Category Archives: Elimu juu ya maisha

“Watu wanafanyaga mambo magumu halafu wanategemea matokeo yawe rahisi INASHANGAZA SANA!!”  ~~~~~ Zamaradi Mketema

                            “Watu wanafanyaga mambo magumu halafu wanategemea matokeo yawe rahisi INASHANGAZA SANA!!”  ~~~~ Zamaradi Mketema

  Dah! Ujumbe mzito huu! Bado natafakari! Lakini ni kweli kabisa kwani huwezi tengeneza uji wa vitumbua ukitegemea kupata maandazi!! Huu ujumbe umenichoma ?? moyo in a positive way!!

LeMutuz umesema kweli lakini…………..!

 LIVE STRAIGHT TALK:- The Art of growing up process historia inatakiwa kuwa @diamondplatnumz ndiye Mtanzania wa kwanza kuandika mafanikio makubwa ya music kuliko Wanamuziki wote wa Taifa hili walio hai na wasiokuwa hilo by FACTS halina ubishi ...leo ninaomba kuwakumbusha WaTanzania wenzangu kwamba kuna wakati tunakosea sana tunapomuhukumu huyu kijana mdogo kwa mapungufu yake huwa tunasahau kuwa ni Kijana mdogo sana mwenye umri wa the 20s so Scientifically au Theologically ni HAKI YAKE YA KIMSINGI kufanya makosa mengi kwa sababu umri wake unamruhusu ...tunamharakisha sana kuwa mtumzima wakati he is not yaani kama Wanawake wengi wanavyowalalamikia Waume zao kuwa hayupo hivi au hayupo vile ukweli ni kwamba he is not what you want now muache au baki naye ila nyamaza ...I mean hebu wale wote mnaomlaumu sana huyu Kijana mdogo sit down and look back ulipokuwa kwenye umri alioano wa the 20s akili zako zilikuwa zinafananaje? makosa mangapi uliyafanya? inaitwa process na ndio makosa makubwa Baba yake Michael Jackson aliyafanya kwa mtoto wake kwa kujali sana kipaji cha mtoto wake bila kujali ubinadam wake akaishia kumnyima nafasi ya kuwa mtoto mpaka kijana matokeo Michael alipokuwa mtu akawa hajielewi kama ni mtoto mdogo au mtumzima now na sisi kama Jamii tunataka kurudia makosa yale yale ya kumnyima Diamond process ya ku Grow up tunataka awe mtumzima ghafla kusudi afanane na muziki wake au our imaginations it is wrong TUNAKOSEA SANA ...sometimes ninashangazwa sana na hata yule Mpenzi wake anapomfanyia mambo ya kumrushia maneno ya shombo kwenye Social Media on a serious note huwa kwa sisi wenye AKILI KUBWAZZ anajichoresha cause alitegemea nini kumpenda Kijana mdogo in his 20s? ....I mean guys everybody back off tumpe nafasi kijana mdogo aishi maisha yake akosee awe sawa ni process ya kukua ambayo wote tumeipitia ..I mean unakuta yule Kibibi kule USA mtumzima Mama wa Watoto 3 Baba mbali mbali kimeachwa na Mume Jobless, Homeless hana hata Taifa maana hawezi kurudi tena Tanzania hata akiwa amekufa na yeye unamkuta anashambulia mapungufu ya Diamond kama vile na yeye ni kijana mdogo badala ya KUJITAFAKARI ATAZIKIWA WAPI NA NANI! ...guys tumuache Diamond awe Diamond! - le Mutuz
 
Ok LeMutuz, uliyoyasema yote ni ya ukweli kabisa nakubaliana na wewe lakini kumbuka Diamond himself decided to wear "big boy's shoes" thus must accept all the responsibilities that comes with it!! Ingekuwa ni mtoto wa kike anafanya hayo afanyayo Diamond naamini hata wewe ungekuwa mmoja wa watu wanaomponda! Tuache double-standard! Kama ameamua kuwa na watoto then he needs to act like someone's parent not a teenager anymore!! Plus ashukuru kuna watu wanajali hata kuamua kumwambia ukweli ili asiangamie kabisa japo wengine ni wivu na roho mbaya ndio zinawasumbua!................When comes to his relationship with Zari; you're absolutely right! Zari should have known the consequences of being in a relationship with a post-teenager boy!! Kwenye hii situation, she's the one who's grown  thus she needs to make some grownup decision to either let Diamond go or pull-up her "big girl panties" and suck it sincerely!! It seems to me Zari wants  husband around but Diamond is not ready to seattle down, he wants to "play house"! It's sad but is the truth!

Tuishi maisha yetu lakini tuwe na mipango endelevu ili majina yetu yasisahaulike!

Elimu juu ya maisha sio lazima ujifunze kutoka kwako au kwa wazazi wako. Muda mwingine unaweza jifunza kitu kikubwa ambacho kitabadilisha mwenendo wako au mtazamo wako wa maisha, jinsi unavyo tafakari mambo, na jinsi unavyo fanya maamuzi toka kwa marafiki au a total stranger!. Sasa Steve Harvey alijifunza kuwa njia pekee ya wajukuu na vitukuu wake kumkumbuka na kujua jina lake ni kuishi maisha yake lakini kwa wakati huo huo lazima awe na “legacy” yake ambayo hata akifa wajukuu na vitukuu wake watamjua jina lake! Na somo hili alijifunza toka kwa bibi wa rafiki yake wakati akimpa wosia kabla hajafariki.

Kuwa na mipango endelevu ni swala hata Biblia (kwa Wakristo) inatuambia ni vizuri kuwa na mipango endelevu, kuzaliana na pia kujiendeleza kiuchumi. Hii kwa Africa ilikuwa ni kuwa na watoto “wakiume” wengi kwasababu watabeba jina la baba forever, waliamini mtoto wakike akisha olewa sio wako tena na anatakiwa kuchukua jina la mumewe!! Mwe, mie shangazi zangu walisema ni mwiko kuchukua jina la mumeo kwani sio baba yako ?? shangazi zangu hakuna aliyebadilisha jina, hata dada zangu / wadogo zangu walio olewa sijaona aliyebadilisha jina. Siku hizi ni wachache sana wanafanya hivyo kutokana na carrier kuanza kubadilisha ni process ndefu sana. Hivyo wanaishia ku hyphenated. Haya nawe jifunze hilo, kama unataka wajukuu na vitukuu wako wakukumbuke anza kuwa na mipango endelevu sio kula bata tu! Kwa mfano, hawa wajukuu wa baba yangu unafikiri watamsahau babu yao? Hata kidogo! kwasababu amewapa kumbukumbu ya kudumu. Sio lazima uache mali hata mafunzo fulani ya hekima kwa wanao ambayo yataishi ndani yao milele nao wata waeleza watoto zao kuwa walifundishwa na baba / mama yake…….. Ishi maisha yako lakini uwe na mipango endelevu ili wajukuu na vitukuu vyako wakumbuke jina lako.

“….labda ningekuwa naanza maisha leo ningerudi mfumo wa wazazi………hawa watoto ndio maisha yangu…….pia katika uzima ni parterns wakudumu”~~~~ Dr Lennard Tenende

Haya msikilize mzee wetu Dr. Lennard Tenende akielezea historia ya maisha yake. Naona ni mzee mwenye uzoefu mzuri sana katika mambo mbali mbali ya taaluma na kijamii. Msikilize mwenyewe.

Kumbe mzee Tenende ndio muanzilishi wa DICOTA?! Mmh! Mimi sio mpenzi wa DICOTA, maybe I need more education about DICOTA lakini niliwahi kumuuliza "Dr Ndaga" alipokuwa President wa DICOTA akasema "ni chama cha Educated Elite" ambao wanafanya mambo "makubwa makubwa" sio kuandaa BBQ na baby-shower parties!! Sasa mimi I don't consider myself "educate" or "elite" hivyo siwezi kujihusisha na DICOTA. Plus inawezekana DICOTA ina nia na malengo mazuri lakini naamini kuna watu fulani wameingia kwenye uongozi wa DICOTA ambao hawana nia nzuri na wataivuruga sana hiyo DICOTA! Kama mnaweza kuwatoa muwatoe. Lakini hayo ni maoni yangu tu, you can ignore me as I'm not a part of "Educated Elite" ??? So funny!.......?? Btw, wale walio wasema Bungeni ni wanachama wa Chadema sio mimi naomba ieleweke hivyo.

"Ni kati ya achievement ni kubwa kuliko hayo ma-PhD unayo yasema"! Hayo ni maneno yake mzee Dr Lennard Tenende kuhusu mkewe. Wow! What a humble man! Yani mwingine angekazana kusifia hayo ma-PhD yake wee mpaka mngekoma, Wahaya mpo? ?? Dr. Mwakasisi umemsikia mwenzako ?? ............. Halafu nyie wadada wa 21st century mnaona wazee wetu walikuwa hawaangalii kama umepaka poda, wewe kwenye mchaka mchaka akaona mdada mrembo wa kuoa! Sasa nyie poda mnapaka na editing juu halafu ndoa baada ya miezi 6 imekwisha ?? Stop being so fake, let the man fall in love with your heart and character not your makeup and lipstick ??............... Nimeona. Mzee Tenende amekuwa emotional kidogo kuhusu kuwa na watoto wengi,  amesema kitu ambacho Vivica Fox alisema kwa Oprah (SomaHapakuwa anajutia kutokuwa na watoto, kama angelijua angezaa hata watano! It really got me thinking ??....... nice interview!

Je, wamfahamu Pili Hussein?! Wanasema kuwa “HER HUSTLE IS TOO REAL!!”

 "Mwana apollo wa kwanza mwanamke kuanza kuzama chini kuchimba tanzanite migodini Mererani! Anaitwa Pili Hussein lakini alibatizwa jina la Mjomba Hussein. Alilazimika awe kama mwanaume kuweza kujichanganya na wanaume aweze kuchimba madini. Wanawake walikuwa hawaruhusiwi kuzama chini migodini...HER HUSTLE IS TOO REAL!! Ukisikia vyuma vimekaza, hii ndio #vyumavimekaza #kilakitubalaa #inspired #watumpakawanazamachini #sisihukujuutunafanyanini? #badounasubirifursa #mjombahussein" ~~~~~Faraja Nyalandu

***Please note hiyo picha ya Faraja na Pili Hussein ni post ya mwaka jana nimerudia tu!***

Je, umewahi sikia history ya madam Rita Paulsen!

Sasa katika kuchungulia kwangu huko Instagram ili nione nini cha kuwaleta hapa, sinikakutana na page ya Madam Rita Paulsen. Nikaamua kuipiga chabo kidogo ?? Mbali na picha zake nzuri nikaona videos clips mbalimbali, nyingine Charles Hillary akicheza. Basi nikaamua kuitazama kwakuwa ilikuwa fupi nikasema ngoja niende kwa YouTube nikaiangalie zaidi. Dah! Si ndio nakutana na hii interview yake alifanya na Mkasi. Hivi kwanza, Mkasi bado ipo au imekufa? Mimi sijui, hata ile Bongo Star Search sijui kama bado ipo. Au ni mimi ndio niko nyuma ya ratiba ?? btw, mimi ni TV addict! Yani kitu Radio hata sijawahi sikiliza unless nipo kwenye gari la mtu  au nyumba ya mtu that I'm  NOT free enough kusema zima ?? tofauti na mdogo wangu Magreth na dada yangu Elline hawa wawili na Radio huwatenganishi Anyway, back to our story.......Sasa katika kujieleza nikagundua kuwa kumbe naye kama mimi! Alizaa akiwa underage  (only 14 yrs old). Dah! Amenigusa sanaaaaaa! Can you imagine having a baby at 14 yrs old?! Jamani, hivi vitu visikie tu kwa mwingine yasikukute! Kama mimi kuzaa at 18 yrs old, nilichekwa na kudhihakiwa hivi yeye aliyezaa at 14 ilikuwaje!! I feel like I wanna hear more about it! Embu msikilize mwenyewe ?

Sasa huyu Madam Rita, mbona sikusikia akipaza sauti yake kuhusu kauli ya kuzuia watoto waliopata mimba kwenda shule? Akaniacha mimi kidogo nimtoe "roho" mama yangu kipenzi mama Salma Kikwete ?? Madam Rita kama utasoma hapa please we need you to be the voice of the voiceless. Denzel Washington anasema, "don't just aspire to make a living, aspire to make a difference". Tafadhali amka madam. Nimependa your new talk show.  So nice!

“kumbuka BOX ni rahisi kulipata popote, ila cha thamani ya kukaa ndani ya Box ndio kigumu,”~~~~ Zamaradi Mketema

Katika maisha ya kawaida zawadi huja zikiwa zimefungwa bila kujua kilichomo ndani, na kwakuwa ZIMEFUNGWA unaweza jikuta unalidharau Box la hovyohovyo ambalo huenda ndio lenye kitu cha thamani ndani, ama ukalipapatikia box kubwa lililofungwa vizuri ambalo ukija kulifungua unakutana na mauzauza. Na ndio hata BARAKA ZETU zinavyokuja pia, sio mara zote MUNGU huziweka wazi mwanzo, ila huzifunga kwasababu yake maalum, na mpaka unapokuja kutambua hiyo ni ZAWADI ambayo MUNGU amekutunukia kuna mengi yanaweza kuwa yamepita ambayo yanaweza kukujenga ama hata kukufunza kuithamini. Mara nyingi NJE kuna uongo mwingi, Kwenye kila jambo yatupasa tuangalie vitu kiundani zaidi na sio juujuu, iwe ni kazi, mapenzi, maisha ama chochote kile, Nje kunaweza kukawa kwa kupendeza lakini uhalisia usiwe kama panavyoonekana, kumbuka BOX ni rahisi kulipata popote, ila cha thamani ya kukaa ndani ya Box ndio kigumu, na mara nyingi nje panapendezeshwa na wengi kwa MAKUSUDI sababu ndio panapoonekana hivyo usiamini sana NJE NA PICHA YAKE, huwa zinatengenezwa kukuvutia, Hivyo kwenye kila jambo jifunze kuangalia kwa picha ya mbali, kutokudharau kitu na kuwa na subira, usije ukatupa zawadi ya thamani kwa kuhangaika na mabox ya nje yanayogeuka dissapointment baada ya kufunguliwa.

The Untold: Siku 30 kwenye koma, jela miezi 27, na madawa ya kulevya!?!

Wahenga wanasema ukiona kwako kwaungua basi jua kwamwenzio kwa teketea! Yani kama wewe unafikiri unamatatizo au umepitia shida na vizingiti katika maisha basi kajaribu kummwambia jirani yako akusimulie yakwake! Utabaki mdomo wazi! …….Embu sikiliza history ya maisha ya Wasia Maya jinsi alivyokuja hapa Marekani, mambo yalimkuta na mitihani aliyopitia utachoka mwenyewe! Kuna wakati alikuwa kwenye koma kwa siku 30, kafungwa jela kwa miezi 27, na tamaa ya kufanikiwa kwa njia za mkato ambazo zilipelekea kutaka kuuza madawa ya kulevya!

Yani the devil! Wewe mwenzio katoka kutumikia miezi 27 jela bado tu unamuweka kwa wishawishi vya madawa ya kulevya?!! Lakini kama roho wa Mungu bado yupo ndani yako kwakweli hawezi kukuacha ukaangamia. Atakugusa kwa mguso wa pekee ambao utatosha kubadili njia zako!

“Sasa nina amani……… Nipo comfortable with my life”! Hongera sana kaka Wasia Maya, najua hii story yako itagusa vijana wengi na kuangalia maisha katika njia tofauti. Ubarikiwe sana.

“I Esther Akoth will never date a celebrity”

this kind of men steal my heart , not social media addicts who worship the no of followers , likes and comments , I told my daughters , I would be happy if you introduce your boyfriend as , ( mum meet my new catch he is a farmer ) but if you tell me he is a celebrity , am out , you will end up funding a lifestyle which will render you broke , I Esther Akoth will never date a celebrity , unless he has some brains & willing to grow, or he is damn rich, but just because he is famous ???? fame can only take you as far as getting free and easy sex, business class tickets , favours , but no stable income , the rest you pay , think !!! my opinion , good morning peeps ??

“Usimuingize mtu shimoni kwa shida na STRESS zako” ~~~~ Zamaradi Mketema.


Wengi wanatamani harusi ila wanasahau kuna maisha ya NDOA baada ya harusi, hivyo Kabla ya kukubali maombi ya mtu hakikisha umeridhika na yote juu yake mazuri na mabaya maana ndio unayoenda kupambana nayo MILELE. Usifurahie kusema I DO bila kujua unakubali kitu gani, unapokubali pale humkubali yeye tu ila yeye na matatizo, vimbwangwa, kasoro na kila alichonacho. 

Lakini inavyoonekana Karibu wengi wako tayari kuvaa shela huku mengine wakijipa moyo kujuana nayo mbele kwa mbele, wanachosahau ndoa sio kitu cha mchezo wala majaribio, ndoa inahitaji UTAYARI na sio kukurupuka. Usiolewe kwakuwa rafiki yako ameolewa huenda yeye amepata mtu sahihi hivyo isikufanye udandie yeyote alie mbele kumbuka kila mtu ataishi nyumba yake Usiolewe kwakuwa umri wako umekata kona, badala ya kupata pumziko unaweza jikuta unamalizia uzee wako vibaya na uchungu mwingi kwa kuparamia tu ukajuta maisha yote Usiolewe kwakuwa umezaa na mtu, kama si mtu sahihi UBABA hauwezi kumbadilisha kwa namna yeyote. 

Usiolewe kwa msukumo wa wazazi, utakapoingia kwenye ndoa kama ni furaha itakuwa ya kwako na kama huzuni utasema nayo mwenyewe wao kazi yao itakuwa maneno tu ambayo hayatakuwa yanasaidia chochote kwa wakati huo. Na wala usiolewe kwakuwa EX kaoa, yeye amepata alieridhika nae na sio dhambi, sasa wewe okota tu yyeyote KUKOMOA, humkomoi mtu na utaisoma mbele kwa mbele OLEWA kwakuwa uko TAYARI na umeridhika kwa HALI YOYOTE ALIYONAYO. Kwenye harusi utakuwa special kupitiliza lkn baada ya pale usitegemee uspecial uendelee, na zaidi hakuna wa kupoteza muda kila siku na nyinyi kwenye ndoa kama walivyokuwa wanapoteza? kwenye vikao vya harusi hivyo lazima ujue jinsi ya kusimama na ya kwako. Kwenye harusi kuna michango kwenye ndoa hakuna wa kukuchangia, JIPANGE. 

lakini KUBWA hakikisha unaeingia nae kwenye ndoa UNAMPENDA KWA DHATI maana ndie utalala na kuamka nae kwa muda wote wa maisha yako, sasa kama utaamua kujibana kwa usiempenda kwa ajili ya visababu fulani jua hujiumizi wewe pekee ila utaitesa hata nafsi ya anaekupenda isiyo na hatia kwa kumfanyia YASIYOSTAHILI maana hutaweza kuigiza milele, kumbuka Hakukuoa ili ATESEKE, usimuingize mtu shimoni kwa shida na STRESS zako. Mwisho ni ADHABU KWAKO pia.

ADD Friends Campaign – Epsd 014: Je, Ni sahihi kumwombea mlemavu apone Ulemavu? -Peter Sarungi

ADD Friends Campaign - Epsd 014
 Je, Ni sahihi kumwombea mlemavu apone Ulemavu?

Peter Sarungi (The Next Speaker)
Na Peter Sarungi (The Next Speaker)

Huu ni mwendelezo wa kuonesha jinsi gani imani zetu zinavyo changia kueneza fikra potofu kwa jamii juu ya watu wenye ulemavu.

Kumekuwa na tabia inayotokana na imani za baadhi ya mathehebu ya kikristu kutumia miujiza ya kuponya matatizo za watu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kukuza imani za waumini wao. Moja ya matatizo ambayo yamekuwa yakiaminishwa kwa waumini ni uwepo wa binadamu mwenye ulemavu. Baadhi ya Viongozi wa dini wamekuwa wakiaminisha waumini wao kwamba Ulemavu ni upungufu, kasoro na uumbaji usio kamilika. Wanaenda mbele zaidi na kuaminisha jamii kwamba Ulemavu ni Kazi ya shetani inayo stahili maombi na kumwomba Mungu afanye miujiza yake ya kubadilisha uumbaji huu wa shetani. Wanaamini kuwa mlemavu ni kufungwa na minyororo ya mateso ya shetani, wanaaminisha waumini sababu ya watu wenye ulemavu wengi kuwa masikini na wasioweza ni kutokana na ulemavu ulio letwa na shetani..

Je, ni kweli watu wenye ulemavu wana kasoro ya muumba?, je ni kweli uumbaji huu ni kazi ya shetani?, je ni kweli kuumbwa na ulemavu ni kufungwa na mateso ya shetani?

Bahati mbaya maombi yasipo zaa matunda yaliyo tarajiwa basi lawama zitatupwa kwa mlemavu kama mtu usiye na imani ama mwenye dhambi nyingi au utaambiwa wazazi wako au babu na bibi zako walitenda dhambi au waliingia maagano na shetani ndio maana unashindwa kupona. Hali hii inatufanya watu wenye ulemavu kujikataa wenyewe, kujiona wadhaifu mbele za Mungu, kusubiria miujiza kwa muda mrefu bila kuchukua hatua. Mnasababisha tunashindwa kuhudhuria mafundisho ya imani maana unahisi nikiingia kanisani basi mada ya mafundisho itabadilika na kuwa ulemavu wangu.

ADD Friends Campaign itafika hadi kwenye makanisa na misikiti ili kutoa elimu hii ili viongozi wa dini wasaidie kuelimisha jamii na kuondokana na fikra potofu juu ya ulemavu.

Ungana nami katika kujenga jamii yenye usawa wa imani na fikra juu ya ulemavu.

“….but attitude hata punda ako nayo” ~~~Akothee Akothee

haki I cant stand seing people asleep when am already awake by 6.00 am, I go round the house expecting to meet them awake about 8.00am, no way, only to find them fully covered in their warm blankets which they dont even know the prizes, then come to the kitchen and harrass the chef for breakfast at about 11.00 am, while the chef is already preparing for lunch, are this kind of people normal or am the abnormal one, or could I be jelouse that I cant sleep past 6.00 am & some could? am I the one who knows the value of time or am I working too hard and they be working smart under the blankets? call me acomplaining molecule, but this generation is lost period ?? I like the way my kids look at me with bad eyes when I knock on their doors ???, but attitude hata punda ako nayo , utaamka mama,
 Rule no. 
1 . No househelps should attend the girls rooms , nor their laundry 
2.  The cheff is for madboss so if you wake up late , prepare your own breakfast 
3. All the rooms in my house shoud ready by 10.00 am , so enda ulale kwa nyasi , ama uende kwako 
4. No one comes to the table for lunch with a night dress , please shower before we meet 
5. No tv during the day , no one is watching tv unless you are done with your work take it or leave it, you have freedom of migration. You cant migrate to anywhere, my girls follow suit, so any visitor should be at par with us ???? Baba Oyoo & Baba Ojwang have no househelps, they do things by themselves yet they should be retiring, with full pockets, you that has no bank account, you are afraid of breaking your nails ?????, come slowly slaying queens, Oyoo and Ojwang knows that after food you take your plate back to the kitchen, so who are you?

“Wabongo hua tunajitoa tu ufahamu lakini tunaujua ukweli tunapouona” ~~~~~~~LeMutuz

LIVE STRAIGHT TALK:- www.lemutuz.com ..."Le Mutuz Online TV" .....ni KAZI JUU YA KAZI yaani Bampa to Bampa ...leo tunaendelea na AWAMU YA PILI ya kufunga Studio's Equipments at Downtown.

Itakuwa ni kazi ya almost Wiki nzima ijayo ...I mean guys it what it is ...ila naomba niseme one thing tena on a very serious tone kumbe Wabongo wanapenda maendeleo ya kweli cause I am a Super Media Man na moja ya kipaji changu namba moja ni I am the best Observer na ndio maana nilipokuwa nasomea Criminal Investigations niliwasumbua sana Wazungu Darasani kule USA cause observations ni my thing that looking at the Facts available I can detect anything Good or Bad before they happens

Now my point is ili niuze my Social Media business ni lazima nijitangaze as I do now nilichogundua ni toka nimeanza mambo ya kujenga Studio mpaka leo sijaona tusi hata moja kuhusiana na the process au hata neno moja tu negative ....ina maana moja tu kwamba kumbe Wabongo hua tunajitoa tu ufahamu lakini tunaujua ukweli tunapouona yaani tunapenda maendeleo ya kweli ila hatupendi Blah! Blah! ....

Na hili somo nilijifunza zaidi last year from @darassacmg alipopiga ule "WIMBO WA TAIFA" na kuwafanya Wasanii wengi wenye maneno mengi waonekane waigizaji na I am also trying to tell you guys hasa Vijana wadogo kwamba unaweza ukadhani waliolkuzunguka wanakuchukia kumbe ni kwa sababu wanakuona huna maendeleo wala huna mabadiliko upo upo tu kama ulivyokuwa Mwaka jana na Mwaka huu upo vile vile hubadiliki kazi kulalamika tu! Pigana piga kelele utasaidiwa tu hakuna mtu anayetaka kusaidia mtu asiyeonyesha hata dalili ya kutaka kusonga mbele kwa matendo wachana na maneno ya "NINA IDEA" cause kuwa na idea bila mfano wa matendo ni sawa na huna kitu upo ground zero ....Idea then Plan A ikishaonekana watakuheshimu tu na kukusaidia.

Unaweza kunisikiliza au ukaniachia mwenyewe ila nimejifunza kwamba Wabongo wanapenda mendeleo na wakiyaona hawahitaji kuambiwa wanayajua...Asubuhi Njema Guys! - le Mutuz Nation

wakati wao wakiendelea kutoa fact kuna wengine wanapiga hatua za vitendo ~~~~~ Zamaradi Mketema

Wabishi waliishi miaka mingi sana, chunguza hata katika wengi waliofanikiwa sio wenye elimu iliyopitiliza ama waliotoka kwenye familia zenye uwezo PEKEE hapana, ila ni wale waliokomaa na NDOTO ZAO haijalishi background zao ni zipi, leo hii wasomi wangapi wameachwa mbali na watu kutoka streets tu, wakati wao wakiendelea kutoa fact kuna wengine wanapiga hatua za vitendo kupigana na haya maisha na WANAFIKA, lengo ni kukupa moyo wewe uliekata tamaa ya maisha eti kwakuwa hukupata nafasi ya kusoma kutokana na uwezo, ama umetokea mtaani tu kwenye familia ya kawaida/maskini, huna connection nakadhalika, usiitumie hiyo kama excuse, nataka nikwambie INAWEZEKANA hebu taja baadhi ya waliofanikiwa KIUKWELI kutoka MITAANI hata kama hawajulikani ili kuwapa NGUVU wale waliokata tamaa na kuhisi Dunia ni ya watu fulani tu.

 

Mama Igogo katika ubora wake!

Mama Igogo akifanya yake katika ubora wake, na Tshirt yake ya “I ❤ Halotel”!  This lady can’t sit down ?? Yani ukimuona mama yangu amekaa chini yani kule ku-relax nyumbani absolutely doing nothing but enjoying yourself; basi jua ni mgonjwa siku hiyo ? Kupika aliacha long time ago, rarely utamkuta akipika ila mambo yake ni kama haya analima bustani zake za mboga, viazi vitamu, mahindi, n.k….. Kama hayupo kwenye bustani ya vyakula basi kwenye banda lake wa kuku wa kienyeji, ni shidaaaa! Btw, hapo ni nje tu ya nyumba yake hivyo haitaji dereva kumpeleka shamba ?? Mama yangu was raised with two great human being I have never met before! Babu yangu na bibi yangu mzaa mama walikuwa watu wakarimu mno! Wenye upendo wa hali ya juu, waungwa sana, na wanyenyekevu kupita kipimo! Hivyo simshangai sana mama yangu kuwa hivi alivyo! Namuombea maisha marefu yenye afya njema sana na amani tele ndani ya moyo wake! Huyu ni my niece Sarah! Ni mtoto wa dada yangu Grace-AnyangoNyoyoo, lakini analelewa na bibi yake (my parents). Naona yupo likizo sasa anadeka na kwa bibi na babu ? Missing you mwanangu mie, love you always! Janeth, katoka kwake Mbezi kuja kuchuma mboga kwa mama,  kaiba na ujuzi akaenda kulima kwake ?……… siye wengine kulima hatukusaidii lakini kwenye kuvuna tutavuna na kuvifaidi wote ?? …….. I ❤ my family!

Kila mtu ni muhimu!~~~~~ Zamaradi Mketeme

Kuna watu hujishusha thamani wanapoangalia wengine wanaoonekana wamewazidi nafasi bila kujua wao huenda ni MUHIMU kuliko hata wanaowaangalia sababu ndio wanaowasababishia UKAMILIFU, 

Natamani ujue kitu kimoja hapo ulipo iwe wewe ni Mpishi, housegirl, shamba boy, messenger ama mwajiriwa tu wa ofisi fulani, thamini na RINGIA unachokifanya na usiruhusu mtu akudharau, hiko unachokifanya Boss wako hata awe na mamilioni bado hawezi kufanya na hiyo ni NGUVU. Ukichukua muda kuchunguza utagundua hakuna alie muhimu zaidi ya mwingine na KILA MTU NI MUHIMU, vipi leo mahousegirl wakigoma wote hata thamani ya hela yako utaiona!? 

Wamama wangapi nyumba zitawashinda, Jiulize Unaweza kufanya wanachokifanya wao fully!? Maana unaitwa Boss sababu kuna watu WALIOKUBALI kukutumikia, Ama hata Kama una ofisi wafanyakazi wakaondoka wote unaweza kufanya kwa ufanisi hiko wanachokifanya wao!?? Kitendo chochote cha kuweza kufanya asichoweza mwingine ni UPEKEE, na upekee ni NGUVU haijalishi unachokifanya ni kitu gani, hivyo usijidharau wala kuona kuna wanaostahili na wasiostahili.. hata kama we ni mpika maandazi mazuri mtaani RINGA, usijidharau halafu ukamuheshimu mama anaepaki gari kila siku kununua maandazi yako kwa kuhisi yeye ndio bora hapana, yeye hawezi kupika kama wewe ndiomana anapaki kwako, na huo uliopewa ni upekee mkubwa ambao wewe ndio wa kuamua uutumie vipi ili uwe na faida sababu hakuna mwingine anaepika kama wewe, 

MUNGU AMEKUPA NGUVU YAKO KUBWA kwa kukutunukia uwezo wa tofauti, hakuna alie BORA zaidi ya mwengine ila tuna MAJAALIWA TOFAUTI, asiekuwa na hiki unakuta ana kingine and viceversa, hivyo heshimu ulichonacho na UJITHAMINI, na zaidi tafuta njia ya kukifanya kwa UKUBWA hata kama ni kitu kidogo kiasi gani maana ndicho ulichopewa na MUNGU!! penye upekee wako ndipo UTAJIRI ULIPO. Haina maana kwakuwa UNATUMWA ukahisi wewe sio muhimu ama anaekutuma ndio mtu hapana, haijalishi unachokifanya ni nini since unaemfanyia hawezi kukifanya mwenyewe basi jua wewe ni wa muhimu pia.

“Hata nikifumba macho sasa nawakumbuka wote walioweka mkono katika safari yangu hata kwa ushauri tu.”~~~~Dina Marios

Katika safari ya maisha yetu kuna namna Mungu aliwatumia watu kutuvusha kutoka sehemu moja kwenda ingine. Pamoja na kupambana na kusherehekea mafanikio mbali mbali tuliyopata wapo watu walituvusha Au kutugusa kwa namna moja ama ingine. Kuanzia mwalimu alokufundisha kwa mara ya kwanza a e i o u...... binaadamu tunategemeana sana ili tuweze kufikia malengo yetu. Hata nikifumba macho sasa nawakumbuka wote walioweka mkono katika safari yangu hata kwa ushauri tu.

Hata wewe hapo ulipo najua unajua wapo waliokuamini hata wakati wewe mwenyewe hujiamini, waliokupa connection flani, waliokufundisha jambo flani, walikupokea kazini kwa mara ya kwanza wakakufundisha kazi, walikukutanisha na watu wakafungua milango ya mafanikio flani n.k

Japo kila siku tunajipa moyo kuwa tunaweza.....  tumefanikiwa......lakini wapo waliotusaidia pia tukaweza kufanikisha.........na pia sio wao ni Mungu aliwainua kwa ajili yako.

Good morning!

MOYO ULIOJERUHIWA DAWA YAKE NI FARAJA

Mr and Mrs Ridhiwani, wamependeza sana! ?
MOYO ULIOJERUHIWA DAWA YAKE NI FARAJA kama huwezi kuwa faraja kwa mwenzi wako basi ujue husitahili kupewa nafasi hata ya kumwambia HABARI... Maana halisi ya mahusiano ni wawili kunia mamoja, Huwezi kuwa MUME wake kama huwezi kuwa rafiki kwake, Kuifikia heshima ya MUME ipo ngazi inayokubidi kuipanda nayo ni "HURUMA" Mtu ambaye hana huruma hawezi kujuwa vile mwenza wake anaumia, Mtu asiye na huruma hawezi kujikosoa, Mtu asiye na huruma hawezi kujifunza maumivu ya mwingine, Mtu asiye na huruma hajui kabisa KUHESHIMU! Na mtu huyo hata mwenza wake akilia mbele yake yeye hufurahia na kujiona mshindi, Mtu asiye na HURUMA NI KATILI tena amejawa dharau na majigambo, ni mwenye kujihesabia haki muda wote... lakini pamoja na yote hayo MWANAMKE NI MVUMILIVU wala asiyekata tamaa akijenga tumaini kuwa MUMEWE ATABADILIKA wakati huo akiendelea kuumia na kulia kila kukicha, Baadaye unakuta Mwanaume huyo amemuolea Mwanamke mwingine lakini mwanamke huyo anahamia kanisani kumlilia MUNGU ili amrejeshe mumewe, Lakini mumewe hubeza na kumwambia anapoteza muda huko makanisani mnakwenda kujifunza umbea, Still Mwanamke huyo yupo tu! MOYO wa Mwanamke ni MTAMBO... Wallah wakiungana wanawake wanne kwa uvumilivu wao ni KIWANDA???

** Writen by: Elista Relief Heart ..........Picha ya Ridhiwani na mkewe haihusiki na story hii! Nimependa tu! **

LETS CHANGE OUR EDUCATION SYSTEM! – le Mutuz

LIVE STRAIGHT TALK:- The Art of Ugly FACT ni kwamba 80% ya Vijana wetu wenye Degree HAWANA UJUZI WA KUAJIRIWA PAMOJA NA KUWA NA GPA KUBWA ni ukweli mchungu ambao kama Taifa tunahitaji kutafakari as JE KUNA MAHALI TULIKOSEA? au HATUJAWAHI KUPATIA KABISA!........ninakumbuka siku moja niliwaambia Wanafunzi wa Marketing pale UDSM kuwa kama wapo waliopo Mwaka wa Pili na hawana kazi au shughuli yoyote nje ya Chuo inayohusiana na Marketing then ina maana mbili aidha Wapo kwenye wrong Field au Hawaelewi masomo sawa sawa cause haiwezekani Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Marketing akawa hana cha kuonyesha as Practical nje ya Darasa!

Leo Vijana wetu wanahangaika sana baada ya kumaliza Vyuo vyetu kwa sababu sio tu kwamba hakuna ajira bali hata zikiwepo hawaziwezi kwa sababu hawana skills inasikitisha sana as what went wrong na our Education System?...Kama Wazazi we have failed our youths na kama Taifa pia like binafsi mpaka ninamaliza High School nilikuwa tayari ninauza Siagi so sikiwahi kuwa na idea ya kuajiriwa ever in my life na bahati nzuri sana nikaenda Majuu kule nikakutana na Education System ambayo ni Full Practical na Self Reliance kwa mfano nilipoanza College Belgium I was shocked kugundua kwamba kila Mwanafunzi Darasani alikuwa anafanya kazi Part Time mahali hakuwepo hata mwanafunzi mmoja aliyekuwa anakaa tuu nyumbani bila kazi analipiwa.

Hata nilipohamia USA nilipoanza College tena mambo yalikuwa yale yale nikajifunza kusoma na kufanya kazi na kujilipia mwenyewe my Education now for that kind of system ni vigumu sana kwa mwanafunzi kumaliza Shule akakosa ajira cause like me mpaka namalizia Degree ya Tatu tayari nilikuwa na kazi nzuri ambayo nilikuwa nimeifanya kwa muda mrefu huku ninasoma Shule so ulikuwa ni uamuzi wangu kuendelea nayo au kutafuta mpya inayofanana na Elimu mpya niliyoipata ...hapa Bongo ni tofauti kabisa Vijana wetu wanasoma wakisaidiwa na Wazazi huku wakisubiri ajira za Serikali wakimaliza Vyuo na Process ya kusoma haina kabisa anything serious cha kuwatayarisha kuingia kwenye ajira au hata kufikiria KUJIAJIRI.

Halafu Wabongo tunatumia muda mwingi kulumbana na mambo yasiyokuwa na Tija kwa Taifa LETS CHANGE OUR EDUCATION SYSTEM! - le Mutuz

“we dont know why & how we ended up on the streets” ~~~~ Akothee Akothee

we were also once a happy family , we were never fatherless, we were happy to see mum and dad chart & laugh , but just from the blues , we dont know why & how we ended up on the streets , its a shock to us thank God for our mum , she walked us through this valleys , hey, where would children be without a mother ? if you are a single mother going through this moment , just know it can be done, we did it , people have been doing it , you are not Alone, get up wipe your tears & move on , type Amen if you believe in God . (Babby Daddy Njugu mawe ) may the almighty forgive those judging women with children , if it has not knocked at your door, its at your, aunties , sisters , causin , neighbours, lets stop stigma towards women & children . women cant get themselves pregnant , behind every pregnant woman , there is A man , a matold grown man . God bless all of you Happy Sabbath. (New song: Baby daddy)