Sikia wewe mwanadada ❤️
Mwenyezi Mungu hakuumba mwanamke dhaifu, kuwa tegemezi kwa mtu zaidi yake yeye Mungu. Maandiko matakatifu yanasema kitabu cha Mwanzo aya ya kwanza mstari wa 27-28; Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba; mwanaume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia; zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini na ndege wa nchi. Kwa maana fupi Mungu ametuumba sote kwa mfano wake na ametupa sote uwezo na mamlaka ya kutawala dunia na kila kitu kilichomo ndani yake. Tumebarikiwa wote sawa kwenye roho. Tofauti ni maumbile ya nje. Ambayo hayana nguvu kabisa mbele ya roho. Roho haiifi, mwili hufa. Kwenye kitabu cha Mithali aya ya 31 kuanzia mstari wa 10. Mungu anazungumza juu ya mke bora. Yaani mwanamke anayefaa kuolewa au kupewa majukumu na vyeo vya juu. Huyu anasema ni mwanamke mwenye akili na busara, mwenye kujitambua, mwenye mali zake mstari wa 16 imeandikwa huangalia shamba akalinunua kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu. Mwanamke jitambue, jithamini. Una uwezo wa kusimama wewe kama wewe ukisimamia neno na kumtumainia Mungu. Umezaliwa kuwa tajiri na mmiliki wa kila kitu kizuri duniani. Tatizo wengi hatujitambui tunafikiria mwanaume ndio wa kutupa furaha/mali tunasahau Mwenyezi Mungu ametupa wote uwezo sawa wa kuitawala hii dunia na vilivyomo na kuboresha nafasi zetu. Tujitafakari na tubadilike. Mungu angetaka usitumie akili yako asingekupa vile alivyokupa vikusaidie kujenga maisha yako. Acha leo kuwa mtumwa. Hata mimi nilipotea na kuwa mtumwa kwa mtu nikadharauliwa na kupoteza thamani yangu kwa Mungu but never again ❤️ @dennis_wisee **Nime post tena hii article kutoka kwa Jojo! Aliandika mwezi wa tatu**