Category Archives: General education

“hardcore truth”!

Hardcore Truth!  Huwezi kuoa au kutembea na warembo wote, wanawake wazuri siku zote wataendelea kuwepo, kila siku utakutana nao wapya. jifunze kuwa na adabu (self discpline) pamoja na kujidhibiti (self control).

Chagua mmoja tu, mjenge awe wako, mfanye awe malikia wako! hii itakupunguzia gharama, itakutunzia muda wako, drama pamoja na magonjwa.

Vile vile hakuna medali, tuzo au nishani ya juu ya ushindi wa kuwa na wanawake wengi, bali ni kuzifungia baraka ambazo Mungu anataka kukupa na kujipeleka mwenyewe kaburini mapema. Jiongeze brother!

Busara yangu; A realman sees no other females becoz he only has eyes for his girl! Mwl Tweve Hezron.

2017-Hottest And Best Couple Of The Year!

Mr and Mrs Joseph Musira ndio Hottest And Best Couple of the Year!……Sababu haswa ya kuichagua hii couple kwanza nimeamua kwa mwaka huu ni enzi wazee wetu. Pili miaka 53 ya ndoa si kitu kidogo lazima kiheshimiwe! Napia ni kwasababu wanastahili!!……Basi ifuatayo ni historia yao fupi ambayo nitaieleza kwa kutumia picha zao za sherehe ya miaka 50 ya ndoa yao (Golden Jubilee of their wedding) ambayo ilifanyika huko Musoma, Mara miaka 3 iliyopita! Sherehe hiyo ilianzia kanisani ambapo walibariki ndoa yao na kuvaa pete ya nadhiri ya miaka hamsini!…….Haya furahia picha and Happy Valentine’s Day to you all! Maombi na kiapo yakiendelea ……….. Mr Joseph Musira na Felister Awiti wao ni wazaliwa wa mkoa wa Mara. Walikutana kwa katika kijiji kimoja kijulikanacho kama Kowak katika wilaya ya Rorya mkoani Mara. Felister yeye ni mzaliwa wa kijiji hicho cha Kowak akiwa ni mtoto wa kwanza wa mzee Cornel Awiti. Wakivishana pete baada ya ndoa kubarikiwa!…….Mzee Joseph Musira yeye ni Mwalimu kwa taaluma; hivyo wakati alipokutana na Felister alikuwa ni Mwalimu wa Kowak Middle School ambayo ipo chini ya missionary ya Wakatoliki. Kwasasa shule hiyo imebadilishwa na kuwa secondary ya wasichana ijulikanao kama Kowak Girls Secondary School ambayo mimi nilikuwa ni miongoni mwa wanafunzi walio fungua shule hiyo kwa mara ya kwanza. Mdogo wangu anaye nifuata kuzaliwa naye alisoma hapo! Picha ya pamoja na viongozi wa Diocese ya Musoma ambapo mzee Musira amekuwa mtumishi wao mpaka leo hii! Alianza kwa kufundisha kama Mwalimu, baadaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa shule zote za mkoa wa Mara ambazo zinamilikiwa na kanisa Katoliki mkoani humo! Ali stahafu akiwa katika cheo hicho zaidi ya miaka 5 iliyopita, lakini kwa uwadilifu wake na maadili mema kazini walimuomba kuongoza charity organization ambayo ipo chini la kanisa hilo hapo Mwembeni street, Musoma. 

Cheti kiki kabidhiwa toka Vatican kwa Papa!….. Furaha iliyoje! Wakielekea ukumbini kwenye sherehe!…..Kama nilivyo waeleza hapo mwanzo kuwa Mzee Musira alikutana na bibi Felister katika kijiji cha Kowak akiwa Mwalimu. Basi naye bibi Felister alikuwa ni Registered Nurse katika hospitali ya Kowak Mission ambayo nayo ipo chini ya missionary ya Wakatoliki. Ambapo pia baba yake mzazi bibi Felister alikuwa akifanya kazi kama Clinical officer katika hospitali hiyo…….Miaka miwili baada ya wapenzi hawa kukutana waliamua kufunga ndoa, kula kiapo kitakatifu mbele za Mungu na uso wa dunia! Hapo ilikuwa tarehe 12 / September / 1964! Kama mnavyo jua kuwa maswala ya kuoa katika familia za Kiafrika si kitu cha mchezo kama wenzetu wa dunia ya Magharibi ambapo wapenzi wanaweza kuwataharifu wazazi wao kupitia Facebook, text msg, Tweeter, na Instagram kuwa wao wamepanga kuoana siku fulani na wazazi wakafurahia kabisa kwa furaha kuu! Hapana, ndoa ni agano takatifu lazima liheshiwe sana kwa kufata taratibu maalum za kimila na kidini! Basi ndivyo hivyo kama wafanyavyo wengine naye alifanya! Mzee Musira alifata mila za Waluo ili kuweza kumchumbia na kumuoa bibi Felister! Yeye aliambiwa atoe mahali ya ng’ombe 12 na pia amjengee mama nkwe nyumba ya mabati ya vyumba vitatu na sebule! Awwwh! Huu ukoo wa Awiti siyo watu wa sport sport ati 🙂 🙂 🙂  Si mnajua kuwa bibi Felister alikuwa msomi (Registered Nurse) wa nguvu 🙂 🙂 hivyo baba mtu hakutaka mchezo na binti yake! …….Ukisikia “mapenzi mubashara” basi haya ndo yenyewe kwani mzee Musira alitekeleza hayo masharti yote bila pingamizi! Hiyo nyumba ndio mama mkwe wake aliishi mpaka mauti ilipo mkuta mwaka 2014! Tutakiane mkono wa amani mpenzi wangu, tumetoka mbali sana. Asante sana kwa “mapenzi mubashara”…..,hayo yalikuwa maneno matamu kabisa kutoka kwa mzee Musira kwenda kwa la azizi wake bibi Felister ???   Champaign zikifunguliwa na watu wenye nyuso za furaha kabisa! Aliye vaa vazi la kitenge ni mdogo wake bibi Felister aitwaye Anna Cornel au Mrs Obure. Yeye ndiye anaye mfuatia Felister, ni Mwalimu mstahafu hapo Musoma. Baada ya kufunga ndoa bibi Felister ilibidi ahame kwenye nyumba aliyopewa kuishi kama nurse mkuu hapo mission na pia alibadili jina lake la mwisho kutoka Awiti kwenda Musira. Hapo ndipo walifanya maamuzi ya kuhamia Musoma, na miezi michache baadaye mzee Musira alipelekwa Germany kuongezea utaalamu zaidi katika fani yake! …….Waliishi Musoma kwa miaka kadhaa na baadaye mwaka wa 1970 waliamishiwa Moshi ambapo waliishi kwa zaidi ya miaka 10 kabla ya kurudishwa tena Musoma……. Mr na Mrs Musira wao wamebarikiwa kupata watoto 6. Watatu wa kiume (Musira, Gerald, na Peter) na watatu wakike (Eddina, Yasinter, na Neema). Eddina a.k.a Eddi yeye ndio mtoto wa kwanza na Neema ndio wa mwisho! Kwa bahati mbaya kijana wao aitwaye Peter yeye alisha lala usingizi wa mauti; hivyo hayupo nao tena! May his soul continue to rest in peace!Mungu pia amewajalia kupata wajukuu wanne! Wakiume watatu na wa kike mmoja!  Wakinyweshana kinywaji maalum cha siku hiyo Mahaba mahabani! Kama walivyo shikamana siku ya kwanza pale Kowak basi ndivyo watakavyo shikana mikono yao mpaka mauti itakapo watenganisha! Waki kata keki kwa upendo na furaha Nilishe nikulishe ndio ishara ya upendo Mungu ni pendo. Penye Mungu kuna upendo mwingi na furaha isiyo elezeka! Hapa siongelei tu ndoa za “maigizo”, zile ndoa za ku-show off picha kwenye mitandao ya kijamii wakati ndani ya nyumba zenu wengine hawahemi! hapana! Naongelea real marriage, real commitment, honoring your vowels!!………. Miaka 53 ya ndoa hakuna michepuko wala mtoto wa “bandia”! Jamani, inawezekana!! These are real people in our communities; nina huwakika wapo wengine wengi tu!………Ee Mwenyezi Mungu endelea kumimina baraka zako kwenye hii ndoa na familia yao, Amen!

Mother and daughter moment

Katika wazazi ambao nawahurumia pia na mu-admire sana ni mama yake Wema Sepetu! Ni mmoja wa wazazi ambao wanapitia changamoto nyingi sana katika maisha ya kila siku kutokana na maisha ambayo binti yake ameamua kuishi; hivyo kahilo namuhurumia sana! Lakini kama nilivyowai kusema huko nyuma (somahapa) kuwa ni mama ambaye ananifurahisha sana na jinsi anavyo simama bega kwa bega na binti yake, katika mabaya na mazuri! Kwa wazazi wa Kiafrika ni ngumu sana! Wachache mno wanaweza fanya afanyavyo mama Sepetu! Na kwasababu hiyo anakua mfano mzuri sana wa kuigwa! Mtoto wako ni mzigo wako mpaka kifo. Huwezi mkana au mkataa mtoto wako eti kwasababu tu haendani na maisha utakayo! Big up mama Wema!

 

ASANTE JPM KUBARIKI VITA HII (Sehemu ya II)- Peter Sarungi

 

Na Peter Sarungi (Next Speaker)“Vita ya dawa za kulevya haina umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu anahusika mkamateni” Raisi Dkt. Magufuli…….Katika vita hii, nilikuwa nasubiri kauli ya mkuu wa kaya ya kutoa support ya ulinzi, usalama na hata kubariki vita hivi alivyo vianzisha Mh. Makonda (RC. Dar)  Kauli alizozitoa Mkuu wa kaya wakati wa kumwapisha Mkuu wa Majeshi Tanzania yana ashiria ushiriki wa moja kwa moja wa mkuu wa kaya. Majibu ya JPM kwa kauli ya Mh. Nape ni firimbi kwa viongozi wengine wanao leta sababu nyingi za kunyamazisha vita hii wakati vijana wana angamia. 

“Kauli ya Raisi ni agizo linalo hutaji utekelezaji bila kusita” Peter Sarungi @2017

TUSIBEZE VITA HII (Sehemu ya I)- Peter Sarungi

 Tusibeze uthubutu wa mtu tena kijana wa kawaida ambaye bado hajawa nguli katika siasa wala uongozi. Tumpe muda maana hiyo vita aliyoichagua ni vita ngumu inayo hatarisha maisha yake. Huyu ndiye kiongozi pekee wa kumuombea tofauti na wengine. Huyu yupo kwenye vita ambavyo kama wewe ungepewa fursa ya kuwa mkuu wa mkoa huu basi inawezekana ungeshindwa kudeal hata na dagaa kama Makonda alivyoanza. Tumpe moyo mkuu na kumwombea kwa Mungu apigane vita vizuri, naamini hata kama hatashindwa kufikia mafanikio tunayoyataka lakini atakuwa amefanya sehemu flani ya kutatua uovu huu ambapo mwingine atakaye jitokeza katika vita hiyo ataanza alipo ishia Makonda. Hatuwezi kunyamaza kimya kwa tatizo kubwa kama hili na asitokee hata mtu mmoja wa kusema hata kidogo alafu tukajiona tupo samala, Laa hasha kukaa kimya ni kuhalalisha uwepo wa tatizo. Vijana wengi wana angamia na kupoteza nguvu kazi na vipaji kwa sababu ya kukaa kimya na hata kubeza jitiada hizi ndogo zinazo chukuliwa na Makonda. Tuungane na Makonda kutenda na kufikiri tofauti kwa kuchukua hatua za kutenda badala ya malalamiko na matamko yasiyo isha wala kusaidia jamii. Tuweke siasa pembeni kwenye majanga makubwa kama haya ili kuunga kila hatua zitakazo chukuliwa na yeyote katikakupambana na Tatizo hili. 

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

Asanteni..

Sabato Njema wana wa Mungu.

If you sign up for a “sex only” relationship in the beginning…..! Don’t ask him to wait if you can’t!

Ujumbe huu unajieleza wazi kabisa! Kama wewe nia yako ni kuwa na mume basi usitafute boyfriend kwani nia ya malengo yako hayata timia! Kama nia yako ni kuwa na mtu wa ku share naye mapenzi maisha yako yote basi usikubali tittle ya “my lover au mwanamke wangu” kwani hivyo ndivyo utakavyo ishia! Respect is earned not given!…………. Na usimwambie mwanaume ngoja mpaka tufunge ndoa wakati wewe si bikira! 😉 😉 ……….. Happy early Valentine to you all!

WIZARA INA MIKAKATI GANI JUU YA WATU WENYE WALEMAVU TANZANIA?- Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

Watu wenye ulemavu ni moja ya jamii iliyo katika makundi nyonge (kwa sasa tumefika milioni 4 kwa idadi). Makundi mengine ni kama wazee, watoto na wanawake, makundi haya yanaitwa ni makundi nyonge kwa sababu yana mahitaji maalumu ya kibinadamu na hayawezi kumudu ushindani ulio sawa katika jamii hivyo ni lazima jamii pamoja na serikali iyatizame kwa jicho la tatu lenye utu, huruma na upendo ili nao wajione wapo katika nchi yao na waweze kuonesha uwezo wao ambao Mungu amewakirimu pasipo kujali mapungufu waliyo nayo. 

Peter Sarungi akiwa na dada zake; Alpha Igogo (kushoto) na Magreth Igogo (kulia) nyumbani kwa Peter huko Chanika.

Mimi ni Mlemavu lakini hata wewe ni Mlemavu mtarajiwa maana kama bado unaishi duniani basi jua Mungu bado anaendeleza uumbaji wake kwako. Hivyo linapotokea jambo linalohusu ulemavu basi jihisi na wewe ni mhusika kwa namna moja ama nyingine.

Katika uchaguzi uliopita 2015, nilitoa tamko kupitia jumuiya za watu wenye ulemavu Tanzania ambao ulilenga kueleza changamoto za walemavu pamoja na mapendekezo yake. Changamto kuu nilizoziainisha kwa msisitizo ni ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika vyombo vya maamuzi pamoja na muundo wa kusimamia maswala ya watu wenye ulemavu. Niliamini kuwa ili kutibu changamoto hizi za elimu, ajira, afya, uchumi, siasa na huduma zingine ni vizuri tukashirikishwa katika kupika chakula na kukiandaa mezani.

Nilifarijika sana baada ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza baraza la Mawaziri pamoja na muundo wa wizara zake, kwa kweli mhe. JPM alitutendea haki ambayo haikuwahi kutendwa na tawala tangu kupatikana kwa uhuru wa nchi. JPM alisikia kilio cha watu wenye ulemavu kwa kutenga wizara itakayo husika na maswala ya walemavu tena ikiwa chini ya ofisi ya waziri mkuu kama tulivyotoa kwenye tamko na pia akateua waziri mwenye asili ya ulemavu (dr. Abdallah posy) na makatibu wa wizara wawili wenye ulemavu akiwemo mwanasiasa Amon Mpanju ili kushiriki kupika chakula cha walemavu. Hakika baada ya uteuzi huu, jamii ya qatu wenye walemavu tulianza kuona nuru na kuona matumaini ya kula chakula tulichoshiriki kukipika na kukiandaa mezani. Nampongeza sana Raisi kwa moyo huu wa kujali makundi manyonge katika jamii(Mungu azidi kumpa afya tele na azidi kutetea wanyonge kama anavyofanya sasa)

TATIZO NI NINI?????

Kwa mtazamo wangu, bado naona hakuna mabadiliko chanya yanayoletwa na wizara hii hasa kutoka kwa waziri husika Mh.Posy. Bado mifumo ya unyonyaji imeendelea kuwepo kwenye vyama vya watu wenye ulemavu, bado uchumi umezidi kudorora kwa watu wenye ulemavu, bado Elimu imekua duni na garama kwa watu wenye ulemavu, Bado siasa haiwatambui watu wenye ulemavu kwa vitendo, Bado sheria No 10 ya watu wenye ulemavu imewekwa kando, Bado ajiri imekuwa ngumu na ya kubagua watu wenye ulemavu na bado huduma bora imekuwa ni kitendawili kwa watu wenye ulemavu.

Je ni nani wa kututetea? Ni nani wa kutusemea kama sio Mh. Posy na wenzake akina stella ikupa, Dr. Macha, Amina Mollel, Amon Mpanju na wengine walio katika kundi hili?. Ni nani wa kulaumiwa ikiwa JPM ametupa nafasi kupitia hawa wenzetu alafu wamekaa kimya? Ni nani wa kuonesha mfano na kuaminisha jamii juu ya uwezo wetu kama sio akina Posy, Mpanju, macha, stella na wenzake? Ni nani wa kupiga kelele juu ya mateso na manyanyaso wanayoyapata wafanyabiashara walemavu wa Tanzania kama sio akina Mh. Posy, Mpanju na wenzake waliopata fursa? Ni nani wa kutuunganisha watu wenye ulemavu na kupata fursa za uchumi na siasa kama sio hawa walio teuliwa na JPM? Mbona wamejisahau utafikiri hawajatoka katika kundi hili? Au wanadhani fursa waliyopata ni kwaajili yao peke yao? Au ndo kusema ni aibu na dhihaka kuwa mlemavu na kutetea jamiiyako? Mbona kasi ya JPM inawaacha mbali? Tatizo ni nini?

Tulikaa kimya na kuwapa ushirikiano ili kuona matunda ya kushirikishwa katika kupika chakula lakini inakaribia mwaka sasa hatuoni kama chakula mnachotupikia ni kizuri…

Tafakarini na chukueni Hatua…. 

Tafadhali, naomba ifahamike yakuwa hii article iliandikwa wiki mbili zilizopita wakati Dr. Posy akiwa bado ni Waziri. Lakini sasa nafasi yake ipo wazi!

Womanhood!

“Sometimes I really wonder!”- Sandra Mushi

Sometimes I really wonder! How we can just wake up and pull ‘sherias’ out of our hats. Sasa ati no spot lights, no fog lights and no tints …

How about you install street lights on ALL streets and actually have them ON and working; and how about having proper and working security measures including when I come report a theft, you actually attend to it and FOLLOW it up!  Instead of asking for ‘chai’ na ‘nauli’ kila kukichwa.

Those lights are our safety so I don’t have to worry about driving into a bridge on a dark night.  They are my safety so I can see clearly on a rainy day.  They are my safety so I can see that drunkard staggering from a far even before I get to that corner.

Those tints are our safety so I don’t have my windows broken as I am sitting in a meeting simply because the street boy saw my gym bag on the back seat.  They are my safety so when they want to follow me home they are not sure who is in the car.  They are my safety so that conniving motor cyclist does not see that its a lone woman driving.

Hembu do your due diligence basi and assure us of our safety before you mercilessly start imposing this ‘out of the hat’ sheria on us.

You do your part and we will humbly oblige and do ours.

TAIFA LA JANA, LEO NA KESHO…. na Peter Sarungi

Imeandikwa….

1. Baba bora ni yule anayelinda na kutetea familia yake, anaye tengeneza urithi mzuri kwa watoto, wajukuu hadi vitukuu na anaye hashimu familia yake.

2. Mke mwema ni yule anaye jenga familia yake bila kuharibu kwa mikono yake, anaye lea watoto katika maadili mema na anaye simama imara na mumewe katika hali ya hatari, dhiki, shida, raha, hofu, furaha, matatizo kama ya siasa, umasikini, chuki, wakati wa ujana na uzee, wakati wa afya na magonjwa.

3. Mtoto bora ni yule anaye heshimu wazazi wake na kujifunza maadili na maarifa kutoka kwa walio mtangulia. Ambaye anapenda kuwa kichwa na si mkia. 

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

#MyTake.

Vijana ambao wamefika umri wa kujenga familia wachukue hatua kufanya hivyo, wasisubiri harusi na madoido ya kifahari maana kuna maisha ya ndoa baada ya kupata sifa za harusi.

??Fidel Pilato alikuwa akiangalia post zangu  za nyuma huku akijaribu kuuliza maswali katika lugha nisiyo tambua.???…Hao ndio watu wazima wadogo, Taifa la kesho. NIWATAKIE MWANZO MZURI WA WIKI………MUNGU BARIKI KAZI YA MIKONO/AKILI ZENU.

Pastor Caleb Migombo: The Most important advice for life’s crossroads is this:

Pastor Caleb Migombo

The Most important advice for life’s crossroads is this:

” Seek God’s will.” He knows what’s best for you and me, and He doesn’t want us to wonder aimlessly through life.

Never forget: God made you, and He knows all about you-including the gifts and abilities He gave you. More that, He loves you and wants what is best for you. Maybe you’ve been living for yourself and for the moment rather for Him and for things eternal. But don’t stay on that path; you will only end up at a blank wall if you ignore God’s plan for your life. 

“I will instruct you and teach you in the way you should go; I will counsel you and watch over you” Psa 32:8

HUYU ANA MOYO MKUU…..by Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker)Kwa sasa ni nadra sana kupata binadamu walio umbwa na Moyo Mkuu, moyo unao weza kuhimili shida, kejeli, dharau, matusi ma vikwazo mbalimbali vyenye lengo la kulainisha Moyo. Mh. Lowasa Edward alikumbwa na kashfa akiwa CCM tena Waziri Mkuu, akasemwa na kutukanwa na viongozi, wanachama na wapenzi wa chama kikuu cha upinzani Chadema Tanzania, huku akiitwa Fisadi nchi nzima… Alikaa kimya bila kujibu.

Alipo hama CCM kwenda CDM, CCM walimuona kama msaliti ingawa kwa CDM alibadilika na kuwa Malaika. Bado aliendelea kutukanwa, kudharauliwa na hata kuombewa mabaya na viongozi, wanachama na wapenzi wa chama tawala kipindi cha uchaguzi 2015… Alikaa kimya bila kujibu.

Pamoja na yote hayo, bado ameendelea kuwa na Moyo Mkuu kwa nchi yake. Huyu namfananisha na Mh. Raila Odinga wa Kenya na Mh. Kiiza Besige wa Uganda kutokana vikwazo wanavyopitia. Mungu awatimizie haja ya mioyo yao.

Tujifunze kitu hapo, unajifunza nini?

MH. LOWASSA ANAIJUA SIASA YA TANZANIA-Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a Next Speaker a.k.a Baba Pilato

Siasa za Tanzania bado hazieleweki kwa wananchi wengi na mimi nikiwemo. Wengine wanaiita siasa maji taka, siasa za kujipendekeza, siasa za mafigisu, siasa za mamluki na usaliti, siasa za propaganda, siasa za nguvu ya umma na nguvu ya dola, siasa za uongo, siasa za kidiplomasia, siasa za matukio, siasa za maigizo, siasa za maonyesho na mimi kwa sasa naziita siasa za Mwendo Kasi.Kwa Tanzania, ni Mh. Lowasa Edward pekee anaye jua siasa za nchi, anayeweza kubadili njano kuwa nyekundu, anayeweza kupanga na kupangua, anayeweza kubadilika kutokana na mazingira, anayeweza kumpenda adui yake hata kwa unafiki, anayeweza kubadili msimamo wa mpinzani wake, anayeweza kumbadili mpinzani kuwa mfuasi wake, anayeweza kupiga ngoma kisha serikali ikacheza, anayeweza kuwa na chama ndani ya chama, anayeweza kusababisha mafuriko ama hata kuyatengeneza, anayeweza kusababisha taharuki mtaani anapo onekana nahata kuwapa hofu watawala.

Kumekuwepo na kauli nyingi za kukubali ama kukataa uwepo wa njaa na uhaba wa chakula kwa muda wa zaidi ya wiki bila kuwepo kwa solution. Lakini Mh. Lowassa alipokuja na kauli ya kuwa na nia ya kutafuta chakula kwa ajili ya wahanga kwa madai kuwa Mkuu kakataa kutoa chakula kwa wahanga ikiwa ni sehemu ya kuleta suluisho la tatizo, jana serikali ikajibu mapigo kwa kusema ita sambaza chakula na ina hifadhi tosha ya chakula.

Viongozi kama akina Mh. Lowassa ni muhimu sana kwa jamii yetu hata kama wasipo weza kutawala nchi lakini uwepo wao na uwezo wao katika siasa za nchi intosha kufanya mabadiliko nje ya ya mfumo rasmi na kuleta matokeo chanya ya maendeleo..

Tutafakari kwa matendo bila hisia za vyama.

Ubaguzi wa watu wenye ulemavu nani alaumiwe na nini kifanyike?!

Hongera sana shule direct kwa jitihada zenu za kuokoa maisha ya watoto katika nyanja ya elimu!……Binafsi najiuliza hivi nani wakulaumiwa na nini kifanyike juu ya watu wenye ulemavu?! Mimi nasema ni ubaguzi wa wazi wazi kwa watu hawa na jamii imelifumbia macho! …….Miaka ya nyuma tulisema kuwa watu hawana uwelewa na leo hii je tunasemaje?! Shule moja ya secondary ya viziwi tena ni private?! Majengo mengi yanajengwa bila kujali kuwa tunao walemavu katika jamii yetu!! Majengo na maeneo mengi hakuna parking za magari specific kwa walemavu! Makanisa mengi sana hayana wakalimani wa viziwi! n.k………Huu ubaguzi ni mpaka lini? Nani wakulaumiwa? Na nini kifanyike? ……..Tafakari na chukua hatua!

Malezi ya watoto na changamoto zake!

Pole sana mpendwa, tunamuombea uponyaji wa haraka! …….tukio hili limenikumbusha jinsi my cousin brother alivyo “piga pasi” tumbo lake!  kaka yangu alikuwa na tabia ya kunyoosha sehemu za shati lake ambazo zimejikunja huku akiwa teyari amevaa!! Kumbe mtoto anamuangalia na siku moja akachukua pasi iliyokuwa yamoto Akanyoosha tumbo lake! It was an awful experience! He was  2.5 yrs old by then sasa hivi anakwenda miaka 30 na sidhani kama anakumbuka hilo tukio!…….Anyway, malezi ya watoto yana changamoto nyingi sana. Wewe mzazi unaweza kuwa makini lakini watu unao ishi nao wakawa ni majanga! Nikuomba Mungu tu kama una amini kuwa Mungu yupo!…..Juzi nilisimuliwa kisa cha mtoto wa cousi-sister wangu ambaye house girl alimfungia ndani ya nyumba akiwa amelala halafu yeye akaenda shule kumfata mtoto mkubwa, with a assumption kuwa “atawahi kurudi”! Too bad alipofika shule, siku hiyo walikuwa wamekwenda picnic picnic wakawa wamechelewa kurudi ikabidi dada wa kazi amsubiri! Mtoto aliye achwa nyumbani he is barely 3 yrs old!! Aliamka usingizini haoni mtu ndani ya nyumba! Mtoto kalia mpaka kachoka ma njaa juu! Mama mtu anarudi nyumbani anakutana na hayo majanga! Yani ni alimfukuza house girl siku hiyo hiyo!…..Sasa can you imagine kama moto ungewaka ndani ya nyumba na mtoto kachwa mwenyewe? Au mtoto angechezea jiko la gas ambalo wanalo hapo ndani! Hivi ingekuwaje?! . ……Malezi ya watoto yanahitaji maombi ya ziada kwani bila Mungu hatuwezi!

Vita ya drugs inatakiwa kuanza na sisi wenyewe majumbani mwetu- Lemutuz

Katika kuitafuta furaha usimuumize mtu mwingine ili wewe uwe na furaha- Dina Marios

Katika kuitafuta furaha usimuumize mtu mwingine ili wewe uwe na furaha.Kila lililopangwa kuja kwako litakuja tu kama Mungu amelipanga kuja.  Huwa nayatazama maua yakiwa bustanini.Ni maua ya aina tofauti lakini hupokezana kuchanua.Hili litakaa miezi hata tisa bila kuchanua lakini siku likichanua linapendeza kweli kweli,lingine huwa limechanua mara zote,lingine huitaji jua kali ili lichanue na kupendeza.Ndivyo hata sisi tulivyo hatufanani na kila mmoja ana wakati wake wa kuchanua…wakati wake wa kufanikiwa.Sidhani kama yale maua huwa yanaoneana wivu mbona yule kachanua mimi sijachanua?Usiitazame furaha ya mwenzako ukateseka nayo,mafanikio yake ukateseka nayo na wewe ukaitaka pengine na yeye ni kama lile ua linalokaa miezi tisa ndio lichanue.Itazame safari yako na wewe wakati wako ukifika utachanua Utang’ara.

Katika  kuitafuta furaha na mafanikio njiani usimkanyage mtu,usimuumize mtu.Unaweza kufanikiwa leo lakini sio milele.Kufumba na kufumbua mambo yanaweza kubadilika.Unaweza kuwa kwenye nguvu na control leo lakini huwezi kuushinda muda…muda hubadilika….Good morning!

MATOKEO YA KELELE ZA #BringBackBenAlive NI YAPI NA YAMEISHIA WAPI?- Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Watu wa Makabila yanayo patikana mkoa wa Mara (Kwetu Pazuri) wana desturi ya kuwa jasiri, wakweli na wenye uwezo wa kusimamia jambo analo liamini. Lakini huku jijini Dar tulipokuja kutafuta maisha, mambo yake yanaendeshwa kwa usanii, unafiki, uoga, dilli, uongo na kutafuta kicky pasipo sababu ya msingi.

Uozo huu umeingia hadi kwenye siasa kiasi kwamba huwezi kutofautisha siasa za chama tawala na zile za Upinzani yaani wote wamekuwa wafuasi wa mambo hayo ya jijini.

Wahusika Tuelezeni, kwanini mpo kimya kwa swala mlilo lianzisha? na mtuambie matokeo chanya ya #Bring_Back_Ben_Alive ?

Msianzishe kampeni katika mitandao halafu mkaziacha katikati bila kujua hatima yake, What if Ben amedhurika? Kelele zenu na ukimya wa Ghafla utakuwa umemsaidia nini Ben? Tafakari, Chukua hatua… 

SIASA NA DEMOKRASIA YA KENYA….. TUNAJIFUNZA NINI KATIKA MIFUMO YAO??-Peter Sarungi

 

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Taarifa zinaonesha kuwa kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Jamhuri ya watu wa Kenya ndio nchi ambayo ina mifumo inayo tekeleza Siasa huru na Demokrasia ya kiwango kizuri ukilinganishs na nchi zingine katika ukanda huo. Pamoja na kuwepo kwa Siasa za Ukanda na Makabila kwa muda mrefu lakini bado siasa zao zimekuwa ni za mfano kupita zetu za Tanzania.

Je, tunajifunza nini? kuna lipi unalo lijua kuhusu mfumo wao ambacho kwetu hakipo? Je, wananchi wao na wana siasa wao wana tabia gani ambazo ni tofauti na kwetu Tanzania? Saidia kujadili ili tupate Ufahamu.

Ladies! Pursuing man is nowhere in the Bible!