotupikia ni kizuri…

Tafakarini na chukueni Hatua…. 

Tafadhali, naomba ifahamike yakuwa hii article iliandikwa wiki mbili zilizopita wakati Dr. Posy akiwa bado ni Waziri. Lakini sasa nafasi yake ipo wazi!

Ubaguzi wa watu wenye ulemavu nani alaumiwe na nini kifanyike?!

Hongera sana shule direct kwa jitihada zenu za kuokoa maisha ya watoto katika nyanja ya elimu!……Binafsi najiuliza hivi nani wakulaumiwa na nini kifanyike juu ya watu wenye ulemavu?! Mimi nasema ni ubaguzi wa wazi wazi kwa watu hawa na jamii imelifumbia macho! …….Miaka ya nyuma tulisema kuwa watu hawana uwelewa na leo hii je tunasemaje?! Shule moja ya secondary ya viziwi tena ni private?! Majengo mengi yanajengwa bila kujali kuwa tunao walemavu katika jamii yetu!! Majengo na maeneo mengi hakuna parking za magari specific kwa walemavu! Makanisa mengi sana hayana wakalimani wa viziwi! n.k………Huu ubaguzi ni mpaka lini? Nani wakulaumiwa? Na nini kifanyike? ……..Tafakari na chukua hatua!

Malezi ya watoto na changamoto zake!

Pole sana mpendwa, tunamuombea uponyaji wa haraka! …….tukio hili limenikumbusha jinsi my cousin brother alivyo “piga pasi” tumbo lake!  kaka yangu alikuwa na tabia ya kunyoosha sehemu za shati lake ambazo zimejikunja huku akiwa teyari amevaa!! Kumbe mtoto anamuangalia na siku moja akachukua pasi iliyokuwa yamoto Akanyoosha tumbo lake! It was an awful experience! He was  2.5 yrs old by then sasa hivi anakwenda miaka 30 na sidhani kama anakumbuka hilo tukio!…….Anyway, malezi ya watoto yana changamoto nyingi sana. Wewe mzazi unaweza kuwa makini lakini watu unao ishi nao wakawa ni majanga! Nikuomba Mungu tu kama una amini kuwa Mungu yupo!…..Juzi nilisimuliwa kisa cha mtoto wa cousi-sister wangu ambaye house girl alimfungia ndani ya nyumba akiwa amelala halafu yeye akaenda shule kumfata mtoto mkubwa, with a assumption kuwa “atawahi kurudi”! Too bad alipofika shule, siku hiyo walikuwa wamekwenda picnic picnic wakawa wamechelewa kurudi ikabidi dada wa kazi amsubiri! Mtoto aliye achwa nyumbani he is barely 3 yrs old!! Aliamka usingizini haoni mtu ndani ya nyumba! Mtoto kalia mpaka kachoka ma njaa juu! Mama mtu anarudi nyumbani anakutana na hayo majanga! Yani ni alimfukuza house girl siku hiyo hiyo!…..Sasa can you imagine kama moto ungewaka ndani ya nyumba na mtoto kachwa mwenyewe? Au mtoto angechezea jiko la gas ambalo wanalo hapo ndani! Hivi ingekuwaje?! . ……Malezi ya watoto yanahitaji maombi ya ziada kwani bila Mungu hatuwezi!

MATOKEO YA KELELE ZA #BringBackBenAlive NI YAPI NA YAMEISHIA WAPI?- Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Watu wa Makabila yanayo patikana mkoa wa Mara (Kwetu Pazuri) wana desturi ya kuwa jasiri, wakweli na wenye uwezo wa kusimamia jambo analo liamini. Lakini huku jijini Dar tulipokuja kutafuta maisha, mambo yake yanaendeshwa kwa usanii, unafiki, uoga, dilli, uongo na kutafuta kicky pasipo sababu ya msingi.

Uozo huu umeingia hadi kwenye siasa kiasi kwamba huwezi kutofautisha siasa za chama tawala na zile za Upinzani yaani wote wamekuwa wafuasi wa mambo hayo ya jijini.

Wahusika Tuelezeni, kwanini mpo kimya kwa swala mlilo lianzisha? na mtuambie matokeo chanya ya #Bring_Back_Ben_Alive ?

Msianzishe kampeni katika mitandao halafu mkaziacha katikati bila kujua hatima yake, What if Ben amedhurika? Kelele zenu na ukimya wa Ghafla utakuwa umemsaidia nini Ben? Tafakari, Chukua hatua… 

lazima tusimame na kusema, tulinde na kutetea wanyama!….Join the march for elephants and rhinos 2017!

Tafadhali Watanzania wote wakubwa kwa wadogo, ungana na mabalozi wa wanyama katika matembezi makubwa yatakayo fanyika mapema mwaka huu kupinga ukatili wanaofanyiwa wanyama haswa Tembo na Faru! Hatuwezi fumbia macho issue ya Faru John na wengine wengi ambao wamefanyiwa ukatili na unyama wa hali ya juu na hawa majangili na waujumu uchumi!! Hawa wanyawa siyo tu fahari yetu bali ni sehemu yetu sisi Watanzania! Hivyo hatuna budi kuwalinda na kuwatete kwa nguvu zote!…….. Ukitaka kujua  watu au jamii ina upendo kiasi gani basi angalia jinsi wanavyo ishi na kuthamini wanyama na mimea! Ukiona familia haina hata Paka au hata ka-ua ndani ya nyumba basi jua upendo ndani ya nyumba hiyo umepowa sana! Nilazima tusimame na tuseme, tulinde na kutetea wanyama wetu! Niwajibu wetu kama taifa! Join the movement now! 

Kumbe na huyu ni shemeji..!

Kumbe na huyu kimbau mbau mwiko wa pilau ni shemeji yangu ?? Yani wewe Max ndio unasumbua kichwa ya baba yangu Dr Magufuli na #FreedomOfSpeech? Utafikiri unaijua vile ??? Kama  kweli wewe unapigania hiyo “huru ya kujielesa”  (in Luo’s voice)   mbona siku ile yule “mwanaharakati” nyenzio alianika wewe na familia yako aka bandika na picha ya mutoto yako kwa mtandao yake ulipiga magoti yako kwa nguvu sana ukaomba msamaha akutoe kwa blog yake nakuwa hauto rudia tena kumuongelea??? Kwani hile haikuwa #FreedomOfSpeech ??  Au nyie hii ya kwenu  ina “discrimination”?? ????? •••••• Anyway pole kwayalio kukuta binafsi sipendi kuongelea mambo ambayo yapo Mahakamani kwani tuache Mahakama zifanye kazi zake bila kuingiliwa na mtu yoyote kwa uhuru na uwazi! Lakini hata hivyo naamini haya yataisha na punde utakuwa huru! And you and your #FreedomOfSpeech can go away ???

 

Happy 70th Annivessary to UNICEF! Thank you for serving and protecting children!

screenshot_2016-12-14-10-46-15-1screenshot_2016-12-14-10-44-58-1screenshot_2016-12-14-10-45-37-1screenshot_2016-12-14-10-45-28-1screenshot_2016-12-14-10-44-04-1screenshot_2016-12-14-10-44-21-1screenshot_2016-12-14-14-48-03-1screenshot_2016-12-14-14-41-26-1screenshot_2016-12-14-14-48-26-1

“Tulinde na kutetea haki za makundi mbalimbali kwenye jamii yetu”-Jokate Mwegelo

screenshot_2016-12-10-21-00-49-1screenshot_2016-12-10-20-45-20-1Asante mrembo wetu kwa kutukumbusha hili swala la kuwatetea na kuwalinda wasio na watetezi! Binafsi siyo kwamba najisifia lakini nimejikuta nikifanya hivyo bila hata ya kumjua mtu huyo najikuta nimesha vaa viatu vya muhusika na kuanza kumpigania! Sipendi watu wanao onea wenzao bila sababu ya msingi! Kama yule Muhaya  Ruge wa Clouds  FM na loser wake walivyo muonea Lady Jadee ??? Nipo very sensitive na maswala ya unyanyasaji kwa binadamu yoyote yule ……..asante sana kwa kutukumbisha!

Siku ya haki za binadamu duniani: “Tuanze kusafisha nyumba zetu kwanza”-Mh. Samia Suluhu Hassan

screenshot_2016-12-10-18-01-57-1

Leo ilikuwa siku ya haki za binadamu duniani ambapo kitaifa kwa Tanzania yamefanyika katika viwanya vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam na mgeni rasmi alikuwa Mh. Samia Suluhu Hassan! Ujumbe wake kwa taifa amesema kuwa tuanze kwa kusafisha nyumba zetu kwanza hivyo kuondoa wala rushwa, watumishi hewa, n.k ni LAZIMA!!………. Hata mimi naungana na mama yetu kuwa tusafishe kwanza kwani mizizi ya hawa watu ilikuwa mikubwa na mirefu sana, kama haito ng’olewa basi itakuwa kazi bure kabisa!! Mtu yoyote yule mwenye akili timamu hata siku moja hawezi kuvaa nguo safi kwenye mwili mchafu naye akaridhika! Hapana! Ni lazima ata OGA kwanza atoe na UKURUTU wote alionao mwilini ndipo avae nguo yake safi hata kama siyo mpya! SAFISHA! SAFISHA!screenshot_2016-12-10-18-07-00-1screenshot_2016-12-10-18-03-23-1 screenshot_2016-12-10-18-04-21-1 screenshot_2016-12-10-18-05-03-1 screenshot_2016-12-10-18-05-16-1 screenshot_2016-12-10-18-05-43-1 screenshot_2016-12-10-18-06-16-1screenshot_2016-12-10-18-02-46-1,

Ukimwi upo lakini tiba yake hakuna!

fb_img_1480632006861Leo ni maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani! Jamani, tunakubali yakwamba UKIMWI ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine lakini tofauti yake ni kuwa UKIMWI HAUNA TIBA NA UNAWEZA KUUEPUKA! Kama unao basi wewe fata masharti ya kula vizuri na kuzuia kuambukiza wengine, kisha mwombe Mungu akupe hekima na amani kwa maisha yako kama wengine kwani wote hapa duniani tunaishi kwa “matumaini” hakuna ajuae atakufa lini, wote sisi ni marehemu watarajiwa!

 #UkimwiUpoLakiniTibaYakeHakuna

#Unaepukika

Say no to violence against women! /Kemea unyanyasaji dhidi ya wanawake

screenshot_2016-11-25-10-19-16-1Leo siku ya kupiga vita dhidi ya unyanyasaji wa waina yoyote ile juu ya wanawake! …..Naamini watu wengi wanafikiria kupiga mwanamke ndio unyanyasaji pekee unao tambulika. Hapana! kupiga wanawake ni tatizo sugu sana Africa ndio maana unalisikia mara kwa mara. Na pia nitatizo ambalo watu wengi wako na hiyaria au comfortable kulizungumza hadharani! Lakini ukweli kuna unyanyasaji wa aina nyingi sana kwa wanawake! kama vile (1) unyanyasaji wa ngono / Sexual abuse  (2) Unyanyasaji wa maneno / Viable abuse  (3) Unyanyasaji wa hisia / emotional abuse  (4) Unyanyasaji wa fikra / psychological abuse  (5) Unyanyasaji wa kiuchumi au kifedha / financial abuse (6) unyanyasaji wa jinsia ya kike  / female gender abuse, (7) unyanyasaji wa kiroho / spiritual abuse (8) unyanyasaji wa kutumia nafasi yake aliyo nayo / power abuse na mwisho ndo huo ambao ni common sana kwenye macho ya watu (9) unyanyasaji wa kimwili / physical abusescreenshot_2016-11-25-16-04-03-1Binafsi hili swala la violence against women linanigusa sana na niko very sensitive nalo kwani nimeshuhudia sana kwa ndugu, jamaa, marafiki na hata mimi mwenyewe. Kwa mfano mwanaume anapo tumia positive image ya kuonyesha jamii kuwa anakupenda na watu wakaamini hivyo kutokana na “image” ambayo anaiweka mbele ya jamii kisha akafanikisha ku’-gain power na trust kwa jamii wakati ukweli huyo mwanaume hata salamu ndani ya nyumba hakupi! Huo  ni unyanyasaji wa kifikra , kihisia, na power abuse. Unyanyasaji wa aina hii unatendeka sana hasa Africa lakini watu hawapo huru kuzungumzia kwasababu society in somehow wame u-legalized  it!! Ni vigumu kwa mwanamke wa Africa ajitokeze mbele ya jamii na kusema huyu mume wangu ananinyanyasa wakati picha iliyopo machoni pa jamani  ni happy family! Jamii ndio itakuwa ya kwanza kumuhukumu japo yeye ni victim!screenshot_2016-11-25-16-04-37-1Nilishawahi wahi sema huko nyuma kuwa haya matatizo ya jamii yatatatuliwa au kukomeshwa na jamii husika. Jamii lazima iseme enough is enough!!……Na jamii ni nani?! Jamii ni wewe na mimi!! Usikubali kuwa sehemu ya hii laana ya unyanyasaji juu ya wanawake. Kemea hadharani na elimisha watu wote wake kwa waume kuwa hili halikubaliki! #ItBeginsWithYou

Wajibika program by NBC

screenshot_2016-11-24-11-30-41-1screenshot_2016-11-24-11-30-36-1Tafadhali naomba ifahamike yakuwa mimi  binafsi (Alpha) sijui kitu chochote kuhusu hii program japo nimeona ni nzuri. Hivyo mtafute Jokate Mwegelo #Kidoti au wakala wa NBC wakuelimishe zaidi kabla ya kujiunga. Asanteni kwa kunielewa. screenshot_2016-11-24-11-31-48-1

***Another rape Technique in Town. Ladies pls be careful***

fb_img_1479843335255I am just doing my part of sharing the information that I have received hoping it might help someone.

 

***Another rape Technique in Town. Ladies pls be careful.***

A woman was taken by 5 men, who according to hospital and po lice report was raped by a gang before being dumped at a bus
station!

Though she was unable to remember the events of the previous evening, tests conducted revealed that she had been raped repeatedly.

There was a trace of Rohypnol in her blood.

Rohypnol, is presently being used as a date rape drug.

It is actually a small sterilization pill which is now being used by rapists to drug their targets at parties.

The drug makes the mind of the target (would be victim) go blank so that she does not remember anything that transpired and worse still, the drug sterilizes the victim so that she doesn’t conceive from the rape and the rapist need not worry about having his identity revealed later by a paternity test.

The real bad news is that the drug’s side effects ARE NOT TEMPORARY, they are
PERMANENT.

Any female that takes it WILL NEVER BE ABLE TO CONCEIVE.

The drug is
administered by dropping it into the target’s drink.

The girl wouldn’t remember a thing the next morning, nothing at all that had taken place the night before will she remember.

Rohypnol, dissolves rapidly and easily in drinks, leaving no taste and no change in color which makes it impossible to detect.

These weasels can get this drug from anyone who is in the vet school or any medical university.

It’s that easy and Rohypnol is about to break out big on campuses everywhere.

Believe it or not, there are even sites on the internet telling people how to use it.

Girls, please be careful when you’re out, especially on a date, don’t leave your drink unattended.

(Buy your own drinks, ensure bottles or cans received are unopened or sealed; don’t even taste someone else’s drink).

There has already been reports of girls’ drinks being spiked by Rohypnol.

For guys – Please inform all your female family members, relatives and friends.

Remember you also have sisters or might one day have a daughter(s).

Important News are meant to be passed on, please don’t keep or ignore.

This was sent to me and I feel I should pass it on so that we are better equipped to protect our loved ones.

Please share to protect and save lives.
?PLS TELL THE GIRLS TO TRUST NO ONE

Source: Foster’s Facebook