Imenichukua muda kupost hili tukio la kuhuzunisha na kusikitisha sana kwasababu this is not kind of posts ningependa kuzipost humu! Kifo cha mtu yoyote is horrifying let alone vifo vya watoto zaidi ya 30?!! Its just too much pain for me!! ………As a mother, I am speechless over the death of these beautiful innocent souls! Like why? And how?!! As Mtanzania I am angry! very disappointed! And confused!! Like until When??!! Hizi ajali za Tanzania when will they end them?? Until when people???!! As I said before at this very moment am speechless can’t put it into right words right now!! Maybe some day I will but for now the only thing I can say; Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe milele zote! Mungu wa rehema awape faraja na amani wazazi, wafiwa wote na Watanzania kwa ujumla! Poleni sana! May their souls R.I.P
Category Archives: Condolences
In loving memory of Ontlametse Phalatse
Ontlametse ni mtoto alikuwa ana ni-inspire sana! Nilikuwa namfatilia sana kwa Instagram, nilivutiwa sana na inspirational speech zake na jinsi wazazi wake walivyo mlea na kumjengea confidence kubwa sana ya kujikubali jinsi alivyo, kujiamini kuwa anaweza na anastahili kuishi kama wengine, na kujipenda! Nimeguswa sana na kifo chake, may her soul rest in peace! ……Ee Mungu naomba uniongezee ujasiri niweze ku-overcome all my fear and conquer them with greatness just like Ontlametse, Amen!
PIGO KWA JAMII YA WALEMAVU! R.I.P Mh. Dr Macha
Jamii ya watu wenye ulemavu imesikitika sana kupokea taarifa za msiba wa mama yetu na mtetezi wetu aliyekuwa anatuwakilisha bungeni kama mbunge viti maalum wanawake kwa upande wa walemavu Mh. Dr. Elly Macha kupitia Chadema Tanzania. Dr. Macha amefariki dunia akiwa nchini Uingereza kwenye Matibabu.
Binafsi mara ya mwisho kuonana na huyu mtetezi ni mwaka 2015 nilipokuwa naomba fursa ya kuwa spika, maneno yake yalinipa nguvu na sababu za kuendelea kutetea jamii ya walemavu katika nchi na hata kimataifa. Aliamini mabadiliko ya kuikomboa jamii ya walemavu yatapatikana kupitia walemavu wenyewe na ikiwa watashiriki katika vyombo vya maamuzi kama bunge, mahakama na hata ndani ya serikali. Bado naamini katika maneno yake na yataendelea kuishi na ipo siku yatatimizwa na walemavu wenyewe.
Natoa pole kwa familia yake,jamii ya watu wenye ulemavu, ndugu, jamaa, marafiki, viongozi na wapenzi wote wa CHADEMA kwa kumpoteza mama yetu tuliye mpenda lakini Mungu amempenda zaidi yetu. Tuwe wavumilivu na wenye matumaini katika kipindi hiki kigumu huku tukiamini ipo siku tuta onana naye.
Amen Nami naomba nitoe salamu zangu za pole nyingi sana kwa wana familia, ndugu, jamaa, marafiki, pamoja na jukwaa zima la walemavu Tanzania na duniani kote! Taifa limepoteza msomi mmoja ambaye pengo lake halito zibika!
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe!……. R.I.P Mh. Dr. Macha
“Sir George Kahama ni moja ya Tunu za Taifa” -Shy-Rose Bhanji
Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Hon. Shy-Rose Bhanji ametoa salamu zake za kuguswa na kifo cha aliyekuwa mtumishi wa umma wa muda mrefu Sir George Kahama kwa kusema haya “Sir George Kahama ni moja ya Tunu za Taifa kwa mchango wake ktk Serikali za Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi na Mkapa…Asante kwa utumishi wako uliotukuka wa kulitumikia Taifa la Tanzania. Mungu akulaze pema Baba Pole nyingi kwa Familia yote Mungu awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu #SirGeorgeKahama #RIP” ……. Muheshimiwa Shy-Rose aliyasema hayo mapema leo kupitia kurasa zake za jamii (Facebook, Instagram). Nami naomba kuungana naye kwa niaba ya familia ya mzee O.O Igogo kuwatakia pole wana familia yote, ndugu, marafiki, na jamaa. Poleni sana kwa msiba huu Mungu aendelee kuwa nanyi wakati wote……….Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote!