Category Archives: General

Matukio katika picha: Mh. ShyRose Bhanji amtembelea Naibu Waziri Office ya Waziri Mkuu

fb_img_1476065228008“Coutesy Call: During this week I was privileged to be received by Hon. Dr. Abdallah Possi,Abdallah Possi Deputy Minister of State PMO in-charge with Persons with Disabilities at his office. In our discussions I obtained a deeper insight about the scope of challenges facing the people with disability. I admire his knowledge, passion and dedication to his ministerial tasks. I thank him for the warm reception and wish him all the best.”….. Hon. ShyRose Bhanji fb_img_1476065221813“Wiki hii nilipata fursa ya kumtembelea Mhe. Dkt. Abdallah Possi- Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ofisini kwake. Katika mazungumzo yetu nimepata uelewa mkubwa na mpana zaidi kuhusiana na masuala na changamoto kuhusu watu wenye ulemavu. Nimevutiwa sana na uelewa wake, fikra zake na kujituma kwake ktk Wizara yake. Ninamshukuru kwa mapokezi mazuri na kumtakia Kila yeri na ufanisi”……….. Mh. ShyRose Bhanji

fb_img_1472436063790Asante Muheshimiwa, tunajifunza mengi sana kupitia wewe sisi wadogo zako wake kwa waume. Ubarikiwe sana

 

Muwe na wiki njema: Mchumia juani hulia kivulini!

img-20161008-wa0000fb_img_1472436063790Mchumia juani hulia kivulini!!………. Najua kwa wenzangu wa Tanzania na East Africa au Africa kwa ujumla sasa hivi ni asubuhi siku ya JumaTatu, watu wameanza na maangaiko ya wiki pamoja na kufanya kazi! Basi naomba niwakumbushe kuwa tafuta tena kwa bidii zote lakini kiwe halali siyo vya mkato wa njia za “panya”! Najua ni ngumu sana kuchumia juani lakini siku zote matunda yake ni matamu sana!! Usiwe na tamaa kwasababu unawaona wengine wanasonga mbele kwa speed ya mwendo kasi ukadhani kuwa wewe unamatatizo, hapana! Siyo vyote ving’aavyo ni dhahabu au almasi!!……..  Usitoe wala kupokea rushwa! Rushwa ni adui wa haki! Rushwa inarudisha maendeleo ya nchi yako na maendeleo yako binafsi nyuma! Rushwa inaondoa amani! Mla rushwa ni wakuogopa kama ukoma!……….Swali la kizushi; nasikia Dr. Magufuli siku hizi wala rushwa wote anawatupia Kigoma mwisho wa reli ??? Muwe na wiki njema. Mbarikiwe sana!

Pole sana Said!

screenshot_2016-10-07-14-11-58-1fb_img_1472436063790What a sad story!……..Kwakweli hii habari imeniuma sana. Nilikuwa sijawahi isikia nilep hii ndio naiyona. Kusema ukweli binadamu tumekuwa viumbe hatari sana si tu kwa wanyama na mazingira tunayo ishi bali hata kwa binadamu wenzetu! How cold is this??!! ……..eeh Mungu tusaidie sisi viumbe vyako shetani ametawala si tu akili zetu bali hata roho na mwili! Tunakuhitaji Baba tusaidie!…..,,,, Pole sana Said Mungu akupe uwezo wa kukubali hali yako mpya na uwendelee na maisha??

“Kama kuna kina mama wengine mliwahi kuibiwa na huyu mtuhumiwa please jitokezeni sasa” Lemutuz

screenshot_2016-10-07-10-24-09-1screenshot_2016-10-07-10-24-03-1

Heshima yangu kwa walimu wote duniani!

fb_img_1475719937795img_20161005_125547fb_img_1472436063790Leo ilikuwa ni siku ya walimu duniani. Nawashukuru na kuwapongeza walimu wote katika dunia hii! Nilishawahi kusema kuwa uwalimu ni wito na karama ya pekee sana ni wachache walio jaliwa nayo. Mimi sikujaliwa ma karama hiyo?? hivyo I salute all great teachers around the globe including my uncle / baba yangu mkubwa kwenye picha hapo juu ? Mzee Joseph Musira (me wa mama yangu mkubwa, first born wa kina mama). Yeye ni Mwalimu mstaafu na pia alikuwa Mkurugenzi wa elimu kwa diocese ya Musoma kwa zaidi ya miaka 20! Yeye ndiye mlezi wa mama yangu pindi mama yangu anasoma secondary kama maelezo yake uanavuosema hapo juu. Vile vilealikuwa mlezi wangu wakati nasoma Kowak Girls Secondary school.  Kwakua yeye alikuwa Mkurugenzi wa elimu Mkowa wa Mara kwa shule zote za Roman Catholic basi kila Mwezi alikuwa anakuja shule hivyo ilikuwa ni rahisi kwani wazazi wangu walikuwa wanaishi Dar es salaam……….Namtakia maisha marefu zaidi na amani tele. Mungu bariki walimu wote dunia.  Happy Teachers  Day to baba mkubwa and all other teachers!

GOLI LA MKONO LIPO HATA KWENYE SIASA-Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

Jana katika jiji la Dar kulikuwa na mpambano wa jadi kati ya Yanga na Simba. Mpambano ulikuwa na mbwembwe nyingi na mwisho wa siku ikawa 1-1. Kilichonifurahisha ni Goli linalioitwa la Mkono alilolipata Tambwe. Mimi ni yanga na kweli furaha yangu ni ushindi tu iwe ni kwa mafigisu ama kwa halali. Goli hili nalifananisha na Goli la Mkono katika siasa, kuna mwanasiasa mmoja aliwahi kusema kuwa watashinda hata kwa bao la mkono…..Magoli kama haya ni adimu sana na ndio yanaleta furaha/huzuni na utamu/uchungu wa mpira kama ilivyo mafigisu ya siasa wakati wa uchaguzi. Goli ni goli tu ikiwa limekubaliwa na mwamuzi.

fb_img_1475607447757Hongereni watani wangu wa Jadi kwa kurudisha kwa Goli zuri la Kichuya. Ila hamkuonesha ustaharabu katika mchezo baada ya kuharibu viti na miundo mbinu mingine. Mkiendelea na ushabiki huo wa vurugu kutakuwa na haja ya anko Magu kuwafundisha adabu ili mje mumuite Dikteta kama kawaida ya wabongo wengi.

Tukutane tena Round ya Pili.

Please Vote for Ali Kiba…!

screenshot_2016-09-27-22-31-31-1 screenshot_2016-09-27-22-31-50-1fb_img_1472436063790Mimi nimeshampigia kura wewe je? Tafadhali weka uzalendo mbele chukua dakika yako moja tu na ulete ushindi nyumbani! Ali Kiba ni fahari yetu sharti tujivunie kwa kuonyesha upendo na ushirikiano wetu kwake! Haya piga kura hiyo!

WIZARA INA MIKAKATI GANI JUU YA WATU WENYE WALEMAVU TANZANIA?-Peter Sarungi

fb_img_1474834103266-1
Peter Sarungi

Watu wenye ulemavu ni moja ya jamii iliyo katika makundi nyonge (kwa sasa tumefika milioni 4 kwa idadi). Makundi mengine ni kama wazee, watoto na wanawake, makundi haya yanaitwa ni makundi nyonge kwa sababu yana mahitaji maalumu ya kibinadamu na hayawezi kumudu ushindani ulio sawa katika jamii hivyo ni lazima jamii pamoja na serikali iyatizame kwa jicho la tatu lenye utu, huruma na upendo ili nao wajione wapo katika nchi yao na waweze kuonesha uwezo wao ambao Mungu amewakirimu pasipo kujali mapungufu waliyo nayo.

Mimi ni Mlemavu lakini hata wewe ni Mlemavu mtarajiwa maana kama bado unaishi duniani basi jua Mungu bado anaendeleza uumbaji wake kwako. Hivyo linapotokea jambo linalohusu ulemavu basi jihisi na wewe ni mhusika kwa namna moja ama nyingine.

Katika uchaguzi uliopita 2015, nilitoa tamko kupitia jumuiya za watu wenye ulemavu Tanzania ambao ulilenga kueleza changamoto za walemavu pamoja na mapendekezo yake. Changamto kuu nilizoziainisha kwa msisitizo ni ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika vyombo vya maamuzi pamoja na muundo wa kusimamia maswala ya watu wenye ulemavu. Niliamini kuwa ili kutibu changamoto hizi za elimu, ajira, afya, uchumi, siasa na huduma zingine ni vizuri tukashirikishwa katika kupika chakula na kukiandaa mezani.

Nilifarijika sana baada ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza baraza la Mawaziri pamoja na muundo wa wizara zake, kwa kweli mhe. JPM alitutendea haki ambayo haikuwahi kutendwa na tawala tangu kupatikana kwa uhuru wa nchi. JPM alisikia kilio cha watu wenye ulemavu kwa kutenga wizara itakayo husika na maswala ya walemavu tena ikiwa chini ya ofisi ya waziri mkuu kama tulivyotoa kwenye tamko na pia akateua waziri mwenye asili ya ulemavu (dr. Abdallah posy) na makatibu wa wizara wawili wenye ulemavu akiwemo mwanasiasa Amon Mpanju ili kushiriki kupika chakula cha walemavu. Hakika baada ya uteuzi huu, jamii ya qatu wenye walemavu tulianza kuona nuru na kuona matumaini ya kula chakula tulichoshiriki kukipika na kukiandaa mezani. Nampongeza sana Raisi kwa moyo huu wa kujali makundi manyonge katika jamii(Mungu azidi kumpa afya tele na azidi kutetea wanyonge kama anavyofanya sasa)

TATIZO NI NINI?????
Kwa mtazamo wangu, bado naona hakuna mabadiliko chanya yanayoletwa na wizara hii hasa kutoka kwa waziri husika Mh.Posy. Bado mifumo ya unyonyaji imeendelea kuwepo kwenye vyama vya watu wenye ulemavu, bado uchumi umezidi kudorora kwa watu wenye ulemavu, bado Elimu imekua duni na garama kwa watu wenye ulemavu, Bado siasa haiwatambui watu wenye ulemavu kwa vitendo, Bado sheria No 10 ya watu wenye ulemavu imewekwa kando, Bado ajiri imekuwa ngumu na ya kubagua watu wenye ulemavu na bado huduma bora imekuwa ni kitendawili kwa watu wenye ulemavu.

Je ni nani wa kututetea? Ni nani wa kutusemea kama sio Mh. Posy na wenzake akina stella ikupa, Dr. Macha, amina mollel, amon mpanju na wengine walio katika kundi hili?. Ni nani wa kulaumiwa ikiwa JPM ametupa nafasi kupitia hawa wenzetu alafu wamekaa kimya? Ni nani wa kuonesha mfano na kuaminisha jamii juu ya uwezo wetu kama sio akina Posy, Mpanju, macha, stella na wenzake? Ni nani wa kupiga kelele juu ya mateso na manyanyaso wanayoyapata wafanyabiashara walemavu wa Tanzania kama sio akina Mh. Posy, Mpanju na wenzake waliopata fursa? Ni nani wa kutuunganisha watu wenye ulemavu na kupata fursa za uchumi na siasa kama sio hawa walio teuliwa na JPM? Mbona wamejisahau utafikiri hawajatoka katika kundi hili? Au wanadhani fursa waliyopata ni kwaajili yao peke yao? Au ndo kusema ni aibu na dhihaka kuwa mlemavu na kutetea jamiiyako? Mbona kasi ya JPM inawaacha mbali? Tatizo ni nini?fb_img_1474834072101Tulikaa kimya na kuwapa ushirikiano ili kuona matunda ya kushirikishwa katika kupika chakula lakini inakaribia mwaka sasa hatuoni kama chakula mnachotupikia ni kizuri…

Tafakarini na chukueni Hatua….

Matukio katika picha: Jokate Mwegelo

screenshot_2016-09-25-15-11-31-1kapendeza sana…… Mie nafikiri Jokate angekuwa Motivational Speaker for youths angefaa sana! I believe she can do a great job!fb_img_1474834252077Beautiful!

“Tupo kwa ajili ya kuliendeleza Taifa letu kwa faida liendelee mbele”- Innocent Mungy

fb_img_1474807609205-1Kumekuwa na Mjadala kuhusu ndege Mpya za ATCL! Nimeikuta hii mahali na naweka hapa wengine nao waone! Nikiwa X-staff wa iliyokuwa ATC, ninaelewa! Wakati mwingine ni vizuri kujua hadi uamuzi unafikiwa watu wamefanya utafiti, hali halisi ya viwanja vyetu na sababu zipi kwa chaguo husika!

BOEING VS BOMBARDIERfb_img_1474548653290KWANINI TUMENUNUA BOMBARDIER?

Shirika letu la ndege lilikufa kwasababu ya kushindwa kujiendesha kutokana na gharama kubwa za uendeshaji pamoja na ufinyu wa abiria wanaotumia usafiri wa anga!

Mwanzo nilifikiri labda ni wizi unafanyika lakini baada ya kujua gharama chache za uendeshaji nikaona ni sawa kwa shirika hili kushindwa kujiendesha.

Naomba nianze na bei ya Boeing

Boeing inauzwa dola milioni mia mbili tisini na sita(US296millions) wakati Bombardier Q400 inauzwa dola milioni 35 tu(US35millions)

Kumbe badala ya kununua Boeing moja ni heri tuongezee dola milioni kumi na tisa(US19millions) tununue Bombardier tisa(Bombardier 9)

Hesabu yake:

Boeing price US296 millions
Bombardier Price US35 millions
(35×9=315)
315-296=19

Ambapo hizi Bombardier tisa zingetusaidia kwa upande wa shirika kujiendesha lenyewe na kutupatia faida kubwa kwa mara tisa kwa Taifa.

Kuhusu Speed ya Boeing ni kweli ni kubwa kuliko Bombardier kutokana na uchomaji wa mafuta, Speed yake ni 590mph wakati speed ya Bombardier ni 414mph au 667km/h

Kama kutoka Dar to Mwanza ni Km 1100 maana yake Bombardier itatumia saa moja na dakika arobaini (1 hr and 40mnts) wakati Boeing itatumia saa moja na dakika kumi na tano(1hr and 15 mnts) tofauti ni dakika 25 tu

Boeing inatumia dumu moja la mafuta la lita 4 kwa sekunde moja kwa hiyo kwa lisaa limoja inatumia lita elfu kumi na nne mia nne (14,400) (4l×60s×60m)

Kwa mfano:

Mafuta ya ndege kwa lita yakiuzwa shilingi 2000 maana yake ili tutie mafuta ya kuelekea safari ya Songea inayochukua takriban saa moja tu tunahitaji milioni 28,800,000(14,400×2000)
Na tunahitaji abiria 96 watakaolipa Tsh 300,000 ili kuweza kulipia gharama za mafuta tu.

Hapo hatujajumlisha gharama za service na wafanyakazi na wala hatujapata faida yoyote

Bombardier inatumia 1.187lita ya madumu ya mafuta kwa mile moja yaani ukikadiria inatumia lita moja ya mafuta kwa mile moja (1mile=1.6kms)
Songea to Dar Air Distance ni takribani kilometa 537=335.625miles

Kwahiyo itatumia lita 398.386875 ambazo ukizizidisha kwa gharama ya Tsh 2000 kwa lita unapata laki saba tisini na sita elfu mia saba sabini na tatu=796,773

Kiuchumi kugharamika 28,800,000 na kugharamika 797,000 bora kipi?

Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu na mwenye kutaka shirika hili kujiendesha kwa kibiashara ni lazima atumie Bombardier ili apate faida.

Pia kutokana na hali ya viwanja vyetu ndege hizi zinafaa kwa sababu zinaweza kutua katika viwanja vya kawaida ndio maana serikali ilizinunua ndege hizi mahususi kwa safari za ndani!

Hizi ndege Bombardier Q400 zinatumika Marekani na wanaendelea kununua Shirika la ndege la American Eagle wanazo Bombardier 35 Uingereza nao shirika la ndege la Flybe wamenunua 40.

Australian Air wamenunua 20
Ethiopia wamenunua 4 kufikisha idadi ya Bombardier 19.

Hatuwezi kutenga bajeti ya serikali iende ikahudumie shirika la ndege ambalo ukitumia akili ya kiuchumi hili shirika linaweza kujiendesha na likaliletea faida Taifa na kuliinua kiuchumi.

Hatupo kwa ajili ya kujishow off kutumia ndege za gharama kubwa na zisizo na faida ili watu watuone tuna ndege kubwa no! 

Tupo kwa ajili ya kuliendeleza Taifa letu kwa faida liendelee mbele. screenshot_2016-09-25-07-13-21-1

Sharing is caring!

Kumbe Joyce Kiria ni wifi yangu!

screenshot_2016-09-22-07-31-32-1Mwe! Leo nilikwenda mchungulia mama wa #Mwanamke Piga Kazi! Eeh! Sinikakutana na hii post yake anasema “harudi mtu Kibosho”! Ndio nikagundua kumbe Joyce ni shangazi yake mwanangu ??? Haya Joyce kuanzia leo mie nakuita wifi ole wako ukatae undugu na mimi ??? Halafu sijui nitoboe siri nyingine ??? ngoja nilewe kwanza zikipanda nitamwaga radhi lol!……. Hongera wifi yangu wewe mchakarikaji sana. Lakini wifi, huoni wewe kufanya biashara ya kupika unawanyima riziki mama ntilie?! Kwa nini wewe using’ang’anie “Wanawake Live”!…….Nawaza tu kwa sauti??

“Ni matarajio yetu kwamba nauli itashuka”- Shy-Rose Bhanji

fb_img_1474548653290Pongezi nyingi zimfikie Kamanda Mkuu Rais JPM kwa uamuzi wake wa kufufua Shirika la Ndege Tanzania-ATCL. Ni faraja kuona ndege 2 mpya baada ya kilio cha wengi kutaka usafiri wa ndege upatikane kila kona ya nchi. Ni matarajio yetu kwamba nauli itashuka na huduma itakuwa ya uhakika. Ni faraja kwamba sasa tutaanza kufanana na nchi wenzetu wanachama wa EAC ktk usafiri wa anga.fb_img_1474548662004Congratulations to our Commander in Chief HE JPM for availing 2 planes for ATCL. It is to our great relief that air transport will improve considerably. We believe the fare and service will be customer friendly and that we shall be at Par with other EAC member states in terms of air travel.

Prayer is a weapon!

screenshot_2016-09-20-14-41-53-1Maombi ndio silaha! Hauitaji kukesha kanisani ndo maombi yako yasikike, hapana! Hata ukiwa unatembea omba kimoyo moyo! Hata ukiwa unaoga wewe omba tu na maombi yako yatasikika! #Usikate Tamaa

Dada wa taifa katika ubora wake!

fb_img_1474291961145fb_img_1472436063790Mie nampenda sana dada yetu! Such a humble lady! Unafiki kwake ni mwiko! Anajali, ana heshimu, na kuthamini watu wote bila kujali rangi zao, wala vyama vyao vya siasa. Ee Mungu tulindie dada yetu na uzidi kumbariki! We love you Shy-Rose Bhanji!

What a tribute! Hongera Diamond!

screenshot_2016-09-19-07-23-38-1fb_img_1472436063790Hongera sana Chibu Dangote umetisha sana “mnyama”! Mie kwakweli nimezipenda zote ila kama nataka ku-dance kisawa sawa then version ya Saida karoli ndo nitaiweka kwani ile migoma na midundo inaniinua kwenye kiti! Lakini kama nataka just to have a little fun na kucheka na marafiki zangu basi version ya Diamond ndo nitaiweka! Mwanangu yeye amependa zaidi version ya Diamond! ………but in general BRAVO! Very well done! Btw, napenda sana yule Harmonize ana nyimbo zenye ujumbe mzuri sana. I love him as well!……. Gosh! Where is my brother Ali Kiba jamani! Aje basi! Mie sina timu I enjoy kusikiliza nyimbo za Diamond more lakini nawapenda wote. Kiba mtoto wa mtaani kwetu tumekuwa wote so he’s my brother and I will always be his fan!!

Nawatakieni wiki njema!

fb_img_1474287833296Wapendwa, nawatakieni wiki njema yenye amani, upendo, furaha, na mibaraka tele! Mbarikiwe!

Jackie furniture store

fb_img_1474033262013 fb_img_1472436063790Haya jamani mrembo wetu Mrs Mengi katufungulia duka la furniture la kisasa kabisa na quality ya hali ya juu huko Sea cliff, Dar es salaam liendalo kwa jina la “Jackie”! Basi kama wewe ni mpenzi wa furniture na uwezo wako unakuruhusu basi Jackie ndo sehemu yako! Usikose!….fb_img_1474033220417Hongera sana! Mlipendeza mno warembo, I loved Nancy’s dress more!

Tunawatakie EID njema!

fb_img_1473683206327fb_img_1472436063790EID njema wapendwa!kumbuka Halotel bado ndiyo habari ya mujini na vijijini! Jiunge nao leo wala hauto jutia!…….. EID Mubarak to all Muslims around the world!

The Flowers of True Love- by Susan Igogo

screenshot_2016-09-11-16-05-19-1img-20160911-wa0000-1-1Wapendwa, wale wanao penda kusoma vitabu haswa romantic books basi hichi kitabu si chakukosa! Wahi leo upate copy yako! Nikitabu kilicho andikwa na mwana dada wa Kitanzania aishie Marekani anaye julikana kwa jina la Susan Igogo. Embu msome kidogo hapa ?screenshot_2016-09-11-16-06-02-1fb_img_1472436063790Kitabu kinapatikana online na offline @Amazon.com, Barnes&Noble katika format ya hardback $24.99, Paperback $15, na Ebook $3.99…….. Get your copy now and enjoy the book without forgetting to give us the feedback! Asanteni sana!

Pata ushauri wa bure toka kwa “Fikia Mafanikio”!

screenshot_2016-09-11-08-52-32-1fb_img_1472436063790Haya wapendwa mliyopo Bongoland, “Fikia Mafanikio” inatoa ushauri wa bure kabisa ya jinsi ya kufikia na namna ya kugimoza ndoto zako ulizo nazo! Nenda Facebook na “LIKE” page yao kisha watafute kama unahitaji msaada wao! Ukiona mtu anakupa free advice katika maswala ya msingi; basi si sehemu pa kukosa hapo. Wahi ujipatie ushauri wa bure toka kwa wataalam!fb_img_1473601933687