BABA WA FAMILIA NI LAZIMA ADUMISHE UHUSIANO MWEMA NA JIRANI ZAKE:
Kiongozi makini ni yule ambaye anatambua ya kuwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi yake hayaji kwa nchi kujitenga na kujifanyia mambo yake peke yake, bali huletwa kwa juhudi za wananchi wake pamoja na kushirikiana vema na nchi majirani zake pamoja na jumuiya nzima ya kimataifa kwa mapana. #VIVA_JPM
Nimekutana na news za Babu Sea na wanawe wakitangaza kurudi kwenye uwanja wa muziki kwa nguvu zote! Sasa nikasikiliza hii video fupi ya mahojiano yao, katika hizo nyimbo mbili zilizopigwa chorus zake hiyo ya pili imeimbwa kwa Kijaluo! Au Wajaluo wenzangu mnasemaje? Nimesikia vibaya hayo maneno au ni Kijaluo chenyewe?!! Embu msilikize….
https://youtu.be/y1L_qid_t-Q
Kijaluo lugha hatari eeh! Inapendwa kila kona, haya mtuletee tuisikilize but honestly I don’t know how to sincerely feel about it! Anyway, who am I to judge!
Katika pita pita yangu huko Instagram nikakutana na huyu mwanamuziki wa Kihaya mwenye asili ya "Donald Trump'' ?? hapana chezea Wahaya siyo watu wa spoti spoti ati ?? wenyewe mambo yao ni ya kimataifa tu kama ilivyokuwa magonjwa yao hayana tiba ndani ya Tanzania dawa zao lazima ziagizwe nje ya nchi ????? wanajua kuringa hawa watu ?? Mzuri eeh! Anaitwa Abela, Instagram page yake ni "Abelamusic" embu follow her ukamsikie mwenyewe. Mie nimempenda sana, yani pamoja na kwamba ana ishi Marekani lakini anakwenda mpaka kwao Bukoba (naona baba yake ndio Muhaya) kusalimia ndugu zake, ana andika Kihaya bila shaka atakuwa anakiongea, huwezi amini anakula mpaka wale "funza wa Kagera" a.k.a "Senene" she is no Diva at all! Very down to earth just by looking at her pictures you can tell all!! Natamani nimjue zaidi! Pia na mama yake mzazi natamani nimjue ili aniambie ilikuwaje akamlea hivi maana wamama wengine mmh! I'm just saying, no judging ??? maybe I'm judging ?? ..........Abela if you happen to read here please get in touch with me ??
Najua kuna nyimbo nyingi sana ambazo ni nzuri zilizo imbwa na wanamuziki mbali mbali lakini #Zezeta bado umekamata macho na masikio yangu! Huu wimbo gives me life kwakweli! Maneno yake yamepangiliwa vizuri, yanaeleweka, ujumbe unaleta maana, sauti na mdundo ni babkubwa! Video ndio usiseme!! Ipo kwenye ubora wakimataifa. Very clear, haina giza giza wala chenga, wachezaji wamevaa vizuri, na rangi za nguo zao ni rangi zilizo tulia hazichoshi macho! Hivyo natangaza rasmi kuwa huu ndio my 2017 best song ??
Kwanza naomba mniwie radhi wapendwa wangu ambao ni Waislam. Mimi ni Mkristo hiyo mambo mengi nikiongea nita refer to the Holy Bible kwani hicho ndicho kitabu nakijua na pia sipo hapa kwaajili ya dini hivyo sitokaa ni compare Quran na Bible! Sasa Biblia katika kitabu kile cha Mithali 22:6 inasema mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee! Hizi picha za birthday ya Nillan ambazo zinaonyesha wako mezani wakila chakula na kunywa zimenifanya nikumbuke hilo fungu la Mithali 22:6! Hivi wazazi wangapi mnawalea watoto wenu kwa kuwafundisha kuwa chakula ni kitu cha kuheshimiwa hivyo ukila lazima uwe na nidhamu?! Kuwa hupaswi kutembea huku unakula kama mkimbizi au mtu aliye vitani!! Unamfunza mtoto kuwa ni lazima ukae chini / mezani wakati wa kula napia ni marufuku kuongea nachakula mdomoni!! Kama wewe ni mzazi unaye ishi katika mazingira mazuri na ungependa mtoto wako aende mbali zaidi ya hapo ulipo wewe, je umemwandaa mtoto wako kukabiliana na mazingira hayo?! Kwamfano, ungependa mtoto wako awe na uwezo wa kwenda naye kwenye 5* hotel nakula chakula mbele za watu nilazima umfunze mwanao kukaa mezani wakati wakula na atulie mpaka atakapo maliza chakula. Nilazima umfunze mtoto kutumia visu, uma, na kijiko tena umfunze mara kwa mara ili azoee kuvitumia kama Zari alivyofanya kwa watoto wake. Hao watoto kukaa mezani kwa utulivu hivyo nakula kwa ustarabu si kitu ambacho wamefanya mara moja, hapana! Hao watakuwa wamefunzwa na wamezoea! Ni malezi mazuri sana haswa kwa karne hii ya 21 ambapo dunia imekuwa kama kijiji huwezi jua ni wapi na nani mwanao atakutana naye hivyo lazima kujua jinsi ya kumudu mazingira! Nilipokua nyumbani Tanzania mwanzoni mwa mwaka huu, watoto wake mdogo wangu walikuja kunitembelea. Sasa wakati wakula mie nikamwambia dada wa kazi kuwa haina haja ya kuweka chakula mezani aweke mkeka tukae chini tule! Tuliokulia kwenye mikeka utatujua tu ??? mwe! Kwani hao watoto waliweza kula?! Mara namuona yule mdogo anaangaika kuvuta kiti karibu na mkeka na mkubwa wa kike kalalia tumbo huku akijaribu kula ?? Nikawa nashanga, ndio mama yao akasema unajua wanangu hawajui kula huku wakiwa wamekaa kwenye mkeka!! Akasema "Wakenya hao wanajua kula ni mezani tu" ?? mbona yalinishuka ikabidi tuhamishie chakula mezani, basi wakawa na amani wakala kwa furaha! Mdogo wangu alipoona hizi picha za Tiffah akanitumia na kusema kama mtoto wake angepiga picha hiyo ambayo ameshikilia glass ya juice baada ya picha za birthday ya Nillan kutoka basi baadhi ya watu angefikiri kuwa ameiga kumbe hivyo ndivyo alivyo walea watoto wake!...... Wazazi embu achaneni na kuwapa watoto glass za plastic kwanza zinaleta Cancer ?? honestly, bora umpe mtoto kikombe cha bati kuliko plastic! Nunua zile glass ngumu mfundishe mtoto kushika na kutumia bila kuvunja ili siku ukiwanae 5* hotel upati shida kwani kazoea! #Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee!!
""* Picha zote za Tiffah nimezitoa kwa Instagram page ya princess_Tiffah***
@Regranned from @wemasepetu - Tanzania Kwanza....... Katika vitu ambavyo Dar pia inatakiwa kujivunia ni kupata RC mwenye akili nyingi.........Mungu akakutangulie katika kazi zako za lengo la kuijenga Tanzania yako izidi kuwa zaidi ya ilipo sasa........... Ipo siku wataelewa tu......... The Man Himself....... Call Him Mr Dar-es-salaam...... Viva RC wangu....... Viva Rais wangu...... #UzalendoKwanza ... cc @paulmakonda May everything you wish well for your Nation Be.... We support you fully... ?????? - #regrann
@Regranned from @mutwiba – Wakati Rais akifanya maamuzi ya kuwaachia familia ya Nguza Viking, anafungua mjadala mpya na muhimu wa kisheria na haki Tanzania
Binafsi ningependa kujua ni kipi ambacho Mahakama ZOTE zilijithibitisha “beyond shadow of a doubt” kwamba familia hii ilitenda makosa yaliyosababisha kuhukumiwa kifungo na kunyimwa dhamana na hata msamaha walioomba, na umekuwaje sasa imejulikana kwamba hayakutendeka?Swali la ziada (ambalo siamini kama kuna atakayeuliza waziwazi ??♂) ni kwamba……
Baada ya Rais kujithibitisha kwamba hali haikuwa imetendeka, ni nini kinafuata kwa waliohusika ama mfumo mzima kuhakikisha kwamba hawatokei kina Babu Seya wengine? – #regrann
Since its Friday, let us flash-back some memories ? Hapa ilikuwa Bongo Star Search ya 2010 behind the scene. Huyo binti ni mwanangu akiwa na Diamond Plutnumz, TMK-Wanaume, na Marlow. Yuko wapi Marlow siku hizi?! Anyway natumaini baadhi ya hizi picha zitakupa faraja na natumaini wewe uliyekata tamaa.! Muwe na weekend njema. Mbarikiwe wote
Haya msikilize kwa makini muimbaji chipukizi anayekwenda kwa jina la Princess Lelya! Ni interview nzuri mtoto kaongea kwa confidence nzuri sana. Nakutakia mafanikio mema Lelya Bezuidenhout ?
Yule Mwanasheria wa kujitegemea, msomi wa kuaminiwa na mataifa yote, Alberto Msando arejea CCM kwa unyenyekevu mkuu! Akiri kuwa alipotea njia, alikuwa kipofu na sasa anaona kwani hataki kuongozwa na chama ambacho kina Mwenyekiti mmoja kwa zaidi ya miaka 10! Kwani huo pia ni udikteta ?? ……Alberto anakuwa mwanasheria wa pili (Lau Masha alirudi wiki iliyopita) ambao walikuwa upinzani na sasa wameamua kurudi kundini! ……As I always say, ” I’m not a politician” hence, my comment is respectfully reserved! Just wishing him the best of all!
#Feud in the WhiteHouse........Mambo hayo! Who does he belong to and whos is the "first"?! Mipasho ndani ya WhiteHouse! Kweli wanawake wote ni sawa hata uwe nani! Wakati mwingine anasema sasa nini mimi ndio mke wake wa kwanza! Mwingine anasema haijalishi kwani mimi ndio First Lady ??? shughuli imewapata washughulikaji ?? yale yale ya Kanye West na Ray J ? ......Kama huelewi hiyo lugha ni hivi aliyekuwa mke wa kwanza (wamesha achana) wa Donald Trump amabye pia ndio mama wa watoto wakubwa watatu wa Mr Trump ambaye anajulikana kama Ivana Trump (hakubadilisha jina baada ya divorce) anasema yeye ni first lady wa Mr Trump kwani ndiye mke wake wakwanza na ndio mama wa hao watoto wenye maadili mazuri! Sasa mke wa Mr Trump wa sasa (mke wa tatu) ambaye ni First Lady Melanie Trump anasema so what!?! kwani yeye ndio First Lady wa Marekani! Mambo ya "title deed" hayo ?? msifikiri ni kwa Zari na Hamissa tu hapana! Mpaka kwenye WhiteHouse ya Marekani ?? Bora hata hawa wanarushiana vijembe kwa millionaire sasa wengine mtukanane kwa mwanaume wa $50 anaye ishi kwa pesa ya paycheck to paycheck kama akina Alpha hapa inahusu ?? mwanaume anaye abudu LIKES kwenye Facebook na followers kwa Instagram ?? pole zenu! Mie nipe kwanza ATM card yako ndio nitafanya huo ujinga. mkono mtupu haulambwi jama ?? ......Nafikiri wakati Melanie Trump anarusha mipasho kwa kutumia wimbo wa "The boy is mine" naye Ivana Trump akatumia wimbo wa "he wasn't a man enough for me" kama ifuatavyo -:
You need to give it up. Had about enough It's not hard to see The boy is mine I'm sorry that you Seem to be confused He belongs to me The boy is mine
Who do you think I am? Don't you know that he was my man? But I chose to let him go So why do you act like I still care about him? Looking at me like I'm hurt When I'm the one who said I didn't want it to work Don't you forget I had him first? What you thinkin'? Stop blamin' me He wasn't man enough for me If you don't know, now here's the chance I've already had your man Do you wonder just where he's been, yeah? Not be worried about him Now it's time you know the truth I think he's just the man for you
Haya mchukuwe notes za jinsi ya kulea watoto haswa nyie wenye pesa zenu!
Nimenyama na hili swala la Lulu siyo kwamba simpendi au namtakia mabaya, hapana! Hili ni swala sensitive sanaaaaaaa! Pia kwenye familia yetu right this very moment tunapitia kitu ambacho karibia kinafanana na hili swala la Lulu japo mdogo wangu haikuwa swala la mapenzi na bado hajafariki!! Yupo kwenye koma wiki ya tatu sasa anapumulia mashine!! Hivyo, nimejaribu kuvaa viatu vya Lulu kwakweli vimenibada mno! Napia nilipojaribu kuvaa viatu vya mama Kanumba kwakweli vimekuwa ni vikubwa sana havinienei! Kwa maneno hayo, nimeamua kunyamaza na kuomba Mungu kuwa hekima itumike zaidi! Mungu ampe huyo Judge hekima na kuzingatia mambo yote kwani hata Lulu naye ni victim. Bila kusahau kuwa Lulu alisha kaa ndani / jela karibia miaka miwii, kama ataweza ampe hata kifungo cha nje! ………..Mungu awe nanyi nyote poleni sana.
Nashindwa kuelewa ni kitu gani huwa kinatokea, ndani ya miezi michache watu wanakataa kabisa kuwa ndoa yao ipo sawa na hizo rumors ni maneno tu yamtaani!! Wanathubutu hata kumtaja Mungu!! Halafu hamjakaa sawa mnasikia wame file for divorce kuwa wameshindwana! Sasa najiuliza why lying!?! Kama ndoa inamatatizo si unasema tu, kuwa ndoa yetu haipo sawa lakini we are working on it, just pray for us!! Kuliko kudanganya!! Kama hapo ?kwenye video Tamar na mumewe walivyo jieleza kwenye Wendy Williams show mwezi wa tatu mwaka huu embu wasikilize
Kana kwamba hiyo haitoshi hata mwezi uliopita alipo ulizwa akasema yupo teyari kufanya chochote kile kulinda ndoa yake. Na hivyo kitu chakwanza ambacho anafanya ili kuokoa ndoa yake ni kuachana na "showbiz business" ataacha kutengeneza album za nyimbo mpya! Sasa within 30 days inakuwaje mtu huyo huyo ndio anakuwa wakwanza kudai talaka ?? I don't get it!.......
Lakini ukiangalia kwaundani utagundua huyu Tamar kuacha kuimba siyo kwasababu alikuwa anataka kuokoa ndoa yake bali ni njia ya kumuondoa mumewe kuwa Manager na producer wake. Kama mnakumbuka how Lady JayDee alivyo mfanyia Captain Garnder Habash ?? smart lady huh! .......Jamani let your husband be your husband! Mambo ya mumeo kuwa Manager wako kwakweli naona ndoa nyingi zinavunjika ni wachache mno wamefanikiwa. Labda kama huyo mumeo hachukui pesa yoyote kwenye hiyo production yako. Your husband / wife is your business partner and advicer but not someone to manage you everyday, no no! You can only meet at the board meetings or kwenye weekly business meeting. Lakini kila mtu awe na ofisi yake na wafanyakazi wake nafikiri kwa njia hii itapunguza tension fulani zisizo na ulazima!
https://youtu.be/qgNAASByIg4
Halafu pia kitu ambacho nimeona wanandoa wengi ambao wako kwenye the same industry ndoa zao hazidumu au zinakuwa na matatizo sana. Kwamfano, hapa Tamar ni muimbaji na reality TV star wakati mume wake ni producer mkubwa kwenye music na TV show hivyo wote wapo kwenye spotlight na mzunguko wa watu hao hao kila wakati! Lazima wanandoa wawe makini sana mnapokuwa kwenye maswala ya business ili ndoa yenu iwe na amani. Sasa Tamar na Vince walipo owana hawakupeana "prenuptial agreements" kwani walikubaliana kuwa divorce is NOT an option! Sasa pale divorce inapokuwa ni the only option sijui itakuwaje kwani Tamar anataka full custody ya mtoto wao na pia anasema Vince asipewe spouse support. Kumbuka wakati Tamar anaolewa na Vince, Vince ndio alikuwa anatengeneza pesa nyingi lakini baadaye Tamar akawa super star na kutengeneza pesa nyingi zaidi ya Vince hivyo sasa itabidi Tamar amlipe Vince pesa za kujikimu baada ya divorce..... Vince ni yatima na kwao alizaliwa mwenyewe hivyo hana ndugu wa tumbo moja wala wazazi! So sad!
Couple nyingine ambayo imeshangaza watu ni ya huyu mwanadada wa The Real talk show ?? Jeanie Mai na mumewe Fredy! Hapa mwanamke ndiye aliyesema kuwa yeye hataki kuwa na watoto kwani haoni kama atakuwa mama mzuri kwani kulea kiumbe kingine na kumfanya awe ni kiumbe bora is a tough job ambayo yeye hawezi. Pia kwasasa yupo busy na "carrier" yake wakati mumewe anataka wazae watoto kitu ambacho hawezi fanya. Kutokana na history yake ya kutoka kwenye familia duni wazazi wake waliangaika sana wakaja Marekani kutafuta maisha bora haswa kwa watoto wao. Hivyo kuwa na watoto kuta slow down dream zake ambazo yeye na wazazi wake wameteseka sana kuzipata. Nabado kuna watu masikini kwenye familia yake ambao anaona kuwa anawajibu wa kuwasaidia hivyo kuleta watoto duniani itakuwa ni mzigo mwingine wa watu wanao mtegemea! Hayo ni maisha ya Marekani kule kwetu Africa masikini ndio wanazaa zaidi ya matajiri wanajua mjomba/ baba mdogo au shangazi atawalea tu bila shida ??
Hivi, mimi nashindwa kuelewa hivi dunia hii kunawatu wanaowana bila kujadili kama wanataka watoto au hapana!! Hivi si vitu vinajadiliwa kabla hata ya kuchumbiana au mie ndio sijui ?? nielewesheni ?? mie I would love to know what am I signing up for, sorry naogopa sana kujifunga kitanzi mwenyewe! Naogopa surprises .........Kumbuka Tamar Braxton alikuwa kwenye show hii kabla ya ufukuzwa mwaka jana!
Wiki iliyopita tarehe 21 na 22 mwezi huu wa kumi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, na Mexico alitembelea jimbo la Houston, katika state ya Texas ili kuwafariji Watanzania waliopatwa na maafa ya mafuriko ya Hurricane Harvey mwishoni mwa mwezi wa nane!
Balozi pia alikutana na viongozi wa jumuiya na kukutana na wanajumuiya wote nakubadilisha mawazo, kutoa muongozo katika maswala yanayohusu Diaspora. Kwa maelezo na picha zaidi bonyeza ?? (TanzanianHoustonCommunity-THC)
Kama binadamu na Mtanzania naomba nichukue nafasi hii kumtakia Mh. Tundu Lissu matibabu mema na uponyaji wa haraka! Mkono wa Mungu wa uponyaji ukawe nawe siku zote! Get well soon ??
“Siku ya Maisha Yangu na @kikizimba @kikisfashion Siku Ya Maisha Yangu Ni show inayo onyesha maisha ya kila siku ya watu mbali mbali wanao toka kwenye mazingira tofauti. Tuna angalia wafanya biashara, wajasiriamali, wana siasa, watu mbali mbali Walio fanikiwa kwenye kazi zao mbali mbali, wakurugenzi, washawishaji, watu wanao julikana kwenye jamii, Na watu ambao wanafanya vitu vikubwa kwenye jamii hata Kama hawa julikani. Je kwenye Siku Yao huwa wana fanya nini tangia Asubuhi mpaka wana maliza siku? Je nini kiini cha mafanikio Yao Na vitu gani vina wasukuma kufanya mambo mengi makubwa wanayo yafanya. Lengo la kipindi cha Siku ya Maisha Yangu Ni kujifunza, kuhamasisha, kuwezesha, kushawishi kupitia watu mbali mbali. Nenda kwenye Bio Na fungua link kuangalia kipindi. #sikuyamaishayangu #kikizimba #kikisfashion” Dorothy Kipeja
Awiiiihh! Wamenoga eeh!! Wow! Super cute, couple yangu ya ukweli hii! Yani wanavutia na kuwapa moyo wengine kuwa True Love still exists ?? Kama wewe ni mgeni basi naomba ujua kuwa hi couple ndio ilikwa my 2016 Hottest And Best Couple Of The Year (SomaHapa). Nawapenda sana ??………Baadaye kuna post inakuja ya kuipongeza LB kwa award waliyo pata. Sasa hivi nipo busy kidogo hivyo naishia hapa!
Nimeenda kuchungulia kwa Mrs Mengi nikakutana na picha nzuri sana zakwake na maneno Fulani amazing hivi, "love is an act of endless forgiveness"! Haya ni maneno rasmi aliyo yatamka Beyonce baada ya kumsamehe Jay Z kwenye ile "cheating scandle" nakusema kuwa amejifunza upendo ni tendo la kusamehe bila ukomo / kukoma! Dah! Haya maswala ya mapenzi namwachia Jacqueline na Dr Mengi wake maana site wengine tulishaga achana nayo ????.
Kuna mtu aliandika article akisema Beyonce amemsaidia sana kwa maneno yake hayo ............."The best part of the show is when Beyoncé gives us the quote about forgiveness.
“Love is an act of endless forgiveness. Forgiveness is me giving up my right to hurt you for hurting me. Forgiveness is the final act of love”
All this while getting shot in a wedding dress. Yes, shit gets THAT real.
We’ve all been there for before where we wanted to hurt the one we love because they hurt us. Why? Because no one can hurt you more than the ones you care for. They know you best and you feel so vulnerable to them.
It is a valuable lesson to be learned here. In order to sustain love, you have continuously BE love. You have to be willing to love through thick AND thin. It’s easy to stop loving once you’ve been hurt but as the late Maya Angelou once said, “Have enough courage to trust love one more time, and always one more time.”
If two people can put aside their ego and realize that mistakes will be made; and know that nothing worth having will come without HARD work to keep it, you can really have that ever lasting love you seek." ............unaweza soma article you kwa kubonyeza ?? (LoveIsAnActOfEndlessForgiveness).
“If you are happy with yourself it’s very easy for others to make you happy”JNM……….Umependeza sana! Super clean and beautiful!
A must watch to all African men!! Hii video niliiona almost two months ago, but nikawa nasubiria a “proper” day kuiweka. Sasa kwakuwa bado tupo kwenye furaha ya maadhimisho ya mtoto wa kike duniani basi nimeona ni vyema kuiweka! Kwakweli huu ni ukweli kabisa! Watoto wa Africa haswa wakike wamewekwa kwenye “pressure” of how to become a good citizens, great mothers, wives, sisters, and aunties bila kujua kuwa it always takes two to tangle!! Unakuta mtoto wa kike very well organized mentally, spiritually, physically, na hata financially lakini anaangukia kwenye mikono ya mwanume asiye jielewa kabisa!! Mnyanyasaji na mambo mengi ambayo yanafanya maisha yao kutokuwa na furaha! A totally unprepared man for familyhood!! Na ukijaribu kuuliza hawa wadada utasikia ma’am! “All men are the same”!! Hivyo hakuwa na chaguo zaidi ya ku settle down for less!! ………Wazazi, waleeni vijana wenu ukijua kuwa kesho atakuwa mume wa mtu, mmoja ya wana jumuiya hivyo lazima awe teyari kuwa good citizen! Kuwa na hela doesn’t make someone a good citizen or good husband tabia yake na malezi ndio vitaeleza huyo kijana wako ni mtu wa namna gani! Nimeona vijana wenye pesa na ni wanyanyasaji wa wanawake mpaka inaogopesha! Wengine ni rapists and molesters! Tuwalee watoto katika njia ipasayo ili wasiwe mzigo kwa wengine na taifa analo ishi ni jukumu lako wewe kama mzazi!