Category Archives: General

Hongera sana Dr. Mwele Malecela! -Alpha Igogo

Kulia nataka na kucheka nashindwa kwani it’s a “Bittersweet moment” kwa Watanzania wazalendo! Kuondolewa kwako kulituumiza sana kwani wengi tunajua dhamani yako na umuhimu wako kwa taifa la Tanzania! Soma hapa ? Dr.Mwele Lakini kama wasemavyo Mungu si Athumani, na kamwe Mungu hamtupi mja wake; basi hatuna budi kusema hongera sana Dr. Mwele kwa kazi yako mpya kwenye shirika la afya duniani -WHO (Africa)! 

Mungu akuongoze na akubariki katika kila jambo jema ulitendalo. I’m very happy for you! Just go and shine-out as you always do! Congratulations! 

“TLS ; CHADEMA’s legal department or another opposition party?!!!” – Chege Kilahala

TLS ; CHADEMA’s legal department or another opposition party?!!! There are legal boundaries within which these institutions can carry out their daily duties……using TLS as a mouthpiece to pursue some political agenda is a no-no-no-no!!!  

TAFAKURI YA LEO JUU YA WABUNGE WA CCM.- Peter Sarungi

Peter Sarungi (The next Speaker)

Tabia ya wana siasa kabla ya kuwa watawala ni kama tabia za wachumba ambao bado hawajafunga ndoa. Tabia yao kuu ni kuhaidiana mazuri, kusifiana, kuelekezana kwa lugha ya kuvutia, kutiana moyo, kuoneshaana upendo wa agape lakini pia kuna tabia moja mbaya ya walioyo nayo ya kuficha udhaifu wao na mabaya yao.

Kila inapoitwa leo, napata fursa ya kujua tabia za mkuu wa nchi kupitia kauli zake na matendo yake. Niliwahi kukiri hapo mwanzo kwa kusema kuwa Mkuu wa kaya anasimamia vizuri kauli na matendo yake wakati wa kampeni nikidhani ataendelea kutawala kupitia kauli zake za kusisitiza umoja wa nchi. Nahisi ni mihemuko ya muda iliyo niathiri.

Pamoja na changamoto hizo bado maisha na siasa zitaendelea na ni lazima tuendelee kuwaoma wabunge hasa wa CCM ambao ni 75% kusimamia kwa kuikosoa, kuisema na hata kuipongeza serikali wanapo kuwa bungeni maana hiyo ndiyo kazi tuliyo watuma. Pamoja na mtikisiko huu ulio wapata wabunge kutoka kwa Mkuu wa kaya kama ilivyo ripotiwa na gazeti la mwananchi bado mtaendelea kuwa wabunge mlio pewa dhamana na wananchi ya kuwa wakilisha bungeni katika kuisimamia serikali.

Tusijenge Taifa la chuki na uadui unao tokana na siasa, tuki ruhusu hilo basi hatutokuwa salama maana ukweli ni kwamba chuki na uadui havina mipaka, nikikuchukia kwenye siasa usidhani nitakupenda uraiani. Hiyo ni mbegu mbaya itakayo tafuna jamii yetu.

Tujitahidi kujenga jamii ya kuvumiliana, kushauriana, inayo heshimu fikra tofauti na inayoweza kuwa karibu hata kama watakubali kutokukubaliana.

Mungu tubariki huko tuendako.

TATIZO MMEKUBALI KUCHEZA NGOMA ZINAZO PIGWA NA UPINZANI.- Peter Sarungi

 Kwenye ngoma zetu kuna wanao piga ngoma na kuna kundi la wanao cheza ngoma inayopigwa. Siku zote mpiga ngoma ndiye mwamuzi wa aina gani ya mdundo upigwe ili mcheza ngoma acheze, mpiga ngoma akizima ngoma basi na mchezaji naye anasitisha kucheza, mpiga ngoma ndiye ana amua speed ya ngoma ama ngoma ipigwe kwa muda gani.

Siasa za sasa za nchi ziko kisayansi sana kiasi kwamba upinzani wametawala njia nyingi za upashaji habari. Siasa hii naifananisha na ngoma zetu za jadi, yaani ni kama vile upinzani wanapiga ngoma ili watawala wacheze.

Hii ngoma ya wapinzani imeanzwa kuchezwa tangu mwaka jana baada ya utawala mpya kuanza kazi, upinzani umeshapiga ngoma kwa midundo mingi sana tofauti iliyomfanya mtawala kucheza bila kuchoka.

Hizi ni baadhi ya ngoma zilizopigwa na upinzani na watawala wakacheza kwa maana ya kujibu mapigo.

1. Ukuta

2. Uchwara

3. Phd

4. Michango ya Tetemeko

5. Njaaa

6. Bring back ben alive

7. Free Lema

8. Free Max wa JF

9. Swala la uteuzi wa wabunge

10. Bashite

Haya ni machache yaliyo vuma na kuchukua headlines za magazeti na mitandao ya jamii. Na hizi zote zimekuwa zikianzishwa kwa malengo ya kuonesha na kuaminisha mapungufu ya serikali kwa wananchi.

Siwalaumu upinzani maana hiyo ndiyo sayansi ya siasa na ndiyo kazi yao, ila nawalaumu sana chama tawala na watawala wenyewe kwa kushindwa kupiga ngoma zao ili upinzani nao wacheze. Ninavyojua mimi, JPM amefanya mambo makubwa ambayo yanatosha kuwekwa kwenye haedline kwa muda mrefu, lakini wasaidizi wa watawala na wapenzi wa chama tawala wamekaa kimya na kujikuta wakijibu mashambulizi ya upinzani katika hoja zao bila kujua kwamba wanacheza ngoma. Hizi kick ndizo zinazo pamba upinzani usisahaulike hadi 2020 hata kama mkikataza siasa za majukwaa.

Au labda watawala wamejitoa kwenye ulingo wa siasa? Au wapenzi wa chama tawala wameshindwa kuusoma mchezo wa siasa? Huu mchezo hautaki hasira wa mabavu ya dola ila unataka mkakati wa kujivunia mazuri yanayo fanywa na Utawala Chama tawala kukaa kimya na kucheza ngoma za upinzani ni sawa na huyu ☝ aliye kabidhiwa brifkes ya ofisini akaringa bila kujua kuwa imetoboka. Amkeni mpige ngoma wapinzani wacheze, fanyeni kama Magoiga SN.

Asanteni

Women to women is an event you don’t want to miss it out!

JUKWAA LA WATU WENYE ULEMAVU TANZANIA-na Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (The next Speaker)

 Nitumie fursa hii kutoa shukurani kwa wote walio jitolea na hata kufuatilia kwa karibu juu ya uundwaji wa Jukwaa la Watu wenye Ulemavu Tanzania. Mpaka sasa tumekamilisha 95% ya taratibu za kusajili Taasisi hii muhimu kwa walemavu. Jamii ya watu wenye ulemavu imeendelea kutengwa katika mipango mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa sababu ya kukaa kimya bila kusema juu ya changamoto zetu, uwezo wetu, vikwazo tunavyokumbana navyo na hata mafanikio yetu. Ni muda sasa umefika wa kusema kwa nia ya kutetea na kushawishi maswala ya watu wenye ulemavu Tanzania ili na sisi Tanzania tufanane na wenzetu wa Afrika Mashariki walio amua kutekeleza kwa maneno na vitendo mkataba wa UN unao husu jamii ya walemavu na ni mkataba ambao Mh. Mkapa aliridhia na kusaini kisha Mh. Kikwete kuruhusu utungwaji wa sera na sheria no.9 ya watu wenye ulemavu na sasa kilichobaki ni kupiga kelele juu ya utekelezaji wake.

Ni jukumu letu sote kupiga kelele tena bila utengano na kwa sauti moja hata kama wewe sio mtu mwenye ulemavu lakini ukiguswa na hili basi ni sahihi kusema kwa nguvu hadi jamii, serikali na wadau wengine wapate kusikia ujumbe huu. Kuna msemo unasema hivi…

“Mtoto anayelia na kupiga kelele sana ndiye anaye pewa nyonyo na mama yake, ukinyamaza maana yake umeshiba”

Sidhani kama sisi watu wenye ulemavu tumeshiba katika nchi yetu, la hasha ila tuna ugulia kimya huku tukifa na tai shigoni. Ukimya wetu ndio unao tufunga, unao turudisha nyuma, unao tififisha ndoto zetu, unao tukosesha thamani na ndio sababu ya kutengwa na fursa.

Tanzania amka useme jambo kwa jamii hii ili na wewe ushiriki katika kutetea na kushawishi maswala ya watu wenye ulemavu Tanzania.

Women to women event, dare not to miss it!

Womanhood!

Jojo and the Carters’!

Awwwih! Umesoma hiyo caption?! Isn’t that something! Nilisema last year around October or November kuwa Jokate is our “Princes Diana” she is going to be big kuliko unavyo fikiria and conquer the unconquerable! Keep on shining Jojo vijana wa Tanzania na Africa wanakutegemea sana. Show them the way!  We love you!Wow! Mungu ajalie kheri tu kwani tunawakaribisha kwa mikono miwili!

Je, upo tayari?! Couple yangu ya pili -2016

Are you ready!!! Hii ndio ilikuwa couple yangu ya pili kuichagua. Mpaka sasa sijajutia kuichagua. Yani couple zote bado zipo kwenye mahaba mazito sana!! Nawaombea Mungu ndoa zao zidumu milele na awatangulie katika kila jambo! Kama ulipitwa soma HottestAndBestCouple-2016 …….. Je, upo tayari kwa 2017?!! Stay tuned!

Pastor Caleb Migombo: If we looked only at the headlines every day……!

If we looked only at the headlines every day, we would have good reason to be pessimistic about the future. But don’t forget two important truths.

First, the future is in God’s hands, and nothing takes Him by surprise. He is sovereign over the history of the world as well as our own personal histories, and behind the scenes He is at work to accomplish His purposes.

Second, never forget that even when the future is unclear, God is with those of us who are trusting Christ as our Savior and Lord, and He helps us. No matter what the future holds for you-no matter what today holds for you-you do not face it alone if you know Christ.

The Lord reigns forever.

Psalm 146:10  Kama tungeliangalia tu vichwa vya habari za kila siku, tungekuwa na kila sababu ya kukata tamaa juu ya siku zijazo mbele yetu. Lakini imetupasa kutosahau ukweli huu.

Kwanza, siku zijazo mbele yetu ziko mikononiu mwa Mungu, hakuna kinachomshangaza au kumshitukiza Mungu. Yeye ni Mtawala juu ya tawala zote za dunia, juu ya matukio yote ya historia ya ulimwengu, na hata matukio na historia ya maisha yetu binafsi. Nyuma ya pazia ya matukio yote haya, Yeye yuko kazini usiku na mchana  kutimiza makusudi yake.

Pili, Kamwe usisahau kwamba hata pale ambapo siku zijazo hazielewekieleweki zitakuwaje (unapoona giza), Mungu yupo pamoja nasi na wote wanaomtumainia Bwana katika maisha yao. Yuko tayari kutusaidia siku zote. Bila kujali lipi litatokea kwako katika siku za usoni- bila kujali leo itakuwaje kwako- kumbuka kuwa hutayakabili maisha na siku zake pekee yako, kama unamjua, na umempa Kristo moyo wako. 

Bwana anamiliki Milele…Kizazi hata kizazi. Haleluya

Zabri 146:10

je, upo tayari?! Couple yangu ya kwanza -2015

Nilipo anza ku-blog ilikuwa ni mwezi wa Pili mwaka 2015. Na hii ndio ilikuwa couple yangu ya kwanza kabisa kuichagua kama Hottest and Best Couple of the yr kwa mwaka huo! Nikitu niliamua kufanya kila tarehe 14/2 ya mwaka (siku ya Valentine day) nitatangaza couple moja iliyonivutia ambayo pia naona kuwa ni mfano mzuri wa kuigwa katika jamii! Kama ulipitwa na tangazo hilo tazama hapa ? HottestAndBestCouple-2015

Je, upo tayari kwa mwaka huu?? Stay tuned!!

WIZARA INA MIKAKATI GANI JUU YA WATU WENYE WALEMAVU TANZANIA?- Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

Watu wenye ulemavu ni moja ya jamii iliyo katika makundi nyonge (kwa sasa tumefika milioni 4 kwa idadi). Makundi mengine ni kama wazee, watoto na wanawake, makundi haya yanaitwa ni makundi nyonge kwa sababu yana mahitaji maalumu ya kibinadamu na hayawezi kumudu ushindani ulio sawa katika jamii hivyo ni lazima jamii pamoja na serikali iyatizame kwa jicho la tatu lenye utu, huruma na upendo ili nao wajione wapo katika nchi yao na waweze kuonesha uwezo wao ambao Mungu amewakirimu pasipo kujali mapungufu waliyo nayo. 

Peter Sarungi akiwa na dada zake; Alpha Igogo (kushoto) na Magreth Igogo (kulia) nyumbani kwa Peter huko Chanika.

Mimi ni Mlemavu lakini hata wewe ni Mlemavu mtarajiwa maana kama bado unaishi duniani basi jua Mungu bado anaendeleza uumbaji wake kwako. Hivyo linapotokea jambo linalohusu ulemavu basi jihisi na wewe ni mhusika kwa namna moja ama nyingine.

Katika uchaguzi uliopita 2015, nilitoa tamko kupitia jumuiya za watu wenye ulemavu Tanzania ambao ulilenga kueleza changamoto za walemavu pamoja na mapendekezo yake. Changamto kuu nilizoziainisha kwa msisitizo ni ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika vyombo vya maamuzi pamoja na muundo wa kusimamia maswala ya watu wenye ulemavu. Niliamini kuwa ili kutibu changamoto hizi za elimu, ajira, afya, uchumi, siasa na huduma zingine ni vizuri tukashirikishwa katika kupika chakula na kukiandaa mezani.

Nilifarijika sana baada ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza baraza la Mawaziri pamoja na muundo wa wizara zake, kwa kweli mhe. JPM alitutendea haki ambayo haikuwahi kutendwa na tawala tangu kupatikana kwa uhuru wa nchi. JPM alisikia kilio cha watu wenye ulemavu kwa kutenga wizara itakayo husika na maswala ya walemavu tena ikiwa chini ya ofisi ya waziri mkuu kama tulivyotoa kwenye tamko na pia akateua waziri mwenye asili ya ulemavu (dr. Abdallah posy) na makatibu wa wizara wawili wenye ulemavu akiwemo mwanasiasa Amon Mpanju ili kushiriki kupika chakula cha walemavu. Hakika baada ya uteuzi huu, jamii ya qatu wenye walemavu tulianza kuona nuru na kuona matumaini ya kula chakula tulichoshiriki kukipika na kukiandaa mezani. Nampongeza sana Raisi kwa moyo huu wa kujali makundi manyonge katika jamii(Mungu azidi kumpa afya tele na azidi kutetea wanyonge kama anavyofanya sasa)

TATIZO NI NINI?????

Kwa mtazamo wangu, bado naona hakuna mabadiliko chanya yanayoletwa na wizara hii hasa kutoka kwa waziri husika Mh.Posy. Bado mifumo ya unyonyaji imeendelea kuwepo kwenye vyama vya watu wenye ulemavu, bado uchumi umezidi kudorora kwa watu wenye ulemavu, bado Elimu imekua duni na garama kwa watu wenye ulemavu, Bado siasa haiwatambui watu wenye ulemavu kwa vitendo, Bado sheria No 10 ya watu wenye ulemavu imewekwa kando, Bado ajiri imekuwa ngumu na ya kubagua watu wenye ulemavu na bado huduma bora imekuwa ni kitendawili kwa watu wenye ulemavu.

Je ni nani wa kututetea? Ni nani wa kutusemea kama sio Mh. Posy na wenzake akina stella ikupa, Dr. Macha, Amina Mollel, Amon Mpanju na wengine walio katika kundi hili?. Ni nani wa kulaumiwa ikiwa JPM ametupa nafasi kupitia hawa wenzetu alafu wamekaa kimya? Ni nani wa kuonesha mfano na kuaminisha jamii juu ya uwezo wetu kama sio akina Posy, Mpanju, macha, stella na wenzake? Ni nani wa kupiga kelele juu ya mateso na manyanyaso wanayoyapata wafanyabiashara walemavu wa Tanzania kama sio akina Mh. Posy, Mpanju na wenzake waliopata fursa? Ni nani wa kutuunganisha watu wenye ulemavu na kupata fursa za uchumi na siasa kama sio hawa walio teuliwa na JPM? Mbona wamejisahau utafikiri hawajatoka katika kundi hili? Au wanadhani fursa waliyopata ni kwaajili yao peke yao? Au ndo kusema ni aibu na dhihaka kuwa mlemavu na kutetea jamiiyako? Mbona kasi ya JPM inawaacha mbali? Tatizo ni nini?

Tulikaa kimya na kuwapa ushirikiano ili kuona matunda ya kushirikishwa katika kupika chakula lakini inakaribia mwaka sasa hatuoni kama chakula mnachotupikia ni kizuri…

Tafakarini na chukueni Hatua…. 

Tafadhali, naomba ifahamike yakuwa hii article iliandikwa wiki mbili zilizopita wakati Dr. Posy akiwa bado ni Waziri. Lakini sasa nafasi yake ipo wazi!

Matukio katika picha: Jesse 11th birthday

Kheri ya siku ya kuzaliwa mwanetu Jesse! Mungu azidi kukulinda, akuongoze, na azidi kukubariku katika ukuaji wako! Ukawe mtoto mwema sana Wapendwa, naomba niseme kidogo kuhusu undugu wangu Jesse……..Bibi yake Jesse mzaa baba ni mtoto wa pili kuzaliwa kwa familia ya mama yangu (familia ya marehemu mzee Cornel Awiti); hivyo Jesse ni mpwa wangu! Siku ya tarehe January 16, 2017 Jesse alitimiza miaka kumi na moja tangu kuzaliwa kwake! Alisherekea na wazazi wake Dr. Joseph Obure, mama yake Venny Mwita, na mdogo wake Jason!  Jesse na wazazi wake wana ishi huko North Carolina, U.S.A Mama na birthday boy!  Lovely! Happy 11th birthday Jesse!

Tafadhali, embu m-follow Miss Universe wetu please!

Wapendwa wasomaji wangu, mmemuona mrembo wetu?! Miss Universe-Tz 2017!! Si mnamuona anavyo lipa? Je, ume m-follow?! Kwanini bado?! Basi mpendwa fanya hima m-follow leo kich weka comments nzuri za kumtia moyo japo “number don’t lie” she is doing great! Please let support our very own Jihan Dimack!………Soon nitakuja na maelezo ya jinsi ya kumpigia kura! Asanteni!

The diary of Lady Jaydee is coming back!!

I’m super happy, the legendary’s reality TV show is coming back!!! #DiaryOfLadyJayDee! Can’t wait to watch it!!…. Yani kipindi kile ilipokuwa inaanza nilikuwa likizo Dar, nilikuwa nakitazama kila siku kilipokuwa hewani sikupitwa! Na ile scene ya mwisho wakiwa Arusha na X-husband wake pamoja na “Machozi” band ndiyo nilianza kuhisi something is seriously wrong kwa ndoa yao kwani things didn’t add-up!! Well, yote maisha tu! Happiness is what matters! …….Jamani tumpe support our JayDee najua sponsors wakubwa watajitokeza sana kwani nakumbuka mama Anna Mkapa alikuwa big fan wa show yako na alikuwa akiitangaza sana! Well done Jide keep it up!

NIWATAKIE HERI YA MWAKA MPYA 2017 WENYE BARAKA NA MAFANIKIO TELE- Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Kwanza: kabisa, tumshukuru Mungu kwayote yaliyojiri mwaka 2016 yawe mabaya ama mazuri bado tuna wajibu wa kushukuru maana fikra na malengo yetu sio ya Muumba

Pili: Tumshukuru Muumba kwa kuendelea kutupa Uhai usiokuwa na upungufu hata kama upo kitandani ukiwa hoi kwa magonjwa na maumivu makali ama upo bar unakunywa pombe na kufanya starehe mbalimbali, wote yatupasa kumshukuru Muumba kwa huruma yake na upendeleo.

Tatu: Tupeane pole kwa wote tuliopatwa na kuguswa na misiba mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2016, tuwaombe wapendwa wetu kwa mungu awarehemu na kuwahifadhi mahala pema mbinguni. Safari ni yetu sote, wao wametangulia tu.

Nne: Tusikate tamaa kwa matarajio tuliyoshindwa kufikia na wala tusibweteke kwa majarajio tuliyafikia katika kipindi cha mwaka 2016 maana Maisha ni mchakato. Ni harakati za kukusanya mambo manne (4) kwa pamoja ili kupata furaha (happy), mambo hayo ni pesa, heshima, afya na mapenzi. Hivyo jua kama wewe una afya njema jua kina mwenzako yuko maututi, kama wewe unapendwa kwa dhati jua kuna mwingine ana danganywa, kama wewe una pesa ya kukidhi mahitaji yako jua kuna mwingi ni fukara asiye na matumaini na kama wewe una heshimika basi jui kuna mwenzako amekuwa teja anayekosolewa mitandaoni. 

Tano na Mwisho, Niwatakie Mwanzo na mwendelezo mwema wa mwaka 2017 ukiwa na baraka, amani, furaha na mafanikio tele katika mipango yako ya mwaka mpya. Mungu akupe nguvu na ujasiri wa kutambua uwezo na karama yako ili uweze kufanya mambo makubwa na uyapendayo katika mwaka 2017. Mwaka 2017 uwe ni mwaka wa kujivunia tofauti na mwaka 2016 ingawa ni mwaka usio gawanyika kwa 2 kama tulivyo aminshwa na wakubwa zetu hapo zamani.

Mungu awa bariki sana na asanteni kwa kuwa mmoja kati ya marafiki wengi, ndugu wengi na jamaa wengi tulio shirikiana kipindi cha mwaka 2016.

Wametengeneza historia kwetu!

Kama maelezo ya picha zao yanavyo someka. Hawa wajukuu wa Chief Sarungi Igogo wametengeneza historia ndani ya ukoo wetu kwa mwaka huu! Mnamo tarehe 11 mwezi wa Kumi; Maria Sarungi-Tsehai alikuwa mmoja wa watu walioalikwa kutembelea WhiteHouse ya Marekani chini ya group lijulikanalo Kama Eisenhower Fellowship ambapo walipokelewa na mwenyeji wao Rais Baraka Obama ••••••• Vile vile wiki hii siku ya tarehe 28 Dec  Janeth Igogo-Nyagilo alibahatika kumtembelea na kuzungumza kidogo na bibi yake  Rais wa Marekani-Baraka Obama huko Kogelo, Kenya ambako bibi huyo anaishi. Janeth yupo huko Kagan, Kenya kwa mapumziko ya Christmas na familia yake. Mumewe Janeth ni mzaliwa wa kijiji cha Kagan, Kenya •••••• ? Haya hongereni kwa kuweka historia hiyo kwenye ukoo wetu kwa kuwa watu wakwanza kufanya hivyo ????

Kumbe mama Mkamba ni mama mkwe wangu eeh!

Poleni sana wapendwa roho yake bibi iyendelee kupumzika kwa amani!……. Nimefurahi kuona kuwa mama Makamba ni mama mkwe wangu ?? watanijua Mjaluo mie hata kama hawataki ?? Tutafungulia Tanga kwa Mzee Yusuph Makamba halafu tunafungia Kyaka kwa mama Makamba wenye wivu wajinyonge tu maana hamna namna ??……… R.I.P Omukare Ma Eugenia!

Jokate naye atakuwepo! ……Dare not to miss it!

screenshot_2016-12-13-14-59-40-1screenshot_2016-12-13-15-00-34-1Mrembo wetu naye kasema atakuwepo! Jamani hii event siyo yakukosa kabisa! Please buy your ticket now!