Category Archives: General

Kama “Boaz” angeambiwa achague mwanamke katika dunia ya leo…..!!

 Embu tucheke kidogo maana hii weekend ndefu hapa U.S.A kwasababu the Independence ya Marekani ni JumaNne!……… Basi kama ilivyo, nimekwenda kwa Instagram ya #Askcheyb nakukutana na hii topic ya wadada kuvaa nguo karibia na nusu uchi! Eti anasema kuwa kama “Boaz” wa kizazi kile cha kwanza angekua ndio anatafuta mke katika karne hii 21 ambapo wasichana wengi wanatembea nusu uchi kila siku mida yote; ingekuaje? Muandishi wa mada anasema wanawake wa namna hiyo wapo kwaajili ya “mburulaz”!  Labda nikukumbushe kuwa muandishi ni mtaalamu wa mambo ya mahusiano!~~~~~ embu jisomee mwenyewe ??

Could you imagine “Boaz” choosing some of these chicks who parade half naked on IG ALL  day everyday? Nah, them chicks are for “Dumbaz” ??” Sasa mimi nashindwa kuelewa kwani jambo kama hili lingeandikwa na “Muafrika” kutoka Africa nisinge shangaaa sana. Lakini huyu ni Mmarekani mweusi ambaye amezaliwa na kukulia hapa Marekani! Watu kutembea nusu uchi hapa Marekani nikitu cha kawaida sana. Sijui tatizo nikuweka hizo picha kwa Social media au ni nini! Kwamfano, mtu kama Oprah aliwahisema kuwa siku ukikutana na picha ya yeye amevaa “bikini” au swimsuit basi jua kuwa ni fake! Kwani hata siku mmoja haitokaa itokee yeye kuvaa hivyo kwa public! Lakini unakuta watu kama wakina Michelle Obama wao wapo free kuvaa swimsuit mbele za watu japo hukuti akizipost picha hizo kwa social media isipokuwa  ma-paparazzi huwa hawapitwi na jambo! ~~~~ Sijajua kwakweli inakuaje watu walio zaliwa kwenye mila na tamaduni sawa wakawa na mtazamo tofauti wa maadili ya mavazi! Embu tujikimbushe na hii topic hapa ?? KamaMkeRaisAnawezaVaa.    

SOMA MAONI YA WENGINE!

 

 

Eid Mubarak wapendwa!

Sheikh Juhju katka ubora wake!

Eid Mubarak to all my Muslim family members, friends, my loyal readers, and. everyone else! Mungu awabariki sana muwe na sherehe njema! Nawapa mkono wa Eid wapendwa!

https://youtu.be/ePeuRYIhZNs

The journey to motherhood: Congratulations Nambua Cassandra!

Alpha Igogo -bloggerWapendwa wasomaji wangu, naomba niwaletee tukio zuri sana la safari ya kuzaliwa mtoto Prince. Ni tukio ambalo limekuwa recorded na shemu ya hiyo video imeonyeshwa na mama mzazi kwa kupitia account yake ya Instagram! ……….. Kwanza nianze kwa kusema hongera sana kwa Nambua kwa kujaliwa mtoto wa kiume! Mungu amlinde akuwe katika kimo na hekima. Akampendeze Mungu kwanza na kisha wanadamu! Karibu katika chama cha wakinamama/ wazazi! Safari hii ni ndefu, yenye changamoto nyingi lakini ni tamu mno! Nasema nitamu mno kwani kama kuna kitu nime furahia kwa 100%  na bado naendelea kufurahia with all the pride is being a mother! Lakini kila siku namrudishia sifa na utukufu kwakwe Mungu maana bila yeye hakuna litakalo wezekana! ……..kwakweli nimependa sana hii familia ya Mr and Mrs Mlaki! Nimependa sana their spirit, wako so open and together, inapendeza sana mfano mzuri sana wa kuigwa katika jamii! Hii dunia imeshabadilika (21st century) kuna mambo mengi ya karne 19 inabidi kuyaacha maana siyo tu jamii haiipi nafasi bali pia hata technology haivitaki! Kwa mfano katika karne hii 21 n* kitu cha kawaida kabisa katika jamii zilizo ona mbele mama na kijana wake kuwa ndani ya chumba cha upasuaji wakimuangalia binti/ dada akileta kiumbe kingine duniani! Wakati jambo kama hilo bado linaweza likawa tatizo katika sehemu nyingi za Africa! ……….. Maelezo yote ambayo yameambatana na picha yameandikwa na Nambua ambaye ni mama mzazi wa Prince!  #NaniKamaMama. Yesterday 4th June, 2017 was one of my big day osn earth. Nimepata experience ya ajabu sana katika maisha yangu. Mwenyenzi Mungu Muumba Mbingu na Nchi amenijalia kujifungua mtoto wa kiume 9.25am South African time. HIYO NI FIRST FOTO ALIPOTOKA TUMBONI KWANGU, ALIPOTOLEWA KAANZA KULIA. Ilikuwa sala yangu kujifungua mtoto wa kwanza DUME. I’M OFFICIALLY A MOTHER. Jana usiku sijalala kabisa nimekaa natoa macho, namshangaa huyu mtoto. Bado siamini kama ni mtoto wangu, namuona stranger, mgeni flani hivi. Na sikujua watoto wanatoka mbali hivi. Heshima kwa wamama wote waliozaa. ??. Napenda kuwashukuru wote waliokuwa na mimi katika hii safari yangu. Nikisema nitaje majina mengi sitamaliza. Surely it was a long trip. My brother @laumlaki huyu ni commando aliingia theatre aka record tukio zima la Cesarean operation na mama yangu @lwisemanka amempokea mjukuu wake. Lord Jesus I give you glory. In Christ I have made it to God be the Glory. Yeremia 29:11 HAKIKA MAWAZO YA BWANA NI MEMA JUU YANGU, Yeremia 33:3…… BWANA AMENIONYESHA MAMBO MAKUBWA MAGUMU NISIOYAJUA.

Hapo niko theatre (operation room) najindaa nimlete mwanangu duniani. Nacheka cheka tu naona wanachelewa……?. Niko na mama na mdogo wangu @laumlaki paparazzi. Hili tukio kwangu ni very historical considering mahala nilipotoka. Nilisema Im going to record kila kitu wakati najifungua niweke ktk dvd. Namshangaa Bwana Yesu na matendo yake makuu juu yangu. Nawashukuru sana MEDICLINIC, SANDTON. Doctors & Nurses are very friendly na makini ktk kazi. Biblia inasema katika torati: Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini BWANA humponya nayo yote.????? Amen. 

My mother @lwisemanka, my mdogo @laumlaki and my photographer ms melody, hawa nilikuwa nao theatre. Walitaka waone ceserean section inavyokuwa, yani kila kitu na wawe wa kwanza to see my baby. Nimewaita mashilawadu wangu.????…….. love you all. Kweli watoto wanatoka mbali sana. Halafu hili zoezi nimelipenda sana la kuingia theatre na familya yako au photographer wako.

Hapo nimetoka kutoa mtoto tumboni naumwa sana, nimezinduka. Koo limekauka kwani niliwekewa oxygen. Yani kuitwa mama aisee ni kazi! Nafundishwa kunyonyesha naona ni adhabu halafu siamini kama nitaitwa mama. Shikamoo mwanamke. Naomba wanaume wawaheshimu wale wanawake waliozaa wakawafanya wakaitwa wababa. Hii experience ni ya ajabu. Wamama shikamooni. Kuanzia leo simgombezi tena mama yangu……. Biblia inasema ZABURI 34:19-21 MATESO YA MWENYE HAKI NI MENGI LAKINI BWANA HUPONYA NAYO YOTE.HUIHIFADHI MIFUPA YAKE MY FIRST BORN,UZAO WANGU WA KWANZA…… BWANA MUNGU AKASEMA HAKIKA NITAKUBARIKI NAE AKANIBARIKI NA HUYU KIUMBE KATIKA JINA LA YESU …………… PRINCE THAT HIS NAME.NI PRINCE MTOTO WA MFALME WA WAFALME, JEHOVAH RAPHA. TODAY HE IS ONLY 15DAYS OLD NA AMEANZA TO POZI TAJIRI MTOTO. I LOVE YOU MY SON. I LOVE YOU. HUYU KIUMBE NIMEMJUA SIKU 15 ZILIZOPITA ILA NAMPENDA KULIKO VIUMBE VYOTE DUNIANI…….???? MY LIFE HAS CHANGED 100%. #nambuacassandra @baby.mix.baby. 

Me and My baby PRINCE that his name (tajiri mtoto)…… hapo yuko 12days old????. Na nilipokuwa natafakari?? siku zangu duniani, Nae Mungu akasema na mimi akaninong’oneza MWANANGU NEEMA YANGU YATOSHA JUU YAKO. MGHH SIKUAMINI……. ILA LEO NIMEIONA NEEMA YAKE KWA KUNIZAWADIA MTOTO WA KIUME SAWASAWA NA HAJA YA MOYO WANGU. (Heart desires) ??? Neno la Mungu linasema (Torati) Zaburi 37:4-6 Nawe utajifurahisha kwa BWANA. Naye atakupa haja za moyo wako. Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya. Ataitokeza haki yako kama nuru. Na hukumu yako kama adhuhuri……. #nambuacassandra #huumchezohauhitajihasira

***HONGERA SANA NAMBUA CASSANDRA***

How can I attract my Boaz? A) Close your legs. Open your heart!

My babybrother na wifi yangu ?

Wataalamu wanakwambia muonyeshe kuwa you are a team player without any benefits attached then you will see kama hajakufanya uwe Malkia wake wanguvu! ………. Ngoja niwadokezee kidogo, this is exactly what happened kati yangu na Muhaya! Kwani unafikiri hiki kiburi cha kusema “haachwi mtu hapa” kinatoka wapi? Pure love will never come back void people!! ?? I will let him aje awaelezee siku moja leo nimewaonjesha tu. ???  “Help a man build his empire without giving him sex and watch him marry you. #Helpmate #close your legs.Open your heart SOMA BAADHI YA COMMENTS: 

Camille Cosby hatimaye bega kwa bega na mumewe!

Mimi naamini kuzaliwa “mwanamke” ni mtihani tosha, lakini kuwa mke unayebeba jukumu lako la kuwa mke kikamilifu ni mtihani mgumu na mzito zaidi! Ukiwa umekula kiapo kile “KITAKATIFU” kuwa KATIKA TABU NA RAHA yani utakuwa unajifikiria mara mbili mbili na kujikuta unasimama hata pale usipo taka! Haya ndio yalio mkuta Mrs Bill Cosby a.k.a Camille Cosby! Baada ya ukimya na kujificha kwa takribani miaka 3, finally amejitokeza saa za mwisho bega kwa bega na mumewe ambaye anashitakiwa kwa makosa ya ku-drug wanawake na kufanya nao mapenzi bila hidhini yao ( sex assault).  As I said before being a woman is not a joke but I can only imagine how hard it is to be a fully committed wife!!

Sidhani kama Camille Cosby angekuwa na uwezo wa kujificha forever asinge fanya hivyo kwani aibu na fedhea ambayo mumewe amempa ni kubwa mnooooo! Angesema akaye pembeni society bado ingemuhukumu kwa kutokuwa “woman enough” kusimama na mumewe!! Shame! As Bill Cosby’s lawyer said in the court room kuwa the real victim here is a long  suffering Camille Cosby! Which in somehow nakubaliana naye kwani huyu ni mke walio owana kwa miaka 53, amemjua mume wake kama; mume muaminifu, baba na mwanaume ambaye siku zote analinda na kuheshimu wanawake. Akajenga “image” hiyo katika dunia kuwa yeye ni “Family man” na mkewe na watoto wake wakawa very proud of him! Sasa leo hii mbele ya uso wa dunia anatakiwa afute hiyo “image” aliyo wajengea na kuwaaminisha watu kuwa Nope! That ain’t him! Ni ngumu kueleweka na fedheha kubwa sana kwa mkewe na watoto wake wakike! Naamini sababu kuu ya Mrs Cosby kukwepa kuwepo mahakamani wakati victim wakitoa ushahidi ni kwasababu hakutaka kuweka mambo yatakayo semwa mahakamani kwenye akili yake ambayo yangemfanya aanze kutafakari na kumuangalia mumewe katika sura mpya! I believe she wants to continue to remember her husband the way she knows / knew him and not otherwise! Maana zile testimony ukizisikiliza unaweza file for Divorce bila kutaka! I truly feel sorry for her! Mungu amsaidie! Hata hivyo yeye si wakwanza kusimama bega kwa bega na mumewe katika scandal kubwa na za kufedhehesha namna hii! Wapo wanawake wengi wamefanya hivyo kama Hillary Clinton wakati mumewe anakesi ya kufanya mapenzi ndani ya moja ya office za WhiteHouse na secretary wake Monica Lewinsky!……… It’s hard to be a woman but it’s more harder to be a fully committed wife!! #StandByYourMan #GodHelpUs!

Alijisemeaga Oprah Winfrey kuwa labda hizo vows zingebadilishwa huwenda angefunga ndoa cause yeye haelewi wanaposema “katika shida na raha” what do they real mean?! ?? Wenyewe wanasemaga hivi “if you can’t stand the heat better stay out of the ktchen” ??? bora yeye kajisemea ukweli lol!………..Huko nyuma niliandika hivi ??  TheBillCosbyTrial

 

The BET AWARDS: Tafadhali piga kura ulete ushindi nyumbani!

Tanzania, Kwa mara nyingi tena kijana wetu katajwa kwenye BET AWARDS! Tafadhali piga kura. ulete ushindi nyumbani! Mpigie Ray Vann wetu kama umesahau sauti yake basi tazama hizi video umsikie! Yani hadi Wamarekani wamemkubali sio mimi tu! Haya hima leta ushindi huu nyumbani!

“MTOTO ANAFUNDISHWA NYUMBANI.”~~~~~`Zamaradi Mketema

TV host Zamaradi Mketema

Kwangu mtoto kufanya hivi sio fahari ni Aibu, Hawa ndio aina ya watoto anakuwa anawaza kitu kimoja tu kichwani mwake, Kumridhisha mwanaume, juhudi zake atazielekeza kwenye kutafuta style mpya, bila kusahau vitu mbalimbali vya kupagawisha wanaume. Na wengi wa aina hii bahati mbaya waliowazunguka wanaendelea kuwatengenezea mazingira ya namna hii, wanakuwa wakiamini MAISHA NI MWANAUME TU, na ili uishi nae nguvu yako uilekeze kwenye KITANDA TU. Asilimia kubwa ya maongezi yao yamejaa hayo akiamini ndio UBORA, wanasahaulishwa kabisa kuwa kuna zaidi ya hayo kwenye maisha, wanabaki na mawazo mgando na kubaki kwenye dunia yao ya peke yao, ndio wale utasikia wanamtukana mwanamke mwenzao eti HUJAFUNDWA WEWE!!

Hapondiohuwainachekeshasababukwabahatimbayaufundajimwingiunaangaliasehemumoja tu and am sorry to say wengi WALIOUABUDU wanakuwa na mawazomgando mno yanayopeleke akuachwa na Dunia nyingine. Wadogozangu kitanda ni muhimu lakini haijawahi kuwasehemu KUU pekee ya UKAMILIFU wa mwanamke ama kumshika mwanaume, na kwa ulimwengu wa sasa kama unachojua ni kitanda tu.kunaathari nyingi utakazo kumbananazo hata katika hiyo ndoa unayoiabudu, na hakuna faida yoyote utakayo ipata, maishani zaidi ya kitanda. Mapenzi ni zaidi ya style mpya! Wamama tunaokuja tujitahidi kutotengeneza kizazi cha aina hii, tunaumiza watoto wetu, wanaishia kuwa malosers, washamba, akili ndogo, na hakuna cha maana kwenye maisha yao. Ninachoamini mtoto hafundwi siku moja, wiki moja, wala mwezi mmoja. Mtoto anaanza kufundwa tangu anazaliwa na katika ukuaji wake, MTOTO ANAFUNDISHWA NYUMBANI, Na ndio mafunzo mazuri au mabaya yanapotokea kulingana na imani unayomlisha, mazingira unayomkuza nayo na hata picha unayoionesha.

Hajawahi tabia mbaya alioishi nayo mtoto ndani ya miaka 13 au 14 ikabadilika ndani ya wiki moja za kumuweka ndani, hakuna!! Atawasikiliza tu lakini kama ana asili ya uchoyo ataendelea kuwa mchoyo, kama ana kaumalaya katakua, n.k Tuangalie RIGHT TIME ya kuwafunza hata hayo tulioamua kuwafunza kama ndio kudumisha mila na tamaduni, hakuna ubaya wa kumfunda mtu anaeingia kwenye ndoa lakini hakuna utamu wowote wa kumfunda mtoto wa miaka 12, 13, 14 au 15 ambae hana pa kuyapeleka hayo mafunzo, na hata hao wanaoingia kwenye ndoa kuna haja ya kuwapa LIFE SKILLS na sio kuwashibisha kimoja tu kisichokuwa na faida ya moja kwa moja katika ndoa yake!! Maisha yana changamoto nyingi sana, tusiwatengenezee utumwa wa akili na kuwafunga humo, kwanza angalia hata watoto ama wasichana wengi waliokulia kwenye imani ya kufundwa na kufundana katika hali ya kuabudu walivyo ama wanavyoishi kwenye jamii zao ama ndoa, kama hajaachika basi ana ndoa ya pili au ya tatu, wengi WANASHINDWA KULINDA NDOA ZAO na mpaka sasa nimefeli kujua kwanini!!

Walichokishiba wao ni kimoja tu. Hakuna bingwa wa malezi lakini mengine tunayatengeneza wenyewe, maana hapo utakuta mama yuko pembeni anashangilia na kupiga makofi huku akiona fahari mwanae anavyoyakata, jamani hata ukate mauno mpaka juu ya dari kama kuna vitu huna na hujielewi na kujitambua HAUTATHAMINIKA hata siku moja kwenye ndoa yako, na hao unaowaita wasiofundwa wataishia kukupiga bao tu kwenye maisha. TUAMKE.

Are they allowed to date?

The O.O Igogo’s daughters! #Sisterhood

Nimekutana na hii topic huko kwa Instagram as usual huko ndipo vituko vyote vipo ?……..Sasa swali ni kwamba; eti umemkaribisha rafiki yako ukamtambulisha kwa ndugu yako halafu wakapendana, je ni sawa hiyo na ungefanyaje? Binafsi sipendi kabisa! Hila sina huwakika kama ni sawa au si sawa japo hii tabia ipo sana Ujaluoni! Yani unaweza kukutana familia imeoa / kuolewa  kwenye mji mmoja. Naposema mji mmoja namaanisha familia ya baba na mama mmoja au baba mkubwa na mdogo. Utakuta dada na mdogo wake wameolewa kwenye familia moja.  Sasa hao wanaoowa kwenye ukoo mmoja ndio usiseme nikitu cha kawaida sana!………..Tatizo kubwa ambalo naliona hapa ni kama ukoo /familia ina magonjwa ya kurithi basi kuna uwezekano mkubwa wa watoto wenu wote wakarithi hayo magonjwa! Otherwise, mmh! Ila wanasemaga “mapenzi hayana macho”! Hata hivyo huo usemi mie sina huwakika nao kwani macho yangu yamemuona Muhaya ??……….. 

Cheka urefushe maisha yako! #AGangster Vs #AGentleman

Never tell a book by its cover! A gangster left THREE KIDS (3) from ONE woman and the gentleman MANY KIDS from DIFFERENT woman the ball is in your court.. ………????

New song: Zezeta by Rayvanny!

Mimi #Zezeta zezeta! Huu wimbo ni mtamu sanaaaaaa! Namshukuru my Muhaya kwa kunitumia huu wimbo lakini bado najiuliza sijui kati yangu mimi na yeye nani #Zezeta kuliko mwenzake ????  au ni Ma-double Zezeta ?? …………Honestly, Rayvanny hajawahi kuniangusha na nyimbo zake. Nimeusikiliza huu zaidi ya mara tano, na hata bado hamu haijaniisha! Safi sana! ??

Man-up and kill it with kindness!

Yess! Keep on moving Bosslady a.k.a the New C.E.O of the “Rich Gang” ?? You Man-Up girl and em haters just kill them with kindness!!……………I just love this, do you guys see what I’m seeing?! The msg is on the shoes people!! While MEN are Manning-Up in ?? “Flat” shoes  the Bosslady is Manning-Up in ? ?HighHeels baby ???You Go Zari! Keep that Legacy going!! Tell them We Run this Planet, of course in HighHeels ?? 

Molocaho by Amorette

Haya furniture nzuri sanaaaaaa zinatengenezwa ndani ya Tanzania. Ni vitu vyenye viwango vya kimataifa, Molocaho by Amorette! Vimeshika nafasi ya juu sana katika ubora wa furniture za ndani huko Dubai na East Africa katika maonyesho ya biashara yalio fanyika mwaka huu! Tafadhali tuweke uzalendo kwa kupenda vyakwetu kwanza haswa kama vikiwa vimekidhi viwango vya kimataifa!! Yani kama wewe bado unaagiza furniture kutoka nje ya nchi basi wewe ni bonge la mshamba!! Yani hujui Molocaho furnitures?! Wao wapo Village mall!… …..Kama budget hairuhusu leo kununua Molocaho toka Amorette basi waweza fika pale ALUTech, nao ni watengenezaji wa furniture nzuri sanaaaaaa kwa watu wa hali ya chini na kati pia wanafanya interior design kwa nyumba na office! ALUTech wanapatikana pale Mivinjeni, Kurasini bara bara ya Kilwa! Weka uzalendo mbele kwa kupenda vya kwenu kwanza! Kumbuka mkataa kwao ni mtumwa!!

Cheka urefushe maisha yako!

Eti na wewe unajiita Mwanaume,Mwanaume kumnunulia Zawadi mwanamke wako ni mpaka uone Valentine’s Day imekaribia ndio unajishaua na Shopping ili kusafisha nyota. Nani aliyekwambia Usela unalipa kwenye Mapenzi?? Unahisi ukimnunulia Zawadi na kumuonyesha unampenda utaonekana Bwege, Kuna kosa gani kuwa bwege kwa mtu unayempenda?? Hata wanafiki wakisema umeshikwa waambie NDIO NIMESHIKWA NIMESHIKAMANA! 
Make your Woman Smile……..Wala huna haja ya kutumia fedha nyingi kwenye Shopping za Mariedo. Ukiona kitu kizuri Karume NUNUA Mpelekee. Ukiona Gauni zuri Posta NUNUA mpelekee. Hamna kitu kizuri Wanawake wanapenda kama ZAWADI, hata kama umenunua JERO mtumbani, ile Feeling kwamba Ulipokiona ULIMKUMBUKA YEYE inampa impression kwamba She is On ur Mind na hilo ndo wanawake wanataka……..
Surprise her pale asipotarajia. Mpigie Simu aje, akifika una Parcel ya Saa nzuri. Utapendwa hadi ushangae……..Hawa watu wanaitwa mafataki hakuna Miujiza yoyote wanayofanya kumuiba mwanamke wako zaidi ya hii. Wanajua Wanawake wanapenda nini na wanawapa hicho. Wewe jifanye Msela halafu Mafataki wakufundishe Caring ni nini. USione Couple zinadumu ukajua jamaa anatumia heeelaaaa nyiiiiingi, walaaa…….Mijisapraiz tu,mwanamke anajiona Malkia masaa 24. Sio kila Limbwata imetengenezwa na Mganga wa Kienyeji,Ukitumia Akili tu sometimes ni Limbwata tosha.

Credit to #ChekaUsipasuke

“Kazi ya kuajiriwa ni nzuri lakini sio yako ni ya mwajiri wako.” Dina Marios

Naomba niongee na wale ambao tumeajiriwa.Pamoja na kuwa tupo katika ajira tujitahidi kuestablish biashara au mradi wako nje ya ajira yako.Angalia katika mazingira yako vitu gani unaweza kufanya ili kuongeza kipato cha pembeni.Kuna wazee wetu ambao labda wanasoma hapa wameshapitia hizi hatua za maisha.Ila wapo vijana wenzangu humu ambao bado hujastuka au kujipanga sawa sawa.

Binadamu unaouwezo wa kufanya mambo mengi sana ukiamua.Hivyo usijibane sana spread your wings hata kama unalipwa mshahara mkubwa ofisini.

Kazi ya kuajiriwa ni nzuri lakini sio yako ni ya mwajiri wako.Mwajiri wako anaweza kudai kazi yake au hata kuifuta wakati wowote na ukabaki unambwela mbwela tu usijue la kufanya.Mpaka uanze kutafuta kazi sehemu ingine hali inakuwa ngumu lakini kama una miradi na biashara zako zingine wakati unasubiria kupata ajira ingine unaendelea na shughuli zako tena na ukaamua kabisa No kuajiriwa.Nakuomba usijisahau unapokuwa kazini ukamfanyia kazi muajiri wako tu na ukaacha kuanzisha jambo lako mwenyewe.Unaweza kuwa na shamba,biashara yako,ufugaji au una talent fulani ukaitumia.

Kuna dada ameajiriwa lakini hodari sana wa kutengeneza pilipili.Ana biashara ya pilipili/chachandu ambayo inamuinguzia kipato.Tena wateja wakubwa ni ofisini kwake na maofisi mengine jirani.Zipo supermarkets kadhaa na min supermarkets.Ananiambia kwa jinsi anavyopata pesa kwenye pilipili hata mshahara wake ana muda hajaenda bank kuugusa.

Huo ni mfano tu Mungu amekusudia kukufanikisha katika mambo yote.Hivyo kujibana katika kazi hiyo tu ni kumuwekea Mungu mipaka ya baraka alizokupangia.Na Mungu mwenyewe anasema usiogope. Jitahidi kabla upepo haujageuka ukaja kukumbuka shuka kumekucha.Maana huwa vinageuka kwa kushtukiza hata kujipanga hujajipanga na kila siku ulikuwa unasema kesho kesho.

Nashukuru Mungu hata mie nje ya ajira nina biashara yangu ya mafuta ya nazi.Dina Marios baby coconut oil bidhaa ambayo naamini miaka kadhaa ijayo itakuwa brand kubwa ya mafuta ya nazi ya watoto.Nina projects nyingi za wanawake na watoto sijatulia kwa sababu Mungu amenipa uwezo na lazima niutumie Sifa na Utukufu ni kwake yeye aliye juu.

Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu,bali shamba langu mwenyewe sikulilinda…wimbo uliobora 1:6

Kila la heri!

Shukuru na furahia maisha wakati bado una pumzi ya uhai!

Wapendwa wasomaji wangu, maisha ni mafupi sana, mshukuru Mungu kwa pumzi ya uhai anayokupa kila siku! Na sio hivyo tu, Shukuru hata kwa vile unavyoviona ni vidogo kwani hivyo ndivyo vitakavyo kukamilisha wewe! Kama huwezi kushukuru hata kwa hivi vidogo Mungu anavyokujalia basi amini usiamini hautoweza barikiwa zaidi ya hapo!Kwamfano, mimi nilipokuwa under age ?, nilikuwa naomba Mungu anijalie niwe na uwezo wa kuwa nakuja Marekani mara kwa mara! Lakini tazama Mungu alivyo mwema, mimi sio tu ninauwezo wa kuja Marekani kama nitakavyo bali naishi Marekani! Kana kwamba hiyo haitoshi Mungu amenibariki zaidi ya mimi nilivyokuwa nikiomba, mtoto wangu amekulia hapa, amesoma hapa, na anaishi hapa! Kila ninapokuwa barabarani huku mwanangu ndiye anayeniendesha huwa na-smile in my heart nakusema ASANTE MUNGU! Najua siendeshi gari la kifahari sana kama wengine lakini namshukuru Mungu kwa kunitimizia ndoto zangu above and beyond my imagination!

Mimi na mdogo wangu Magreth, tukifurahia kufika kijijini kwetu Utegi salama! February 2017

Kuna watu wapo hapa hawajaona wazazi wao miaka chungu mzima! Wengine mpaka wazazi wao wanafariki lakini hawawezi hata kutoka kwenda kuwazika wazazi wao au ndugu zao! Sasa kwanini mimi nisimshukuru Mungu na kufurahia maisha wakati ninakila sababu!! Vile vile  namshukuru hata kwa zile ndoto ambazo ameona zisitimie kwa wakati huu kwani yeye ndio mpangaji wa vyote najua atanitimizia tu! Natamani kuwa bilionea, najua hii ndoto itatimia tu kwa uwezo wake??? Nakama haitotimia bado maisha yatasonga na nitamshukuru kwa yote! Furahia maisha katika hali uliuonayo sasa kwani maisha ni mafupi sana usipo furahia sasa utafurahia lini?! …….Nawatakieni weekend njema kwenu wote! Hapa U.S.A hii weekend ni ndefu kidogo sababu Monday ni public holiday, nawatakieni happy memorial! Ngoja nifurahie maisha by sorrounding myself with LOVE! Eeh, niwape umbea? Muhaya kakasirika, mmh! Wivu ukizidi nao ni shidaaaa ???? but still  nashukuru kwa yote ??  Mbarikiwe wote!

“21 years ago when there was nothing but dreams and a vision” -Joseph Kusaga

“21 years ago when there was nothing but dreams and a vision. Learning from DJ Mind motion in San Francisco, back then Clouds Media was just a dream……………. Trust me, if you truly believe, dreams do come true. From DJs to DJ makers. -Joseph Kusaga, Mind motion, Ruge Mutahaba in San Francisco” Joseph Kusaga

***Kama kusoma hujui hata picha ukitazama itakuwa imekupa somo la kutosha kuhusu maisha! Huyo ni Joseph Kusaga (Kulia) na Ruge Mutahaba (Kushoto) miaka 21 iliyopita katika harakati za kufanikisha ndoto zao!! Amka wewe uliekata tamaa, maisha ni kupambana na kung’ang’ania! Wacha wakucheke leo lakini kumbuka yule anayecheka wamwisho ndio atacheka zaidi!! Usitishwe na vicheko vyao kwa leo kwani mla ni mla leo mla jana kala nini??! Kesho yao itakuwa imepita na hakuna atakaye wakumbuka itakuwa story tu, na pengine hao wanao kucheka leo ndio watakao kupigia magoti na kuinamisha vichwa vyao kesho! #UsikateTamaa

“Let people get inspired by how you deal with your imperfections” ~~~~ShyRose Bhanji

“You don’t need to be perfect to inspire others. Let people get inspired by how you deal with your imperfections”………………… Maneno ya hekima haya toka kwa Dada wa Taifa! Maisha yako unayopitia au wewe mwenyewe jinsi ulivyo (your character) yawe mazuri au mabaya kwa namna moja ama nyingine lazima yatakuwa yanatoa mafunzo kwa wengine.  Huitaji kuwa mkamilifu kama “Malaika” ili kuwafanya wengine waone kuwa unafaa! Hakuna aliye mkamilifu hapa duniani na kama unafikiria wewe ni “Malaka” basi simama na uwe wakwanza kuturushia mawe sisi wadhambi!

Dr. Ntuyabaliwe Foundation yakabidhi Library!

Naamini wengi mtakuwa mmesikia kuhusu hii giving back to community foundation ambayo inakwenda kwa jina la “Dr Ntuyabaliwe”. Kama hujawahi kusikia habari hiyo basi huu ni mfuko ulio anzishwa na Jacqueline Mengi kumuhenzi baba yake mzazi ambaye alikuwa medical Dr I believe alikuwa Gynecologist  (please kama nimekosea unaruhusiwa kunisahihisha) lakini naamini alikuwa Gynecologist. Anyway, Jacqueline amekuwa anasaidia mambo mbali mbali kwenye jamii kwa kutumia mfuko huu.  Amekuwa akitoa vifaa vya hospitali (incubator)  vya kutunzia watoto ambao wanazaliwa premature / njiti, madawati ya shule na vifaa mbalimbali vinavyotumika mashuleni. Wiki iliyopita alikabidhi Maktaba / Library kwa shule ya awali ya Makumbusho iliyopo jijini Dar es salaam. Na hii ilikuwa mara ya pili kwa Jacqueline kujenga library kwa shule kwa kutumia mfuko huu wenye jina la baba yake. Kama picha inavyo jieleza hapo ilikuwa wanakabidhi library ya kwanza. Hongera sanaaaaaa Jacqueline, such an inspirational. Kama unafatilia hii blog basi utakumbuka huko nyuma niliwahi kusema kuwa sasahivi Jacqueline yupo kwenye “public eyes”  hivyo jamii itapata nafasi ya kumjua Jacqueline ni nani haswa ( her character) and I have to  admit the more I look at her the more I love her! Just lovely and beautiful. Haya na Molocaho hiyo inakwenda Dubai kwa maonyesho. Mungu akisema Yes hakuna wa kukuzuia! You go girl! Hongera Sanaaaaaa ??

Happy birthday baba Juju a.k.a Ruge Mutahaba! a.k.a Shemeji yangu!

Kheri ya siku ya kuzaliwa Mkurugenzi, baba yake Juju, Shubi, na wengine ambao sijawataja. Nakutakia furaha nyingi sana katika maisha yako, afya njema, amani, na upendo mwingi kwa familia yako, ndugu, jamaa, marafiki, na jamii inayo kuzunguka! Mungu azidi kukubariki ukawe mibaraka kwa wengi! Happy birthday mume wa Zamaradi, shemiji yake na mimi hapa ??……….. Haki kabisa, nilitamani niandike ujumbe uhu kwa Kihaya!! Tatizo mdogo wako MuhayaMmarekani basi ni shida tupu ??? Happy birthday Ruge be blessed always!

Matukio katika picha!

Hizi picha naweka tu ili ufurahishe macho kwani najua saa zingine unahitaji break ya kusoma articles  😉 😉 …….. Ni picha zilipigwa kwenye mji wa Beijing, China, kwenye picha nipamoja na Sir O.O. Igogo na binti yake Advocate Janeth Igogo (Mrs Nyagilo), na Mwanasheria Tarimo. Hii ni moja ya board meetings ambazo wanazifanya kila mwaka na wamekuwa wakikutana hivyo kwa muda wa miaka 10 sasa. Na mara nyingi huwa wana alternate kati ya Tanzania na China. Mwaka jana ilifanyika Tanzania soma ? HolleyPharm …… Haya enjoy the pictures