Peter Sarungi (The next Speaker)Ipo siku masikio yata ona badala ya kusikia na macho yatasikia badala ya kuona. Wakati ambapo utatamani ujifiche chini ya milima lakini haitawezekana, wakati ambao wanawake wengi wataomba kuitwa kwa jina la mwanaume mmoja huku wakijilisha na kujivisha wenyewe.
Kwa sasa namfananisha Tundu Lisu na mwanasiasa mkongwe wa vikwazo kutoka kwa jirani zetu Uganda Mh. Kiiza Besigye. Kwa hivi vikwazo vya kuwekwa korokoroni na kupewa kesi nyingi za uchochezi kwa Mh. Tundu Lissu huku akiendelea kuwa jarisi na mwenye kutetea ukweli na hata kutenda na kuheshimu sheria. Sasa ninaona umuhimi wa Tundu Lisu kuwa Raisi wa TLS maana kwa sasa tunahitaji viongozi wanao hoji mifumo kandamizi bila uoga ili kulinda maslahi ya Taifa na watu wake. Kwa courage aliyonayo Mh. Tundu Lissu katika siasa za kweli, naamini hichi ni kipindi cha watu kama akina Lissu kunyanyuka na kuungwa mkono kwa makusudi.
Ningekuwa ni mwanasheria, ningemchagua Lissu kuwa Raisi wa TLS. By the way hiyo TLS na majukumu yake nimeifahamu kipindi hiki kupitia Lissu na inawezekana sio mimi tu, tupo wengi.
Tabia ya wana siasa kabla ya kuwa watawala ni kama tabia za wachumba ambao bado hawajafunga ndoa. Tabia yao kuu ni kuhaidiana mazuri, kusifiana, kuelekezana kwa lugha ya kuvutia, kutiana moyo, kuoneshaana upendo wa agape lakini pia kuna tabia moja mbaya ya walioyo nayo ya kuficha udhaifu wao na mabaya yao.
Kila inapoitwa leo, napata fursa ya kujua tabia za mkuu wa nchi kupitia kauli zake na matendo yake. Niliwahi kukiri hapo mwanzo kwa kusema kuwa Mkuu wa kaya anasimamia vizuri kauli na matendo yake wakati wa kampeni nikidhani ataendelea kutawala kupitia kauli zake za kusisitiza umoja wa nchi. Nahisi ni mihemuko ya muda iliyo niathiri.
Pamoja na changamoto hizo bado maisha na siasa zitaendelea na ni lazima tuendelee kuwaoma wabunge hasa wa CCM ambao ni 75% kusimamia kwa kuikosoa, kuisema na hata kuipongeza serikali wanapo kuwa bungeni maana hiyo ndiyo kazi tuliyo watuma. Pamoja na mtikisiko huu ulio wapata wabunge kutoka kwa Mkuu wa kaya kama ilivyo ripotiwa na gazeti la mwananchi bado mtaendelea kuwa wabunge mlio pewa dhamana na wananchi ya kuwa wakilisha bungeni katika kuisimamia serikali.
Tusijenge Taifa la chuki na uadui unao tokana na siasa, tuki ruhusu hilo basi hatutokuwa salama maana ukweli ni kwamba chuki na uadui havina mipaka, nikikuchukia kwenye siasa usidhani nitakupenda uraiani. Hiyo ni mbegu mbaya itakayo tafuna jamii yetu.
Tujitahidi kujenga jamii ya kuvumiliana, kushauriana, inayo heshimu fikra tofauti na inayoweza kuwa karibu hata kama watakubali kutokukubaliana.
Nimepata taarifa juu ya kuzaliwa CCM mpya iliyo badilika katika muundo wa chama na uendeshaji lakini ikiendelea kubaki na itikadi yake ya zamani. CCM Mpya iliyosemwa na mwenyekiti wake kwamba itakuwa chama kwa wanachama yaani chama kitakacho milikiwa na wanachama wenyewe tofauti na mwanzo. Inasemekana kabla ya upya huu, chama kilikuwa kina endeshwa na wanachama wenye nguvu za fedha, vyeo na hata umaarufu. Sasa kwa upya huu, chama kitaendeshwa hata na mlalahoi bila kujali umaarufu wake, cheo chake ama fedha zake… (SAFIII SANAAA..)
LAKINI..????? Tafakuri yangu ni jinsi gani chama hiki kitaendeshwa na kumilikiwa na wanachama kama inavyoitwa CCM Mpya… ………Ikiwa kiwango cha uwakilishi wa wanachama hawa kwa idadi katika vikao muhimu na vinavyo toa maamuzi muhimu ya chama umepunguzwa kwa zaidi ya nusu??? Yaani kutoka mia tatu na kitu hadi mia moja na kitu..!!!Ikiwa idadi ya vikao vilivyokuwa viki tathmini utendaji wa chama na serikali vimepunguzwa???Chama chenye wanachama na wapenzi wapatao milion 8, kutoka mikoa 35, ikiwa na jumuiya mbalimbali karibia tano na matawi lukuki, chama kinacho ongoza nchi kuongozwa na wajumbe 165 badala ya 385 alafu tuna sema CCM mpya ya kumilikiwa na wanachama??
Hili panga ni kali na sijui kama hawa vijana wenzangu Benard R. Shigela ?na Yesaya Shamsele ?walio anza vizuri kujifunza siasa na uongozi kama watapata nafasi na fursa ya kuwepo kwenye vikao vya CCM mpyaJJk alidokeza sababu ya mabadiliko haya kuwa ni UKATA…. Tunasoma Namba.. Hii sababu ya kuifanya CCM kumilikiwa na wanachama bado kwangu haija ingia akilini labda wadau watufafanulie..
Is he a firm proponent of a free market economy or he simply “dont get it” with regard to the economics behind the agricultural industry???
Or are we witnessing the absence of “coherent and consistent” agricultural policy?
Magufuri told farmers that, the govt will not provide assistance in case of food shortage…..the implication is that, it will be farmers’ fault that there will be food shortage…….mhhh!!
Overall, this just says one thing; either there is no such a thing as an agricultural policy or it is not well developed to reflect some unforessen contingents like bad weather.
European have Common Agricultural Policy(CAP); that have emerged from its birth in the 60s. The aim is simply this; to help farmers in case there is a need for that. The philosophy behind the policy is that, unprotecting the industry will lead to food shortage. What else? Prices fluctuations caused by alternating good and bad season is not a welcome for a smooth economic growth of any country. To stabilize agricultural products prices, and ensure a good standard of living for its citizens, countries enact these kind of policies.
USA has what it calls Agricultural Adjustments Act; with the same goal. The policy has evolved from its inception in the 1930s.
Tanzania should not second-guess itself when it comes to the agricultural sector. The industry needs govt protection. Magufuri’s statements were so unfortunate.
If more diverse economies; less-dependent on agriculture as the engine of their economic growth like EU and USA have the policy in place,…..why not Tanzania?!!!
Huwa sipendi kuingilia siasa za ndani za vyama vingine lakini huwa inanilazimu kwa sababu chama kama cha ccm kinatawala serikali hivyo maamuzi yake yana athari kwa uendeshaji wa serikali na Taifa kwa ujumla.
Nimeona mjadala wa wafuasi wengi wa upinzani wakilalamika juu ya maamuzi ya fukuza fukuza ya wanachama wa ccm wanao itwa wasaliti. Wanapinga na kulaani maamuzi halali yaliyotewa kutokana na vikao halali.
Mimi naunga mkono maamuzi hayo maana watu walio fukuzwa wamepatwa na mazingira ya kusaliti chama. Ni kama Mh. Zitto alivyo vuliwa uana chama wa Chadema Tanzania kwa tuhuma za usaliti ulio elezewa na viongozi wa kushirikiana na chama tawala. Walio fukuzwa wana mazingira ya kusaport harakati za Lowasa Edward kushika dola kupitia vyama vya upinzani wakati wao wakiwa na vyeo katika chama cha ccm, huu ni usaliti usio takiwa kufumbiwa macho.
Fukuza, fukuza, fukuza hadi wale wote karibia 75% ya wajumbe wa almashauri kuu ya NEC walio imba wimbo wa kuwa na imani na Lowasa wafutike katika vyeo vyao ndani ya ccm, mkìweza wafukuzeni na wabunge ambao bado ni waumini wa Lowasa.
Mkiamua kujenga safu ya mwenyekiti wenu kwa mgongo wa kusafisha chama, nawashauri mfanye kwa uhakika na asibaki hata mmoja aneyeweza kuhoji na hata kusema tofauti na mkuu. Hilo ni jambo lenu la ndani na wala sisi tusio wanachama hatupaswi kuingilia na ndio maana nina pinga kwa nguvu zote wanao laani na kubeza maamuzi haya.
Nawatakia mkutano mwema katika kujenga ccm mpya na kuiacha ccm ya Nyerere, ccm ya mwinyi, ccm ya mkapa na hata ccm ya Jk.
In politics, don’t ever let your opponents have a chance “to define” you before you have defined yourself. Thats why politicians in the western world like to write books about their life stories. It gives them a chance to “set the records straight” before their political opponents hijack their stories and paint them however they see fit.
Considering his background, Makonda should have dealt with his past a while ago……! And he still can……..
He has a personal story to tell….of a guy who…despite many obstacles….swam against the tide to reach where he is…..a story that can resonate with a lot of aspiring young men and women…..from all those failures in school and yet be able to pick up yourself and get going…..thats inspiring….! Of course, he will have to start by admitting his blunder and failure to be honest with Tanzanians upfront……My wish is that, there were good PR (public relations) experts in Tanzania….
Moja ya sifa ya Mkuu wa kaya katika hotuba zake ni kupenda kutoa mifano ama utani yenye chembechembe za ukweli. Sifa kama hizi akipewa mama, mke, dada au hata bibi inaleta furaha na inajenga kujiamini kwao.
Nitumie fursa hii kumpongeza Mama Salma Kikwete (Malkia wa nguvu wa Taifa) kwa kuteuliwa kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naamini sifa ulizo pewa na Mkuu zita akisi uwezo wako wa kutetea maslahi ya Taifa na wananchi wake.
Nafasi uliyopata sasa inakusogeza karibu zaidi na matatizo ya wana wa nchi lakini pia inakupa uwezo zaidi ya kuleta suluhisho ya matatizo hayo tofauti na ulivyokuwa First Lady. First Lady ni ceremonie title, ulikuwepo kwaajili ya kupamba kazi ya baba, kumshauri na kusapoti kazi zake kupitia WAMA. Uwezo wako binafsi ulifichwa ndani ya mafanikio na sifa za baba. Sasa ni zamu yako kuonesha ushujaa wako kwa nchi na hasa kwa wale wanao beza uteuzi huu, onyesha umuhimu wa fursa kwa wamama kama alivyo onesha Mama Hilary Clinton.
Nakutakia Kazi njema na utendaji mzuri katika kutumikia wananchi wa tanzania kupitia Bunge. Mama usiogope kukemea na kusema ukweli. Ni Haki yako kusema ukweli hata kama utabaki peke yako, bado ukweli huo ulio usema utaishi zaidi yako.
Kuna msemo unasema “Adui mwombee njaa, atainua mikono juu hata kama ni Shujaa”
Msemo huu unatukumbusha kwamba siku zote binadamu umuombea mabaya mpinzani wake, ndivyo tulivyo umbwa na hata katika siasa ndivyo ilivyo tena ni zaidi ya kuomba mabaya na kutenda mabaya kwa mpinzani wake.
Upinzani una kabiliwa na kesi nyingi sana katika mahakama zetu. Kesi hizi zipo kwa viongozi kuanzia ngazi ya ya mwenyekiti Taifa hadi kwa wenyeviti wa vijiji mikoani. Uwepo wa kesi hizi zina athiri upinzani kwa njia tatu.
1. Ki Uchumi: Uendeshaji wa kesi una gharama kubwa mno na kwa nchi zilizoendelea, kesi ni njia moja wapo ya kufilisi au kupunguza uchumi wa mtu ama kampuni. Mfano: Mike Tyson pamoja na mambo mengine ali filisika baada ya kugharamia kesi yake ya kubaka.
2. Ki Siasa: Baada ya uendeshaji wa kesi, kinacho fuata ni hukumu. Hukumu yaweza kuwa nzuri ama mbaya kwa upinzani, inapokuwa mbaya inaleta pengo kubwa la kisiasa kwa upinzani. Mfano: Mh. Peter Lijualikali (MB Kilombero) anatumikia hukumu ya kifungo cha miezi sita jela. Hukumu hii ina dhoofisha nguvu ya siasa na hata kuleta pengo la utendaji wa mwanasiasa huyu kwa walio mchagua.
3. Ki Jamii: Inapotokea kiongozi wa kisiasa anapatwa na tuhuma, anashitakiwa na kuhukumiwa basi wanao umia kisaikolojia ni jamii yenye imani kubwa na kiongozi huyo. Mfamo Mh. Mbowe (MB Hai, KUB na M/kiti Chadema) anapopatwa na tuhuma ya kukwepa kulipa kodi au kujihusisha na Dawa, wanao umia zaidi kisaikolojia ni wakereketwa, wapenzi, mashabiki, wananachama na viongozi wa Upinzani walio chini yake.
Hizo njia tatu kwa pamoja zinaleta athari za kudhoofika kwa wanasiasa mahiri na machachari wa upinzani
#Kumbuka Dhamani sio ushindi, Tunaye kaimu judge mkuu kwa mhimili huu, Kuna wanasiasa walio nyamaza baada ya kesi. Pole G. Lema (MB Arusha) na wananchi wa Arusha kwa mateso ya kisaikolojia mliyo yapata kwa muda wote.
Nakumbuka enzi za Nyerere……wakati alipokuwa anakamata vijana wasio na kazi kwa kosa la “uzururaji”…..kwangu mimi naona kazi ya serikali ni kuweka sera za kuinua uchumi na kuongeza kazi (to create economic policies that will create opportunities for young people)…….kukamata vijana ambao wanatafuta riziki wakati serikali yako imeshindwa kuinua maisha yao kwa kuweka uchumi bora ni “morally wrong”. Na nalaumu hiyo sera ya Nyerere wakati ule. Nyerere was supposed to own his failure; failure to enact laws that will create policies for economic opportunities for young people.
Likewise, while I don’t support impersonation and forgery, I think we should be considerate of people who seeks second chances in life…..using other people’s certificates to advance their career opportunities etc etc
Who is to blame for that? Again; the government and its education policies. For not enacting laws that will give second chances to these kind of people. In most developed countries, you can opt for other educational alternatives that are equivalent to the education level you seek.
The govt needs to work harder to create an environment in which people who failed in their exams, young girls who caught pregnancies while at school and other who dropped out of school for any reason, can do “a comeback” later in life. Lack of opportunities and alternatives makes these people turn to forgery and impersonation.
It is “morally wrong” to punish them for their efforts to better themselves; regardless of how they seek to better their lives (except if its killing or stealing).
Kwenye ngoma zetu kuna wanao piga ngoma na kuna kundi la wanao cheza ngoma inayopigwa. Siku zote mpiga ngoma ndiye mwamuzi wa aina gani ya mdundo upigwe ili mcheza ngoma acheze, mpiga ngoma akizima ngoma basi na mchezaji naye anasitisha kucheza, mpiga ngoma ndiye ana amua speed ya ngoma ama ngoma ipigwe kwa muda gani.
Siasa za sasa za nchi ziko kisayansi sana kiasi kwamba upinzani wametawala njia nyingi za upashaji habari. Siasa hii naifananisha na ngoma zetu za jadi, yaani ni kama vile upinzani wanapiga ngoma ili watawala wacheze.
Hii ngoma ya wapinzani imeanzwa kuchezwa tangu mwaka jana baada ya utawala mpya kuanza kazi, upinzani umeshapiga ngoma kwa midundo mingi sana tofauti iliyomfanya mtawala kucheza bila kuchoka.
Hizi ni baadhi ya ngoma zilizopigwa na upinzani na watawala wakacheza kwa maana ya kujibu mapigo.
1. Ukuta
2. Uchwara
3. Phd
4. Michango ya Tetemeko
5. Njaaa
6. Bring back ben alive
7. Free Lema
8. Free Max wa JF
9. Swala la uteuzi wa wabunge
10. Bashite
Haya ni machache yaliyo vuma na kuchukua headlines za magazeti na mitandao ya jamii. Na hizi zote zimekuwa zikianzishwa kwa malengo ya kuonesha na kuaminisha mapungufu ya serikali kwa wananchi.
Siwalaumu upinzani maana hiyo ndiyo sayansi ya siasa na ndiyo kazi yao, ila nawalaumu sana chama tawala na watawala wenyewe kwa kushindwa kupiga ngoma zao ili upinzani nao wacheze. Ninavyojua mimi, JPM amefanya mambo makubwa ambayo yanatosha kuwekwa kwenye haedline kwa muda mrefu, lakini wasaidizi wa watawala na wapenzi wa chama tawala wamekaa kimya na kujikuta wakijibu mashambulizi ya upinzani katika hoja zao bila kujua kwamba wanacheza ngoma. Hizi kick ndizo zinazo pamba upinzani usisahaulike hadi 2020 hata kama mkikataza siasa za majukwaa.
Au labda watawala wamejitoa kwenye ulingo wa siasa? Au wapenzi wa chama tawala wameshindwa kuusoma mchezo wa siasa? Huu mchezo hautaki hasira wa mabavu ya dola ila unataka mkakati wa kujivunia mazuri yanayo fanywa na Utawala Chama tawala kukaa kimya na kucheza ngoma za upinzani ni sawa na huyu ☝ aliye kabidhiwa brifkes ya ofisini akaringa bila kujua kuwa imetoboka. Amkeni mpige ngoma wapinzani wacheze, fanyeni kama Magoiga SN.
Nitumie fursa hii kutoa tafsiri ya katiba juu ya Malengo yake kwa kufuata Ibara ya II.C. Malengo hayo yatajumuisha yafuatayo.
Jukwaa litasimama kama sauti ya kuwakilisha maoni na mapendekezo ya watu wenye ulemavu.
Kusimamia maoni na mapendekezo yanafanyiwa kazi katika vyombo vya serikali, mashirika, almashauri na taasidi mbalimbali wakati wa kuunda sera na sheria katika jamii.
Kuratibu vikao, mikutano na makongamano ya kueneza na kukuza uelewa wa watu wenye ulemavu juu ya sera, taratibu na sheria katika kupata fursa mbalimbali za nchi.
Kujenga mahusiano na muingiliano mzuri kati ya jamii ya watu wenye ulemavu wenyewe na jamii zingine tukilenga ushirikishwaji katika kutumia fursa mbalimbali.
Kufanya tafiti mbalimbali za maswala ya watu wenye ulemavu kwa kutumia chombo kitakachoundwa ili kutambua changamoto na mafanikio ya utekelezaji wa sheria na sera mbalimbali zinazohusu watu wenye ulemavu.
Kutoa taarifa mbalimbali zenye lengo la kubainisha fursa za kijamii, siasa na uchumi zilizopo kitaifa na kimataifa ili kuhamasisha ushiriki wa watu wenye ulemavu.
Kuratibu uanzishwaji wa vikundi mbalimali vyenye malengo ya kuungana ili kupata fursa za uchumi na jamii ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa majukwaa madogo ya ukanda, mikoa,miji na vijiji katika kueneza sauti ya watu wenye ulemavu.
Kushawishi, kutetea na kukuza haki na wajibu wa watu wenye ulemavu kupitia usimamizi wa sera na sheria No.9 ya watu wenye ulemavu.
Hayo ndio malengo hasa ya kuanzisha Jukwaa hili. Nitaanza kuchambua umuhimu wa kila lengo ili kujua uhitaji wa lengo hilo katika jamii ya watu wenye ulemavu.
Tafadhali share, like, tag na comment kushiriki katika malengo haya ili jamii na wadau woye wapate taarifa.
Malkia wetu wa nguvu anarudi tena kwenye macho ya jamii! Mama Salma Kikwete anarudi tena baada ya kuteuliwa na Rais Dr. Magufuli kuwa Mbunge wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hapo jana!
Wengi tulimzoea kumuona akitumikia jamii kama First Lady lakini sasa atatumikia jamii kama Mbunge. Ile nafasi ya kwanza ya kuwa First Lady ilitokea tu (by default) kwasababu ni mke wa JK. Lakini sasa lazima atakuwa ameombwa na Rais Magufuli na amekubali kwa hiyari yake mwenyewe! Hata hivyo, nani ajuae?! yawezekana hata akapewa wizara fulani kuiongoza ambapo binafsi naamini atafanya kazi nzuri sana kwani ametuonyesha kwa vitendo alivyo kuwa First Lady! Haswa natamani apewe wizara inayo husiana na mambo ya maendeleo ya wamama na watoto!
Katika maisha kila mtu ana ndoto zake na wito wake. Watu wengine wamebahatika kuweza kutimiza ndoto zao wakiwa na umri mdogo. Lakini kuna wengine kwasababu ambazo pengine ni Mungu tu ndio ajuae ndoto zao huchelewa kutimia na wengine zisitimie kabisa! Basi si ajabu kumuona Malkia wetu wa shoka akitumikia jamii tena akiwa na cheo cha chini. Kwani hiyo ni dalili nzuri ya mtu mnyenyekevu ambaye yupo teyari kujishusha kwa faida ya taifa lake. Pia bado haja chelewa kutimiza ndoto zake ndio maana hata Hilary Clinton alikubali kufanya kazi ya kuwa Secretary of State chini ya uongozi wa Rais Baraka Obama.
Hivyo basi, tunamtakia utumishi mwema kwa kuweka uzalendo kwanza. Natumaini ile kauli mbiu yake ya “Mtoto wa mwenzio ni wako” ataiendeleza ili kuokoa vijana wa taifa hili kutoka kwenye madawa ya kulevya!
Nitumie fursa hii kutoa shukurani kwa wote walio jitolea na hata kufuatilia kwa karibu juu ya uundwaji wa Jukwaa la Watu wenye Ulemavu Tanzania. Mpaka sasa tumekamilisha 95% ya taratibu za kusajili Taasisi hii muhimu kwa walemavu. Jamii ya watu wenye ulemavu imeendelea kutengwa katika mipango mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa sababu ya kukaa kimya bila kusema juu ya changamoto zetu, uwezo wetu, vikwazo tunavyokumbana navyo na hata mafanikio yetu. Ni muda sasa umefika wa kusema kwa nia ya kutetea na kushawishi maswala ya watu wenye ulemavu Tanzania ili na sisi Tanzania tufanane na wenzetu wa Afrika Mashariki walio amua kutekeleza kwa maneno na vitendo mkataba wa UN unao husu jamii ya walemavu na ni mkataba ambao Mh. Mkapa aliridhia na kusaini kisha Mh. Kikwete kuruhusu utungwaji wa sera na sheria no.9 ya watu wenye ulemavu na sasa kilichobaki ni kupiga kelele juu ya utekelezaji wake.
Ni jukumu letu sote kupiga kelele tena bila utengano na kwa sauti moja hata kama wewe sio mtu mwenye ulemavu lakini ukiguswa na hili basi ni sahihi kusema kwa nguvu hadi jamii, serikali na wadau wengine wapate kusikia ujumbe huu. Kuna msemo unasema hivi…
“Mtoto anayelia na kupiga kelele sana ndiye anaye pewa nyonyo na mama yake, ukinyamaza maana yake umeshiba”
Sidhani kama sisi watu wenye ulemavu tumeshiba katika nchi yetu, la hasha ila tuna ugulia kimya huku tukifa na tai shigoni. Ukimya wetu ndio unao tufunga, unao turudisha nyuma, unao tififisha ndoto zetu, unao tukosesha thamani na ndio sababu ya kutengwa na fursa.
Tanzania amka useme jambo kwa jamii hii ili na wewe ushiriki katika kutetea na kushawishi maswala ya watu wenye ulemavu Tanzania.
Katika kila jambo au shughuli yoyote lazima kuna fedha zitatumika tu! Hii haijalishi ni shughuli ya chama, kanisa, msikiti, kijamii, au za kipagani lazima fedha zitahusika! Lakini sasa uingizaji na utoaji wa hizo fedha zinaweza kuwa katika mfumo uliyo rasmi (yani kuna kuwa na budget, mfumo wa malipo, na washuhudiaji) au siyo rasmi (yani hakuna accountability ya aina yoyote ile).
Tukirudi katika mada yetu kama kichwa cha habari kisemavyo, kuwa, “kulipwa kwa kazi ya campaign ya chama ni halali yako” basi ngoja tuzungumzie hilo kwa sasa. Kampeni za siasa huwa lazima chama kinajipanga kwa mikakati (strategies) ya jinsi ya kufanya campaign yenye mafanikio. Na moja ya mikakati hiyo ni jinsi ya kukusanya pesa rasmi kwaajili ya kukamilisha mikakati hiyo! Hapo ndipo utasikia kitu ‘budget ya campaign’. Pia kwa serikali ya Tanzania huwa wanakitu kinaitwa posho / ruzuku ya chama wakati wa campaign!
Hiyo budget ya campaign haitumiki tu kununulia vitendea kazi vya campaign bali pia kuwalipa wanachama / makada watakao kuwa teyari kufanya campaign hiyo kulingana na malengo ya chama chao. Ndio maana wakati wa campaign huwa wana aajiriwa watu maalum wa kufanya campaign au kikosi maalum cha nguvu kazi kwa ajili ya campaign husika kwa mfano anaweza ajiriwa Campaign Manager, au Financial Controler kwa ajili hiyo tu!
Sasa wewe kama ni mwanachama uwe mtu wa kawaida au “celebrity” kupewa fedha kwa ajili ya campaign ni kitu cha kawaida, ni swala ambalo linatambulika kisheria, na zaidi ya yote ni halali yako!
Wewe unapo acha shughuli zako za uzalishaji wa kila siku nakwenda kufanyia chama campaign nilazima chama kikupe hela za kujikimu maana utahitaji hela ya kukutoa point A to Z, utahitaji kula, utahitaji kulala kama ni nje ya mahala unapo ishi! Huwezi kuchukua pesa zako binafsi kufanyia chama campaign wakati kwanza umeacha shughuli zako za uzalishaji, pili kama una familia inamaana budget ya familia utaivuruga kwa mambo ya campaign.
Jamani, hata makanisani kuna budget ya kutembelea washiriki ambao ni wagonjwa, wajane n.k nawatu huwa wanapewa pesa za kujikimu na safari kama hizo. Hivyo si ajabu mtu kulipwa kwa shughuli ya campaign kwani hizo ndizo zile hela wenyeviti na viongozi wengine wa chama wanatumia kwa matumizi yao binafsi haswa kama hakuna mwanachama au wanachama ambao wanaweza ku-question uongozi! Kiwango / kiasi cha ulipwaji waweza tofautiana kutokana na nguvu aliyo nayo mtu huyo pamoja na makubaliano yao. Fedha zote zinazo ingia kwenye budget ya campaign ya chama lazima ziwe kwenye mfumo rasmi unao eleweka!
Labda kama baba yako ni Mzee wa “Vijisenti” (you don’t need that kind of “petty” money) kama sivyo kulipwa kwa kazi ya campaign ya chama ni halali yako!
HATA SAULI ALIKUJA KUITWA PAUL Injili ya Yesu kristu inaeleza kuwepo kwa Sauli aliyebadilika na kuitwa Paulo. Injili inamwelezea Sauli kama kiongozi wa kijeshi aliyekuwa ni katili kupita kiasi, asiyekuwa na huruma, aliye chukia, kuwatesa na kuwa hukumu kifo wana wa Mungu. Lakini pamoja na machukizo haya yote mbele za Mungu bado Mungu alikuwa na mpango mzuri naye.
Mpango wa Mungu ulikuja kutimia na Sauli akaitwa Paulo. Kupitia jina la Paulo, tabia zake zilibadilika na akawa mtumishi wa Mungu aliyeweza kuhubiri injili na kuandika vitabu vingi vya injili kuliko wanafunzi wote wa Yesu kristu alio wachagua na kuwapa kazi ya kueneza injili.
Hivyo sishangai kama Daudi akikimbia jina lake na kuitwa Poulo, maana yawezekana kwa jina la Daudi alikuwa mnyonge, kilaza, mvivu, mwoga, aliyefeli kwa kupata fa fa fa zote katika matokeo ya fom 4. Lakini kwa kuitwa Paulo emebadilika na kuwa jasiri, mchapa kazi, kiongozi mbunifu na mwenye kuthubutu, aliye faulu hadi chuo kikuu, aliyetenda makubwa katika uongozi wake kuliko hao wateule wa Mkuu.
#MyTake
Kuna majina mengine yana Nuksi, hayaendani na ndoto zako na wala hayakusaidiiii. Unaweza ukawa una lalamika kushindwa kila jambo jema unalo jaribu kwa nguvu zote huku ukimshirikisha Mungu wako bila mafanikio kumbe ume sahahu kwamba jina lako halijabeba future unayotaka. Tuchunguze majina yetu hasa haya ya Ulaya.
Mwanangu Fidele siku akiona jina lake halimsaidii kufikia ndoto zake nitamruhusu na kumsaidia kubadili jina ???? Joks..
Niliwahi kusema kwamba vita alivyo chagua Makonda ni vita vinavyo hatarisha ustawi wa maisha yake. Mpaka sasa Mh. Makonda anapigana vita nne kwa yeye kuanzisha vita moja ya madawa.
1. Vita juu ya uhalali wa mali zake
2. Vita juu ya uhalali wa Elimu yake
3. Vita vya kisheria dhidi yake mahakamani
4. Vita dhidi ya Bunge na maazimio yake Maandiko matakatifu yanaeleza jinsi Yesu kristu alivyotoa kauli kwa wayahudi waliotaka kumwadhibu mwanamke aliye fumaniwa akizini kwa kutumia sheria za Musa……Alisema, “Kama kuna aliye msafi(asiye na dhambi) kati yenu basi na awe wa kwanza kumpiga mawe huyu mwanamke aliyefanya dhambi”
Hii ni kauli nzito sana kwa dunia ya sasa, Dunia inayotawaliwa na uwazi na kumbukumbu za kiteknologia, Dunia iliyo na macho pande zote, Dunia iliyojaa unafiki, usaliti, chuki, visasi, uongo, uzandiki, kashfa, fitina na machikizo mengi baina ya binadamu mmoja na mwingine.
Kwa Dunia kama hii… Ni vizuri tukaishi vizuri na jamii, tukaheshimu uongozi kam dhamana, tukajitakasa na dhambi kabla ya kuwatafuta na kuwahukumu wenye dhambi, tukajifunza kubakisha maneno ya kesho na keshokutwa.
Pole Mh. Makonda, ulianzisha vita moja lakini sasa unapigana vita nne tofauti.
Mungu akusaidie na akulindie roho yako isije ikapondeka kwa maneno na matendo ya binadamu wenzio…..Amina
Ikatokea Mungu akakubariki kufika 2020 ukiwa hai na mwenye afya nzuri basi utakumbana na changamoto ya joto kali la siasa ambalo halijawahi kutokea nchini. Kwa Lowasa Edward, 2020 ni mwaka wake wa mwisho kujaribu kufikia ndoto zake za kutawala nchi, ni kama ana bunduki iliyobaki na risasi moja ndani ya mapambano, hivyo ni lazima apambane kwa akili sana tena kimya kimya ili kutafuta target sahihi ya kufyatua risasi yake kwa adui. Ndio maana kwa sasa Lowassa anajipanga kimya kimya akiamini matokeo yake ni 2020.Kwa JPM, 2020 ni mwaka wake wa kuimarisha utawala wake na hasa kupata matokeo yatakayo leta taswira ya kupwaya kwa upinzani nchini. Hivyo kwa sasa anajipanga kwa matendo na kwa mifumo ndani ya chama na nje. Kutokana na nguvu alizopewa Raisi kupitia katiba ya nchi, ni kazi nyepesi sana kutengeneza mfumo utakao kusapoti mbele ya safari hivyo tutegemee mifumo hiyo kukamilika 2019.
Kwa wananchi, 2020 ni mwaka wa majaribu sana kwao. Mpaka sasa bado wananchi wengi hawajui mwisho wa utawala huu ukoje, hawajui kama kutakuwa na mazuri ama mabaya ndani ya miaka hii mitatu iliyobaki (2017, 2018 na 2019) ikitokea uchumi wa mwananchi ukakua hadi kufika kipindi cha JK basi JPM atakuwa amepiga risasi ya ushindi kwa wananchi maana mpaka sasa amefaulu sehemu kubwa hasa ya ufisadi na nidhamu lakini amefeli kwenye UKATA wa wananchi, kuna malaika wameanza kuishi kama mashetani.
Na Peter Sarungi (Next Speaker)“Vita ya dawa za kulevya haina umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu anahusika mkamateni” Raisi Dkt. Magufuli…….Katika vita hii, nilikuwa nasubiri kauli ya mkuu wa kaya ya kutoa support ya ulinzi, usalama na hata kubariki vita hivi alivyo vianzisha Mh. Makonda (RC. Dar) Kauli alizozitoa Mkuu wa kaya wakati wa kumwapisha Mkuu wa Majeshi Tanzania yana ashiria ushiriki wa moja kwa moja wa mkuu wa kaya. Majibu ya JPM kwa kauli ya Mh. Nape ni firimbi kwa viongozi wengine wanao leta sababu nyingi za kunyamazisha vita hii wakati vijana wana angamia.
“Kauli ya Raisi ni agizo linalo hutaji utekelezaji bila kusita” Peter Sarungi @2017