Regrann from @lemutuz_superbrand – FACT: LE MUTUZ KOKOBANGA ……NA NDAMBO ….HAHAHAHAHAHAHA……Nimewahi kusema hapa mara nyingi sana kua kuna Wabebezz wa Batazzz tu na Wabebezz wa kuoa USICHANGANYE ni tofauti na hawafanani….now tizama mke anavyofanana Thank U @officialalikiba kwa kunisaidia hili somo..ndugu zangu Wabebezzz jifunzeni hapa darasa la bure mke wa nyumbani anatakiwa kuwa kama huyu …sio sijui Analicious mara Janebosslady mara ohhh official mary..mara amina chocolate …mara queensweetlicious gademiti hamuolewi ….hahahaha …mtaishia kuchezewa tu humu Instagram na I bet U huyu Mke wala hayumo Instagram …sio wale ze gademu mtindizz nje nje yaani unaona kila kitu kabla hata ya kumsalimia HAMTAOLEWA cause hamna huruma kazi kukomoa pesa tu….I mean unamuita date linakuja nauli ya Bajaji hana lakini anataka kunywa gademu CHAMPAIGNE mara AMARULLA hajali bei wala nini mazafantazzz ….mtajioa na mamitindizzz yenu hahahahaha U know….ingawa pia kuna somo zito hapa like in USA Niggaz wakitoboa tu wanaoa wabebezzz weupe tu ….now naona kama na Bongo tunaaanza kwa mbali vijana wakitoboa wanaenda kuoa nje ya Bongo WHY? hii ni ishu ya kujadiliwa na Jamii something is wrong somewhere Vijana wetu wanapokimbilia kuoa nje ya Nchi kuna kitendawili kizito sana ni nini hasa? ….U know! …..LE MUTUZ NYE! NYE! NYE! – @lemutuz_superbrand – #regrann Nimesoma hiyo ☝ msg ya Lemutuz kwa Instagram page yake nikasikitika halafu nikajiuliza hivi kweli mtu kama yeye kusema maneno kama haya je anastahili?! Nimesikitika siyo kwa maneno aliyo yaandika kwani hayo aliyo yaandika yana ukweli ndani yake. Kinacho nisikitisha ni kwamba hao wanawake aliowataja hapo ndio marafiki zake ambao siku zote amekuwa akipiga nao picha na kurusha Instagram!! Sijui kama hawa wanawake wanajielewa vyakutosha na kuona huu ujumbe ni wake-up call to them and stop acting like fools!! Lakini wakati huo huo kweli kati ya wanaume wote ninao waona kwa social media Lemutuz ndio mtu wa kusema maneno haya?! Mbona yeye nasikia anakaribia miaka 60 na bado yupo single?! Ni kitu gani kinakufanya usioe katika umri huo?? Tumetangaziwa wachumba na wengine picha za vikao vya harusi tukaona mbona bado upo single?! Halafu yule mchumba wake aliyeachana naye juzi juzi si alikuwa ana hayo majina ya "nanilious" ?? au hili ni dongo kwake? ?? na, ni mwanamke gani atakayetaka kuolewa na mwanaume ambaye video zake za uchi zipo kwa social media ?♂️?♂️ Lemutuz acha "ngebe" mimi sijaona tofauti yako wewe na hao wanawake unaosema wanaweka "mtindizz" nje! Though I do agree you are smart but your morals are questionable!!
Category Archives: General
My International nephew met the Legendary Zahir Zorro!
Heri imekwisha!
Kuishi nje ya mji kuna raha na karaha zake haswa ndani ya Bongoland! Huku kwa wenzetu ukikaa nje ya mji unaweza uwe mbali na night clubs, cassino, au maduka makubwa lakini huduma zote muhimu utazipata tena katika ubora ule ule kama wa mjini though your Gynecologist can be your very next door neighbor ?? Basi, hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika njia ya kuingia nyumbani kwa wazazi wangu wakati wa mvua kunyesha wiki iliyopita. Undogo wa kule ni udongo mfinyanzi unateleza balaa wakati wa mvua. Yani ukishatoka barabarani kuna kipande hapo cha mtaa wa ‘Utegi’ basi unaweza ukatumia masaa kutoka kama ukikwama. Siyo kikubwa sana lakini kinatoa jasho hata wenye uzowefu wa kuendesha kama unavyoona hapo ☝☝ gari imegeuka kabisa!
https://youtu.be/OM5q_lG8X10
“Peeping through my up stairs window at Kibada Villa this morning, rain is pouring like hell. The road is my first concern, my hard working, loyal, very honest Supervisor Daudi worked the whole night piling and spreading kifusi with his team, but unfortunately a loaded truck once again got stuck!!” Huo ulikuwa ujumbe wa mzee Igogo hapo juzi kati
Sasa juzi kati mvua ikapungua, mzee Igogo akaamua kuita wamwaga kifusi ☝☝ ili kutengeneza barabara kwa kuweka kifusi juu yasikwameje?! Yani yalikwama na kuzuia magari kutoka ndani na kuingia ndani ya mji?? Mzee Igogo akanitumia mag kwa WhatsApp akisema ” The Kibada Villa access desaster continues in a bigger way. Loaded trucks with morrum for making the road passable, are stuck along the the road, blocking us completely from going either way by our vehicles. Me and Lawyer Rhoda are Victims, I think of pleading to Hon. Makonda the RC for sending us rescue helicopter!!!???????” Mtu anatamani kumuomba Rc Makonda msaada wa helicopter ??? Siyo vyakuchekesha lakini inabidi maana shughuli zako zote za uzalishaji zinakwama kwasababu ya miundo mbinu mibovu!! Jamani ni karne ya 21 hii shouldn’t we have lami kila eneo lenya makazi ya watu?? just imagine kama kungekuwa na mtu anaumwa uchungu wa kuzaa ingekuwaje? Brother Paul Makonda embu tupigie debe basi nasisi kwenye hii mitaa! Umeme tulivuta wenyewe baada ya kuona hatutaweza tumia genereta milele kwa kusubiria Tanesco watuwekee umeme. Sasa basi hili la barabara simtufikiriapo basi?! eti Dr Magu haswa kwenye ule mgao wa 1.5 trillion ?? Mimi sijasema ni Mh Zitto huyo ?♂️?♂️Sijui kama mvua zimekwisha msimu wake au zimepumzika sisi tunashukuru Mungu maana sasa magari yameweza kutoka na kifusi kumwagwa. Mwezi uliyopita Mzee Igogo alisawazisha hiyo barabara vizuri kabisa akijua hiyo itasaidia wakati wa mvua lakini jitihada zake hazikuzaa matunda!
Blessing akutana na Dr Mpanju!
Hapa kazi tu!
Roving camera of mzee Igogo caught these two young street boys at work, carrying a wooden box to their homestead along Indhra Gandhi street, in Dar es salaam, Tanzania. When asked why, the elder one responded that ” HAPA KAZI TU”! ……….. Wishing you all a very productive and fruitful week. #HapaKaziTu
Zamaradi Mketema: Katika kipindi cha Dawa usikimbie Dozi, na wala usilaumu mtu kwa ugonjwa wako
Regrann from @zamaradimketema - Kabla ya kupona kila mtu lazima apate Dawa yake, nyingine huwa chungu, nyingine tamu lakini ndio DAWA. Kwa bahati malengo ya dawa si mabaya ila kukusimamisha tena, kukufanya uogope ugonjwa ulioumwa ili uepuke vyanzo vyake, kutahadharisha na wengine waepuke sababu unajua uchungu wa matibabu yake, kwenye maisha DAWA tunazipata kupitia MATOKEO ya matendo yetu, yale tuliyoyatengeneza ndio yanatupa majibu yake, kwenye dawa hapa unaweza kudhalilika, kuumia, kutaka hata kujiua, kushuka thamani na vingi vingine, kutegemea ukubwa wa ugonjwa wako na ndio Dozi itakavyoenda, lakini uzuri ukishatambua unachoumwa na kukubaliana na hali bila kusahau kufata masharti ya ugonjwa unavyotaka unapona tu na mwisho wa siku maisha yanarudi kuwa mapya. Katika kipindi cha Dawa usikimbie Dozi, na wala usilaumu mtu kwa ugonjwa wako, pambana nao mpaka usimame upya, kiufupi usiyakwepe masharti maana kipindi cha Dawa ndio kipindi cha kujifunza, jua tu SIO PEKE YAKO mwenye ugonjwa huo, kuna wengi walioamua kuugua kwa siri ama kuficha matokeo yake tumewazika, kataa kuondoka na gonjwa lolote, ujinga ni wakati wa kwenda hivyo kikubwa jifunze athari zinazoweza kusababishwa na matendo yako, na kupona kwake ni kutotafuta yeyote wa kumuangushia mzigo wa lawama ila kuangalia mianya uliyoitoa iliyosababisha ugonjwa kuingia, kisha chaguo ni lako kuidhibiti ama kuachia nafasi ya ugonjwa kukushambulia kwa mara nyingine. - #regrann
Once you stop hating, you’ll start loving. Once you stop loving, you’ll start hating. Make love your choice!
Regrann from @cheyennebbostock – Yes, we descend from Africa, yes our ancestors were brought here against their free will, yes they were raped, tortured and killed, yes they were sold into slavery, yes they were not paid for their labor, yes we are still affected mentally, emotionally, and financially as a result of their wrong doings, yes racism still exists, BUT… what was done to our ancestors is nothing in comparison to what was done to Jesus and he forgave them, and he died for us. Are you willing to forgive and love again? Not just black people, but ALL people. Even your enemies.
Once you stop hating, you’ll start loving. Once you stop loving, you’ll start hating. Make love your choice! We all have sins we wish could be forgiven and forgotten. Extend the same grace you would want others to extend to you. Everyday should be Love Day! Everyday is Black History and ALL History! Make love your choice! Not hate. ?? – #regrann
The Taste of Tanzania by Miriam Kinunda
Miriam Kinunda ni author of the Taste Of Tanzania. Kitabu cha mapishi kinachoelezea kwa mahiri jinsi ya kupika mapishi ya Kitanzania na East Africa. Kitabu kinapatika Amazon. Kuona kipaji chake cha mapishi nenda kwa YouTube channel yake, na Instagram page yake; vyote vinapatikana kwa kuandika jina lake Miriam Kinunda.
2018 Hottest And Best Couple Of The Year
Tulikutana na mke wangu Sayuni kwenye harusi ya mdogo wangu Linda iliyofanyika Dar miaka saba iliyopita. Sayuni alikuwa mmoja wa wasimamizi kwenye harusi ya Linda na walisoma darasa moja Chuo Kikuu cha Mlimani Dar. Tuliendelea kuwasiliana niliporudi Columbus na mwaka uliofuata alihamia Columbus..Tulikuwa katika urafiki kwa muda wa karibu miaka miwili na uhusiano wetu ulizidi kuimarika na kufikia makubaliano ya kuoana. Tulipendana na kukubaliana kufunga ndoa Septemba 2012 hapa Columbus. Ni mambo mengi yalinivutia kwake na kunifanya nizidi kumpenda na hasa busara zake na ushirikiano wake katika mambo mbalimbali ya maisha. Baada ya kukubaliana kuoana, tulianza maandalizi ya harusi. Tulipata ushirikiano mkubwa wa marafiki na ndugu mbalimbali hapa Columbus na nje ya Columbus. Tulifanya vikao vya maandalizi na tunamshukuru Mungu tulipata ushirikiano mkubwa na mzuri kutoka kwa kamati ya maandalizi. Kama nilivyosema hapo juu, busara za Sayuni na ushirikiano zilizidi kunivutia. Kila nilipokuwa napata changamoto za kazini au za kimaisha na kumshirikisha alikuwa akinishauri vizuri na kufikia hatua ya kuaminiana zaidi. Na mpaka sasa ni mshauri wangu mkubwa na ninathamini hekima na busara zake. Vilevile Sayuni ni mtu asiye kata tamaa katika kutimiza malengo aliyoyapanga au malengo tuliyokubaliana kuyatimiza. Nimezaliwa na kukulia katika familia ya kikristo. Moja ya imani niliyokuwa nayo ni kumcha na kumwamini Mungu. Ninaamini kwamba ndoa ni baraka na pia agizo la Mungu hasa inapofika muda wa kuanzisha familia. Katika sala zangu ilikuwa ni pamoja na kumwomba Mungu anifunulie na kunionyesha mke mwenye busara, hekima, mcha Mungu na tutakayeelewana. Hivyo kabla hatujaoana na Sayuni, niliona hizi sifa nilizokuwa nikiziweka kwenye sala zangu. Katika ndoa, sio wakati wote ni wa raha. Kuna wakati ambao tunatofautiana katika maamuzi. Kutofautiana ni jambo la kawaida. Kwa mtazamo wangu, kutofautiana katika maamuzi/mitazamo ndio kunakamilisha mapungufu ya kila mmoja wetu. Hivyo, ni vema kila mmoja akaheshimu tofauti za mwenzake hata kama hakubaliani nazo. Hii inachangia kuendelea kujenga uhusiano imara na kila mmoja kuwa wazi kwa mwenzake badala ya kuogopana. Communication is the key thing to us. Pia learning to compromise/meet each other half way inatusaidia kuimarisha umoja wetu.
Mimi ni kaka mkubwa katika familia yetu, ninapenda kuona wadogo zangu hasa wa kike waliopo kwenye ndoa wana amani na furaha na ndoa zao. Ushauri wangu kwa vijana wanaotaka kuoa, ndoa ni baraka. Kila ndoa ina changamoto zake. Kabla ya kufikia hatua ya ndoa, omba Mungu akuongoze katika kumpata mke mtakayeelewana na kupendana. Wapendwa wasomaji wangu, niliwaahidi kuwa sita waangusha! Hii ndio 2018 Hottest And Best Couple Of The Year. Nakumbuka katika busara za marehemu Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere siku moja alikua akitoa busara juu ya kuchagua viongozi wa Taifa la Tanzania alisihi Watanzania kuwa mchague kiongozi ambaye hata wakimtizama machoni utajua huyu anasema kweli tunaimani naye! Basi hivyo ndivyo nami nilivyo itizama hii couple haswa nimemtizama kwa kina sana kaka yangu Jackson Lyimo nikaona moyo wangu unaimani naye, na hata macho yake yananipa imani kuwa siyo tu kaka bora bali pia ni mume mwema! Heshima yake kwa wanawake ni kubwa sana, matendo yake yanajidhihirisha hilo! Hivyo pasipo shaka naomba nitamke rasmi kuwa hii couple ndio chaguo langu kwa mwaka huu. Nawaombea ndoa njema sana, iliyojaa baraka nyingi mno na amani tele. Wabarikiwe wao na uzao wa tumbo lao pamoja na wageni wote waingiao ndani ya malango yao!. Congratulations to Mr and Mrs Lyimo and happy Valentine's Day. I love you guys so much ??
Happy Valentine’s Day to you!
Watoto wanahitaji malezi ya mzazi! Mali na pesa siyo malezi!
Wahenga walisema kulea mimba si kazi kazi kulea mwana! Ukiwa mjamzito kike kiumbe ulichobeba hata kama hutaki kikuwe kitakuwa tu! Sasa ni hiyari yako kula vizuri na kujijali ili uzae kiumbe chenye afya bora na salama. Mama uliyebeba hicho kiumbe ni jukumu lako kutafakari matendo na tabia zako wakati wa ujauzito huo kwani huyo mtoto anauwezekano mkubwa sana wa kuhakisi tabia zako akiwa tumboni mwako! Huo ni mtihani wa kwanza katika malezi ya mtoto! Jana nilisoma post ya Jackie ikanikumbusha mtihani wa pili katika malezi ya mtoto ambapo wazazi wengi huwa wanafeli! Pia ikanikumbusha kuhusu wazazi fulani ambao wapo kwenye reality show fulani inaitwa “Married to Medicine” wote ni madaktari na mama anaumizwa na kitendo cha wao kuwa busy na kazi kiasi kwamba wanakuwa hawana nafasi ya kukaa na watoto zao! Napia ikanikumbusha interview ya Naomi Campbell aliyofanyaga na Oprah Winfrey mwaka 2010 ambapo Naomi alisema kuwa siku zote amejisikia mpweke toka akiwa mdogo kwani wazazi wake wahakuwa nae karibu. Mama yake Naomi yeye aliamini kuwa anafanya kitu kizuri kufanya kazi sana ili kuweza kumpatia mtoto wake vitu vizuri, kusoma shule za private n.k ………. Soma na tazama video hapo chini ?@Regranned from @j_n_mengi – Dear parents, I know you’re busy working hard to feed and raise your kids but please remember that your physical presence is very important to your child. You need to invest more than money to your child, they need to talk to you, they need your hugs and reassurance and most importantly they need you to teach them to be good human beings.”
Pesa na mali ni vizuri kama ukiwawekea watoto wakawa navyo kwani hilo ni jukumu lako kama mzazi! Kumbuka “Pesa na mali ni urithi mtu apataye kutoka kwa babaye” hayo ni maandiko ya Biblia siyo mimi! Lakini kabla ya kuwapa hizo pesa na mali ni vyema ukawafundisha jinsi ya kupata hizo pesa na mali ili nao waweze fundisha watoto zao! Hata hivyo, kabla ya kuwafundisha jinsi ya kutafuta pesa na mali watoto wanatakiwa kufundiswa maadili!
Watoto wanatakiwa kuonyeshwa upendo iliwajifunze kwa matendo, watoto wanatakiwa kufundishwa elimu ya Mbingu kabla hujampa elimu ya duniani! Kwamfano, kabla ya kumfundisha mtoto wako kuhesabu embu hakikisha anajua kusali au kusema sala ya Bwana kwanza! Mfano mwingine, kabla hujamfundisha mtoto wako kusema “naomba” mfundishe kushukuru kwa kila kitu anachopewa, hakikisha anajua kusema “asante” kwanza kabla ya kusema “naomba”!
Kumvalisha mtoto wako nguo za designer maharufu siyo malezi! Surely, itamfanya aonekane vizuri lakini haita msaidia kuwa kiumbe bora! Kumlaza mtoto wako kwenye nyumba ya mamilioni ni vizuri lakini haita mpa confidence au kuacha kuwa muongo na mwizi! Watoto wanahitaji malezi ya wazazi! Pesa na mali siyo malezi!!
Repost:- Je, Zari ataweza kubeba “bendera” za nchi mbili?
Katika Biblia kuna maneno yanasema ‘hakuna mtu awezae kutumikia mabwana wawili’! Yani kiufupi lazima mmoja utampendelea na mwingine utamuonea kwa mapenzi ya uwongo! Sasa, wote tumeshuhudia maisha ya Zari na Ivan mpaka kuachana kwao. Lakini pamoja na hayo Ivan bado hakuona mtu mwingine ambaye angefaa kulinda mali zake, watoto wake, na kuhakikisha kuwa his Legacy forever lives zaidi ya Zari. Na Zari mwenyewe kwa mdomo wake alitamka mbele ya kadamnasi siku ya mazishi ya Ivan Ssemwanga (SomaHapa) kua atavaa viatu vya Ivan Ssemwanga, kwani yupo tayari, anaona kama she was prepared enough for it!! Na kwamba she will do it for his boys, his family, friends, and his legacy! Swali ambalo ninajiuliza will Zari be able to be a “flag bearer” for the two men from different countries?! Can she honestly, sincerely, and lovingly serve the “two masters”! ……..Personally, I’m not sure but very curious to see how will this go down considering one of her “men” is still living and 100% involving in her life!………Will Zari disappoint many or will she continue to shine and come-out as a shero? Will this be Zari’s downfall as she may lose some sort of “respect” from Ugandans who are / were hardcore fans of the “Rich Gang” particularly The Don- Ivan Ssemwanga?! Will Watanzania accept Zari and give her 100% support to carry their flag as Diamond’s wife especially after his bizarre behaviors of abusing and disrespecting women!?! Remember “The B**** is dying for fame” and “the baby is not mine”! And finally, the boys are growing up, one day they will have bunch of questions to ask! How will her children feel? Will they feel a sense of betrayal from their own mother; the only living parent?! Can’t get any better than this!! I will surely keep up with the story. And You be the judge!
*** Hii ni Repost, niliandika August 31st mwaka jana. Tujikumbushe na tutafakari kama niliyosema yametokea au bado au kuna dalili ya kutokea!****
Mr and Mrs Mengi ni Watanzania wakwanza kupata E-passport!
Wamenoga eeh? real man knows how to wear pink ati ?? ......... Mr and Mrs Mengi walipokuwa wamekwenda kuchukua passport mpya za kieletronikia ambazo Rais Dr Magufuli alizizindua juzi! Haya yamefanyika leo majira ya hasubui saa za Africa Mashariki hivyo wamewafungulia mlango Watanzania wengine! ........... Wamependeza sanaaaaa! Haya Jacky njoeni Houston basi ?? ??
Muacheni Mungu aitwe Mungu!
I am over the moon about this! Yule Shemeji yetu ambaye walimwita mission town (SomaHapa) mume halali wa Zamaradi Mketema ndio anafanya hii miujiza eeh?! Hata miezi SITA haijafika mibaraka imeshaanza kumwagika namna hii!! Ndoa zilizo chagulia na Mungu utazijua tu, wengine miaka kumi lakini bado wanaangaika na pesa ya kulipa rent ???? Kweli muacheni Mungu aitwe Mungu!!! Mume / Mke mwema mtu upewa na Bwana hatokani na vyeti vya degree ulizo nazo au umaharufu wako!!!…….. Mungu aendele kumimina baraka zako katika hii familia katika jina la Yesu ?? Kama unataka kuifaidi video ya “kaSmall White House” ketu nenda kwa Instagram page yake please!
Regrann from @zamaradimketema –
In love with my kasmall White House
Things in Progress
Swimming Pool
Little Playground for Shubi and JuhJuh.
Basketball Court for my Darling Husband (Half Court)
and of course Garden to spice up mazingira.. I love Space ?
Asante MUNGU
#mamamwenyenyumba – #regrann
Baba na mama Ariel!
Hii couple naipenda hila sijuwagi Sir name yao ?? Ni wale wenye watoto wazuriiii ?? Sijui ni Mkony au? Ila najua mtoto wao mmoja anaitwa Ariel, hivyo nimewaita baba na mama Ariel ?? wamefanana eeh? Utasema mtu na dada take, so lovely! .......Jamani Poleni sana kwa kuuguza mtoto. Mungu awe nanyi wakati wote wote na namtakia uponyaji wa haraka baby girl!
Hata mwenye mkoa wake kasema “save the date”!
Mbiu ikilia ujue kuna jambo kwani hata mwenye mkoa wake kasema “save the date”! Rais wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh RC Paul Makonda naye kwa kupitia Instagram page yake ameweka tangazo la Tanzania’s Sweetheart kuwa tarehe 30 mwezi wa Sita mwaka huu siyo siku ya kukosa!! Iwe umealikwa kushuhudia LIVE, au utatizama kwa runinga, au utakuwa ukichungulia live coverage kwa social media vyovyote vile haijalishi ila panga mambo yako vizuri ili siku hiyo uiache wazi kwa kumuangalia huyu “Peacock wa Tanzania”! Siyo siku ya kukosa!!……… Mimi naonaombeni kaka yangu Paul Makonda mnikumbuke kwenye zile offer za bure za ticket ya ndege??? jamani nami niwepo nishuhudie LiVe mambo ya kusubiria Millard Ayo TV inahusu ??? Jamani, SAVE THE DATE! Mwambie na jirani yako ??
Shikamoo Wabongo!
Kumbe kuna ubuyu mtamu hivi unanipita ?? Sorry wapendwa, nimebanwa kidogo!........... Jamani Instagram mambo ni ??? mambo hayasemeki!! Huku bado nashangaa King Kiba akicheza "seduce me" na bibi kule Chato (Mama yake mzazi Rais Magufuli) Mara paap! Nakutana na ya "Mr and Mrs Tanzania" a.k.a Wema na Diamond! Mara vichambo vya kudai lakimoja ya bia kutoka kwa Moses Iyobo! Sijakaa sawa wengine wanadaiana viwanja, mara mama Cookie naye kapandisha ??? nageuka nisome vizuri mara wengine wana "rambana rambana" na Kinje Ngombale Mwiru ??? Jamani!! Shikamoo Wabongo!! Hivi hivyo ndivyo mnavyotumia social media??!! Halafu huu ukimwi unawapataga Wasabato tu ????? hivi kwa jinsi ambavyo mnachangia wanaume / wanawake mbona haujawakamata?? ??? Dah!! So sad to say the least!! Haya Mr and Mrs Tanzania are back in the postlight, najua Shingongo na timu yake wamefurahi sanaaa ??? Swali, will they get married this time?!! ?? Well, Diamond hajaoa na Wema yupo available it's all about "survival for the fittest" ???? Huu uCelebrity wenu mtakuja kutoana roho siku moja!! It's only the last day of January but ma'am!!! It's going to a very interesting year, andaeni papocorn movie ndio kwanza inafanyiwa majaribio ??? Mungu awasaidie! Poleni wenye waume zenu maana siyo kwa evidence zile ???
Hoyce Temu: shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ?? Mh. John Magufuli na mkewe Mama Janet
@Regranned from @hoycetemu - Done! Mungu ni Mkubwa na kwa Mara nyingine miminatanzania inatoa shukrani za Pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ?? Mh. John Magufuli na mkewe Mama Janet kwa kuchangia milioni 15 ambapo Sasa zikichanganywa na milioni 15 zilizopatikana kutoka kwa watanzania kupitia miminatanzania tutakuwa tumefikia kiwango na hata kuvuka. @wastara84 mdogo wangu, kila la kheri na muamini Allah na usikate tamaa. Hivyo basi mahesabu ni kama Ifuatavyo: Mh. Rais-15m, Miminatanzania 15m, Msamaria mwema aliyeweka kwenye account ya Hospitali India 7m, familia ya Wastara 5m JUMLA ni 42m zaidi ya lengo la milioni 37! Kila la kheri Wastara! Asante Tanzania! ????#tumeweza #jamii
Joyce Kiria: Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua
@Regranned from @joycekiriasuperwoman - Changamoto kubwa 2018 #Kipigo Sikutegemea kama ipo siku kwa mkono wako ungeunyanya KUNIPIGA @kilewo2020mwanga ???? * Ukasahau kabisa! Ukasahau yooooote.. nimeharibu career yangu kupigania ndoto yako kwa kugawa watu wangu kwenye biashara zangu, nimepoteza ndugu jamaa na marafiki, umeniachia nimebeba mzigo wa familia kwa muda wote... Malipo yako ni KUNIPIGA/ KUNIDHALILISHA/ KUNITOA MACHOZI???
Umenipiga kwa sababu Mimi Ni MNYONGE siyo! SINA NGUVU, kwa sababu ni MWANAMKE Sina nguvu za kupigana na MWANAUME ... Umeniumiza mwili wangu unauma kila mahali umefiria damu na kichwa ukanigongesha kwenye gari, ili iweje? Nia yako ilikuwa ninini? kuniua??? Mungu amenipigania. Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua...?????? Kama NI Mimi niliandamana na watoto, nikakufanyia kampeni na deni kubwa nikaingia mpaka nikafungiwa Kipindi hewami, ninakutunza wewe na Watoto wako kwa miaka yote, MUNGU YUPO.... LEO UMENIPIGA @kilewo2020mwanga ??? Sawa watakusifia hao wanaokusifu ujinga, wanaokuambiaga Mimi sikuheshimu, badala wakwambie ufanye kazi utunze familia, Leo watakuona wewe ni MWANAUME kwa KUNIPIGA... - #regrann
Tegemeo Sambili: Ili tuendelee kwa haraka na watu wayaone maendeleo, nashauri tuongeze nguvu kwenye yafuatayo:-
Moja ya Makosa tunayoyafanya ni Kutaka Kuendelea kama Walivyoendelea Wajeruman, Wamarekan, China, France……. Kwa Upande wangu, Maendeleo yanaanza kwa Kula vizuri, Kulala vizuri, Kuvaa vizuri na kuwa na Afya njema. Ili tuendelee kwa Haraka na Watu Wayaone Maendeleo, nashauri tuongeze nguvu kwenye Yafuatayo:-
1. Kilimo Tulime sana kiasi cha kuwawezesha Watanzania kupata Chakula bora na cha kutosha. Nataman kuona Chakula kinakuwa kingi kiasi cha kilo 1 ya unga iwe Tsh 500, kilo 1 ya mchele iwe Tsh 1200, Karoti 1 iwe Tsh 50,pilipili hoho iwe Tsh 50, Nyanya fungu 1 liwe Tsh 200, Vitunguu Tsh 50, Nyama, Samaki….vipatikane kwa bei nafuu. Ikiwa Watu watapata Chakula bora, kwanza watakuwa na Afya , Miili yao itakuwa na uwezo wa Kujikinga na magonjwa na Wataweza kuishi miaka mingi. Life span ya Watanzania ni Fupi kwa sababu ya Chakula dhaifu…. JKT itumike kulima Chakula kwa ajili ya Watanzania.
2. Nyumba na Makazi bora Nataman kuona kila Kaya inaishi kwenye Nyumba ya kisasa.Lazima tuhakikishe watu wetu wanalala sehemu nzuri na salala.Katika kutekeleza hilo, serikali kwa kutumia Watalamu wa Majengo na Mipango miji, Wanaweza kuandaa Ramani za Nyumba za Mwongozo, zitakazoelekeza aina ya Nyumba ambazo watu Watatakiwa kujenga na Zigawiwe bure. Vifaa vya ujenzi Viondolewe Kodi na Serikali inaweza kushiriki katika kuvisafirisha hasa maeneo ya Vijijini ili Wakazi wa maeneo hayo Waweze kuvipata kwa gharama Nafuu. Serikali iwahamasishe watu Kujenga nyumba zao..
3. Mavazi Tuongeze nguvu katika kujenga Viwanda vya nguo. Watalamu wa Mavazi, wabuni nguo zinazowafaa Watanzania wa kike na kiume.Watu maarufu kama akina Kikwete watumike kuzitangaza ili kuwahamasisha Vijana kuvaa nguo hizo.Vijana wetu wanavaa uchi Kwa sababu wamehamasishwa kufanya hivyo na Hatuna Mavazi yetu mazuri
4. Huduma za Afya Tuwekeze nguvu kwanza katika kutokomeza vyanzo vya magonjwa…Pili tuhakikishe huduma bora za afya Zinazotibu Maradhi yanayowasumbua watu wetu haraka. Kuongezeka kwa Vituo vya tiba mbadala ni Ishara kwamba Hospital zetu zimeshindwa kutibu Maradhi yanayowasumbua watu wetu. Tukitaka kuendelea kama Wao, Hatutafika Leo wala kesho…… Tukiyafanya Mambo haya, Maendeleo yataonekana kwa kila MTU na kila Kaya ndani ya muda mfupi. Tunataka Kuona Tanzania inakuwa nchi ya kwanza Dunian kwa Watu wake Kula Vizuri…. Kulala vizuri , Kuvaa vizuri…..na kuwa na Afya njema…