Katika pita pita yangu huko Facebook nikachungulia kwa mama wa “Wanawake Live” a.k.a “Mwanamke piga kazi” a.k.a “Super woman”……….. Nilipochungulia nikaona post ambayo chanzo chake ni Jamii Forum! Post hiyo ilikuwa inamuhusu yeye Joyce Kiria kuwa kwanini havai pete ya ndoa? Embu soma hiyo post hapa chini kabla ya kusoma maoni yangu Mimi naamini kuwa kuna umuhimu wa kuvaa pete ya ndoa lakini si lazima kwasababu zifuatazo:- (1) kama wewe ni mtu upo kwa macho ya jamii kila wakati basi ni muhimu watu wakajua your identification ya mambo ya msingi kama marriage status yako. Lakini si lazima! Yani nisawa na kusema wakristo wabebe Biblia mikononi au vichwani muda wote ndio tuamini kuwa ni wakristo! Hapana! (2) Kuvaa pete ya ndoa 24/7 haichangii kuongeza wala kupunguza upendo kati yenu nyie wawili kama kweli mna mapenzi ya dhati! Upendo wa kweli hutoka moyoni nasio kwenye pete! (3) Sio wote waitao Bwana Bwana watakao uona ufalme wa Mungu! Basi ndivyo ilivyo kwa wanandoa; sio wote wavaao pete ya ndoa 24/7 ni waaminifu katika viapo vyao! Tabia ya mtu haibadilishwi na pete! Rejea scandal ya Bill Clinton na Monica Lewinsky au Tiger Woods (4) Kuvaa pete siyo guarantee ya kupata heshima. Heshima ya mtu hujengwa na mtu mwenyewe! Mfano Oprah Winfrey na Stedman (5) Pete ya ndoa haiongezi wala kupunguza amani ndani ya ndoa. Kuna mifano hai ambayo nimeona japo siwezi zisema hapa. (6) Furaha ya ndoa hailetwi na pete ya ndoa. Kuna wanadoa wengi tu hawavai pete ya ndoa na wanapenda na furaha tele. Mfano hai ni Wasabato hatuamini kuwa pete ni sehemu muhimu ya ndoa. Hivyo kuvaa au kutokuvaa ni maamuzi yenu nyie wawili. (7) Kuvaa pete ya ndoa 24/7 doesn’t validate your marriage! Kuna watu wana vaa pete ya ndoa 24/7 lakini hata “kiss” tu hawapeani ?? ndoa za maigizo ??? (8) Jamani hata Yesu alifunga kwa siku arobaini na si mwaka mzima. Hivyo saa nyingine acha kidole kipumbue kidogo kha! (9) Thamani ya ndoa yako haitokani na pete bali inatokana na nyie wawili jinsi mnavyo heshimiana, thaminiana, na kupendana ndani ya nyumba na nje ya nyumba! (10) Adamu na Eva hawakuvaa pete ya ndoa ??
Category Archives: General
Manhood!
Wewe ni nani hata ucheke wengine?!
Mpendwa hii dunia ya Musa nenda nayo polepole eeh! Haihitaji ujuwaji wala kimbele mbele…….!! Nilishawahi kusema huko nyuma kuwa siku zote dharau maiti lakini si binadamu mwenye pumzi ya uhai toka kwa Mungu kwani ya Mungu mengi! Sasa wewe jifanye ndio mtaalamu wa kucheka watu kwa mapungufu waliyonayo au kwa hali yoyote ile ambayo wewe unaona kuwa siyo nzuri! Waswahili tunasema “Mungu hamtupi mja wake”! Ipo siku fimbo ya Mungu itakuchapa pasipo wewe kujua na hapo ndipo majuto huwa mjukuu! Heshimu, ombea na watakie kheri watu wote bila kujali hali zao kwani aliyekupa wewe ndiye aliye ninyima mimi! ………. Hapo ulipo hata kuumba sisimizi huwezi pamoja na udogo wake ule alionao lakini huwezi muumba! Sasa ni nini kinakupa kiburi na jeuri ya kucheka wenzako?? Wewe ni nani hata ucheke wengine?!………Tafakari, fanya mabadiliko!
Shukuru kwa ulicho nacho sasa ndipo utabarikiwa zaidi!
Jifunze kushukuru kwa ulicho nacho kwanza ndipo utabarikiwa zaidi! Sasa kuna watu ambao hata kile kidogo walicho nacho hawalidhiki kutwa kujenga chuki na wengine bila sababu za msingi! Hawa watu wasio ridhika ndio unakuta hata awe na pesa na mali kiasi gani lakini HANA AMANI NDANI YA ROHO YAKE!! Yani akikuta hata watu wasio na uwezo kifedha na mali (masikini) wanajichekea na kufurahia maisha kwake ni tatizo kubwa! Kwani anaumia na kuchukizwa kuona masiki anafurahia maisha kana kwamba ni mtu tajiri sana!! Siri ni moja tu……….!! Huyo masiki unaye muona ni masikini wa pesa na mali tu lakini Mungu kampa amani tele moyoni kwa kuwa kashukuru kuwa ni sawa kutokuwa na vyote. Hivyo kama ni mtu wa kujishughulisha na kupigania maisha bora zaidi ya aliyokuwa nayo sasa basi ipo siku Mungu atamwona na kumbariki zaidi! Haina aja ya kuchukia mtu kwasababu anafuraha moyoni mwake! Hakuna sababu ya kumchukia mtu Kwasababu ana wazazi wake ambao wanampenda, hakuna haja ya kuchukoa mtu Kwasababu kajaliwa watoto na wewe hauna! E t c ………… Shukuru kwa ulicho nacho sasa ndipo utabarikiwa zaidi!
“Wanaume wengi wa Bongo wanaamini wanawake ni sex object” -Lemutuz
Picha iliyo nivutia zaidi
Tafadhali tumuunge mkono Miriam Mchirwa!
Hot pic of the day
Hongera sana Frank!
Naomba nichukue nafasi hii kumpa pongezi my cousin-brother Frank Laurent Sarungi wa Mbagala, Dar es salaam kwa kufunga pingu za maisha.Nawaombea kheri, ndoa yenu idumu katika Bwana siku zote! Upendo, amani, vitawale daima ndani ya nyumba yenu. Kwa faida ya wale msiomjua Frank: Ni mtoto wa marehemu baba yangu mkubwa. Yeye alizaliwa na ulemavu wa kuto sikia (kiziwi) na pia ana ongea kwa tabu labda niseme ni bubu kwa kiasi fulani ila anaeleweka…….Frank aliamia nyumbani kwetu baada ya kumaliza darasa la saba. Kwasababu ya upungufu wa shule nzuri za secondary na elimu ya juu kwa watu wenye aina ya ulemavu kama Frank, basi aliamua kujiunga na English course kwa muda wa mwaka mmoja na baada ya hapo alijiunga na chuo cha viziwi kilichopo Baltimore, Maryland, U.S.A ambapo alisoma hapo na kuhitimu degree yake ya Theology. Kwani nia yake ilikuwa awe Pastor kwa watu wenye ulemavu kama wake. Alijaliwa kumaliza chuo na kurudi nyumbani Tanzania ambapo amefanikiwa kufungua kanisa la watu wenye ulemavu wa kutokusikia. Na siku ya jana alifunga pingu za maisha. Blessing naye alikuwepo kushuhudia
cake ikikatwa na Blessing naye hakutaka kupitwa ?? Nifuraha sana Wifi mtu Maseline Obago akifungua champagne kwa madaha kabisa Si kwa kucheza huko ???? Mzee Igogo na mama Igogo wakikumbushia enzi zao ……..yani hapo ilibidi mama Igogo aweke mambo ya usabato pembeni ?? ……. mzee Igogo na mama Igogo ndio wazazi walezi wa Frank toka alipo malizia darasa la saba na kuhamia kwenye himaya yao. Wao ndio walio msomesha Frank hapa Marekani na kumsaidia kuanza maisha alivyo rudi nyumbani Tanzania. nafikiri hapa ulikuwa ni mwendo wa Arutu (Luo dance) nahisi ulikuwa ni ule wimbo wa “???bilima Cecilia, jaber osekao pacha?? bilima Cecilia awinjo chunya gombi ndi” ???……..Congratulations Frank. All the best!
Hot pic of the day
#FBF #Mahojiano na Linda Bezuidenhount
Leo nimeamua ku “Flash Back” videos za interview ambazo nilifanya na mwanamitindo wa kimataifa Ms. Linda Bezuidenhout mnamo mwezi wa Pili mwaka jana 2015!
https://youtu.be/7tmJgxbmB1A
Hapo juu ?nisehemu ya kwanza ya mahojiano. Na hapa chini ? nisehemu ya pili au ya mwisho ya mahojiano yetu.
https://youtu.be/rELfTBwva9g
Haya yalikuwa ni mahojiano yangu ya kwanza kabisa kufanya huku nikirekodiwa. Nilipewa hii nafasi ghafla, yani nilijua nataka kufanya mahojiano na Linda lakini sikujua lini yatafanyika. Mara ilikuwa siku ya juma Tatu napigiwa simu na kaka yangu Dj Luke wa Vijimambo blog nakuambiwa kuwa Linda ametukaribisha kwake siku ya Juma Mosi na yupo teyari kufanya mahojiano nami! Nilisita, lakini kaka yangu akasema nitaweza nisiogope! Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa. Kama hujawahi yaona basi nakuomba uyatazame na niruhusa kutoa maoni yako! ……….Kwakweli siku zote nitamshukuru sana Linda kwa nafasi hii aliyonipa na pia sito choka kuwashukuru kaka yangu Dj Luke wa Vijimambo blog pamoja na mtani wangu Mubelwa Bandio wa Kwanza Production kwa kunisaidia kufanikisha hii ndoto. Sina chakuwalipa bali nawaombea baraka siku zote! ??
Hoja: Ni laana au?!
Katika pita pita yangu huko Facebook nikakutana na huu mjadala ambao ulianzishwa na Stephen Mndalila kuhusu njinsi wenzetu (Wakenya) wanavyo waza mambo makubwa ya maendeleo na kuyatekeleza wakati sisi mambo tunayo yawaza na kutafakari ni aibu tupu……..! stephen alitoa hiyo comment ?baada ya kuona picha ya Mark Zuckerberg (Facebook owner) akiwa Nairobi, Kenya kwenye mazungumzo ya mambo ya maendeleo ya technology! …….embu jisomee mwenyewe halafu utafakari kwa kina ni nini wewe kama Mtanzania utafanya kusaidia nchi yako isonge mbele!
Mungu ibariki Africa. Mungu ibariki Tanzania ?
Kutoka Facebook
HolleyPharm (T) LTD board meeting
Siku ya jana August 31st, 2016 HolleyPharm (T) Ltd walifanya mkutano wao mkuu unao fanyikaga kila mwaka (Annual Board Meeting). Mkutano huo huwa unahusisha all board members ambao ni shareholders, Directors, legal team, na top management kama wanavyo onekana hapo juu. Mkutano huo ulifanyika Slip Way Hotel, Dar es salaam, Tanzania.Kushoto ni Mrs. Cecilia Igogo ambaye ni mmoja wa shareholders na Deputy Director wa HolleyPharm (Tanzania) akiwa sambamba na binti yake Mrs. Janeth O.O. Igogo-Nyagilo ambaye ni mmoja wa board members na mwanasheria wa HolleyPharm (Tanzania).
Mr and Mrs O.O Igogo ambao ni shareholders wa HolleyPharm, board members na majority shareholders wa HolleyPharm (Tanzania) Hapa ni top Directors wakiwa na Mwanasheria Janeth Igogo-Nyagilo Waliokaa ni shareholders, kushoto ni top management team, na kulia ni legal team ya HolleyPharm Mr O.O Igogo (shareholder), Mrs Janeth O.O Igogo-Nyagilo (Lawyer, board member), Mrs Cecilia O.O Igogo (Shareholder, Deputy Director, and board member) Mr and Mrs O.O IgogoMother and daughter
Manhood!
Kutoka Facebook
Hot pic of the day
Linda Bezuidenhount akiwa huko NY katika business trip napia kum-support rafiki yake (KK) ambaye pia ni partner wake kwenye new clothing line ijulikanayo kama ID´EAL wakati alipokuwa anafanya surgical procedure kwa mwili wake! …….amependeza sana. Kutoka na maneno yake yeye mwenyewe amesema amekata na kushona hii jumpsuit ndani ya masaa mawili ??
Neema ndani ya Tanzania! Je tupo salama?!!
Haya, Mungu hamtupi mja wake! Na mwenye nacho atazidi ongezewa! Baraka ndani ya baraka katika nchi yenye madini ya pekee duniani (Tanzanite) kote! Hivi karibuni tuliongezewa mibaraka mingine ya ⛽ ⛽ (gas), Mungu akaona hapa nyie wana wangu nawapenda sana mmekuwa wavumilivu miaka mingi mno! Sasa ni zamu yenu; pokea mbaraka mwingine wa mafuta (oil) mjifute kabisa katika nchi masikini duniani………!! Je hii mibaraka viongozi wetu wapo teyari kuipokea kwa unyenyekevu kutoka kwa Mungu na uzalendo mkuu kwa nchi yao?!! Je tupo salama?? Amani yetu ambayo ni nguzo kuu na msingi wa nchi yetu itabaki imara au tuanze kujaza fomu za ukimbizi?!! Mimi sijui bado natafakari!!…………. Embu soma habari hii kisha soma baadhi ya maoni ya watu hapo chini……. ?
MUNGU IBARIKI AFRICA. MUNGU IBARIKI TANZANIA………….!!
Kutoka Facebook
beautiful babies……..ni watoto wa Christina Silasi sema sikupata majina yao ……..nimependa their swagThe newly wed, Mr and Mrs Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji…….. Wamependeza sana
Those ‘golden’ moments that bring peace to many! Mr and Mrs Mkapa golden wedding anniversary………walipendeza sana Elizabeth (Moshi) nimependa sana vazi lake la Batiki limempendeza!