Category Archives: Congratulations /Pongezi

Temeke SDA Nursery and Primary School watoa shukrani kwa mama Igogo!

Mama Igogo akitazama kwa furaha picha iliyochorwa kwa taswira yake.

Wanao onekana kwenye video hapo juu ni baadhi ya wafanyakazi wa Temeke SDA Nursery and Primary School walifika nyumbani kwa mama Igogo mchana wa jana tarehe 09/27/2021, masaa ya Africa Mashariki, kwaajili ya kutoa shukrani zao za dhati kwa mchango wake wa hali na mali ambao aliutoa toka kuwaza yakwamba kanisa la Temeke SDA linahitaji kuwa na shule, kuisimamia kuanzishwa kwakwe toka elimu ya awali ya chekechea (Nursery school) mpaka kufikia kuwa na darasa la kwanza mpaka la saba.

Kuhakikisha kuna kuwa na boarding (hostel) kwa wanafunzi wanao kaa mbali haswa wanafunzi wa jinsia ya kike! Mama Igogo alikuwa full time Mkurugenzi mkuu (Director) ambaye hakuwai kulipwa mshahara hata mara moja kwa miaka 7! Alifanya kazi ya kujitolea kwa asilimia 100%! Na baada ya miaka 7 aliomba “kung’atuka” na kuwaachia vijana waikimbize. Yeye alibakia kuwa mshauri kwenye bodi ya shule. Mungu ni mwema shule ilisimama na inaendelea vizuri! Mwanangu ni mmoja wa wanafunzi wa mwanzo kabisa wa shule hii! Alianzia  Nursery hadi darasa la sita. Mungu azidi wabariki wote walimu, wanafunzi, pamoja na watu wote wanaojitoa kwaajili ya huduma hii muhimu sana kwa jamii. ????

Kwenye video ya pili ni Mama Igogo akitoa shukrani zake za dhati baada ya kupokea shukrani na zawadi ya picha kutoka kwa wafanyakazi wa Temeke SDA Nursery and Primary School. 

Na hapa, mama Igogo akitoa ufafanuzi wa zawadi ya picha iliyochorwa kutoka kwenye moja ya picha zake ambazo alipiga akiwa kwenye Makao Makuu ya Wasabato ulimwenguni yaliopo Silver Springs, Maryland/ Washington DC eneo la kumbukumbu za Ellen G. White (mmoja wa waasisi wa dhehebu la Wasabato). Mama yangu hajatembea dunia nzima, Mungu ni mwema amembariki kutembelea nchi kadhaa hapa dunia na ameona mengi; lakini safari ya kutembelea kijiji cha history ya Wasabato huko Battle Creek, Michigan na safari ya kutembelea Makao makuu ya Wasabato ulimwenguni kwakweli ni moja ya safari ambazo zimemgusa sana moyo wake na siku zote huwa anaziongelea kwa hisia sana! Namshukuru Mungu kuwa amenichagua mimi binti yake kuwa kiungo kikuu cha mbaraka huo. Si kwamba asingeweza kufika Marekani hapana! Naamini Mungu kama alimpangia kufika angefika tu bila ya mimi kuwepo kama hizo nchi zingine alizo tembelea bila mimi kuwepo! Lakini kufika sehemu kama hizo kwa urahisi na kwa furaha kupitia mwanae naamini nikitu kinampa faraja kubwa sana moyoni! ?? No mama ain’t done yet! Mungu atupe uhai utakula more good time very soon! ?????

Mzee O.O Igogo, Magreth Otieno Igogo, na mama Igogo

Hapa juu ni moja ya picha waliyopiga wakati walikuwa wamekwenda kutembelea kijiji cha historia ya Wasabato huko Battle Creek, Michigan mwaka 2014 mwezi wa 11. Picha A siku hii zipo nyingi lakini zipo kwenye Flashdisk, sijapata muda wa kuziangalia.

Kama ulipitwa na picha za mama Igogo kutembelea Washington DC basi bonyeza ???? Safari ya mama Washington DC , na Safari ya mama Washington DC

Twamshukuru Mungu kwa yote kwani ni kwa neema yake tu ndio maana haya yote yanatokea. Sifa na utukufu ni zake yeye tu milele na milele. ????

Sherehe ya kipekee ya kumuaga Dorice Sassi Igogo!

Ameagwa rasmi! Siku ya Jumatano, tarehe 06/02/2021 zilisikika nderemo na vigelegele vingi sana kutoka kwa familia ya Mr. Emmanuel Agonda Sassi (marehemu) na Mrs. Magreth Cornel Awiti a..k.a Mrs Agonda, a.k.a Mrs Sassi pamoja na wanaukoo wote wa Adol Igogo. Ilikuwa ni furaha ya kumuaga rasmi binti yao kipenzi Mwalimu Dorice Sassi Igogo ambaye anakwenda kuanzisha rasmi kaya (familia) yake.

Dorice akiwa na mtarajiwa wake

Ndoa ni jambo la kheri, ndio maana wazazi hufanya sherehe ya kipekee kabisa ili kumuaga mpendwa wao, kama njia mojawapo ya kuonyesha furaha yao na shukrani kwa Mungu.

Dorice a.k.a Vumilia ni binti aliyezaliwa katika familia ya watoto (3) watatu, yeye akiwa mtoto wa pili kuzaliwa na msichana pekee.

Mtoto wa kwanza ni Yustor Sassi (Kulia), Dorice, na Joseph (kushoto). Katika picha hii inaonyesha makaka wakimlisha keki dada yao, na mama mzazi akiwa pembeni anaangalia.

Yustor akiwa nafuraha nyingi wakati wa kulishwa keki na dada yake.

Joseph naye akifurahia kulishwa keki na dada

Yustor akimpigia saluti mdogo wake, kwa heshima kubwa kama afanyavyo huko jeshini!

Tazama jinsi kaka wa bibi harusi mtarajiwa akitoa saluti kwa mdogo wake kwa furaha na ushupavu wa kijeshi.

Bibi harusi mtarajiwa akielezea historia yao, wapi walikutana na nini kiliwakutanisha.

Zawadi kwa bwanaharusi mtarajiwa

Bibi harusi mtarajiwa akiwa na Mc wa shughuli hiyo ajulikanaye kama McKatokisha

Wamazazi wa upande wa bibi harusi mtarajiwa

Yani mdogo wangu huyu kwa kuchakarika aaah! Ni Mwalimu na pia ni mjasiriamali wa nguvu. Hii keki ametengeneza mwenyewe kwa mikono yake kupitia kampuni yake ya isadoricakes and sassyjuice! Izidi barikiwa kazi ya mikono yake.

Mtarajiwa akikata keki

Akilimlisha mama mzazi kwa unyenyekevu na upendo mwingi

Akimpatia mama mzaa chema keki yake kama ishara ya upendo na ukarimu wake kwake na ukoo wa mumewe mtarajiwa.

Mama mzazi naye alipata kipande chake

Mama wazaa chema na binti yao

Wamependeza kwakweli

Haya ngoja nikusaidie kidogo kama haujui, bibi harusi mtarajiwa ni mtoto wa mama yangu mdogo. Mama yake ndio kitinda mimba kwa uzao wa bibi yangu mzaa mama. Sasa basi, kama ilivyo kwa mama yake Geoffrey Kateti (kama mnamkumbuka) ndivyo ilivyo kwa mama yake na bidada hapa. Mama yake naye alifuata nyayo za dada yake (mama yangu) akaolewa Utegi! Utegi oyeeee! ?? Tofauti na mama yake Geoffrey, mama yake Dorice ameolewa ukoo mmoja na dada yake ?? chezea ukoo wa Odol! Hivyo Dorice ni mdogo wangu pande zote; kwa baba na kwa mama.

Mapenzi ya Mungu yalitimizwa baba yangu mdogo (baba wa bibi harusi mtarajiwa) aitwae Emmanuel Agonda Sassi, alishalala usingizi wa mauti takriban miaka 4 iliyopita. Twamshukuru Mungu kwa yote.

Once again, hongera sana mdogo wangu, shemeji tunakukaribisha kwetu kwa mikono miwili. Mungu awe nanyi siku zote. Amen! ????

?@lush___makeup

? @mckatokisha

? Decor@lillies_luxe_decor

#FBF

Embu tujikumbushie mambo yalivyo kuwa siku ya kuvikana Pete ya ahadi ya ndoa /uchumba, siku ya Jumatatu ya mwezi wa kwanza tarehe kumi na mbili mwaka huu, 01/12/2021. Love is the beautiful thing.

Kitchen party ya RHoda Igogo

Bibi harusi mtarajiwa Rhoda Alexander Igogo

Wakati tukisubiria picha kutoka kwa wataalamu waliolipwa kufanya kazi hiyo, basi tuanze na tulizonazo.

Siku ya jumapili tarehe 05 /16 /2021 ilifanyika sherehe ya kumfunda mwali (bibi harusi mtarajiwa) a.k.a Kitchen party ya Rhoda Alexander Igogo. Sherehe hii aliandaliwa na mama yake mlezi akishirikiana na ndugu na jamaa pamoja na marafiki. Ilifanyika kwenye makazi ya wazazi walezi huko Segerea ambapo bibi harusi mtarajiwa ndipo anapo ishi na ndipo atakapotokea kwenda kwa mwenza wake.

Akiingia ukumbuni mwenye nyuso ya furaha na tabasamu kama lote ndio mama mzazi wa Rhoda na Isaka, Mrs Joyce Alexander Igogo. Ni mke wa marehemu baba yangu mkubwa (wapili kuzaliwa kwenye familia yao baba, watoto bibi Rhoda Nyakanga Olwengo). Babu yangu mzaa baba (Marehemu mzee William Olung’a Igogo) alikuwa na wake watano (5) ??? usishangae sana maana marehemu babu yake baba (my great grandfather) Chief Sarungi Igogo yeye alikuwa na wake 19 ??????? welcome to our ukoo ?? …… Rhoda ndio mtoto wa mwisho kwao. Akitoka kuzaliwa Isaka ndio Rhoda anafuata. Na harusi zao zimekuwa ndani ya mwezi mmoja. Familia hii inajumla ya watoto 7 walio hai, mmoja alifariki. Grace a.k.a Anyango, Aphino a.k.a Nyawade, Kenneth (Marehemu) a.k.a Ukombozi, William a.k.a Mzee, Dr. Obadiah, Isaka, na Rhoda a.k.a Nyolwengo, na Emilia Igogo! ….. Mungu ni mwema sana.


Haya embu tufurahishe macho kwa hizi tilizonazo!

Pichani ni Dia Alex Odemba na bibi yake mama Igogo.

Dada kama dada! Huyu ni dada yake Rhoda aitwae Aphino.

Dia Alex Odemba katika ubora wake!

Mama wa isadoricakes_and_sassyjuice. Dogo langu Mwalimu mwenye ujasiriamali wake! ??

bibi harusi mtarajiwa akikata cake yake

Kwamahitaji yako ya Cake nzuri zenye ubora wake, juice fresh tamu, na Mc wa kitchen party, tafadhali husisite kumtafuta @isadoricakes_and_sassyjuice ndio habari ya taifa! ???

Kutoka kushoto ni mama yangu mzazi, akifuatiwa na mdogo wangu Vumi Sassi, anayefuata ni mdogo wake mama yangu (kitinda mimba kwa familia yao) napia ni mama yake Vumi aitwaye Magreth Cornel Awiti a.k.a Mrs Agonda Sassi, na anayefuata ni mdogo wangu kipenzi Magreth Rhoda-Nyasungu a.k.a Mrs Massawe.

?? mama zangu hao! ??

Rhoda akiingia ukumbini kwa furaha kabisa

Mama mlezi wa Rhoda

Mrs Vetto Igogo (kushoto) pamoja na Mrs Isaka Igogo (kulia). Mmemuona bibi harusi wetu wa wiki iliyopita?! ?? Miguu imeiona? Miguu halisi ya Kiafrika! Yani wana miguu ya bia kama mawifi zao! ??

Baba naye hakutaka kupitwa na matukio katika picha ?? akiwa na furaha kubwa pamoja na binti zake akitaniana na ucheshi wa hapa na pale.

Mtu na wifi zake! Mrs. Massawe kwa mbele hapo, Mrs Vetto Igogo mtu kati, na Mrs Isaka Igogo nyuma hapo.

Wifi karibu sana Utegi!

Watu wakiserebuka kwa raha zao!

Mke ya Mrombo! ??

Mwenye nguo ya njano, anayecheza kwa hisia zote, ni dada wa bibi harusi mtarajiwa, aitwaye Grace Alexander Igogo a.k.a Anyango, yeye ndio mzaliwa wa kwanza kwa familia yao. Anafurahia kusindikiza kitinda mimba kuanzisha familia yake. Pembeni yake ni mama mlezi wa Rhoda.

Mama naye hakutaka kujivunga kwani wimbo wenyewe siunausikia? ???

Haya tunamtakia Rhoda safari njema katika kuhitimisha kilele cha sherehe za kuagwa kwake na familia yake mpaka siku ya harusi. Jumapili hii ni Send-off yake na Jumapili ijayo ndio harusi. Mungu awatangulie katika kila jambo!

BTW, hii siyo mara yakwanza kwa familia yetu kuwa na harusi mbili kwa mpigo (double wedding), kaka yangu mkubwa Vetto Igogo na dada yangu Elline Igogo harusi zao zilipishana wiki tu, tuliserebuka kwa wiki mbili mfululizo! Yani tulianza na kitchen party ya dada Elline, ikafuta harusi ya kaka Vetto, ikaja Send-off party ya dada Elline kisha harusi yake. Na baada ya hapo ikafuata sherehe ya kuvunja kamati. ??? I tell you, this familia loves to partyyy! Nahiyo ni miaka ishirini na mbili (22 yrs ago) iliyopita. Na sherehe zao Ilikuwa kubwa kweli kweli hizi ni chamtoto! Mama zigi-zig catering na Dotnata Catering walipika mpaka walishangaa. ???

***Updates: picha za nyongeza***

Rhoda na binamu yake Honorable Madam Judge Dr Modesta Opiyo.

Rhoda na mama yake mzazi

Juu ni mama mkwe wake Rhoda Mrs Scola Oguna Ollal.

Mawaidha ya akina mama, shangazi, na wanawake wachanga kwenye ndoa.

Mama mdogo Mrs O.O Igogo akitoa ombi la kwanza.

Mama mdogo Mrs Agonda Sassi akitoa ombi la mwisho. Walianza na Mungu wakamaliza na Mungu. Amen!

Kwa picha zaidi bonyeza ????

https://RHEVANSTUDIO2021.pixieset.com/pendokitchenpartyphotos/

Rhoda na rafiki yake, hizi ni pre-wedding pictures

Blessing latika ubora wake

Wadada hao! ??

Kwa picha zaidi bonyeza ????

https://RHEVANSTUDIO2021.pixieset.com/rhodapresendoffphotos/

Hongera sana Isaka na Sarah!

Mr and Mrs Isaka Alexander Olung’a Igogo

Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Wamehalalishwa duniani na Mbinguni yakwamba wawili hawa ni mwili mmoja!

Sarah akila kiapo kitakatifu

Agano hili takatifu lilifanyika siku ya Jumosi tarehe 05 /08/2021 katika kanisa la viziwi lililopo huko Bunguruni, Dar es salaam. Tunawaombe baraka nyingi sana katika familia yao hii mpya walio ianzisha!

Bibi harusi

Bwanaharusi akihakikisha je kweli ni yeye?! Kabla ya kula kiapo, maana hukawii kubadilishiwa mke kama Jacob (Yakobo)! ? mjini mambo mengi jama! ?

Bwanaharusi amehakikisha na ameridhia! ?? Kama hujawahi sikia kisa cha Jacob (Yakobo) basi chukua Biblia yako na ufungue kitabu cha mwanzo sura 29 yote itakupa stori kamili!

Kwaufupi ni kwamba, Jacob baada ya kutumikia miaka saba kwa mzee Labani kama mahari ya kumuoa binti yake Rachel (Raheli), siku ya harusi akakuta amebadilishiwa mke anaye mpenda kwa dhati na kupewa Lea ambaye alikuwa ni dada wa Rachel (Raheli). Kwani kulingana na mila na desturi za kabila na ukoo wa mzee Labani ni kuwa mkubwa lazima aolewe kwanza ndipo mdogo anafuata. Kwa maana hiyo Jacob ilibidi atumikie miaka 7 mingine ili aweze kumpata Rachel. Kwa maana hiyo Jacob alitumikia miaka 14 kwa mzee Labani kama mahari ya kumuoa kipenzi cha roho yake! …… Sikilizeni wanawake wenzangu, kama mwanaume anakupenda basi hakuna gumu wala zito mbele ya macho yake! He will move mountains just to have you! Tena bila hiyana yoyote! Wanawake wazuri ni wengi sana lakini Mke ni mmoja tu ambaye kila mwanaume anajua hilo!

Maharusi na wapambe wao
Wasimamizi wao
Mchungaji aliye idhinisha ndoa hii

Sarah akisindikizwa na kaka yake aitwaye Alex ambaye ndiye aliyemlea toka wazazi wake wamefariki hadi leo hii anapokwenda kuanzisha nyumba yake mwenyewe. Kwa Sarah hamuoni Alex kama kaka bali ni baba yake mlezi na mke wa Alex ni mama yake mlezi, hao ndio wazazi wa Sarah.

Hapo juu ni baba mlezi wa Isaka ajulikanaye kama mzee O.O Igogo. Yeye ndio amemlea Isaka toka akiwa na miaka 5. Baba mzazi wa Isaka amefariki takribani miaka 7 iliyopita. Mzee 0tieno Igogo ni mdogo wake na marehemu mzee Alexander Igogo ambaye ndiyo Baba yake na Isaka.

Mama mlezi wa Isaka Mrs O.O Igogo akisalimia maharusi, nyuma yake ni mjukuu wake aitwaye Essy.

Mashangazi na mama wakubwa kwa wadogo upande wa bwanaharusi.

Baba mlezi akiwa na furaha nyingi usoni kwa kuongeza mtoto mwingine kwa familia.

Madada, mabinamu, na mashemeji wakiingia kwa shangwe!

Kutoka kulia, ni mdogo wa bwanaharusi aitwaye Blessing, akifuatiwa na mpwa (niece) wa bwanaharusi Essy, akifuatiwa na shemeji mkubwa Mrs. Vetto Igogo, na dada mkubwa (wapili kuzaliwa kwenye familia ya kina Isaka) Aphino Alexander Igogo (Mrs Ogoche).

Mdada mwenye nguo ya blue kutoka kushoto, huyo ndio kitinda mimba kwenye familia ya akina Isaka. Anaitwa Rhoda Alexander Igogo. Naye harusi yake ni mwishoni mwa mwezi huu. Wiki hii ni kitchen party yake.

Bibi harusi mtarajiwa Rhoda Alexander Igogo akiwa na maharusi Mr and Mrs Isaka Alexander Igogo.

Bibi harusi mtarajiwa, bi Rhoda akifurahia kaka kupata “jiko”!

Mama mlezi wa bwana harusi pamoja na baba msimamizi wa ndoa hii mzee Samuel Olung’a Igogo wakitoa nasaha zao.

Baba mlezi akitoa neno kwa niaba ya kamati!

Mama mlezi akiwa na maharusi

Maharusi wakikata keki!

Wapendwa, kwamahitaji yako ya Cake nzuri zenye ubora wake, juice fresh tamu, na Mc wa kitchen party, tafadhali husisite kumtafuta @isadoricakes_and_sassyjuice ndio habari ya taifa! ???

nnnnn

Maharusi wakifungua dancing floor kwa kucheza ziro-diatance music ?? asiye na wake akumbatie chupa ya soda! ???

Meza kuu upande wa bibi harusi

The Olung’as!

Hawa ni baba zake Isaka, wadogo kwa wakubwa. Kutoka kushoto ambaye kichwa tu ndio kimeonekana ni mzee Samuel Olung’a Igogo (baba mkubwa na msimamizi wa ndoa hii), akifuatiwa na mzee Charles Olung’a Igogo (baba mkubwa), akifuatiwa na mzee Otieno Olung’a Igogo (baba mdogo na mlezi wa Isaka), akifuatiwa na Genga Olung’a Igogo (baba mdogo)

Walianza na Mungu, wakamaliza na Mungu. Mama mdogo wa Bwanaharusi Mrs Emmanuel Agonda Sassi Igogo akitoa sala ya mwisho!

Mathayo 19:5 “akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja”!

Marko 10:9 “Basi, alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe” ….. I present to you Mr and Mrs Isaka Alexander Olung’a Igogo

Mc Rhevan mtu kati hapo

picha zote shukrani kwa Mc Rhevan studio. Ukitaka kuona picha za tukio nzima tembelea ????https://RHEVANSTUDIO2021.pixieset.com/isakaandsarahweddingphotos/

Tunawaombea kheri na baraka nyingi!

Bwana harusi mtarajiwa-Isaka akiwa kwenye pozi na bibi harusi mtarajiwa-Sarah

Kesho ndio siku yenyewe kuu, ambapo wawili hawa wataunganishwa kuwa kitu kimoja na koo mbili zitaunganishwa rasmi mbele za Mungu.

Naam, kwamara nyingine tena tunapenda kutoa pongezi nyingi sana kwa watarajiwa hawa kwa kufanya maamuzi mazito yenye busara. Mungu azidi kuwatangulia katika kila jambo ambalo limepangwa kufanyika kesho basi likapatae kibali mbele ya uso wa Bwana na lifanyike kama lilivyopangwa kwa utukufu wa Mungu.

Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa rehema na neema awazidishie ulinzi wake na mibaraka yake siku zote za maisha yao. Ndoa yao ikajae amani na furaha, naye Mungu Baba awe mgeni wao siku zote. Wakabarikiwe wao na uzao wao wote. Twaomba kwa imani katika jina la Yesu. Amen! ????

akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja!” *** Matayo 19:5

“Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe” ****Marko 10:7

Jana ilikuwa siku ya kuagwa kwa bibi harusi mtarajiwa. Bi. Sarah alifiwa na wazazi wake wote wawili akiwa mdogo. Kaka yake Alex akamlea hadi sasa anatokea kwao kwenda kwake na mumewe mtarajiwa. Ni mlemavu wa kusikia na kusema??‍♂️ Hapo anatoa shukrani zake za moyoni kwa walezi wake siku ya kuagwa, na kuwapa zawadi alizomudu kama ishara ya shukrani na kumbukumbu. Mume wake mtarajiwa naye ana historia inayotaka kufanana na yake! Hawa wawili ni kielelezo halisi na ushuda hai kwamba kazi ya Mungu haina makosa.

Mimina neema zako Bwana mimina ????

??? mnaona mama zangu na shangazi yangu aliyegoma kuzeeka pale nyuma na tabasamu kama lote wakikumbushia enzi zao?! ?? so sweet!

Wababa nao hawakubaki nyuma! ??

Picha zote shukrani kwa Mc Rhevan , mtembelee Instagram @mc_Rhevan au website yake ???? https://mc.rhevan.com/

Magreth Nyasungu sendoff party

Magreth Nyasungu’s pre wedding photos moment

Magreth, bibi harusi mtarajiwa siku ya tarehe 27 December, 2018 alipiga picha za kumbu kumbu akiwa na ndugu zake pamoja na marafiki zake wa karibu.

Magreth akiwa na dada yake Mrs Nyagilo

Magreth (pichani juu) anatarajia kufunga ndoa takatifu hivi karibuni, tunamuombea Mwenyezi Mungu awatangulie katika safari yao.

Picha hizi zimepigwa na Rhevan studio, hivyo shukran zetu za dhati ziwafikie.

Kwa picha zaidi tembelea Rhevanstudio.com

Matukio katika picha: Peter and Janet baby shower

Kwanza kabisa naomba nianze kwa kumpongeza Janet kwa mbaraka huu mkubwa ambao Mwenyezi Mungu amemjalia. Hongera sana Janet Mungu azidi kuwa nawe ujifungue salama, I'm super happy for you.  Najua  Shiro hatokua mtoto wako wa kwanza lakini I can only imagine how happy you are kwani watoto wakike ni mibaraka mikubwa  sana katika hii dunia ?  Bibi yake Shiro, mama mzazi wa Janet Kisyombe Dr. Victoria Kisyombe naye alikuja kutoka Tanzania kushuhudia tukio hili, ubarikiwe sana mama yetu!      Kwa kupitia account yake ya Facebook Janet Kisyombe ameandika huu ujumbe kwa rafiki yake Tumaini ambaye ndio mastermind wa hii shughuli pamoja na watu wote waliofanikisha tukio hilo ?? "BLESS ME INDEED" Peter and I are Speechless. All we can say is "THANK YOU GOD". Our Baby Shower was nothing BUT Beautiful, Stunning, absolutely Breathtaking. All this work was done by the one and only my Beautiful Sister Tumaini Kaisi-Katule (The Best Event planner/ MC /Decorator). This God Fearing Woman planned the whole event out of her Good Heart. Iska Kauga Joshua The Best photographer in East Coast, My life savior, Your work needs no Explanation. It is without a doubt done with perfection and Love. Many Thanks also Goes to KCFA Community, Love Foundation, Organizing team, and All my Beatiful sisters of TANO LADIES. Last But not Least - without forgetting each and everyone who attended our Baby shower and shower us with beautiful baby gifts. "May Our All Mighty GOD Pour Out Blessings upon each and everyone of you". #BlessMeIndeed"  Baba na mama Shiro wakiwa katika pozi la picha huku wakisikiliza mapigo ya Shiro ? how beautiful! Mungu awe nanyi siku zote Kwa faida ya wasomaji wangu, najua wengi mtakuwa mnajiuliza Janet ni nani? Huyu ni rafiki yangu, ni mmoja ya watu wakwanza kabisa niliowajua hapa Marekani. Huko nyuma nilishawahi kuelezea jinsi nilivyo kutana na Janet na urafiki wetu ulipo anzia. Kama hukuwahi kusoma basi soma hapa ?? JanetKisyombe   Shughuli hii ilifanyika tarehe 20 mwezi wa 10 mwaka huu huko Maryland, U.S.A Licha yakwamba Janet ni rafiki yangu, Janet pia ni Muandishi wa vitabu. Kama wewe ni mfatiliaji mzuri wa hii blog basi nahakika utakua umeshawahi kuona natoa matangazo ya kitabu kinachopendwa na wengi sana kiendacho kwa jina la "Bless me indeed"! Ni moja ya vitabu vingi vijavyo kutoka kwa Janet. Kama hujakisoma basi wahi chukua kopi yako pale Amazon nawala huto jutia!Huyu ndio Tumaini Kaisi-Katule ambaye ndio aliandaa hii shughuli yote na team yake. Yeye ndio Mc anayesifika sana, lakini kumbe siyo mtu mwenye maneno mazuri kutoka mdomoni tu, anaroho nzuri kupita kiasi. Kwa maneno yake Janet mwenyewe amenisimulia kuwa Tumaini alimwambia nakuandalia baby-shower akafikiri ni utani. Siku zilipo karibia akajua kumbe si utani ni kweli ila alijiua ni kitu kidogo tuu, kha! Kumbe hakujua anaandaliwa one of so many to come life time surprises. Janet anasema hakuchangia hats dollar moja kila kitu kimegharamiwa na dada Tumaini na baadhi ya marafiki zake Janet. Kuanzia ukumbi, mapambo, kadi za mualiko, vyakula, vinywaji n.k! Jamani, ukisema duniani hakuna waungwana mimi nitakukatalia kwani najua wapo japo ni wachache lakini wapo! Hata watakatifu wapo, kwasababu watakatifu watakao kwenda Mbinguni watatoka hapa hapa duniani! Mungu azidi kumbariki kazi za mikono ya dada Tumaini pamoja na wote waliyo shiriki katika shughuli hii wote mbarikiwe sanaaaa!  Nani kama mama! Ubarikiwe sana mama yetu                
 
  Janet, asante sana kwa ku-share hizi picha pamoja nami na wasomaji wangu. Mungu azidi kukuminia baraka zake. Ukutangulie ukajifungue salama na ubarikiwe uzao wako wote ????               

                    **Credit to** 

**Wahusika wa shughuli: Peter na Janet 
**Muandaaji wa shuguli nzima: Tumaini Kaisi-Katule                                      **Mc wa shughuli: Tumaini Kaisi-katule  
**Mpambaji wa shughuli: Tumaini Kaisi-katule                     **Photographer: Iska Kauga Joshua

“Ndugu zangu Watanzania…….!”

#regrann  Regrann from @queenelizabethtanzania -  Ndugu zangu Watanzania, sidhani kama nitakuwa na maneno ya kuisha kuelezea shukrani zangu za hali ya juu, amani , furaha na nderemo. Kuanzia taji la Miss Kinondoni (Asante sana waandaaji na wadhamini), Miss Marcelina Dar es Salaam zone (Asante sana waandaaji na wadhamini) mpaka kufikia taji la juu kabisa la The New Miss Tanzania 2018; Dada Basilla Mwanukuzi, The Look Company, dada yetu mpendwa wa kambi, Marion Elias na wengine wote napenda kuchukua fursa hii kusema NAWAPENDA na kuwathamini SANA! Ndugu zangu watanzania kupitia mitandao ya kijamii na hata tuliobahatika kuonana mmenipa moyo sana mpaka kufikia hapa nilipo; sina cha kuwalipa; Nashukuru sana! Washiriki wenzangu wa The New Miss Tanzania 2018; ninawapenda sana na bila nyinyi mimi nisingeweza kuwa mshindi. Tushirikiane zaidi kuweza kufikisha tasnia hii mbele.

Taifa langu, wanahabari, kamati na uongozi wa kampuni ya The Look, Dada Basilla Mwanukuzi; Asanteni sana!

Asante TANZANIA! @newmisstanzania - #regrann

From a regular girl to District Commissioner!

Regrann from @jokatemwegelo -  From a regular girl to beauty queen to pan-african media personality to one of the top university graduates at the University of Dar Es Salaam- with honors to owning my own business, landing on Forbes Africa @forbesafrica to being a politician to being appointed by the President of Tanzania as District Commissioner - Kisarawe and to many more accolades, Amen. Dear Girl child let no one tell you can not do it all and achieve greatness on your own terms. 
 Many congratulations to our newly crowned Miss Tanzania @queenelizabethtanzania Go fly the Tanzanian flag ?? higher. You have all our blessings. To all the contestants of Miss TZ this year, congrats for making it this far. You now have a platform to make a difference in your life and our country. The choice for greatness is in your hands. And to you my sister @basillamwanukuzi , thank you for restoring the respect of Miss Tanzania. Through you, girls will be inspired to go after their dreams. As the saying goes, ‘When something is important enough, you do it even if the odds are not in your favor’.. You organized a great show even without enough sponsors and resources, but you my sister did it! Well done to you ????Looking forward to what the future holds for Miss Tanzania under your leadership and thank you for making that contribution for education in Kisarawe @newmisstanzania @mac_couture @the_queen_of_fabrics @americannailstz @kisarawe_mpya #kisarawempya #jokatekisarawe  - #regrann

Hongera sana Magreth Rhoda Nyasungu!

Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza mdogo wangu pamoja na shemeji yangu kwa maamuzi waliyochukua ya kujulisha koo mbili kuwa wanataka tuungane na tuwe wamoja. Hongera sana mdogo wangu kwa kuvishwa rasmi pete ya uchumba na kututambulisha shemeji / mkwe wetu rasmi.  Mungu akulinde na akutangulie mpaka siku ile tutakapo shuhudia ukila kiapo kitakatifu mbele za Mungu.  Ubarikiwe sana, we love you so much. To my handsome brother inlaw pongezi nyingi kwako kwa kufuata taratibu za kimila za kabila la Waluo na Wachagga katika kumposa binti yetu / mdogo wetu Magreth. Wewe sasa ni mmoja wa familia ya Igogo kwani posa na mahali umesha kabidhi, hivyo na penda kusema karibu sana ujaluoni, na karibu sana katika familia yetu..... nimekubatiza jina la "shemeji mzungu" kwani hiyo rangi adimu kwetu ?? Kwa faida ya wasomaji wangu ambao ni wageni humu; Magreth ni mdogo wangu tumbo mmoja, yeye ndio mtoto wa mwisho kwa mama yetu. Jina lake ni Magreth alipewa jina la mke wa family friends wetu ambao wana asili ya kijerumani (Germany). Sasa basi kwakuwa wajina wake ana asili ya watu weupe ndio akapewa nick name (jina la utani) ya lugha ya kiluo "Nyasungu" tafsiri yake ni mtu mweupe au mzungu. Hiyo "Nyasungu" kwasababu ni mwanamke angekuwa mwanaume angeitwa "Jasungu"! Wanawake katika mila za Mluo akitaka kutambulishwa kwa kutumia ubini wake au mahala alipozaliwa au asili yake lazima uwanze na "Nya" na kwa wanaume ni "Ja". Kwa mfano binti kutoka Kenya tutamuita 'Nyakenya' na mwanaume 'Jakenya'. Hilo jina la Rhoda ni jina alipewa ukubwani akiwa primary  school.  Ni jina la marehemu bibi yetu mzaa baba. Yani jinsi alivyokuwa akikuwa ndivyo kila mtu alikua akishangaa jinsi anavyofanana na bibi yani mpaka kucha za miguu. Wakati ule bibi alikuwa bado yupo hai hivyo hata yeye akawa anashangaa jinsi wanavyo fanana. Basi baba akawa anasema japo nimekupa jina la rafiki yetu Magreth itabidi nikubatize jina jipya la mama yangu. Basi toka wakati huo mpaka leo watu wengi wameshazoea kumuita Rhoda unless wale aliosomanao, wafanyakazi wenzake au wanao sali wote ndio wanamuita Magreth.

Mama mzaa  chema na binti yake Kutoka kushoto ni mama mdogo (Mrs Igogo-Junior), anyefuata ni Mrs Igogo -Senior, na kulia ni dada yetu Mrs Margreth Olambo Mabada Mama mzaa chema na wadogo zake Baba mzazi, baba mzaa chema  Sir O.O Igogo  Baba mdogo wa bwana harusi mtarajiwa kafunga safari kutoka Moshi kuja kushuhudia kijana wake akiposa. Ubarikiwe sana  baba. Mashangazi kutoka upande wa bwana harusi mtarajiwa   babu na wajukuu zakeNdugu wa bibi harusi mtarajiwa
Kwa mara nyingine tena, hongera sana Magreth Rhoda Nyasungu ??

Mr and Mrs Sande Wedding

New couple in town ? Kwanza nianze kwa kuwapongeza maharusi Ken and Christine kwa kuachana na maisha ya u-bachelor na kuamua kufunga ndoa takatifu siku ya JumaMosi tarehe 11 mwezi wa 08 mwaka 2018.   Ndoa hii takatifu ilifungwa kwenye Chaple ya Sterling Banquet Hall lililopo Houston, Texas. Ambapo ilifuatiwa na sherehe nzuri sana kwenye ukumbi huo huo. Tunawaombea neema nyingi kwenye ndoa yao, Mungu akawe kiongozi wao siku zote, ndoa yao ikajae amani na furaha nyingi sana. Wakabarikie na uzao wa tumbo lao hata kizazi cha tatu na cha nne. AMEN Kwafaida ya wasomaji wangu, bwana harusi ni rafiki yangu wa miaka mingi tuliishi wote Kalamazoo, Michigan, huwa napenda kuwaita “my Kalamazoo family members” kwani tuliishi kwa amani na upendo. Kwasasa yeye anaishi Dallas, Texas na mimi naishi Houston, Texas.  Bibi harusi yeye alikuwa akiishi Spring, Texas lakini sasa amekuwa mwana Dallas, Texas kwani huko ndiko makazi yake mapya. Gosh! Ain’t they pretty ? Wasimamizi wa kiume na bibi harusi katika pozi. Kutoka kushoto ni Sammy: yeye alikuwa ndio Bestman. Nirafiki wa bwana harusi wa miaka mingi sana toka Kalamazoo, Michigan na sasa wanaishi wote Dallas, Texas.

Anayefuata anaitwa Gittu: Yeye pia ni mmoja wa “Kalamazoo family members”. Nirafiki wa bwana harusi wa miaka mingi toka Kalamazoo na sasa wanaishi wote Dallas, Texas.

Na huyo gentleman wa mwisho anaitwa Charles Nyakure kutoka Dallas, Texas ni rafiki mwema wa bwana harusi. Naye tumemu adopte kuwa mmoja wa “Kalamazoo family members”  ?? Mmenionaa ?? mimi hapa upande wa kushoto, mwanangu upande wa kulia pamoja na Mr and Mrs Sande Dada wa bwana harusi all the way from Nairobi, Kenya akiwa na bestman-Sammy Wazazi! Kutoka kushoto ni baba mzazi wa bibi harusi. Anayefuata ni dada wa bwana harusi. Mwenye nguo ya blue ni mama mzazi wa bibi harusi, na wa mwisho ni baba mzazi wa bwana harusi. Wote wamekuja rasmi kutoka Nairobi, Kenya kwaajili ya kushuhudia tukio hili takatifu.    Picha zote kwa hisani ya Charles ?…… Thank you so much Charles be blessed!

Hongera sana Mr and Mrs Paul Makonda

Mwacheni Mungu aitwe Mungu! Asante Baba Mungu kwa kumuaibisha shetani mchana kweupe!!! Tumzomeeni shetani kwa nguvu zote na tulitukuze jina lake Mungu milele zote! Hakika wewe ni mweza wa yote hakuna lishindikalo mbele yako. Pongezi nyingi kwa Mr and Mrs Makonda, Mwenyezi awajalie ulezi mwema, mototo Keagan akuwe katika kimo na hekima akampendeze Mungu kwanza kisha wanadamu. Mungu abariki uzao wenu hata kizazi cha tatu na cha nne, Amen!

Mr and Mrs Abayo wedding

Harusi ilifungwa siku ya Jumapili July 1st, 2018 katika kanisa la Houston International S.D.A…. bibi harusi alisindikizwa  na kukabidhiwa kwa Bwana harusi na kaka yake (mdogo wake) aitwaye Robert.  Mchungaji aliye fungisha ndoa alikuwa mtumishi wa Mungu Pastor Caleb Migombo kutoka North Carolina.  Maharusi wakitoka kanisani baada ya kuunganishwa kuwa mwili mmoja. Tunawaombea kheri katika safari yao hii.

MUngu awatangulie katika yote, hongereni sana ??

Matukio katika picha

Hili nitukio la harusi limetokea jana huko Tabata, Dar, Tz . Nawafahamu vizuri sana wazazi wa bwana harusi lakini sina maelezo mazuri ya kuwapa kuhusu maharusi kwani siwafahamu na picha nimetumiwa tu! Hivyo naomba niwakilishe kwa kuwapongeza maharusi....... Nawapongeza maharusi kwa kufunga pingu za maisha na nawatakia maisha mema.  Mrs  Awiti  L.C. and Ms Doreen L.C. Awiti dancing their heart off at the wedding ceremony of Wasongas son. This night of 6.5.018. Tabata Dar.
 
     Jamani hawa ni ndugu zangu kabisaaa sijikombi ?? Mrs Awiti L.C au mama Awiti ni shangazi yangu mke wa mjomba wangu Leo Awiti. Mzee Awiti ni kaka yake mama yangu mzazi tumbo moja! Hivyo Doreen Awiti  ni cousin yangu kabisaaa! Bwana harusi ni mjukuu wa Mrs Awiti L.C  na baba mzazi wa Bwana harusi ni former employee wa Utegi Tech...... si mshanipa mpaka hapo?! ?

Hongera Mr and Mrs Ali Kiba!

https://youtu.be/bSxhKFeEPME

Sijachelewa, simnajuag8ina mimi huwa sifanyi vitu kutoka na ushabiki wa watu! I like to do this my way at my own convenience time! That is what means by being a C.E.O of your life! That what makes you unique! Yani sipendi kupangiwa maisha wala kupewa kanuni ya kufanya mambo yangu kwani I am not in a competition with nobody but myself!! Anyway, ngoja nimpongeze King Kiba kwa kuuacha U-singleman a.k.a U-bachelor. 

Mc anakwambia "mwanaume pochi mwanamke matumizi"! ?? Yap! Mtunze mkeo lasivyo wajanja watakutunzia ???? Utalea watoto wa wanaume wenzako kwa madai ya "kitanda hakizai haramu" ?? Chakunishangaza kama kweli "kitanda" hakizai haramu mbona Chawa na Kunguni huwa wanazaliana kwenye kodoro chini ya kitanda ?? natafakari tu ?? Mpende na umtunze mkeo Mr King! 

Honestly hakuna kitu kibaya kama meanaume asiyejua kuchakarika kutafuta pesa na mwanaume baili!! Pesa utafute halafu kuzitumia hutaki abeee! Sasa ulizitafuta za nini?! Fungulia makumbusho basi uziweke kwa maonyesho kha! Au unakuta mwanaume hajui kujiongeza hata umsukume kwa greda hasongi mbele!! Awiih! I am not a " Gold digga" but can't stand a broak-lazy nigger ?‍♂️?‍♂️ #MwanaumePochiMwanamkeMatumizi  Anyway, nakutakia ndoa njema iliyojaa mafanikio mengi sana, amani, furaha, na afya njema kwenu wote. Mungu awaongoze siku zote. Hongera sana Mr and Mrs Ali Kiba 

The best movie Director!

Regrann from @wemasepetu  -  Rafiki, Ndugu, Mshauri, Muongozaji... Bila wewe safari yangu itakuwa ngumu sana... Mungu akuweke kwa ajili yangu... Hakika najiona mwenye bahati sana... Ntakuthamini na kukupenda mpaka mwisho... @neema_ndepanya @neema_ndepanya @neema_ndepanya @neema_ndepanya  - #regrann   Nimefurahia sana kuona mdogo wangu tuliye kuwa naye mtaa mmoja akifanya mambo mazuri hata kuwezesha wengine kufanikiwa katika ndoto zao na hata kushinda taji! Hongera sana Neema Ndepanya! Endelea na moyo huo huo na mumsaidie Wema kufanya maamuzi mazuri. Proud of you!

Hongera sana Wema, nakutakia mafanikio zaidi ya haya!

Regrann from @wemasepetu – Napenda kuchukua nafasi hii Kumshukuru kwanza Allah Sub’hannah wata’Allah kwa kunifkisha hapa nilipo sasa… Najua ni mambo mengi sana yanafanyika kwa ubaya juu yangu ila yeye ndo amekuwa Tumaini langu kubwa… Nimshukuru Mama angu mzazi pamoja na familia yangu yote kwa ujumla kwa kusimama na mimi bega kwa bega katika kila kitu… . Nitoe n shukran zangu za dhati kabisa kwa Azam Tv kwa kutupa wasanii wote wa Tasnia ya Filamu fursa hii kubwa ya kuweza kujua nani zaidi… Hakika ni Changamoto nzuri sana na naiona inakuja kuleta mabadiliko makubwa kwenye Tasnia yetu…

Napenda kutoa Special thanks to my Love, The Woman behind The Best Actress 2018, My Tyler Perry, wanamuita Neema Ndepanya kwa kuniamini na kuniongoza vyema katika kazi… Najua upo very proud na nakuahidi kuendelea kuku make proud… We have so much to do mamy… @neema_ndepanya ….

Wema Sepetu Empire, Nawapenda sana watoto wangu… Nyinyi ni zaidi ya Ndugu sasa… Na tunaenda kufanya mapinduzi makubwa sana .. Maana sio kwa hasira nilizonazo sasahivi… . Last But Not Least…. Wema Lovers… Hizi tuzo ni zenu… Nawashukuru kwa kunipa endless support kila ninapohitaji… Bila nyinyi siwezi… Ntaendelea kuwapenda na kuwathamini mpaka siku nakata kauli…

Pia nichukue nafasi hii kuwashkuru wasanii wenzangu wote tulioshiriki kwenye tuzo hizi na kuwapa hongera maana hata kuwa nominated tu ni hatua kubwa sana… . Mwisho kabisa nawashkuru wasanii WOTE wa Tasnia ya Filamu kwa ujumla… Tutakutana mwakani tena kwenye TUZO… Inshallah…….. ?????? – #regrann
Ni bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa! Hongera sana Wema kwa tunzo ulizoshinda. Nakutakia mafanikio mengi na makubwa zaidi ya haya!…. Nimeona ile interview umesema Naseeb a.k.a Diamond atakuwa boss wako. Hakuna ubaya wowote japo kwakweli nimesikitika! Sijasikitika kitendo cha wewe kuwa na show yako ndani ya Wasafi TV hapana! Hilo halina shida kabisa kilichonisikitisha ni kuwa Naseeb / Diamond anakwenda kuwa “boss” hapo ndipo nilipo natatizo nalo! Like why?! Ungenunua airtime ya kipindi chako kwa Wasafi TV au Radio lakini uendelee kuwa your own boss na Management yako mwenyewe?! Why are you degrading yourself my dear! Who is your advisor if any? Umeonyesha udhaifu mkubwa mno kwamba huwezi endesha maisha yako au kufanikiwa bila mkono wa Diamond!! Ona sasa wanavyo kufanyia vituko mbele ya kadamnasi dunia yote ikishuhudia!! Anyway, nimesikitika sana lakini ni mitihani ya maisha uichukulie katika positive angle though najua ni ngumu sana…… Kwa mara nyingine hongera sana. ?❤

Hongera bwana na bibi Mandela!

Hongera Mr na Mrs Mandela kwa kufunga ndoa takatifu. Mwenyezi Mungu awe ndio ngao na kimbilio lenu wakati wote. Hongera sana Mzee Igogo na vijana wake ?? kwa faida ya wasomaji wangu, Mandela ambaye ni bwana harusi  yeye ni msaidizi wa wazazi wangu huko nyumbani. Wiki iliyopita siku ya Juma Mosi alifunga ndoa na lazizi wake huko Kibada, Dar, Tz.  Waliporudi mzee Igogo naye akajisogeza kupata kumbukumbu japo ilikuwa usiku! Mdogo wangu Magreth yeye alihudhuria kwa niaba ya familia. Kwa mara nyingine, hongereni sana.

Hongera Mr and Mrs Uchebe

Vitu kama harusi au interview ukiona nimechelewa kuweka jua bado sijatizama nikitizama lazima niweke. Bora niwe wa mwisho kutoa pongezi au kusema lakini niseme kitu ambacho ni sahihi! Mimi siyo shabiki wa "breaking news" hivyo nablog kwa style yangu ambayo napenda nikiandika kitu naandika  from the heart na siyo ushabiki "maandazi"! Naamini ndio maana wasomaji wangu wako loyal sana kwani kunakuwa na emotional attachment.  ??? Imenibidi nicheke kwanza, mnamkumbuka Muhaya eeh? Naye amekuwa zilipendwa ?? Nani anataka kufa kwa stress maisha yenyewe mafupi haya ?? Sasa kuna siku aliniambia kuwa eti "wasomi" wengi hawana emotional attachment kwa watu au situation kwani hicho ndio kitu kikubwa wanafundishwa shuleni ???? halafu huyo huyo akimaliza kuongea na wewe anasema "I love you" ??? I wonder kumbe ndio maana maisha ya wasomi wengi wa Tanzania ni Fake kama degree zao eeh!! Ile degree ya Dr Mengi ndio yakweli  peke yake ?? ?? well,  mimi sijui kuishi a fake life sina sababu ya kunifanya niishi maisha ya uongo and I don't consider myself msomi so wakwende huko na degree zao ??........ Anyway back to Mr and Mrs Uchebe Hii harusi ya Shishi babe binti wa Donald Trump  niliona picha  nikampa hongera kwa Instagram account yake lakini nilijua lazima nikipata muda wa kuitazama nitatoa pongezi rasmi hapa kwa blog! Wenyewe  wanasemaga "better late than never"! ....... Hongera sana Mr and Mrs Uchebe, ndoa yenu idumu katika Bwana. Ukabarikiwe uzao wa tumbo lenu milele na milele!

Shilole ulipendeza sana mno! Ulikuwa kama katoto fulani hivi ambaye baba yake anapesa fulani za kumwagwa ?? tatizo sasa bibi harusi wewe ukawa unaongea utadhani MC ??  jamaniii! Najua unapenda kuongea lakini kha!  Mpaka unamwita mtu " Mbwa wewe" ? wewe kiboko ?? Halafu Mungu alivyokujalia sasa amekupa mume mpole utadhani siyo Muhaya ???  Yani huyu kaka ni muungwana sana, halafu siyo mtu wa social media muombe Mungu sana ili aendelee hivyo hivyo! Huyu Shilole atakufaa sana hakuna raha kama kuwa na mume mwenye kumjua na kumpenda Mungu na anajitahidi kukuweka wewe karibu na Mungu! Maisha bila Mungu ni ushetani mtupu asikwambie mtu! Mpende mumeo mwaya!

Nimempenda sana jinsi marafiki zako walivyokupa zawadi za kukujenga! Yale mambo ya kununuliwa dinner set na TV is sooo 70's!! Watu wanakuletea zawadi ya vyombo vya plastic?!  vyanini? kwanza vinaleta cancer ??? hizi ndio zawadi!

My JoJo!! Kanoga eeh!! CCM oyee indeed ??  Hongera sana kwa kumpa zawadi nzuri sana hakuna kama elimu haswa ya kujua jinsi ya kufanya kile kitu unacho kipenda! ........ Halafu nyie wasichana ambao mnajiita "celebrity" embu muige mfano wa kuongea kama Jokate hapo! Hakuna kitu kina boa nakuonyesha some sort of kutokuwa smart and insecure kama msichana asiyejua kuongea kwa mpangilio wa maneno ya kueleweka!!! Yani wale wasichana ambao wanaongea utadhani ndio wanaanza kuota meno!! Au utafikiri hajui kiswahili kabisa anaishia  na "aaa" nyingi zisizo na mpango!! It's just boaring kwakweli! ..........Mwisho huyo MC aliyevaa T-shirt like really!!! Huo ni utovu wa nidhamu kwakweli! Umeonyesha dharau sana kwa Mr and Mrs Uchebe!! Shame on you!! Kila vazi na mahali pake, huwezi hata siku moja ukavaaa T-shirt au ndala kwenye harusi ya mtu!! Labda kama wewe unaroho ya kichawi!! Halafu T-shirt yenyewe mbaya utafikiri umetoka mazoezini!! Kwa mara nyingine tena, hongera sana Mr and Mrs Uchebe, mbarikiwe sana.