Category Archives: Food

My weight loss journey has begun!

Well, well! My long overdue goal / journey sasa nimelivalia “njuga”! Jana tarehe 2, May, 2017 ndio nilianza rasmi. Nafikiri ni fair nikisema kuwa kilicho kuwa haswa kinanizuia kurudi katika uzito wangu wa miaka ya nyuma ni nilikuwa na a lot of personal issues going on ambazo zilikuwa zinaniongezea a lot of stress in my life! Yes, mie ukiniona naongezeka is more of stress issues na siyo vyakula kama baadhi ya watu wanavyo fikiria. But, I thank God now I’m in a very-very better place na naamini this time everything will be under control!!

 Malengo yangu ni ya mwaka mzima; hivyo nafuata taratibu za kiafya za kupunguza uzito wa mwili. Situmii dawa wala supplementary diet medicine ya aina yoyote! Ni mazoezi na kuzingatia nini nakula na portion gani. Mimi napenda sana smoothie? hivyo ili kuhakikisha napata virutubisho vyote vinavyo hitajika mwilini basi natengeneza smoothie za green (kama mixture ya mastafeli (sour sop), spinach / kale green, jinger kidogo, na organic unsweeten coconut milk au cashew nut milk) zingine ni kuongeza damu na calcium mwilini kama mixture ya beets roots, carrots, na a little bit of mandarins orange!……Btw, mimi napenda kutengeneza smoothie angalau za siku mbili hivi na huwa nakunywa na mwanangu. So msifikirie kuwa hilo jagi lote ni langu kwa siku moja ?? hapana! Plus bado nakula chakula mchana hizo ni morning starters na usiku tu! Well, kama nimeamua ku-share nanyi my weight loss journey basi sioni sababu ya kuwaficha my current weight! Kama mzani inavyo someka hapo juu kwa sasa nina pound 225 ?? Kulingana na urefu  na umri wangu natakiwa niwe na pound 140! Hivyo natakiwa kuondoa takribani pounds 80 ?? Je nitaweza? Naamini nitaweza! Nimejiwekea malengo ya mwaka mzima! Nitafanya juhudi zote nifikie malengo, but kama sito fika siyo mwisho wa maisha! Maisha yataendele kama kawaida! Kikubwa ni kuendelea na program yangu bila kuchoka!  Nitakuwa napima uzito kila wiki na ku-share nanyi hapa kwa blog hii! Kama nikipungua wiki hiyo basi nitamshukuru Mungu! Nakama sijapungua basi napo namshukuru Mungu and the journey continues!………Naomba ieleweke siko hapa kushindana na mtu yoyote yule!! I do me and you do you end of story!! Nafanya mambo au vitu kwa style yangu mimi na uwezo wangu mimi! Ukiwa inspired basi ni ruhusa kuniiga but am not going to sit here telling you what you should do with your body or life! And I expect you to do the same to me! Fanya yako!

Harmonize! Harmonize! Thank you So Much For This song! Yani huu wimbo keeps me moving like crazy!! Ukinikuta kwenye treadmill navyo cheza mwe! Yani nasikia mafuta ya tumbo yanakatika ??? such a nice song kwa mazoezi!…….Myweight loss journey has begun ??Mengine namwachia Mungu ??