Haya leo nawaletea designer mpya anakwenda kwa jina la Bonuzi! Nimeangalia kazi zake nimeridhika nazo. Ndio maana namleta kwenu. Tafadhali m-follow kwa Instagram yake na uweze kujionea mwenyewe! Safi sana!
Category Archives: Beauty and fashion
Hii picha imenikosha moyo wangu!
Kwamnao nijua lazima mtajua jinsi gani huwa naishukuru hii familia. Yani nimekuwa nikitumia picha zao sana mpaka mwenyewe nikaona aibu ?? Ndio maana siku hizi nawaweka mara moja moja ili niwape brake kidogo lakini hii picha imenikuna sanaaaa ikabidi niwaweke tu! What a lovely family! Symbol of UNITE as a family! Yani wanasonga mbele wote hawaachani juma. Sijui mama tu ndio awe "super star" hapana! Wanavutana mmoja baada ya mwingine kila mtu kwa karama yake! And please, let us give Mali a credit! Jamani wanaume wangapi wa Kitanzania ambao wangeweza kuzungukwa na team kama hii with their full energy na kumudu?! Kwakweli anastahili pongezi sana! He is one of the very few best father! Mungu azidi mbariki. Na hii familia izidi barikiwa zaidi ya hapa. ❤ it! Mfano mzuri sana huu wa what should family be! "The Grand Opening of Linda Bezuidenhout Couture Boutique at Phipps Plaza. The navy blue dresses are LB Couture, the Cream dress dressed by Linda's 3rd born Maryam and the Red dressed, dressed by the last born Marlinda are designed by Maryam. Linda's third born has been designing from a very early age she started with doll clothes @fashionadoz." ~~~~ Ms LB
Mother and daughter moment!
Womanhood!
Pendeza sana mama Double G! Nimependa gauni lako na umepungua vizuri sana. ❤ it!.........Siku zote nitakushukuru kwa support yako! Ubarikiwe sana! ...... Mr&MrsNyongo
The shade of Blue by Wema Sepetu!
What a beauty! Wema mdogo wangu wewe ni mrembo mno! Mungu took some extra time just for you! Naamini mama Sepetu kila mara akuonapo machoni pake lazima atakuwa anasema " Alhamdulillah" na tabasamu laini moyoni ?? You are so beautiful my dear and Yes! BLUE is your color! Inakupendeza sana na kukupa nuru nzuri mno! I just love it on you! "Rolls-Royce or Bentley don't have to run commercials because they know the values of their product & that value brings customers to them. When you know your value you don't have to beg for anybody to spend time with you or even love you. Everybody can't AFFORD or even HANDLE luxury.......or your trials ..........The diamond cannot be polished without friction, nor the man perfected without trials" >>>>>>>>>> Bishop Larry Boyd Stay strong our sweetheart. God will surely grant you all the good things that your heart desires! ? ?
“Mungu ni mwema”-Mrs Mengi!
Yes my dear, Mungu ni mwema wakati wote! Wakati wote Mungu ni mwema! Enjoy your life Mrs Mengi, and say hello to my Billionaire friend ?? We love you mama na baba wawili ? " when you have something good you don't play with it. You don't take chances with it. You don't take risk with it. When you have something good you give every single thing you can because when you take care of something good that something good takes care of you" 》》》》Michael Baisden
Baba na mama Cookie katika ubora wao!
Please Cookie Iyobo!! Si kwa uzuri huo jamani!!
Wee Cookie!! Jamani mbona umzuri hivyo! Honestly, your beauty is driving my uterus crazy!! I can feel the "baby Vibes" all over me ?? Now I am confused, I was longing for a baby boy but ma'am!! With that kinda beauty I don't mine to go through the "shades of pink" again! ??? You too cute baby girl! ?? maana nimeudhika na uwo uzuri if mama knows what I mean ❤❤❤..........Mungu akulinde mwanetu, mashetani yamejaa kwenye hii dunia inatisha sana!
Mama na baba wa 8020Fashion blog katika ubora wao! #ZezeTV
Sasa sikiliza, niliona hii short video kwenye Instagram ya Shamimu Mwasha kuhusu kwanini wanawake hatuna ujasiri wa kutongoza wanaume? Yani hata kama umemuona mwanaume unaye mpenda huwezi kumtokea na kumwambia?? embu msikilize ??
Basi nikaona kuwa video ni fupi nikasema ngoja niende YouTube nitafute labda nitapata yenye full length! Too bad sijapata lakini nikakutana na hii video nyingine ambayo mama wa Zeze TV akitengenezwa nywele na mumewe Abdul Nsembo! Embu itizame kwanza ??
Jamani si wamependeza eeh! Halafu eti Shamimu kamuitaje mumewe?? Mie nimejaribu kurudia mara kadhaa lakini sijamuelewa ??.........Nani alikwambia wakaka wa Kibongo hawajui kupenda?! Wapo wanaojua kupenda kwa dhati kabisa simnamuona Dr. Mengi na Jackie wake, na sasa Zeze na Abdul, haya subirini na mimi na Muhaya wangu mtakoma wenyewe ?? Sasa hivi bado tunajifunza mapozi ya picha na kuongea simnajua lazima nitoe hii accent ya Kijaluo ??? Anyway, nice video mama ZezeTV. Ninejifunza kitu fulani juu ya nywele fupi za twist, kazi yake yataka moyo kwakweli! Maana vitu vilivyopakwa humo si mchezo! Lakini naipenda sana, Shamimu huwa anapendeza sana na hizo nywele......halafu you got really beautiful voice! ❤
“Kuwa imara, hakuna alichokiumba Mungu asicho na kusudi nacho”~~~ Faraja Nyalandu
Live your life thinking of who you think you are and not what others think of you. Ukiishi kwa mawazo ya wengine wanavyokufikiria, kuna siku utaishi kama malaika na siku nyingine utaishi kama shetani. Kwasababu binadamu ana uwezo wa kufikiri vyote viwili juu yako. Kuwa imara, hakuna alichokiumba Mungu asicho na kusudi nacho. #WeekendWisdom P. S my country is BEAUTIFUL ?? #Kilimanjaro
your lifestyle & dreams will determine the kind of a man you would like to marry ~~~Akothee Akothee
It’s a free world , date whoever you feel like , even baboons attract tourist, as long as you are happy , then we should be happy for you, be proud of your Man /woman, we all have different tastes, ambitions, lifestyles, etc , your lifestyle & dreams will determine the kind of a man you would like to marry ??? usisumbue watu akili, gone are days when even parents would choose who you settle down with , today, they can only make noise & adjust to it . Choose your rib wisely, for when it is sweet , you won’t tell us , you will only share with us the challenges! & we will either laugh at you or do very little,in short LIVE & LOVE YOUR LIFE DONT LISTEN TO THOSE WHO HAVE BEEN SINGLE FOR TOO LONG , THEY ARE TOO SELFISH TO SHARE THEIR EXPERIENCES, but for sure every woman needs someone to hold, laugh, & cuddle Hakuna age kwa hizi
Katarina Karatu then and now!
Kweli Akothee Akothee alisema ukweli kuwa “We are not ugly, mapato ndio kidogo na mahitaji ni mengi” soma ?? WeAreNotUgly …… Tazama jinsi Katarina anavyo ng’ara sasa! Yani tofauti sana na alivyokuwa wakati anapesa za “kubangaiza” yani pesa zisizo kuwa na huwakika! Ni mrembo wa kuzaliwa lakini makeup imemuongezea mvuto zaidi! Alijisemea Chris Rock kuwa “Money is the best lotion ever”! Nahapa tunapata kuthibitisha LIVE! Kapendeza sana! ?❤
Wema Sepetu katika ubora wake!
Wema Sepetu katika ubora wake! Vazi limemkaa haswa aaa! Kapendeza sana! My dear Wema naomba leo nikushauri, unajuwa wewe ni our Sweetheart! Tunakupenda sana na kukutakia mema! Naomba usichukie kuhusu ushauri wangu kwani unatoka from a good place of my heart, na pia sio lazima uhufuate unaweza ukasoma na ukauwacha kama ulivyo! Na ninakuhakikishia bado nitakupenda bila kinyongo! …… Wema sikiliza: 《1》Hii karne ya 21 kuzaliwa mzuri tu haitoshi! Wewe ni mzuri sanaaaaaa! Lakini unamengi ya ku-prove ili umpate yule mume / partner unaye stahili kuwa naye KAMA KWELI HILO NI HITAJI LA MOYO WAKO!
《2》 Achana kabisa na watu /fans wako ambao saa zote wanakueweka katika muonekano wa “mashindano” na mtu fulani haswa Zari, wakati Zari got no time for nobody yani yupo busy na maisha yake! Wewe ishi maisha yako bila kupigizana kelele na mtu! Au kuweka mazingira fulani yanayo onyesha some sort of competition! Kumbuka mtu yeyote yule ambaye anataka kushindana na mtu jua huyo mtu teyari umesha mzidi ndio maana anataka aku-drug down to his /her level! Always choose “highway” na sio mashindano! 《3》Ngoja nikwambie ukweli, wewe na Zari wote ni wazuri sana tena to be fair labda niseme wewe umependelewa zaidi na figure kuliko Zari! Hata hivyo any man ambaye ni potential au well successful will absolutely pick Zari over you! Unajua kwa nini? Zari has proven herself kuwa (a) she knows what she wants in her life! And happiness is her number one priority! Na ndio maana aliamua kuachana na marehemu Ivan Ssemwanga na kuwa na Diamond! She prefers happyness over money (b) Zari has proven kuwa she can make her man to be the best of all! She did that twice! Kwa marehemu Ivan Ssemwanga na sasa kwa Diamond! Ndio, unaweza sema ulimpenda Diamond akiwa bado “Nasib Abdul” but mdogo wangu, wenyewe wanasema hivi “a man with dreams need a woman with vision”! Na hapo ndipo Zari alipokupiga bao! You knew Nasib’s dreams but you didn’t have VISION to take Diamond where he needs to be! Plus badala ya kuwa team player ukawa kama una compete na Diamond; kumbuka zile kauli kuwa “anatembelea nyota yako” toka kwa mashabiki wako na watu wako wakaribu! Zari aliacha yote kumjenga Diamond at least for the first two yrs ya relationship yao. Building Diamond ikamsaidia kujiendeleza na yeye pia kwa ku-expand her empire in Tanzania. Wakati alionekana kama amepoteza Dira ya maisha kwenye macho ya watu wenye mtazamo finyu lakini kwetu sisi wengine tulijua Zari is going to surprise them big time and she surely did! Kumbuka nimekwambia kuwa Zari nia yake ni kuwa na mwanaume ambaye will make her happy, and that is what exactly Diamond is doing! Spoiling her right before your eyes! Pia angalia Ivan Ssemwanga, pamoja na yote bado Zari alikuwa ndio Kimbilio na tegemeo lake! Kitu ambacho wewe mpaka dakika hii pamoja na kuteka people’s heart but none of them can trust you with their “treasure” or legacy! (c) Zari has proven kuwa she is not only a great partner but she can hold down a family as well! She’s strong, has good family values enough to make her own family kitu ambacho wanaume wengi waliofanikiwa wanapenda kuwa nacho! Na hapa siongelei kuwa na watoto kwani watoto ni mipango ya Mungu! Ninacho kisema hapa nikuwa “grounded” enough to make someone’s house a family friendly place ambapo mtu kama Dr. Mengi atakuwa excited, and proud enough kusema I’m going home na once in a while kuwaita some of his friends for dinner! Mpaka sasa kwa hili mdogo wangu Wema, umefeli kabisa! Siku zote waliokuzunguka mmh! only God knows who they are! Embu jifunze kitu kutoka kwa aunt Ezekiel! 《4》 My dear Wema, achana na kutafuta attention zisizo na kichwa wala miguu! Don’t let them losers and fools use you my dear! Kama kweli you want to have that potential man holding your hand then you need to prove kuwa you are a woman of character! Make your man feel secured kuwa hayupo kwenye “competition” with another man! Yani kuwa akija mwenye hela zaidi yake he’s out of the league! Hii inaweza ikawa ngumu kunielewa lakini mpaka utakapo elewa hichi ninacho kwambia basi tegemea kutumika na wanasiasa pamoja na wenye pesa za “mission-town” ambao wanatafuta kuandikwa kwenye magazeti ya udaku!
《5》 Kama nilivyo sema kuwa you’ve a lot tu-prove na kitu kingine ni kuonyesha kuwa you can stand strong alone na kua-achieve something for your own good! Kwamfano mimi sio such a “career woman” but I managed to get my college education. Nasio hivyo tu, nimelea mwanangu ambaye niko so proud of her! Plus, naishi mwenyewe hapa Marekani bila msaada wa mwanaume hivyo mwanaume yoyote yule atajua kuwa kama tumependana ni kwasababu zingine na mapenzi ya kweli nasio ugumu wa maisha wa hapa Marekani! Angalia, mfano wa karibu ni Jokate, she’s a great example kama utataka kujifunza kutoka kwake! You have to show some potentials!
《6》Lamwisho, achana na mashoga a.k.a “wadada wa mujini”! You have your sisters make them marafiki zako wa karibu. Unaweza ukawa na baadhi ya marafiki wazuri kwa kula “bata” but don’t let them be your close friends! Kwasababu naona wengi wao sio wazuri na mkikorofishana siri zako zote wanakutolea nje wakati wewe sioni kama unatabia ya kutoa siri za watu! Hivyo achana nao kabisa! Otherwise, mie nakupenda sana na nakutakia mafanikio mema. Najua bado unanafasi ya kufanya matengenezo! Kama nimekosea naomba unisamehe sana. ❤
“Mimi nimejifunza kutonung’unika sana kwa kila linalotokea”Jacqueline Mengi
Umeshawahi kulia na kusononeka kwa mfano kwasababu ya kukosa maelewano na mwenzi wako mpaka ikapelekea kuachana halafu baada ya muda kupita ukagundua kuwa kilichotokea ilikua ni njia ya kukufungulia mlango mpya wa baraka? Kama binaadamu tungekua tunajifunza kutokana na historia hata kama sio yetu binafsi tungeepusha masikitiko mengi sana. Mimi nimejifunza kutonung’unika sana kwa kila linalotokea maana kila nililoliona ni tukio baya baada ya muda niliona jinsi ambavyo ilikuwa ni njia ya kuruhusu baraka ziingie kwenye maisha yangu.Everything happens for a reason therefore be grateful for everything. Asubuhi njema…..
Baba na mama wawili katika ubora wao!
“Nilikupenda, nakupenda na nitazidi kukupenda……Mpaka kifo”…….hayo ni maneno yake mke mwema ambayo aliambatanisha na hii picha!
Jamani, mama wawili alisha semaga na bado anasema ni mpaka KIFO! Kwa mahaba hayo, nini tena Mungu akupe! Tulia mama tulele #Bilionea wetu, aje aone watoto wake wakiingia college na hata kuwa na miji yao ati!!………Kila siku baba na mama wawili wanazidi kunoga! Kupendana raha sana! Nimesema Kupendana siyo kupenda! Kupenda mtu asiye thamini penzi lenu ni Majanga! Utateseka mpaka basi! Lakini mkipendana kwa dhati kama Dr Mengi na Jackie wake aaah! Mbona raha sana dunia yote unaona ipo kwenye kiganja cha mkono wako ?? Wenyewe wako zao vacation na watoto wao huko Britain! I’m jealous kwakweli, can’t wait kwenda vacation na Muhaya wangu na mimi nikaige mapozi haya ?? ……..nimependa sanaaaaaa!
Man-up and kill it with kindness!
Yess! Keep on moving Bosslady a.k.a the New C.E.O of the “Rich Gang” ?? You Man-Up girl and em haters just kill them with kindness!!……………I just love this, do you guys see what I’m seeing?! The msg is on the shoes people!! While MEN are Manning-Up in ?? “Flat” shoes the Bosslady is Manning-Up in ? ?HighHeels baby ???You Go Zari! Keep that Legacy going!! Tell them We Run this Planet, of course in HighHeels ??
Mr and Mrs Obama katika ubora wao!
Wow!! Mr and Mrs Obama katika ubora wao ?? Michelle is looking hot ??……wenyewe wana enjoy weekend kwa raha zao! ……..unajua kuna watu wengi haswa Wabongo wana “act” mapenzi yao kama Barack na Michelle bila kujua kuwa hawa hawakuanzia kwenye kula bata na kuvaa nguo ambazo rangi zinaendana NOPE! Walichafuka vumbi kwanza kujijenga financially na kutengeneza “brand” yao! Yes! They knew what they wanted, Obama alijua ndoto yake kubwa ni kuwa kiongozi wa juu wa hii inchi (U.S.A) na Michelle alikuwa anajua anataka a man who will spoil her like crazzzy! Ndio maana katika kumsaidia mumewe ku-achieve his dream Michelle akaacha one of the most highly pay job na kuamua kufanya community work ili kumtengenezea njia mumewe!! Sasa ndoto zilipotimia Mr “lover man” naye akatimiza ahadi yake. He’s spoiling her like crazy and I’m sure he loves it as you can see his ego through his body language ?? Girl it doesn’t come that easily! You have to give all your energy / invest in what you want!! …….I just love them!……….Eti nyie wenzangu mnataka wanaume wa kuanza kuvaa sare ili mpige picha za kuweka kwa social medias wakati bank account inasomeka (-50) ?!! Mapenzi bila pesa hayanogi jamani!! I ain’t a gold-digger but can’t stand a broken lazy nigger!…..just saying!
Hongera sanaaaaaa Jokate!
“Nafurahi kutajwa na jarida la Forbes na pia kupamba ukurasa wao wa juu kama mmoja kati ya vijana 30 Afrika wanaofanya vyema katika ujasiriamali na kutengeneza uchumi unaohamasisha mabadiliko chanya kwenye jamii zetu. Mungu yu Mwema. Tunaendelea kupambana mpaka kieleweke.” Hongera sana Jokate! Uzidi kwenda mbele na ubarikiwe sanaaaaaa zaidi ya hapo! ??
Jojo katika ubora wake!
Womanhood
“If you stop chasing meaningless friendships and relationships and look after and love yourself,you will enjoy your own company while the right people find their way to you??❤️”~~~~May Charles Igogo
*****Very well said! Labda niongeze kwa kusema kuwa jinsi mtu (uwe mwanamke au mwanaume) unavyo zidi kujitambua na kujua thamani yako ule urafiki wa kama teenagers ni lazima u-cut off!! Sijui shoga yangu kutwa kuongozana kama matahira ni ujinga mtupu! If someone doesn’t add any value to you yani ukifika 33+ yani ni bora uwa drop off kwani mnapotezeana muda urafiki wenu hauna tija! Yani mimi hata rafiki anaye chukia kuona mwingine yupo happy au anafanikiwa huyo mie simtaki kabisa karibu yangu tutabaki story tu za hapa na pale tunapo kutana basi lakini ukaribu Nope! Kwani kama unachukia maendeleo na furaha ya mtu mwingine ambaye hajakukosea lolote basi hiyo nitosha kusema mimi will be next!………Hakuna kitu kizuri kama kujifunza ku-enjoy your own company kwani utakuwa na amani sana kuliko kuwa na marafiki chungumzima ambao hawakusaidii kwa lolote zaidi ya starehe!